Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

PROFESA MKUMBO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUWEKEZE KWENYE MIRADI YA MAJI

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa semina ya miradi ya maji iliyofadhiliwa na Water Aid uliojengwa Kibondemaji na Toangoma.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa serikali imezitaka mamlaka za maji kujiendesha kikamilifu ikiwemo  kuwekeza moja kwa moja kwenye miradi ya maji.

Hayo ameyasema Profesa Mkumbo wakati wa semina iliyowahusisha wadau mbalimbali wa maendeleo inayohusu miradi ya maji ya Toangoma na Kibondemaji.

Amesema kuwa, kumekuwa na utelekezaji mbalimbali wa miradi ya maji unaofanywa na serikali kwa kuwekeza kikamilifu ila kwa sasa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuwa kwa sasa mamlaka zote zianze kujiendesha.

Ameeleza kuwa, wadau mbalimbali wa maendeleo wamekuwa wanashiriki kwa kiasi kikubwa kwenye uwekezaji wa miradi ya maji na suala hilo limekuwa na mchango mkubwa sana kwa serikali.

Profesa Mkumbo amesema zaidi ya mamlaka za maji 14 nchini kote kwa sasa zinajiendesha zenyewe na wamefanikiwa kwa asilimia 100, ambapo mamlaka hizo ni Kama Dar es Salaam, Kilimanjarao, Arusha, Sumbawanga, Mtwara na zingine.

Akizungumzia mradi wa Toangoma na Kibondemaji, Mkumbo amesema kuwa utasaidia wananchi wa maeneo hayo kuachana na uharibifu wa mazingira kwa kutiririsha maji taka.

Kwa upande wa Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Temeke Damas Primy amesema Manispaa nzima ina kata 23 na idadi ya watu Milioni 1.3  na mradi Toangoma wa Kuchakata maji taka utawanufaisha zaidi wananchi kutokana na faida zitakazopatikana kwenye maji hayo.

Primy amesema kuwa, manispaa imeshirikiana na nMamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika ujenzi wa mradi huo wa kuchakata maji taka uliodhaminiwa na Water Aid.

Mradi huo utawasaidia wananchi walio na kipato kidogo kuweka kuondoa maji hayo majumbani kwao kutokana na gharama za usafirshaji wa maji taka hayo, na utasaidia katika kuondoa uchafu majumbani, kupunguza magonjwa ya mlipuko, kuongeza kipato kutokana na mazao yanayotokana na maji hayo ikiwemo mbolea, maji kutumika kwa shughuli za kilimo, upatikanaji wa Biogas.

Kwa upande wa DAWASA, wameweka wazi kuwa mradi huu ulianza 2016 na kumalizika Mei 2018 na utakuwa ni wa majitaka na wakiwa umefadhiliwa a Water Aid ila wao kama mamlaka ya maji ya Mkoa wa Dar es Salaam wameweza kuwa nao kwenye masuala ya miundo mbinu na mfumo huo wa uchakataji maji ni wa asili na hautatumia dawa.
Mkurugenzi wa Tanzania wa Water Aid Ibrahim Kabole akielezea jambo kwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo kuhusina na mradi wa uchakataji maji uliofadhiliwa na tasisis yao uliojengwa Kibondemaji na Toangoma.
Mwakilishi kutoka Chuo cha Ardhi Edward Ruhinda akizungumzia mradi wa Uchakataji maji na namna wananchi wanavyo haribu mazingira kutokana na maji taka.
 Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiendelea kufuatilia  semina ya mradi wa uchakataji maji taka uliojengwa Kibonde maji na Toangoma.


ALIYEKUWA RAIS WA MIGODI YA MADINI AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

0
0
Na Karama Kenyunko, glogu ya jamii
ALIYEKUWA Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo leo Oktoba 17.2018 wemefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD milioni  112.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja  Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Shadrack  Kimaro na Jackilline Nyantori.

Mbali na Mwanyika na Lugendo, washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama 3, mashtaka yavkughushi 7.

Utakatishaji wa fedha 17, Kuwasilisha nyaraka  za uongo  kwa  Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa shtaka moja, kukwepa kodi, mashtaka 8 na shtaka moja la kutoa Rushwa.
Akisoma hati ya mashtaka wakili Nchimbi amedai washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali huko washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.

