Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MPINA AWATAKA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE ULINZI WA RASLIMALI ZA MIFUGO

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifunua kitambaa katika jiwe la msingi  la ufunguzi  wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel }kushoto}.Picha na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikata utepe kufungua Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kushoto},Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi}kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel.Picha na Mpiga Picha Wetu.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifunua kitambaa katika jiwe la msingi  la ufunguzi  wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel }kushoto}.Picha na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyenyanyua mkono akiwa na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia kwake)  wakati wa ufunguzi wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi. Picha na Mpiga Picha Wetu.

NA JOHN MAPEPELE, MARA
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi za vijiji,wilaya kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali za mifugo badala ya hali ilivyo sasa ya kuiacha ikitoroshwa kwenda nchi za nje kwa kuamini kwamba jukumu la ulinzi wa rasilimali hizo ni la Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake na ikosesha serikali mapato.

Waziri Mpina ameyasema hayo wakati akizundua mnada wa mpakani wa Kimataifa wa Mifugo katika eneo la Kirumi Wilayani Butiama mkoani Mara ambapo ameagiza kufungwa kwa minada yote ya mifugo iliyofunguliwa kinyemela kwani imekuwa kichocheo cha upotevu wa mapato wa Serikali na kuonya wanaoanzisha minada hiyo bila kufuata taratibu zilizopo watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel kuanza mara kuihakiki minada yote iliyopo nchini ili kuibaini ambayo imeanzishwa kinyume cha sheria iweze kufutwa.

“wako watu wanafungua minada kila sehemu wanaamua tu wakati taratibu za ufunguzi wa minada wanazijua kabisa ya kwamba ni lazima wizara iridhie kufunguliwa kwa mnada huo”alisisitiza Waziri Mpina

Amesema Serikali inapotaka kuanzisha mnada inakuwa na malengo ya kuhakikisha biashara ya mifugo inafanyika vizuri na kwamba uanzishaji holela wa minada unadhoofisha mipango inayowekwa na Serikali jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Naye Katibu Mkuu Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel alisema kufunguliwa kwa mnada huo kutasaidia usimamizi na kudhibiti utoroshaji wa mifugo na kuongeza mapato ya Serikali ambapo amesema mnada wa Kirumi umewekwa kimkakati na unatarajia kuvuta wafanyabiashara wa mifugo kutoka katika nchi za jirani na kuliingizia taifa mapato makubwa.

Waziri Mpina amewataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanapanga matumizi bora ya ardhi na kuwawezesha wafugaji kupata huduma zinazostahili ikiwemo malisho na maji badala ya hali ilivyo sasa ambapo kila kiongozi anaona mifugo ni laana kwa taifa.

Pia Waziri Mpina pia alimuagiza Katibu Mkuu Mifugo kuanzisha haraka ofisi itayotoa huduma ya vibali kwa watu wanaotaka kusafirisha mifugo nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo wafanyabishara hao hulazimika kwenda hadi jijini Mwanza kufuatilia vibali hivyo.

Ameagiza kupelekwa kwa mitungi ya kupandikiza mbegu bora ya mifugo katika Mkoa wa Mara na kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa gharama isiyozidi sh 5,000 tofauti na ilivyo sasa ambapo hulazimika kugharamia hadi sh, 100,000 kupata huduma hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alisema Serikali ngazi ya mkoa huo itaendelea kuwachukulia hatua kali watu wote wataoshiriki vitendo vya utoroshaji mifugo nje ya nchi huku akiwaonya watu wanaondeleza vitendo vya wizi wa mifugo kwamba hawatapata tena nafasi katika kipindi hiki cha utawala wa Serikali ya awamu tano.

Malima alisema tayari mkoa huo umepokea mwekezaji wa kiwanda cha maziwa kitakachokuwa na uwezo wa kusindikiza tani 200,000 kwa siku na kusema kuwa itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wafugaji wa mkoa huo kupata soko la uhakika la maziwa yao.


Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Mara, Mrida Mshoja amesema ngombe zilikuwa zinatoroshwa kwenda Kenya na kwamba kufunguliwa kwa mnada huo kutawezesha wafugaji kupata soko la uhakika la mifugo yao na kumshukuru Waziri Mpina kwa kufanikisha azma ya kuanzisha mnada huo.

MASAUNI AZINDUA KAMPENI MAALUMU YA USALAMA BARABARANI NA UDHIBITI WA AJALI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, amewatadharisha wamiliki wa shule zinazotumia magari mabovu kubebea wanafunzi ikiwa ni kinyume na sheria za usalama barabarani hali ambayo inaweza kupelekea ajali. 

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, Naibu Waziri Masauni aliwataka wamiliki wa shule kuhakikisha wanatumia mabasi imara ili kuepusha ajali na kuwaasa madereva wa magari hayo kufuata sheria za barabarani 

“Wamiliki wa shule wanatakiwa wafuate sheria kwa kuacha kutumia mabasi mabovu na kujaza wanafunzi kupita kiasi na tutatumia kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote wakiwa wanaenda shule na kurudi nyumbani. 

“Nawaagiza askari wa usalama barabarani kusimamia sheria ili wamiliki watakaokiuka sharia hizo waweze kuchukuliwa hatua pamoja na madereva watakaobainika kuendesha magari mabovu ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi,” alisema Masauni 

Akitoa ripoti ya matukio ya ajali za barabarani Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Shukuru Amir Ally alisema jumla ya ajali 229 zimeripotiwa ndani ya mwaka huu tofauti na mwaka 2017 ambapo jumla ya ajali 391 zikiripotiwa huku akitoa siri ya kupungua kwa ajali hizo ni ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau wa usalama barabarani. 

