Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

MSIMU WA FENESI

$
0
0
Mafenesi yakiwa juu ya  mti.
  Mafenesi yakiwa  kando ya Barabara ya Kilwa kwaajili ya kusafirishwa katika  kijiji cha  Kimanzi chana leo Wilaya Mkuranga mkoa wa Pwani.
 Mfanyabiashara wa  mafenesi katika kituo cha mabasi Mbagala jijini Dar es Salaam   akiwauzia wateja wake baada ya msimu wa matunda hayo kuanza ambapo fenesi moja huuzwa kati ya sh 1500 hadi sh 4000 kutokana na ukubwa wake.
(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Fenesi Sokoni.

NDITIYE AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA TEHEMA, KAMPUNI YA BCX YAWA KIVUTIO KWA WADAU

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian0-Uchukuzi na Mawasiliamo Atashasta Nditiye  amezindua mkutano wa siku 3 wa wanatehama ili  kujadili masuala ya tehama na maendeleo ya viwanda nchini.

Nditiye amesema kuwa mkutano huo utawasaidia wananchi kutapata uelewa wa matumizi bora na usalama katika mitandao ya kijamii na amewataka wanatehama wote kutambulika na vyombo husika na wao kama serikali wanafanya kazi na watakaovuruga tasnia hiyo hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

Kwa upande wao kampuni ya Bussiness Connexion (BCX)  wanaojihusisha na masuala ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa mbalimbali pamoja na komputa za aina zote  kutoka makampuni ya HP  na DELL, kutoa wataalamu wa kompyuta kwa makampuni, kutengeneza programu za simu na huduma za malipo wameshiriki semina hizo na kuwa kivutio kwa wadau wengi wa tehama.

Akizungumza na blogu ya jamii Afisa mauzo na masoko wa BCX  Justine Lawena amesema kuwa wameshiriki semina hiyo katika kujitangaza na kuonesha uwezo wao kwa serikali na wadau wa tehama na wao kama kampuni wana wataalamu wa kompyuta wakutosha  hivyo serikali na taasisi binafsi kutumia fursa hiyo.

Ameeleza kuwa katika kuendeleza sekta ya tehama wanatoa huduma za kuuza na kutengeneza mashine za kutoa pesa (ATM) na hadi sasa wanamiliki na kuendesha mashine zaidi ya 200 nchini.

Aidha amesema kuwa katika kurahisha huduma za malipo kwa kipindi cha mwaka mmoja wamekuwa wakifanya majaribio kupitia kadi zao za uhuru pay ambazo huwasaidia wananchi  kulipa nauli katika usafiri wa daladala na majaribio yalifanywa kwenye daladala zinazofanya safari kutoka Kivukoni hadi Tegeta nyuki na imeonesha mafanikio makubwa na wamejipanga kueneza huduma hiyo katika maeneo mbalimbali.

Akizungumzia mafanikio ya kampuni yao Lawena amesema kuwa hadi sasa wanatoa huduma za kibenki kwa benki 28 kupitia huduma ya umoja switch na kutoa huduma za kibenki kupitia mawakala na kubwa zaidi ni kumiliki na kuendesha zaidi ya mashine za ATM zaidi 200 nchini.

Lawena amewashauri na kuwahimiza wamiliki wa mabenki nchini kutumia huduma zao kwani wanauwezo wa kufungua matawi kupitia (ATM) katika maeneo yote nchini na kuziendesha ipasavyo.
 Afisa mauzo na masoko wa kampuni ya BCX  Justine Lawena akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian0-Uchukuzi na Mawasiliamo Atashasta Nditiye  katika banda lao katika maonesho ya wadau wa tehama nchini.
 Afisa mauzo na masoko wa kampuni ya BCX Justine Lawena (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau waliotembelea banda lao.
Afisa mauzo na masoko wa kampuni ya Bussiness connexion (BCX) Justine Lawena (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian0-Uchukuzi na Mawasiliamo Atashasta Nditiye wakati wa ufunguzi wa semina ya tehama kwa wadau.

MAHAKAMA YAAMURU PEDESHEE NDAMA MTOTO WA NG'OMBE AKAMATWE

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru kukamatwa kwa Mfanyabiashara, Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe, baada yakushindwa kufika Mahakamani bila kutoa taarifa. 

Hati hiyo ya kukamatwa imetolewa leo Oktoba 24.2018 na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Maira Kasonde, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani. 

