Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

WAZIRI MAJALIWA AFANYA ZIARA WILAYANI CHAMWINO

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara za mitaa katika mji wa Chamwino zinazojengwa kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 3.5,  Oktoba 20, 2018. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa na watatu kushoto ni Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shamba la zabibu katika kijiji cha Chinangali wilayani Chamwino, Oktoba 20, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mashine za kusukuma  maji ya umwagiliaji wakati alipotembelea shamba la zabibu katika kijiji cha  Chinangali wilayani Chamwino, Oktoba 20, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wagogo wakati alipowasili katika kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino kuakagua ujenzi wa Kituo cha Afya na kuhutubia mkutano wa hadhara, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MICHUZI TV: KIJANA ALIEISHI JUU YA MTI TANGU MWAKA 2016 JIJINI MBEYA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA USHIRIKA WA MAMLAKA SACCOS ZANZIBAR LEO

0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kwenye ukumbi wa Abdul Wakiil, Baraza la Wawakilishi la Zamani, Kikwajuni, Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa ameshikilia bango lenye maneno ya uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akionyesha picha yake aliopewa kama zawadi  wakati uzinduzi wa Ushirika wa Mamlaka Saccos kama ishara ya uzinduzi rasmi, wengine pichani ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico (kulia) kushoto ni Mwenyekiti wa Ushirika Ndugu Mohammed Khamis Ali. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MICHUZI TV: Haikuwa rahisi Twanga Pepeta kufika hapa - Asha Baraka

RAIS WA ZANZIBAR, DKT. ALI MOHAMED SHEIN AFUNGA MAONESHO YA KWANZA YA UTALII ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein katikati akiwa amefuatana na Waziri wa Habari Utalii na mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo (kulia)na viongozi wengine mara alipowasili katika hafla ya Ufungaji wa Maonesho ya kwanza ya Utalii Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein katikati alipokabidhi zawadi kwa Uongozi wa Hotel ya Pack Hayati waliopata ushindi wa kwanza katika mashindano mbalimbali ya mahoteli katika hafla ya Ufungaji wa Maonesho ya kwanza ya Utalii Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein akitoa hotuba ya ufungaji wa Maonesho ya Kwanza ya Utalii yaliochukua muda wa siku Tatu hafla iliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.

WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

0
0
Na Frankius Cleophace, Serengeti.

Wasichana zaidi ya  400 (Mianne) wa shule za sekondari wilayani Serengeti Mkoani Mara wamepatiwa elimu ya kupinga Ukeketaji kwa mtoto wa kike pamoja na elimu ya Afya ya Uzazi na utunzaji wa Mazingira kwa lengo la kukomboa Mwanamke huku wengine 1160 wakitarajia kupatiwa elimu hiyo. Hayo yamebainishwa na Frida Mollel ambaye ni  Meneja Idara ya Maendekeo ya jamii kampuni ya  Singita Grumeti Fund iliyopo wilayani  Serengeti  Mkoani Mara  katika viwanja shule ya Msingi Makundusi baada ya kutoka Shule ya Msingi Natta kwa kukikbia mbio fupi.

Frida amesema kuwa wao kama kampuni wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na wanakijiji kutoka vijiji 21 vinavyozunguka hifadhi ya Ikorongo Grumeti Reserves ili kuendelea kutunza mazingira na jamii kuondokana na ujangiri ili kulinda hifadhi pamoja na wanyama ili kunufaisha kizazi kijacho.
Meneja Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa elimu ya kupinga Ukeketaji na mila kandamizi kwa wasichana pamoja na wanawake katika viwanja vya shule ya Msingi Natta wilayani Serengeti mkoani Mara.

Licha ya kutolewa kwa elimu ya kutunza mazingira Frida amesema kuwa wanafunzi hao wamepewa elimu ya kupinga suala zima la ukeketaji na mila kandamizi ambazo zinazidi kundamiza mwanamke pamoja  na msichana mpaka kushindwa kutimiza ndo zake ambapo elimu hiyo imeanza kutolewa tangu mwaka jana lengo ni kukomboa mwanamke.

