Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA

$
0
0
NA ELISA SHUNDA,KIBAHA.

KONGAMANO la Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Iimetoka na Azimio la Pamoja la Wazazi katika Jamii Husika Kuhakikisha Inasimamia Maadili ya Vijana kwa Kuwa Chanzo cha Mmomonyoko wa Maadili Unaanzia kwenye vitongoji na mitaa ambako familia zao ndipo zinapoishi.

Maadili ni Mjumuisho wa Tabia Watu Zinazokubalika Mahali Fulani au Katika Jamii Fulani au Jumuiya Fulani au Nchi, Mjumuisho wa Tabia za Watu Unatokana na Kujumuisha Tabiaza Mtu mmoja Mmoja Tabia Hizi Ndizo Zinatufikisha Kule Tunapokuthamini.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda,alisema kuwa kwa mjumuisho wa kongamano hilo lililoshirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali,wananchi na wanachama wa CCM imeazimia kwa pamoja kuwa mmomonyoko wa vijana katika maadili yao inatokana na malezi ya wazazi lakini pia katika mitaa na vitongoji ambavyo vijana hao wanatokea hakuna malezi ya pamoja ya wazazi kwa vijana wa sehemu husika kwa kuogopa lawama kwa wazazi wa motto au watoto waliovunja hayo maadili.

“Katika majadiliano yaliyofanyika leo katika kongamano hili la maadili wajumbe wengi na wadau mbalimbali wamesema sababu kubwa inayochangia kupolomoka kwa maadili kwa watoto wetu ni wazazi sisi kwa sisi wenyewe kuogopana kuwa huyu mtoto siyo wangu ukimuadhibu au kumkanya kwa kosa ulilomkuta nalo kwa hali ya sasa unaweza ukanunua ugomvi kwa familia ya mtoto aliyefanya kosa hivyo kupitia kongamano hili tumeazimia kwa pamoja tunapotoka hapa tunaanzisha mabaraza ya jamii yatakayoanzishwa kwenye vijiji na mitaa kwa ajili ya kusimamia malezi na maadili ya watoto wetu” Alisema Mwenyekiti Shunda.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda (katikati) akizungumza katika Kongamano la Maadili lililokuwa likijadili mmomonyoko wa maadili ya vijana yaliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Elimu Kibaha jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo,Mwalimu Charles Maguye na Katibu wa Jumuiya Hiyo,Ruth Rutashiba. Picha na Elisa Shunda

 Wajumbe na wanachama wa Chama Hicho wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU SABA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro tayari kwa ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Anna Mghwira akisoma taarifa ya Mkoa mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TAZAMA MIRADI YA USHIRIKIANO BAINA YA SERIKALI YA TANZANIA NA JAMHURI YA WATU WA CHINA

MAHAKAMA YAAMURU MBOWE NA MATIKO WAKAMATWE

$
0
0


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kumkamatwa kwa Mwenyekiti Wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge Wa Tarime Mjini, Esther Matiko ili waje kujieleza kwa nini wasifutiwe dhamana zao baada ya kukiuka masharti ya dhamana

Amri hiyo imetolewa leo Novemba 8.2018 na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya Awali (PH).

Akitoa uamuzi huo Hakimu Mashauri amesema, Novemba Mosi mwaka huu, Mdhamini wa mshtakiwa Mbowe, alifika mahakamani hapo na kudai kuwa, mshtakiwa amepelekwa South Afrika kutibiwa akiwa Mahututi na Mahakama iliamuru leo (siku ya kesi) alete taarifa kuhusu kuumwa kwake lakini hajaleta na badala yake amefika na kudai kuwa mshtakiwa yuko Dubai.

"Hii inaonesha kuwa, mdhamini huyu wa mshtakiwa Mbowe siyo muaminifu", amesema hakimu Mashauri.Pia kuhusu Mshtakiwa Matiko Hakimu Mashauri amesema kitendo cha mshtakiwa Matiko kusafiri nje ya nchi bila ridhaa ya Mahakama wala Polisi wanapotakiwa kuripoti kama masharti ya dhamana yanavyowataka ni matumizi mabaya ya haki yake ya dhamana.

Kutokana na sababu hizo mahakama inaamuru mshtakiwa Mbowe na Matiko wakamatwe na kufikishwa mahakamani hapo ili kujieleza kwanini wasifutiwe dhamana zao" amesema Mashauri.Awali kabla ya amri hiyo Wakili Nchimbi, alihoji kwanini  Mbowe na Matiko hawapo mahakamani.

