Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA PHAUSTINE KASIKE AFUNGA MKUTANO MKUU WA SITA WA MAGEREZA SACCOS, LEO JIJINI DODOMA

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS nchini akitoa hutuba ya ufungaji wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili leo Oktoba 30, 2018 jijini Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(hayupo pichani) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS nchini .
Wanachama mbalimbali wa Saccoss ya Magereza wakiwa mbele ya wajumbe wakati wa uchaguzi wa Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara katika Mkutano huo.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakifuatilia ufungaji wa Mkutano huo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(katikati) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS nchini akiondoka ukumbini mara baada ya ufungaji wa Mkutano, aliyeambatanaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya Magereza Saccos, SACP. Mbaraka Semwanza(kushoto). Kulia ni Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu, Gaston Sanga(Picha zote na Jeshi la Magereza).

MZEE ALIYEKAA HOSPITALI YA KIOMBOI IRAMBA MIAKA 10 AOKOLEWA NA ZIARA YA DKT. NDUGULILE

$
0
0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi kuhakikisha Bibi. Aisha Hamisi aliyeishi zaidi ya miaka kumi katika Hospitali ya Kiomboi iliyopo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida anapelekwa katika Makao ya kuhudumia Wazee na Wasiojiweza.

Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Waziri huyo kuongea na Mzee huyo na kupata taarifa kuwa hana ndugu wala Jamaa wa kumlea hivyo anakosa huduma muhimu za kibinadamu wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Kiomboi iliyopo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Iramba amemueleza Naibu Waziri Ndugulile kuwa Bibi Aisha Hamisi amekaa zaidi ya miaka kumi katika Hospitali ya Kiomboi alikuwa akitibiwa na kuendelea kukaa hapo kwa kukosa ndugu wa kumchukua na kumtunza.

Aidha Dkt. Ndugulile ameagiza Mzee huyo apelekwe katika Makao ya kuwahudumia Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela yaliyopo Wilaya ya Manyoni ili kupata huduma muhimu. Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali ina jukumu la kuwatunza Wazee na Wasiojiweza kwa wale ambao hawana ndugu wala jamaa wa kuwatunza.

Akipokea maelekezo hayo Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi amesema kuwa suala la kumuhamishia Bibi Aisha kwenye Makao ya Wazee litafanyika mara moja na hatahamishiwa katika Makao ya Wazee ya Sukamahela.

Kwa upande wake Bibi Aisha Hamisi amemshukuru Naibu Waziri kwa kuja kutembelea Hospitali ya Kiomboi na kumwomba kutatua changamoto za matibabu zinazowapata Wazee.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisaliana na Bibi Aisha Hamisi wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba Mkoani Singida kuangalia hali ya utoaji wa huduma za Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu amewataka wananchi wa Kibaha Mjini Mkoani Pwani ,wajipange kuchagua viongozi wepesi kufuatilia maendeleo na kwenda mbio badala ya kuchagua mazezeta na mananga ,katika uchaguzi unaokuja wa serikali za mitaa- 2019.

Akihitimisha ziara yake ya siku sita mkoani hapo katika mkutano wa hadhara ,Mailmoja Samia aliwasihi wasichague watu wazito,wezi na mafisadi bali waweke viongozi watakaojenga Kibaha .

"Wanasema mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe ,mimi nikija ninaona kasoro zilizopo nitakwambieni kuna kasoro lakini warekebishaji ni nyinyi na viongozi mtakaowachagua ""Mkichagua wazuri wataondosha kasoro zilizopo haraka lakini mkichagua wazito na mananga hapa yatazama tuu chini kunyanyuka hayanyanyuki ,kutembea hayatembei "alisisitiza Samia .

Akizungumzia suala la ardhi anasema",Wakati napita ,mheshimiwa mkuu wa mkoa alinionyesha eneo kubwa halina kitu chochote nikamwambia mnataka manispaa ,lakini mbona eneo hili mwitu mtupu hakuna kuendelezwa akaniambia linamilikiwa na taasisi fulani "

Aidha ,ameitaka wilaya na halmashauri ya Mji huo kukaa chini na taasisi ambazo zimehodhi maeneo bila kuyaendeleza katika kipindi kirefu ili ziweze kuingia ubia .Awali Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka aliomba mji huo upandishwe hadhi na kuwa manispaa kama vigezo vinaruhusu.Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni ,usambazaji wa maji kwenda kwa wananchi unasuasua kasi iongezwe kwani mji unakua ila maji hayajawafikia .