Akisoma risala ya uzinduzi huo Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya usalama barabarani ya New Vision, Pily Hamis Ladya alisema wamedhamiria kufikia mikoa yote ya Zanzibar na katika awamu hii ya kwanza wanaanza na shule kumi huku akiahidi kuzifikia shule zote katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi. 

“Tunategemea kutoa elimu hii ya usalama barabarani ili kuweza kuwaepusha na kuwalinda wanafunzi wetu na majanga ya barabarani ili waweze kwenda shule na kurudi nyumbani salama,” alisema

 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati  ya  Uzinduzi  wa  Kampeni  Maalumu  ya  Usalama  Barabarani na Udhibiti  wa  Ajali  katika  Uwanja  wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar.
 Mwanafunzi  wa  Shule  ya  Msingi  Jang’ombe, Aisha Abdallah Haji, akiuliza swali  linalohusiana  na  uvukaji  wa  barabara kwa watu wenye ulemavu wakati wa  Uzinduzi  wa  Kampeni  Maalumu  ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika  Uwanja  wa  Skuli  ya  Jang’ombe, iliyozinduliwa  leo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti  wa  Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), Visiwani Zanzibar.

Mkurugenzi  wa Taasisi  inayojishughulisha  na  masuala  ya  usalama  barabarani ,Pily  Hamisi  Layda (kushoto)  akimkabidhi  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi  Hamad  Masauni, mpango kazi wa  Kampeni  Maalumu  ya Usalama  Barabarani  na  Udhibiti wa Ajali iliyozinduliwa  katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo  Visiwani Zanzibar
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

NDITIYE AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI A BANDARI KAVU, KWALA VIGWAZA

$
0
0

 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala eneo la Vigwaza mkoani Pwani. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Charles Otare na wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT Raymond Kweka.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama katikati) akipata maelezo kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare (anayetoa maelezo). Wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT, Raymond Kweka.
Muonekano wa eneo linaloandaliwa kujenga njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo inayoingia na kutoka bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo.

KOMU,KUBENEA WAWEKWA CHINI YA UANGALIZI CHADEMA

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imewavua nafasi zote za uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu baada ya kukiri kuwa sauti zilisombaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ni za kwao.


Sauti hizo ni zile ambazo wabunge hao wanasikika wakipanga namna ya kumshughulikia Meya wa Ubungo, Boniface Jacob huku Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, akitajwa.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamini Oktoba 18, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya wabunge hao kuhojiwa na kamati kuu na kukiri sauti hizo ambazo zilihusisha mazungumzo ya kuashiria utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho ni za kwao.


“Tumewapa adhabu mbalimbali kwa mujibu wa kanuni 6.5 (d) za chama na kamati kuu iliwaita wabunge hao kuja kujibu tuhuma na walifika na kuhojiwa na walikiri mbele ya kamati kuu ya chama kuwa sauti zilizosikika ni zao.


“Tukafikia maamuzi ya kuwapa adhabu mbalimbali pamoja na kuwavua uongozi tuliwapa onyo kali na kuwataka waandike barua ya kuomba radhi kwa chama na kwa watu waliotajwa katika sauti hizo,” amesema Mnyika.

RC GAMBO:MTUMISHI ALIYECHUKUA PESA ZAIDI(YA MWANANCHI) YA KUUNGANISHA UMEME AIREJESHE HARAKA

$
0
0

Na Vero Ignatus, Karatu


MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Wilaya ya Karatu, Edward Mwakapaju kuhakikisha mtumishi wa shirika hilo aliyechukua pesa kiasi cha Sh. 70,000/= kwa mmoja kati ya mwananchi wa eneo la Mang'ola badala ya Sh. 27,000/= za kuunganishiwa umeme wa REA kuzirudisha mara moja.

Gambo  amesema kuwa haridhishwi na kasi ya usambazwaji umeme unaofanywa na Kampuni ya NIPO Group Ltd kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali vya wilaya hiyo na kumpa agizo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Henry Mhina kuhakikisha anachukua hatua ili wananchi waweza kuunganishiwa umeme.

RC Gambo  aliyasema hayo katika ziara yake ya siku tatu kwaajili ya kukagua miradi ya umeme wa Vijijini ( REA) miradi ya maji  na barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Alisema mtumishi huyo wa Tanesco (jina hakumtaja) alichukua fedha kwa mwananchi wa Man'gola kiasi cha Sh. 70,000 ili amuunganishie umeme wa REA ilihali akijua kuwa gharama ya kuunganisha umeme huo ni Sh. 27,000/= huku wananchi wengine wa vijiji vya Tloma na Ganako wakitozwa Sh. 177,000/= badala ya Sh. 27,000/=.  