Aidha Hakimu Maira ametoa barua ya wito kwa wadhamini wa mshtakiwa huyo kufika mahakamani na kueleza alipo mshtakiwa. 

Kabla ya kutolewa kwa amri hiyo ya kukamatwa kwa mshtakiwa, wakili wa Serikali, Mosia Kaima, alidai kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini mshtakiwa hayupo n ahata mashaidi wake pia hawapo. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 12. 2018 kesi hiyo itakapokuja kwa kutajwa. 

Ndama anakabiliwa na mashtaka matano yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, 

Mshtakiwa anadaiwa kughushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Pia anadaiwa kughushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

KIGAMBONI INTERNATIONAL MARATHONI KUFANYIKA DESEMBA 2 MWAKA HUU

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


KATIKA jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni International Marathon, mbio hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio hizo ambaye pia ni kocha wa michezo ya riadha na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Riadha ya Walemavu Tanzania alisema, Lengo kuu la “Kigamboni International Marathon” ni kuchochea shughuri za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji,Biashara na vivutio vya kitalii Vilivyopo Kigamboni na maeneo ya karibu, Kuimarisha Afya pia Kuhamasisha michezo ya Riadha kwa maendeleo ya Taifa letu.

Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa „kigamboni International Marathon‟ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.

Muandaaji wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Kigamboni Dimo Debwe akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kutambulisha Mbio hizo zitakazo fanyika Desemba 2 Mwaka hu kuanzia eneo la Fun City Mpaka Daraja la Kigamboni.

Mmoja wa Wafadhili wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa, Sunil Rodrigues akieleza kwanini mbio hizo zitafanyika katika eneo la Fun City Kigamboni.

Mratibu wa Masuala ya Habari wa Mbio za Kigamboni, mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya ushiriki wa Wanahabari Kumi katika Mashindano hayo.

Uongozi wa Mashindano ya Riadha ya Kigamboni Marathoni wakionyesha Flana zitakazotumika katika Mbio za Kigamboni Intenational Marathon.

NORA MZERU KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUGUSHI CHETI CHA NDOA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa. 

Wakili wa serikali Mwandamizi, Ester Kyara amedai mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule. 

Kwa kua katika siku isiyojulikana jijini Dar, es Salaam, kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati wakati wakijua si kweli. 

Hata hivyo, mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, amekana na ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana. 

Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya Sh 2milioni.  Kesi imeahirishwa hadi Novemba 21, mwaka huu.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru (Picha ya zamani).
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru akiwa katika mahakama ya Wilaya ya Ilala leo akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa. 

BENKI YA TIB CORPORATE YASHIRIKI MAONYESHO YA SIDO YA KITAIFA MKOANI SIMIYU

$
0
0
BENKI ya TIB corporate  imeshiriki katika maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.


Maonyesho hayo yalizinduliwa jana  Oktoba 23 na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa na kuudhuriwa pia na viongozi wengine pamoja na waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashra Dkt.Stella Manyanya.

 Kauli Mbiu ya maonyesho haya ni “Pamoja Tujenge Viwanda kufikia Uchumi wa Kati”

Benki ya TIB Corporate ikiwa ni mdau wa karibu wa maendeleo mbali mbali tayari imeshatoa mkopo wa shilini bilioni 1.5 kwa wilaya ya Bariada kuwezesha mradi wa upimaji wa Viwanja vya mipango miji mkoani humo.


 Kwa sasa Benki ya TIB Corporate inashirikiana na SIDO ili kuvumbua fursa ambazo benki itaweza kuwapatia wajasiriamali wa viwanda vidogo na kukuza biashara zao

Benki ya Corporate ni Benki ya biashara na inatoa huduma zote za kibenki kwa watu binafsi, Makampuni Binafsi, taasisi za serikali, NGOs na watanzania wote kwa ujumla.

Lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanaweza kupata huduma bora za kibenki kwa ufanisi Zaidi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege mara baada ya kutembelea banda la TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu. 
Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka akimkabidhi mkoba kutoka benki ya TIB Corporate mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea banda la Benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka mara baada ya kutembelea banda la benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka mara baada ya kutembelea banda la benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.