" Eneo la Tamco-Mapinga zaidi ya miaka mitano wapo wananchi walifanyiwa tathmini lakini hawajalipwa fidia zao ,tunaomba utusaidie wananchi hawa waweze kufaidika na fidia hizo"alielezea Koka.Koka alitaja tatizo jingine ni ucheleweshaji wa nishati ya umeme , kasi ni ndogo kufika kwa baadhi ya maeneo na wawekezaji ,ameomba uwafikie maeneo yaliyo katika miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.

DKT KALEMANI: AWATAKA MAMENEJA WA TANESCO NCHINI KUWAKATIA UMEME WADAIWA SUGU KWENYE MAENEO YAO.

$
0
0
WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaagiza Mameneja wa shirika la Umeme (Tanesco) kote nchini kuhakikisha wanakata huduma ya umeme kwa wadaiwa sugu ikiwemo sekta binafasi na serikalini. 

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Morogoro iliyokuwa na lengo la kutembelea maeneo yanayozalisha umeme ikiwemo Kidatu ambako uzalishaji wa umeme ni 204 mw. 

Licha ya kutembelea eneo hilo lakini pia alizindua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro. Alisema kwamba hatua hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa kuweza kusaidia kukusanya madeni hayo ambayo yamekuwa kwa muda mrefu na hivyo kupelekea kukwamisha malengo yao waliojiwekea. 

Aidha alisema kwamba haiwezekani shirika hilo likawa linawadai watu fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwenye kutekeleza shughuli za kimaendeleo na kuweza kuwafikia wananchi wengi huku wakiacha kuwachukulia hatua ambazo zinaweza kusaidia kupata ufumbuzi wake. 

“Ndugu zangu mameneja wa mikoa hakikisheni mnawakatia umeme wadaiwa wote sugu kwenye maeneo yenu wakiwemo wale wa sekta binafasi na serikali kwani hii ndio njia inayoweza kuwasaidia kukusanya madeni hayo “Alisema Dkt Kalemani. Akizungumzia kitengo cha huduma kwa wateja ndani ya shirika hilo Dkt Kalemani alisema ni muhimu watumishi wa kada hiyo wakabadilikana kitabia kwa sababu imedodira sana na kwenye maeneo mengi hazifanyi kazi zao ipasavyo. 
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo akishuhudia 
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani kulia akizundua mradi wa umeme wa gharama nafuu (REA awamu ya tatu) kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa ziara yake
 WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kwenye Kijiji cha Katurukila wilayani Kilombero mkoani Morogoro mara baada ya kuzindua Rea awamu ya tatu
Sehemu ya wananchi wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Waziri wa Nishati Dkt Kalemani

Wafanyabiashara Tabora mjini matatani kwa kukwepa kodi

ZIARA YA NAIBU WAZIRI DKT FAUSTINE NDUGULILE KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA RU

TAARIFA KWA UMMA


Advocating for nationwide connectivity/Connecting the unconnected Tanzanians – One region at a time.

$
0
0
No matter what part of the world you live in, communication is a vital aspect of everyday life facilitating connection between people. The use of phones has evolved from interactions with friends and family to tools that enable commercial transactions for businesses. In Tanzania, the highest rate of mobile phone penetration is in urban areas however 67.6% of the population resides in rural areas where connectivity remains a challenge.

A Deloitte study of 40 African economies reveals that the introduction of mobile networks has the potential to influence socio-economic development for individuals and villages in remote areas.  Additionally, the study shows that 1% increase in market penetration leads to an increase of 0.28 percentage points in GDP and 1% increase in internet penetration increases the GDP growth rate by 0.077 percentage points in the economy.


We live in a world where a person in the southern highlands of Tanzania needs to be able to access breaking news as it happens from his mobile phone and also have the ability to use the same phone to source commercial opportunities in other parts of Tanzania. Without enabling rural access it would take a long time for information to reach people in rural areas thus hindering their progress. 


