Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 255 | 256 | (Page 257) | 258 | 259 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Senior Agriculture Advisor at SERA Policy Project, Alex Mkindi (R ) briefs journalists at a one day seminar on food security in Dar es Salaam today. SERA is the policy arm of the Feed the Future Initiative supported by the American people through the United States Agency for International Development (USAID) with him is the USAID supported Feed the Future Senior Advisor, Tom Hobgood.
  Ministry of Agriculture and Food Security National Food Director Karimu Mtambo talking to media during the SERA Policy project workshop in Dar es Salaam today.
  A cross section of journalists during the SERA Policy Project workshop on Food Security in Dar es Salaam today.
  A cross section of participants attending the USAID supported SERA Policy Project workshop to present the results of cutting edge research studies on food security in Dar es Salaam today.

  0 0

   Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.

  Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.

  Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.

  Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili kuendelea na biashara.

  Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.

  Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.

  Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.

  Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
   Katapila likiendelea kubomoa....

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi

  Jeshi la Polisi la Uturuki limetoa ufadhili wa masomo kwa askari kumi na saba ( 17) wa Jeshi la Polisi Tanzania kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya upelelezi wa wahalifu na mbinu za uchunguzi wa kimaabara pamoja na usimamizi na uendeshaji wa gari la matukio yatakayochukua muda wa mwezi mmoja nchini Uturuki.

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Kamishina Robart Manumba aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi.

  Alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya maboresho yanayolenga kuwaongezea askari weledi na kuwajengea uwezo wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi juu ya mbinu mbalimbali za kiuchunguzi na upelelezi pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya kiupelelezi.

  Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi kuweza kufanikisha kuwakamata wahalifu na kutambua uhalifu uliotendeka kwa haraka, hivyo, kupunguza uhalifu nchini.

  Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya uchunguzi ya Jeshi la Polisi Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Abdularahaman Kaniki alisema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Polisi la Uturuki ambao ulianza katika mafunzo ya upelelezi na ukusanyaji wa vielelezo katika eneo la tukio uliofanyika hapa nchini mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.

  Aidha, aliwataka askari waliochaguliwa kushiriki mafunzo hayo kutumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii ili kuongeza ufanisi pamoja na kuboresha utendaji katika maeneo mbalimbali ya upelelezi na Maabara ya uchunguzi ya Polisi ili kufanikisha utambuzi wa uhalifu na wahalifu kwa haraka.

  0 0

  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitio ofa hio, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Kushoto ni msanii wa muziki ya kizazi kipya, Diamond Platinumz na kulia ni Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.
  Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitia ofa hio, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) na kulia ni Salum Mwalim, Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania.
  Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, punde baada ya kusaini mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Anayeshuhudia ni Salum Mwalim , Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania.
  Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (mwenye fulana nyekundu) akiucheza wimbo wake mpya ujuikanao kama My Number One, wakati wa uzinduzi wa mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo huo kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Mkataba huo ni baina ya Diamond Platinumz na Vodacom Tanzania.

  0 0

  Bibi Silvana Nhungwe akivuna zabibu katika shamba la Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda lililopo eneo la Zuzu mjini Dodoma Septemba 11, 2013.

  Watu wakivuna zabibu kwenye Shamba la Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo PInda lililopo Zuzu mjini Dodoma Septemba 11, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye bendera ya taifa) akimsikiliza Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Petra Diamonds Bwana Jeschie Widawski. Balozi Kamala ametembelea Kampuni hiyo leo Antiwerpen Ubelgiji . Kampuni hiyo inauza Almasi kutoka Tanzania.

  Bwana Widawski alimweleza Balozi Kamala kwamba kwa mwaka Kampuni hiyo inauza wastani wa crat 20,000 za Almasi yenye thamani ya Dora za Kimarekani millioni 45. 