SWALA LA HUDUMA YA JAMII NI LAZIMA KWA WAMILIKI WOTE WA MIGODI NCHINI-BITEKO

$
0
0
Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Madini, Dotto Butiku ameagiza wamiliki wote wa migodi nchini kuzingatia takwa la kutoa huduma  kwa jamii katika sehemu ilipo migodi yao kuwa sio ni ombi ni lazima kwa mujibu wa sheria ya Huduma kwa Jamii.

Waziri Biteko amesema hayo alipokuwa kifunga ziara yake katika Wilaya ya Mkuranga ambapo alitembelea katika Mgodi wa Mchanga Mwanadilatu na Kiwanda cha Kioo ambao wanachimba Mchang akatika eneo la Vianzi.

"Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na Marekebisho yake ya mwaka 2017 inamtka kila mwekezaji kuandaa mpango wa huduma kwa jamii na kuupeleka Halmashauri kwa ajili ya kupitishwa lakini tumeona wachimbaji wengi wamekuwa wakifanya vile wanavyotaka wao hivyo tunawaomba wote wawasilishe mpango huo hili wanachi ambao ndio waathirika wakubwa na uchimbaji huo nao wapate faida kwani jambo hili sio la hiari ni lalazima "amesema Waziri Biteko.

Aidha Waziri Biteko ametoa Maagizo kwa Mwekezaji wa Mwekezaji wa Kioo kuwasilisha risiti zote za uuzaji na ununuzi wa mchanga kwa watalaamu wa madini wa Kanda ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro hili waweze kupangiwa kiasi sahii cha Mrabaha unaotakiwa kuingia Serikalini kama kanuni zinavyotaka kulipa pesa kutokana na bei ya mauzo ya Mwisho.
 Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Mchanga wa Mwanadilatu Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wakati wa Ziara yake ya kukagua migodi na mfumo wa ulipaji mirabaha kwa wachimbaji.
 Mmoja wa Wamiliki wa Mgodi wa Mchanga katika Mtaa wa Mwanadilatu Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Francis Magua akitoa Malalamiko yake mbele ya Naibu waziri wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini katika migodi ya Wilaya hiyo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Juma Abedi akizungumza na Naibu waziri wa Madini juu ya Matatizo yanayofanywa na Muwekezaji wa Kiwanda cha Kioo ambaye anajiusisha na uchimbaji mchanga katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa Madini,Dotto Biteko akikagua eneo la Kiwanda Cha Kioo ambao wanajihusisha na shughuli ya uchimbaji wa Madini ya Mchanga kwa ajili ya utengenezaji wa Vioo.

PICHA MBALIMBALI ZA USAFIRISHAJI WILAYANI MKURANGA

$
0
0
 Mmoja waendesha Pikipiki Katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani akiwa amepakia Mzigo wa Mkaa kuzidi uwezo wa chombo chake akipita katika Barabara ya Kilwa kuelekea Dar es Salaam, hali inayohatarisha usalama wake.
Wasafirishaji wa Mkaa kwa kutumia Baiskeli katika kata ya Vianzi wakielekea barabarani kwa ajili ya kutafuta Masoko 
Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Mwanadilatu wakidandia gari ambalo limefika mgodini hapo kwa ajili ya kupakia Mchanga  (PICHA ZOTE NA HUMPHREY SHAO)

Twanga Pepeta yatoa reflekta kwa bodaboda Kinondoni

MUHEZA WAMEELEWA KUWA NYUMBA NI CHOO-MPOTO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MSANII wa Muziki wa Kughani na Kiongozi wa Mjomba Bendi, Mrisho Mpoto amesema kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa  Mazingira na uhamasishaji wa ujenzi wa Vyoo bora iliyoanza mkoani Tanga katika Wilaya ya Muheza imeweza kubadilisha jamii ya wilaya hiyo kwa kiasi kikubwa.

akizungumza na Michuzi Media Mpoto amesema kuwa sote kwa umoja wetu kama Mjomba Bendi tumedhamiria kila jamii tutakoyoifikia inabdilika kwa kuwa na choo bora ambacho kitasadia kutunza na Mazingira hili kuepukana na magonjwa ya Mlipuko yanayotokana na kujisaidia hovyo.

"Sote kwa pamoja na umoja wetu Watnzania tudumishe uzalendo na kuhakikisha tunalinda afya zetu na familia kwa kuwa na vyoo vilivyobora kwa kuambiana ukweli kuwa 'tusichukulie poa nyumba ni choo"amesema Mpoto.

