Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

BENKI YA NMB KUONGEZA MARA MBILI KIWANGO CHA MIKOPO KWA KAMPUNI NDOGO NA ZA KATI

0
0

BENKI ya NMB imesema itaongeza kiwango cha mikopo inayoitoa kwa kampuni ndogo na za kati mara mbili zaidi na kufikia Shilingi trilioni tatu kwa miaka mitatu ijayo. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtengaji wa benki hiyo Bi – Ineke Bussemaker wakati akizungumzia udhamini wa NMB kwa hafla ya Kampuni Bora 100 zamwaka 2018/2019 (Top100 Mid-sized Companies' Survey).

Kwa miaka mitatu iliyopita, NMB imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.5 kwa kampuni ndogo na za kati. Akizungumza katika uzinduzi wa utafiti wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019 jijini Dar es Salaam jana, Bi. Bussemaker alisema kampuni zinazowekeza katika kufanya biashara kidigitali zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri kibiashara.

"Hatima ya uchumi wa nchi upo katika kufanya biashara kidijitali ili kuhakikisha mifumo ya utendaji inakwenda kwa kasi,” alisema na kuongeza kuwa kampuni zilizoweza kuweka mifumo sawa ya dijitali zipo katika nafasi bora zaidi ya kupata mikopo kutoka katika benki yake.

Alisema Benki ya NMB inazidi kuwekeza katika mifumo ya utoaji huduma kwa njia za kidijitali ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wanaohitaji huduma zake nchini kote. Kampuni Bora 100 Tanzania ni shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na KPMG.

Mbali na NMB, wadhamini wengine wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019 ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam na Azam Media na Hoteli ya Hyatt Regency.

Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu. 
Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu. 
Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu. 


NBC yapongezwa kwa kudhamini maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji mjini Mbeya

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo kutokana na udhamini wa benki hiyo katika maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya leo. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mariam Mtunguja. 
Mkuu wa Uhai wa Wateja wa NBC Tanzania, Gaudence Shawa (kulia) akizungumza na Mshauri wa Kilimo na Huduma za Fedha Vijijini wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Samora Lupalla (katikati) huku Ofisa Habari wa mfuko huo, Victor Kyando akiangalia katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya leo. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, William Kallaghe. 
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC Mkoa wa Tawi la Mbeya wakihudhuria hafla ya ufungaji wa meonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini humo leo. 

Dkt. Abbasi na Ujumbe wake watembelea Magazeti ya China, Atoa Wito Kuhusu Habari za Afrika

0
0

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, CHINA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano Oktoba 24, 2018 ametembelea magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

Akiwa katika vyombo hivyo, Dkt. Abbasi amesema kuwa China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu kwenye masuala mbalimbali hivyo ni muda sasa wa kufanyia kazi mkataba wa ushirikiano wa Tanzania na China kwenye masuala ya utamaduni na habari uliosainiwa mwaka 2016

"Lengo la ziara yetu ni kujifunza wenzetu mnavyofanya kazi na pia kutafuta namna ya kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya habari," ameongeza Dkt. Abbasi akiwa People's Daily. Amelitaka gazeti hilo linalomilikiwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na linalofikisha habari zake kwa wasomaji milioni 700 duniani kupitia mitandao mbalimbali kuenzi ushirikiano huo wa muda mrefu kwa kuzipa nafasi pia habari za maendeleo za Afrika na Tanzania.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete amewakumbusha viongozi wa chombo hicho kuzipa fursa habari za utalii hasa vivutio vingi vilivyoko Tanzania. Akiwa katika gazeti la China Daily lililoanzishwa na Serikali ya China zaidi ya miongo mitatu iliyopita, Dkt. Abbasi aliwaeleza wahariri wanaohusika na toleo maalum la Afrika kuzingatia kuwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania zina maendeleo na vivutio vya uwekezaji vinavyopaswa kujulikana kwa wekezaji wengi wa China maombi ambayo wahariri wa gazeti hilo waliyakubali.