“Mwaka jana tuliweza kukutana na wasichana wakatupa changamoto zinazowakumba kipindi cha ukeketaji na mwaka huu Serengeti kulingana na mila na desturi watakeketa sasa tumeona tutumie fursa hii kutoa elimu ili kukomboa mtoto wa kike ukiangalia pia kuna wanawake ambao wametoka nje ya nchi ya Tanzania kwa maana ya Afirika kusini na Marekani ili kutuunga mkono lengo ni kutoa hamasa kubwa kwa mabinti hao pia wameweza kukimbia mbio fupi ni wasichana hao alisema Frida.” alisema Frida.
Rnonda Vetere Kutoka New York City Marekani akiongea na wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu mwanamke kijiamini ambapo amewasihi kudhubutu na kujiamini kwa lengo la kufanikiwa huku wakiendelea kutoa elimu juu ya kupinga mila kandamizi.

Katika kutoa elimu hiyo na kutoa hamasa kwa mabinti hao baadhi ya washiriki ambao wamekuwa wakitoa elimu wametoka nje ya Nchi huku baadhi yao wakitoka  Afrika Kusini, na Marekani  Rnonda Vetere kutoka New york City Nchini  Marekani  amezidi kuhamasisha wanawake Nchini Tanzaniakuendelea  kujiamini na kudhubutu kwa lengo la kupata mafanikio ili kuendeleza mapinduzi katika kutokomeza Mila kandamizao ukiwemo Ukeketaji kwa mtoto wa kike.

WAZIRI MKUU AAGIZA MRADI WA UMWAGILIAJI MPWAYUNGU UKAGULIWE

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wananchi wa kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahengeampeleke Afisa Kilimo wa mkoa Bw. Bernad Abraham  akakague mradi wa umwagiliaji wa Mpwayungu wilayani Chamwino ili kubaini waliohusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 1.2 za mradi huo.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) baada ya mbunge wa jimbo Mtera, Livingstone Lusinde kumuomba awasaidie kuhusu upotevu wa sh. bilioni 1.2 zilizotolewa kwa ajili ya mradi wa umwagiliaji ambazo matumizi yake hayajulikani.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi wilayani Chamwino, Dodoma alipokea ombi hilo la mbunge wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Mpwayungu, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mpwayungu.

Alisema mara baada ya Afisa Kilimo, Bw. Abraham kukamilisha ukaguzi wa mradi huo wa umwagiliaji apelekewe taarifa ili waliohusika na ubadhilifu wa kiasi hicho cha fedha wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alivunja kamati ya kusimamia huduma maji ya kijiji cha Mpwayungu na alimuagiza Mhandisi wa Maji wa wilaya ya Chamwino Bw. Godfrey Mbabaye aunde kamati mpya.

Waziri Mkuu alichua hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa kamati hiyo ambayo ilishindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo ujenzi wa vituo vya kuchotea maji licha ya kukusanya sh. milioni 20 kwa mwezi, mradi huo unavituo vinne tu.

Alisema kitendo cha kamati hiyo kushindwa kuongeza kujenga vituo vingine vya kuchotea maji licha ya kukusanya fedha nyingi kwa mwezi kinasababisha malalamiko kutoka kwa wananchi ambao ndio wanufaika wa mradi huo.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza mhandisi huyo aombe taarifa ya akaunti ya benki ya mradi huo ili kubaini katika mfuko wa mradi huo una fedha kiasi na ndipo aunde kamati mpya ya maji ambayo anatakiwa ashirikishe wanawake kwa kuwa wao ndio wahusika wakuu.

