Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Monalisa atakiwa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini

0
0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Mwanatasnia wa Filamu Bi. Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda. 
 Pongezi hizo amezitoa leo ofisini kwake Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam alipokutana na Muigizaji huyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. 
Bi. Fissoo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii. 
“Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako” Alisema Fissoo. 
Kwa upande wake Monalisa alimshukuru Katibu Mtendaji Bi. Fissoo kwa kuendelea kuwapa ushrikiano akiwepo yeye mwenyewe na Bodi kuwa sehemu ya kuhimiza na kusimamia Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. 
Monalisa alimuahidi kuendelea kushirikiana na Bodi hiyo katika kuendeleza na kutangaza sekta nzima ya Filamu kila apatapo fursa ndani na n je ya nchi. 
“Bodi ya Filamu imekuwa ni muhimili mkubwa katika kuiongoza Tasnia ya Filamu nchini hivyo nitahakikisha naendelea kushirikiana nayo bega kwa bega ili tuweze kuipa heshima Tasnia na nchi yetu kwa ujumla kupitia kazi bora tutakazo zizalisha” 
Alisema Monalisa. 
 Monalisa amepata Tuzo ya heshima kama Mwanamke wa Mfano na mwenye Ushawishi kwa Jamii kupitia kazi zake za Uigizaji ambapo Tuzo hiyo kutoka nchini Uganda atakabidhiwa Tarehe 1 Disemba 2018 jijini Kampala.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na nguli wa Filamu nchini mara baada ya kumaliza kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Tasnia hiyo na kupokea taarifa ya kupata Tuzo ya heshima Mwanatasnia Yvonne Cherrie (Monalisa) kutoka nchini Uganda. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Monalisa (Masafa Mwalimu), anayefuatani Bi. Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa na wa kwanza kulia ni Bi. Suzan Lewis ambae pia ni Mama mzazi wa Monalisa.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 9,2018

DC DAQARRO ATAKA WADAU WA ELIMU KUHAKIKISHA MPANGO WA LANES UNAENEA ARUSHA NA KULETA MATOKEO CHANYA

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha .

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka waalimu na Afisa elimu kuhakikisha mpango wa KKK (LANES) unatiliwa mkazo sanjari na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma kuandika na kuhesabu ili kuleta matokeo chanya na kufikia malengo ya serikali ya wananchi wote kujua kusoma. 

Akiongea wakati akifungua wiki ya kusoma na stadi za kukuza kusoma kuandika na kuhesabu (LANES) iliyofanyika katika Maktaba ya mkoa Dc Daqarro amesema kuwa wajibu huo ni wetu sote kuanzia nyumbani hadi mashuleni kuhakikisha kila moja wetu anatimiza wajibu wake. 

Amesema kuwa wiki kama hiyo ni ya kujitathmini tumefika wapi na tunaelekea wapi kama taifa kwa ajili ya kukuza uelewa wa vijana wetu kujua kuhesabu kusoma na kuandika ili kuwa na taifa linalopiga hatua kwa wananchi wake kujua kusoma. 

“Taifa limejipanga kuondoa wananchi wasio jua kusoma na kuandika ndio maana ilikaja na mkakati wa kkk hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuhakikisha tunafikia malengo ya mkakati huu”alisema Daqarro
Kwa Upande wake Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na wao kama waalimu watahakikisha kila kijana anayepata nafasi anajua kusoma kuandika na kuhesabu lengo ni kuondoa vijana wanaomaliza elimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika. 
Mkuu wa wilaya Arusha mjini Gabriel Daqarro akifungua wiki ya usomaji iliyofanyika kwenye maktaba ya mkoa Arusha pembeni ni mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Bi Rafiki Mvamba na kushoto ni Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu huyo wa wilaya
Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa wiki ya usomaji Lanes kabla ya kumkaribusha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro 
Meza kuu wakiwa wanajadiliana mkuu wa wilaya na mkutubi mkuu wa maktaba bi Rafiki Mvamba ambapo afisa elimu akiendelea kutoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi 
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa shule sita za wilaya ya Arusha walioshiriki mashindano mbali mbali ya kusoma kuandika na kuhesabu wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi Mwangaza na sombetini wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yalioendelea kwenye hafla hiyo .