According to FinScope Tanzania 2017, 78% of Tanzanian adults in rural areas have a financial access point within a 5km radius. Due to the limited footprint of traditional bank branches, the majority of financial service providers found within a 5km radius are mobile money agents whose presence facilitate transactions that allow for residents to participate in economic activities that improve their livelihoods.  Rural connectivity empowers the lives of those that reside great distances from urban centers.


Vodacom Tanzania named the Best Employer in Africa 3rd year in a row

$
0
0

Tanzania’s leading telecommunication service provider Vodacom has been named as the best employer in Africa and Tanzania for the 3rd time in a row by global company Top employer Institute. Top Employer Institute is a global certification company recognizing excellence in the conditions that employers create for their people.

The Global Top employer institute, now in its 25th year conducts in-depth assessment to identify top employers in the world who meet set criteria which include best HR practices. Vodacom Tanzania PLC has been certified as a 2019 Top Employer after leading the way in outstanding ‘people-first’ HR practices and qualified as one of the successful organisations.

A statement from the company signed by Human Resources Director Perece Kirigiti detailed that the exciting achievement was officially announced last week as a result of global research and subsequent certification of only the very best employers worldwide.

She hinted that as a proud Top Employer 2019, Vodacom’s practices were assessed through the analysis of 100 questions which covered 600 people practices across 10 Human Resources topics including but not limited to Talent Strategy, On-boarding, Learning & Development and Compensation & Benefits. The Top Employers Institute Programme provides organisations with the ability to leverage employer branding, benchmark practices against other top performers and globally align policies.

Kirigiti concluded that the award means a lot to Vodacom saying “As a certified Top Employer 2019, we have the honour of showcasing our Certification seal with pride for the upcoming year. This seal serves as a reminder that we are a part of a global community of forward-thinking organisations that continue to strive for only the best people practices, and this seal further cements our commitment to optimizing and improving our business performance.”

Gavana wa Jimbo la Shandong atembelea JKCI na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo

$
0
0
Na Anna Nkinda – JKCI
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imejipanga  kutanua huduma zake  kwa kutoa  matibabu ya moyo kwa kuwafuata wananchi wenye matatizo hayo katika hospitali za kanda zilizopo hapa nchini.

Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na ujumbe kutoka jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing nchini China waliotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Prof. Janabi alisema Tanzania ni nchi kubwa na ina idadi kubwa ya watu hivyo basi ili huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi  ni lazima wawafuate katika Hospitali za Kanda.

“Lengo letu la baadaye ni kuhakikisha huduma tunayoitoa katika Taasisi yetu inawafikia wananchi wengi zaidi wenye matatizo ya moyo walioko mikoani pia kutoa mafunzo kwa madaktari walioko katika hospitali za Kanda kwa kufanya hivyo tutasaidia wagonjwa wa moyo kupata matibabu kwa wakati”, alisema Prof. Janabi.

Aidha Prof. Janabi alisema tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo mwaka 2015 idadi ya wagonjwa wa moyo wanaokwenda kutibiwa  nje ya nchi imeweza kupungua kutoka wagonjwa 159 kwa mwaka 2012 hadi kufikia wagonjwa wawili kwa mwaka 2017.

Prof. Janabi alimalizia kwa kuzitaja changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na  kutokuwa na nafasi  ya kutosha kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa hii ni kutokana na idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka wagonjwa 100 kwa mwaka 2016 hadi  kufikia wagonjwa 300 kwa mwaka 2018 .
 Gavana wa Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing nchini China Yu Xiao-ming akimsililiza mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.  Gavana huyo pamoja na ujumbe wake walitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea zawadi ya picha ya moyo kutoka kwa Gavana wa  Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing  nchini China Yu Xiao-ming alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
 Gavana wa Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing  nchini China Yu Xiao-ming akizungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya jimbo hilo na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake aliyoifanya hivi karibuni katika  Taasisi hiyo  kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na  Genofeva Matemu – JKCI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Gavana wa  Jimbo la Shandong lililopo mjini Beijing  nchini China Yu Xiao-ming wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa JKCI na wajumbe kutoka China mara baada ya kumalizika kwa ziara ya kutembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI KARAGWE MKOANI KAGERA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka, wakati alipowasili wilayani humo mkoani kagera kwa ziara ya kikazi leo 31/10/2018. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili wilayani humo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.

