Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109980 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa katika mazungumza na Balozi wa Japan nchini, Shinichi Goto, aliyemtembelea ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 9, 2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Shinichi Goto, ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma Novemba 9, 2018.

WIZARA YA FEDHA YATOA SEMINA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI

$
0
0
 Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Utafiti Kitengo cha Maendeleo ya Sekta ya Fedha  Michael Nyagoya ambae ni akitoa Mada wa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia jambo katika Semina iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Sehemu ya watumishi kutoka Ofisi ya Bunge pamoja na Wabunge wakifuatilia jambo katika Semina iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)

WIZARA YA FEDHA YATOA SEMINA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakifuatilia jambo katika Semina iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Ndg. Michael Nyagoya ambae ni Kaimu Kamishna Msaidizi Idara ya Sera na Utafiti Kitengo cha Maendeleo ya Sekta ya Fedha akitoa Mada wa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Sehemu ya watumishi kutoka Ofisi ya Bunge pamoja na Wabunge wakifuatilia jambo katika Semina iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Ewura yatakiwa kupitia upya gharama za umeme zinazotozwa na wazalishaji binafsi

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na waendelezaji wa miradi midogo ya umeme wanaonufaika na ruzuku ya Mfuko wa Nishati Vijijini ulio chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kikao kimefanyika jijini Dodoma katika ofisi za Wizara ya Nishati.
Na Teresia Mhagama, Dodoma

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuangalia upya gharama za umeme zinazotozwa na wazalishaji binafsi wa umeme kwa wananchi ili kuwa na muongozo wa pamoja badala ya kila mzalishaji  kutoza gharama yake. Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na waendelezaji wa miradi midogo ya umeme wanaonufaika na ruzuku ya Mfuko wa Nishati Vijijini ulio chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

“ Suala la gharama za matumizi ya umeme wanazotozwa wananchi lazima EWURA mpitie upya na kuweka muongozo, mfano kuna wananchi waliopo vijijini wanatozwa shilingi 750 kwa uniti moja badala ya shilingi 100 na unaweza kuta gharama anazotoza  mzalishaji  wa umeme jua wa eneo moja  zinatofautiana na mzalishaji wa umeme jua wa eneo jingine,” amesema Dkt Kalemani.

Amesema kazi ya kujadili bei za umeme ishirikishe pia watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na REA na kueleza kuwa kama kuna sababu za msingi zinazosababisha wazalishaji  hao wa umeme kutofautiana katika utozaji wa bei za umeme, ziwekwe wazi kwa Serikali. Aidha, Dkt Kalemani amewaeleza wazalishaji hao wa umeme kuhusu  msimamo wa Serikali wa kuunganisha umeme vijijini kwa gharama ya shilingi 27,000 tu kwani kuna wananchi wamekuwa wakilalamika kutozwa gharama kubwa.

Dkt Kalemani amewakumbusha kuzingatia gharama hiyo ya Serikali baada ya wazalishaji hao kutaja gharama za uunganishaji umeme wanazotoza katika maeneo tofauti, ambapo sehemu nyingine wananchi wanatozwa shilingi 40,000 au 150,000 au 50,000 na sehemu nyingine wanaunganishwa kwa kukatwa katika bili za umeme.

Katika kikao hicho, wazalishaji hao wameeleza kuhusu utekelezaji  wa kazi ya kuunganishia umeme wananchi ambapo Waziri aliwapongeza kwa kazi hiyo ambayo imepelekea wateja zaidi ya 10,000 kuunganishwa na umeme na vijiji zaidi ya 40 kusambaziwa umeme. Hata hivyo, Dkt Kalemani amewataka kukamilisha kazi ya usambazaji umeme kwa maeneo waliyopangiwa ifikapo Juni 2019, na kuwataka Mameneja wa TANESCO kuhakikisha kuwa wanasimamia pia miradi hiyo badala ya kusimamia miradi ya Serikali pekee ili kuhakikisha kuwa inafanyika kwa ufanisi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na watendaji wa Wizara ya Nishati, REA na TANESCO wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu, Raphael Nombo ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.