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA

0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke akiwa katika Picha ya pamoja na Wabunge ambao ni wajumbe wa Chama cha urafiki wa kibunge baina ya Bunge la Tanzania na nchi ya China alipokutana nao leo Bungeni Jijini Dodoma.Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke akizungumza na Wabunge ambao ni baadhi ya wajumbe wa Chama cha Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Nchi ya China alipokutana nao leo Bungeni Jijini Dodoma.

    RC Wangabo afika kwenye ghala la TFC na kukuta patupu

    0
    0
    Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembela ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) na kutokuta hata mfuko mmoja wa mbolea huku wakulima wakijiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 huku mvua zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.

    Mh. Wangabo amefanya ziara fupi katika maghala kadhaa ya wafanyabiashara binafsi pamoja na makampuni yaliyopo mjini sumbawanga na kukuta shughuli za uletaji wa mbolea ukiendelea kwa maandalizi yam simu wa kilimo huku Kampuni ya Mboleaa Tanzania (TFC) ikikosa hata mfuko mmoja katika ghala lao jambo lililowashanga walioambatana na Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo.

    “Tutawasiliana na viongozi wa TFC ili tuweze kujua kwanini hawaleti mbolea ya kutosha wakati hii ni kampuni ya serikali inaweza ikaleta mbolea nyingi kuliko hata hao wengine lakini badala yake “godown” (ghala) kubwa lakini hakuna kitu, nini manufaa ya TFC sasa,” Alihoji.

    Awali akisoma taarifa ya kampuni hiyo msimamizi wa ghala hilo Jelio Mahenge alisema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 207/2018 kampuni ilifanikiwa kusambaza tani 1082 na kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 kampuni imejipanga kuleta jumla ya tani 2500 kwa awamu ya kwanza.

    “Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kampuni inafanya jitihada zote za hali na mali kuhakikisha uletaji wa mbolea unatekelezeka ndani ya mwezi huu wa kumi na moja ili kuendana na msimu wa kilimo na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla,”

    Msimu wa Kilimo wa mwaka 2017/2018 Mkoa ulitumia zaidi ya tani 24,000 za Mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 mkoa unatarajiwa kutumia zaidi ya tani 34,000 na mpaka mwanzoni mwa mwezi huu Mkoa umepokea tani 363.75 ambazo tayari zikiwa ndani ya maghala ya wafanyabiashara wa mbolea na nyingine zikiwa njiani.
    Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga walipotembelea moja ya maduka ya wauzaji wa mbolea yaliyopo mjini Sumbawanga.

    KUMBUKUMBU

    MADAKTARI BINGWA 42 KUTOA HUDUMA YA UCHUNGUZI URAMBO

    0
    0


    NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA 

    JUMLA ya Madaktari Bingwa 42 wanatarajia kutoa huduma ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo tezi dume na kansa ya matiti kwa wakazi wa Wilaya ya Urambo kuanzia wiki ijayo. 

    Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta wakati akitoa taarifa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani jan. Alisema madaktari hao watato huduma ya uchunguzi wa dezi dume kwa wanaume na uchunguzi wa satani ya matiti kwa wanawake kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo. 

    “Nawaombeni Waheshimiwa Madiwani fikisheni ujumbe huu kwa watu wenu ili wakazi wengi kujitokeza kupata huduma hizo…haitakuwa vizuri Madaktari bingwa wamekuja kutoa huduma kwetu kasha wakute hakuna watu.”alisema. Alisema zoezi limeandaliwa na Ofisi ya Mbunge kwa kushirikiana na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwa lengo la kuhakikisha wakazi wake wanapata huduma ya uchunguzi huduma karibu yao. 

    Mganga Mkuu wa Wilaya ya Urambo alisema kuwa huduma zitakazotolewa ni pamoja uchunguzi wa tezi dume, uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wakinamama na macho. Alisema wameamua kutoa huduma hizo pamoja na uchunguzi wa tezi dume ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Marehemu Spika Mstaafu Samwel Sitta kwa kuwa tatizo hilo ndilo lilisababisha kupoteza maisha. 

    Mganga huyo wa Wilaya aliwataka wananchi wengi kujitekeza kupata huduma hizo Urambo kwani nje ya hapo katika Hospitali nyingine kama ile ya Taifa Muhimbili, Bugango na KCMC ni kubwa.
    Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta akichangia taarifa ya utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo jana. 


    Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’

    0
    0

    Mjadala Mkali wa kujadili Ripoti ya kamati ya fedha katika Bunge la NNE la Afrika Mashariki,EALA umeendelea Jana huku wabunge mbalimbali wakiendelea kumtupia lawama katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC,Liberat Mfumukeko kuwa ndo chanzo cha ubadhidifu wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 10 za jumuiya hiyo.
    Katika kikao hicho Mbunge wa Kenya Simoni Mbugua alitishia kujihudhulu nafasi yake ya ubunge iwapo wahusika hawatachukuliwa hatua za kinidhamu.
    “Katibu Mkuu kwa muda mrefu amekuwa akifuja fedha na si pesa kidogo ukijumlisha fedha ambazo zimepotea ni zaidi ya dola Milioni 10″Amesema.
    Amesema fedha hizo zinatoka kwa wachuuzi wa nchi wanachama ili zitumike kwa watu wa EAC lakini zimekuwa zikipotelea Mifukoni mwa wachache bila sababu za msingi
    “Fedha hizo zikitolewa zinakuja zinaporwa na Katibu Mkuu na watu wake, wanapora na kuweka kwenye mifuko yao  ,Kwenye Masoksi wanabeba pesa zote ,sasa mwananchi aliyeko kule anajua mambo yanaenda vizuri lakini sisi kama wabunge tunasema inatosha ,hatutakubali tena” Amesema Mbugua
    Aidha alisema kuwa yeye kama Mbunge  afadhali atoke kwenye nafasi yake kuliko kuona jumuiya ikiharibiwa kwa kiasi hicho.
    Aliongeza kuwa kulitaka Bunge hilo kuiga utendaji wa Rais  John Magufuli na Rais Kenyatta wa Kenya ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na ufisadi  kwa kuwafunga watuhumiwa wanaopatika na hatia.

    MADIWANI URAMBO WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI TATIZO LA MBOLEA YA TUMBAKU KUCHELEWA

    0
    0
    NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA.

    UZALISHAJI na ubora wa tumbaku msimu ujao wa kilimo unaweza kushuka baada ya mbolea ya kukuzia zao hilo kuchewewa kuwafikia wakulima hadi hivi sasa.Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi kwa niaba ya Madiwani wenzake wakati wa kikao cha Baraza hilo.

    Alisema hadi hivi sasa mbolea ya aina ya N.P.K bado hajifika kwa wakulima wakati msimu wa mvua umeshakaribia kuanza jambo linalotishia ubora na uzalishaji.Malunkwi alisema kitendo hicho sio tu kitamwathiri mkulima pekee pia mapato ya Halmashauri ya Urambo yataathirika kwa sababu sehemu kubwa inategemea tumbaku ili kupata mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

    Alisema kwa mujibu wa taarifa za Mzabuni ambayo amepewa jukumu la kusambaza mbolea kwa wakulima wa tumbaku, meli iliyobeba mbolea hiyo itawasili nchini tarehe 11 mwezi huu na inaweza kuchukua wiki mbili na kendelea kuwafikia wakulima jambo ambalo litafanya mazao ya wakulima yapitwe na wakati.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Magreth Nakainga akitioa ufafanuzi kwa Madiwani wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa utekelezaji kwa kila Kata wilayani humo jana.
    4a
    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo jana.
    A
    Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta  akichangia taarifa ya utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo jana.

    KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

    SERIKALI YATOA SIKU NNE KWA WANUNUZI WA KOROSHO

    0
    0

    *Yawataka waandike barua wakionesha tani wanazohitaji na lini watazichukua
    *Yasema zaidi ya hapo haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena

    SERIKALI imetoa siku nne kwa wanunuzi wote 35 waliojiandikisha kununua korosho wawe wamepeleka barua katika Ofisi ya Waziri Mkuu wakionesha  kiasi cha tani wanazohitaji na lini watazichukua.

    “Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale wote ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidogo, wahakikishe ndani ya siku hizo nne kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24.”

    Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Novemba 9, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu ununuzi wa zao la korosho, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.Baada ya kupita siku hizo Serikali italazimika kufuta usajili kwa wote waliojisajili kununua zao hilo kwa sababu walikubaliana kwenda kununua lakini hali inayoonekana sasa ni kama kumkomoa mkulima kitu ambacho imesema haitakubaliana nacho.

    “Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua kwani ofisi yangu ipo wazi saa 24 wana nafasi ya kuleta barua wakati wowote wakionesha nia yao na kiwango wanachokihitaji. Zaidi ya hapo Serikali haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena.”