Mdhamini wa Mbowe alisimama na kueieleza mahakama kwamba Mbowe yupo Dubai kwa ajili ya matibabu na hajawahi kusema kwamba yupo Afrika Kusini."Nimeongea naye moja kwa moja yupo nchini Dubai,"ameeleza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

SPIKA WA BUNGE AZINDUA KIKUNDI CHA WABUNGE CHA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati akizundua Kikundi cha Wabunge cha Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Jijini Dodoma.
Katibu wa Kikundi cha Wabuge wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Mhe. Salome Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wabuge wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Mhe. Augustine Vuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge katika picha ya pamoja na Kikundi cha Wabunge kinachojishughulisha na Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Jijini Dodoma.
PICHA NA BUNGE

CHIRWA ASAINI RASMI AZAM, AAHIDI KUIFANYIA MAKUBWA AZAM

$
0
0
Na Agness Francis, Globu   ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya soka ya Azam fc umefanikiwa  kuinasa saini ya mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Ni baada ya dili lake la kurudi Yanga kugonga mwamba.

Uongozi  wa Azam FC umesema kuwa usajili wa Chirwa ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam chini ya kocha mkuu Hans Van der Plujim katika kuboresha eneo la ushambuliaji la  kikosi hicho. 

Chirwa amejiunga na Azam baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri ambayo alisajiliwa hivi karibuni.Mshambuliaji huyo ametua Azam akiwa ameshawahi pia kuichezea Yanga na kisha baadaye kukimbilia huko Uarabuni baada ya mambo ya kifedha na mabingwa hao wa kihistoria kutokuwa sawa.

Baada ya kurejea nchini, awali ilielezwa Chirwa angeweza kurudi Yanga lakini mambo yamekwenda tofauti.Kupitia ukurasa wa Istagram wa klabu ya Yanga,  Uongozi huo umebainisha  kuwa awali mshambuliaji  huyo alikuwa arejee klabuni  licha ya kocha mkuu wa  klabu hiyo mwinyi Zakhera kupinga usajiri wake."Kilichomkwamisha Chirwa kurudi Jangwani ni dau la mshahara alilotaka kulipwa alitaja kiasi kikubwa  cha fedha ambacho Yanga hawakukubali"

Licha ya Octoba 20  mwaka huu Chirwa  alionekana  uwanja wa Taifa katika uchezo uliopigwa na Yanga dhidi ya Alliance  akiwa na kaimu katibu Mkuu wa Yanga Omary  Kaya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Husein Nyika na Mdau mkubwa  Yanga  Abbas Tarimba, ambapo pia aliingia vyumba vya kubadilishia nguo na kusalimiana na wachezaji wa Yanga

Chirwa sasa ataanza rasmi kuitumikia Azam kuanzia Novemba 15 2018 ambapo dirisha dogo la usajili litakuwa limeshafunguliwa.Na baada ya kutambulishwa, Chirwa amesema kwamba amejiunga na Azam FC kukiongezea nguvu kikosi ambacho tayari ni bora ili wafanikishe azam ya kutwaa mataji.Kwa upande wake, kocha Pluijm ambaye alifanya kazi na Chirwa katika klabu ya Yanga, alisema kwamba  amefurahi sana kumpata mchezaji huyo anayejituma na mwenye bidii kubwa uwanjani.

Chirwa sasa anakwenda kukutana na mshambuliaji raia wa Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliyewahi kufanya naye kazi FC Platinums ya Zimbabwe na Yanga.Kama ilivyokuwa Yanga, Ngoma alianza kuja na baadaye akamvuta Chirwa akimshawishi Pluijm aje kuongeza nguvu na kwa Azam hivyo pia, inaaminika Donald amemshawishi tena Pluijm kumsajili mchezaji huyo. .
Mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa akikabidhiwa Jezi ya timu ya Azam fc na Kocha Mkuu wa Kikosi hicho Hans Van De Plujim mara baada ya kusaini kandarasi za kutumikia  klabu hiyo  kwa mwaka mmoja leo Jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MADAKTARI BINGWA WA MOYO TOKA ISRAEL NA MAREKANI

NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA CHANZO CHA MMOMONYOKO WA MAADILI UNAANZIA KWENYE VITONGOJI NA MITAA

$
0
0
NA ELISA SHUNDA,KIBAHA
KONGAMANO la Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Iimetoka na Azimio la Pamoja la Wazazi katika Jamii Husika Kuhakikisha Inasimamia Maadili ya Vijana kwa Kuwa Chanzo cha Mmomonyoko wa Maadili Unaanzia kwenye vitongoji na mitaa ambako familia zao ndipo zinapoishi.