Pia mshtakiwa Mwanyika (56), na Lugendo (46), wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

 Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Mei 16.2008 na Desemba 31,2008 huko Kahama na Biaramulo, walitoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa TRA kwa nia ya kukwepa kodi kulipa USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Aliyekuwa Rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo mwenye shati ya drafti akitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kujibu tuhuma zinazomkabili.

RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA KWANZA YA UTALII ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein kulia  alipotoa hotuba  ya Ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.katikati ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan na Mwisho kushoto ni Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo.
 Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi wa Serikali waliohudhuria katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed
Shein kushoto akipata maelezo kuhusiana na Vitu mbalimbali vya kizamani ikiwemo Pishi katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein wapili kushoto akiuliza maswali kwa Meneja Mkuu  wa Kampuni ya Com Net Keith McCormick alipotembelea Banda hilo katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV

0
0
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekutana kujadili suala la ufungaji kamera maalumu za kudhibiti na kuzuia uhalifu.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema Serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera hizo katika miji yote mikuu nchini.
Waziri Masauni alisema lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani, uporaji wa fedha katika taasisi za fedha.
“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu.
“Teknokolojia haiepukiki katika kudhibiti, Serikali tumejipanga na hivi karibuni tutaanza kufunga kamera za CCTV  katika miji mikuu na maeneo ya mikoa iliyoko mipakani ili  kudhibiti wahalifu kutoka nje ya Tanzania,” alisema Masauni
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub alisema tayari washafunga kamera hizo ambazo zilizinduliwa Oktoba 3, mwaka huu.
Alisema uzinduzi wa kamera hizo ulifanywa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.
“Mfumo huo ni muhimu na tumehakikisha unaimarisha usalama katika mji wa Zanzibar ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na salama na tayari ushaanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa Zanzibar,” alisema.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub (kushoto), wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto).​Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto).​Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

ALIYEKUWA MKURUGENZI TPA NA WENZAKE WAPELEKWA KIZIMBANI KWA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),  Ephraim Mgawe na wenzake watatu wamefikiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 984.8.

Mbali na Mgawe washtakiwa wengine ni, Wajumbe wa Bodi ya Manunuzi ya TPA, Happiness Senkoro, Apolonia Mosha na Theophil Kimaro.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita akisaidiana na Wakili wa Takukuru Maghela Ndimbo, amedai, Septemba 28,2010 katika ofisi za TPA zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa walitenda kosa

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Wilbard Mashauri. Imedaiwa, siku hiyo mshtakiwa Mgawe akiwa mtumishi wa umma kama Mkurugenzi Mkuu na ofisa masulufu,  alitumia madaraka yake vibaya kwa kushuhudia mikataba kati ya TPA na Kampuni Leighton Offshore Pte Ltd 19800397 na kupata faida ya Sh. 984,828,000 baada ya kuvunja sheria ya manunuzi kwa kuiwezesha kampuni hiyo kupata upendeleo.

Aidha mshtakiwa senkoro, Mosha na Kimaro wanadaiwa Julai 13,2010 katika ofisi ya TPA, wakiwa watumishi wa umma na wajumbe wa bodi ya manunuzi, walitumia vibaya madaraka kwa kuidhinisha zabuni na kuvunja sheria ya manunuzi ya umma kwa kuiwezesha Kampuni ya Leighton Offshore Pte Ltd kupata faida ya Sh. 984,828,000.

 Katika shtaka la tatu imedaiwa Siku na mahali hapo, washtakiwa wote waliisababishia TPA kupata hasara ya Sh. 984,828,000.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na kesi imeahiriashwa hadi Oktoba 30 itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Akitoa masharti ya dhamana, Hakimu amewataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa wenye barua na nakala za vitambulisho vya uraia watakaweka bondi ya sh.. Milioni 15.

Pia wametakiwa kuwasilisha fedha taslimu Sh. milioni 100  au kuweka hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.