Mpoto amesema kuwa hakuna Raha Kubwa kama kuwa na nyumba yenye choo bora ambayo unasikia furaha kumkaribisha mgeni pindi anpohitaji kwenda msalani kuliko vile mtu anaomba kwenda msalani alafu unashikwa na kigugumizi.
Msanii wa Muziki wa Kughani na Kiongozi wa Mjomba Bendi Mrisho Mpoto akzingumza na Wakazi wa Kata ya Tingeni Wilayani Muheza Mkoani Tanga ambapo mrsho mpoto ameweza kufikisha ujumbe wa ujenzi wa Choo Bora kwa wakzi wa kata hiyo ambao wamehamsika kuwa na kuta nne za choo kwa kila nyumba kwa kuungna nae kuwa 'Usichukilie Nyumba ni Choo'
Mkuu wa Wilaya ya Muheza akiwasalimia wakazi wa Wilaya hiyo ambao wamefika kusikiliza kampeni ya Nyumba ni choo inayoongozwa na Mrosho Mpoto
 Wasanii wa Mjomba Bendi , Ismail na Nuruelly wakiwatumbuiza wakazi wa Muheza katika Kampeni ya Wizara ya Afya Msichukulie Poa Nyumba ni Choo.
 Sehemu ya Wakazi wa Kata ya Tingeni Wilaya ya Muheza wakifatilia Kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendeshwa bendi ya Mjomba chini ya mrisho Mpoto
 Sehemu ya Wakazi wa Kata ya Tingeni Wilaya ya Muheza wakifatilia Kampeni ya Nyumba ni Choo inayoendeshwa bendi ya Mjomba chini ya mrisho Mpoto.

UNICEF KUISAIDIA SERIKALI KUFANYA TAFITI ZA MAENDELEO YA MTOTO

$
0
0
Na: WFM – Dodoma

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), wameonesha nia ya kuisaidia Serikali ya Tanzania kufanya tafiti mbalimbali kuhusu maendeleo ya mtoto ili kukabiliana na changamoto zinazomkabili.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, baada ya mkutano wake na Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Leila Pakkala, uliofanyika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dodoma.Dkt. Mpango alisema kuwa Shirika la UNICEF, lina nia yakushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ili kuweza kufanya tafiti katika mikoa mbalimbali, kuzichapisha na kuzisambaza ili kuongeza uelewa wa watu kuhusu maendeleo ya watoto.

“Watu wengi wanajua uwekezaji kwa maana ya barabara na miundombinu mingine mikubwa lakini katika mazungumzo yetu tumesisitiza kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya watu hasa katika umri mdogo kwa kuwa usipowekeza katika umri huo na kuwekeza katika umri mkubwa matokeo yake hayawi mazuri.”, alisema Dkt. Mpango.

Alisema kuwa, maeneo ambayo ni muhimu kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na UNICEF ni pamoja na udumavu, elimu kwa ajili ya watoto hasa ambao hawajafikia umri wa kwenda shule na sheria ya mtoto katika kuhakikisha anakua salama kwa lengo la kulitumikia taifa kwa siku za usoni, hivyo alisisitiza kuwekeza mapema kwa mtoto katika afya, lishe, elimu, uhuru wao na usalama hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kulitumikia Taifa kwa wakati ujao.

Aidha Dkt. Mpango alisema kuwa, Serikali inafanya jitihada kubwa kusimamia maendeleo ya uchumi kwa ujumla, kwa kuwa Taifa lisipokuwa na uchumi imara haliwezi kuwekeza katika maendeleo ya watoto.Alisema bajeti zinatakiwa kuweka umuhimu wa kuwekeza katika mtoto hivyo kuna Kitengo kinachohakikisha bajeti ya Serikali Kuu na Halmashauri zinazingatia mambo ya msingi ambayo yatasaidia watoto wa Tanzania kuwa na maendeleo stahiki.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Leila Pakkala, amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika maendeleo ya mtoto jambo ambalo linastahili pongezi na pia ameipongeza Serikali kwa ukuaji wa uchumi, kupambana na rushwa, ujenzi wa miundombinu na kuongeza mapato ya ndani kupitia kodi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto- UNICEF, kwa juhudi zinazofanywa kuhakikisha maendeleo ya mtoto nchini Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla kwa kuwekeza katika lishe na elimu ili kuwa na kizazi kijacho chenye uelewa wa kutosha ili kuleta tija katika Sekta za Maendeleo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akieleza kuhusu Serikali kuwa na Dawati linaloshughulikia bajeti ya maendeleo ya watoto wakati wa Mkutano na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Leila Pakkala (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

Ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ukiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Leila Passala (katikati), wakifatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, (hayupo pichani) kuhusu elimu, lishe na sheria ya mtoto, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango na Ujumbe wa UNICEF ukiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Leila Pakkala katika Mkutano Jijini Dodoma.