Dkt. Abbasi anaendelea na ziara yake ambapo atatembelea television za China za CCTV na CGTN na baadaye kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Redio China.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano akifafanua jambo wakati kwenye kikao cha pamoja mara baada ya kutembelea waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi sambamba na Ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na baadhi ya Waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
Baaadhi ya waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China wakifafanua jambo kwa wageni wao kutoka nchini Tanzania (hawapo pichani) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,wakati wa kikao chao cha pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali kwa kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
Picha ya pamoja
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ( wanne  kulia ) akiwa na ujumbe wake ambapo Jumatano Oktoba 24, 2018 walitembelea magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

IGP SIRRO AWATAKA WANANCHI WA UVINZA MKOANI KIGOMA KUENDELEA KUTOA TAARIFA SAHIHI ZITAKAZOFANIKISHA KUWAKAMATA WALIOJIHUSISHA NA MAUAJI YA ASKARI POLISI

0
0




Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mlindoko, wakati alipowasilia wilayani Uvinza Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, kwa lengo la kuzungumza na wananchi kufuatia tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa askari wawili na wingine mmoja kujeruhiwa wakati wakitekeleza zoezi la kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Ufugaji Ranchi ya Taifa NARCO kwa kuendesha shughuli za kilimo kinyume cha sheria na taratibu za nchi. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wananchi (hawapo Pichani) wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kufichua uhalifu na wahalifu pamoja na watu wanaojihusisha na matukio ya mauaji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiondoka baada ya kumaliza mkutano na wananchi wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliojihusisha na tukio la kuwashambulia na kuwaua askari wawili na wananchi wawili wilayani humo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiondoka baada ya kumaliza mkutano na wananchi wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliojihusisha na tukio la kuwashambulia na kuwaua askari wawili na wananchi wawili wilayani humo. Picha na Jeshi la Polisi. 

KATIKA KUHAKIKISHA VODACOM INAWAFIKIA WATEJA WAKE,YAFUNGUA DUKA WILAYANI HAI,KILIMANJARO

0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai, Bw. Lengai Ole Sabaya akizindua rasmi duka la Vodacom Tanzania jana wilayani hapo ikiwa ni mpango wa kuhahakikisha wanafikia wateja wao wote, popote walipo. Kando yake ni Agripina Boisafi, Mkuu wa Duka hilo. 
Picha 3648: Mkuu wa Wilaya ya Hai, Bw Lengai Ole Sabaya akisaini kitabu cha kumbukumbu baada ya kuzindua duka la Vodacom Tanzania wilayani hapo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kazkazini, Brigita Steven na Mkuu wa duka hilo, Bi Agripina Boisafi (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom. 

HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA

0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

Hatimaye Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na viongizi wenzake nane wa Chadema, leo amepata wakili wa kumtetea dhidi ya kesi hiyo inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, 

wakili Jamuhuri Johnson amejitambulisha leo Oktoba 25.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja leo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH).Hatua hiyo imefikwa baada ya Wakili aliyekuwa akimtetea Msigwa, Jeremiah Mtobesya kujitoa Agosti 23, mwaka huu.

Wakili Jamuhuri amedai kulingana na umuhimu wa kesi hiyo ameomba ahirisho ili apate muda wa kupitia jalada la kesi hiyo na na pia ameomba kupatiwa mwenendo mzima wa kesi tangia ilipoanza ili aweze kumwakilisha mteja wake huyo vizuri.

Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo ya wakili Jamuhuri na kudai kuwa wanapinga kwa sababu kwa kuangalia mwenendo wa kesi hiyo ni wazi katika kesi ya msingi hakuna hatua yoyote iliyopigwa zaidi ya washtakiwa kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Katika kuwasomea washtakiwa Maelezo ya awali (PH) wahusika wakuu ni washtakiwa ambao wakisomewa ndiyo wanawajibu wa kujibu kipi wanakubali na kipi hawakikubali. Baada ya Nchimbi kueleza hayo, wakili wa Msigwa, Jonson alieleza kuwa mteja wake siyo mwanasheria kuna maelezo ambayo amempatia hayaelewi vizuri ndiyo sababu aliomba kupitia jalada.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi, mwaka huu asubuhi kwa ajili ya PH.Mbali na Msigwa washtakiwa wengine ni ambao wanatetewa na Wakili Kibatala ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WANAOPISHA MRADI BANDARI MPYA BAGAMOYO KUVUTA SUBIRA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WAKAZI wa kijiji cha Pande, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ambao wamehamishwa kupisha mradi wa bandari mpya ya Bagamoyo wameiomba serikali kuwasaidia kulipwa fidia na kuhamishiwa katika makazi mapya .