KUKANDA ASHUSHA RUNGU KWA WALIMU WATATU WA SHULE ZA MSINGI ZILIZOSHIKA NAFASI ZA MWISHO KITAIFA KUTOKA IGUNGA

$
0
0
Na TIGANYA VINCENT
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Joseph Kakunda ameagiza kuvuliwa wadhifa wake Afisa Elimu Kata ya Malagano  Wilayani Igunga Raphael Kapela kwa kusema hawezi kuhamia kwenye kituo chake cha kazi kwa sababu ya kuwa na familia kubwa inayomtegemea.

Alisema kitendo cha Afisa huyo kuishi Nkinga badala ya Malagano kumesababisha Shule ya Msingi Malagano kufanya vibaya katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi ya darasa la saba mwaka huu.

Kakunda alichukua hatua hiyo wilayani Igunga wakati wa ziara yake ya kutembelea shule mbili za Shule ya Msingi zilizofanya vibaya na kisha kutembelea Shule ya Sekondari ya Bukoko ambayo Hosteli yake iliungua moto.

Alisema kuwa Afisa huyo kwa kitendo cha kusema kuwa hawezi kuishi Malagano kwa sababu hakuna nyumba za  kuishi watumishi na kwa sababu pia ana familia kubwa kinaonyesha kuwa hatoshi kushika nafasi hiyo.

Kakunda alisema kuwa nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine ambaye atakuwa tayari kuishi Malagano hata kama ni nyumba ya nyasi ili aweze kusimamia maendeleo ya elimu na nidhamu ya walimu katika Shule hiyo ili isifanye vibaya tena.

Alisema kitendo cha Mtumishi kukaa sehemu kwa sababu ya kuwepo kwa nyumba ya nyasi hakiwezi kuwa kinga na uhalali kwake kuishi mbali na kituo chake cha kazi kwa sababu kinapunguza ufanisi katika kutekeleza majukumu yake.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Joseph Kakunda akiongeza na baadhi ya Viongozi na wanakijiji  alipotembelea Shule ya Msingi Mwazizi kufuatilia kwanini ilifanya shule hiyo ilifanya vibaya katika mtihani wa kumaliza la saba na kuwa ya pili kutoka mwisho kitaifa.
 Mwalimi Mkuu wa Shule ya Msingi Mwazizi wilayani Igunga Musa Kitenya akisoma taarifa inayoonyesha sababu za kufanya vibaya kwa shule yake katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kuifanya kuwa ya pili kutoka mwisho kitaifa.
 Baadhi ya Viongozi na wanakijiji wa Kijiji cha Mwazizi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (hauyopo kwenye picha) wakati alipotembelea Shule ya Msingi Malagano kufuatilia kwanini ilifanya shule hiyo ilifanya vibaya katika mtihani wa kumaliza la saba na kuwa ya pili  kutoka mwisho kitaifa.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Malagano wakiwa mapunziko .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Milioni 151 zatumika kuongeza nguvu ya kupambana na Ukimwi Rukwa

$
0
0
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na mradi wa Military HIV Research Program (MHRP) imenunua gari aina ya Land Cruiser Hardtop kwaajili ya shughuli zinazohusiana na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Gari hiyo ambayo alikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Bw.Msongela Palela na mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo imenunuliwa kutokana na fedha zilizovuka mwaka 2016/2017 ikiwa ni makubaliano baina ya katibu tawala na mradi juu ya fedha zilizovuka mwaka kupangiwa matumizi yanayolenga kuboresha huduma za Ukimwi.

Wakati akikabidhi gari hiyo Mh. Wangabo alitahadharisha matumizi ya gari hiyo huku akipiga mfano wa gari ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) ya halmashauri ya Wilaya ya Kalmabo iliyokuwa na mazoea ya kwenda kwenye sehemu za starehe kuwa mshauri wa mradi huo tayari ameshachukuliwa hatua za kinidhamu.

