Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 252 | 253 | (Page 254) | 255 | 256 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKKT) Iringa Mhadhamu Owdenburg Mdegela (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Habari Assah Mwambene (kushoto) leo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKKT) Mkoa wa Iringa Mhadhamu Owdenburg Mdegela (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari (MAELEZO) Assah Mwambene ofisini kwake alipotembelewa jijini Dar es Salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA), Mhe. Jaji Ferdinand Wambali aliwasilisha mada katika mafunzo ya kazi kuboresha huduma ya utoaji haki nchini,yalifanyika leo kwenye Ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hilux mjini Morogoro.
  Baadhi ya Makarani wakiwa katika mafunzo ya kazi kuboresha huduma ya utoaji haki nchini,yalifanyika leo kwenye Ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hilux mjini Morogoro.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha Ushoni cha wajasiri amali wa Kibweni kilichoanzishwa na Jumuiya ya Vijana wa Kibweni { Kibweni Yourth Organization - KYO } katika Mtaa wa Kwa Botoro Kibweni Jimbo la Bububu.
  Balozi Seif akiangalia mmoja miongoni mwa wafanuzi wa chuo cha ushoni cha ujasiri amali kiliopo Kwa Botoro Kibweni mara baada ya kukizindua rasmi chuo hicho.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi vyarahani Vitano Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa Kibweni Kassim Ali ikiwa mchango wake kusaidia nguvu za nutendji Jumuiya hiyo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi mzima wa Jumuiya Vijana ya Kibweni pamoja na wadau wao mara baada wa uzinduzi wa chuo cha Jumuiya hiyo cha Ushoni cha ujasiri amali kiliopo kwa Botoro Kibweni. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  MMK MEDIA GROUP SWAHILI TV, SWAHILI RADIO na DMK411

  Tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mwana habari mwenzetu ndugu Issa Michuzi na Blog yake 
  www.issamichuzi.blogspot.com kwa kazi kubwa walioifanya na wanayoendelea kuifanya ya kuhabarisha jamii yetu kwa muda wa Miaka tisa (9) mfululizo bila kupumzika.

  Blog ya Issa Michuzi imetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa  tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland. 
  Kwanza kabisa; tunampa hongera Ndugu  Michuzi kwa kuandika historia kwa kuleta mapinduzi ya habari ndani nchini na nje ya Tanzania.

  Pili; tumefurahishwa sana kwa kitendo cha Ndugu Michuzi kurudisha shukrani na fadhila kwa Baba wa Ma-blog Bwana Ndesanjo Macha kwa kumtambulisha, kumuingiza na kumfungulia blog ya jamii ya  www.issamichuzi.blogspot.com mnamo tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland. 


  Tatu; Pongezi za kipekee zimuendee Ndugu Issa Michuzi kwa kazi kubwa ya kutuhabarisha usiku na mchana pamoja na majukumu yake ya  kikazi akilitumikia vyema Taifa letu la Tanzania katika Ofisi Kuu kuliko zote akiwa kama  Mwanahabari Mpiga Picha (Photo Journalist) mwajiriwa wa Serikali akifanya kazi chini ya  Kurugenzi ya Mawasiliano, Ofisi ya Rais Ikulu ya Tanzania.

  Nne; Ni ukweli usiopingika kwamba Issa Michuzi ni mtu wa watu, anapenda watu na ucheshi wake umemletea mafanikio makubwa katika tasnia ya habari. Kwa upande mwingine Michuzi ameitumia vyema nafasi ya kipekee aliyopata kutuhabarisha kwa kutujuza mambo mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi. Hakuna ubishi tukijiuliza swali ni wafanyakazi wangapi waliopo sasa hivi Serikalini katika nafasi kama ya  Michuzi, ama waliopita ambao wamefanya mapinduzi ya habari kama Michuzi? 
  Ndugu msomaji, ukweli unabaki palepale Michuzi anastahili pongezi za kipekee kwa kuthubutu.

  Mwisho kwa kumalizia napenda kuufahamisha Umma kwamba  Bwana Issa Michuzi amekuwa mfano wa kuigwa na jitihada zake na mazingira yake kikazi yamekuwa chanzo cha mafanikio na umaarufu mkubwa aliojizolea na kujijengea jina nchini na nje ya nchi. Hongera kwa jitihada na harakati zako.
  Tunatambua pia kwa nafasi uliyonayo kikazi inakupa mlango wa kupata habari kabla ya vyombo vingine vya habari kupata,  na vilevile kwa kuwa mwajiriwa wa Serikali umejijengea heshima kwa taasisi, wizara na vyombo vingine vya Kiserikali kukuleletea habari zao moja kwa moja wewe kwanza kabla ya vyombo vingine, kitu ambacho kimefanya watu wengi tuwe tunasoma blog yako na kuipenda kitu ambacho ni kuzuri na cha kuigwa.

  Mwisho tunakuomba ukaze mwendo na uendelee kutuhabarisha
  ALUTA KONTINUA
  MMK MEDIA GROUP
  www.mmkmediagroup.com
  www.swahilitv.info
  www.swahilitv.blogspot.com
  www.dmk411.blogspot.com

  www.swahilitv.info www.swahilitv.blogspot.com

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa amewataka waimbaji wa nyimbo za injili nchini, kuhubiri zaidi amani ya Tanzania katika tungo zao.

  Lowassa aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa album ya mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili hapa nchini,Bahati Bukuku iitwayo dunia,wakati wa Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.

