Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

ARUSHA KUJA NA VITUO 4 MAALUMU VYA POLISI VILIVYOGHARIMU ZAIDI YA MIL. 80

0
0
Na Vero Ignatus, Arusha.

Kikao cha Sekta ya wadau wa Utalii kimefanyika Mkoani Arusha kikiwa na lengo la kuona namna wanatekeleza azimio la kusimika vituo vinne Maalum vya Polisi kwa ajili ya Ukaguzi wa magari yanayosafirisha watalii.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ambapo Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo amesisitiza azma yake katika kuhakikisha utalii unatengenezewa mazingira mazuri ya ukuaji.“Hakuna kitu kinatupa sifa mbaya kwa wageni kama kusimamishwa na askari kila baada ya kilomita moja''alisema Gambo

Amesema Vituo hivyo maalum vya ukaguzi vitasaidia kuondokana na changamoto hiyo kwakuwa sekta ya utalii inategemewa sana katika kuliingizia taifa pato ."Magari yote yatakua na vituo maalum vya ukaguzi, tunafanya yote haya kwakua sekta ya utalii tunaitegemea sana kama taifa kwa kutuingizia pato la taifa.” Alisema Gambo.

Vituo hivyo vinne vinavyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 80 vimetengenezwa kwa michango ya wafanyabiashara ya Utalii TATO na vinatarajiwa kuwekwa katika maeneo ya Kikatiti, Ngaramtoni, Makuyuni na Karatu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Mdau wa Sekta ya Utalii wakitoa maoni yao juu ya zoezi la uwekaji wa vituo maalum vya polisi.
 

Kutoka kushoto ni mhifadhi mkuu wa mamlaka ya Ngorongoro Dkt. Fredy Manongi akifuatiwa na Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Alan Kijazi
Wamiliki wa makampuni ya Utalii wakifuatilia mjadala wa kuweka vituo maalumu vya polisi mkoani Arusha.


HOJA ZA KAMATI ZA BUNGE ZA PAC NA NUU, ZAJADILIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kulia) akiongoza kikao cha Watendaji Wakuu wa Wizara yake, cha kujadili hoja zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam leo.
PIX 2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) akitaka ufafanuzi kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike, katika kikao cha Watendaji Wakuu wa Wizara yake, cha kujadili hoja zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam leo.
PIX 3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati) akiongoza kikao cha Watendaji Wakuu wa Wizara yake, cha kujadili hoja zilizotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi.

NGARIBA WABADILI MBINU ZA UKEKETAJI

0
0

Na Mwandishi Wetu Manyara. 

Mangariba nchini wamebuni njia mpya za kuendeleza vitendo vya ukeketaji nchini kwa kutofanya sherehe wakati wa ukeketaji lakini pia kukeketa watoto wachanga na kufanya vitendo ua ukeketaji nyakati za usiku. 

Hayo yamesemwa Wilayani Babati Mkoani Manyara na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizindua Kamati za Ulinzi kwa Wanawanke na Watoto kwa mkoa wa Manyara. 

Naibu Waziri Ndugulile amesema kuwa kuanzia Januari mpaka Septemba 2017 jumla ya vitendo 41,000 vya ukatili viliripotiwa na jeshi polisi nchini akifafanua kuwa kama takwimu hizi zingekuwa za ujambazi katika mkoa mmoja hali ya wananchi ingekuwa mbaya sana huku akiviita vitendo hivyo na ujambazi katika sura mpya. Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imejipanga kutokomeza vitendo vya Ukeketaji kwa kuanzisha Mpango Mkakati wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2016/2017 utakaoisha mwaka 2021/2022. 

Dkt. Ndugulile amesema kuwa kwa mujibu wa Takwimu inaonyesha Mkoani wa Manyara una Asilimia 27 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo nguvu inahitajika sana katika kupambana na vitendo hivyo akiitaka kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuweka suala hilo katika mipango yao ili kudhibiti ukatili huo. 