Alisema ingawa mtumishi huyo wa Tanesco amefukuzwa kazi lakini hela alizochukua Sh. 70,000/= kutoka kwa mwananchi huyo haijarudishwa hivyo ni vyema sasa hela hizo zikarudishwa kwa mwananchi huyo mara moja huku akiziagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia tatizo hilo mara moja.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo wakipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa TARURA wilaya ya Karatu juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Getamong wilayani humo. Picha na Vero Ignatus

Meneja wa TANESCO Wilaya ya Karatu Edward Mwakapaju akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo juu ya hali ya utekelezwaji wa mradi wa umeme vijijini REA wilayani humo.Picha na Vero Ignatus

Wananchi wa eneo la Kilimamoja wilayani Karatu wakiwa katika mkutano wa hadhara kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Picha na Vero Ignatus.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUONGEZA KASI YA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO KWA KUWA NA WODI YA WATOTO

$
0
0
 Katika kuimarisha na kuboresha matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeendelea kuboresha wodi ya watoto iliyopo katika jengo la watoto ili ifikapo Desemba mwaka huu wodi hiyo ianze kutoa huduma zote kwa watoto.

Wodi hiyo inatarajiwa kuwa na vitanda 32 ambapo vitanda nane vitakuwa katika chumba cha kulaza watoto wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na vitanda 24 katika wodi za kawaida za watoto, vyumba vitatu kwa ajili ya kliniki za watoto pamoja na vyumba kwa ajili ya ofisi .

Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015 hadi 2018 Taasisi imeona jumla ya watoto 8,000 wenye matatizo mbalimbali ya kuzaliwa nayo na yasiyo ya kuzaliwa nayo. Kwa upande wa upasuaji wa moyo jumla ya watoto 889 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na upasuaji wa bila kufungua kifua

Watoto 519 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na kati ya hao watoto 238 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo huku watoto 281 walifanyiwa upasuaji wakati wa kambi maalum zilizowaunganisha madaktari wetu na madaktari kutoka shirika la Mending Kids International, SACH, na mashirika mengine. Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa watoto 370

Kwa upande wa kliniki ya watoto kila siku inatoa huduma ya kati ya watoto 30 hadi 40 na kulaza mtoto mmoja hadi wawili. Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2018 jumla ya watoto 95 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua watoto 60

Zaidi ya asilimia 75 ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na magonjwa yanayoshambulia milango ya mishipa mikubwa na midogo ya moyo. Asilimia 25 ni wale ambao walizaliwa salama na kupata matatizo hayo baada ya kuzaliwa.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
18/10/2018.

RC GAMBO:MTUMISHI ALIYECHUKUA PESA ZAIDI(YA MWANANCHI) YA KUUNGANISHA UMEME AIREJESHE HARAKA

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Karatu. 

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Wilaya ya Karatu, Edward Mwakapaju kuhakikisha mtumishi wa shirika hilo aliyechukua pesa kiasi cha Sh. 70,000/= kwa mmoja kati ya mwananchi wa eneo la Mang'ola badala ya Sh. 27,000/= za kuunganishiwa umeme wa REA kuzirudisha mara moja.

Gambo  amesema kuwa haridhishwi na kasi ya usambazwaji umeme unaofanywa na Kampuni ya NIPO Group Ltd kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali vya wilaya hiyo na kumpa agizo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Henry Mhina kuhakikisha anachukua hatua ili wananchi waweza kuunganishiwa umeme.

RC Gambo  aliyasema hayo katika ziara yake ya siku tatu kwaajili ya kukagua miradi ya umeme wa Vijijini ( REA) miradi ya maji  na barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Alisema mtumishi huyo wa Tanesco (jina hakumtaja) alichukua fedha kwa mwananchi wa Man'gola kiasi cha Sh. 70,000 ili amuunganishie umeme wa REA ilihali akijua kuwa gharama ya kuunganisha umeme huo ni Sh. 27,000/= huku wananchi wengine wa vijiji vya Tloma na Ganako wakitozwa Sh. 177,000/= badala ya Sh. 27,000/=. 

Alisema ingawa mtumishi huyo wa Tanesco amefukuzwa kazi lakini hela alizochukua Sh. 70,000/= kutoka kwa mwananchi huyo haijarudishwa hivyo ni vyema sasa hela hizo zikarudishwa kwa mwananchi huyo mara moja huku akiziagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia tatizo hilo mara moja.
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo wakipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa TARURA wilaya ya Karatu juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Getamong wilayani humo. Picha na Vero Ignatus
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Karatu Edward Mwakapaju akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo juu ya hali ya utekelezwaji wa mradi wa umeme vijijini REA wilayani humo.Picha na Vero Ignatus
Wananchi wa eneo la Kilimamoja wilayani Karatu wakiwa katika mkutano wa hadhara kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Picha na Vero Ignatus .

MPINA AWATAKA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE ULINZI WA RASLIMALI ZA MIFUGO

$
0
0
NA JOHN MAPEPELE, MARA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi za vijiji,wilaya kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali za mifugo badala ya hali ilivyo sasa ya kuiacha ikitoroshwa kwenda nchi za nje kwa kuamini kwamba jukumu la ulinzi wa rasilimali hizo ni la Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake na ikosesha serikali mapato.

Waziri Mpina ameyasema hayo wakati akizundua mnada wa mpakani wa Kimataifa wa Mifugo katika eneo la Kirumi Wilayani Butiama mkoani Mara ambapo ameagiza kufungwa kwa minada yote ya mifugo iliyofunguliwa kinyemela kwani imekuwa kichocheo cha upotevu wa mapato wa Serikali na kuonya wanaoanzisha minada hiyo bila kufuata taratibu zilizopo watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel kuanza mara kuihakiki minada yote iliyopo nchini ili kuibaini ambayo imeanzishwa kinyume cha sheria iweze kufutwa.“wako watu wanafungua minada kila sehemu wanaamua tu wakati taratibu za ufunguzi wa minada wanazijua kabisa ya kwamba ni lazima wizara iridhie kufunguliwa kwa mnada huo”alisisitiza Waziri Mpina
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikata utepe kufungua Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kushoto},Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi}kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifunua kitambaa katika jiwe la msingi la ufunguzi wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel }kushoto}.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyenyanyua mkono akiwa na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia kwake) wakati wa ufunguzi wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi.