Maadili ni Mjumuisho wa Tabia Watu Zinazokubalika Mahali Fulani au Katika Jamii Fulani au Jumuiya Fulani au Nchi, Mjumuisho wa Tabia za Watu Unatokana na Kujumuisha Tabiaza Mtu mmoja Mmoja Tabia Hizi Ndizo Zinatufikisha Kule Tunapokuthamini.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda,alisema kuwa kwa mjumuisho wa kongamano hilo lililoshirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali,wananchi na wanachama wa CCM imeazimia kwa pamoja kuwa mmomonyoko wa vijana katika maadili yao inatokana na malezi ya wazazi lakini pia katika mitaa na vitongoji ambavyo vijana hao wanatokea hakuna malezi ya pamoja ya wazazi kwa vijana wa sehemu husika kwa kuogopa lawama kwa wazazi wa motto au watoto waliovunja hayo maadili.

“Katika majadiliano yaliyofanyika leo katika kongamano hili la maadili wajumbe wengi na wadau mbalimbali wamesema sababu kubwa inayochangia kupolomoka kwa maadili kwa watoto wetu ni wazazi sisi kwa sisi wenyewe kuogopana kuwa huyu mtoto siyo wangu ukimuadhibu au kumkanya kwa kosa ulilomkuta nalo kwa hali ya sasa unaweza ukanunua ugomvi kwa familia ya mtoto aliyefanya kosa hivyo kupitia kongamano hili tumeazimia kwa pamoja tunapotoka hapa tunaanzisha mabaraza ya jamii yatakayoanzishwa kwenye vijiji na mitaa kwa ajili ya kusimamia malezi na maadili ya watoto wetu” Alisema Mwenyekiti Shunda.

Aliongeza kwa kusema maazimio hayo pia yameitaka jumuiya ya wazazi itoe maelekezo kwa mwenyekiti wa halmashauri na katibu wa baraza la madiwani ni wajumbe basi wapewe maagizo hayo ili kwa utaratibu ulio sahihi maazimio hayo yawasilishwe kwenye halmashauri ya wilaya na wao kwa utaratibu wa uanzishwaji wa sheria ndogo juu ya uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza hayo ya jamii.

“Kutokana na Tulichokijadili katika Kongamano pia mabaraza hayo yataanzisha na kutekeleza dhana ya uwajibikaji wa kijamii badala ya jamii kuilaumu serikali na vyombo vya dola jamii kwa pamoja itahakikisha inasimamia majumba ya starehe hayajengwi jirani na makazi ya watu ili kuwatenga watoto na majumba hayo,watoto chini ya umri wa miaka 18 hawaingii kabisa kwenye majumba ya starehe,udhibiti wa mabanda ya video mitaani katika kusimamia kwa usiri filamu zinazoonyeshwa zisiwe za kuvunja maadili kwa vijana hao ambapo athari yake ni kubwa sana;

“Udhibiti wa sherehe mbalimbali za kijamii zitakazokuwa na sura ya kuchochea mmomonyoko wa maadili kwa vijana pamoja na utoaji wa vibali vya kufanyia shughuli hiyo,pia jamii ndio itakayokuwa ikiongoza serikali katika mtaa na vijiji chake katika kushughulikia matatizo ya sehemu husika pindi yanapotokea siyo kuwaachia wenyeviti na wajumbe kushughulikia tatizo hilo badala yake kwa pamoja watashirikiana kulitatua changamoto iliyojitokeza” Alisema Mwenyekiti Shunda.

Pia Mwenyekiti huyo alisema kuwa maazimio waliyopewa katika kongamano hilo ni uongozi wa jumuiya ya wazazi ihakikishe kuwa ajenda ya mahudhurio ya wananchi kwenye mikutano mikuu ya mitaa na vijiji inasimamiwa kimkakati ili wahudhurie kwa wingi ili wapate kujadili kero zao na pia halmashauri ihakikishe wale watakaopata huduma za jamii mbalimbali kama vile mikopo ya vijana wawe ni wale walioanzisha ajenda hiyo kwa kuhudhuria kwenye mikutano ya mitaa na vijiji ambao watakaokuwa wameorodheshwa kwenye madaftari ya mitaa na vijiji na kutoa taarifa za maendeleo kwenye mikutano ya mitaa,Hii Itahusu vilevile uanzishwaji wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali vianzie kwenye mikutano ili iwe mvuto kwa vijana kuhudhuria kwenye mikutano ili kuwasaidia vijana hao kupokea ushauri kutoka kwa wazazi wao,kuchangia na kutoa mawazo yao kwa jamii husika inayowazunguka.