Idadi wa wachangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF)waongezeka

$
0
0

Na.WAMJW,Bungeni,Dodoma
Idadi ya wanachama wachangiaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708 waliokuwa wameandikishwa  mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi Septemba 2018.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.
“Ongezeko hili limetokana na kanuni na misingi  inayotumika katika kuendesha utaratibu wa mfuko huu ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia viwango vya mshahara,usawa katika kupata huduma na ushiriki wa Serikali katika usimamizi kwa faida ya wanachama” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa kwa upande wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), jumla ya kaya zilizojiunga hadi Septemba mwaka huu ni 2,220,953 ikiwa ni sawa na wanufaika wapatao 13,506,330 sawa na asilimia 25 ya watanzania wote’ kwa hiyo mifuko hii yote inatoa huduma kwa watu 17,656,697 sawa na asilimia 33 ya watanzania wote kwa mujibu  wa idadi ya makadirio ya watanzania kwa sasa.Idadi ya wanufaika imeongezeka  kutoka 691,774 mwaka 2001/2002 hadi wanufaika 4,150,367 sawa na asilimia 8 ya watanzania wote” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka sasa idadi ya wanachama wengi waliojiunga  asilimia 67 ni watumishi wa umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa sharia.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema mfuko unaendelea kutoa elimu na kubuni vifurushi mbalimbali vitakavyovutia wananchi wengi kujiunga na kufaidika  na mfuko ambapo utawawezesha wanachama wengi zaidi kujiunga hasa wale wa sekta isiyo rasmi na kujiwekea malengo ya kuwafikia watanzia asilimia 50 mwaka 2020.
“Mfuko umekamilisha uandaaji wa vifurushi vya michango na mafao kulingana na uwezo wa wananchi kulipia bima  ya afya,suala hili lipo katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kwa utekelezaji”. Alisisitiza Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa mpango huo utamwezesha mwananchi kuchagua vifurushi vya aina mbalimbaliu vya huduma  anayoitaka kwa utaratibu utakaojulikana kama ‘JIPIMIE’ na wanachama watalipa kidogo kidogo kwa utaratibu ujulikanao kama ‘DUNDULIZA’ ambao tayari umeshakamilika.
 
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo  jijinini Dodoma ambapo alisema wachangiaji wa mfuko huo wameongezeka kutoka wanachama 164,706 mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 septemba mwaka huu.
IMG-20181024-WA0025
Mkurugenzi wa NHIF Bw.Bernad Konga akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ambapo alisema mfuko wake upo tayari kuanza mara moja kutoa huduma kupitia vifurushi vipya vitakavyojulikana kama JIPIMIE ili watanzania waweze kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini
IMG-20181024-WA0028
Wakurugenzi wa NHIF wakipitia taarifa ya mfuko huo wakati ikiwasilishwa kwenye kamati mapema leo
IMG-20181024-WA0030
Katibu Mkuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya(wa kwanza kulia),Mkurugenzi wa NHIF Bw.Benard Konga(anayefuata)pamoja na wakurugenzi  wengine wa Wizara na NHIF wakifuatilia taarifa hiyo.
IMG-20181024-WA0032
.WazirinUmmy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

KAMISHNA WA MAADILI AWATAKA VIONGOZI WA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) KUJIEPUSHA KUPOKEA ZAWADI

$
0
0
Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela amewataka viongozi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kujiepusha kupokea zawadi wakati wanapotekeleza majukumu yao. 

Wito huo aliutoa wakati akiwaapisha Kiapo cha Uadilifu Viongozi wakuu wa Baraza hilo wakiongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Adolf Babiligi Rutayuga katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kamishna alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ipo katika mchakato wa kulifanyia kazi jambo hilo ambapo viongozi wa umma watatakiwa kutamka katika fomu zao zawadi wanazopokea ili kuwapa urahisi Sekretarieti kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu zaidi.

