Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

MABINTI TGGA TEMEKE WAPINGA NGONO,MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

$
0
0
 Girl Guides wa Wilaya ya Temeke, wakikataa ndoa na mimba za utotoni  wakati wa maadhimisho a Siku ya Mtoto wa Kike yaliyoandaliwa na uongozi wa  TGGA Temeke, kwenye Ukumbi wa Idd Nyundo Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam. Katikati aliyevaa miwani ni Mgeni rasmi Mwalimu Hawa Chanafi wa Shule ya Tandika. Chanafi alimwakilisha Meya wa Temeke.

TGGA Temeke hadi sasa ina wanachama 5200. Tamasha hilo lilihudhuriwa na wanafunzi kutoka shule za Wailes, Likwati, Keko Magurumbasi, Tandika, Chamazi na Uwanja wa Ndege.
 Girl Guides wakiwa na bango lenye ujumbe wa Nguvu ya Mtoto wa Kike.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakiigiza kusikitika jinsi baadhi ya wanaume wanavyotoa vishawishi kwa watoto wa kike kwa lengo la kufanya nao ngono na kuwapatia mimba.
 Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maadhimisho kumalizika.

KAMISHNA MKUU WA TRA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WAKE KUHUSU UBORESHAJI WA HUDUMA MBALIMBALI ZA WALIPAKODI

$
0
0
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza leo na watumishi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi waliopo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam juu ya uboreshaji wa huduma mbalimbali za walipakodi.
 Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Gabriel Mwangosi (katikati) akitoa maoni wakati wa kikao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
 Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Bi. Agnes Kitwanga akifafanua jambo wakati wa kikao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

Muogeleaji Mhini sasa kusoma na kujifunza kuogelea Uingereza kwenye klabu ya St Felix

$
0
0
 MUOGELEAJI nyota wa klabu ya kuogelea ya Morogoro, (Mis Piranha) , Dennis Mhini amepata nafasi ya kusoma na kujifunza mchezo wa kuogelea kwenye klabu maarufu ya St Felix  ya Uingereza.
Dennis aliyeiwakilisha Tanzania katika michezo ya  Olimpiki ya Vijana nchini, Argentina amepata nafasi hiyo baada ya kufikiwa viwango vilivyowekwa na shule hiyo chini ya kocha maarufu, Sue Purchese.
Kigezo cha kwanza ni ubora wake katika mchezo kuogelea baada ya kufikia muda unaotakiwa na pili uwezo wake wa darasani.
Baba wa mchezaji huyo, Hamis Mhini alisema kuwa mwanaye pamoja na kutoweza kutwaa medali Argentina, alifanikiwa kupunguza muda wake wa kuogelea, jambo ambalo limewavutia sana walimu na kocha maarufu wa mchezo wa kuogelea nchini uingereza, Sue Purchase.
Mhini alisema kuwa hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini kwani anaamini kuwa mwanaye ataiva na kuwa muogeleaji bora Tanzania na dunia.
Alisema kuwa Dennis anapenda sana mchezo wa kuogelea na ndiyo maana waliamua kumpa nafasi ya kufanya kile ambacho anakipenda na kufikia kiwango cha kufuzu michezo ya Olimpiki ya Vijana iliyofanika mjini Buenos Aires.
Katika michezo hiyo, Dennis aliweza kushika nafasi ya tatu katika kundi la kwanza kweye staili ya freestyle ya mita 100 kwa kupata muda wa sekunde, 58.53 na pointi 514 na vile vile kumaliza katika nafasi ya tatu kwa upande staili ya backstroke kwa mita 50 kwa kutumia sekunde 29.79 na kupata pointi 525.
Dennis alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo na kuahidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa lake.
Alisema kuwa atahakikisha anakuwa na kiwango cha kufuzu katika mashindano mbalimbali duniani ikiwa pamoja na Mashindano ya Dunia, Jumuiya ya Madola na Olimpiki ya wakubwa.Dennis Mhini (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na kocha Michael Livingstone (wa kwanza kulia) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina. Wengine katika picha ni wanamichezo na viongozi.
Kocha wa mchezo wa riadha, Mwinga Mwanjala (kulia) akimkabidhi shada la maua, Dennis Mhini (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya vijana. 
 Muogeleaji, Dennis Mhini (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wazazi wake, Hamis Mhini (wa kwanza kushoto), Bhoke Mukoji Mhini ( wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina kwa ya mashindano ya vijana ya Olimpiki. Wa nne kushoto ni kocha wa timu ya Taifa, Michael Livingstone ambaye anafuatiwa na Eugenia Kaitesi, Derick Mhini. Pia katika picha ni Deborah Mhini (katikati). 
Timu ya Tanzania iliyoshriki katika mashindano ya vijana ya Olimpiki katika picha ya pamoja na makocha wao na mkuu wa msafara.

MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuhakikisha hakuna mtoto anayeanza Darasa la Kwanza bila kuwa amepitia darasa la Awali.

Hatua hiyo inalenga kuondoa tatizo la kuwa na wanafunzi wanaoingia Darasa la Kwanza ambao hawajui kusoma, kuhesabu na kuandika.

Mwanri alitoa kauli hiyo hivi wakati akifungua mkutano wa kutathmini masuala ya elimu mkoani humo na kuhimiza walimu kuhakikisha wanaondoka tatizo la KKK shuleni kwao.

“Msingi mzuri wa mtoto lazima uanzie elimu ya awali na ndio maana nasistiza kuwa mtoto asiingie la kwanza kama akupitia Chekechea …kule ndipo mtoto anapoandaliwa kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma …ukikosea toka hapo basi mtoto anaweza kutokuwa na maendeleo mazuri darasani” alisema.

Alisema vitendo vya baadhi ya walimu kutozingatia hilo na kuchukua watoto ambao hawakupita elimu za awali ndiko kunakosababisha baadhi yao wanapofanya mitihani ya kujipama ya Darasa la Nne matokeo yao sio mazuri kwa sababu ya kuanza la kwanza hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Aidha Mwanri aliwapongeza walimu wa Shule za Awali na msingi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwatengenezaea msingi mzuri watoto hao ili wanapoendelea na masomo yao waweze kufanya vizuri.

Katika hatua nyingine amewataka wamiliki na walimu wa Shule za Awali kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa watoto hao ili wapende kwenda shule.

Alisema maeneo hayo lazima yawe na vivutio wa michezo mbalimbali ya watoto wadogo ili pamoja na kujifunza wawe na muda wa kucheza kama sehemu ya burudani na elimu kwao.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa wazazi na wadau wengine kuweka mazingira mazuri ambayo yatawavutia  walimu hasa wale ajira mpya kupenda kufanya kazi katika maeneo yao.

Alisema mazingira hayo ni pamoja na kuwawekea vivutio kama vile kuwapa maeneo ya kulima , nyumba za kuishi kama hakuna nyumba za shule na wakati mwingine kuwapa chakula cha kuanzia maisha.

Mwanri alisema kuna baadhi ya maeneo hapa nchini yamefanikiwa kielimu kutokana na wazazi kuweka vivutio ambavyo vimewafanya walimu wanaporipoti kutofikia kuhama katika shule walizopangiwa.

“Tujenge utamaduni wa kuweka motisha kwa walimu wetu…kwa mfano mnaposikia leo kuna mwalimu mpya anaripoti katika shule yetu , mnaweza kukusanyika na kumlaki ili ajiene kuwa amefika nyumbani na sio ugenini” alisema.

RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI MBUNGE WA MAKETE PROFESA NORMAN SIGALA AMBAYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI DAR

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mbunge wa Makete Profesa Norman Sigala King ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Makete Profesa Norman Sigala King ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam akizungumza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumjulia hali leo tarehe 22/9/2018.

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON ATEMBELEA BENKI YA CRDB NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI, ABDULMAJJID NSEKELA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson leo ametembelea Benki ya CRDB na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, AbdulMajid Mussa Nsekela. 

Dkt. Tulia alisema dhumuni la Mkutano huo ni kumpongeza, Nsekela kwa uteuzi wake wa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya CRDB na kufanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na maendeleo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Mussa Nsekela, walipokuwa wakizungumza ofisini kwake, Azikiwe jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Mussa Nsekela wakati alipokuwa akisaini kitabu cha wageni.

