Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

SIMBA SC YATOA ZAWADI YA USHINDI KWA MO DEWJI, YAILAZA STAND UNITED 3-0...


TAARIFA YA HABARI YA ITV SAA MBILI USIKU 21 OCTOBA 2018

DKT. MWAKYEMBE AZINDUA TAMASHA LA 37 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akijaribu moja ya fulana alizopatiwa na Mjasaliamali mchoraji Baraka Aj (kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo yanaliyofunguliwa rasmi jana jumamosi Oktoba 20, 2018.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akicheza ngoma pamoja na kikundi kimojawapo kilichotumbuiza katika Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo muda mfupi kabla ya kuzindua Tamasha hilo jana Jumamosi Oktoba 20, 2018
 Mkuu wa Chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA), Dkt. Herbert Makoye (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika banda la Chama cha wasanii na wachoraji Tanzania muda mfupi kabla uzinduzi wa Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana jumamosi Oktoba 20, 2018 Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
.
 Wakufunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TASUBA) iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni lililofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani jana Jumamosi Oktoba 20, 2018.
 Wasanii wa Kundi la Ngoma Kali lenye makazi yake nchini Finland wakitazama burudani kutoka katika vikundi mbalimbali vilivyotubuiza katika Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililozunduliwa jana Jumamosi Oktoba 20, 2018  Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.


Mahakimu waaswa kuepuka mgongano wa kimasilahi katika maamuzi ya utoaji haki.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mahakimu wameaswa kuzingatia maadili katika utoaji haki ili kulinda heshima yao wenyewe na kuwajengea wananchi imani juu ya mhimili huo.

Hayo ameyasema Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Joachim Tiganga wakati akifungua mafunzo wa mahakimu wanawake katika jiji la Mkoa wa Dar es Salaam yaliyoandaliwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Dar es Salaam.

Tiganga amesema mafunzo yatawajengea uwezo katika utoaji wa haki wa kuepuka mgongano wa kimasilahi.Tiganga amesema ikiwa mahakimu hawatatenda haki katika maamuzi wanayoyafanya watasababisha watu kujichukulia sheria mkononi hali inayoweza kusababisha utovu wa maadili kwa wananchi.

"Nafahamu kuwa Mahakama ya Tanzania iko kwenye kampeni kubwa ya kuhubiri na kusimamia maadili kwa viongozi wa umma na watumishi wake."Mafunzo haya kwetu yamekuja katika muda mwafaka na hii ni ishara kwamba maadili sasa ni wimbo wa kila taasisi ya umma, hasa kwa viongozi wa Umma.Amesema kuwa mafunzo hayo kwa mahakimu wanajibu wa kuzingatia kuzin suala la mogongano wa maslahi kwa sababu ni moja ya mambo yanayosababisha ukiukwaji wa maadili.

Amesema tatizo la mogongano wa kimasilahi limekuwa likizimba nchi nyingi duniani na kusababisha athari katika maendeleo ya nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.Aliongeza kuwa mogongano huo wa maslahi hutokea pale ambapo kiongozi mwenye dhamana anapofanya maamuzi na kutumia nafasi yake kutoa haki ndugu, jamaa na marafiki bila kufuata sheria."Unapofanya maamuzi kwa kulinda maslahi ya mtu fulani basi ujue kuwa umejiingiza katika mgongano wa maslahi. Mgongano wa maslahi unasababisha watu wengine kukosa haki na fursa sawa."Jambo hili lisipodhibitiwa linasababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya utoaji haki"amesema Tiganga.

Tiganga amesema kuwa ni vema kiongozi yeyote kujaribu kwa kiasi kikubwa kuepuka mgongano wa kimasilahi na kufanya maamuzi kwa kuzingatia matakwa ya sheria zinazohusika bila upendeleo wala ubaguzi ili kujenga Taifa lenye maendeleo endelevu kwa wote.

Naye Katibu wa Idara ya Ukuzaji Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika kukuza na kusimamia maadili kutokana na utafiti uliofanywa na sekretarieti hiyo kuonesha kuwa ni asilimia moja pekee ya viongozi wanawake ndiyo wanaoshiriki katika utoaji wa taarifa za ukiukwaji wa maadili."Kwa sababu wanawake ni sehemu kubwa wazazi na walezi, mafunzo haya yatawasaidia kuwalea watoto katika maadili, kwa sababu naamini maadili yanajengwa kuanzia utotoni ndipo tunajenga jamii ya watu wenye maadili," amesema Kipacha.
.Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Joachim Tiganga akuzungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya Mahakimu Wanawake yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma yalifanyika jijini Dar es Salaam.