Ni mshtakiwa wa pili na wa tatu ndio waliofanikiwa kutimiza masharti ya dhamana huku mshtakiwa wa kwanza na wa nne wakipelekwa mahabusu
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),  Ephraim Mgawe na wenzake watatu wakiingia katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 984.8.

CARDINAL PENGO: MIAKA 150 YA KANISA KATOLIKI ITUMIKE KUIMARISHA UMOJA NA AMANI YA KITAIFA ILIYOPO

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
ASKOFU  Mkuu Kanisa Katolini Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycap Cardinali Pengo ametoa salamu na ujumbe kwa Wakatoliki wote nchini kutumia muda huu wa kuadhimisha miaka 150 ya ujio wa kanisa  yatakayofanyika bagamoyo kwa kudumisha amani na unjilishaji hapa nchini.

Cardinal Pengo amesema tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo hapa nchini Kanisa nchi yetu imetuwekea mazingira mazuri ya kuabudu na uhuru wa kuabudu nchini.

"Tunao uhuru wa kuabudu maana yake sio kanisa katoliki ndio libaki peke yake ibada zinafanyika kulingana na madhehebu na dini kama dini nyingine nchini na mashariki hatugombani licha ya kusikia watu wanamulekeo tofauti lakini bado atujasikia watu wakigombana kwa ajili ya dini"amesema Pengo.

Cardinal Pengo amesema kuwa katika miaka 150 ya Kanisa hapa Tanzania Bara Kanisa limeweza kutoa huduma za kijamii kwa kujenga Vituo vya Afya, Shule na huduma za Mawasiliano katika maeneo mbalimbali.

Pia amesema juu ya migogoro katika Makanisa na kusema kuwa migogoro katika Kanisa jambo linasikitisha haipaswi kuwepo kama watu wapo wanatafuta amani na wanamalengo kama ya Kanisa ni vyema ikakoma kabisa.

amemaliza kwa kusema kuwa katika kuhadhimisha miaka 150 ya Kanisa angetamani matokeo yake ni kuimarika kwa uinjilishaji na chimbuko lake jambo kuu lilete Mungano kwa wananchi wote licha ya kuwa na tofauti zetu za kidini na kiimani.
 Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Cardinali Pengo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Jubilei ya Miaka 150 ya kanisa Katoliki tangu liingie Tanzania bara na kusambaa mikoani.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifatilia Mkutano wa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar es SalaamMwadhama Polycap Cardinali Pengo uliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam leo.

INTRODUCING NEW SONG "POVU" BY TWANGA PEPETA BAND

Acacia is again facing a serious hardship following accusation for involvement in criminal offences of tax evasion in Tanzania.

0
0

Today, the then Vice President Corporate Affairs of Acacia, Mr Deo Mwanyika (front)  and Mr. Alex Lugendo - Chief Advisor - Government Relations (between policemen), together with Pangea Minerals Limited, North Mara Gold Mine, Exploration Minieres Du Nord Ltee and Bulyahulu Gold Mine Limited, were brought by the Director of Public Prosecution in Tanzania before Resident Magistrate's Court at Kisutu, Dar es Salaam  to answer  charges for  offences of conspiracy to commit  organized crimes of defrauding the Government of Tanzania,  money laundering, tax evasion and corruption.  