Naibu Waziri Ndugulile amewataka wajumbe wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na Watoto aliyoizindua jana mkoani humo kusoma na kuelewa majukumu yao kama ilivyabainishwa katiaka mkakati wa MTAKUWA kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Mkoani Manyara. 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Kaimu Katibu Tawala wa MKoa wa Mnyara Bw. Anza-Amen Ndossa wakionesha Wajumbe wa Kamati ya Dawati la Ulinzi wa Wanawake na Watoto Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MATAKUWA) mara baada ya kuzindua kamati ya hiyo ya Mkoa jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa Manyara.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kuzindua Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa Manyara pembeni yake ni KaimuKatibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Anza-Amen .Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

Dira ya Kitaa na Tabia za wajomba kutoka Dar

WAZIRI MKUU AFUNGA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA MKOA WA PWANI

0
0
 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Masoko wa kampuni ya Chumi 'Neel Salt', Vivian Stephan, wakati alipofika Uwanja wa Sabasaba Picha ya Ndege Mkoa wa Pwani jana kwa ajili ya kufunga maonesho ya Wiki ya Viwanda.
 WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi, Cyprian Luhemeja, wakati alipofika Uwanja wa Sabasaba Picha ya Ndege Mkoa wa Pwani jana kwa ajili ya kufunga maonesho ya Wiki ya Viwanda
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Utawala wa kampuni ya Terra inayobangua Korosho, Peter Christopher, wakati alipofika Uwanja wa Sabasaba Picha ya Ndege Mkoa wa Pwani jana kwa ajili ya kufunga maonesho ya Wiki ya Viwanda. (Picha na Muhidin Sufiani)


Mamia wajitokeza kupima tezi dume Muhimbili tawi la Mloganzila

0
0
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya zoezi la kupima bure tezi dume (prostate) na mfumo wa njia ya mkojo kwa kutumia ultrasound.

Zoezi hilo limeandaliwa na Hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Matumizi ya Mionzi katika uchunguzi na Tiba Tanzania (TARA) ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya wataalam wa mionzi tiba duniani.

Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia, Dkt. Lulu Sakafu amesema umri unavyozidi kwenda juu, wanaume wanakuwa katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, hivyo wameshauriwa kujenga utamaduni kwa kupima afya zao mara kwa mara.Amesema watu wasiofanya mazoezi wako katika hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, wanaume wanaopenda kula chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta na wengine wanaweza pata ugonjwa huo kutokana na historia ya familia zao.

“Katika maadhimisho ya mwaka huu tumeamua kupima tezi dume kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 ili kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa huu kwa sababu kansa ya tezi dume duniani inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo kwa wanaume kutokana na saratani ya tezi dume,” amesema Dkt. Sakafu.

Akizungumzia dalili za tezi dume, Dkt. Sakafu amesema kuwa kupata shida wakati wa haja ndogo, kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza haja ndogo, kujisaidia mkojo wenye mtiririko dhaifu, kukojoa mara kwa mara nyakati za usiku na kujikamua wakati wa kujisaidia na kushindwa kumali mkojo wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo amesema wanaume wasiogope kujitokeza kupima tezi dume kwa kuwa hivi sasa inatumika njia nyingine ya ultrasound badala ya ile ya zamani ya vidole.Naye Rais wa TARA, Stephen Mkoloma ambaye ni mtaalam wa radiolojia amesema wamechangua kupima tezi dume kwa kuwa takwimu za wagonjwa wanaoripotiwa hospitali kutokana na matatizo ya tezi dume imeongezeka.

“Nawashauri watu kupima afya zao mara kwa mara ili kujua afya zao mapema kwani ukigundua ugonjwa mapema gharama za matibabu zinakuwa chini kuliko kusubiri ugonjwa unapokuwa mkubwa au sugu,” amesema Mkoloma.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam akipima tezi dume katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Kulia ni mtaalam wa radiolojia, Burhani Abdul akimpima tezi dume kwa kutumia Utrasound.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakisubiri kupima tezi dume katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Rais wa Chama cha Wataalam wa Matumizi ya Mionzi katika uchunguzi na Tiba Tanzania (TARA), Stephen Mkoloma akitoa elimu kwa wanaume kuhusu tezi dume ikiwamo sababu, dalili na jinsi ya kujikinga.
Pichani ni Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa

Tume ya maadili yatoa zawadi kwa wanafunzi wa klabu za Maadili walioshinda katika uandishi wa insha na uchoraji wa katuni

0
0

Kamishna wa Maadili Jaji Harold Nsekela katikati (mwenye miwani), Katibu Ukuzaji wa Maadili toka Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha na Katibu Msaidizi Kanda ya Pwani Getrude Cyliacua wakitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika uandishi wa insha wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa klabu za Maadili walioshinda katika uandishi iwa insha na uchoraji wa katuni. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa IEC, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.