WAZIRI MWAKYEMBE ATEUA WAJUMBE WATANO WA BODI YA BASATA,YUMO MSANII MWANA FA NA SINGLE MTAMBALIKE

KLINIKI YA HEAMEDA ILIYOPO BUNJU B DAR YAWEKA KAMBI KUPIMA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

$
0
0
*Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Dk. Mwandolela azungumzia mfumo wa maisha unavyochangia

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KLINIKI ya Magonjwa ya Moyo Heameda iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam imeanzisha kambi maalumu ya siku mbili kwa lengo la kupima na kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo huku ikielezwa sababu za kuongeza kwa magonjwa hayo ni mfumo wa maisha.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa kambi hiyo Mkurugenzi wa Kliniki hiyo ambaye pia ni Daktarii Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Dk. Hery Mwandolela amesema watatoa huduma hiyo kwa siku tatu kuanzia leo, kesho na keshokutwa watafunga rasmi ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi.

Amesema kuwa wameamua kutenga siku hizo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wananchi mbaliimbai ambao wamefika kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza na kwamba uamuzi huo ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii ya Watanzania.

“Tunatoa mwito kwa wananchi waje wapime afya zao bure, Heameda tumeamua kutoa huduma ya matibabu kama sehemu ya kutoa shukrani kwa wananchi wote.Hivyo kwa mwaka huwa tunatenga siku maalumu za kuwa na kambi hiyo.Kwa leo waliofika hadi saa saba mchana ni watu zaidi ya 130 na wanaendelea kuja.Nasi tunawakaribisha maana tupo kwa ajili ya kuwahudumia,”amesema Dk.Mwandolela.

Kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini amesema kasi imekuwa kubwa sana na takribani kwa miaka 30 hali inazidi kuwa mbaya hasa katika magonjwa ya kupanda kwa shinikizo la damu, sukari na saratani.”Mfumo wa vyakula tunavyokula na kutofanya mazoezi ni moja ya sababu kubwa ya magonjwa hayo.Pia msongo wa mawazo nao umechangia kuongeza kwa ugonjwa wa kupanda kwa shinikizo la damu,”amefafanua.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo . Dk. Henry Mwandolela wa Heameda Madical Clinic akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali yake iliyoko Bunju B jijini Dar es salaam wakati wa kambi ya siku mbili ya uchunguzi wa Magonjwa mbalimbali inayofanyika hospitalini hapo kuanzia saa mbili asubuhi mpaka jioni , Kiliniki hiyo itafungwa rasmi ziku ya jumamosi 
Baadhi ya madaktari wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi mbalimbali waliokwenda kupata huduma ya matibabu 
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo wakitoa huduma kwa wananchi waliofika katika kambi hiyo.
  
Baadhi ya wananchi wakisuburi huduma wakati kambi hiyo ikiendelea kwenye hospitali ya Heameda Medical Clinic.


SERIKALI KUREJESHA HALI YA WANANCHI KUJILETEA MAENDELEO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Kibiti, Pwani
Wananchi wa Kijiji cha Mweyubaruti Kata ya Mwambao Wilaya Kibiti wametakiwa kujenga hali ya kujiletea maendeleo badala ya kusubiri serikali kwakuwa mwelekeo wa serikali ni kurejesha hali iliyopotea  ya wananchi kuchangia   maendeleo yao wenyewe. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile amesema hayo wakati alipotembelea Kijiji hicho kujionea shughuli za wananchi kujiletea  maendeleo.

"Zamani wananchi walikuwa wanajenga shule wao wenyewe au kushiriki kwa kujitolea nguvu zao na serikali inataka kurejesha hali hii na huu ndio mwelekeo wa serikali". Alisema Dkt.Ndugulile.

Wananchi kwa kutumia nguvu juhudi zao wamefanikiwa ku 
anzisha  mradi wa  shule shikizi kwa ajili ya watoto wadogo ambao hawawezi kwenda umbali mrefu kuhudhuria masomo ya awali.

Wakati huhuo Katibu wa Kitongoji Kijiji hicho Bw. Alfan Matimbo akitoa taarifa Kwa Naibu Waziri Ndugulile  kuhusi  taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo alisema wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhulia masomo katika shule ya  Msingi Kivinje B kutokana umbali mrefu kwani shule hiyo iko umbali wa km.5 kutoka Kijijini hapo.

Aidha Mzee Matimbo aliongeza kuwa umbali wa Kijiji hicho na shule ya Msingi Kivinje B ni chanzo cha utoro kwa watoto wa Kijiji chake  lakini pia wanafunzi wengi wamekatiza masomo hivyo wananchi wamejipanga kujenga shule ili kuwezesha watoto wao kuendelea na masomo.