“Tarehe 7 mwezi wa 10 gari hii tulilishika hapa Sumbawanga likiwa eneo la starehe na huyo mshauri wa mradi huo ndiye aliyekuwa anaendesha gari hilo, tulichukua hatua kali za kumuondoa na kumrudisha kwa mwajiri wake kwaajili ya hatua nyingine za kinidhamu, nitoe wito kwa madereva wa serikali kutumia magari kwa mambo yao binafsi, suala hili lisijitokeze, hatua kali zitachukuliwa,” alisisitiza.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa mradi huo Bw. Riziki Kasimu ameshukuru ushirikiano anaoupata kutoka katika halmashauri na serikali ya Mkoa ili kuhakikisha wanashusha na kutokomeza maambukizi ya Ukimwi na ameiomba serikali ya Mkoa wa Rukwa kutoa kipaumbele kwa kazi za Ukimwi katika matumizi ya gari.

“Pamoja na Kazi zote zilizopo Mkoani, tungependa kazi za mradi zipewe kipaumbele katika matumizi ya gari, ni kweli kwamba tuna kazi nyingi ama majukumu mengi ambayo hayo magari yangepaswa kufanya na sisi kama washirika kwenye maendeleo hatuwezi kusema gari hili litumike moja kwa moja kwa Ukimwi tu, lakini pale tunapokuwa na majukumu ya msingi ya Ukimwi tungependa msisitizo utolewe huko,”Alisema.

Mtadi huo tayari umeshatoa gari 7 katika Mkoa wa Rukwa, 4 katika Halmashauri zote za Mkoa na 3 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa jambo lililosaidia kurahisisha shughuli za kupambana na maambukizi ya Ukimbwi na hatimae kushuka kutoka asilimia 6.2 mwaka 2015 hadi asilimia 4.4 mwaka 2018. 
 Mwakilishi wa Mradi wa MHRP Bw. Riziki Kasimu (kulia) akimkabidhi funguo za gari litakalotumika kuongeza nguvu za mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) mbele ya wadau dhidi ya maambuzi hayo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo akiwasha gari lililokabidhiwa kupitia ushirikiano wa Ofisi yake na Mradi wa MHRP kwaajili ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
 Gari aina ya Land Cruiser Hardtop lililokabidhiwa kwa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwaajili ya kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

WAFANYABIASHARA WAKIWA KAZINI

$
0
0
Wafanyabiashara ndogondogo wa Kilumba jijini Mwanza wakiuza bidhaa zao nje ya soko la kimataifa Kilumba leo Wafanyabiashara hao hukosa mikopo katika taasisi za fedha kutokana na biashara zao kufanyia katika sehemu zisizo rasmi. (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG )
 Wafanyabiasha ndogondogo  wa mkoa wa Mwanza wakisubili wateja wanotoka sehemu mbalimbali za jiji la Mwanza
Wafanyabiasha ndogondogo  wa mkoa wa Mwanza wakisubili wateja wanotoka sehemu mbalimbali za jiji la Mwanza

TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari

$
0
0

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Kompyuta katika shule ya Sekondari Misitu iliyopo Wilaya ya Ilala, jijini Da es Salaam.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere, ametoa mchango huo ikiwa ni sehemu ya kuchangia maendeleo kwa jamii alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 9 ya kidato cha Nne katika shule hiyo ambapo wanafunzi 205 wanaotarajia kuhitimu masomo yao mara baada ya kufanya mtihani wa Taifa mwezi Novemba 2018.
Kamishna Mkuu Bw. Kichere, amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitachangia ujenzi wa Maabara ya Kompyuta na kuwafanya wanafunzi kujifunza na kuongeza uelewa zaidi wa  masuala ya Teknolojia.
“Nimesikia katika changamoto mlizozitaja kuwa mnahitaji jengo la maabara ya kompyuta, uzio pamoja na jengo la utawala na mimi nimeona vyema nichangie ujenzi wa jengo hilo ili wanafunzi wapate kujifunza na kuwa na uelewa wa teknolojia kwani dunia sasa inatumia zaidi teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuleta maendeleo”, alisema Kichere
Aidha, Bw. Kichere aliongeza kuwa, ujenzi na maendeleo ya shule za serikali unatokana na kodi hivyo aliwataka wanafunzi, walimu na wazazi kuwa na utamaduni wa kudai risiti za mashine za kielektroniki (EFD) ili kuchangia Mapato yatakayotumika kuboresha ujenzi na uboreshaji wa shule pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii.
Bw. Kichere alisisitiza kuwa matunda ya kodi zinazopatikana pia hutumika kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile ununuzi wa vitabu kwa ajili ya maktaba, utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, ujenzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu na ununuzi wa vifaa vya maabara na kufundishia.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akimkabidhi cheti mwanafunzi bora katika masomo yote wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam, Richard Sagwe wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwahutubia Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akiangalia baadhi ya kazi mbalimbali za Sanaa zinazofanywa na Wanafunzi katika shule ya sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Bw. Richard Kayombo (kushoto) pamoja na uongozi wa shule ya sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
(PICHA ZOTE NA TRA)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKONDA AUNDA KAMATI KUKOMESHA USHOGA DAR