Akitoa kilio hicho kwa niaba ya wakazi wa maeneo hayo ,wakati makamu wa Rais Samia Suluhu alipokwenda eneo la Mbegani kutembelea ujenzi huo, mwenyekiti wa kitongoji cha Pande Muhsin Mweka alisema  walipangiwa kwenda eneo la Kitopeni na Kidagoni lakini wameshindwa kwenda kutokana fidia kutokamilika.

Alisema kuwa  baadhi ya watu walilipwa fidia lakini wengine hawajalipwa huku wengine wakiwa wamepunjwa fidia zao kwa kulipwa kidogo fedha ambazo hazitoshi kununulia maeneo mengine."Wapo waliolipwa hapa hadi laki moja, milioni tano na milioni moja kiasi ambacho hakikidhi, hatujakataa kupisha mradi ila makubaliano yetu hayajatekelezwa "alisema Mweka. 

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa Kijiji hicho kina kaya 2,200 sawa na watu 16,500 ambao wanatakiwa kuhama eneo hilo.Kawambwa alieleza, jambo hilo limekuwa ni changamoto kubwa hivyo kuna haja ya kuhakikisha suala hilo linafikia mwisho.

Akijibu hoja hizo,makamu wa Rais  Samia Suluhu alisema , suala hilo amelichukua na atalipeleka kwa Rais baada ya kukaa na mamlaka husika ,wizara ya ardhi, bandari na EPZA ili kulipatia ufumbuzi. Samia alifafanua malalamiko yote yatafanyiwa kazi na serikali haitadhulumu mtu haki yake.

Alisema kuhamisha watu hao ni fedha nyingi zinahitajika na kuna taarifa kuwa hata wale walioko eneo la Kitopeni na Kidagoni bado hawalipwa fidia zao .Alifafanua apewa taarifa awali kuna watu 600 walipatiwa fidia ambazo hazikuwa haki zao ambazo zingesaidia kuwalipa waliostahiki. Samia aliwahakikishia serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinafuatilia wahusika hao ili kurejesha fedha hizo. 

Aliitaka halmashauri kuziweka fedha za fidia ya shule na zahanati zinazotolewa eneo hilo bila kutumia kwa matumizi mengine kwani inapaswa nguvu zao zibakie. 

Mtaka atoa wito kwa NSSF kuhamasisha zaidi wajasiriamali wadogo wadogo kujiunga na mfuko huo

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa NSSF alipotembelea banda hilo katika maonesho ya SIDO mkoani Simiyu.(wa pili kushoto ni Afisa matekelezo wa NSSF Simiyu Mr Khalid Omar, wa Tatu kushoto ni Stara Masatu ambaye ni Afisa mwandamizi wa NSSF Shinyanga,Katikati ni Abasi Cothema, Afisa mwandamizi sekta isiyo rasmi, na wa kwanza kulia ni Nuhu Ramadhani ambaye ni Mkuu wa Kituo cha NSSF Simiyu.Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Mtaka ametoa wito kwa NSSF kuwekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha wajasiriamali wadogowadogo wanajiunga na NSSF
Afisa matekelezo wa NSSF Bwana Abdul- Aziz Abed akitoa elimu kwa wageni waliotembelea Banda la NSSF wakati wa maonesho ya SIDO yanayoendelea Mkoani Simiyu

WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA WAPIGWA MSASA KUHUSU UHIFADHI WA MAZINGIRA NA WANYAMAPORI

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET) John Chikomo akifafanua jambo kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) wa kwanza kushoto pamoja na waandishi wengine wa vyombo vya habari wakisikiliza mada kwenye semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi kuhusu sekta ya uhifadhi wa wanyamapori
 Mwanasheria kutoka Timu ya Wanasheria  waliobobea katika  mazingira (LEAT) Stanslaus Nyembea akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari za mazingira inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
 Mwakilishi kutoka USAID Protect Symphrose Makungu akizungumza kwenye semina ya Waandishi  wa habari za mazingira ambayo imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) nchini ya ufadhili wa USAID Protect
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) na watoa mada.

Makamu wa rais atembelea mradi wa ujenzi wa tenki la maji la Bagamoyo leo

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ametembelea mradi wa ujenzi wa  tenki la maji la Bagamoyo lililojengwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA).

Mama Samia akiwa katika ziara ya siku tano Mkoa wa Pwani kuanzia Oktoba 24 hadi 29 atatembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Kisarawe ulio chini ya Mamlaka hiyo.