Katibu Msajili wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha akitoa maelezo kwa Mahakimu Wanawake katika mafunzo yaliyoandaliwa na Sekretarieti hiyo.
Picha ya pamoja Mgeni Rasmi Sekretarieti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Katibu Msajili wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri Kipacha akitoa maelezo kwa Mahakimu Wanawake katika mafunzo yaliyoandaliwa na Sekretarieti hiyo.
picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na Mahakimu Wanawake Katika Mikoa wa Dar es Salaam.

BREAKING NYUUUUZZZZ.....:SOKO LA MATUNDA NA MBOGAMBOGA LA AFRIKASANA, SINZA LAPIGWA NYUNDO USIKU HUU, DC CHONGOLO AKISIMAMIA ZOEZI

HIFADHI YA SAADANI WATOA OFA KWENYE TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO 2018

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisoma kijarida cha Hifadhi ya Taifa ya Saaadani alipotembelea banda la maonesho la Hifadhi hiyo katika Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo jana Oktoba 20,2018. Kulia ni Mhifadhi Utalii wa Saadani Bi. Apaikunda Mungure.

Hifadhi ya Taifa ya Saadani kupitia Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo limetangaza ofa Watanzania na wasio Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kuanzia Oktoba 25, 26 na 27 mwaka huu kujionea vivutio mbalimbali vya Utalii.

Akizungumza Mhifadhi Utalii, Hifadhi ya Saadani, Bi. Apaikunda Mungure amesema ofa hiyo ni maalum kwa msimu huu wa tamasha la Sanaa Bagamoyo  ambapo kwa kiasi cha Tsh. 91,000   ni gharama kwa Raia wa Tanzania pamoja na Afrika Mashariki huku wageni kutoka nje ya Afrika Mashariki hao watalipia US$120 tu.

“Ofa hii itanda kwa muda wa siku tatu. Oktoba   25, 26 na 27. Wageni wataenda Saadani na kurudi hapa Bagamoyo. Kwa kiasi hicho cha Tsh. 91,000 inajumlisha usafiri wa magari ya Kitalii, usafiri wa kuzunguka na boti kwenye makutano ya Mto Wami na bahari ya Hindi.

Pia watapata kifungua kinywa, chakula cha mchana na vinywaji na kutembelezwa kwa safari za kuangalia wanyama na magari” alieleza  Bi. Apaikunda Mungure.

Ameongeza kuwa kwa familia itakayokuwa na motto atamlipia Tsh. 71,000.

Saadani  ni hifadhi ya kipekee ambapo Nyika na bahari  vinakutana pamoja. Ndani ya hifadhi hiyo ina aina mbalimbali za wanyama pori, fukwe ya bahari ya hindi.

Iko katika mkoa wa Pwani na Tanga

Watanzania ambao wapo Bagamoyo na miji jirani ya Dar es Salaam ni fursa ya kujitokeza kwenda kujionea Utalii wa ndani wenye kila aina ya vivutio vya Wanyama na safari zitakuwa kila siku kwa wageni kuanzia saba ambao wao kila mmoja atakaa kwa siti tena dirishani (window seat).

WAZIRI MBARAWA AMEAGIZA KUFANYIKA KWA UTAFITI WA KINA KWA WAKANDARASI KABLA YA KUINGIA NAO MIKATABA

$
0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame ameziagiza Halmashauri zote kufanya utafiti wa kina kwa wakandarasi kabla ya kuingia nao mikataba ya ujenzi wa miradi ili kuweza kumaliza tatizo la utekelezaji mbovu wa miradi ya maji nchini.

Amesema tatizo la miradi mingi ya maji kwenye halmashauri ni kwa sababu zabuni nyingi zinatolewa kwa wakandarasi wasio na sifa, wengine wakishindwa hata na miradi midogo wakati akikagua miradi ya maji ya Kumbara-Litola, Milonje-Matemanga na Milonde katika Wilaya za Namtumbo na Tunduru, mkoani Ruvuma.

Profesa Mbarawa amesema halmashauri nyingi zimekuwa zikitoa zabuni kwa wakandarasi katika mazingira ya rushwa, bila kuzingatia uwezo wao kifedha, vifaa vya kazi na kazi zao kwa sababu hawafanyi uchunguzi wa kina hivyo kusababisha matatizo kwenye utekelezaji wa miradi. Jambo linalosababisha kubadili wakandarasi mara kwa mara kutokana kuvunja mikataba mara mara kwa sababu ya utendaji mbovu wa wakandarasi, na kurudisha nyuma juhudi za Serikali kuwapatia wananchi wake huduma ya majisafi na salama.