Akinukuu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995, kifungu cha 12(2) kinachosema kuwa Kiongozi wa umma pale atakapopokea zawadi yenye thamani inayozidi shilingi 200,000/= atatakiwa kutaja zawadi aliyopokea na thamani yake na kukabidhi zawadi hiyo kwa Afisa Mhasibu wa Ofisi inayohusika ambaye atatoa maagizo kwa maandishi kuhusu matumizi ya zawadi hiyo au jinsi ya kuishughulikia kwa njia nyingine yeyote. Alifafanua Mhe. Nsekela. Hata hivyo Mhe. Nsekela aliwaasa viongozi hao kujiepusha kupokea zawadi kwa namna yeyote ile.

Kuhusu Kiapo cha Uadilifu ambacho aliwaapisha viongozi hao, Mhe. Nsekela aliwaasha viongozi hao kuzingatia vipengele vyote 12 ambavyo walikiri mbele yake na kwamba hizo ni taratibu za ajira zao na sio mageni katika utumishi wa umma. Aidha, Mhe. Nsekela aliwataka viongozi hao kujiepusha kutumia vibaya madaraka yao na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazowaongoza.

Pia, Mhe. Nsekela aliwakumbusha viongozi hao kutoa Matamko ya Rasilimali na Madeni yao, ya Wenza wao pamoja na Watoto wao ambao wana umri chini ya miaka 18 kwa mujibu wa Sheria. Sambamba na hilo, Kamishna wa Maadili alitumia fursa hiyo kuwaomba wenza wa viongozi hususani wanaume kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la uhakiki wa Rasilimali na Madeni ya Viongozi linapofanyika.

Viongozi wengine walioapishwa Kiapo cha Uadilifu na Kamishna wa Maadili ukiacha Dkt. Adolf Babiligi Rutayuga ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo ni Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi, Dkt. Gemma Kishari Modu.
Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela (kulia) akiwaapisha Kiapo cha Uadilifu Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu. 
Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Wakila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu. 

Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) wakisaini Hati zao za Ahadi ya Uadilifu baada ya kuapishwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu.


Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE). Wengine Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, anayefuata baada ya Kamishna wa Maadili ni Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake

VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI

$
0
0

Na.Alex Sonna,Dodoma

Kufuatia ongezeko  la magari yanayoendeshwa na madereva wa Serikali kupata ajali, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania limeibuka na  kutoa tamko la kufuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari ya viongozi wa Serikali wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.

Akizungumzana na waandishi wa habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo,Hamadi Masauni wakati akitoa tamko la kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwa baraza hilo  huku akiwa ameongoza na Makamu Mwenyekiti wa baraza,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa na wajumbe wengine wa Baraza hilo.

Mhe.Masauni amesema kuwa baraza lilopita lilifanya kazi nzuri ila baraza jipya lina malengo yake ya kupunguza ajali nchini hasa za viongozi wa Serikari kwa kuwafuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari hayo wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.

Aidha amesema kuwa kwa sasa wanaishauri Serikali kutoa waraka maalum utakaosaidia kuwadhibiti viongozi ambao wanatoa maelekezo kwa madereva wakimbize magari kwa mwendokasi na malengo ya baraza hilo ni kuimarisha utendaji wa kamati za usalama za mikoa na kuweka mikakati ya pamoja ya utendaji na usimamiaji wa majukumu ya kamati hizo.

“Kudhibiti mwendokasi na kuovateki kunakofanywa na madereva wa magari kwa kuwakamata,kuwaweka mahabusu na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao hivyo kukosa sifa ya kuondesha magari hayo,”amesema Masauni
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani  pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.
PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani  pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


SAMIA -TUTAFUATILIA WAFANYABIASHARA WANAOINGIZA BIDHAA FEKI NA KUUZA KWA GHARAMA NAFUU NA KUSHUSHA SOKO LA NDANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itafuatilia baadhi ya wafanyabiashara wanaodaiwa kuingiza bidhaa feki na kuuuza kwa gharama nafuu hali inayosababisha kushusha soko la ndani. 

Akizindua kiwanda cha African Dragon kinachotengeneza malighafi ya mabati, Zinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kilichojengwa kwa thamani ya bilioni 11 ,alisema kuwa suala hilo amelichukua na kuahidi kulifanyiwa kazi.

Alieleza, kwa hali hiyo inakatisha tamaa na jitihada za wawekezaji wa ndani katika juhudi za serikali kuhamasisha wawekezaji kuwekeza nchini. Samia alielezea ,sekta ya viwanda kwa sasa ndiyo mpango wa serikali wa kihakikisha nchi inakuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda."Ofisi yangu imelichukua suala hilo na italishughulikia "alisisitiza Samia. 