Mr. Blue amuibua Ali Kiba kwenye Vibe la Tigo Fiesta Tanga

$
0
0
 Msanii Khery Sameer Rajabu maarufu kama Mr. Blue jana alimpandisha msanii Ali Kiba kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Mkwakwani mjini  Tanga kwa kushirikiana nae kwenye wimbo wao uitwao MBOGA SABA . Mr Blue alianza kwa kusema "nataka niwape 'surprise"leo toka kwa ndugu yangu mwenye roho ya pekee aje apande hapa juu awasalimie na niimbe nae,".

Ndipo Kiba akapanda na kuulipua uwanja  Mkwakwani kwa mayowe, baada ya kumalizika kwa wimbo huo Kiba alisalimia na kushuka jukwaani kitu ambacho mashabiki walitamani aendelee kuimba lakini hakuwa kwenye orodha.

Kwa upande wa wasanii wengine  Rostam na Maua Sama waliendeleza "Remix" yao ya IOKOTE na kuwapa mashabiki Vibe Lote. Nao kundi la Weusi kushirikiana na Nandy waliweza kuimba pamoja na kukonga nyoyo za mashabiki uwanja wa Mkwakwani.
Tamasha la Tigo Fiesta linaambatana na shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tigo Fiesta Supa Nyota na kwa mkoa wa Tanga, msanii Faraji Majimoto aliibuka mshindi atayeiwakilisha mkoa wa Tanga.

Wadhamini wa Tamasha hilo Kampuni ya Tigo, wamewaletea wateja wao ofa kabambe ya intaneti wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz

Tamasha hilo litaendelea ijumaa hii kwenye uwanja wa Kiruma mkoani Mwanza.
 Dogo Janja aki vibe na mashabiki wa muziki waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini  Tanga, wakati wa muendelezo wa tamasha kubwa la burudani nchini la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote.

USHINDI UNAZIDI KUTUPA MORALI KILA SIKU - AGGREY MORRIS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BAADA ya kikosi cha Azam FC kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), Nahodha wa timu hiyo, Agrey Moris, ameweka wazi kuwa kwa sasa wanachoangalia ni kushinda mechi zote zilizo mbele yao.



Azam FC imekaa vema kwenye msimamo baada ya kuichapa African Lyon mabao 2-1 na kufikisha jumla ya pointi 21 kwa mabao yaliyofungwa na Yahya Zayd, Abdallah Kheri huku lile la Lyon likitupiwa na Hood Mayanja.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kupata ushindi katika mchezo huu (African Lyon) kiukweli mechi ilikuwa ngumu, African Lyon nawapongeza wamecheza vizuri ila naipongeza pia timu yangu tumeweza kujitolea kupata pointi tatu kuhakikisha tunapata matokeo katika mchezo wa leo (jana),” alisema.


Alisema timu hiyo kuendelea kupata ushindi kunazidi kuongeza morali kikosini. “Kila unaposhinda mchezo inaongeza morali katika timu, sisi tunachokiangalia ni kushinda kila mchezo uliokuwepo mbele ili tutajua mwisho katika ligi tupo katika nafasi gani,” alisema.


Nyota huyo aliyedumu kwa takribani miaka tisa ndani ya kikosi hicho, alizungumzia mechi tatu zijazo wanazoenda kucheza ugenini na kudai kuwa zitakuwa ngumu lakini watahakikisha wanajipanga na kupata matokeo.

“Kusema kweli mechi za ugenini ni ngumu ukiangalia pia kwa sababu ni viwanja vibovu ninavyosema hivyo nadhani watu wengi watakuja kusema ooh mmeanza kucheza mpira viwanja gani lakini ukiangalia hali ya viwanja vyetu haiku vizuri na ukingalia timu kama ilivyo Azam mechi zote watu wanavyokuja wanakamia kwa kutaka matokeo.

“Ila huu ni mpira ndivyo ulivyo tunatakiwa na sisi tujipange kuhakikisha tunashinda kila mchezo uliokuwa mbele yetu,” alisema.

Mechi hizo tatu za ugenini, Azam FC itacheza dhidi ya JKT Tanzania (Oktoba 24), Singida United (Oktoba 28), Kagera Sugar (Novemba 4) kabla ya kurejea nyumbani kukipiga na Mbao Novemba 08 mwaka huu.

Aidha Moris alizidi kuwavuta mashabiki wa Azam FC kujitokeza kwa wingi kuwasapoti kwenye mechi wanazocheza kwani timu sio wachezaji tu na benchi la ufundi bali mashabiki nao wana nafasi yao.