  Aidha, Bwana Widawski alisema Kampuni ya Petra Diamonds baada ya kununua Mgodi wa Almasi wa Mwadui iliwekeza Dora za Kimarekani milioni 45 na imefanikiwa kuongeza ubora wa Almasi inayozalishwa na hivyo kuongeza bei ya Almasi kutoka wastani wa Dora za Kimarekani 90 hadi wastani wa Dora za Kimarekani 250 kwa crat. 

  Balozi Kamala ameomba Kampuni hiyo kuongeza uzalishaji na ubora wa Almasi inayozalishwa hili Tanzania iweze kunufaika zaidi na Almasi inayozalishwa Tanzania.

  Aidha Balozi Kamala akizunzungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo alisema yapo mambo muhimu ya kujifunza kutoka Uholanzi katika uendelezaji na usimamiaji wa sekta ya gesi. Uholanzi walipongundua gesi mara ya kwanza katika eneo la Groningen ilikadiriwa kwamba kulikuwa na gesi yenye ujazo wa 2 TCF. Eneo hilohilo baada ya kuanza kuvuna gesi ilibainika lilikuwa na gesi yenye ujazo wa 99 TCF.

  Kwa sababu hiyo kiwango cha 43 TCF ambacho kinatajwa kwamba ndicho kimeishagundulika Tanzania, kuna uwezekano mkubwa baada ya kuanza kuvuna kiwango hicho kuongezeka hadi 15,000 TCF ukizingatia uzoefu wa Uholanzi.

  Vilevile Serikali ya Uholanzi inapata asilimia 85 ya mapato yote yanayotokana na biashara ya gesi. Kwa sababu hiyo Tanzania lazima tujipange ili tuhakikishe Serikali inapata mapato ambayo hayatapishana sana na Serikali ya Uholanzi inavyopata mapato kutoka kwenye gesi.

  Balozi Kamala alisema pia amejifunza kutoka Serikali ya Uholanzi kwamba Serikali inamiliki kwa asilimia zaidi ya tisini miundombinu na biashara ya gesi kwa kutumia Kampuni za Serikali kama vile Gusuine, GasTera na EBN. 

  Aidha, Balozi Kamala alisema Serikali ya Uholanzi ina sera mbili zinazoongoza sekta ya gesi ambazo ni sera ya visima vikubwa na sera ya visima vidogo inayotoa fursa ya uwekezaji na uchimbaji wa gesi katika visima vidogo.

  Mwisho, Balozi Kamala alimshukuru Bwana Edward Rweyememu wa TANSORT anayefuatilia kwa karibu uuzaji wa Almasi ya Tanzania katika Soko la Almasi la Antiwerpen. Alimweleza kwamba yeye ni jicho la Tanzania na hivyo lazima awe mzalendo na ahakikishe Tanzania inapata mapato yanayotarajiwa kutokana na uuzaji wa Almasi kwa kutumia utaratibu wa tenda.

  Aidha, Balozi Kamala ametoa wito kwa Wataalam wote katika sekta ya madini kuwa Wazalendo na wajue Taifa linawasomesha kwa fedha nyingi ili wasaidie Taifa na siku zote waepuke kulipwa na mtu yoyote kwa nia ya kutaka kutoelewa au kuacha kusimamia raslimali za Taifa kwa umakini.

  0 0

  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inaendelea na zoezi la uchukuaji alama za vidole, picha na kuweka saini ya kieletroniki kwa wakazi wa Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam. Zoezi hili kwa Temeke linatarajiwa kukamilika Jumapili ya tarehe 15 Septemba, 2013.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya VItambulisho vya Taifa (NIDA) akikagua uchukuaji alama za vidole, picha kwa wakazi wa Temeke.