CGP KASIKE ATEMBELEA MAGEREZA YA MGAGAO NA ISUPILO, LEO MKOANI IRINGA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) akiangalia vitalu vya miche ya miti aina ya misindano(pines) alipowasili katika Gereza la Mgagao, Wilaya ya Kilolo leo Novemba 10, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Gereza hilo, ASP. Peter Sahani(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Iringa, ACP. Hassard Mkwanda.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(wa kwanza kulia) akikagua moja ya shamba la miti aina ya misindano alipofanya ziara ya kikazi leo Novemba 10, 2018 katika Gereza la Mgagao, Wilayani Kilolo.
Askari wa Gereza Mgagao, Koplo Stephen akieleza changamoto mbalimbali za kiutendaji mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza alipotembelea gereza hilo leo Novemba 10, 2018.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA UNUNUZI KOROSHO

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amekutana na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, baadhi ya watendaji wa Serikali na Wakurugenzi wa mabenki na CBT jijini Dodoma Novemba 10.2018, kujadili maandalizi ya ununuzi wa korosho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AZINDUA BARABARA MPYA YA BONITE MANISPAA YA MOSHI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kupeleka huduma bora za kimaendeleo kwa wananchi wote nchini.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami ya Bonite yenye urefu wa kilometa 2.93 iliyopo katika Manispaa ya Moshi. 
Makamu wa Rais yupo mkoani Kilimanjaro kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
“Nawapongeza kwa Usafi na nawapongeza kwa miundombinu ya ndani katika Manispaa ya Moshi, Serikali yetu inaleta maendeleo kwa kila Mtanzania” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais anaendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na kufungua barabara ya Bonite pia aliweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Pasua ambacho kimegharimu shilingi za Kitanzania milioni 400 na kitakuwa na Wodi ya Mama na Mtoto, Chumba cha Upasuaji, Xray na Maabara.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema ndani ya miezi 18 Vituo vya Afya 350 vinategemea kukamilika na kwa mwaka wa fedha 2018-2019 hospitali mpya 67 za wilaya zitajengwa ambapo katika Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Rombo na Siha zitajengwa hospitali hizo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa barabara Bonite yenye urefu wa kilomita 2.93 iliyojengwa kwa kiwango cha lami wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira(katikati), Meya wa Manispaa ya Moshi Ndugu Raymond Mboya (kulia)  Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ndugu Kippi Warioba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (kushoto).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya Bonite yenye urefu wa kilomita 2.93 iliyopo Moshi Manispaa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Moshi Ndugu Raymond Mboya wakati wa kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa barabara ya Bonite yenye urefu wa kilomita 2.93, wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira(katikati),Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ndugu Kippi Warioba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MIAKA 65 YA GOJU RYU KARATE-DO, JUNDOKAN YATIA FORA HUKO OKINAWA, JAPAN

$
0
0
Takribani nchi zaidi ya 30 na washiriki wa Karate wapatao 300 ikiwemo Tanzania kuwakirishwa na sensei Fundi Rumadha Dan 4 wa chama cha Jundokan Tanzania, wamekamilisha sherehe maalum toka chama cha Jundokan kuanzishwa na master Eiichi Miyazato, baada ya kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Karate wa Goju Ryu master Chojun Miyagi sensei kufariki. Hizi ni sherehe kubwa hufanyika kila baada ya miaka mitano, zimewakusanya walimu na wanafunzi toka mabara yote, ikiwemo na Tanzania.

Sherehe hiyo inaendelea katika ukumbi maalum wa michezo ya sanaa za mapambano " Okinawa Karate kaikan Hall ", ukumbi mpya kabisa uliofunguliwa na mfalme Akihito miaka miwili iliyopita. Ukumbi huu, utakuwa umeupumzisha ule wa zamani wa " Budokan Hall".

