CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kimetoa bati 500 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8.5 kwa mwalimu mstaafu 25 kama sehemu ya kuwaaga na kuwapongeza kwa utumishi bora katika kazi hiyo ya ualimu .
Akikabidhi bati hizo jana wakati wa hafla fupi ya kuwaaga walimu hao mgeni rasmi katika hafla hiyo afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Josephat Kayombo pamoja na kupongeza CWT wilaya ya Kilolo kwa kutambua mchango wa walimu wenzao ambao wamestaafu bado alitoa wito kwa walimu waliopo kazini kuendelea kujituma kufanya kazi hiyo na kujiepusha na utovu wa nidhamu .
Kayombo alisema serikali imeendelea kuwajali watumishi wote wa umma wakiwemo walimu na kuendelea kulipa stahiki zao ambazo wamekuwa wakizidai hivyo ni lazima kwa watumishi hao kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na kuepuka kuonyesha utovu wa nidhamu na jeuri pale mwajili ambapo amua kumpangia kituo kipya cha kazi .
" Walimu ni kielelezo tosha kwa jamii na hakuna yeyote anayeweza kujisifu kwa mafanikio yake bila kutambua mchango wa mwalimu hivyo ni vema walimu kwa umuhumu wenu huo kuendelea kulenda heshima yenu kwa kuonyesha nidhamu na kuzingatia kanuni na taratibu za kazi na kujiepusha kuwa na nidhamu mbovu " alisema Kayombo
Pia alisema kwa kuwa serikali imeendelea kuwalipa mafao yao wastaafu ni vema walimu wastaafu kuwa makini na wimbi la matapeli ambao wamekuwa wakizunguka katika vijiji mbali mbali vya wilaya ya Kilolo na kuorodhesha majina ya walimu wastaafu kwa lengo la kuwatapeli mafao yao ya ustaafu .
Alisema kuwa kiasi cha fedha ambacho wanakipata baada ya kustaafu kinaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwao mbele ya safari hivyo umakini unahitajika kwa kuwaepuka matapeli hao.
Afisa utumishi wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Joseptah kayombo (kulia) akiwa na viongozi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Kilolo wakiwakabidhi bati walimu wastaafu 25 kila mmoja bati 20.
Viongozi wa CWT Kilolo (kulia) wakiwakabidhi walimu wastaafu 25 zawadi ya bati 20 kila mmoja .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA