Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

ZAWADI ZATAJWA KICHOCHEO CHA UKEKETAJI TARIME

0
0

NA BALTAZAR MASHAKA, TARIME

ZAWADI zimetajwa kuwa chanzo na kichocheo kikubwa cha vitendo vya ukeketaji na tohara kwa watoto wa kike na kiume wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi walioshiriki tamasha la kupinga Ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na Shirika la ATFGM Masanga na kufanyika katika Shule ya Sekondari Kemambo kwa ufadhili wa Terre des Homes tamasha ambalo lilishirikisha shule 10 mbili za msingi na nane za msingi wilayani Tarime.

Wanafunzi hao walieleza kuwa kipindi cha ukeketaji mabinti (watoto wa kike) wanapotoka kukeketwa huzunguka kwenye jamii inayowazunguka ili kupatiwa zawadi ya fedha, nguo na vitu vingine jambo ambalo huwashawishi wengine ambao hawajakeketwa kwenda kufanyiwa vitendo hivyo vya ukatili ili nao wapatiwe zawadi.

Pia waliishauri serikali kusimamia Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na kanuni zake kupiga marufuku vishawishi vya zawadi za nguo na fedha ili kudhibiti uketetaji wa watoto wa kike na tohara isiyo salama kwa vijana wa kiume.

“Mtoto mmoja anaweza kupata nguo (vitenge) na fedha nyingi ambazo huzibana kwa pini kichwani hivyo wale ambao ni wadogo kama hawajakeketwa wakiona hizo zawadi wanatamani na kushawishika kukeketwa, hivyo serikali ipige vita zawadi hizo kwa kusimamia Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na kanuni ” alisema ( Maria Marwa jina la linahifadhiwa) mwanafunzi huyo wa Shule Msingi Nyabusara.
 Mwanasheria wa Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia la ATFGM Masanga wilayani Tarime, Dora Luhimbo akitoa elimu ya kupinga masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni lililoandaliwa na shirika hilo na kukutanisha shule 10 za msingi na sekondari ambalo lilifanyika katika Shule ya Sekondari Kemambo wilayani humo.
 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za kata za Matongo na Kemambo wakiwa katika tamasha la elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia, Ukeketaji, Ndoa na Mimba za utotoni lililoandaliwa na shirika la ATFGM Masanga Tarime.
 Mwanasheria wa Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime, Mara ( ATFGM Masanga) Dora Luhimbo akicheza muziki na baadhi ya wanafunzi katika tamasha hilo la kupinga ukatili wilayani humu.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kemambo Matinde Gimonge akifungua tamasha la kupinga Ukatili wa Kijinsia na kuwataka wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kufikisha elimu kwa jamii, elimu ambayo wanaipata kupitia kwenye matamasha ya namna hiyo.



"Ushiriki wa Wananchi Katika Miradi ya Kimkakati Kuchochea Ukuaji wa Uchumi"-Waziri Jenista

OLE NASHA:VETA NI CHOMBO MUHIMU KATIKA UJENZI WA VIWANDA NCHINI

0
0
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema kuwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni chombo muhimu katika kuzalisha mafundi watakaohudumia viwanda vinavyojengwa nchini.

Ole Nasha ameyasema hayo jana wakati alipotembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni kujua utendaji wa mamlaka hiyo katika uzalishaji wa ujunzi kwa vijana nchini, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipambanua kuwa ni nchi viwanda hivyo licha ya kuwepo kwa wahandisi ni lazima kuwepo kwa mafundi.

Amesema kuwa VETA ni lazima waonyeshe njia katika uzalishaji wa vijana wenye ujuzi ambao watatumika katika viwanda na miradi mbalimbali ya serikali inayojenga wakiwemo mafundi wa reli.