Pia, sensei Fundi Rumadha, alipewa fursa ya kuwa miongoni mwa walimu au masensei wa nje ya Japan kufanya maonyesho ya kata mbele ya masta wa karate maarufu toka kisiwani hapo Okinawa. Pia hii ilikuwa fursa pekee kwa watu wa Okinawa kuona kwamba Tanzania inalo tawi la chama hicho na kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye sherehe hizo.
Zaidi ya hayo, sambamba na hii sherehe kubwa kisiwani hapo,  kutakuwa na mahudhurio ya makumbusho na kuona  minara ya kumbukumbu za waasisi wa mitindo mbalimbali ya Karate kwa washiriki wote.
Pia, wakati wa shughuli hizo, sensei Fundi Rumadha alipata fursa ya mahojianona gazeti la "Okinawa Times", na kutaka kujua, kuna hamasa gani na jinsi gani watanzania wanavyoona kuhusu mchezo wa Karate huko Tanzania.

Sherehe ya kufunga maadhimisho hayo zitafanyika usiku wa leo Jumapili kwa masaa ya Japan. Baada ya mitihani ya mikanda tofauti miesi ya walimu toka shule au dojo mbalimbali kumalizika asubuhi ya leo.
Sensei Rumadha (wa kwanza kushoto) na washiriki wenzie wakifanya Sachin kata. Angola na Tanzania ni moja ya nchi za Afrika kushiriki.

RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA MAGARI YA JESHI YA KIKOSI CHA USAFIRISHAJI CHA 95KJ AMBAYO YANAWEZA KUTUMIKA KUBEBEA KOROSHO KATIKA MIKOA YA KUSINI (LINDI NA MTWARA) IWAPO WANUNUZI WA KOROSHO HAWATANUNUA KOROSHO HIZO BAADA YA SIKU YA JUMATATU SAA KUMI JIONI

$
0
0


 
 Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo wakielekea kwenye viwanja vya Kambi ya 95KJ kukagua magari ya Kikosi hicho ambayo yatatumika kubeba korosho katika mikoa ya Kusini iwapo Wanunuzi wa Korosho hawatatii agizo la Serikali ifikapo siku ya jumatatu saa kumi alaasiri.

 Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Madereva wa Kikosi cha Usafirishaji cha Jeshi 95KJ ambao wapo tayari kutekeleza maagizo ya Serikali baada ya siku ya jumatatu saa 10 alaasiri iwapo Wanunuzi wa Korosho hawatanunua korosho zilizopo katika mikoa ya kusini.
 Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania CDF Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kukagua magari hayo ya Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam
 Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askari mbalimbali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) hawaonekani (pichani) katika Kambi ya Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli ametoa maagizo kwa Kikosi hicho cha 95KJ kubeba Korosho zote zitakazo nunuliwa na Serikali iwapo Wanunuzi wa Korosho hawatatii agizo la Serikali ifikapo siku ya jumatatu saa kumi alaasiri.
 Askari mbalimbali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakimsikiliza Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza katika Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam

  Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimiana na Askari mbalimbali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimiana na Askari mbalimbali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam.

 Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jaamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania CDF Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kukagua magari hayo ya Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ Temeke jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA MAGARI YA JESHI YATAKAYOTUMIKA KUSAFIRISHA KOROSHO

BREAKING NEWZZZZ: RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI, MWITA WAITARA AULA

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI ATOA SIKU NNE KWA WAFANYABIASHARA WA KOROSHO KUZINUNUA

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI ATOA SIKU NNE KWA WAFANYABIASHARA WA KOROSHO KUZINUNUA

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI ATOA SIKU NNE KWA WAFANYABIASHARA WA KOROSHO KUZINUNUA

BASATA YAVUTIWA NA MAFANIKIO YA MSANII NANDY


MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO

$
0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wa Serikali Wilayani Rombo kufanya kazi kwa kushirikiana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jana  mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Agnes Hokororo.

“Wote tunajenga nyumba inayoitwa Tanzania katika nafasi yako yoyote ulipo unajenga nyumba inayitwa Tanzania, kwa itikadi yako yoyote uliyonayo unajenga nyumba inayoitwa Tanzania tunatawaliwa na sheria moja, tunataliwa na miongozo hiyo hiyo ya Serikali, kanuni na mambo mengine na hiyo hiyo Serikali”.