ZIARA YA DKT NDUGULILE KATIKA VIKUNDI VYA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MVOMERO MOROGORO

0
0




Seriklai imeziagiza Mamlaka ya Udhiti Ubora Tanzania (TBS), Mamlaka ya Udhiti wa ubora wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na SIDO kuwapa elimu Wanawake wajasiliamali wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ili kuongezea thamani katika bidhaa zao kwa kuwapa wabunifu na kuhakikisha bidhaa zao zinakuwa vifungashio vyenye ubora ili ziweze kushindana katika soko na bidhaa nyingine.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Wilaya ya Mvomero katika ziara yake Mkoani Morogoro kuangalia utoaji huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Ndugulile amesema ili wanawake hao waweze kufikia malengo yao na kukuza biashara yao lazima bidhaa ziwe na nembo ya biashara ambayo itatambulisha bidhaa zao na kusaidia kuvutia wateja.

‘’Wekeni nembo katika bidhaa zenu na serikali ya Wilaya iwasaidie ili muweze kuwa na viwanda vidogo vya uzalishaji mali jambo ambalo lipo pia katika Nchi zinazoendelea ambapo viwanda vidogo vimekuwa vikisaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi mfano mkiongezea thamani bidhaa zenu na kuzipa nembo ya Movomero itakuwa bora zaidi’’. Alisisitiza Dkt. Ndugulile.


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongozana na Wananchi wa kijiji cha Wami Luwindo kilichopo Dakawa Wilaya ya Mvomero kukagua mradi wa skimu ya umwagiliaji uanondeshwa na Serikali ya kijiji hicho. 
Wajasiliamali wadogo kutoka vikundi vya mbalimbali vilivyopo wilayani Mvomero wakitoa maelezo kuhusu bidhaa wanazozalisha kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Wilaya hiyo jana kujionea kazi za vikundi hivyo wakati wa ziara yake ya siku tatu Mkoani humo. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi milioni moja kwa Mwenyekiti Skimu ya Umwagiliaji wa kijiji cha Wami Luwindo kilichopo Dakawa Wilaya ya Mvomero Bw. Juma Achumu kama mchango wa Wizara yake kuwezesha na kuamsha hari ya Wananchi kijiletea maendeleo. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW .


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

FAINALI ZA MASHINDANO YA VILABU VYA KODI ZAFANA

0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Fainali za mashindano ya vilabu vya kodi zilizoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zimefanyika kwa mafanikio makubwa ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa kwa Shule za Sekondari zilizoibuka na ushindi na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano hayo.

Fainali hizo zilizofunguliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zilifanyika jana katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo, Shule ya Sekondari St. Joseph iliibuka mshindi wa kwanza kati ya shule 28 za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na kuzawadiwa runinga, kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti.

Shule ya Sekondari Tumbi imeshika nafasi ya pili ambayo ilijinyakulia kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali, ngao, na cheti ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Dar es Salaam ambayo ilipata ngao, kompyuta ya mezani, saa ya ukutani na cheti.

Kwa upande wa uwasilishaji mada zinazohusu masuala ya kodi, Shule ya Sekondari Zanaki iliongoza na kuzawadiwa kompyuta ya mezani, printa, saa ya ukutani, medali na cheti ikifuatiwa na Kerege ambayo ilijibebea printa, saa ya ukutani na cheti huku Shule ya Sekondari Misitu ikishika nafasi ya tatu na kuondoka na kompyuta ya mezani, ngao, na cheti.

Kwenye kipengele cha Ukusanyaji wa Risiti za Kielektroniki za EFD, walioibuka washindi ni Shule ya Sekondari Gerezani ambayo ilizawadiwa runinga, fedha taslimu shilingi 1,000,000, cheti na medali. Mshindi wa pili ni St. Joseph iliyojitwalia ngao, cheti na fedha taslimu shilingi 750,000 ikifuatiwa na Shule ya Sekondari Benjamini iliyopata ngao, cheti na fedha taslimu shilingi 500,000.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwakabidhi zawadi wanafunzi wa St. Joseph wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye umri wa mika 12 wa Shule ya Sekondari Mbezi Inn, Charles Denis wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora wa mwaka 2018 Runi David kutoka Shule ya Sekondari Tumbi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akimvisha mmoja wa wanafunzi ambaye shule yake iliibuka mshindi wakati wa fainali za mashindano ya vilabu vya kodi kwa Shule za Sekondari za Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani zilizofanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA TRA).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

JESHI LA POLISI LAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU UTEUZI WA BAADHI YA MAKAMISHNA WA JESHI LA POLISI ,LATOA ONYO.