    Waziri Mkuu amesema kwenye msimu wa ununuzi wa korosho wa mwaka huu, walishuhudia kusuasua kwa minada, ambapo Serikali ilikutana na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ambapo walikubaliana kununua kwa bei inayoanzia sh 3,000 na kuendelea.

    “Mjadala ulikuwa wa wazi na wafanyabiashara wenyewe walipendekeza bei ambayo ilikuwa inaanzia sh. 3,000, hata hivyo baada ya kikao hicho ununuzi katika minada imeendelea kusuasua na hata tani zilizokuwa zikinunuliwa zilikuwa kidogo sana. Sisi tunaiona hali hii kama mgomo baridi ambao si sawa sawa sana kwani malengo yetu sisi na sekta binafsi ni kumfanya mkulima apate bei nzuri.

    Hali hii haifurahishi kwa sababu Serikali imedhamiria kuboresha mazao yanayolimwa na wakulima kwa kuwasaidia kuanzia katika hatua za utayarishaji wa mashamba, upatikanaji wa pembejeo na masoko ili waweze kunufaika na kilimo na kupata tija katika mazao hayo.”Waziri Mkuu amesema baada ya kugundua bei imekuwa tatizo Serikali ilifanya jitihada za kupeleka wataalamu wake katika masoko makuu duniani na kupata bei halisi ambayo bado  inatosha kumlipa mkulima sh 3,000.

    Hatua hiyo imekuja baada ya zao la korosho kuendelea kununuliwa kwa bei ya chini na idadi ya wanunuzi kuwa ya chini licha ya uzalishaji wa mwaka huu kuwa mdogo ukilinganisha na msimu wa mwaka jana.Amesema msimu wa mwaka jana uzalishaji ulikuwa zaidi ya tani 300,000 na mwaka huu zinatarajiwa tani zaidi ya 200,000 hivyo wafanyabiashara wanao uwezo kununua korosho zilizopo.

    Hata hivyo Serikali imewataka wananchi hususani wakulima wa korosho nchini kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu wakati ikiendelea kushughulikia suala hilo.


    IMETOLEWA NA:
    OFISI YA WAZIRI MKUU,
    S. L. P. 980
     41193 – Dodoma
    IJUMAA, NOVEMBA 9, 2018.

    TAMKO LA SERIKALI KUHUSU WANUNUZI WA KOROSHO

    WIZARA YA MADINI, MKANDARASI SUMAJKT WAJADILI MAENDELEO UJENZI WA VITUO VYA UMAHIRI

    0
    0
     Na Asteria Muhozya, Dodoma
    Waziri wa Madini Angellah Kairuki tarehe Novemba 8, aliongoza kikao cha kujadili Maendeleo ya Ujenzi wa Vituo vya Umahiri vinavyojengwa maeneo mbalimbali nchini.

    Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri Stanslaus Nyongo na Doto Biteko pamoja na Menejimenti ya Wizara ambapo Mkandarasi SUMAJKT na Washauri Elekezi kampuni za Y&P Architects, InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujezi wa vituo hivyo walieleza kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa za ujenzi wa vituo hivyo.

    Vituo vya umahiri vinajengwa maeneo ya mbalimbali nchini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ulio chini ya wizara.

    Vituo hivyo vinalenga katika kutoa mafunzo ya jiolojia katika utafiti wa madini, mafunzo ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia zebaki.

    Vilevile, vinalenga katika kutoa mafunzo ya biashara kwa wachimbaji wadogo wa madini, mafunzo ya usalama na afya sehemu za kazi na mafunzo ya namna bora za utunzaji wa mazingira kwenye migodi ya wachimbaji.

    Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki alisisitiza kuhusu kuzingatiwa kwa ubora wakati wa  ujenzi wa vituo husika na kusisitiza Mkandarasi SUMAJKT kukamilisha ujenzi huo katika muda uliopangwa. 

    Vituo vya umahiri viko katika hatua mbalimbali za ujenzi na vinajengwa Bariadi, Bukoba, Handeni, Musoma, Songea, Chunya, Mpanda na Chuo Cha Madini Dodoma.