 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Morogoro Noela Conradi (Kushoto) na Zainabu Hamisi (kulia) wakijadili mada ya mgongano wa maslahi kwa viongozi wa umma mbele ya Kamishna wa Maadili Jaji (Mst) Harold Nsekela (aliyekaa mwenye miwani) wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa klabu za Maadili walioshinda katika uandishi wa insha na uchoraji wa katuni. 


Kulia kwake ni Katibu Msaidizi Kanda ya Pwani Bi. Getrude Cyliacua na kushono ni Katibu Ukuzaji wa Maadili toka Sekretarieti iya Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa IEC, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
 Kamishna wa Maadili Jaji Harold Nsekela katikati (mwenye miwani), Katibu Ukuzaji wa Maadili toka Sekretarieti ya maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha na Katibu Msaidizi Kanda ya Pwani Getrude Cyliacua wakiimba wimbo wa Tanzania nakupenda wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa klabu za Maadili walioshinda katika uandishi iwa insha na uchoraji wa katuni. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa IEC, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.


 Wanafunzi wa Klabu za maadili wa manispaa ya Morogoro ya wakiimba wimbo wa Tanzania nakupenda wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa klabu za Maadili walioshinda katika uandishi wa insha na uchoraji wa katuni. Hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa IEC, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.

NEWZ ALERT: WATU SABA WAPOTEZA MAISHA AJALI YA CHALINZE MKOANI DODOMA

0
0
Watu saba waliokuwa wakisafiri katika gari STL 6250 mali ya CAG wamekufa papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari SU 41173 mali ya PSSSF, katika eneo la Chalinze Mkoani Dodoma leo.
 
 Taarifa za awali zinaeleza kuwa waliofariki katika ajali hiyo mkoani Dodoma leo katika gari la Ofisi ya CAG ni dereva wa ofisi hiyo na wengine 6 ni ndugu wa Naibu CAG waliokuwa wakitoka katika msiba huko Chato mkoani Geita. 

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Giles Muroto, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba watu saba wamefariki katika ajali iliyohusisha magari mawili ya serikali ikiwemo, STL 6250 Toyota Land Cruiser kutoka ofisi ya CAG, baada ya kugongana uso kwa uso na gari yenye nambari SU 41173.


Milioni 302 zakusanywa mashindano ya baiskeli

0
0
ZAIDI ya Sh milioni 302.6 zimekusanywa katika kilele cha mashindano ya baiskeli ya ACACIA Imara Pamoja Cycle Challenge, ambayo lengo kuu ni kuchangisha fedha kutekeleza miradi itakayoboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka migodi kampuni Acacia kanda ya ziwa. 

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji Madini –ACACIA kwa kushirikiana na Taasisi binafsi kutoka nchini Canada (CanEducate), yameshirikisha wanaume katika mbio za Kilomita 140 na wanawake km 87. 

Mzunguko wa mashindano hayo yaliyofanyika leo jijini Mwanza ulianza na kumalizikia katika Hoteli ya Malaika Resort kwa kupitia maeneo ya Kibandani, Igombe, Sangabuye, Kayenze, Nyanguge na Usagara, Buhongwa. 

Akizungumza katika kilele cha mashindano hayo, Meneja Uboreshaji tija wa kampuni hiyo, Janet Reuben alisema jumla ya washiriki 211 wameshiriki katika mbio hizo. Alisema kila mwaka ACACIA imekua ikidhamini mashindano ya baiskeli ya kanda ya ziwa chini ya jina la Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challenge. 

“Hata hivyo, mwaka huu mashindano hayo yamepewa jina Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge ili kuakisi dira mpya ya kampuni inayolenga kujenga mahusiano imara zaidi na jamii na wadau wetu. “Pia uamuzi huu wa kubadili jina unatokana na kuongezeka kwa kipengele cha uchangishaji fedha katika mashindano ya mwaka huu kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu. 

“Kwa niaba ya uongozi wa Acacia kwa kupitia migodi yetu ya dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, wadau wetu CanEducate na kamati ya maandalizi, nipende kuwashukuru kwa uwepo wenu leo, pia nawapongeza washindi na washiriki wote kwa kumaliza mbio hizi salama,” alisema. 
   Meneja Uboreshaji Tija kutoka ACACIA, Janet Reuben akizungumza katika mashindano mbio za baiskeli yaliyopewa jina la Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge. Jumla ya Sh milioni 302.6 zimekusanywa katika mashindano hayo yaliyofanyika leo jijini Mwanza.