WAZIRI MKUU AAGIZA KUBOMOLEWA KWA UZIO NA KUSITISHA UJENZI

0
0
*Ni baada ya kujengwa kwenye eneo la wazi na kuziba barabara
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo.

Uzio huo ambao mbali na kujengwa katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto kwenye mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia umeziba barabara ya tisa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 21, 2018) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini Dodoma, ambapo alitembelea eneo hilo na kuagiza libomolewe na lisalie kama inavyoonekana katika ramani na aliyeuziwa atafutiwe eneo lingine.

“Huu mji umejengwa kwa ramani, hamuwezi kubadili ramani kwa lengo la kumpa mtu eneo. Kwa nini mmeziba barabara ya tisa na huu mji unatambulika kwa barabara, sasa bomoeni hapa nataka barabara iendelee kutumika na eneo la kuchezea watoto libaki wazi,”Waziri Mkuu amemuagiza mkurugenzi wa jiji ahakikishe wanayatumia maeneo ya wazi kwa ajili ya kujenga sehemu za mapumziko ili kuwawezesha wananchi kupata maeneo ya kupumzika mara wanapomaliza kufanya shughuli zao za kikazi.

Amesema ni vema jiji likatenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za jamii, viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko. “Msifanye makosa kama yaliyofanyika Dar es Salaam.”Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipangomiji wa jiji la Dodoma, Bw. Joseph Mafulu alimuonyesha Waziri Mkuu ramani ambayo iliyotolewa na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ambayo ilibadilisha matumizi ya eneo hilo na kumpa muwekezaji.

Baada ya Bw. Mafulu kuonesha ramani hiyo Waziri Mkuu alitoa ramani halisi ya jiji la Dodoma ambayo inaonesha eneo hilo ni la wazi na ni mahususi kwa ajili ya michezo ya watoto, hivyo alisisitiza kuwa litumike kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo. Pichani, Waziri Mkuu akimwonyesha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi   ( wapili kushoto) ramani ya jiji la Dodoma inayoonyesha matumizi sahihi ya eneo  hilo, Oktoba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_9573
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo. Pichani, mabati yakiwa yamezungushwa kwenye eneo hilo wakati Waziri Mkuu alipolitembelea, Oktoba 21, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

NEWS ALERT: AJALI YA GARI YAUA WATUMISHI WATANO WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WATUMISHI watano wa Wizara ya Kilimo na Chakula wamefariki dunia leo asubuhi baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupata ajali wilayani Manyoni mkoani Singida.

Taarifa ya Katibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ambayo ameitoa leo kwa vyombo vya habari amesema kuwa Wizara yao imepatwa na msiba wa watumishi wake watano.

Amesema watumishi hao waliopata ajali leo asubuhi wilayanu Manyoni mkoani Singida, walipokuwa safarini kuelekea Mwanza kikazi.

Amewataja watumishi hao waliofariki ni Stella Ossano (39), Esta Mutatembwa (36), Abdallah Mushumbusi (53), Charles Somi na Erasto Mhina (43)

"Miili ya marehemu ipo njiani kuja Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo Oktoba 21, 2018.Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi, Amina," amesema Katibu Mkuu kwenye wizara hiyo.
Baadhi ya wananchi wakitazama namna ajali hiyo ya gari yenye namba za Usajili STK 8925 ikiwa imepta ajali eneo la Njirii Manyoni. Ambapo Gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula, iliyokua imebeba Wataalam wane pamoja na Dereva Wote wamefariki papo hapo. Wanaume watatu, na wanawake wawili. Miili imehifadhiwa katika Hosptal ya Wilaya Manyoni. Mwenyezi Mungu Awarehemu
Baadhi ya Maofisa wa Polisi wakitazama gari yenye namba za Usajili STK 8925 ikiwa imepta ajali eneo la Njirii Manyoni. Ambapo Gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula, iliyokua imebeba Wataalam wane pamoja na Dereva Wote wamefariki papo hapo. Wanaume watatu, na wanawake wawili. Miili imehifadhiwa katika Hosptal ya Wilaya Manyoni. Mwenyezi Mungu Awarehemu.