“Wahandisi kazi yao kuweka michoro lakini kazi ya kujenga ni mafundi hivyo ni wajibu wenu VETA wa kuzalisha rasimali hiyo katika ujenzi wa taifa na kazi yenu inaonekana baadhi ya vijana wamemaliza shahada ya kwanza na sasa wanajiunga mafunzo ya ufundi stadi”.amesema Ole Nasha.

Ole Nasha amesema kuwa vyuo vyote vinatakiwa kuangaliwa mitaala na VETA na visivyo na vigezo wavifungie .Nae Mwenyekiti wa Bodi ya VETA , Peter Maduki amesema kuwa wanajenzi wa vyuo vya VETA kata Mikoa Mitatu na Wilaya moja moja ambavyo vitagharimu sh. bilioni 38.

Amesema Mikoa vitavyojengwa vyuo vya ufundi Geita , Simiyu , Rukwa pamoja wilaya ya Chato ikiwa kuhakikisha kila mkoa unakuwa na chuo cha ufundi stadi. Nae Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk.Pancras Bujulu amesema kuwa changamoto yake ni kutafuta fedha kwa ajili ya kuismamamisha Vete.


Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na Menjejimenti ya VETA pamoja na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Peter Maduki akizungumza kuhusiana na mipango ya bodi katika ujenzi wa vyuo katika Mkutano wa Menejimenti na wafanyakazi.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt Pancras Bujulu akizungumza katika Mkutano wa Menejimenti na wafanyakazi kuhusiana mikakati ya VETA leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na Menejimenti katika Mkutano na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha 

NAIBU WAZIRI NDITIYE ATEMBELEA MRADI WA DGMP BANDARINI

0
0
Na Leonard Magomba
MRADI mkubwa wa kuboresha Bandari ya Dar es Salaam ‘Dar es Salaam Maritime Gateway Program’ (DGMP) umefikia asimilia 42 ya ujenzi wake hadi sasa.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa gati maalum ya kushushia magari (RORO), gati Na. 1-7, kuongeza kina cha maji katika magati hayo pamoja na kutanua lango la kuingia meli bandarini.

Mradi huo ambao umelenga kuifanya Bandari ya Dar es Saalam kuwa ya kisasa zaidi na kuongeza uwezo wake wa kuhudumia meli kubwa kwa wakati mmoja unatarajia kukamilika mwezi Juni, 2020.

Hayo yamebainika leo wakati Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea mradi huo bandarini ili kukagua maendeleo ya ujenzi wake.

“Nimefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huu ambao hadi sasa umefikia asilimia 42 amesema Mh. Nditiye na kuongeza kwamba matarajio yetu mradi huu utaisha kwa wakati uliopangwa.”
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye kuhusu ujenzi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam alipofika eneo la kutengenezea zege linalotumika kwa ajili ya ujenzi huo.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa gati namba moja (1) ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya Waziri huyo kufanya ziara bandarini kukagua mradi huo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya kufika katika moja ya maabara zinazotumika kupima udongo kwa ajili ya ujenzi huo bandarini.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

HALMASHAURI YA CHALINZE YATAKIWA KUZIBA MIANYA INAYOSABABISHA KUSHUKA KWA UKUSANYAJI WA MAPATO.

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

KAMATI ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo ,,imeiasa halmashauri ya Chalinze kuongeza usimamizi na jitihada ili kuinua ukusanyaji wa mapato yake ya ndani.

Kwa miaka miwili mfululizo halmashauri hiyo imesifika kwa ukusanyaji mzuri unaovuka malengo lakini kwa taarifa kutoka wizara ya TAMISEMI inaonyesha haimo kwenye halmashauri bora kwa ukusanyaji wa mapato .

Mwenyekiti wa CCM Bagamoyo,alhaj AbdulZahoro Sharif alisema ,kamati hiyo imelazimika ,kukutana na wakuu wa idara,wataalamu na madiwani wa halmashauri hiyo,kuangalia endapo kuna mapungufu ama mianya yaliyosababisha kushuka kwa makusanyo hayo ili yadhibitiwe .