    Ujenzi wa vituo hivyo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 11.9 zinazotokana na mkopo wa Benki ya Dunia.
     Waziri wa Madini Angellah Kairuki(katikati) Naibu Waziri Stanslaus Nyongo (kulia) na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko wakifuatilia kikao  kati ya wizara  na Mkandarasi SUMAJKT anayejega vituo vya umahiri maeneo mbalimbali nchini na Washauri Elekezi Kampuni za Y&P Architects, InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujenzi wa vituo hivyo. Kikao hicho kilijadili maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo.
     Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao kati ya wizara na na Mkandarasi SUMAJKT anayejega vituo vya umahiri maeneo mbalimbali nchini na Washauri Elekezi Kampuni za Y&P Architects, InterConsult Architects, Sky Architects. Anayefuatilia ni Naibu Waziri Stanslaus Nyongo.
     Sehemu ya Menejimenti ya Wizara wakifuatilia kikao hicho.
    Mkandarasi SUMAJKT anayejega vituo vya umahiri maeneo mbalimbali nchini na Washauri Elekezi Kampuni za Y&P Architects, InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujenzi wa vituo hivyo wakifuatilia kikao hicho baina yao na Wizara.

    SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA PALESTINA NCHINI

    0
    0
     Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Palestina nchini Hamdi AbuAli alipomtembelea mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
      Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Hamdi AbuAli alipomtembelea mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
     Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika picha ya pamoja  na Balozi wa Palestina nchini Hamdi AbuAli mara baada ya kuzungumza naye mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
     Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia )katika picha ya pamoja  na Balozi wa Palestina nchini Hamdi AbuAli (wa pili kushoto) mara baada ya kuzungumza naye mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kushoto ni Mhe. Amina Makilagi na Kulia ni Mhe. Lolesia Bukwimba.

    PICHA NA BUNGE

    PWANI YAKAMATA LUNINGA KUMI ZA WIZI,WEZI TISA AKIWEMO WA MAFUTA KWENYE MRADI WA UJENZI WA STANDARD GAUGE-WANKYO

    0
    0

    Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
    JESHI la polisi mkoani Pwani, limekamata luninga kumi flat screen zenye thamani ya sh. mil.18, ambazo ziliibiwa katika matukio mbalimbali ya uvunjaji, mkoani humo. 

    Aidha linamshikilia mtu mmoja jina limehifadhiwa baada ya kukutwa akiwa na madumu kumi yenye ujazo wa lita 20 ya mafuta aina ya dizeli  ,aliyoiba katika mradi wa ujenzi wa reli ya standard gauge , Soga wilaya ya kipolisi Mlandizi. 

    Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa alisema, wanashikilia watu nane kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio hayo. 

    Nyigesa alieleza katika msako huo wamekamata jenereta mbili kubwa zenye thamani ya milioni 6.5 ambazo ni aina ya Euro power EP. 6500E na boss BG -2500 .

    Alifafanua, vitu vingine vilivyokamatwa ni deki mbili, vingamuzi viwili, speaker mbili, music system mbili, home fieta moja, rimoti sita, speaker twiter mbili, flash moja kapeti za chini ya sakafu mbili, stendi ya vyombo moja na extention moja. 

    Hata hivyo kamanda huyo alisema , mtuhumiwa aliyekamatwa kijiji cha Mperamumbi akiwa amepakia mafuta kwenye pikipiki aina ya sanlg namba MC. 197 BJD kutoka mradi wa standard gauge wanamhoji na atafikishwa mahakamani. 

    Katika tukio jingine wamekamata pikipiki saba na bangi kiroba kimoja kilichokuwa kinasafirishwa kwenda kuuzwa. 

    Nyigesa alibainisha, katika tukio hilo mmiliki wa pikipiki yenye namba za usajili MC 951 BSA  anaombwa kujisalimisha mwenyewe kituo chochote cha polisi ndani ya siku tatu vinginevyo watamsaka popote ili kueleza kuhusu bangi hiyo. 
    Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa akionyesha baadhi ya luninga flat screen zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo (picha na Mwamvua Mwinyi)

    Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa akielezea msako endelevu unaendelea mkoa humo huku akieleza kauli mbiu yake ya Tindua Tindua hadi kieleweke. (picha na Mwamvua Mwinyi)

    Mmoja wa watu walioibiwa luninga zao, mzee Lebul Mfinanga (wa kulia aliyebeba luninga) akiwa ametoka kutambua luninga yake makao makuu ya polisi Pwani . (picha na Mwamvua Mwinyi) 

    KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

    SERIKALI YAKIWA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA KUTUNZA VIELELEZO VYA MADAWA YA KULEVYA

    0
    0
    Na Ahmed Mahmoud Arusha
    Jaji mstaafu wa makahama kuu Aishieli Sumari Ameitaka serikali kuhakikisha kuwa ina weka mazingira mazuri kwa kupata kinga kwa wale wanaosikiliza kesi katika mahakama nchini kwa kuangalia ni namna gani vielelelzo vinavyotunzwa ili mwisho wa siku kinapofunguliwa kisiwadhuru wahusika ndani ya mahakama.