"Serikali haitakubali kurudishwa nyuma kimaendeleo na mtu yeyote, tutawafukuza wakandarasi wasio na sifa na tutashughulika na wale wote wanaotoa zabuni pasipo kufuata utaratibu lazima niwaambie ukweli'', amesema Profesa Mbarawa.

"Ni lazima mfanye uchunguzi wa kina kwa kila mkandarasi kwa kuzingatia vigezo vyote, ikiwa ni pamoja na kwenda kuangalia kazi walizozifanya kwa lengo la kujiridhisha uwezo wake kabla hamjaingia nao mkataba'', ameonya Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameagiza Kampuni ya Service Plan Ltd isipewe tena kazi na wizara yake, baada ya kubainika imetoa taarifa ya usanifu wa mradi wa Kumbara-Litola isiyo sahahi uliopo Wilaya ya Namtumbo ambapo ungeigharimu Serikali fedha nyingi bila sababu.

Kulingana na usanifu wa awali kuonyesha gharama kubwa, ililazmika kufanya usanifu upya na kuonekana unaweza kutekelezwa kwa Shilingi Bilioni 1.2 baadala ya Shilingi Bilioni 6 kama ilivyoonyesha awali na mradi huo unategemewa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo (kulia) na wataalamu katika chanzo cha mradi wa Milonde, Namtumbo, mkoani Ruvuma.
Mradi wa maji Milonde ukiwa katika hatua ya utekelezaji.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua tenki la mradi wa Kumbara-Litola, Namtumbo na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 22,2018


MKUTANO WA NNE WA UONGOZI WA BIASHARA WA WANAWAKE KUFANYIKA OKTOBA 27, JIJINI DAR

$
0
0
Hii ni nafasi pekee kwako mfanyabiashara kuuza, kujitangaza, kupata network na kufurahi kwa pamoja tukutane Golden Jubilee Hall tarehe 27/10/2018
Kwa mawasiliano zaidi tupigie 0657106218 | 
0786908470 

Naibu Mkurugenzi UNEP azungumzia kujitambua kupata mafanikio

$
0
0
Na Mwandishi wetu
SUALA la kujitambua na kutambua nini mahitaji yako ni moja ya chanzo cha mabadiliko yanayohitajika katika maisha, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Joyce Msuya amebainisha.
Alisema hayo akizungumza na wanawake mbalimbali waliofika kusikiliza historia yake na jinsi alivyoweza kumudu maisha ya mama, mke na mfanyakazi katika mashirika mbalimbali ya kimataifa na kupanda ngazi.
Aidha alisema pamoja na kujitambua mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kuwajibika, kujisukuma zaidi katika kazi na kufanya maamuzi ya kushirikisha familia hasa patna.
Msuya ambaye alianza kazi ya UNEP mwaka huu mwezi wa nane baada ya kupitia Benki ya dunia na mashirika mengine kadhaa alisema mfumo wa Tanzania wa shule, malezi ndiyo iliyofanya kuunganisha nguvu, uwezo na ujasiri wa kuweza kufanya mambo ambayo yamemfanya kupata nafasi kubwa zaidi.
Alisema mfumo wa Tanzania wa maisha umekuwa msukukumo mkubwa kwake kwani  aliweza kuishi na watu tofauti na kuvumilia huku akitekeleza wajibu wake kwa kujiongeza zaidi.
Alisema kutokana na juhuzi za wazazi wake katika kusimamia malezi aliweza kupata maarifa zaidi ya kuishi kwa kuhudhuria shule za umma za Forodhani, Jangwani na Weruweru kisha kuchukua mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) Mafinga na kumalizia mafunzo hayo Mlalakua.
“Ukweli ni kuwa wazazi wangu walitaka tuishi maisha ya kawaida kama watanzania wengine ndiyo maana walinipeleka shule za bweni na kuhakikisha naenda jeshini. “ alisema Mkurugenzi huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Anasema malezi ya kujitegemea yamemfanya awe na uwezo wa kufanya bajeti hali ambayo ilimwezesha kuishi vyema Scotland na hata alipoenda kuchukua shahada yake ya pili nchini Canada.
“Kusema ukweli  Baba na mama walinitengenezea mfumo mzuri wa kuishi hasa pale walipojenga na kunihimiza kufanya kazi na kusoma wakati nikiwa mdogo.” Alisema Msuya.
Anasema amevuka vigingi vingi hasa kwenye muwashawasha wa masomo lakini kama walivyo watu wote alifanya maamuzi makini kuzingatia ushauri na kile anachokipenda.
Akiulizwa nini hasa kinamsukuma, alisema kwamba familia ni kitu muhimu kwake na kwamba amefanya mambo mengi akiwa na familia yake kuanzia mume wake ambaye wamo katika ndoa kwa miaka 20 na kujaliwa kuwa na watoto wawili.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya akizungumza viongozi wanawake vijana kwenye mdahalo ambapo aliutumia kuhamasisha wanawake wengine kujituma uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bi. Natalie Boucly. 
 Mkurugenzi wa uendeshaji wa Doctors’ Plaza, Bi. Sophia Byanaku akiuliza swali kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) wakati wa mdahalo maalum kwa viongozi wanawake vijana ambapo walipata fursa ya kuhamasishwa kujituma na kujitambua uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wanawake vijana walioshiriki kwenye mdahalo ulioendeshwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) ambapo aliutumia kuhamasisha wanawake wengine kujituma uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam
Baadhi ya viongozi wanawake vijana wakiuliza maswali kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) wakati wa mdahalo maalum uliotumika kuhamasisha wanawake wengine kujituma na kujitambua ambapo umefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya katika picha ya pamoja na viongozi wanawake vijana mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MEYA MSTAAFU KINONDONI AMPONGEZA RAIS MAGUFULI MFUMO WA ELIMU BURE