Alisema kamati haijaridhishwa kwa kushuka kwa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ya Chalinze, kipindi cha mwaka 2017/2018 hivyo ijitahidi kusimamia vyanzo vyake vya mapato."Achane kufanya kazi kimazoea ,usimamizi sio mzuri ,;" bado sijaridhishwa na hali ya makusanyo na mtasababisha ilani kushindwa kutekelezeka kwa wakati ,alisema alhaj Sharif.Aliwataka washirikiane baina ya wataalamu, watendaji na madiwani kwa pamoja kubuni vyanzo vipya vya mapato.Kwa upande wake ,mweka hazina wa halmashauri ya Chalinze (DT) David Rubibira alisema kwa siku moja wanakusanya makusanyo katika malori ya kokoto 197-200 ambapo kwa siku wanakusanya sh.mil.8.9 .#

Ofisa mipango wa halmashauri ya Chalinze ,Shabani Millao alisema ,kuhusu suala la kushuka kwenye makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo linatafsirika sivyo kwani wapo vizuri katika makusanyo .Millao alitaja sababu za kutofikia kwenye makusanyo kwa kipindi hiki kuwa ni pamoja na kushushwa kwa makusanyo ya mazao ya chakula yasiyozidi tani moja ,na kuzuiwa kwa ushuru wa mabango .Alisema ,wamejipanga kurekebisha makadirio hivyo watafanya maotei kutegemeana na hali halisi ya makusanyo kulingana na chanzo husika.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu alifafanua ,ukusanyaji 2016/2017 walikusanya kiasi cha sh .bilioni 3.800 wastani wa asilimia 118."Tukaona kama tumevuka lengo tukaona tujiwekee malengo ya juu na tuongeza ongezeko la asilimia 26 ambalo tumekisanya sh.bilioni 4 badala ya kukusanya bilioni 4.3"alisema Zikatimu.

Alisema, katika malengo ya mwaka huo manake walivuka lengo kwa kukusanya kwa asilimia 17 badala ya asilimia 26 .Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Amina Kiwanuka alisema wamepokea maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo na wataifanyia kazi ili kuboresha makusanyo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Saidi Zikatimu,akitoa ufafanuzi wa jambo wakati kamati ya siasa ya CCM Bagamoyo ilipokwenda kukutana ,kuzungumza na wakuu wa idara ,wataalamu na madiwani wa halmashauri ya Chalinze .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Wajumbe wa Mkutano
Mwenyekiti wa CCM wilayani Bagamoyo ,alhaj Abdul Sharif akizungumza na wakuu wa idara ,wataalamu na madiwani wa halmashauri ya Chalinze (hawapo pichani),wa kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Saidi Zikatimu.(picha na Mwamvua Mwinyi).

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 17,2018

TAARIFA MUHIMU KUTOKA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA).

ITV HABARI ZA SAA 17 OKTOBA 2018.


SPIKA NDUGAI ATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA TAASISI YA KIMATAIFA YA KIDEMOKRASIA (NDI)

0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI) Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings wakati Mkurugenzi huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo walipomtembelea Ofisini kwake leo Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI), katikati ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo Ndg. Sandiy Quimbaya. Wageni hao walimtembelea Mhe. Spika leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI), kushoto kutoka kwa Mhe. Spika ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo Ndg. Sandiy Quimbaya. Wageni hao walimtembelea Mhe. Spika leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI) Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings wakati Mkurugenzi huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo walipomtembelea Ofisini kwake leo Jijini Dodoma.

Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi wa Uganda,Uingereza na Kaimu Balozi wa Marekani

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro(Mb.) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wamekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Patterson. Katika mazungumzo yao Bi. Patterson alitumia firsa hiyo kujitambulisha na kuwampongeza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Aidha, Dkt Ndumbaro amemuhakikishia Bi. Patterson kumpa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu yake. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke, katika Mazungumzo hayo Mhe. Cooke ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kuwapongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani). Aidha, Balozi Cooke alitumiafursa hiyo kumweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza ni wa muda mrefu sana ambapo nchi hizi mbili zinashirikiana katika sekta mbalimbali za kukuza uchumi. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero. Katika Mazungumzo hayo Mhe. Kabonero ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kumpongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani).
Aidha, Balozi Kabonero alitumiafursa hiyo kumweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa mahusiano kati ya Tanzania na Uganda ni ya muda mrefu, ambapo kutokana na mahusiano mazuri kati ya nchi hizi imepelekea Serikali ya Uganda kuamua kupitisha ujenzi wa bomba la mafuta tanzania, ambapo ujenzi huo utazalisha fursa mbalimbali na kukuza vipato vya wananchi wa pande zote mbili pamoja na kukuza uchumi baina ya mataifa hayo mawili.
Kwa upande wa Dkt. Ndumbaro amemuhakikishia Balozi Kabonero kumpatia ushrikano wa kutosha wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuiwaikilisha Taifa lake hapa nchini, Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO

0
0

ZAIDI ya kaya 200 katika mtaa wa Mnyanjani kata ya Myanjani Jijini Tanga zitanufaika na mradi wa ujenzi wa mtaro kwa ajili ya kuondoa tatizo la mafuriko linalotokea kila nyakati za msimu wa mvua. 

Hayo yamebainishwa na Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya jitihada za kuzinusuru kata hizo. 

Mhandisi Saidi alisema mradi huo unaokadiriwa kutumia Shilingi Milioni 170 umeelekezwa katika eneo hilo lililokuwa na hali ya kutuama kwa maji kila mwaka nyakati zote za mvua na kusababisha mafuriko na kupelekea wananchi kulazimika kuyahama makazi yao. Alisema mradi wa mtaro huo ambao utakuwa na urefu wa mita 512 utakuwa na uwezo wa kusukuma maji kuelekea bahari na kuzifanya kaya hizo na maeneo ya pembezono mwa mtaa huo kuishi kwa amani hasa nyakati za mvua. 

“Ni kweli hali ya mtaa huu haikua ya kuridhisha sisi tarura ambao tunamamlaka sasa tumeona hiki ndio kipindi cha kurekebisha miundombinu ya mifereji namea mvua zitakapo nyesha kaya hizi zitakuwa sehemu salama”Alisema Saidi. Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Alhaj Mussa Mbaruku ambae alitembelea mradi huo jana alisema matumaini makubwa yanaonekana ya kuwanusuru wananchi hao na mafuriko yanayotokea kila mwaka.

 Alhaj Mbaruku alisema eneo hilo limekuwa kero kwa wananchi hao ambao kila nyakati za mvua maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na hofu ya mafuriko yanayosababishwa na mvua za misimu na kulazimika kutafuta makzi mapya. 

“Taratibu hali ya maeneo yaliyokuwa yanakumbwa na mafuriko ndani ya Jiji yanaanza kuwa na hali nzuri baada ya taasisi hiyo kuwa makini na utekelezaji wa ujenzi wa mifereji hasa katika maeneo yanayotuama maji”Alisema Alhaj Mbaruku. Hata hivyo aliiomba taasisi hiyo kuendeleza kasi yao na mbali ya miradi ya mifereji pia ihakikishe kuwa barabara zote ndani ya Jiji hili zinaweza kutumika nyakati zote na zinajengwa kwa kiwango cha lami huku akiongeza kusema kuwa ulazima wa uwepo wa barabara za lami ndani ya jiji lazima uzingatiwe. 