    Aidha Amewataka majaji nchini kuhakikisha wanatafsiri  Sheria na kuzitolea adhabu zinazoendana na makosa yatakayoonekana kama Adhabu kwa wahusika badala ya kuziona adhabu kama sehemu ya kuondoka eneo moja kwenda jingine na kujikuta wahusika wakitumia fedha za serikali bure kwenye magereza.

    Jaji Sumari ameyasema hayo wakati wa Misa ya Shukran iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheri usharika wa Patandi wilayani Arumeru ambapo alitolea mfano wa Adhabu aliyotoa hivi karibuni kabla ya kustaafu ya Usafirishaji wa Madawa ya Kulevya aina ya Mirungi na kumuhukumu mshtakiwa Kifungo cha maisha.

     Amesema kuwa japo alikuwa akitoa adhabu za kifungo cha maisha na kunyonga kwa kesi moja katika maisha yake ya kasi ila sehemu kubwa ya vifungo hivyo vinaipotezea serikali fedha nyingi kwani naamini kuwa kumfunga mtu maisha ni kumuhamisha mtu sehemu moja akizoea anakuwa anakula bure na kuwa huru kwa kuwa anakuwa ameyazoea mazingira hayo.

    Akagusia kesi ya kifungo cha maisha yaliyoihukumu kabla ya kustaafu kwa kuzungumzia sheria aliyoshitakiwa nayo inasemaje kwa kuwa sheria hii mpya imembana mwamuzi kwani sheria haina mbadala kwani yeye kama jaji haamini katika kutoa adhabu kubwa ndio kutoa adhabu bali hukumu ndio ionyeshe adhabu iliyotolea.

    “Alisema kuwa vielelezo katika kesi za madawa ya kulevya zimekuwa zikichukuwa muda mrefu na kutumia fedha nyingi kwa kuhakiki vielelezo na utunzaji ambapo wakati vielelezo vinapatikana gharama zinakuwa kubwa na kuigharimu serikali”alisema Jaji Sumari.

    Akaitaka serikali kuhakikisha kuwa ina weka mazingira mazuri kwa kupata kinga kwa wale wanaosikiliza kesi hizo kwa kuangalia ni namna gani vielelelzo vinavyotunzwa ili mwisho wa siku kinapofunguliwa kisiwadhuri wahusika ndani ya mahakama.

    Amewataka Mahakimu na majaji wote kusimamia Haki na wajibu sheria katika siku zote kwa kusimama kwenye viapo vyao kwa kutopemndelea upande wowote kwa kuangalia kuwa kiapo hakiishii kwenye siku ile moja kina upana wake na kusimamia sheria inavyosema kwa kusimamia Haki.

    “Sheria na haki zitakaposimamiwa vizuri wananchi wataiona mahakama kama kimbilio lao hivyo nawasihi wenzangu katika kutafisiri sheria waangali viapo vyao kwa kutoa adhabu ambazo wengi wataona adhabu hizo kama kumkomoa mtu bali ni fundisho kwa kuangalia mazingira” alisema Jaji Sumary.
    Jaji mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Moshi akiongea na wanahabari wakati wa Misa ya Shukran iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheri usharika wa Patandi wilayani Arumeru.

    WAFANYAKAZI WAWILI WA TBS WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSABABISHA HASARA ZAIDI YA MIL 977

    0
    0
    Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
    AFISA  Manunuzi  Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula, Mohamedx Mzingi na Mkuu wa Textile Leather wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa miwili likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 977.
    Akisoma hati mashtaka wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Aneth Mavika amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustina Mmbando kuwa kati ya Julai 16 na 30, mwaka 2013 katika ofisi za Makao Makuu ya Hifadhi ya Chakula (NFRA) washtakiwa walitenda kosa.

    Imedaiwa siku ya tukio washtakiwa hao kwa nafasi zao na wakiwa wajumbe wa uthamini wa zabuni walitumia madaraka yao vibaya katika uthamini wa  zabuni namba AE-054/2013/2014/HQ/G/02 Lot namba 01.