On diverse  dates and places, between 2008 to 2017, the accused are alleged to conspired  in committing crime of tax evasion.  In a 39 Counts charge sheet, the six accused are alleged to have committed serious crime related to non-remittance of tax withheld; non-payment of tax upon payment; unlawful cash distributions; non-payment of corporate tax on profit distributions; non-payment of withholding tax on payment of dividends to shareholders; employment  a tax evasion scheme by sheltering  investments; charging interest on interest free loans hence enjoying unlawfully, the benefits of Mining Development Agreements  which exempted tax on loan interest and at the same time eroding profit for corporate tax purposes; Abuse of tax exemptions facility granted to mining companies; fraudulent  computation and payment of royalties from mineral and mineral concentrate sales; overstating expenses through inclusion of unexempted entities in their returns and physical acquisition of unlawful funds and corrupting public officials in Tanzania.  The charges include also, restructuring  of the mining  companies to evade payment of various taxes and illegal dealing with profits obtained from mineral sales. 
Under Tanzanian Anti-Money Laundering Act, 2006 a body corporate may be liable to a fine of not less than five hundred million shillings or be ordered to pay the amount equivalent to the total amount of money involved or market value of the property, which ever amount is greater and also every director, manager, controller or principal officer of the company, partner, or a principal officer of the partnership shall be deemed to have committed the offence. 
The Anti-Money Laundering Act, 2006 also mandates the High court of Tanzania to have jurisdiction to try a person from a foreign state for an offence committed outside the United Republic which would constitute an offence under theAnti-Money Laundering Act. 
Under the provisions of the Extradition Act in Tanzania, the Government in Tanzania may possibly seek  assistance from other countries  to bring Senior officers of the accused companies to be before the  court in Tanzania to face charges. 
Where a person is convicted of a serious offence including offences of tax evasion and money laundering,  the Government may, apply to the convicting court, or to any other appropriate court, for a forfeiture order against any property that is tainted property in respect of the offence; or  a pecuniary penalty order against the person in respect of any benefit derived by the person from the commission of the offence




MICHUZI TV: Twanga Pepeta balaa...Full story Miaka 20 na Asha Baraka.

KIPINIDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 18,2018

TAASISI YA USTAWI WA JAMII BADO INAENDELEA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI AWAMU YA NNE KWA MWAKA WA MAOSOMO 2018/19

TAASISI YA CORNELL ALLIANCE FOR SCIENCE YA MAREKANI YAWATUNUKU VYETI WAANDISHI WA HABARI KILIMO SAYANSI

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Tekonolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, akimkabidhi cheti, Mwandishi wa Habari Suleiman Msuya, baada ya kushiriki mafunzo ya kuandika habari za Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO), yaliyofanyika New Dodoma Hoteli mkoani Dodoma na kuibuka Mshindi wa Pili katika Mashindano ya uandishi wa habari  juu ya teknolojia hiyo kwa kundi la Waandishi wa habari za magazeti. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa la Wazi la Kilimo na Teknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cornell cha Marekani, Cornell Alliance For Science na African Agricutural Technology Foundation (AATF). 
Mshindi wa  Kwanza kwa upande wa Waandishi wa Habari za Magazetini Bw. Daniel Mkate akipokea cheti.
 Mshindi wa jumla wa kuandika habari za GMO kwa njia ya magazeti katika mafunzo hayo, Rose Milondo akikabidhiwa cheti.
 Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WIZARA ZAKUTANA KUJADILI MFUMO WA UFUNGAJI CAMERA ZA CCTV

0
0
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekutana kujadili suala la ufungaji kamera maalumu za kudhibiti na kuzuia uhalifu. 

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema Serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera hizo katika miji yote mikuu nchini. 

Waziri Masauni alisema lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani, uporaji wa fedha katika taasisi za fedha. 

“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu. 

“Teknokolojia haiepukiki katika kudhibiti, Serikali tumejipanga na hivi karibuni tutaanza kufunga kamera za CCTV katika miji mikuu na maeneo ya mikoa iliyoko mipakani ili kudhibiti wahalifu kutoka nje ya Tanzania,” alisema Masauni 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub alisema tayari washafunga kamera hizo ambazo zilizinduliwa Oktoba 3, mwaka huu. 

Alisema uzinduzi wa kamera hizo ulifanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein. 

“Mfumo huo ni muhimu na tumehakikisha unaimarisha usalama katika mji wa Zanzibar ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na salama na tayari ushaanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa Zanzibar,” alisema.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub (kushoto), wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto).
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto).
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BARAZA LA BIASHARA MKOA WA DODOMA LAASWA KUONGEZA USHIRIKI SEKTA BINFASI

0
0
Frank Mvungi- MAELEZO
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, ameongoza mkutano wa majadiliano ya Baraza la Biashara la mkoa huo ili kupitia na kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili usaidie kukuza ushiriki wa sekta binafsi na kuchochea ukuaji wa sekta zinatoa ajira kwa wananchi walio wengi kama kilimo.


Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo  leo Jijini Dodoma  na wadau wengine, Dkt. Mahenge amesema kuwa, mkutano huu una lengo la kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ngazi ya Mikoa na Wilaya.