   Baadhi ya washiriki wa mashindano mbio za baiskeli yaliyopewa jina Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge wakiwakata upepo katika mashindano hayo yaliyofanyika jijini Mwanza. Jumla ya washiriki 211 wametimua mbio katika mashindano hayo.

   Mshindi wa mashindano ya mbio za baiskeli yaliyopewa jina Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge, Masunga Duba akishangilia kuibuka mshindi na kujinyakulia Sh milioni 1.2, wa pili Gerald Konda (sh 900,000) na watatu Mungu Ataleta (Sh 500,000).

    Baadhi ya washiriki wa mashindano wakikata utepe kuanza mashindano hayo yaliyofanyika leo jijini Mwanza. Jumla ya washiriki 211 wametimua mbio katika mashindano hayo.

WAKULIMA WAKUBALI KUANZA KUUZA KOROSHO KWA BEI ISIYOPUNGUA 3000

0
0
Na Mathias Canal-WK, Mtwara

Wakulima wa zao la korosho wa Wilaya ya Tandahimba na Masasi wamekubali kuuza korosho zao mbele ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kutokana na kuridhia na kukubaliana na maamuzi ya serikali.


Hayo yamejili katika mnada wa nne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 uliojumuisha kampuni za ununuzi 11 katika maghala tofauti uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara.


Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba, Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba alisema kuwa bei ya zao la korosho imeonyesha mwelekeo wa kushuka katika mwaka 2018/2019 tofauti na hali ilivyokuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo bei ya zao hilo ilifikia shilindi 4,128


Katika mkutano huo wakulima wa korosho walikubali mbele ya waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Tizeba kuanza kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya shilingi 3,016 huku bei ya chini ikiwa ni shilingi 3000.


“Wafanyabiashara wasipangiwe muda wa kuchukua korosho ghalani kwa ajili ya usafirishaji na wasipangiwe kutumia bandari gani, wawe huru kulingana na maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli’’

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.


NIMERIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA SGR-MAJALIWA

0
0
*Ni baada ya kuhakikishiwa kipande Dar-Morogoro kitakamilika Aprili 2019 badala ya Julai

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.

Amesema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa kukamilika Julai 2019, wataalamu wamesema watakamilisha Aprili 2019.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar esSalaam hadi Soga, Pwani.

“Nimeridhishwa na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii.”Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka kuona SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.

Kuhusu suala la ajira, Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uaminifu na muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze wapate ajira.”

Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.Alisema mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na kitagharimu sh. trilioni 2.7.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania  (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya SGR wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Markezi inayojenga Reli hiyo,  katika eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam, Novemba 3, 3018
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua maandalizi ya  ujenzi wa madaraja  ya  kupitisha treni  juu  wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya Kisasa ya SGR   Oktoba 3, 2018. Kambi hiyo ipo eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya utengenezaji mataluma ya reli ya SGR wakati alipotembelea Kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa  reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018.  Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA TAMASHA LA MVINYO JIJINI DODOMA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo lililofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni kwa mchango wa nchi yake katika kusaidia kilimo cha zabibu wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu  Hassan akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika sekta ya mvinyo na zao la zabibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alkovintages Bw. Archard Kato wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde  akizungumza na Waziri Wakuu wa Staafu Mhe. Peter Mizengo Pinda (katikati) na John Samuel Malecela (kulia) wakati wa halfa ya uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo lililofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu  Hassan akipata maelezo ya umuhimu wa zabibu ya Dodoma katika uzalishaji  mvinyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alkovintages Bw. Archard Kato (kulia)  wakati wa hafla ya uzinduzi wa tamasha la mvinyo Dodoma.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

TAASISI YA KHOJA SHIA YAANDAA KAMBI YA MATIBABU YA MACHO NA MENO KWA JAMII

TATA Motors yazindua magari yake aina ya Tata Hexon na Tata Hexa

0
0
Kampuni ya Magari ya TATA Motors kwa kushirikiana na msambazaji wake nchini Tanzania Tata Africa Holdings imezindua magari aina ya Tata HEXON na Tata HEXA ambayo na kutangaza kuyaingiza katika soko  la Afrika huku mnunuzi akipewa chaguo la kuamua kulipa kidogokidogo kila mwezi.