Akielezea mradi huo kwa Makamu wa Rais, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa mradi huu ni msaada kutoka benki ya Exim unaotarajiwa kukamilika Desemba Mwaka huu.

Kwenye mradi huo wa Bagamoyo, Mama Samia ametembelea  ujenzi wa tenki  lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milioni 6 kwa siku likiwa ni moja kati ya mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.

Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ulianza rasmi mwezi Machi mwaka 2016 na utakamilika 2018.

Kazi zinazofanyika chini ya mradi huu na katika mfumo unaohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita Milioni 3.0 hadi 6.0.

Mbali na mradi wa matenki, kuna ujenzi wa vituo vinne vya kusukumia maji, ununuzi wa transfoma na ufungaji wa umeme wa msongo Mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji mitaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya Kilometa zipatazo 80.

Utekelezaji wa mradi huo kwa sasa  unaendelea vizuri na mwaka huu wananchi wa maeneo yatakayopita mradi wa Bagamoyo wameanza kufaidika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan akizungumza mara baada alipotembelea mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita Milioni sita kwa siku.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akzungumza wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan alipotembelea mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita Milioni sita kwa siku.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuelezea Makamu ww Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu mradi wa maji wa Bagamoyo unaotekelezwa na Mamlaka hiyo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati alipotembelea ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita Milion sita kwa siku.

Benki ya Exim Tanzania yajipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa msimu wa 2018

0
0
BENKI ya Exim Tanzania imejipanga kusaidia wakulima wa korosho mkoani Mtwara kwa uwekezaji wa shilingi milioni 200 ili kuongeza uzalishaji wakati wa msimu wa korosho wa 2018.


Sekta ya ulimaji wa korosho nchini Tanzania hivi karibuni imeshuhudia ukuaji wa kiasi kikubwa kwa kuongezeka uzalishaji na bei ya kuuza ambayo ikiwa ni hatua muhimu ya kuboresha maisha ya mkulima.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania Jafari Matundu, alisema katika mahojiano kwamba benki hiyo imekuwa ikisaidia wakulima na wasafirishaji wa korosho kwa miaka mingi kwa kuwapatia huduma mbalimbali za kifedha zilizo bora kabisa. "Tumekuwa mkoani Mtwara kwa miaka mingi sasa tukifanya kazi pamoja na wakulima na wasafirishaji wa korosho kwa kuwapa huduma za kisasa za kibenki kwa nia ya kusaidia kukuza biashara zao."

Benki ya Exim Tanzania ilifungua biashara mkoani Mtwara kusaidia wakulima wa korosho kwa sababu ni sehemu muhimu katika sekta ya kilimo nchini Tanzania. Kwa sasa, nchi inasafirisha korosho ghafi zaidi ya tani 350,000, ambayo ni ongezeko la karibu asilimia 100 kutoka miaka ya nyuma.

Benki ya Exim Tanzania imedhamiria kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania na kupanua biashara yao ili kufikia maeneo mengi zaidi nchini ili kuweza kutoa huduma za kibenki za kibunifu na muhimu kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kilimo. Benki ya Exim hutoa huduma kwa wakulima kupitia Vyama vya Ushirika vya Kilimo na Masoko (AMCOS) Mtwara na Tandahimba. AMCOS ni jukwaa muhimu linalosaidia wakulima katika hatua za uzalishaji, usindikaji, usafirishaji na masoko wa mazao mbalimbali ya biashara ikiwa ni pamoja na korosho.

Mkurugezi Matundu aliongeza, "Kutokana na kuongezeka kwa bei za usafirishaji na uuzaji benki yetu iliona ni muhimu kuongeza uwekezaji kwenye kitabu cha mikopo ili kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zao na hivyo kuongeza mapato yao kupitia mauzo yao. Wakulima wanahitaji usaidizi katika hatua zote za kilimo, kuanzia katika kuvuna, kununua mifuko, kulipa wafanyakazi hadi bidhaa kufikia mnunuzi.

Benki ya Exim imeadhimisha miaka 21 ya mafanikio katika ukuaji na uongozi katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim Tanzania ilianzishwa mwaka 1997 na kupanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika visiwa vya Komoro (2007), nchini Djibouti (2011) na Uganda (2016). Exim inajivunia kuwa benki kwanza kufungua matawi nje ya nchi. Lengo lake kuu ni kujenga thamani ya uwekezaji kwa wanahisa wake na kufikia ukuaji kupitia utoaji wa huduma za tofauti na zinazolenga mteja.