  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Maria Stop ya jijini Arusha wakisalimiana na warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati warembo hao walipotembelea Makao Makuu ya Kanda ya Kaskazini mjini Arusha hivi karibuni na kupatiwa mafunzo juu ya uzazi wa mpango
  Warembo wa Miss Tanzania wakifuatilia mafunzo juu ya uzazi wa mpango na wakati salama wa umri wa kuanza kupata mtoto.
   Meneja wa Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa wa Maria Stop Tanzania, Dk Abraham Msaki akizungumza na warembo wanaoshiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 na kuwapatia elimu ya uzazi wa mpango wakati warembo hao walepotembelea taasisi hiyo mjini Arusha hivi karibuni.
   Mmoja wa washiriki Salsha Isdori  akiuliza swali...
   Picha ya pamoja kati ya warembo na wafanyakazi wa Maria Stop Kanda ya Kaskazini ilipigwa.

  0 0

  Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson(wapili kushoto)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua ya mazungumzo waliyofikia na kujenga kituo cha michezo katika Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua mchezo wa mpira wa miguu(wakwanza kulia)Mkurugenzi wa Michezo Nchini bw.leonard tadeo(wapili kulia)Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki(wakwanza kushoto)Mwakilishi wa klabu ya Sunderland Tanzania,Bw Edmund Hazzad.
  Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.akifafanua kuhusu sekta ya Utalii inafanikiwa na kuinua uchumi wa nchi kupitia michezo Nchini.
  Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson,(kushoto)akimkabidhi mkurugenzi wa wizara ya michezo bw.leonard Tadeo.jezi ambao imesainiwa sahihi na wachezaji wa sunderland.
  Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki(kulia)akimkabizi Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson,Tisheti ya Bodi ya Utalii.
  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali walioudhuria kwenye mkutano huo.

  SERIKALI imesema ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na uongozi wa klabu ya soka ya Sunderland ya Uingereza ili kuwekeza kwenye maendeleo ya sekta ya Utalii pamoja na kuinua mchezo wa mpira wa miguu nchini.

  Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Uwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki alisema lengo la kufanya hivyo ni kutafuta wawekezaji wa kuhakikisha sekta ya Utalii inafanikiwa na kuinua uchumi wa nchi kupitia michezo.

  Alifafanua kuwa tangu kuanza kwa mazungumzo hayo Tanzania imeanza kunufaika kwa kuwa na ongezeko la watalii la asilimia 30 hali ambayo inaonekuwa kuwepo kwa mafanikio yanayohitajika.

  Alisema Uingereza ndio nchi inayoongoza kwa utalii nchini na kwamba uwekezaji huo unalenga kuinua pato la nchi kwa kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini.

  "Vivutio vya Tanzania vinaoneshwa kupitia Uwanja wa timu hiyo nchini Uingereza katika michuano ya Ligi Kuu ya huko inayoonekana na mashabiki wengi duniani na kutoa fursa na hamasa kuja nchini kutembelea vivutio vyetu na kuongeza uchumi wa nchi," alisema.

  Pia Dk. Nzuki aliushukuru uongozi wa klabu ya Sunderland kwa kuendeleza ushirikiano katika kuinua utalii wa Tanzania kupitia sekta ya michezo kitu ambacho kila mdau anasubiri mafanikio hayo kwa hamu kubwa ili Tanzania ifanye vema katika mashindano ya kimataifa.

  Wakati huo huo Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland Gary Hutchinson, alisema moja ya hatua ya mazungumzo waliyofikia na kujenga kituo cha michezo katika Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua mchezo wa mpira wa miguu.

  Licha ya kujenga kituo hicho cha michezo (Academy), watajenga uwanja wa kisasa wa michezo utakaokuwa moja ya sehemu ya uwekezaji katika sekta ya michezo itakayoleta maendelea katika nyanja hizo na kufikia mafanikio kwa ushirikiano na kampuni ya Marekani ya Simbion.

  "Tutaanzisha kituo cha michezo (Academy) katika eneo la Kidongo Chekundu wilayani Ilala, Dar es Salaam ambayo itasaidia kutangaza utalii kimataifa kupitia sekta ya michezo na kufikia mafanikio yanayohitajika," alisema.

  Mkutano huo wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Sunderland pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo.

  0 0

  H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania is received by Namibia’s Minister for Home Affairs, Mrs. Rosalia Nghidinwa at the Hosea Kutako International Airport in Windhoek Namibia ahead of a one-day Summit of the Southern Africa Development Community (SADC) Troika-Organ on Politics, Defence and Security Summit today September 11, 2013 held at the State House in Windhoek.
  H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania ( attends a one-day Summit of the Southern Africa Development Community (SADC) Troika-Organ on Politics, Defence and Security today September 11, 2013 at the State House in Windhoek, Namibia, under its chairman President Hifikepunye Pohamba of Namibia. Second left if the SADC Chairperson Dr Joyce Banda,second right is President Joseph Kabila of the Democratic Republic of Congo.STATE HOUSE PHOTOS.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili uwanja wa mkutano katika kata ya Salawe.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakati wa kata ya Salawe na maeneoya jirani waliofika kusikiliza sera na misimamo imara ya Chama Cha Mapinduzi.
   Mbunge wa Viti Maalum  Azah Hilal Hamad akihutubia wananchi  kwenye mkutano wa hadhara na kuelezea namna gani serikali sikivu ya CCM inavyojali wananchi wake.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kwenye ujenzi wa Birika la kunyweshea mifugo katika kata ya Didia.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na mafundi ujenzi wanaoshiriki kujenga birika la kunyweshea maji mifugo katika kata ya Didia.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa akitoa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mwananchi aliyeomba kupiga nae picha nje ya soko jipya katika kata ya Didia.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi baada ya kutembelea soko la jipya katika kata ya Didia na kuwapongeza sana wakazi wa kata hiyo kwa kushirikiana na uongozi wake kwa kufanikisha ujenzi wa soko hilo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amebeba nyoka aina ya chatu nje ya jengo la soko jipya katika kata ya Didia, Nyoka huyo huchezwa kwenye ngoma inayoitwa Wagoyangi.
   Katibu Mkuu akipata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali ktika kata ya Iselamagazi.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 09/11/13--13:52: SCHOLARSHIP


 • 0 0
 • 09/11/13--13:55: TANGAZO LA KUIBIWA GARI
 • SERENGETI FREIGHT
  GARI LIMEIBIWA
  MAKE: NISSAN NAVARA
  MODEL: AVENTURA 
  REG : AD07 MWK

  TUNAWATANGAZIA NDUGU ZETU WATANZANIA WENZETU KUWA TUMEIBIWA HILI GARI KUTOKA KWENYE OFISI YETU HAPA LONDON 
  TUNADHANI KUWA WEZI WA GARI HILI WATAKUWA WAMELISAFIRISHA KWENDA DAR AU ZANZIBAR 
  TUNAOMBA MTU YEYOTE ATAKAE LIONA KAMA NI  BANDARINI AU HATA BARABARANI ATOE TAARIFA KITUO CHA POLISI CHA JIRANI AU ATUPIGIE MOJA KWA MOJA KWENYE NAMBA ZETU ZIFUATAZO

  CHRIS LUKOSI +44 (0) 7903828119
  TORNADO - DAR - 0713607116

  ZAWADI YA SHS MILIONI KUMI (SHS 10,000,000) ITATOLEWA KWA ATAKAEFANIKISHA UPATIKANAJI WA HILI GARI

  ASANTENI SANA 

  CHRIS LUKOSI

  0 0
 • 09/11/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • Ujumbe mkali katika ngoma hii ya Kenny Rogers ya 'Lucille' ni mzito...

  0 0

   
  Balozi wa Sierra Leone Ubelgiji Mhe. Ibrahim Sorie akizungumza na Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa). Balozi Sorie alifika kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kushauriana na Balozi Kamala kuhusu masuala mbalimbali ya Kidiplomasia.

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Rose Mary Lulabuka (Wapili toka Kushoto) akipokea hundi ya Shilingi milioni Kumi na Tano kutoka kwa meneja mkuu wa Golbal Publishers, Masha Bukumbi (Wapili Kulia).