Mwenyekiti Shunda Alimaliza kwa Kusema kuwa Kongamano limeshauri kuwe na utaratibu makini wa ufuatiliaji wa karibu wa maadili ya watanzania inawezekana kurekebishika na wananchi wakaishi kwa heshima,wananchi wakiwezeshwa kwa kujengewa stadi za uwajibikaji wa kijamii wataweza kuendesha mambo yao wenyewe na kuyasimamia bila kuhitaji nguvu nyingi kutoka ndani au nje ya nchi,hii itapelekea kujenga wazalendo wa kweli wa nchi hii na wakasiamama kama taifa lenye uwezo wa kujenga nchi katika misingi ya ujamaa na kujitegemea kama ilivyo kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda (katikati) akizungumza katika Kongamano la Maadili lililokuwa likijadili mmomonyoko wa maadili ya vijana yaliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Elimu Kibaha jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo,Mwalimu Charles Maguye na Katibu wa Jumuiya Hiyo,Ruth Rutashiba. Picha na Elisa Shunda

 Wajumbe na wanachama wa Chama Hicho wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo.

VODACOM KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA M-PAWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KAMPUNI ya Vodacom kwa kishirikiana na benki ya Commercial Bank of Afrika (CBA) wametangaza rasmi kampeni ya shinda na M -pawa itakayowasaidia wateja kujishindia zawadi kemkem.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa benki ya CBA, Mkuu wa kitengo cha masoko wa benki hiyo Julius Konyani amesema kuwa wateja watakaoweka amana, kukopa na kulipa kwa wakati ndani ya wiki 6 kuanzia Novemba 1 watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali. 

Amesema kuwa wateja 200 watakaopatika ndani ya wiki 6 ambao huweka amana katika akaunti zao za M-pawa watashinda mara mbili ya amana walizoweka.Aidha amesema kuwa wateja 15 wanaokopa na kulipa kwa wakati watazawadiwa kiasi cha shilingi laki moja na kwa wiki 6 jumla ya wateja 96 watanufaika na zawadi hizo.

Konyani amesema kuwa droo kubwa itakayochezeshwa mwishoni kabisa jumla ya zawadi zenye thamani ya shilingi milioni 100 zitatolewa, na hizo ni pamoja na bajaji tano zitakazotolewa kwa wateja watano ambao hukopa na kulipa kwa wakati kupitia M-pawa na mteja wa jumla atapata zawadi nono ya shilingi milioni 10.

Kwa upande wake Meneja masoko wa kampuni ya Vodacom Noel Mazoya amesema kuwa wao na washirika wao ambao ni benki ya CBA wataendelea kuleta karibu huduma za kijamii kwa mfumo wa kidigitali.Amesema kuwa hadi sasa wamewafikia zaidi ya wateja milioni 7 ambao wanatumia huduma ya Mpawa katika kuweka faida na kukopa na kwa usalama zaidi.

Mazoya amesema kuwa wateja wa Vodacom waendelee kutumia huduma hiyo ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa na kampuni hiyo.
Meneja Masoko wa Vodacom,Noel Mazoya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wateja wa mtandao huo waendele kutumia ili waweze kunufaika na zawadi zinazotolewa.kulia ni Mwakilishi wa Meneja wa CBA,Julius Konyani (Picha na Emmanuel Massaka MMG).
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa CBA,Julius Konyani wa (kwanza kulia) akishangilia mara baada ya kupatikana ya mshindi katika droo iliyochezeshwa leo jiji Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WAPYA WA UAE, CANADA NA SPAIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na  Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na  Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na  Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018. Picha na Ikulu

RC Wangabo asisitiza upandaji miti kuzuia maafa huku wa mabondeni wakiamuliwa kuhama

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Joachim Wangabo amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kuhakikisha wanatekeleza sheria ya upandaji miti kwa kila nyumba ili iwe ngao dhidi ya upepo mkali unaosababisha maafa na kuwafanya wanachi hao kukosa mahala salama pa kukaa na wengine kuharibikiwa na vyombo vyao.

Ameyasema hayo alipokwenda kuwatembelea walioathiriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyoezua paa za nyumba zipatazo 27 na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 26 katika Tarafa ya kirando, Wilayani Nkasi.

“DC tuwe wakali katika hili, kuhakikisha kwamba nyumba ambayo haina miti inayozunguka lile eneo la makazi tuhakikishe kwamba tunachukua hatua stahiki za mazingira, halmashauri mnajua hata kwenye vibali vya ujenzi huwa mnasema lazima muwe na miti angalau minne kama sio mitano lakini hakuna anaefuatilia kwamba hiyo miti ipo? Sadsa ni wakati muafaka wa kufuatilia taratibu zote,” alisisitiza.