$
0
0
*Awataka wakazi wa Dar es salaam wenye picha za ngono kwenye simu zao kuzifuta kabla ya jumatatu.


Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametangaza kamati ya watu 17 na kuwapa majukumu ua kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa na amani, maadili na utamaduni wa mtanzania unadumishwa.

Akizungumza na wanahabari leo jijini, Makonda amesema kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuhakikisha na kuwatambua mashoga wanaojitangaza na wasiojitangaza katika mitandao ya kijamii wanajulikana ikiwemo facebook, whatsaap na Instagram.

Aidha kamati hiyo itakuwa jukumu la kuwatambua wanaojitangaza na kufanya biashara ya ngono katika mitandao ya kijamii na wale wanaofanya utapeli hasa wa kutumia mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya watu maarufu.

Makonda amesema kuwa kamati hiyo itahusisha bodi ya filamu, Mamlaka ya mawasiliano (TCRA,) polisi na madaktari na kituo cha huduma hiyo itakuwa Mburahati na amesema kuwa kwa yeyote atakayegundulika kujihusisha na vitendo hivyo atatangazwa na kutaja anayeshiriki naye na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha amesema kuwa kabla ya jumatatu wana Dar es salaam walioweka picha za ngono kwenye simu zao wajitahidi kuzifuta kwani TCRA wana uwezo mkubwa.Mwisho ametoa rai kwa kwa wakazi wote wa Dar es salaam kushikamana dhidi ya mapambano hayo ili kulinda maadili yetu.
 MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,wakati akitangaza kamati ya watu 17 na kuwapa majukumu ua kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa na amani, maadili na utamaduni wa mtanzania unadumishwa.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokuwa akizungumza nao leo ofisini kwake jijini Dar kuhusu kukomesha Ushoga Dar

BENKI YA KCB TANZANIA YATOA MSAADA WODI YA WANAWAKE KATIKA HOSPITALI YA RUFAA AMANA

$
0
0
 Benki ya KCB Tanzania imekabidhi msaada wenye thamani ya milioni 6 kwa wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa benki hiyo, Christine Manyenye alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu, Mazingira, Ujasiriamali na masuala ya ubinadamu”, Bi. Manyenye alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofungua milango yake hapa Tanzania mwaka 1997, imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

Benki ya KCB ilikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda 10 magodoro 10, mashuka 20, vyenye thamani ya shilling 6,017,000 katika Hospitali hiyo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa upungufu wa vitanda, magodoro na masuka katika hospitali nyingi nchini ni changamoto hasa katika wodi za akina mama na watoto Benki ya KCB iliamua kutoa msaada huo ilikupunguza changamoto hizo.

Akitolea mfano wa michango iliyotolewa na benki hiyo katika kupunguza viwango vya vifo vya kinamama na watoto nchini, Manyenye alisema: “Kupitia miradi hiyo Benki ya KCB Tanzania imeshazisaidia hospitali zaidi ya 15 kwa kuzipatia vifaa tiba mbalimbali.”