UNESCO kufunza elimu ya dijiti kwa wanafunzi 200

0
0
SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepanga kufunza wanafunzi 200 kutoka shule sita nchini namna ya kutengeneza mfumo wa alama zinazotumiwa katika maandishi ya kompyuta na matumizi yake.

Wanafunzi hao 200 watakuwa miongoni mwa vijana zaidi ya 2,489 waliofunzwa kuendeleza utaalamu wa kidijiti kwa ajili ya maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa yenye kauli mbiu “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” mafunzo yalifanyika katika shule ya sekondari ya Chazinge.Hatua hizo zimelenga kuwezesha njia ya kuelekea uchumi wa viwanda nchini Tanzania.

Pamoja na shule ya sekondari ya Chazinge na Kimani iliyopo Kisarawe mkoani Pwani nyingine ni Jamhuri, Gerezani na Benjamin Mkapa zilizopo Ilala mkoani Dar es Salaam.Katika mafunzo hayo UNESCO watahakikisha kwamba vijana wanakuwa wavumbuzi, wabunifu na hivyo kutumiwa kuboresha namna bora ya kufanya biashara miongoni mwa vijana wa kike na wakiume.

Taarifa hiyo imesema kwamba lengo kuu ni kuwezesha vijana hasa wanawake kutumia kikamilifu mifumo ya tehama kujiendeleza katika masomo ya  Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM).
Alisema mafunzo hayo yataongeza pia uwezo wa vijana kujiajiri na kuajiriwa kwa kuwa na ujuzi zaidi.Mradi wa mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa UNESCO unaofanyiwa kazi katika nchi zaidi ya 25 unatambuliwa kama Youth Mobile Initiative kwa lengo la kuboresha hali za uchumi za mataifa hayo kupitia matumizi ya kompyuta.

UNESCO katika kuendeleza vijana imeshirikiana na Apps and Girls kuendesha tamasha la nne la Africa Code Week linalofanyika katika nchi 36 za Afrika tangu lianzishwe mwaka 2015.Imeelezwa katika taarifa hiyo kwamba jumla ya vijana milioni 1.8 wamefunzwa masuala ya dijiti kuelekea karne ya 21.Mafunzo hayo yamalenga kuhakikisha kwamba wanakuza uwezo wao wa kutumia alama za siri kutengeneza programu mbalimbali kwa matumizi anuai.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chanzige iliyopo wilayani Kisarawe kuhusu nafasi ya vijana katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo  hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Mkufunzi Kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bw. Wilhelm Oddo akitoa utangulizi wa elimu ya Tehama kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe. Haya ni moja kati ya mafunzo ya Tehama yameandaliwa na Shirika hilo lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO  wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yenye lengo la kuongeza ushiriki wa mtoto wa kike katika masomo ya Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM) yaliyoambatana na sherehe za  maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo  hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
 Wakufunzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Balbina Gulam (kushoto) na Raymond Benedict (kulia) wakiendesha mafunzo ya Tehama kwa vitendo kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.

MKUCHIKA AMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU DKT. GARIB BILAL

0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali..
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (kulia) akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

WATENDAJI WAKUU MAMBO YA NDANI YA NCHI WAENDELEA NA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE JIJINI DODOMA

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (katikati), akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba (kulia) wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. 
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

JET YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI KUHUSU UHIFADHI WA WANYAMAPORI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET)kimeamua kuwajengea uelewa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanyamapori nchini

Akizungumzia semina hiyo inayofanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Mkurugenzi Mtendaji John Chikomo amefafanua lengo kubwa la mafunzo ni kuwajengea uelewa waandishi hao kuhusu sekta yenyewe na kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori.

Pia amesema lengo lingine la semina hiyo ni kutangaza utalii wa ndani ili uweze kueleweka kimataifa na kuwashawishi sekta binafsi kuwekeza kwenye uhifadhi na utalii.Chikomo amefafanua ni matarajio yao baada ya mafunzo hayo waandishi watakuwa na uelewa mpana kuhusu uhifadhi wa mazingira na wanayama pori na baada ya semina hiyo waandishi watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo kwa kutembelea hifafhi za wanyamapori.