Aidha katika juhudi za kupambana na tatizo hilo Kijiji kinamlipa mwalimu wa kujitolea ambaye analipwa sh. 1500 kwa kaya kwa mwezi lakini pia wale wanaoshindwa kutoa fedha hii uchangia mazao ya chakula kama miogo na nanasi.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea Maelezo ya Mradi wa ujenzi ya Shule Shikizi iliyopo kata ya Mwambao Kijiji cha Mweyubaruti Kibiti Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea mchango wa ujenzi wa shule ya Mradi wa ujenzi ya Shule shikizi iliyopo kata ya Mwambao Kijiji cha Mweyubaruti Kibiti Mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhiwa  mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa shule shikizi iliyopo katika Kijiji cha Meyebaruti  kilichopo katika Kata ya Bungu Kibiti Mkoani Pwani. Picha Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEC YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI NA UKEREWE

$
0
0
Na Idara ya Habari-NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo kwenye majimbo mawili na kata 26 za Tanzania Bara.

Majimbo hayo ni pamoja na Jimbo la Babati Mjini lililopo Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara na Jimbo la Ukerewe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza

Akisoma taarifa kwa umma Jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi) Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salum Mbarouk amesema kwamba uchaguzi huo utafanyika sambamba na uchaguzi wa Jimbo la Simanjiro na Serengeti pamoja na kata 21 za Tanzania Bara uliotangazwa awali.

“Nafasi hizo wazi zimetokana na waliokuwa Wabunge wa Majimbo hayo Bwana. Joseph Michael Mkundi (Ukerewe) na Bi. Pauline Philipo Gekul (Babati Mjini) kujiuzulu kutoka kwenye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),” alisema Jaji Mbarouk.

Alifafanua kwamba Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Majimbo hayo mawili.

“Uchaguzi huu mdogo katika Majimbo ya Babati Mjini na Ukerewe utafanyika sambamba na uchaguzi katika Majimbo ya Serengeti, Simanjiro pamoja na Kata 21 zilizotangazwa awali….,” alisema.

Akisoma ratiba ya uchaguzi huo, Jaji Mbarouk amesema “fomu za uteuzi  wa  wagombea zitatolewa kati ya  tarehe 28 Oktoba hadi 3 Novemba mwaka huu, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu, kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 4 Novemba  hadi tarehe 1 Desemba mwaka huu na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 2 Desemba, mwaka huu”.

Ametoa wito kwa wadua wa uchaguzi “Tunapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo”. 

Katika hatua nyingine, Jaji Mbarouk amesema Tume imepokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 26 za Tanzania Bara.  

Aliongeza kuwa kwa  kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa taarifa kwa Umma kuhusu uwepo wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Majimbo ya Babati Mjini na Ukerewe   pamoja na Udiwani katika Kata Ishirini na Sita (26) za Tanzania Bara.

Majina ya Halmashauri na Kata zenye uchaguzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo, Halmashauri ya Wilaya ya Temeke (Mtoni), Halmashauri ya Manispaa ya Ilala (Mnyamani), Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa (Salanka), Halmashauri ya Wilaya ya Magu (Kabila), Halmashauri ya Misungwi (Sumbugu, Buhingo), Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe (Bukiko), Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Miteja, Kivinje, Singino, Somanga na Mitole).

Nyingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Songea (Matarawe, Ruvuma), Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa (Mtipwili), Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti (Magange, Ring’wani, Rung’abure, Natta na Rigicha), Halmashauri ya Mji wa Babati (Maisaka), Halmashauri ya Wilaya ya Meru (Nkoanekoli), na Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti (Salale).

Wakulima wachangamkia fursa za Sim Akaunti ya Benki ya CRDB

$
0
0
 Meneja usambazaji wa Sim Akaunti wa benki ya CRDB, Yusuph Mwenda akizungumza jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa kuchezesha droo ya promosheni ya SimAkaunti, iliyofanyika leo, Mikocheni jijini Dar es salaam.

MKAZI wa mkoani Ruvuma, Zenidius Luwo na mfanyabiashara wa nafaka kutoka Arusha, Hanset Munisi leo wameibuka washindi kwenye promosheni ya SimAkaunti inayondeshwa na benki ya CRDB.

CRDB imekuwa ikitoa zawadi kwa wateja wake wanaojisajili na kutumia huduma hiyo ambapo huwapatia fedha tasrimu. Luwo aliibuka mshindi wa shilingi milioni mbili huku Munisi akipata milioni moja. Tangu kuanzishwa kwa promosheni hiyo mwezi huu, wakulima wameoongoza kujishindia zawadi kutoka benki hiyo.
Akizungumza baada ya kuchezesha droo ya kuwapata washindi hao, Meneja Masoko wa benki hiyo, Ariel Mkony, alisema mbali na washindi hao wawili, pia benki hiyo imewapata washindi wengine 10 wa shilingi 100,000.

"Lengo letu ni kuona wateja wetu wananufaika na bidhaa zetu.. SimAkaunti inaweza kuwasaidia sana watu wa aina mbalimbali, kuanzia mtu mmoja mmmoja na hata vikundi," alisema Ariel.

Aidha, mmoja wa washindi hao, Munisi, alisema fedha hizo alizozipata kama zawadi zote ataziingiza kwenye biashara yake ya vyakula.

Kwa upande wake, Meneja usambazaji wa Sim Akaunti wa benki hiyo, Yusuph mwenda, alisema wataendelea kuiboresha huduma hiyo kuwanufaisha zaidi wateja wao. Promosheni hiyo itadumu kwa kipindi cha miezi minne ambapo wataendela kutoa zawadi kwa wateja wao.