Wangabo aliongeza kuwa wale wote waliojenga kwenye mabonde ya mpunga wajue kwamba maeneo hayo si salama na kama watapatwa na maafa yoyote wasiitegemee serikali kuwahudumia kwasababu serikali imeshatoa onyo juu ya uhatari wa makazi hayo na kuwataka wananchi wasiishi kwenye maeneo hatarishi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda amesema kuwa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi inaendelea kutoa elimu ya ujenzi wa nyumba bora na katika kuhakikisha jambo hilo linatekelezwa kamati za ujenzi za vijiji zinaendelea kuundwa katika kila kijiji ikimabatana na jukumu la kuhamasisha upandaji wa miti.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyenyoosha kidole) akionyesha moja ya nyumba zilizoathirika na upepo mkali na mvua kubwa zilizonyesha mapema mwezi huu katika kijiji cha Kichangani, kata ya kirando Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa, alipokwenda kutoa pole kwa waathirika hao. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiingia katika moja ya nyumba zilizoathiriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua pamema mwezi huu katika kijiji cha Kichangani, kata ya kirando Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa.
 Miongoni mwa nyumba zilizoathiriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua pamema mwezi huu katika kijiji cha Kirando, kata ya kirando Wilayani Nkasi, Mkoani Rukwa.

NEWS ALERT: RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA ALPHAYO J. KADATA

Ecobank Tanzania Limited yakutana na wateja wao jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza na wateja wa  Ecobank  wakati wa hafla ya kuongea na wateja lengo ikiwa ni kukutana na wateja wao kuwasikiliza ili kuboresha huduma, ufanisi pamoja na kuwa karibu zaidi na wateja wao wakati wa siku ya wateja wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha biashara Ecobank Tanzania Respige Kimati akiwasilisha mada kwa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla iliyowakutanisha wateja mbalimbali wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Mkuu wa kitengo cha Kidigitali Ecobank Tanzania, Filemon Tesha akiwasilisha mada mada kuhusu utumiaji wa benki hiyo kwa njia ya kidigitali wakati wa hafla iliyowakutanisha wateja mbalimbali wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akiwa kwenye picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla iliyowakutanisha wateja mbalimbali wa benki hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wateja pamoja na wafnayakazi wa benki ya Ecobank  wakiwa kwenye hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wao ili kutambua  mchango wao katika benki hiyo.

ACP ABDI ISANGO AWAPA SOMO MADEREVA JUU YA USALAMA BARABARANI NA KUPIMA AFYA KATIKA KITUO CHA NORTH STAR ALLIANCE (KURASINI) , JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, anamuwakilisha kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani Taifa akizindua rasmi shughuli hizo za upimaji wa afya kwa madereva wasafirishao mizigo masafa ya mbali iliyoandaliwa na North Star alliance kwa kushirikiana na Puma Energy Foundation , Impala Terminals na Trafigura Foundation.
Ndg. Henry Mgala Bantu mtaalam wa usafirishaji na uchukuzi na mbobezi wa usalama barabarani na Mjumbe wa Balaza la taifa la usalama barabarani na mwenyekiti wa elimu mafunzo na uenezi katika balaza hilo, akiwakumbusha madereva mambo mbalimbali muhimu yahusuyo Sheria za barabarani na somo muhimu la madereva kujitambua.
Mrakibu Msaidizi  wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania, akiendesha chemshabongo fupi kwa madereva wa magari ya mizigo yaendayo safari ndefu lengo ni kuwakumbusha tu kuendelea kuwa makini pindi wawapo safarini.
Mrakibu  Msaidizi wa Polisi Yoronimo Kwesibaga Saimon Mkuu wa kituo cha Polisi Bandari, akitoa salam zake wakati wa wiki ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya barabarani.
Madereva pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika wiki ya kuelekea siku ya Usalama na Afya barabarani katika viwanja vya Impala Terminals. 

MICHUZI TV: Mh.Mwita Waitara atoa kauli hii Bungeni baada ya kuhamia CCM.


MICHUZI TV: SABAHA MUCHACHO KUNOGESHA UZINDUZI ALBAM YA MAMA WA HIARI YA AMIGO

MICHUZI TV: WABUNGE WAPYA WAONGEA BAADA YA KUAPA BUNGENI DODOMA

MICHUZI TV: CHEKA UNENEPE - Mwizi KONKI na mjanja

MICHUZI TV: WANANCHI WA DAR NENDENI KWENYE WILAYA ZENU KUCHUKUA VITAMBULISHO - NIDA

MICHUZI TV: KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA DOTTO JAMES AIPONGEZA BENKI YA CRDB

Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images