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MEYA  Mstaafu  wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amempongeza Rais John Magufuli kwa kuruhusu mfumo wa elimu ya bure  katika shule za Msingi na Sekondari na kuwataka wazazi kushirikiana na shule hizo katika maendeleo mbalimbali.

Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya  Shule ya Sekondari ya Mikocheni,Mwenda alisema hatua hiyo ya Rais Magufuli imesaidia wanafunzi pamoja na wazazi wengi kunufahika na elimu hiyo.

Alisema ukilinganisha na miaka ya nyuma,hivi sasa wanafunzi wengi  wanapata elimu tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo wengi waliikosa kutokana na kushindwa kulipia ada za shule.Mwenda alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wake tangu aingie madarakani, amejenga shule nyingi katika kata mbalimbali, jambo lililowawezesha wanafunzi wengi na jamii kunufahika.

"Kinachotakiwa kwa sasa ni wazazi kutoa ushirikiano kwa shule hizo ili ziweze kupata nguvu ya kusonga mbele kimaendeleo na kuinua kiwango cha elimu nchini alisema Mwenda.Aliwataka wazazi pia kutambua kuwa licha ya Serikali kutoa elimu  bure, bado wanapata kuchangia maendeleo ya shule hizo hatua itakayozisaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Aidha aliwapongeza wahitimu katika mahafali hayo na kuwataka kuwa mfano kwa kufanya vizuri katika mtihani wao mwisho na hivyo kufungua njia yao ya kimaisha lakini pia kuwapa hamasa wanafunzi waliobakia shuleni hapo. Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Salama Ndyetabura alisema shule hiyo iliyoanzishwa miaka minne iliyopita pamoja na mafanikio baadhi iliyoyafikia,bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa maabara.

Alisema pamoja na changamoto hiyo,pia shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madras pamoja na walimu wa masomo ya sayansi suala aliliiomba Serikali kulitatua.Jumla ya wanafunzi 158 walihitimu katika mahafali hayo wakiwemo wavulana 79 na wasichana 79.

TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUTOA ELIMU YA NIDHAMU YA FEDHA KWA WAJASIRIAMALI

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,KIBAMBA.
 
TAASISI mbalimbali za kifedha zimeaswa kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusiana na nidhamu ya matumizi ya fedha katika biashara zao ,kabla ya kuwakopesha ili waweze kunufaika na mikopo wanayowapatia.
 
Pamoja na hayo, wajasiriamali hao wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa zilizo bora na kuhifadhiwa vizuri ili kuendana na soko la ushindani wa kibiashara.

Hayo yalisemwa na Beatrice Mbawala ambae alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, kilichopo kata ya Kibamba .Alieleza, elimu juu ya fedha wanazokopa wajasiriamali ni muhimu kwani baadhi yao wamekuwa wakifilisika kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya fedha .
 
Beatrice alisema kuwa ,baadhi ya wajasiriamali wameshindwa kufikia mafanikio  na kuwa wajasiriamali wakubwa kutokana na kushindwa kuwa na nidhamu ya fedha wanazokopa .“Akinamama ,wajasiriamali mliopo hapa mhakikishe mnakuwa waaminifu na kuwajali wateja wenu,kuzalisha bidhaa bora na kuacha kutumia mikopo mnayochukua kutafuta kiki mitaani,kwa kufanya ufahari”alieleza Beatrice.
 