  0 0

  TEMEKE, MJINI MAGHARIBI KUCHEZA NUSU FAINALI COPA
  Temeke na Mjini Magharibi zinapambana kesho (Septemba 13 mwaka huu) katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es Salaam.

  Timu hizo zimetinga hatua hiyo baada ya kushinda mechi zao za robo fainali ya michuano hiyo zilizochezwa leo (Septemba 12 mwaka huu) asubuhi kwenye uwanja huo huo.

  Wakati Temeke imetinga hatua hiyo baada ya kuilaza bao 1-0 Iringa lililofungwa dakika ya 18 na Ramadhan Mohamed, Mjini Magharibi imeing’oa Mtwara kwa ushindi wa bao 1-0.

  Robo fainali nyingine zinachezwa leo (Septemba 12 mwaka huu) jioni kwa Kilimanjaro kuvaana na mabingwa watetezi Morogoro huku Arusha ikioneshana kazi na Ilala.

  TFF YATOA ITC KWA WAWILI, MAULID RUKSA
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania wawili kucheza mpira wa miguu nchini Afrika Kusini.

  Wachezaji hao; Robert Kobelo na Mohamed Ibrahim wamepewa hati hizo baada ya kuombewa na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kama wachezaji wa ridhaa ili wajiunge na klabu ya Cacau United ambayo timu yake inacheza Ligi Daraja la Pili katika Wilaya ya Cacau.

  Naye mchezaji Said Maulid aliyejiunga na Ashanti United akitokea nchini Angola msimu huu amepata ITC ambayo sasa inamwezesha kuchezea timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoingia mzunguko wake wa tatu keshokutwa (Septemba 14 mwaka huu).

  MVELLA AJIONDOA KWENYE UCHAGUZI TFF
  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Eliud Mvella amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba 27 mwaka huu.

  Mvella amemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni akielezea uamuzi wake huo pamoja na mambo mengine umetokana na kile alichodai kuwa Kamati hiyo haikumtendea haki kwa kumwondoa.

  Mbwezeleni amekiri kupokea barua hiyo, na kuongeza kuwa licha ya uamuzi huo wa Mvella aliyekuwa ameomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda Namba Saba ya mikoa ya Iringa na Mbeya, bado suala lake litasikilizwa na Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.

  Kamati ya Mbwezeleni ilimuondoa Mvella katika kinyang’anyiro hicho kwa kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa.

  FDL SASA KUPIGWA UWANJA WA KAWAWA
  Mechi za nyumbani za timu ya Kanembwa JKT ya Kigoma iliyoko Ligi Daraja la Kwanza (FDL) sasa zitachezwa katika Uwanja wa Kawawa badala ya ule wa Lake Tanganyika.

  Uamuzi wa kuhamishia mechi hizo Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji umetokana na Uwanja wa Lake Tanganyika kutumiwa na Serikali katika Operesheni Ondoa Wahamiaji Haramu inayoendelea nchini kwa sasa. Uwanja huo hivi sasa unatumika kuhifadhi wahamiaji hao.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa idara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. Dk Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, jijini Dar es Salaam leo.
   
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam. Dk Nchimbi alifanya ziara ya siku moja katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao masuala mbalimbali ya utendaji kazi..
   
  1. Kamishna wa Pasipoti na Uraia, wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya idara hiyo. Watumishi mbalimbali waliuliza maswali pamoja na kutoa maoni yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto (Meza Kuu) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).


  0 0


  0 0

   Gari imetembea kama 137000km hivi sasa, gharama yake ni sh. Mil 8.
  Kwa mawasiliano zaidi 0716125551 au 0754021471.
  Sababu ya kuuza gari, mmiliki anaondoka nchini, hivyo gari ipo kwenye hali nzuri.


older | 1 | .... | 255 | 256 | (Page 257) | 258 | 259 | .... | 3284 | newer