    Wakili huyo aliendelea kudai kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakati wakitekeleza majukumu yao ambapo kwa makusudi walipendekeza kampuni ya Bajuka International (T) Ltd ambayo ilikuwa haina sifa kupewa zabuni ambayo haikuendana na matakwa ya kitaalam kama yalivyokuwa kwenye nyaraka za zabuni kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

    Pia washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kutimiza majukumu
    yao kikamilifu na kuisababishia Wakala wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kupata hasara ya Sh milioni 997, 040,000.

    Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo ambayo wanashtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi kwa sababu yaliambatanishwa na kibali cha DPP ambacho kiliipa ridhaa Mahakama hiyo kusikiliza Kesi hiyo na kutoa dhamana.

    Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai  kuwa upelelezi bado haujakamilika.

    Akitoamasharti ya dhamana, Hakimu Mmbando alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini Wakili wanaoaminika ambao kila mdhamini asaini bondi yaSh165 milioni huku mmoja kati ya wadhamini hao ametakiwa kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha Fedha. Pia washtakiwa hao wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria mahakamani.

    Hata hivyo mshtakiwa Mohammed alikamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa huru huku mwenzake Peter alishindwa kuyakamilisha na kupelekwa rumande. Aidha Mahakama imetoa hati ya wito kwa mshtakiwa Edward Mtango ambaye hakuwepo mahakamani wakati wenzake wakisomewa mashtaka.

    Watendaji Mamlaka za Maji Watakiwa Kuimarisha Huduma Wanazotoa kwa Wananchi

    0
    0

       Frank Mvungi- MAELEZO
    Naibu Waziri wa  Maji Mhe. Jumaa Aweso amezitaka Mamlaka za Maji nchini kuhakikisha kuwa zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma ya majisafi na salama katika maeneo yote.
    Akizungumza wakati akifunga Kikao kazi cha siku mbili kwa watendaji wakuu wa Mamlaka za Maji na wahandisi amesema kuwa  wanalo jukumu kubwa la kutekeleza majukumu yote kwa weledi na kuimarisha huduma za maji kwa wananchi.
    “ Kwa yoyote atakayejaribu kuturudisha nyuma katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano hatutaweza kumvumilia kwa namna yoyote zaidi yakumuweka pembeni “; Alisisitiza Aweso
    Akifafanua Aweso amesema kuwa watendaji hao wanatakiwa kuhakikisha kuwa sekta  ya maji inachochea maendeleo na ustawi wa wananchi.
    Pia alizitaka Mamlaka za maji kutangaza miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuonesha juhudi zilizochukuliwa na Serikali katika kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi kote nchini.
    Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa sekta ya maji ina mchango mkubwa katika kutekeleza dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda inayosisitizwa na Serikali  ya Awamu ya Tano.
    Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa Mamlaka za maji kutekeleza miradi ya maji kwa kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuchochea  ukuaji wa uchumi wa viwanda  na kusaidia katika kukuza ajira.
    Kikao Kazi cha Watendaji wakuu wa Mamlaka za maji na wahandisi wa mikoa kimefanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili kikilenga kuimarisha huduma hiyo katika maeneo yote hapa nchini.
     Naibu Waziri wa Maji Mhe.  Jumaa   Aweso akisisitiza Watendaji wa Mamlaka za Maji kuwajibika  kuimarisha huduma zinazotolewa kwa wananchi ili kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza huduma Bora kwa wananchi wote.hiyo ilikuwa tarehe 8 Novemba, 2018 wakati  wa kufunga kikao kazi hicho Jijini Dodoma.
     Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akizungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha kuwa huduma ya maji inaimarishwa katika maeneo yote hapa nchini. hiyo ilikuwa tarehe 8 Novemba, 2018 wakati  wa kufunga kikao kazi hicho Jijini Dodoma.

    Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha siku mbili kilichowashirikisha  Watendaji Wakuu wa Mamlaka za Maji, Wahandisi wa Maji wa mikoa yaliyofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma.

    (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

    VYAMA 14 VYAJITOKEZA KUGOMBEA UDIWANI, UBUNGE

    0
    0
    Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa jumla ya wagombea 13  walichukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Majimbo ya Babati Mjini, Ukerewe, Simanjiro na Serengeti.