Katika ziara yake Wilayani Rombo Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo, mradi wa maji Shimbi Mashariki,kukagua shamba la Miti Rongai.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo pia alipata nafasi ya kuwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza barabarani kumsalimia na alihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Keni-Mengeni.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Serikali hii inafanya jambo la kihistoria kwa kukamilisha ujenzi wa vituo vya Afya 350.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungungumza na Watumishi wa Wilaya ya Rombo mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
2 4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri Mhandisi Boniface Vedasto. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
5 6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza kumsalimia wakati alipokuwa njiani kuelekea kwenye shamba la miti Rongai. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua kitalu cha miche wakati alipotembelea shamba la miti la Serikali lililopo Rongai Rombo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 

KOKA ACHANGIA MIL 3 KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI WA LUMUMBA KATA YA PANGANI UJENZI WA KIVUKO CHA MUDA

$
0
0
Baadhi ya Wananchi wa mitaa ya Lumumba na Muheza kata ya Pangani ,mjini Kibaha wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini, Silvestry Koka wakikagua kivuko mtaa wa Lumumba kuvuka mto Mpiji kwenda Kibwegere Kibamba Dar es salaam, wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo.

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

WAKAZI wa mitaa ya Lumumba na Muheza kata ya Pangani ,mjini Kibaha wameanza kujitolea kujenga kivuko cha muda kuvuka mto Mpiji ili kuepukana na maafa ya kujeruhiwa na mamba kutokana na kero kubwa ya ukosefu wa kivuko cha kudumu. Kufuatia jitihada hizo ,mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka amechangia milioni tatu ili kuunga mkono juhudi za wananchi hao.

Akikagua mradi wa ujenzi wa kivuko hicho kuvuka mto kwenda Kibwegere Kibamba Dar -es salaam, wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo, Koka alisema wakati wakielekea kwenye mkakati mkubwa ,hakuna budi kuanza na mkakati wa muda mfupi.Alibainisha ,serikali kupitia wakala wa barabara mijini( TARURA )imetenga sh.mil 500 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko hicho kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kujenga kivuko kikubwa na cha kudumu .

"Nilipiga kelele kuhusu kivuko hiki na kimeitikiwa na TARURA kuna mpango wa kujengwa ambapo imeshatengwa mil 500 ila tatizo lililopo ni mvutano kati ya TARURA Kibamba na Kibaha,jambo ambalo linafanyiwa kazi  ".
Mbunge Wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka (wa pili kulia) akizungumza wakati alipokwenda kukagua kivuko mtaa wa Lumumba kuvuka mto Mpiji kwenda Kibwegere Kibamba Dar -es salaam ,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo ,wa kwanza kulia mwenyekiti wa ujenzi Jerome Munisi.

" Nia yangu ni kuona kivuko cha kudumu ila wakati mambo hayo yakiendelea kufanyiwa kazi ,nawaomba mhusishe wataalamu katika harakati hizi ili kuondokana na hasara ya kujenga kisha kivuko kusombwa na maji ya mvua mara kwa mara ,

"Kipindi cha nyuma nilishatoa milioni nne kwenye kivuko ambacho kilisombwa na mvua kubwa iliyonyesha ,sasa inahitajika milioni 28 kukijenga kingine,mimi nachangia milioni tatu tena"alifafanua Koka.

Mwenyekiti wa mradi huo ,Jerome Munisi alisema wameungana mitaa ya Lumumba ,Muheza na Kibwegere (LUMUKI)kukabiliana na tatizo hilo baada ya watu kujeruhiwa na mamba. Alielezea, mchango wa kaya wametoa mil 3.9,kanisa katoliki 530,000,chemchem ya uzima 750,000 jumla mil. 5.250 hivyo kwasasa mahitaji ya mafundi bado ni milioni 20 ambazo zitasaidia kujenga kivuko hicho.
Mkazi wa Lumumba Frenk John ,aliomba jitihada ziongezwe kwa kuitisha mkutano utakaolenga kuhamasisha wananchi kujitolea kujenga kivuko cha muda ili kuondokana na adha zilizopo kabla ya mvua kuanza. Hata hivyo ,Koka alikagua kivuko kingine cha Mkombozi kinachojengwa kwa kushirikiana na Jeshi kwa kushirikiana na wananchi na serikali ambapo yeye alishachangia milioni 11.