“Mashabiki waendelee kuisapoti timu kwa sababu tunawategemea sana, mpira sio wachezaji wa ndani tu na benchi la ufundi, mashabiki wana nafasi yao kubwa katika mpira waendelee kuisapoti timu na sisi tutawapa wanachokihitaji,” alisema.

Azam kwa sasa wanaongoza ligi kwa alama 21 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 19 ma katika nafasi ya tatu mabingwa watetezi Simba wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 17 sambamba na Singida United.

Balozi wa Tanzania China Azitaka Taasisi za Umma Kuchangamkia Masoko China

$
0
0
Na Beatrice Lyimo - MAELEZO, CHINA

Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa  Kairuki amezitaka Taasisi zenye dhamana ya kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali nchini ikiwemo TANTRADE , Bodi ya Kahawa, Bodi za Chai, Korosho, Nafaka na Mazao mchanganyiko kushiriki kwenye maonesho mbalimbali yatakayofanyika nchini China ili kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao. Balozi Kairuki ameyazungumza hayo alipokutana na ujumbe wa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipotembelea nchini China kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya China na Tanzania katika tasnia ya habari na mawasiliano.

"Uzoefu wa hivi karibuni umekuwa wa kukatisha tamaa kutokana na Ubalozi kutafuta fursa mbalimbali kwa ajili ya bidhaa za Tanzania kutangazwa lakini wadau wameshindwa kushiriki" ameongeza Balozi Kairuki. Aidha, Balozi Kairuki amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya kahawa miongoni mwa Watu wa Jamhuri ya China na kahawa ya Tanzania ni miongoni mwa kahawa zinazopendwa sana na watu hao hivyo hiyo ni nafasi ya kupata soko la uhakika nchini humo endapo itafanyika kampeni mahususi ya kuitangaza kahawa ya Tanzania.

Vilevile amesema kuwa Madini mbalimbali na vito kutoka Tanzania yana nafasi ya kupata soko nchini China endapo patakuwepo na mifumo mizuri ya kisasa ya kuendesha mnada ya madini. Mbali na hayo, Balozi Kairuki ametaja baadhi ya matarajio ya Ubalozi wa Tanzania nchini China katika kipindi cha miaka minne ijayo ikiwepo kuongeza idadi ya sasa ya watalii toka China kutoka 30,000 hadi 100,000 ifikapo mwaka 2020.

Aidha, amesema kuwa Ubalozi unatarajia kuongeza uwekezaji kutoka China hususani kwenye ujenzi wa viwanda ikiwa na lengo la kati ya sasa hadi 2021 kuvutia viwanda 100 ili kufanya ongezeko la uwekezaji kutoka dola za Kimarekani Bilioni 3.6 za sasa hadi kufika dola za Kimarekani bilioni 7 ifikapo 2021.

"Pia Ubalozi unatarajia kuongeza idadi ya fursa za mafunzo kwa Watanzania katika fani mbalimbali hususani uhandisi ikiwa na lengo kuu la kuhakikisha watanzania 1,000 wapate mafunzo ya uhandisi ifikapo mwaka 2021.

Dkt. Abbasi ameambatana na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Habari na Uhusiano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya Tanzania na China katika sekta ya mawasiliano.

Upelelezi dhidi ya kesi ya aliyekuwa mke wa bilionea msuya wakamilika

$
0
0
BAADA ya kusota rumande kwa zaidi ya miaka miwili, hatimae upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyella umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika. 

Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Patrick Mwita ameieleza hayo leo Oktoba 22,2018 Mahakama wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. 

Akitoa taarifa hizo, Wakili Mwita  amedai kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika hivyo, wanaiomba Mahakama ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakia maelezo ya mashahidi na Vielelezo (Committal).

"Mheshimiwa Jalada la kesi hii limeshatoka kwa DPP na sasa tunalo hapa,  hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi na Novena amedai Mwita.

Kufuatia taarifa hiyo, wakili wa utetezi Peter Kibatala ameomba Mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe fupi ili wateja wake waweze kusomewa maelezo hayo. 

Baada ya kusikiliza maelezo hayo Hakimu Simba amahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi mwaka huu. 