MAKAMU WA RAIS AHUDHULIA MCHAPALO NA WADAU WA UTALII

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Sekta ya Utalii imeendelea kukua kwa kasi sana Duniani kutokana na maendeleo ya teknolijia na upatikanaji taarifa.

Makamu wa Rais aliyasema hayo jana jioni wakati alipokutana na Wadau wa sekta ya utalii katika Mchapalo ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

Sekta ya Utalii imeendelea kukua ambapo mwaka 2017 zaidi ya Watalii 433,474 waliitembelea Zanzibar ambao ni asilimia 32 zaidi ukilinganisha na mwaka 2014.

Idadi ya Watalii walioandikishwa kwa Tanzania nzima ni milioni mbili kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na milioni 1.28 mwaka 2016.

Makamu wa Rais amesema kuwa ujenzi wa mahoteli, kuongezeka kwa ndege, na juhudi za kukuza masoko kunakufanya Zanzibar kuwa eneo zuri zaidi linalovutia watalii.

“Tunahitaji wawekezaji binafsi ili kupanua na kuendelea kuboresha Utalii, kwa kufanya hivyo, tunahitaji kuwezesha miradi kubwa ya uwekezaji. Aidha, kufikia ukuaji wa juu wa utalii ni jitihada za pamoja, ambapo ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ni muhimu.” alisema Makamu wa Rais.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alimshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Utalii Zanzibar 2018 (Zanzibar Tourism Show 2018) ambapo aliuambia umma wa shughuli hiyo kuwa Mhe. Samia ni mmoja wa msingi muhimu wa ukuaji wa Utalii Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wadau wa utalii katika mchapalo ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale katika hoteli ya Park Hyatt Zanzibar jana jioni tarehe 17, Oktoba 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wadau mbalimbali wa utalii katika mchapalo ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale katika hoteli ya Park Hyatt Zanzibar jana jioni tarehe 17, Oktoba 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

TFDA YAIKUTANISHA TBS,GCLA,TAFFA KUJADILI UBORESHAJI WA UINGIZAJI WA BIDHAA NCHINI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii 
MAMLAKA ya chakula na dawa nchini (TFDA) kwa kushirikiana na shirika la Viwango nchini (TBS) , Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) chama cha mawakala wa forodha nchini (TAFFA) wamekutana na kujadili namna ya kuimarisha na suala zima uingizaji wa bidhaa nchini. 

Akizungumza katika mkutano huo kaimu mkurugenzi mkuu wa TFDA Agnes Kijo ameeleza lengo la mkutano huo ni kukumbushana ili kuweza kusaidia kuboresha huduma kwenye taasisi hizo katika utoaji wa mizigo kwa kufuata sheria kwani bila kufanya hivyo hawatafikia malengo ya taifa. 

Amesema kuwa waingizaji wa mizigo na mawakala wa forodha lazima wawe pamoja katika kulinda afya za wananchi. 

Ameeleza kuwa wamekaa na wadau wengi wakimemo wenye viwanda na awamu hii wameamua kukaa na mawakala hao wa uingizaji mizigo nchini ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuweza kuzitatua na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao. 

Agnes ameeleza kuwa wote wapo kwa ajili ya kuijenga nchi hivyo ni lazima kuhakikisha kila mamlaka inasimamia ipasavyo majukumu yao ili kuhakikisha kuwa suala la uingizaji wa mizigo kwa kuzingatia umuhimu wa wadau hao na amehaidi kuwa taratibu zitaenda kufanyika kielektronoki ili kurahisisha mchakato mzima. 

MKemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ,Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelince Mafumiko amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa wadau hao hasa katika uingizaji wa kemikali kwa ajili ya viwanda na ameeleza kuwa wadau hao ndio huwezesha uingizwaji wa bidhaa hizo hivyo ni fursa kwao katika kutoa taratibu na mrejesho wa changamoto katika kutekeleza ufanisi, na changamoto zitakazotolewa na wadau watazifanyia kazi na amesema kuwa huo ni mwanzo mzuri katika utoaji wa huduma. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa shirika la viwango (TBS) Lazaro Msasalaga amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuongeza ufanisi katika mchakato wa utoaji wa mizigo bandarini pamoja na changamoto zinazogusa taasisi zao na kuendeleza uchumi wa nchi. 
Kaimu Mkuruergnzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Agnes Kijo akizungumza na wadau wa wakala forodha katika mkutano wa kujadili masuala mbalimbali ya utaoaji wa huduma katika bandari kwa bidhaa za vyakula uliofanyika jijini Dar es Salaam. 
Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akizungumza na vyombo vya habari wakati wa mkutano wa uliowahusisha wakala wa uingizaji wabidhaa ndani ya nchi kupitia kwa mawakala wa forodha juu ya uingizaji wa bidhaa hizo na mamlaka za utoaji wa vibali uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa wadau wa forodha katika mkutano wa ulioitishwa na TFDA kwa ajili ya uboreshaji wa huduma katika uondoshaji wa mizigo katika bandari.

TMA YATABILI MVUA KATIKA MIKOA YA PWANI, KUANZA KUNYESHA NOVEMBA 23

$
0
0
Na Karama Kenyunko, glogu ya jamii

MAMLAKA ya hali ya Hewa nchini,( TMA) imesema mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.

Pia TMA imetoa utabiri wa msimu wa mvua wa kuanzia mwezi Novemba 2018 hadi Aprili 2019 kwa mikoa inayopata mvua Mara moja kwa mwaka ambazo zinatarajiwa kuwa za juu na wastani.