Aliahidi kuendelea kuwahimiza wajenzi wa daraja ambao ni jeshi na kwamba atawasiliana na makao makuu ya jeshi ili kuweka msukumo kitako cha daraja kipelekwe kabla ya mvua kubwa kunyesha.

Pia, mbunge huyo alitembelea ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Kidimu katika kata hiyo, na kudai atahakikisha anasimamia ujenzi huo ukamilike mapema ili wanafunzi waingie mwakani.

RESIDENTAL FOOTBALL CAMP AT BAOBAB SEC SCHOOL

MICHUZI TV: KUTANA NA BABU MTUNZI WA MASHAIRI KONKI

Lugola awaondoa madarakani Kaimu RPC, Mkuu wa Operesheni Mkoa, OCD, Mkuu wa Intelejinsia Uvinza

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Uvinza

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuwaondoa katika madaraka Mkuu wa Utawala wa Jeshi l aPolisi Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Operesheni wa Mkoa huo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza na Mkuu wa Intelejinsia wa wilaya hiyo.

Pia Lugola ameagiza askari wote wa kituo cha polisi Mpeta na Nguruka wilayani vinza wwahamishwe haraka iwezekanavyo katika vituo hivyo. Lugola ametoa kauli nzito kwa kuwaondoa katika nyadhifa zao maafisa wa juu wa jeshi hilo, kutokana na mapungufu aliyoyaona katika operesheni iliyofanyika mwezi uliopita ya kuwaondoa wakulima na wafugaji waliovamia ranchi za Taasisi ya NARCO ambao ipo chini ya Wizra ya Mifugo, ambayo katika operesheni hiyo askari polisi wawili na raia wawili waliuawa.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Mwanduhubandu, Kijiji cha Mpeta Wilayani Uvinza, leo, Waziri Lugola alisema viongozi hao wa Polisi wameshindwa kuifanya kazi hiyo kwa umakini ndio mana kulikua upungufu mkubwa katika operesheni hiyo, hivyo damu za waliouawa zinakua juu ya hao viongozi wa polisi mkoa na wilaya.

“Kutokana na hali hiyo, namuagiza IGP Sirro kuwaondoa kwenye madaraka hao wote niliowataja ifikapo kesho, na kesho Jumatatu nitakapo kuwa Dodoma nitakutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuona hatua nyingine za kinidhamu zitakazochukulia kwa hao niliowataja,” alisema Lugola.

Waziri Lugola aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi halina nia ya kuua mtu, kumuonea mtu, kudhulumu mtu lakini pale inapotokea jeshi hilo limeshindwa kutekeleza wajibu wake vizuri, lazima yeye Waziri achukue hatua.
Hata hivyo, Lugola alisema Jeshi la Polisi halipaswi kuvunjika moyo, litaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika kuhakikisha linapambana na uhalifu, kwa hayo ambayo yanayojitokeza hayana nafasi ya kuwakatisha tamaa wala kuwavunja moyo.

“Mimi Waziri wa Wizara hii, dhamana yangu na haya ninayoyafanya, vyombo vyangu vya ulinzi na usalama ninavyovisimamia msinione mimi kama mwanasiasa, msichukulie maagizo yangu na matamko yangu kama ya mwanasiasa, atyakaye jidanganya hivyo, itakula kwake,” alisema Lugola.

Lugola alioagiza waondolewe madaraka ni Mkuu wa Utawala wa Jeshi l aPolisi Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wakati operesheni hiyo ilipotokea, ACP Simon Ngowi, Mkuu wa Operesheni wa Mkoa huo, SP Msembele, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza, SSP Mwakisambwe, na Mkuu wa Intelejinsia wa wilaya hiyo, InspektaDotto Daudi.
Viewing all 109980 articles
Browse latest View live




Latest Images