“Tunategemea utakuwa rejea thabiti kwa viongozi na watendaji ambao wamekuwa wakibadilika mara kwa mara kutokana na uteuzi au chaguzi”. Alisisitiza Dkt. Mahenge


Akifafanua zaidi, mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amesema mkutano huo wa majadiliano una lengo la kuhakikisha ushiriki wa sekta binafsi unaongozeka ili kuchochea maendeleo ya mkoa na taifa.


Aliongeza kuwa, majadiliano hayo yatasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza mara kwa mara ambazo zimekuwa zikifubaza upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kijamii na yanategemewa kutoa ufumbuzi wa changamoto  hizo kwa kuzingatia maandalizi ya majadiliano, kanuni za majadiliano na utekelezaji baada ya majadiliano.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akifungua  mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.
 Mhadhiri  kutoka  Chuo  kikuu  Mzumbe Prof. Honest   Ngowi akiwasilisha rasimu ya mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  wakati wa kikao cha kujadili muongozo  huo leo Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wakuu wa Wilaya wa mkoa wa Dodoma wakifuatilia mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma. 

(Picha zote na MAELEZO)


MAJAJI NA MAHAKIMU WAKUMBUSHWA KUTOA ADHABU ZINAZOIREKEBISHA JAMII

0
0
 Na Lydia Churi-Kwimba Mwanza 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewakumbusha  Majaji na Mahakimu kutumia Mamlaka waliyonayo kisheria kutoa adhabu zinazoirekebisha jamii kwa makosa yanayojirudia mara kwa mara.
Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kwimba leo Jaji Mkuu alisema Mahakama ni sehemu ya jamii hivyo inalo jukumu la kuhakikisha kuwa jamii inaishi kwa amani na salama.
Kuhusu ushirikiano kati ya Mahakama na mihimili mingine, Jaji Mkuu alisema katiba ya nchi imegawanya majukumu kwa kila mhimili lakini yote inaunganishwa  na dhana moja ya kuwatumikia wananchi, hivyo aliahidi kuendeleza ushirikiano na wadau wote ili wananchi wapate haki kwa wakati.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama haiwezi kufanya kazi peke yake bila kushirikiana na mihimili mingine. “Nguvu ya Mahakama inatokana na nguvu kutoka kwenye mihimili mingine”, alisema.  
Awali akimkaribisha Jaji Mkuu ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi  Ngaga alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao hulazimika kukatisha masomo yao.
Kuhusu ushirikiano na Mahakama, Mkuu huyo wa wilaya alisema ofisi yake inashirikiana kwa karibu na Mahakama katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara yake katika mkoa wa Mwanza ambapo anakagua shughuli za Mahakama. Tayari ameshatembelea baadhi ya Mahakama zilizopo kwenye  wilaya za Ukerewe, Sengerema na Kwimba.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kwimba (hawapo pichani) kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika na Kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Huduma za kimahakama wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Happyness Ndesamburo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na viongozi wengine wa Mahakama pamoja na Mahakimu wa Mahakama zilizopo wilayani Kwimba mara baada ya kuzungumza nao.
.Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga pamoja na Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Mansoor Shanif Hiran.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kwimba baada ya kuzungumza nao leo katika ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika.