Mkuu wa Masoko, Mawasililiano na Mahusiano wa Benki ya KCB, Christine Manyenye (kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni moja kati ya Vitanda na Vifaa vingine vyenye thamani ya Tsh 6,017,00/= kwa wodi ya wanawake Hospitali ya Amana, Dar Es Salaam
Wafanyakazi wa KCB na Wauguzi wa Hospitali ya Amana wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Benki ya KCB kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya TSh . 6,017,000 kwa wodi ya wanawake leo kwenye Hospitali ya Amana Ilala, Dar Es Salaam.  

MAKAMU WA RAIS AISHUKURU BENKI YA NMB KWA KUTOA MSAADA WA VIFAA VYA AFYA NCHINI

$
0
0
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan, ameishukuru Benki ya NMB kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 108, mashine za kupumulia wagonjwa mahututi, vitanda maalum vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 kwenye kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Akipokea vifaa hivyo aliushukuru ongozi mzima wa Benki ya Nmb kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la afya katika wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine hapa nchini.Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Bi. Vicky Bishubo juzi alimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu msaada huo kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vyote vya wilayani Kisarawe.

Makamu wa Rais Suluhu Hassan alipokea msada huo mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Pwani.


Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu akiangalia mashine ya Oxygen iliyokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, NMB - Joseline Kamuhanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB – Vicky Bishubo kwaajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe. NMB ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Wa pili kutoka (kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya kitanda cha kujifungulia kilichokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Pia benki ilikabidhi jumla ya mashuka 108, vitanda vya kujifunguliwa, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 15. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Serikali wa Benki ya NMB, Vicky Bishubo na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa NMB - Joseline Kamuhanda.
 

SERIKALI YA TANZANIA YAANZA MAZUNGUMZO NA UJERUMANI YA MGAO WA MAPATO YATOKANAYO NA MJUSI MKUBWA ‘DINOSAUR’ KUPITIA WATALII

$
0
0
 Serikali ya Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  imesema ipo kwenye hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii  kupitia mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs ambaye ni kivutio cha kikubwa cha  utalii  katika jumba la  Makumbusho nchini Ujerumani

Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa  miaka  100 iliyopita katika eneo la Tendaguru  mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa  nchini Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho hiyo.

Amesema lengo la mazungumzo hayo ni kutaka  kujua kiasi gani  cha mapato yanayokusanywa na  namna gani  wanavyoweza kugawana mapato hayo   yatokanayo na watalii kupitia mjusi huyo baina ya Serikali hizo mbili.

Amesema mwelekeo wa  mazungumzo hayo yaitapelekea Serikali ya Tanzania kufanya uamuzi   wa kumrudisha mjusi huyo  au kumuacha kule kule   lakini akiwa  analiingizia pato taifa  

Ameyabainisha hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mIkakati ya  Serikali ya kuendeleza vivutio vya utalii kwa mikoa ya Kusini.

 Hata hivyo, Mhe.Hasunga amesema  uamuzi wa kumrudisha  mjusi huyo nchini utakuwa mgumu kwa vile sehemu kubwa ya mjusi huyo ameunganishwa unganishwa kwa kutumia vifaa maalumu.

Ameongeza kuwa kutokana na jinsi alivyounganishwa unganishwa na anakadiri wa kuwa na  urefu wa mita 13.7 kwenda juu  hivyo kumsafirisha itakuwa ngumu.

Katika hatau nyingine, Mhe Hasunga amesema hadi hivi sasa  Serikali ya Ujerumani haijaweza kuweka bayana kiasi cha mapato yanayokusanywa  kupitia Mjusi huyo licha ya kuwa Serikali hiyo  imekuwa ikifadhili miradi mingi ya uhifadhi nchini.

"Tunaamini kuwa pesa wanazofadhili miradi mingi ya Uhifadhi imekuwa inatokana na makusany okupitia Mjusi huyo Mkubwa" amesema Hasunga 

Hata hivyo,kuendelea kuwepo kwa masalia ya mjusi huyo katika Makumbusho hiyo kuna manufaa makubwa kwa vile anatambuliwa kuwa ni wa kutoka Tanzania,Hivyo ni Balozi wa Utalii na utafiti wa kisayansi anayeitangaza Tanzania sehemu mbalimbali duniani.
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live


Latest Images