Akizunguza wakati akitoa utabiri huo, jijini Dar es Salaam leo Oktoba 18, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Agnes Kijazi amesema mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kisini mwa mkoa wa Morogoro, Lindi na Mtwara. Huku maeneo ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songea yakitarajiwa kuata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

"Kutokana na mifumo ya Hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka, maeneo yaliyosalia ya mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Amesema, mvua za msimu ni mahususi kwa maeneo ya magharibi mwa nchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini magharibi, kusini mwa nchi, ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro ambayo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.


Aidha Kijazi amezitaka sekta mbalimbali zinazotumia taarifa ya hali ya hewa katika kutekeleza majukumu yao kama vile, kilimo na usalama wa chakula, Afya, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, uchukuzi na Mawasiliano, Nishati, Maji na nyingi za kuchukua taathari kufuatia mvua hizo nyingi kwani inaweza kusababisha madhara mengi katika Jamii nzima.


Kwani matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza kupelekea maji kutuama na kusababisha mafuriko.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (katikati) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa ya msimu wa mvua leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utabiri, Samwel Mbuya na Mkurugenzi wa Utabiri TMA, Dk. Hamza Kaberwa (kulia).
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya Hewa nchini( TMA) Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya Hewa nchini( TMA) Agnes Kijazi  jijini Dar es Salaam leo kuhusu mvua katika Mikoa ya Pwani ikiwemo Dar es Salaam zinatarajiwa kuanza Novemba 23 mwaka huu.

JESHI LA POLISI LAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KUKUTWA NA GONGO

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunamshikilia mtu mmoja aitwaye Bilenjo Paul, miaka 46, mkazi wa Igombe, kwa kosa la kupatikana na pombe ya moshi (gongo) kiasi cha lita arobaini (40) pamoja na dawa ya kulevya aina ya bhangi kiasi cha kilogram mbili (2) , huko maeneo ya Igombe Wilaya ya Ilemela Jiji na Mkoa wa Mwanza, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Tukio hilo limetokea tarehe 17.10.2018 majira ya saa 11:00hrs baada ya Polisi kufanya doria maeneo tajwa hapo juu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na kiasi hicho cha pombe ya moshi/ gongo pamoja na dawa ya kulevya aina ya bhangi. Jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tunatoa onyo kali kwa wananchi wote wanaojihusisha na shughuli hizo za uuzaji na utumiaji wa pombe haramu ya gongo na dawa za kulevya waache mara moja na endapo mtu/watu watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Katika tukio la pili, mwanafunzi mmoja wa shule ya secondary ya Sengerema high school aitwaye Ayoub Yahya @ Petro , miaka 19, anayesoma kidato cha 5 mchepuo wa PCB, mwenyeji wa Kyerwa-Kagera, amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya neti (chandarua) aliokua ameifunga kwenye mti uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa shule hiyo, iliyopo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Tukio hilo limetokea tarehe 18.10.2018 majira ya saa 06:00hrs asubuhi, hii ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.

Polisi tulifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu mahali hapo. Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafaamika, Polisi bado tunaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

Imetolewa na;
Advera Bulimba –ACP
Kaimu Kamanda wa Polisi (M) Mwanza
18, October 2018.

AWESO AITAKA DAWASA KUWEKA MIRADI MIPYA PEMBEZONI MWA MIJI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amewataka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) kuweka miradi ya maji pembezoni mwa miji ili wananchi wapate maji.

Aweso amewashukuru pia Shirika la PDF chini ya Shirika la maji la Water Aid kwa kufanikisha miradi ya majisafi na majitaka ya kibondemaji na Toangoma.

Akizungumza baada ya kuzindua mradi wa majisafi wa Kibondemaji uliojengwa kwa ushirikiano wa DAWASA NA  Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid Tanzania.

Aweso amesema kuwa, utekelezaji wa mradi huo ni katika kukabiliana na changamoto ya ukuaji wa watu kwa haraka katika miji na lengo kuu ni kuona 2020 asilimia 95 wananchi wanapata maji safi na salama ya uhakika.

Amesema kuwa, kuna miradi 12 ya maji ya visima virefu vinavyojengwa katika Manispaa ya Temeke inayojengwa ikiwemo na mradi wa majitaka na vyoo vya umma uliochini ya Benki ya umma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kukamilika kwa mradi wa Kimbiji Mpera utaweza kuondoa changamoto kubwa ya maji pembezoni mwa Mji ambap kufikia Desemba mkandarasi atawakabidhi visima vinane.

Luhemeja amesema kuwa, tayari ana Bilioni 3 mkononi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundo mbinu ya maji na kupitia mapato ya DAWASA wametenga asilimi 35 kwa ajili ya kuweka miundo mbinu kwenye maeneo tofauti ikiwemo Kipawa kuelekea Buza, Kibamba , Kisarawe hadi Pugu.

Mradi wa Majisafi uliopo kata ya Kibondemaji na Charambe unalenga kuhakikisha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wakazi wa mitaa ya Kibondemajj A na kurasini mji mpya kata ya Charambe watakaonufaika na mradi huo.

Mradi wa maji kibondemaji -Charambe utahudumia mitaa minne ambayo ni mtaa wa Kibondemaji A, majimatitu C , Mchikichini na Kimbangulile pamoja na Mtaa wa Kurasini Mjimpya uliopo kata ya Charambe.