Nae mkufunzi wa vicoba kutoka taasisi ya Pamoja Entrepreneurship Support for Community  Development (Pescode) Enethlena Wadelanga alisema ,wanawapa mafunzo ya ujasiriamali kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kifikra na kujitetea kwa kuunganisha nguvu ujuzi na uzoefu.Alifafanua ,jamii inapaswa kuamka ili kuleta maendeleo kwa kuungana kwani vita ya kiuchumi ni ya pamoja kwa ajili ya kuboresha maisha kupitia shughuli zao za kila siku za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kila mwanachama.  
 
Enethlena alifafanua, wanatarajia kujenga ofisi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na kuanzisha ufugaji wa kuku na kuwaomba wadau kuwaunga mkono hasa taasisi za kifedha ili waweze kujiinua kiuchumi.Mwanachama Mariam Kawawa alisema kuwa wangehitaji kutengewa eneo kwa ajili ya wajasiriamali kufanyia kazi kuliko kila mtu kufanyia sehemu yake ambapo baadhi ya bidhaa huzalisha uchafua na kutupwa holela.
 
Mariam alibainisha, kutokana na kujiunga kwenye vicoba hiyo ameweza kunufaika na mafunzo mbalimbali ambapo kwa sasa anazalisha bidhaa mbalimbali na kuweza kujikwamua kiuchumi huku akiwa ametoa ajira kwa watu wengine ambao anashirikiana nao.Gogoni Investor ilianzishwa mwaka mmoja uliopita na ina wanachama 50 ambao kuna makundi mawili A na B ikiwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi .
 Beatrice Mbawala (wa pili kushoto) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, wakati alipomwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, katika uzinduzi wa kikundi hicho, kilichopo kata ya Kibamba ,(wa kulia) ni mkufunzi wa vicoba kutoka taasisi ya Pamoja Entrepreneurship Support for Community  Development (Pescode) Enethlena Wadelanga
IMG-20181021-WA0023
Beatrice Mbawala akizungumza wakati alipomwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, katika uzinduzi wa kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, kilichopo kata ya Kibamba.Picha na Mwamvua Mwinyi

WAKAZI WA KITAME WAKERWA NA MIUNDOMBINU MIBOVU YA BARABARA

$
0
0
Na Mwamvua  Mwinyi,Babamoyo.
WAKAZI wa Kitame kata ya Makurunge wilaya ya Bagamoyo,Pwani wametoa kilio chao cha miaka mingi cha ubovu wa miundombinu ya barabara kutoka Gama-Kitame,yenye urefu wa km.9.5.

Ubovu wa barabara hiyo ,husababisha kutumia njia ya maji kwa kutumia majahazi nyakati za mvua njia ambayo ni ndefu na kuwapa tabu hasa wagonjwa watoto na akinamama wajawazito.

Akitoa kero hiyo katika ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo ,alhaj Dk.Shukuru Kawambwa aliyoifanya kata ya Makurunge ,mwenyekiti wa kitongoji cha Kitame ,Silvester Kangwe alisema ,
kukiwa na mvua barabara haipitiki kwakuwa huweka mfinyanzi.

Awali nao baadhi ya wakazi wa Kitame akiwemo Tobias Saidi na Lulu Seif walimuomba mbunge huyo ,kuwasaidia kufuatilia namna ya kujengwa kwa barabara hiyo .

"Kilio hiki ni cha kipindi kirefu ,tunaomba utumie nafasi yako kutusaidia ,tuweze kuondokana na changamoto hii, Tunahofia mvua zikianza kunyesha tena, mafuriko huzidi na kuharibu kabisa barabara hii " walisisitiza.

Akieleza ufuatiliaji wa suala hilo ,Dk.Kawambwa alisema kwa kushirikiana na mhandisi wa wilaya waliandika ombi kuangalia namna ya kujenga ujenzi wa uhakika wa kipande hicho cha barabara.

"Sasa barabara hizi zipo chini ya TARURA na fedha zilizotengwa kwa mwaka 2018/2019 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati ama matengenezo madogomadogo na sio ujenzi mkubwa "

"Habari hii sio nzuri kwenu ,"Kwa hesabu za harakaharaka inaweza kutumika zaidi ya sh.bilioni mbili ,fedha hiyo sio mchezo wa kitoto ,hivyo sitoweza kufanya danganya toto ,nitaendelea kufuatilia hadi hapo kero hii itakapopatiwa ufumbuzi";:alifafanua Dk.Kawambwa.