CHAMA CHA MAPINDUZI KUWACHUKULIA HATUA KALI WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WASIO SOMA MAPATO NA MATUMIZI

0
0
Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitawachukulia hatua kali Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanaotokana na CCM wasio soma mapato na matumizi kwa wananchi kwa mujibu wa Sheria.

Akifafanua suala hilo Ndg. Polepole ameeleza kuwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Mwaka 2019 CCM inahitaji watu watakao kuwa Viongozi wa wananchi kupitia CCM wenye sifa nzuri kwenye mitaa yao, amekemea suala la urafiki, undugu na upangaji wa safu katika mchakato wa kuwapata viongozi wa wananchi na amewataka Viongozi wa CCM na Viongozi wa Serikali ngazi zote kuwa na ushirikiano kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi kwa haraka.

“Wapo wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa CCM wasio soma mapato na matumizi…watu jeuri… wanafanya nini kwenye Chama chetu..? hawa hatuendi nao hadi mwaka 2019…kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwakani tunataka watu wenye sifa nzuri” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha Ndg. Polepole ametumia mkutano huo kusisitiza kuhusu suala la  Viongozi wa Serikali hususani wakuu wa Wilaya kuendeleza utaratibu wa kusikiliza wananchi na utolewaji wa mikopo ya Halmashauri bila riba kwa makundi ya kina Mama, Vijana na Watu wenye ulemavu ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na kutatua shida na changamoto zao kwa haraka.

Huu ni muendelezo wa vikao vya ujenzi na uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha dhana ya Chama imara, Serikali imara inadhihirika.
 Katibu Mwenezi wa CCM Ndg. Humphrey Polepole akizungumza Katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Kata ya Mtoni Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam 

DC MURO ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MBUYUNI

0
0



Imma Msumba, Arumeru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni kilichopo katika Halmashauri ya Arusha Dc  ambacho Serikali imetenga fedha Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara na Nyumba ya Mtumishi wa kituo hicho pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 
 IMG-20181021-WA0010
IMG-20181021-WA0013
Dc Muro akikagua ujenzi wa Kituo hicho ameleza kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya kwa kuimarisha huduma za Afya na kujenga vituo vyenye hadhi vijijini.
 IMG-20181021-WA0006
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Ujenzi wa Kituo hicho Ndg.Leskara Olerangai Ambaye pia ni Diwani mstaafu wa kata ya Oljoro ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa  kuwezesha kutoa fedha kwa wakati huku akimpongeza Dc Muro kwa jitihada zake anazozifanya ili kuhakikisha ujenzi una kamilika kwa wakati.

AZAM TV: MAGOLI YOTE: SIMBA SC 3-0 STAND UNITED; (TPL - 21/10/2018)


AZAM TV: Magoli yote: Yanga ilivyoipa Alliance kipigo cha mabao 3-0 (TPL – 20/10/2018)

WANACHAMA 15 KUTOKA VYAMA VYA UPINZANI WAJIUNGA NA CCM

0
0
WANACHAMA 15 wa vyama vya siasa vya upinzani wilaya ya Temeke wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam leo.

Wanachama waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM ni aliyekuwa katibu CHADEMA kata ya chang'ombe Abduli Kheri, Mwenyekiti CHADEMA Kata ya toangoma John Matugura, aliyekuwa katibu CHADEMA kata ya Temeke na katibu na mwenyekiti wa Bavicha wilaya ya TemekeChales Gahu, Afisa uchaguzi CHADEMA katibu mwenezi ACT WazalendoSteven Shekumkae.