Hata hivyo Samia, aliwaasa wazazi na walezi kusimamia vijana wao kupata elimu ya ujuzi wa kuweza kuajiriwa ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira. 
Alipongeza mkoa wa Pwani kwa kuongoza kwa kusheheni viwanda kitaifa, amewaomba kujipanga na kuvutia wawekezaji katika mkoa, kwani sio kazi rahisi. 

"Katika utekelezaji wa Uchumi wa viwanda ,mtoe ushirikiano kwa wawekezaji ili kuweza kutimiza malengo ya serikali ya kuelekea uchumi wa kati "alieleza Samia. Akimkaribisha makamu wa Rais, Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema mkoa huo, una jumla ya viwanda 429 ikiwemo vya kati, vikubwa na vidogo ,na kutengeneza ajira za moja kwa moja zaidi ya 20,000 na kunufaika na ushuru na kodi inazolipa viwanda hivyo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza kumsikiliza alipotembelea eneo la Mbegani itakapojengwa Bandari Mpya ya Bagamoyo ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa mchoro na kupata maelezo ya itakavyokuwa Bandari Mpya ya Bagamoyo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Mhandisi Karim Mataka ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


TASWIRAZZ MBALIMBALI ZA MTANANGE WA TANZANIA PRISON NA AFRICAN LYON...

$
0
0
Mshambuliaji wa Prisons Jeremia Juma akiwa anaambaambaa na mpira wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya African Lyon uliomalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mtanange Ukiendelea
Beki wa Tanzania Prisons Leon Mutalemwa (23) akiwania mpira na mchezaji wa African Lyon Ismail Gambo (17) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya African Lyon uliomalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mchezaji wa African Lyon Adam Omary (7) akiwania mpira na beki wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile (6) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliomalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu ya 0-0 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.PICHA ZOTE NA MR.PENGO MICHUZI MEDIA.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 25,2018

TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8

$
0
0
Ahmed Mahmoud Arusha

Taasisi ya mfuko wa mgunduzi wa madini ya Tanzanite inatarajia kufanya Tamasha na maonyesho ya madini ya Tanzanite lengo likiwa ni kumuenzi mgunduzi wa madini hayo Mzee Jumanne Ngoma.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti mtendaji wa Taasisi hiyo Bi Asha Ngoma alipokuwa akiongea na wadau wa sekta ya madini mkoani hapa na kueleza kuwa katika tamasha hilo watashiriki kuonyesha zana mbalimbali alizokuwa akitumia mgunduzi huyo pamoja na madini aliyowahi kupata.

Amesema kuwa lengo la kikao kuongea na wadau kuhusu uandaaji wa tamasha la madini hayo ambapo maonyesho hayo kutangaza nchi ili madini hayo yajulikane yanatoka hapa nchini kwani sekta hiyo na wadau wake watanufaika kutokana na maonyesho hayo.

“Tunaenda kukutana na Serikali kwani wadau wamefurahia kuaandaa tamasha hili kutimiza miaka 50 tokea kugunduliwa kwa madini ya tanzanite na maonyesho hayo yatafanyika mwezi wa 12 tarehe 6-8 mwaka huu”alisema Ngoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini na vito hapa nchini(Tamida) Sammy Mollel alisema kuwa tamasha hilo limekuja wakati muafaka na kuunga mkono uwepo wa tamasha hilo kwani litasaidia ukuaji wa kiuchumi na udhibiti wa madini ya Tanzanite ambapo madini haya yanatoka hapa nchini pekee amhali yalipogunduliwa madini hayo.

Amesema kuwa kutakuwa na maonyesho ya uzaji na ununuzi wa madini ya vito na pia kutembelea sehemu ambayo yaligunduliwa madini hayo ambapo tunatarajia kujenga mnara wa kuenzi ugunduzi wa madini hayo eneo hilo na tunaendelea kumpongeza mh.Rais kwa kujenga ukuta ambao unadhibiti madini hayo.

Aidha kwa upande mwingine Makamu mwenyekiti wa wafanyabiashara wa madini ya vito Tamida Thomas Munnisi alisema kuwa ni jambo jema kwa tamasha hilo kuweza kuenzi kazi nzuri ya Mzee Jumanne Ngoma na wadau wa madini ya Tanzanite wana wajibu mkubwa kuweza kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono kazi hiyo kwa kufanya Harambee kuunga mkono juhudi zake kama mh.Rais Dkt.John Magufuri alipoweza kumchangia million 100.