Akijibu suala la ukosefu wa nishati ya umeme, Dk.Kawambwa alieleza, kupitia REA ahadi aliyopatiwa kipindi cha nyuma imekwenda ndivyo sivyo ambapo kwasasa amepewa ahadi kwa baadhi ya vitongoji na vingine vimetolewa huku Kitame ikiwa haimo.
 Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Alhaj Shukuru Kawambwa akitolea ufafanuzi kero alizofikishiwa na wakazi wa Kitame wakati wa ziara yake aliyoianza ya kata kwa kata jimboni humo
 (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Wananchi wa jimbo la Bagamoyo, wakimsikiliza mbunge wao akitolea ufafanuzi kero alizofikishiwa na wakazi wa Kitame wakati wa ziara yake aliyoianza ya kata kwa kata jimboni humo (picha na Mwamvua Mwinyi)

RIDHIWANI KIKWETE AUNGANA NA WASANII KUMZIKA MASHAKA

$
0
0
Na Shushu Joel, Dar
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete ameungana na wasanii wa kada mbalimbali katika kumzika msanii maarufu wa maigizo nchini Ramadhani Ditopile aliyewai kuwa msanii wa kundi la sanaa la kaole.

Mashaka alifariki juzi asubui wakati akiwa anapata matibabu katika hospital ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Ridhiwani alisema kuwa pengo la msanii huyo ni ngumu kuliziba kwa kipiondi hiki kutokana na jinsi alivyokuwa akifanya kazi zake kwa weredi.

“Mashaka alikuwa si msanii tu kwangu bali alikuwa ni mjomba wa mfano kwani alikuwa akinipatia ushauri mkubwa juu ya kazi zangu za siasa hivyo nimepoteza mtu wa muhimu sana kwangu”Alisema Ridhiwani.

Aliongeza kuwa anawapongeza wote waliofika katika kuhakikisha tunamzika ndugu yetu,kwani maziko ni wajibu wetu sote kwani ni ibada.

Aidha mbunge huyo alisema kuwa marehemu mashaka atakumbukwa kwa kupitia kipaji chake cha uigizaji ambapo katika uhai wake aliwai kutamba na kundi la kaole kupitia tamthilia za mambo hayo,kidedea,jumba la dhahabu na nyingine nyingi.

Kwa upande wake msanii maarufu wa uigizaji nchini Mzee chilo alisema kuwa Mashaka alikuwa ni mtu wa pekee katika tasinia ya kuigiza kutokana na kupenda kutumia kipaji chake kuwaelekeza wenzake pindi mnapokuwa katika kazi.

Aliongeza kuwa ni pengo kubwa katika fani yetu lakini kutokana na kuwa hapa duniani tunapita hakuna budi kumuombea kwa Mungu ili apumzike kwa amani.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Abdallah Ditopile,baba yake aliugua ghafla usiku wa kuamkia juzi na kisha kupelekwa hospital ya Amana ambapo alilazwa kabla ya kufariki akiendelea kupatiwa matibabu.

Aidha alisema kuwa baba yake alizidiwa na kupewa rufaa ya kwenda mloganzila lakini wakiwa wanasubili gari ili waelekee huko baba alipoteza maisha”Alisema Abdalaah.

Aliongeza kuwa anawashukuru watnzania wote waliojitokeza kwenye makaburi ya kifamilia yaliyoko Tabata Kinyelezi kwa ajili ya kumzika baba sina la kuwalipa ila Mungu atawalipa kwa wema mliotufanyia wanafamilia.
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete akibadilishana mawazo na msanii maarufu Mzee Chilo kwenye makaburi ya Tabata jana alipozikwa msanii Mashaka.
 Ridhiwani Kikwete akiteta jambo na wasanii mbalimbali waliojitokeza kwenye maziko ya msanii mwezao Mashaka jana.
Wasanii, viongozi mbalimbali wa kisiasa waliojitokeza kwenye makabuli ya Tabata jana wakati wa maziko ya msanii maafuru wa maigizo Mashaka.

Wafanyakazi wa Vodacom watoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa wanafunzi wasioona Jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, kupitia mpango wake wa Pamoja na Vodacom leo wametoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa Wanafunzi zaidi ya 150 wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo iliyoko Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Elimu bora kwa wote ni moja kati ya nguzo kuu za asasi ya Vodacom Tanzania Foundation hivyo msaada huu wa nyenzo za kujifunzia pamoja na vifaa mbalimbali vya elimu kwa ajili ya wasioona pamoja na wale wenye uoni hafifu utaisaidia shule kukabiliana na matakwa mbalimbali ya kuhudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Upatikanaji wa vitabu vya nukta nundu (vitabu maalum kwa Wasioona) pamoja na maandiko mengine, ni hafifu na msaada huu utasaidia katika kupunguza ukubwa wa tatizo hili. Msaada huu kutoka kwa Wafanyakazi wa Vodacom unahusisha mashine kumi na karatasi maalum za kuchapia maandishi ya nukta nundu (Maandishi maalum kwa Wasioona), viti, faili za plastiki (maalum kwa ajili wasioona), vifaa hivi vitasaidia zaidi ya wanafunzi 67 wenye shida ya macho katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. 