Awali akizungumzia kero hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bakari Haule alisema tatizo la mafuriko katika eneo hilo lililkua ni kubwa mbali ya nyumba hizo kujengwa katika mpangilio lakini adha kubwa ilikuwa ni kutuama kwa maji nyakati za mvua.
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa Mradi wa Mfereji utakaopitisha maji kutoka kwenye makazi ya watu nyakati za mvua na kupelekea baharini 
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro eneo la Mnyanjani Jijini Tanga ambao utasaidia kuondoa kero ya kutuama maji kwenye makazi ya wananchi wakati wa mvua wakati alipofanya ziara ya kuutembelea
Mtaro utakaopitisha maji kwenye eneo la Mtaa wa Mnyanjani Jijini Tanga ya mvua na kupelekea baharini ili kuwaepusha wananchi na mafuriko nyakati za mvua
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia aakimuonyesha kitu Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa Mtaro 

TFDA YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAWA ZINAZODAIWA KUTIBU MAGONJWA YA FIGO NA HOMA YA INI

SHIRIKA LA MARIE STOPES TANZANIA LARUHUSIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZAKE HAPA NCHINI

MAHAKAMA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTOA HAKI

0
0
Na Lydia Churi-Mahakama Sengerema
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema Mahakama itaendeleza ushirikiano uliopo kati yake na mihimili mingine ili kurahisisha suala la utoaji na upatikanaji wa haki nchini.
Akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Sengerema ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Jaji Mkuu alisema Mahakama inapata nguvu zaidi ya kutekeleza majukumu yake ya msingi pale inapopata ushirikiano kutoka mihimili mingine yaani Bunge na Serikali.
Alisema endapo Mihimili yote mitatu ya dola haitashirikiana ni wazi kuwa kazi ya utoaji na upatikanaji wa haki itakuwa ni ngumu. Aliongeza kuwa mihimili hii imewekewa utaratibu wa kutekeleza majukumu yake pasipo kuingiliana.
Aidha, Prof. Juma aliipongeza Mahakama ya wilaya ya Sengerema pamoja na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema kwa kuwa na uhusiano wa karibu na ushirikiano kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumzia kuhusu rushwa na uvunjifu wa maadili, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania imeamua kupiga vita rushwa na ukosefu wa maadili kwa watumishi wake ambapo pia alimtaka Mkuu wa wilaya ya Sengerema kutosita kuwaita na watumishi wa Mahakama watakaopotoka kwenye suala la rushwa na maadili.
Alisema Mahakama imeamua kutoa nakala za hukumu bure pamoja na kuingia mkataba na shirika la Posta ili kusambaza nakala hizo pamoja na nyaraka nyingine, kama hatua ya kupambana na vitendo vya rushwa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bwana Emmanuel Kipole alisema mahusiano kati ya Serikali na Mahakama kwenye wilaya yake ni mazuri kwani wamekuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na kuheshimiana bila kuingiliana majukumu.
 Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole akizungumza wakati alipotembelewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ofisini kwake leo.Wa kwanza kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika na wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Sengerema Mhe. Monica Ndyekobora.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimuelezea Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Mhe. Emmanuel Kipole kuhusu kitabu cha Mpango Mkakati wa Mahakama kabla ya kumkabidhi. 
  Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Bwn. Samson  Mashalla (wa pili kushoto) akifuatilia jambo wakati wa ziara ya Jaji Mkuu wilayani Sengerema. 
  Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Anatory Kagaruki akielezea jambo kuhusu masuala ya Utumishi wakati Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Sengerema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

IGP AKUTANA NA BALOZI WA KOREA NCHINI

0
0

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na  Balozi wa Korea nchini Song, Geum-young wakati balozi huyo alipotembelea Makao makuu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walizungumza mambo mbalimbali ya kuimarisha Uhusiano. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi jarida la Polisi Balozi wa Korea nchini Song, Geum-young baada ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano Makao makuu ya Polisi Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).

KIONJO CHA BAGAMOYO ARTS FESTIVAL 2018

KAIMU MKURUGENZI TPA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
KAIMU Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.

Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Lizy Kiwia mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imedaiwa, Oktoba 25, 2012  huko katika ofisi kuu za TPA zilizopo, Temeke mshtakiwa huyo  wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722A kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. 

Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa huyo wakati akijua na kwa nia ya kumdanganya muajiri wake alitumia nyaraka ya malipo ya kodi (Invoice) namba MKOO/722B kutoka Kampuni ya Bob investment Ltd. Akidai kuwa, garama ya  semina ya siku tatu ilikuwa ni sh. 47,935,140 wakati akijua alikuwa na lengo La kumdanganya muajiri wake huyo TPA.

Katika shtaka la tatu mshtakiwa anadaiwa, Desemba 5 2012 akiwa TPA alitumia hati ya malipo namba MKOO/1203 Kutoka huko huko Bob yenye garama ya sh, 97,178,664

Katika shtaka la nne imedaiwa kati ya Oktoba 30 na Desemba 12/2012  huko TPA, mshtakiwa kwa nia ovu aliisababishia TPA hasara ya sh 158,947,584.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa Kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na wadhamini mawili wenye barua za utambulisho.

Pia, Hakimu alisema mshtakiwa atatakiwa kuweka nusu ya fedha hizo au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi imeahirishwa hadi hadi Oktoba 29, 2018 kwa kutajwa na kuangalia upelelezi umekamilika au la.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa mamlaka ya bandari Tanzania, (TPA) Peter Gawile akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kujibu mashtaka matatu likiwemo la kuisababishia TPA hasara ya zaidi ya sh milioni 150.

Hakuna cha msalia mtume usipotekeleza sheria- Profesa Kikula

0
0
Na: Rhoda James - Singida
Mwenyekiti wa Tume ya madini, Profesa Idris Kikula amesema kutokujua sheria ya madini si kigezo wala sababu ya kukwepa adhabu ya ukiukwaji wa sheria hiyo na kuwataka wachimbaji wa madini kuzingatia na kufuata sheria na taratibu za kujihusisha na biashara hiyo.
Ameyasema hayo jana tarehe 16 October 2018 mkoani Singida alipokuwa katika  kikao na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi, Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, viongozi wa wachimbaji wadogo pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa Jasi na madini ya dhahabu.

Profesa Kikula ameeleza kuwa, kazi ya tume ni pamoja na kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini, Hii ni sababu kubwa ya kuwatembelea siku hii ya leo, “tumewatembelea ili kuwafundisha na kuwakubusha kuhusu sheria zilizopo pamoja na marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017”. 

Tunapita ili kutoa elimu katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kutuza kumbukumbu, mazingira na usalama migodini, utoaji wa tozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria ili tutakapokuja tena awamu nyingine na kukuta mmekiuka taratibu sheria ichukue mkondo wake. 

Aidha, Profesa Kikula amewataka wachimbaji wadogo, wa kati na hata wakubwa nchini kuhakikisha kuwa wanakaa pamoja na uongozi wa  wilaya au mkoa husika ili kukubaliana juu ya namna ya uwajibikaji katika kutoa huduma kwa jamii (CSR). 

“Mikataba hii mnayoingia itasaidia kujua ni kiasi gani mnapata, kiasi gani unatakiwa kulipa kuligana na unachokipata ili Serikali ipate stahiki zake. Alisema Profesa Kikula.

Pamoja na hayo,  Profesa Kikula amewasihi viongozi wa wachimbaji wadogo (REMA) kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu  na wachimbaji wadogo ili kuhakikisha kuwa wachimbaji hao wanajiunga katika vikundi na kuvirasimisha ili Serikali iwatambue na kuwapa huduma wanayostahili kwa wakati. 


Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi, amewataka viongozi wa mkoa, wilaya, kata na hata vijiji kubadilika na kushiriki katika kutatua matatizo ya wananchi kwa karibu.
Aidha, amewataka , watumishi kujishughulisha kwa juhudi na kujituma pasipo kusubiri kuambiwa jambo la kufanya na badala yake wajifunze kufikiri jambo jema linalohitaji kufanyiwa kazi na kutekeleza kwa wakati ili kupunguza changamoto zinazojitokeza.