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Dada  wa marehemu bilionea, Erasto Msuya, Aneth Msuya.

Kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo, Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada,  wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

TCCIA NA TPSF KUADHIMISHA MIAKA 30 NA 20 TANGU KUANZISHWA KWAO

NAIBU WAZIRI WA MADINI DOTTO BITEKO AFANYA ZIARA MIGODI YA KISARAWE

$
0
0



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko ametembelea Migodi ya Kaolin ya Wilaya Kisarawe Mkoani na kujionea uzalishaji na kukagua migodi ambayo imefungiwa kwa muda na kutoa maelekezo hili waweze kufunguliwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara hiyo Naibu Waziri Biteko amesema lengo la ziara hiyo ni kuhimiza ulipaji wa kodi katika sekta ya madini, kwani kulikuwa na changamoto nyingi katika sekta hiyo hasa ulipaji wa mrabaha.

"Tunalipa kodi ya madini haya kulingana na unapouzia sio kulipa mrabaha kwa eneo unalochimbia hivyo tumewaeleza wale wote ambao watakwenda kinyume nataratibu hizo atakuwa amekwepa kodi kwa makusudi kwa tayari wameshapewa taharifa hivyo kwa sehemu kubwa ya wachimbaji niliyowatembelea wamefuata sheria na kanuni tulizowaelekeza "amesema Naibu Waziri Biteko.

Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa wachimbaji wote waendelee kushirikiana na ofisi za madini kwani serikali ipo kwa ajili ya kuwalea wachimbaji wadogo hili waweze kufikia maelengo.amessisitiza kuwa sheria ya Madini ya mwaka 2018 inamtaka kila mwenye leseni ya madini kutunza kila nyaraka ya uchimbaji na mauzo hivyo inamtaka kutoa nyaraka hizo kwa afisa yoyote atakayefika katika eneo hilo na yoyote atakeyshindwa kufanya hivyo atatozwa faini ya Milioni 50 hadi 150 

kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mtera Mwampamba amemshukuru Naibu Waziri kwa Maelekezo yake na ofisi ya Mkuu wa Wilaya inaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za sekta ya Madini hili waweze kuwa na uzalishaji mzuri wenye tija kwa wawekezaji na Serikali.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akimsikiliza Fundi Umeme wa Magari wa kampuni ya Madini ya Caolin, Asinine Ahmed akiteta jambo na Waziri mara baada ya kutembelea mgodi huo kujionea uchimbaji wa madini ya Kaolin yanayotumika kujtengenezea Vigae na Gypsum.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akimsikiliza Mkurugenzi wa Mgodi wa Rak Caolin ,Adam Nyimbu akieleza namna mgodi wake unavyofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
Kamishna wa Madini Kanda ya Pwani akitoa Maelezo kwa Kamishana wa Madini namna Migodi ya Kaolin inavyoendeshwa.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akitoa Maelekezo kwa Mmoja wa Wawekezaji kutoka Twyford, Andy He mara baada ya kutembelea eneo la Mgodi wa kaolini Wilaya ya Kisarawe na kumkuta muwekezaji huyo ambaye ni mnunuzi.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akiwa katika eneo la mgodi wa Rak Caolin Mining Wilaya ya Kisarawe.
Naibu Waziri wa Madini , Dotto Biteko akiwa katika eneo la mgodi wa Madini ya Kaolini Wilaya ya Kisarawe.

RC MAKONDA ATANGAZA FURSA KWA VIJANA WENYE UTAALAMU WA IT.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika vijana wote wenye utaalamu wa Teknolojia yani IT kufika Ofisini kwake Tar 01/11/2018 Asubuhi kwaajili ya kuunda Mfumo wa kuratibu Uwajibikaji wa Watendaji wa Umma ilikuhakikisha kero na malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa uharaka.

Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na viongozi Wakuu akiwemo Mkuu wa mkoa,Katibu tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara Watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua kero za wananchi.

RC Makonda amesema hataki kuona wananchi wanafika kwenye ofisi za umma na kuambia "Njoo kesho" kila siku pasipokujua kuwa wanatumia nauli na kupoteza muda.

Mfumo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.

SHAUKU YA RC MAKONDA NI KUONA UWAJIBIKAJI NA UTENDAJI KWENYE OFISI ZA UMMA UNAONGEZEKA ILI KUPUNGUZA KERO KWA WANANCHI.

USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano mzuri baina ya taasisi mbalimbali za dini nchini na Serikali ni jambo la muhimu katika kuboresha na kuimarisha amani.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 22, 2018) alipowasili jijini Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa Serikali na wa dini mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mkakati wa viongozi wa dini wa kuunda kamati za amani nchini ambapo walianzia kwenye ngazi ya mkoa na sasa wamefikia katika kata.“Viongozi wa dini mnadhamana kubwa katika kulifanya Taifa liendelee kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hivyo ushirikiano wenu na Serikali ni muhimu.”

Amesema viongozi wa Serikali wakati wote wamekuwa tayari kufanyakazi na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali za dini, lengo ni kuimarisha amani na utulivu uliopo nchini.Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza inawajibu wa kuhakikisha kwamba maeneo ya mkoa huu yanaendelea kuwa salama.

Pia, Waziri Mkuu amempongeza Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hassan Bin Mussa Kabeke kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.“Nakupongeza kaimu sheikh wa mkoa kwa kuteuliwa na ninakutakia kila la heri katika kazi yako na kwamba dhamana yako kubwa ni kuwaunganisha waislamu na waumini wa dini zote.”


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMATATU, OKTOBA 22, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hasani Bin Mussa Kabeke wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  Oktoba 22, 2018 akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.   Sheikh huyo amechaguliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  (katikati) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VIFUNGASHIO NA MASOKO KILIO KIKUBWA KWA WAJASIRIAMALI


TFDA YATOA ELIMU YA MADHARA YA SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI

$
0
0

Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hususani unga wa mahindi na siagi ya karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa sumukuvu ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji na wakati mwingine husababisha vifo. 

Mafunzo hayo yanatokana na ripoti ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa bidhaa zitokanazo na unga mchanganyiko na siagi ya karanga uliofanywa na mamlaka hiyo ya mwaka 2015-2018 na kubaini mazo hayo huzalishwa kwa wingi mkoani humo yana dalili ya uwepo wa fangasi na sumukuvu. 

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka amesema kuwa  Mamlaka imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hasa Unga wa Mahindi na Siagi ya Karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Sumukuvu.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy amesema kuwa ugonjwa huo hujitokeza baada ya mlaji kutumia bidhaa zenye vimelea vyake kwa kiasi kikubwa huathiri Ini,kusababisha Saratani na hata vifo kwa watumiaji ambao ni nguvukazi ya Taifa. 

Kessy amesema kuwa mwaka 2015 hadi 2016 na mwaka 2017 hadi 2018 TFDA ilifanya ufuatailiaji wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko na siagi za karanga zilizokuwa zikiuzwa katika soko nchini. 

“Katika ufuatiliji huo ilibainika kuwa bidhaa hizi zilikuwa na dalili ya uwepo wa sumukuvu,hususani katika bidhaa zitokanazo na mahindi na karanga hizi ndizo wajasiliamali wengi wanauza”amesema Bw.Kessy 

Kwa upande wa baadhi ya Wasindikizaji wamekiri kutokuwa na uelewa juu ya sumukuvu kwani awali walikuwa wakisindika Nafaka Kienyeji bila kuchagua mazao ambayo mengine yana dalili za uwepo wa vimelea vya ugonjwa huo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndugu Maduka Kessy akizungumza na wajasiriamali hawapo pichani, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour) na siagi ya karanga yanayofanyika Jijini Dodoma. 
 
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour)na siagi ya karanga wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo 
Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka akitoa ufafanuzi mbalimbali husiana semina hiyo kwa waandishi wa habari ( hawapo Pichani) wakati wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour) na siagi ya karanga yanayofanyika  jijini Dodoma. 
Washiriki wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour)na siagi ya karanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waliokaa kwenye viti kulia ni Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy 

DC PANGANI AOMBA SEMINA YA FURSA IFANYIKE WILAYANI MWAKE MWAKA 2019

VIFUNGASHIO NA MASOKO KILIO KIKUBWA KWA WAJASIRIAMALI MBEYA

VOA SWAHILI: Zulia Jekundu October 19, 2018

INTRODUCING SINGELI HIT "Umeniacha" by Dj Hunter Ft Stizzo X Mafioso #Prod By PAPA

Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images