Mwanachama CHADEMA Saidi Mohamed Ngaola,Mwenyekiti CHADEMA kata ya Kurasini James Nyaki, Mwanachama CHADEMA Mahamudu Saidani, Katibu mwenezi CHADEMA kata ya MtoniThomas Elia, Mwanachama CHADEMA Juma Said, Mwenyekiti Vijana Chama cha ACT Wazalendo KelvinAbiud ,Wanachama wa ACT Wazalendo Editha Bunjoro (Mama Kelvini,) Taifa baraza la wadhamini CHADEMA,Katibu kata CUF Toangoma Ally Mbonde,Renaty Lipambile Mwenyekiti CHADEMA wilaya ya Temeke na diwani wa kata ya mtoni Bernard Mwakyembe.



Akizungumza wakati wa kuwapokea katika chama cha Mapinduzi CCM katibu Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM, Humfrey Polepole jijini Dar es Salaam leo amewakaribisha katika kwenye chama Tawala CCM  na kuwaasa kushirikiana na wananchi kwa kufanya kazi na kutekeleza miradi ya chama tawala.

Wakizungumza mara baada ya kurudisha kadi za vyama vyao wanachama hao wamesema kuwa hawajanunuliwa bali wanaunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli baada ya kuona utekelezaji wake.

Amesema kuwa utaratibu wa kupata kadi zao za Chama cha mapinduzi watazipata kwenye mashina wanakoishi kama utaratibu ulivyopangwa na Chama cha Mapinduzi.

Pia Polepole amesema kuwa Wanawake wa chama cha mapinduzi watanufaika na mikopo isiyona riba kwani chama kimechoka na mikopo kutoka sehemu nyingine na yenye riba.

 Baadhi ya wanachama kutoka vyama vya upinzani wilaya ya Temeke wakiwa mbele mara baada ya kupkelewa katika chama Cha Mapinduzi CCM jijini Dar es Salaam leo.

 Mwanachama mpya akifungwa skafu ya CCM.
 Wanacham wapya wa CCM wakirudisha kadi zao za vyama walikokuwa.

DC Kinondoni aahidi kutatua kero ya barabara inayokwenda Kliniki ya Heameda, Mengi ashangazwa na maajabu ya Dk.Mwandolela

0
0

VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es  Salaam wamepongeza uongozi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B ambayo imekuwa ikitoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa wilaya hiyo na maeneo mengine huku ukiahidi kushughulikia kero ya ubovu  barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo ambayo imetajwa kutoa mchango mkubwa kuokoa maisha ya Watanzania.

Hayo yamesemwa jana na ujumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kupitia Mkuu wake wa Wilaya Daniel  Chongolo na Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dk.Christowell Mande wakati wa uzinduzi rasmi wa Kliniki ya Heameda ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Reginald Mengi.

Akizungumzia Kliniki hiyo Chongolo amesema Serikali inathamini mchango wa kliniki hiyo kwa kutoa huduma kwa wananchi wa Kinondoni na hasa walioko maeneo hayo ambayo hayana vituo vingi vya afya.Pia amejibu kuhusu ombi kero ya barabara inayoingia kwenye  kliniki hiyo kwa kuahidi kuishughulikia mara moja kwa kuitengeneza.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Dk.Mande amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kutoa huduma za afya na iko tayari kufanya kazi na kliniki hiyo."Tunawakaribisha muda wowote kufanya kazi katika dhana ya PPP.Kikubwa ambacho tunaweza kueleza hapa ni kwamba tunathamini mchango wenu na tunaomba tuedelee kushirikiana katika kuwahudumia Watanzania,"amesema.

Wakati huo huo mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda Dk.Reginald Mengi amesema kijana wa Kitanzania Dk.Hery Mwandolela ambaye ndio mmikili wa Kliniki hiyo amefanya maajabu makubwa na anastahili kuwa mfano wa kuigwa.
 Mwenyekiti wa Kampuni za IPP Media Dk.Reginald Mengi (katikati) akiwa pamoja na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dk.Hery Mwandolela(kulia) na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo wakiangalia ujumbe uliopo kwenye jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya kuzinduliwa rasmi kwa Kliniki ya Heameda ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu ya magonjwa ya moyo.
 Mkuu wa Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam ambapo ameahidi kutatua kero ya barabara inayoelekea kwenye kliniki hiyo
 Mmiliki wa Kliniki ya Heameda ambaye pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Dk.Hery Mwandolela akizungumza wakati wa uzinduzi wa kliniki hiyo leo jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Kliniki ya Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam Dk.Reginald Mengi akikabidhi cheti maalum kwa Dk.Isaac Maro kwa kutambua mchango wake  katika kliniki hiyo.