Akijibu swali la mchimbaji mdogo wa madini(Jina halikufahamika), aliyehoji  juu ya leseni ya utafiti kuchukua muda mrefu pasipo wananchi kupewa maelezo yoyote Kamishna wa Tume ya Madini Abudulkarim Mruma  alifafanua kuwa leseni ya utafiti inatolewa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza inachukua miaka minne, ya pili miaka mitatu na ya tatu miaka miwili kwa mujibu wa sheria ya madini na baada ya hapo kama mchimbaji hajapata chochote anarudisha eneo hilo kwa Serikali.
Mwenyekii wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula akizunguamza na wajumbe wa mkutano katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi (kulia kwa Prof. Kikula), wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi D. Muragili akifuatiwa na Katibu Tawala Dkt. Angeline Lutambi.
Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma( wa tatu kushoto mbele) akichukua taarifa juu ya maagizo yanayotolewa na Prof. Kikula (hayupo pichani), Kamishna wa Tume ya Madini Athanas Macheyeki (wa nne kushoto) pamoja na wajumbe mbalimbali walioshiriki katika kikao baina ya wadau wa madini na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi (hayupo pichani)


SERIKALI IMEZITAKA HALMASHAURI KUWA NA ONE STOP CENTRES KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI NCHINI

0
0
Na Mwandishi wetu Pwani
Serikali imezitaka Halmashauri  zote Nchini kuhakikisha zinakuwa na vituo vya huduma za  mkono kwa mkono (Ones Stop Centre) ili kuunga mkono serikali katika juhudi zake za kupambana na vitendo vya ukatili hapa Nchini.

Hayo yamesema leo wilayani kibaha mkoani Pwani Naibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea kituo cha huduma za mkono kwa mkono kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani iliyoko Kibaha mkoani humo. 

Dkt. Ndugulile amesema kuwa lengo la vituo hivyo linalenga kupunguza mlolongo wa huduma kwa muhanga wa ukatili kwani vituo hivyo vinatoa huduma za matibabu, huduma za polisi na ushahuri wa kisaikolojia kutoka kwa Afisa Ustawi wa Jamii kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema nchi kwa sasa ina vituo vikumi tu hivyo kutaka maeneo Mikoa mingine kuiga Mkoa wa Pwani kuhunga mkono juhudi hizi kwa kuwa takwimu zilizopo zinaonesha Tanzania ina ina matukio ya ukatili 41,000 na kati ya matukio hayo 13,000 ni ukatili dhidi ya watoto akitaja hali hiyo kuwa ni ujambazi mpya zidi ya binadamu.

Amezitaja juhudi nyingine za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kuwa ni kuwepo kwa madawati ya Jinsia katika vituo vya polisi akitaja idadi ya vituo hivyo kote Nchini kuwa ni jumla ya madawati 500.

Ameongeza kuwa Serikali inawajengea uwezomwalimu wa Shule za Msingi na Sekondari ili kuwa na madawati ya ukatili wa kijinsia kwani vitendo vingi vya ukatili kwa watoto vinatokea katika eneo la shule.

Dkt. Ndugulile pia ameitaka jamii kutofumbia macho vitendo vya ukatili vinavyotokea katika maeneo yao hasa nyumbana katika familia na amesema Serikali itawachukulia hatua watoa huduma za fya watakaojihushisha na uitoaji wa taarifa za uongo kuhusu mashauri ya vitendo vya ukatili.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Engineer Evalist Ndikilo  kuhusu masuala Afya pamoja na Maendeleo ya Jamii mapema leo ofisini kwake Kibaha Mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugezi Mkuu wa hospitali ya Tumbi Dkt. Edward Wayi akitoa maelezo ya Kituo cha Mkono kwa Mkono (one stop centre) kwa waandishi wa habali kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia mapema leo Tumbi Kibaha Mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Mkurugezi Mkuu wa hospitali ya Tumbi Dkt. Edward Wayi akiongea na wagonjwa alipotembelea na kufanya ukaguzi wa hospitali ya rufaa ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WANAFUNZI 25,532 WAPANGIWA MIKOPO KATIKA AWAMU YA KWANZA