    Akizungumza  ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu uteuzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Giveness Aswile amesema kuwa,  wagombea  hao wanatoka katika vyama sita vya siasa ambavyo ni AFP, CCM, CUF, NCCR Mageuzi, NRA na UDP.

    Amesema kuwa, hadi muda wa mwisho wa uteuzi Novemba 02, mwaka huu saa 10:00 jioni, jumla ya wagombea wane wa Ubunge kutoka CCM, waliteuliwa na hivyo kutangazwa kuwa wamepita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

    Wagombea hao walitangazwa kupita bila kupinga baada ya wanachama wengine kutoka vyama vilivyochukua fomu za uteuzi, kukosa sifa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kushindwa kurudisha fomu hizo kwa wakati na wengine kutojaza fomu hizo kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutojaza fomu ya kuheshimu na kuyazingatia maaadili ya uchaguzi

     Aidha kwa upande wa udiwani katika kata 47 za Tanzania Bara, Aswile ameeleza kuwa, vyama 14 vya siasa vilishiriki ambapo wanachama 102 kutoka vyama hicvyo walichukua fomu za uteuzi.

    “Vyama vilivyoshiriki ni AAFP, ACT – WAZALENDO, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CUF, DEMOKRASIA MAKINI, NCCR – Mageuzi, NRA, SAU, TLP, UDP na UPDP” alisema Aswile na kufafanua kuwa,

     Hadi Novemba 03, 2018 saa 10:00 jioni wanachama 73 tu ndio waliorejesha fomu na kuteuliwa kuwa wagombea Udiwani.

     Wanachama wengine 29 hawakuteuliwa kuwa wagombea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kurejesha fomu za uteuzi, kutojaza fomu za uteuzi kwa usahihi, kutosaini fomu za kuheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi na kukosa sifa za kugombea udiwani kwa mujibu wa sheria.

    KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

    Ni vita ya Wababe wikendi hii kwenye Bundesliga

    0
    0
    Kwa wapenzi wa soka kote duniani hakuna raha kama kuona timu mbili kubwa zikivaana Uso kwa Uso tena zikiwa na mashabiki lukuki. Miongoni mwa mechi za kusisimua sana katika Ulimwengu wa soka ni ile ya watani wa jadi wawili nchini Ujerumani, ni miamba wa jiji la Dortmund na wababe wa jiji la Munich. Borussia Dortmund vs Bayern Munich na Der Klassiker ndio jina halali la mchezo huo.
    Dortmund ambao wanaongoza ligi watakuwa nyumbani katika dimba la Signal Iduna Park Jumamosi hii tar 10, majira ya 2:30 saa za Afrika Mashariki, kuwakabili mabingwa wa ligi hiyo  msimu uliopita Bayern Munich.
    Mpaka sasa Dortmund hawajapoteza mchezo wowote katika Bundesliga msimu huu huku Bayern wao wakiwa wameshapoteza michezo miwili hadi sasa. Pia Dortmund waliambulia vipigo katika mechi tatu zilizopita za Der Klassiker, lakini wikendi hii wanayo nafasi ya kubadilisha  bahati yao kwani wanacheza kandanda safi msimu huu huku wapinzani wakionesha kutowepo katika kiwango kilichozoeleka kwa miaka kadhaa sasa.

    Kwa wapenzi wa Soka hapa nchini mchezo huu utakuwa MUBASHARA kupitia chaneli ya ST World Football ndani ya king’amuzi cha StarTimes ambao ndio warushaji pekee wa ligi hiyo yenye kasi zaidi barani Ulaya.
    Kuchagiza burudani hiyo mtazamaji ana nafasi ya kuchagua kupata uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi cha StarTimes kwenye luninga yake ili kuongeza umakini wa ufatiliaji wa mchezo huo.

    Ligi ya Bundesliga inapatikana kwa urahisi  sana ambapo mteja wa StarTimes atatakiwa kulipia kifurushi cha MAMBO kama anatumia kisimbuzi cha Antenna kwa Tsh 14,000 tu, na kwa watumiaji wa Visimbuzi vya Dish ni kifurushi cha SMART ambacho kinapatikana kwa Tsh 21,000 tu.
    Mbali na ligi ya Bundesliga, StarTimes wanaonyesha ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, UEFA EUROPA league na Coppa Italia ambazo hupatikana katika chaneli zao za michezo kwa kiwango cha HD (High Definiton).
    Viewing all 109589 articles
    Browse latest View live




    Latest Images