"Tumeanza na mafunzo haya na baadae tutaendelea na hatua nyingine zinazofuata ikiwemo ya waandishi husika kwenda kufanya uchunguzi kwa kuandika habari zinazohusu mazingira na uhifadhi." Mafunzo haya ni sehemu ya mradi unaoshughulikia kuendeleza uhifadhi mazingira ambapo ndani yake pamoja na kuangalia mafanikio pia unashughulika na changamoto zinazohusu uhifadhi,"amesema.

Wakati huo huo baadhi ya watoa mada wameeleza kwa kina kuhusu historia ya uhifadhi wa wanyamapori na mazingira pamoja na sheria mbalimbali zilizopo kwa nyakati tofauti na namna ambavyo zinafanyakazi nchini.

Mmoja wa watoa mada Stanslaus Nyambea kutoka Timu ya Wanasheria wabobezi kwenye masuala ya mazingira( LEAT) amezungumzia sheria ya fidia kwa watu wanaopata madhara kutoka kwa wanyama aidha iwe kwa kusababisha kifo au kuharibu mali ambapo sheria hiyo inaonekana kuwa na mlolongo mrefu wa kupata fidia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET) John Chikomo akifafanua jambo kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina ya mafunzo ya waandishi wa habari za mazingira.

Wanaotoa Vitisho kwa Walimu Wapewa Angalizo

0
0
Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutaindurwa amewashauri watendaji wanaojikita katika kutoa vitisho kwa walimu badala ya kutafuta mbinu bora za kuwasaidia kuacha kufanya hivyo ili Walimu wasijiingize katika makosa ya kinidhamu kwa kisingizio cha kuogopa vitisho.

Rutaindurwa ametoa kauli hiyo hivi karibuni jijini Dodoma alipokutana na Maafisa Elimu, Wathibiti Ubora, Waratibu Elimu Kata (Maafisa Elimu Kata), Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Lengo la mkutano huo lilikuwa kuwaelimisha Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kuzingatia  maadili na nidhamu kwa mujibu wa  Sheria, Kanuni, Taratibu pamoja na Miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.

Alisema kuwa walimu hawapaswi kuishi kwa hofu kila wakati kutokana na vitisho wanavyopata kutoa kwa baadhi ya watendaji badala yake wanatakiwa kutekeleza majukumu yote kwa kuzingatia misingi na taratibu za utumishi wao.

Rutaindurwa alionesha kukerwa na baadhi ya watendaji wanaowasimamia walimu ambao kazi yao ni kutoa vitisho vya kuwafukuza kazi au kuwavua madakara endapo malengo flani hayatafikiwa bila kusaidia kutatua changamoto zinazokabili Walimu kufikia malengo.

“Unakuta mtu anakuambia wanafunzi wote wasipofaulu nakushusha cheo au nakufukuza lakini wala hamsaidii mkuu wa shule au mwalimu mkuu kutatua baadhi ya changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wake” alisema.

Aliongeza kuwa vitisho hivyo vimesababisha baadhi ya walimu kujikuta wakitenda makosa ya kinidhamu ili waonekane wamekidhi matakwa ya wanaowasimamia na matokeo yake wanachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.
 Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akitoa hotuba mbele ya Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata na Wathibiti Ubora (hawapo pichani) wa Manispaa ya Jiji la Dodoma katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Msaidizi Wilaya ya Dodoma, Bibi Leticia Mwakasitu na Kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Bw. Abdallah Membe.
 Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule wa Halmasahauri ya Jiji la Dodoma wakiwa katika hali ya furaha wakati wa Mkutano wao na Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutaindurwa ( hayupo pichani) uliofanyika jijini Dodoma.
 Walimu wakiwa katika hali ya utulivu wakimsikiliza Katibu, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutaindurwa (hayupo pichani) akiwaelimisha juu ya Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Walimu.
 Mmoja wa Walimu akiuliza swali kwa Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutaindurwa (hayupo pichani) katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Dodoma.
 Mmoja wa Walimu akiuliza swali kwa Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutaindurwa (hayupo pichani).
Mmoja wa Walimu akiuliza swali kwa Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu, Winifrida Rutaindurwa (hayupo pichani).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA RIPOTI YA KAMATI YA KUCHUNGUZA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa  ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo.

Amepokea ripoti hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 25, 2018) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao.Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini.

“Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.”Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa kazi.

MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40 waliokolewa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara (kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera na Uratibu, Profesa Faustin Kamuzora na  wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera  na Uratibu) Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti wa Kamati  iliyoundwa na Serikali  Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali, George Waitara  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT TIZEBA ATEMBELEA MAONESHO YA SIDO ASISITIZA UMUHIMU WA VIWANDA VIDOGO NCHINI

0
0

Na mathias Canal-WK, Bariadi-Simiyu

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) leo Alhamisi Octoba 2018 amewataka wajasiriamali kote nchini kuchangamkia fursa ya kutembelea katika Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Katika maonesho hayo ambayo yalianza Oktoba 23 mwaka huu, Dkt Tizeba amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wananchi kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

"Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani kama Mara, Mwanza na Shinyanga wajitokeza kwa wingi kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa muhimu kwao katika kuakisi kwa vitendo Tanzania ya viwanda" Alisema Dkt Tizeba

Dkt Tizeba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa kubuni jambo hilo sambamba na kumpongeza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwa kuwaalika wajasiriamali, na wataalamu waoneshaji wa teknolojia mbalimbali kwani jambo hilo litatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

Aidha, Dkt Tizeba amesema kuwa Maonesho hayo ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao.Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO) yakiwa na Kauli Mbiu isemayo PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”. yalifunguliwa rasmi na Waziro Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo wakati akikagua mashine zinazotengenezwa na SIDO TDC kwa ajili ya uchakataji wa mazao mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.

DKT SHEIN .AKUTANA NA MRATIBU WA UN

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) hapa Zanzibar Bibi.Dorothy Temu-Usiri (katikati) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.] 25/10/2018. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akimsikiliza  Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) hapa Zanzibar Bibi.Dorothy Temu-Usiri walipokuwa katika mazungumzo wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao (hawapo pichani),[
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na ujumbe wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) hapa Zanzibar Bibi.Dorothy Temu-Usiri (wa pili kulia) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo

Tanzania na Ubelgiji Kushirikiana Sekta ya Uwekezaji

0
0
Na  Paschal Dotto-MAELEZO 

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imezitaka sekta binafsi na makampuni kuchangamkia fursa za uwekezaji na biashara ili kuweza kuimarisha mitaji yao pamoja na kupanua wigo wa masoko na kutangaza fursa za uwekezaji kwa kushirikiana na makampuni ya nchi za nje.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika kongamano la kibiashara linalohusisha makampuni zaidi ya 41 kutoka nchini Ubelgiji na sekta binafsi 200 kutoka Tanzania, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Injinia Stella Manyanya, amesema kuwa Tanzania na Ubelgiji zimekuwa na mashirikiano ya siku nyingi katika masuala ya kiuchumi.

“Nchi ya Ubelgiji tunashirikiana nayo kwenye masuala ya bandari za Dar es Salaam na Zanzibar, lakini pia natambua kuwa Ubelgiji wana mahusiano na nchi za Rwanda na Congo kwa hiyo ni rahisi kuunganisha ukanda huu kwa kutumia bandari zetu na kufungua biashara katika ukanda huo”, alisema Injinia Manyanya.

Aidha, Injinia Manyanya alibainisha kuwa kongamano hilo litafungua ukurasa mpya kwa jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwani amekuwa akisisitiza masuala ya uwekezaji ili kujenga Tanzania ya Viwanda ambapo ameweza kuzuia rushwa, urasimu na ufisadi kitu ambacho kimevuta wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.
Naibu Waziri , Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Injinia Stella Manyanya akiwahutubia washiriki wa kongamamano la uwekezaji na biashara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo uliofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki wa kongamano la uwekezaji baina ya Makampuni 41 kutoka Ubelgiji na Sekta binafsi 200 kutoka Tanzania wakifuatilia mazungumuzo ya kongamano hilo yaliyofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),John Mnali akiwasilisha maada kwa washiriki wa kongamano, kuhusu fursa zinazopatikana nchini pamoja na huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa wawekezaji .

Washiriki kutoka Tanzania wakifuatilia mazungumuzo katika kongamano la uwekezaji na biashara yalifanyika mapema leo katika ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),John Mnali akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano ( hawapo pichani), kuhusu fursa zinazopatikana nchini pamoja na huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania, katika kongamano linalofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO) .


Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images