Mradi wa Majisafi una jumla ya urefu wa Kilometa 11 na kisima chenye urefu wa mita 180 chenye uwezo wa kutoa maji kiasi cha Lita 224,000 kwa siku ikijumuisha vibanda 7 vya kuchotea maji (water Kiosks).

Gharama ya mradi wa Majisafi ni Milioni 187 za Kitanzania ukiwa na malengo ya kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Kibondemaji, mbali na hilo pia kuwajengea uwezo wa kibiashara wajasiriamali wadogo wa shughuli za usafi wa mazingira.

Pia mradi huo utasaidia upatikanaji wa huduma za udhibti wa majitaka kwa wakazi wa kata za Kibondemaji, mianzini, Charambe, Kiburugwa na Kulingule.

Shirika PDF chini ya Shirika lla Water Aid limetumia kiasi cha Milioni 547.4 kwa miradi ya Majisafi na Majitaka  na kwa pamoja wamesaini mkataba maalumu unaompa mamlaka kamili ya usimamizi wa mradi huo kwa DAWASA
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akimtua mama ndoo kichwani baada ya kuzindua mradi wa majisafi Kibondemaji uliojengwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya shirika la Water Aid Nchini Tanzania. Kulia ki Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja
Meneja Mradi wa Majisafi na Majitaka kutoka Shirika la PDF Mhandisi Elias Kazingoma akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa mradi wa majisafi Kibondemaji uliofanyika leo Mbagala Charambe Jijini Dar es Salaam.
Utiaji saini wa makubaliano ya kukabidhiwa mradi wa majisafi Kibondemaji na majitaka Toangoma kuanza kusimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Watiaji saini ni Water Aid, Manispaa ya Temeke, Shirika la PDF, DAWASA na Wadau wengine.
Wadau wakifuatilia uzinduzi huo.

DC MURO AVIONYA VYAMA VYA SIASA KUTODUMAZA MAENDELEO

$
0
0
Na Imma Msumba, Arumeru

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro amevitaka vyama vya siasa kuacha  malumbano na mvutano isiyokuwa na tija kwa wananchi wa Arumeru na badala yake amewataka kuungana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru.

Mh. Muro ameyasema hayo baada ya kuingilia kati mgogoro wa umiliki wa jengo ambalo awali lilikuwa likitumiwa na chama cha ushirika kata ya Ilikiurei hatua iliyosababisha kufungwa kwa ofisi ya serikali ambayo ilikuwa ikihudumia wananchi wa vitongoji viwili.

Kwa upande wao wananchi wanaoishi katika vitongoji hivyo mbali na kumpongeza Dc Muro kwa kuchukua hatua kwa haraka kuwa ofisi hizo zifunguliwe wamesema uamuzi huo utawasaidia kupata huduma ambazo wamekuwa wakizikosa kwa muda mrefu kutokana na mvutano wa umiliki wa jengo hilo kutoka kwenye vyama viwili vya siasa.

Baadhii ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro alipokuwa akizungumza nao

SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

$
0
0
Na Khadija Seif, Blogu ya Jamii
KAMPUNI ya mchezo wa kubashiri ya sportpesa  imechezesha droo   ya 28 ya promosheni ya shinda zaidi na sportpesa, ambapo Amri Nicolas(28) kutoka Kigoma ameibuka mshindi wa Bajaji RE.

akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa sportpesa Abass Tarimba ameeleza kuwa kuna  ongezeko kubwa la zawadi Kwenye promosheni hiyo. 

Tarimba ameeleza kuwa  wachezaji wa sportpesa kupitia mitandao yote wana nafasi ya kushinda  zawadi mpya .

Amesema kuwa  zawadi hizo zikiwemo smartphone, jezi za klabu ya Simba au Yanga pamoja na tiketi ya kuhudhuria mechi za ligi ya hispania na Uingereza kila mwezi.

Tarimba amesema kuwa  kutokana na ukubwa wa promosheni hiyo kwa sasa wameamua kuongeza zawadi zitakazotoka kila wiki na kila mwezi na
Ongezeko hilo la zawadi  limewekwa kwa lengo la kuhamasisha  wateja waweze kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali kupitia mchezo huo wa kubashiri.

Amefafanua pia wateja waendelee kubashiri kwa wingi ili kujiweka Kwenye nafasi ya ushindi mnono ambapo unaweza kucheza kupitia mitandao yote, na mpaka sasa washindi kutoka Mikoa 13 wamepatikana ikiwemo Dar es salaam, Kigoma, Mwanza,Tanga, Singida, Ruvuma , Morogoro, Iringa, Kahama, Songwe, Mbeya, Pwani na Lindi. 
 Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa sportpesa Abass Tarimba(kulia) pamoja na  Mtangazaji wa Kipindi cha shinda  zaidi na SportPesa  Happiness Wandela(kushoto) wakionyesha Jezi ya Yanga kama zawadi kwa mshindi wa Promosheni ya Sinda na Sportpesa ambayo inatoa zawadi hizo zikiwemo smartphone, tiketi ya kuhudhuria mechi za ligi ya hispania na Uingereza kila mwezi.
 Mtangazaji wa Kipindi cha shinda  zaidi na SportPesa Happiness Wandela(kushoto) akizungumza na mmoja wa shindi wa shindano hilo leo. Kulia ni  Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa sportpesa Abass Tarimba
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images