Alieleza jusikitishwa kwake na wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo kumsahau mgunduzi hiyo Mzee jumanne ngoma kwa mchango wake kwani alitumia uwezo na rasilimali zake katika kugundua madini hayo ambayo yameweza kuwatajirisha watu wengi ilhali yeye akibakia maskini.

“Naipongeza Taasisi hii ya mgunduzi wa madini ya Tanzanite kwa uamuzi wao wa kuaandaa tamasha hilo ambalo litakuwa na maslahi mapana kwa taifa na wadau wa sekta ya madini ya vito nchini napenda kuishauri tamasha hilo likafanyika eneo la merelani ndani ya ukuta au nje ya ukuta lengo ni serikali kupata mapato yake”alisisitiza Munisi

WAZIRI AWESO AELEKEZA TIMU YA WATALAAM WA MAJI WA WIZARA KUKAGUA MIRADI YA MAJI WILAYANI MBULU

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza timu ya wataalam wa maji kutoka Wizara ya Maji kukagua miradi yote ya maji katika wilaya ya Mbulu mkoani Manyara na kuainisha changamoto za miradi hiyo na namna ya kuzimaliza ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama kama Serikali ilivyopanga. 

Mhe. Aweso ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mbulu ambapo amekagua mradi wa maji wa Arri, mradi wa maji Mongahay – Tumati, na mradi wa maji Dongobesh.

Mhe. Aweso (Mb) amesema miradi hiyo imechukua muda mrefu kukamilika wakati wananchi wanapata adha ya kutokua na uhakika wa majisafi na salama kwasababu mahitaji yameongezeka. Amesema baadhi ya miradi wamepewa wakandarasi wasio na uzoefu wa kutosha hivyo kushindwa kuikamilisha kama kwa mujibu wa mikataba waliyopewa.

Waziri Aweso (Mb) akiongea na wakazi wa Mbulu amesema hatavumilia kuona rasilimali za serikali zinatumika vibaya katika sekta ya maji, na kuainisha kuwa wakandarasi wanaoharibu miradi ya maji, watachukuliwa hatua za kisheria, pamoja na kufungiwa kushiriki kazi yoyote inayohusu sekta ya maji hapa nchini.

Pamoja na hilo, Mhe. Aweso (Mb) ameelekeza Jumuiya za Watumia Maji nchini zisajiliwe, na ziweke mikakati ya kutunza miradi ya maji ili idumu na kuwa endelevu. Aidha, viongozi wawashirikishe waanchi kulinda vyanzo vya maji na watoe elimu zaidi ili kuzuia kazi ya aina yoyote katika vyanzo vya maji ndani ya umbali wa mita 60. Aidha, Mhe. Aweso (Mb) ameagiza fedha za dharura kiasi cha shilingi milioni 60 zitumike kuchimba kisima cha maji kwa wakazi wa Haydom. 

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), anayetizama kamera, akiwa katika mradi wa maji wa Mongahay – Tumati wilayani Mbulu, ameagiza wataalam wa maji kutoka Wizara ya Maji kukagua miradi yote ya maji wilayani Mbulu ili kubaini changamoto za kitaalam na kutoa ushauri kuhusu namna ya kukamilika kwa miradi hiyo mara moja ili huduma ya majisafi iwafikie wananchi kwa uhakika. 
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia upatikanaji majisafi na salama kwa wananchi katika kioski cha Kwa Zacharia mjini Hanang’. Hata hivyo, Waziri Aweso ameelekeza miradi ya maji ikaguliwe kwasababu kiwango chaupatikanaji maji wilayani Mbulu hakitoshi. 
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipewa maelezo kuhusu mradi wa maji wa Dongobesh kutoka kwa mtalaam wa maji wa wilaya ya Mbulu Onesmo Mwakasege.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akishiriki kazi ya kuchimba mtaro kupata nafasi ya kukarabati bomba linalosambaza maji kwa wananchi katika mtaa wa Stendi ya zamani, mjini Haydom Mbulu. 
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), watatu kushoto mstari wa mbele-meza kuu, akiwa katika moja ya mkutano wa hadhara wilayani Mbulu. Pichani ni katika uwanja wa kata wa Haydom
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images