RELI TVL UJENZI SGR - Hizi hapa Kilomita 10 Zilizotandikwa Reli, Uzalishaji Mataluma Kuongezeka Hadi 1500

SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE

0
0
SHULE ya sekondari ya Imperial kwa mara ya kwanza imesheherekea 
mahafali ya kwanza ya kidato cha nne mahafari yaliyofanyika jana Oktoba 20,2019.

Akizungumza Katika mahafali hayo Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda  alisema kuwa shule zinajukumu la kuwaandaa vijana kuwa Viongozi Bora kwani waliowengi hutokea shuleni.

Pia alizindua kampeni maalum ya Shule hiyo inayotambua mchango wa viongozi mbalimbali katika kuhamasisha uongozi bora, alisema wanafunzi wanaoaminishwa kuwa wanaweza kuwa viongozi bora tangu wakiwa wadogo hujenga tabia ya wao kujilinda na kujichunga wenyewe.

Mbali na kusifia mandhari nzuri ya shule hiyo Anne alisema anaamini Viongozi wazuri watatoka shuleni hapo, na kuwasihi wazazi kutohangaika kuwapeleka watoto wao mbali ili hali kuna shule kama Imperial yeye viwango vya kimataifa. 

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo bwana Lincolin Mashanda, alisema nayo Imperial Sec School imejiandaa kuzalisha Viongozi hao wa Kesho katika fani na nyanja mbalimbali katika ubora kwa kuzingatia, maadili mema na kwa  kuhamasisha hilo kuanzia Shuleni hapo. 

Mashanda amesema 
"Yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora, mambo haya yakianza kuzoeshwa mapema huwa tabia na muongozo kwa vijana wetu..

Mashanda alikinukuu Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinachosema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti wala sura bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza.

Kiongozi bora ni yule anayeweze Kuyakabili Matatizo au Changamoto
Kiongozi bora ni yule ambaye ana ujasiri wa kutosha wa kukabiliana na kila aina ya changamoto inaweza kujitokeza kwa busara."

"Dunia ya leo imejaa changamoto za kila aina. Kila kukicha kuna jipya na gumu zaidi. Taswira ya uingozi bora inamjenga kijana kujiamini na kujilinda hivyo kuwa sababu ya yeye kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujana kwa matumaini."

"Kiongozi bora lazima awe muaminifu. Uaminifu unaanzia kwenye kuwa mkweli. Na hii nitabia inayoanza utototoni."

"Kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa kusimamia ahadi yake na jitihada anazofanya kutimiza ahadi yake."

"Kiongozi bora lazima ajiheshimu. Na dhana ya kujiheshimu ni pana. Hii ni pamoja na kuheshimu wazazi wako, ndugu, jamaa  marafiki na watu wote. Unapojiheshimu, inakuwa rahisi kuongoza wengine."
:Kiongozi bora huwa anakiu ya kujifunza zaidi na ni mtafiti. 
Kiongozi bora ni Mtendaji
Yote niliyoyataja hapo yanafundishika."

:Sasa pamoja na masomo mengine Imperial secondary school inamuandaa mwanafunzi wake katika mazingira ya kuyatambua haya na kuyafanyia kazi mapema kipindi awapo shuleni. '

Alisema 'Tunaamini ugeni wa  mama Anne S..Makinda katika mahali yetu utaongeza tija na hamasa kwa kile tulichokuwa tukiwaandaa nacho wanafunzi wetu.
 Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda  akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne Imperial Secondary School (ISS) yaliyofanyika jana Msolwa Chalinze.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusheherekea Mahafari ya kwanza ya kidato cha nne. 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu pamoja na wazazi wao katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images