Kwa sasa Walimu wataweza kuandaa lesoni na vifaa maalum vya kufundishia kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu. Zaidi ya hayo, Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wamejitolea nguo, sabuni na vyakula mbalimbali ili kuwasaidia wanafunzi hao.

Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Lugata alisema, “elimu ni haki ya msingi na kipengele muhimu cha malengo endelevu ya milenia, tunatambua mchango muhimu wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko katika kuwalea Watoto walio pembezoni wenye ulemavu kwa kuwapa elimu bora inayoendana na mahitaji ya wanafunzi.” 


Kamishna msaidizi watu wenye ulemavu, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, ajira na watu wenye ulemavu, Beatrice Fungamo (Kushoto) akipokea moja ya mashine maalum za kuandikia maandishi ya nukta nundu (Braille) zilizotolewa jana na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiongozwa na mkurugenzi wa kanda ya Pwani George Lugata, vifaa hivyo vitaleta ufanisi katika kutoa elimu bora kwa wasioona na wale wenye uoni hafifu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

KAWAMBWA AWATOA HOFU WATAKAOPITIWA NA UJENZI WA BARABARA YA MAKOFIA MLANDIZI

$
0
0
Na Mwamvua  Mwinyi, Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo, mkoani Pwani, Dk.Shukuru Kawambwa, amewatoa hofu wananchi watakaopaswa kupisha ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Makofia -Mlandizi kwa kiwango cha lami kuwa watalipwa fidia utekelezaji utakapoanza. 

Aidha amewaeleza, wakala wa barabara (TANROADS) bado haijawa tayari katika utekelezaji huo lakini wale wanaopitiwa na bomba kuu linaloelekea Bagamoyo ,kuanzia eneo la Sunguvuni -Sanzale watarajie kulipwa fidia zao na DAWASA hivi karibuni . 

Akitolea ufafanuzi suala hilo kwa wakazi wa Chasimba na Magoza,kata ya Yombo wakati wa ziara yake ya kata kwa kata, Kawambwa alisema walengwa wanaoguswa na miradi hiyo wavute subira. 

Aidha alieleza, ahadi ya malipo ambayo DAWASA  italipa anaendelea kufuatilia ili kupata taarifa zaidi ya malipo hayo . 

"Serikali imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara mbalimbali, hii barabara nayo ipo katika utekelezaji wa ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi, "

"Tanroads na DAWASA wamekubaliana wakati ikisubiriwa kufikia ujenzi wa  barabara hiyo, imeingiliana na mradi wa bomba kuu la maji ambapo DAWASA italipa wale  watakaopitiwa na ujenzi huo "alifafanua Kawambwa. 

Kuhusu barabara ya Yombo-Kiegea ,mbunge huyo alisema inatafutwa fedha ili iweze kuboreshwa kwa kiwango cha changalawe .

"Kwa bajeti ya mwaka 2018/2019 TARURA haina fedha hivyo kwasasa ni matengenezo madogo madogo wakisubiri utengenezaji mkubwa baadae endapo kukipatikana fedha"alibainisha .

Akijibu suala la ukosefu wa umeme huko Chasimba na Magoza alisema maeneo hayo yameingizwa katika mradi wa Peri Urban na mkandarasi atakapopatikana watarajie kunufaika na mradi huo mpya. 

Awali wakazi wa Chasimba, Magoza kata ya Yombo walisikitishwa umeme kuwekwa mijini na vijiji kusahaulika kwa miaka mingi. 

Walisema ,wanatumia solar kila siku kwa gharama ya sh.3,000, gharama ambayo ni kubwa kwao kwa maisha ya sasa .

WAZIRI WA UJENZI, MHANDISI KAMWELE AKAGUA UJENZI BARABARA SITA DAR-KIBAHA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Injinia Patrick Mfugale (kushoto) akimwelezea Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele (kulia) maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara sita kutoka Dar es Salaam hadi Maili Moja Kibaha unaojengwa na fedha za Serikali kwa gharama ya takribani zaidi ya shilingi bilioni 140.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama (aliye nyoosha kidole) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Issack Kamwele alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na msafara wake wakitembelea mradi wa barabara sita unaoendelea eneo la Kimara Dar es Salaam hadi Mail Moja Mkoa wa Pwani.
Ujenzi wa barabara sita kutokea Dar es Salaam hadi Mail Moja Kibaha ukiendelea. Eneo hili unajengwa ukuta kuzuia maji ya mto kuingilia barabara hizo.