Wachimbaji Madini Songwe waruhusiwa kuendelea na shughuli za uchimbaji madini

0
0
Na Greyson Mwase, Songwe
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka wachimbaji wa madini  wanaoendesha shughuli zao za uchimbaji wa madini ya chokaa na ujenzi katika  kijiji cha Nanyala kilichopo katika Wilaya ya Mbozi iliyopo mkoani Songwe kuendelea na shughuli zao wakati wakisubiri  suluhu ya  mgogoro baina yao na kiwanda cha saruji cha Mbeya.
Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo tarehe 17 Oktoba, 2018 alipokuwa akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo  uliofanyika katika kata ya Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika  mkoa huo  yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.
Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, John Palingo, Afisa Madini Mkazi katika Mkoa wa Mbeya, Sabai Nyansiri, Afisa Madini anayesimamia wilaya za Songwe na Chunya, Athuman Kwariko, Afisa Madini kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Ndege Bilagi, vyombo vya ulinzi na usalama vya wilaya pamoja na waandishi wa habari.
Nyongo alifafanua kuwa, awali maelekezo yalitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ya kutaka viongozi kutoka katika mikoa ya Mbeya na Songwe kukaa pamoja na kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa ardhi kati ya  wakazi wa Songwe na Mbeya na kiwanda cha kuzalisha saruji nje ya mahakama jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa sasa.
Alielekeza viongozi kutoka katika mikoa husika kuhakikisha wanashughulikia mgogoro wa ardhi kati ya mikoa miwili na kiwanda cha saruji cha Mbeya kwa wakati huku wananchi wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji madini wakiendelea na shughuli zao kama kawaida katika maeneo husika.
Aliendelea kusema kuwa, jukumu kuu la Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini ni kuhakikisha wanatoa leseni za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuwa leseni ya uchimbaji wa madini ni tofauti na  hati ya ardhi kwa kuwa inahusisha madini yaliyopo chini ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia mbele) na Meneja wa Kiwanda cha chokaa cha Lime Africa kilichopo katika Kata ya Nanyala Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, Fredy Msindo (kushoto mbele) pamoja na msafara  wakiendelea na ziara katika eneo la kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Songwe yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 17 Oktoba, 2018.
 Meneja wa Kiwanda cha chokaa cha Lime Africa kilichopo katika Kata ya Nanyala Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, Fredy Msindo (katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na kiwanda hicho kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo pamoja na msafara wake.
 Kutoka kushoto Afisa Madini Mkazi katika Mkoa wa Mbeya, Sabai Nyansiri, Afisa Madini kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Ndege Bilagi na Afisa Madini anayesimamia wilaya za Songwe na Chunya, Athuman Kwariko wakinukuu maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano wake na wachimbaji wadogo uliofanyika katika kata ya Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe .
 Sehemu ya wachimbaji wa madini ya chokaa na ujenzi kutoka katika kata ya Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe, wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani)
Diwani wa Viti Maalum kutoka Tarafa ya Iyula iliyopo Wilayani Mbozi mkoani Songwe, Messiah Swella akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PROFESA MBARAWA AZINDUA KAMPENI YA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI

0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa  amezindua rasmi Kampeni ya Upandaji Miti kandokando ya vyanzo vya maji nchi nzima mkoani Mtwara kwa lengo la kuhakikisha vyanzo hivyo vinatunzwa na kuwa endelevu kwa miaka mingi ijayo.
Profesa Mbarawa amezindua kampeni hiyo kwa kupanda miti nane katika chanzo cha Mtawanya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mjini na kuzitaka Bodi zote za Mabonde tisa nchini kuweka mkazo na mipango madhubuti ya kusimamia na kutunza rasilimali za maji ziweze kuwa endelevu.
Ametoa agizo hilo kutokana na uvamizi na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji katika maeneo mengi kwa sasa nchini, hali inayohatarisha kiasi kikubwa cha maji kupungua kutokana na vyanzo vingi kukauka, hali inayoweza  kusababisha ukosefu wa maji ya kutosha kwa ajili ya miradi inayoendelea kutekelezwa na Serikali.
Na kutaka vyanzo vyote vya maji vitunzwe na kulindwa kwa kupandwa miti maalumu inayohifadhi maji na kuagiza wale wote wanaofanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo waache tabia hiyo na watakao kaidi wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine kwa kuwa sheria inaweka bayana kuhusu jambo hilo. 
Ametoa tamko hilo kwa kuzingatia Sheria ya Maji Na, 11 ya Mwaka 2009 inayokataza kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, na ikieleza shughuli zote za kibinadamu zifanyike umbali wa mita 6o kutoka chanzo cha maji kilipo na kutaka maeneo yote yawekewe mipaka na vizuizi kuonyesha ukomo wa watu kuingia kwenye vyanzo hivyo.
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mzingira Mtwara (MTUWASA), Mhandisi Mashaka Sita katika Mitambo ya Maji Mangamba, Mtwara MJini.
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wakazi wa Msanga Mkuu, Mtwara Vijijini.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiinama kwa ajili ya kuonja na kujua ubora wa maji katika mradi wa Mpapura, Mtwara Vijijini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA MAJI AWESO AZINDUA MRADI WA UCHAKATAJI MAJITAKA TUANGOMA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amezindua mradi wa uchakataji majitaka wa Toangoma Wilaya ya Temeke.