Magari hayo ambayo yamezinduliwa India mwaka 2017 hapa Tanzania
yamezinduliwa Novemba 2.2018 na Kampuni hiyo imesema  magari hayo yatakuwa yakipatikana nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla kupitia kwa mawakala wao walioidhinishwa.

“Tunafurahi kutangaza uzinduzi wa gari zetu hapa nchini. Gari zote hizi zimetengenezwa kwa ubunifu,  viwango bora na teknolojia endelevu. amesema Mkuu wa biashara za kimataifa wa Tata Motors, Sujan Roy.

Ameongeza, kwa uzinduzi huo wanatarajia kupanua ukubwa wa soko hapa nchini na ana imani bidhaa hiyo imeingia sokoni wakati mwafaka na wanunuaji wote watapata ofa ya bima isiyozidi Sh2.5 milioni sanjari na waranti ya miaka 3 kwa Kilimeta 60,000 tu.

Kadhalika amesema uuzwaji wa gari hizo umewekewa urahisi kwani mtu ataweza kulipa kwa kila mwezi “Tunafikiria kujenga kiwanda cha kuunganishia magari hapa kwa baadaye ili kuendelea kuweka unafuu zaidi wa bei ya magari yetu”.

Mkuu wa Tata Holdings Limited kanda ya Arika Mashariki, amrsema: “Hii ni hatua ya kwanza kubwa kufikiwa . Tunajivunia na tuna imani kuwa tutafanya hivi tena katika bidhaa nyingine bora kwa siku zijazo.”
 Pichani juu na chini ni aina ya Magari  ya Tata HEXON na Tata HEXA yamezinduliwa na Kampuni ya Magari ya TATA Motors kwa kushirikiana na msambazaji wake nchini Tanzania Tata Africa Holdings 

FELIX SIMBU APANIA KUWATOA KIMASOMASO WATANZANIA KWENYE MBIO ZA NEW YORK MARATHON

0
0

Felix Simbu ni Mtanzaia anaekimbia mbio ndefu Simbu ameshika tafasi ya tano kwenye mashidano Rio Olympic 2017 , na akashika nafasi ya 3, IAAF World Championships London 2017, yupo New York na yupo tayari kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindani hayo makubwa duniani. Simbu ni mategemeo ya Watanzania kwa sasa katika anga za kimataifa kwenye nyanja za mbio ndefu. Kwiyo macho na masikio ya Watanzaia ni kwake jumapili hii wakiona na kusikia ametutoa kimasomaso kwa kushika nafasi ya juu na kuitangaza vyema bendera ya Tanzania katika mashindano haya yanayojulikana duniani kote kama New York Marathon na kushikirisha wakimbiaji zaidi 50,000 kutoka duniani kote. 


Hapa Simbu akisubiri kufanyia massage katika hotel aliyofikia ya Hilton New York City


Hapa akipata Simbu akipata ukodak na Charles, Charles nae anashirikia Mashindano haya kila mwaka kwaiyo watakuwa wote wakiitangaza vyema bendera ya Tanzania.

Mchua misuri wake akiwa kazini na yeye akisubiri zamu yake

Hapa akiingia Hotel akiwa na NY Ebra!

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGA MAONESHO YA VIWANDA KIBAHA,AZITAKA WIZARA,MIKOA KUANDOA VIKWAZO

0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo Novemba 3, 2018, amefunga wiki ya maonesho ya viwanda Kibaha, Mkoani POwani, yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, eneo la Picha ya Ndege.

Moanesho hayo yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Oktoba 29, 2018, yalilenga kuwakutanisha wazalishaji bidhaa za wviwanda na wanunuzi (masoko), ambapo pia taasisi za serikali zinazohusika na utoaji huduma mbalimbali zilishiriki pia.

Miongoni mwa taasisi hizo, ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, ambao kazi yake kubwa ni kutoa Fidia kwa wafanyaklazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.Moja ya ujumbe mkubwa alioutoa siku anafungua maonesho hayo kwa waajiri kote nchini, Makamu wa Rais aliuagiza

uongozi wa (WCF), kuendelea kuwafuatilia waajiri ambao bado hawajajisajili ili waweze kufanya hivyo.Makamu wa Rais alitoa wito huo leo Oktoba 29, 2018 alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya viwanda Mkoa wa Pwani kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, Picha ya Ndege Mkoani humo.