VIFAA TIBA,VITENDANISHI VINATAKIWA KUOMBEWA NA KUPATA KIBALI KUINGIZWA NCHINI-TFDA

VITILIGO SI UGONJWA, WALA MADHARA YA VIPODOZI NA HAINA TIBA

$
0
0
 Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii


KUNA muonekano ambao jamii umekuwa ukiunasibishwa na matumizi yaliyopitiliza ya vipodozi, ugonjwa au kasoro ila ni hali ya kawaida inayoweza kumpata mtu yeyote. 

Vitiligo ni hali ya ngozi kupoteza rangi yake na kuacha madoa/ mabaka katika sehemu fulani za mwili hasa zile zinazopata mwanga wa jua haraka kama mikono, uso na macho.

Hali hii husababishwa na seli zinazoipa ngozi rangi ya mwili zijulikanazo kama Melanocyte kufa au kushindwa kufanya kazi.

Daktari John Bergman kutoka Marekani ameeleza kuhusu hali hiyo na kusema kuwa seli zinazoipa ngozi rangi ya mwili zikifa mtu hukumbwa na Vitiligo na sababu za tatizo hilo hazijafahamika licha ya baadhi ya wataalamu kueleza kuwa Vitiligo husababishwa na mwili wenyewe kwa baadhi ya seli kuvamia kazi katika sehemu nyingine ya mwili, wengine husema kuwa seli hizo za Melanocyte zinazotengeneza rangi ya mwili hujiharibu zenyewe na baadhi ya wataalamu hueleza kuwa Vitiligo husababishwa na mwili kuchomwa sana na jua licha ya kutothibitisha.

Dalili za vitiligo ni pamoja na kuanza kutokea kwa mabaka katika sehemu mbalimbali hasa macho, mikono, miguu na uso.

Pia Vitiligo huweza kugundulika kwa kutokea kwa rangi nyeupe au kijivu kwenye nyusi, kope au ndevu na hata kupotea kwa rangi ya retina (eyeball) na rangi kwenye tishu ndani mdomo na pua.

Inashauriwa kuwa  mwanga wa jua ni muhimu hasa asubuhi na jioni  kwa dakika 20 na matibabu ya Vitiligo ni kurudisha rangi ya ngozi inayopotea  ila sio kuzuia kuendelea kupungua kwa rangi ya ngozi.

Ukweli kuhusu Vitiligo; Rangi ya nywele huweza kutabiri nguvu ya Melanin, huathiri watu wa kila aina ila huonekana sana kwa watu wenye rangi nyeusi na huwapata watu katika umri wowote kabla ya kufikia umri wa miaka 20 bila kujali jinsia wala kabila na ni ngumu kutabiri kuenea kwake.

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA WILAYA YA DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ofisi Kuu ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha Makutupora jijini Dodoma, Oktoba 21, 2018.  Watatu kushoto ni Mkuu wa Kikosi, Luteni Jenerali Regina Matina, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua ofisi kuu ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha Makutupora jijini Dodoma Oktoba 21, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na wapili kushoto ni Mkuu wa Kikosi, Luteni Kanali Regina Matina. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa mvinyo  kutoka kwa Bw.  Archard Kato ambaye ni  Mkurugenzi Mkuu wa   kiwanda   cha Alko Vintage cha jijini Dodoma wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Oktoba 21, 2018. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi (aliyeshika kinasa  sauti)  kuhusu ujenzi wa soko kuu la jiji hilo kwenye eneo la Nzuguni, Oktoba 21, 2018.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa stendi kuu ya mabasi ya Dodoma inayojengwa na Jiji la Dodoma kwenye eneo la Nzuguni, Oktoba 21, 2018. 
 Mafundi wa Kampuni ya Ujezi ya Mohammed Builders wakijenga msingi wa kituo kikuu cha mabasi kinachojengwa na jiji la Dodoma katika eneo la Nzuguni wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipoembelea eneo hilo, Oktoba 21, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi (kulia) kuhusu michoro ya stendi kuu ya mabasi inayojengwa na jiji la Dodoma katika eneo la Nzuguni, Oktoba 21, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua Mradi wa Maji wa Njedengwa wilayani Dodoma akiwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma, Oktoba 21, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha mashine ya kusukuma maji wakati alipofungua mradi wa maji wa Njedengwa akiwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma, Oktoba 21, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya (wapili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi  (kulia) kuelekea kwenye jengo la Mama na Mtoto wakati  alipotembelea hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Oktoba 21, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya rufaa  ya Mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika hospitali hiyo, Oktoba  21, 2018. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images