0
0
Wanafunzi 25,532 wa mwaka wa kwanza wapangiwa mikopo ya TZS 88.36 bilioni.
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuwa imetoa orodha ya Awamu ya Kwanza yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 25,532 waliopangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 88.36 bilioni. 

Akitangaza orodha hiyo leo (Jumatano, Oktoba 17, 2018) jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema kati ya wanafunzi hao, wanaume ni 16,085 na wanawake ni 9,447.

Bw. Badru ameongeza kuwa katika awamu hiyo ya kwanza HESLB pia imetoa mikopo yenye thamani ya TZS 850.35 milioni kwa watanzania wanafunzi 69 wanaoendelea na masomo nje ya nchi chini ya makubaliano maalum na nchi rafiki zipatazo saba ambazo ni Msumbiji, Algeria, Cuba, Urusi, Serbia, Urusi na Ujerumani.

Bajeti ya TZS 427.5 bilioni zimetengwa kwa mikopo ya elimu ya juu 2018/2019 

Katika mkutano huo, Bw. Badru ameeleza kuwa bajeti ya fedha za mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 ni TZS 427.5 bilioni na tayari Serikali imeshatoa TZS 137.06 bilioni zinazohitajika wakati vyuo vinafunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba na mwezi Novemba (2018). Kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi wapya na wanaoendelea na masomo wapatao 123,285. 

“Fedha nyingine tutazipokea baadaye katika robo ya pili ya mwaka wa fedha kwa ajili ya malipo ya wanafunzi watakaopangiwa mikopo … kwa hiyo kwa sasa, tuna fedha tunazohitaji kwa waombaji wote wenye sifa,” amesema Bw. Badru katika mkutano uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa HESLB Dkt. Veronica Nyahende.

Kuhusu kutangaza Awamu ya Pili

Bw. Badru amesema kuwa HESLB itaendelea kutoa awamu nyingine za orodha za wanaopangiwa mikopo kadri itakavyokamilisha uchambuzi wa orodha za wanafunzi walioomba mikopo na ambao pia wamepata na kuthibitisha udahili wao katika chuo kimoja ili kuhakikisha fedha za mikopo zinawafikia wanafunzi wahitaji katika vyuo walivyothibitisha.

Upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na kuendelea

Aidha, Bw. Badru amesema kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo wataendelea kupata mikopo ikiwa wamefaulu mitihani yao na matokeo yao kuwasilishwa HESLB na vyuo husika.

“Tunatoa mikopo ili mwanafunzi asome, kwa hiyo tutaendelea kuwapa mikopo wanafunzi wenye mikopo na wanaendelea na masomo ikiwa tumepokea uthibitisho kuwa ana sifa za kuendelea na masomo katika mwaka unaoanza hivi punde,” amesema Bw. Badru.

Upatikanaji wa orodha kamili ya waliopangiwa mikopo

Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo katika awamu hii ya kwanza yataanza kupatikana baadae leo katika mtandao wa HESLB wa uombaji mkopo (https://olas.heslb.go.tz) na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha ya majina hayo pia zinatumwa vyuoni kwa ajili ya kurahisisha taratibu za usajili wa wanafunzi hao.

Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa ya kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2018/2019, wanapangiwa mikopo kabla vyuo kufunguliwa mwishoni mwa mwezi Oktoba, mwaka huu (2018).

Aidha, Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa kwa awamu inayofuata ukiendelea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Jumatano, Oktoba 17, 2018
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipotoa taarifa ya wanafunzi wa vyuo vikuu wa awamu ya kwanza waliopata mkopo.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images