Alisema viwanda vimeongezeka nchini na kwamba huduma za WCF zitahitajika sana kwa wakati huu na hivyo kuutaka uongozi wa Mfuko, kuhakikisha unaendelea na ufuatiliaji kwa waajiri wa zamani na wapya ambao bado hawajajisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko watekeleze takwa hilo la kisheria ili mfanyakazi anapoumia aweze kupata haki yake ya fidia.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kushoto), akitoa elimu kuhusu kazi za Mfuko huo kwa baadhi ya watumishi wa umma na binafsi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho hayo leo Bovemba 3, 2018 
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter(kulia), akimsikilzia mwananchi huyo aliyetembelea banda la Mfuko aliyetaka kujua kazi za Mfuko huo.  
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (kushoto), akimkabidhi cheti cha shukrani Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala mwishoni mwa maonesho hayo leo Novemba 3, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Florence Max Mambali wakati alipotembelea banda la Kampuni ya kufuga kuku na kuzalisha vifaranga vya kuku ya Mkuza Chicks katika Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba uliopo katika eneo la Picha ya Ndege, Kibaha, Oktoba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri na viongozi wengine wa juu serikalini, wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wawakilishi wa taasisi za umma na binafsi waliowezesha kufanyika kwa maonesho hayo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

INTRODUCING MC KOBA-NGEKEWA

KUONDOA ADHA YA KUKATIKA UMEME,VITUO VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VIFANYIWE UKAGUZI WA KILA SIKU ASUBUHI-KALEMANI

0
0


Na Zuena Msuya, Mbeya

Mameneja wote wanaosimamia vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini wametakiwa kufanya ukaguzi ( checkup) wa kila siku asubuhi katika mitambo na mashine zilizopo katika vituo hivyo kuondoa adha ya kukatika umeme kutokana na hitilafu au uharibifu katika vituo hivyo.

Licha ya kuwa vituo hivyo vinafanyiwa ukarabati na ukaguzi wa kila mara au hata baada ya miezi kulingana na utaratibu waliojiwekea.

Hayo yameleezwa na Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani , wakati wa ziara yake ya kikazi katika Jiji la Mbeya, baada ya kutembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Mwakibete na kukagua miradi ya kusambaza umeme katika kijiji cha Nsalaga na Iduda inayotekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

Alieleza kuwa kumekuwa na changamoto ya kukatika umeme kwa muda mchache katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ya ikielezwa kuwa ni hitilafu katika vituo au kuharibika kwa kifaa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme.

Alifafanua kuwa changamoto hiyo inaepukika na kutoweka kabisa endapo wahandisi na mafundi watakuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa mitambo na mashine zao kila siku asubuhi kubaini tatizo kabla ya kutokea.

Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani, (katikati) akipita katika mitaa ya kijiji cha Nsalaga kukagua Miundombinu ya usambazaji wa huduma ya Umeme, unaotekelezwa na Shirika la Umeme, nchini (Tanesco) ambapo ametoa siku 14,kwa wananchi hao kuunganishwa na huduma hiyo. 
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (katikati mwenye kipaza sauti) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Iduda, ambao bado hawajaungwanishwa na huduma ya Umeme Licha ya miundombinu kuwafikia. 
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akikagua miundombinu ya kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mwakibete, Jijini Mbeya na kuagiza mafundi na wahandisi katika Vituo vyote nchini kufanya ukaguzi wa kila siku kuepusha kukatika Umeme kutokana na hitilafu zinazojitokeza katika Vituo hivyo. 
Mafundo na wahandisi wakiendelea na Kazi za ukarabati wa machine na mitambo katika kituo cha kupoza na kusambaza Umeme cha Mwakibete jijini Mbeya.
 

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU VIONGOZI KUWATISHA, KUWANYANYASA ASKARI, WATUMISHI WANAOTOA KERO ZAO KATIKA VIKAO VYAKE, AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA GEREZA MBIGIRI MKOANI MOROGORO

0
0

Na Felix Mwagara, MOHA-Morogoro

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka askari pamoja na watumishi mbalimbali waliopo ndani ya Wizara yake wawe huru kuuliza maswali, kusema kero zao zinazowakabili katika vikao vyake na hakuna kiongozi yeyote atakaye wanyanyasa baada ya yeye kuondoka.