Mradi huo uliotekelezwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid Tanzania.

Akiwa katika mradi huo, Aweso amezindua mradi huo ukiwa na vipengele vikuu vinne ambavyo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma za uhifadhi na udhibiti wa taka ngumu kwa wakazi wa kata 23 za Manispaa ya Temeke.

Mradi wa Tuangoma umetumia kiasi cha Milioni 359 ukijumuisha ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ambayo ni pamoja na  sehemu ya Kuchujia taka ngumu (screening chamber), tenki la kuhifadhia majitaka kwa muda mrefu (balancing Tank), mtungi wa kuchakata majitaka na kutengeneza gesi (biogas Dome) sehemu ya kuchujia majitaka (perforated grave  filter) na sehemu ya kukaushia tope la majitaka.

Mtambo huo una uwezo wa kuhifadhi majitaka kiasi cha lita elfu hamsini (50m3) na uwezo wa kuhudumia wananchi 93,000 na uwezo wa kuzalisha gesi kiasi cha lita 4000 kwa siku ambayo inaweza kuhudumia takribani kaya 250 kwa mwezi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hususani kupikia.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mradi wa uchakataji majitaka Toangoma uliojengwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA)  na Shirika Shirika la PDF chini ya Shirika la Water Aid TanzaniaKushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mbagala Ally Mangungu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majitsafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja na Kulia ni Mkuu wa  Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva.

Mhandisi Kazingoma kutoka Shirika la Water PDF (Kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso moja ya sehemu inayotumika kuhifadhia majitaka kwenye mradi wa Uchakataji majitaka wa Toangoma.

 Mhandisi Kazimoto kutoka Shirika la Water Aid akimuelezea Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mradi mzima wa kuchakata majitaka uliojengwa  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya Shirika la Maji la  Water Aid.

SERIKALI YAWATAKA WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA RASILIMALIWATU SERIKALINI KUSIMAMIA VIZURI RASILIMALIWATU

0
0
Serikali imewataka Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Taasisi za Umma nchini kuhakikisha rasilimaliwatu inasimamiwa vizuri ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Dkt.Ndumbaro amesema kuwa, rasilimaliwatu ikisimamiwa vibaya matokeo yake ni kushuka kwa utendaji kazi, na utendaji kazi ukishuka unasababisha uchumi  wa nchi kutokukua inavyotakiwa, hivyo Taifa kushindwa kufikia lengo lake la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt.Ndumbaro amewasisitiza Wakurugenzi wanaosimamia rasilimaliwatu katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala na Mashirika ya Umma kuwa taasisi zote za Umma zifanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza vipaumbele vya Taifa.
Aidha, Dkt.Ndumbaro amewakumbusha Wakuu hao wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuzingatia maadili katika utendaji kazi ili wawe mfano wa kuigwa na watumishi wengine.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko amewaasa watendaji hao kuwa washauri wazuri, walezi bora, walimu wazuri  na watatuzi wa changamoto zinazowakabili watumishi wa umma wanaowasimamia ili wawe na tija katika maendeleo ya Taifa.
Bi. Mwaluko amewataka Watendaji hao kuhakikisha wanasimamia vema nidhamu ya watumishi wa umma ili kujenga taswira nzuri ya utumishi wa umma.
Mkutano kazi huo wa Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma una lengo la kuwakumbusha na kuwahimiza watendaji hao utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiutendaji, uendeshaji na usimamizi wa rasilimaliwatu kwa kuzingatia malengo,shabaha na vipaumbele vya kitaifa.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akiendesha kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kinachofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akifungua rasmi  kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainab  Chaula akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kuhusu masuala ya kiutumishi katika kikao kazi kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu waliohudhuria kikao kazi kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

 Baadhi ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha watendaji hao  kinachofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images