Waziri Lugola amesema hayo baada ya kuona baadhi ya watumishi katika ziara mbalimbali anazozifanya nchini, wanakua na woga wa kusema kero zao wakihofia watapata matatizo baada ya yeye kumaliza kikao. , wakati anapata mambo mengi ambayo yanamsaidia kutatua kero za watumishi wake licha ya kuwa baadhi ya watumishi wanakua na woga wa kusema matatizo yanayowakabili.

Akizungumza katika kikao na askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri, liliopo Wami-Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro, jana, Lugola alisema ili aboreshe utendaji kazi wa Wizara na Idara zake, anahitaji kujua matatizo mbalimbali ya watumishi wake, hivyo katika kikao chake ruksa watumishi kuuliza maswali kwasababu kupitia maswali hayo yanamsaidia sana kutatua kero zao.

“Mimi ndio Waziri wenu, ulizeni swali lolote, toeni kero zenu na hakuna wakuwafuatilia baada ya kikao hiki, hiki ni kikao cha Waziri wenu mmepata nafasi hii ulizeni, niambieni matatizo yenu yanayowakabili ili tuyafanyie kazi,” alisema Lugola. Pia aliwaambia watumishi hao endapo watapata matatizo baada ya kusema kero zao katika kikao chake, wawe huru kumuambia japo anaamini hakuna chochote kitakacho wakuta maana kikao chake ambacho ni huru.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akionyesha moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, ambayo inahitaji matengenezo. Lugolo alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo la Kilimo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kulia ni askari wa Gereza hilo, Sajenti Lubimbi Sayi. Lugola alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikikiliza Mkuu wa Gereza la Mbigiri, Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe (kulia) alipokua anatoa taarifa ya utendaji kazi wa Gereza hilo la Kilimo. Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na askari na Maafisa wa Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri lililopo Mvomero, Mkoani wa Morogoro, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kushoto kwa Waziri huyo ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola aliwataka na askari na Maafisa hao kusema kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akichungulia ndani moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri ambayo inahitaji matengenezo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupokea kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

DKT TIZEBA AWAPONGEZA WAKUU WA MIKOA KWA USIMAMIZI BORA ULIOPELEKEA KUONGEZEKA KWA UZALISHAJI WA PAMBA

0
0
Na Mathias Canal-WK, Mwanza

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewapongeza wakuu wa mikoa yote nchini inayozalisha pamba, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwa usimamizi bora uliopelekea uzalishaji wa zao hilo kuwa maradufu katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/2019.

Dkt Tizeba ametoa pongezi hizo leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018 wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza na kusema kuwa Uzalishaji wa pamba katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/19 umeongezeka kwa asilimia 67 kutoka tani 133,000 hadi tani 221,600. 

Pamoja na pongezi hizo waziri huyo amewataka viongozi hao kuongeza ufanisi wa usimamizi wa zao hilo kwani pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji lakini bado matarajio ya uzalishaji hayakufikiwa kwa mujibu wa makubaliano.

Alizitaja sababu zilizopunguza uzalishaji kuwa ni pamoja na Ukame mkali kati ya mwezi Januari na Februari ulipukutisha vitumba vichanga; Mripuko wa wadudu wakiwemo viwavi jeshi vamizi, vidung’ata, chawa jani, vithiripi, vidukari. Wadudu wanaofyonza miaka ya nyuma halikuwa tatizo kwenye pamba; Mvua kubwa kupita kiasi kati ya Machi na Mei ilizamisha pamba kwenye maeneo yote ya mbuga na mabondeni; sambamba na Ufahamu mdogo wa wakulima kuhusu matumizi ya viuadudu. 

Alisema, mfumo wa kuzalisha mbegu bora za pamba umefufuliwa na unafanya kazi. Mbegu mama (Breeder seed) inazalishwa katika Taasisi ya Utafiti ya Ukiriguru na inakwenda kupandwa katika shamba la Nkanziga lililopo Wilayani Misungwi ili kuzalisha (Prebasic seed)
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Shinya Mhe Zainabu Telack, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri wakifatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) Ndg Japhet Justine akifuatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dkt Joel Kabisa akizungumza wakati wa mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images