  "Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba waimbaji wa injili, kuhubiri zaidi amani ya nchi yetu,amani ni muhimu sana jamani,mkitumia kipaji chenu hiki kuhubiri amani, taifa letu litaendelea kuwa na Umoja,upendo na mshikamano" alisema Lowassa huku akishangiliwa na maelfu ya waumini wa kanisa la EAGT city center pamoja na wananchi wengine.

  Awali katika risala yake, Bahati Bukuku alisema ameanzisha kampuni ya kurekodi na kusambaza Kazi za waimbaji wa nyimbo za injili, hivyo anahitaji msaada kufanisha lengo lake hilo.

  Moja wapo ya hatua za kufanikisha lengo lake hilo, ni kufanyika kwa Harambee sambamba na uzinduzi huo, ambapo Mh Lowassa na mkewe walichangia shilingi milioni kumi, marafiki zake watatu, akiwemo Philemon Mollel, Anoj Shaha ambaye ni mkurugenzi wa kiwanda Cha A to Z waliyotoa milioni tano kila mmoja.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa ameketi kusikiliza lisala ya hafla hiyo iliyokuwa ikisomwa na Bahati Bukuku (hayupo pichani) huku umati wa waumini wakifatilia kwa umakini.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiombewa na mchungaji Katunzi wa EAGT pamoja na waumini wengine,wakati wa hafla ya uzinduzi wa albamu ya Nyimbo ya Injili iitwa Dunia,iliyoimwa na Mwanamama Bahati Bukuku.
  Muchungaji wa kanisa la EAGT City Center,Florian Katunzi (mwenye kipaza sauti) akiombea baadhi ya cd za album ya Bahati Bukuku iitwayo dunia,Kabla ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa (katikati).Watatu kulia ni mwimbaji huyo Bahati Bukuku.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendesha Harambee hiyo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya watu wakati alipokuwa akiondoka ukumbini hapo.

  0 0

  Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wamerejea nyumbani baada ya mechi yao na Gambia ambapo walifungwa 2-0 huku matarajio yote sasa yakiwa ni kufuzu kucheza Kombe la Afrika 2015.

  Wachezaji hao 18 pamoja na benchi la ufundi waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa nane mchana kwa ndege la shirika la Kenya.

  Hii ni mechi ambayo Taifa Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, ilitakiwa kushinda lakini ilikosa wachezaji tisa muhimu ambapo baadhi yao hawakuruhusiwa na vilabu vyao na wengine walikuwa majeruhi.

  Akizungumza baada ya kuwasili kocha Kim Poulsen alisema kuutkana na hali halisi alilazimika kuwachezesha wachezaji vijana ambao uzoefu wao sio mkubwa sana kama ule wa wachezaji wa kawaida ambao mara nyingi huwa wanaanza.

  “Tumesikitishwa na matokeo haya lakini kama nilivyosema Gambia waliita wachezaji wao wote wanaocheza nje lakini sisi tulikosa timu karibu nzima….vijana waliocheza walijitahidi lakini wenzetu waliwazidi uzoefu,” alisema.

  Alisema ni muhimu watanzania watambue kuwa mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia zimekuwa muhimu sana kwa Tanzania kwani wachezaji wengi wametambulika na wameitwa nje. “Kuna wachezaji kama Shomari kapombe, Mwinyi Kazimoto, ambao kutokana na mechi hizi wamepata nafasi ya kwenda kucheza nje,” alisema.

  Kocha huyo alisema yuko makini sana kutekeleza mpango wa muda mrefu ambao ni kuhakikisha Tanzania inafuzu kucheza Kombe la Afrika 2015,” alisema na kuongeza kuwa timu anayoendelea kujenga itafanya kazi hiyo.

  Alisisitiza kuwa ni lazima TFF ihakikishe wachezaji wote muhimu wanakuwepo wakati mechi za kufuzu kucheza Kombe la Afrika zitakapoanza mwakani.

  “Kwa sasa wachezaji watarudi vilabuni kwao na baada ya muda mfupinitawaita tena ili tujiandae na Mashindano ya CECAFA Senior Challenge yatakayofanyika Nairobi,” alisema.

  Aliwataka watanzania wawe na subira kwani ana imani na timu anayoijenga.

  Akiunga mkono maneno ya Poulsen, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema ni lazima nguvu zote zielekezwe katika AFCON 2015.

  “Tungefurahi kama tungefuzu kucheza Kombe la Dunia lakini ni mapema sana kwa timu yetu ambayo bado inajengwa…tumpe kocha nafasi aweze kutimiza haya malengo na sio kumkatisha tama,” alisema.

  Alisema wao kama wadhamini wanafarajika na mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika katika Timu ya Taifa tangu waanze kuidhamini Timu hiyo mwezi Mei mwaka uliopita.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akisalimiana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ,Mastidia Rutaihwa baada ya kumkabidhi moja ya boksi la dawa na vifa vilivyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa Uzinduzi rasmi wa Huduma za Tiba kutoka kwa Madaktari Bingwa kwa wanachama wa NHIF katika jamii ya Mkoa wa Pwani uzinduzi huo ulizihusisha wilaya zote tata za Rufiji, Mafia na Bagamoyo.Katikati anaye shuhudia ni Mjumbe wa Bodi ya NHIF Charles Kajege.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwatumu Mahiza akiteta jambo na Madaktari Bingwa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya baada ya kuzindua zoezi la kutoa Huduma za Tiba kutoka kwa Madaktari Bingwa kwa wanachama wa mfuko wa NHIF. Uzinduzi huo ulifanyika katika Wilaya ya Bagamoyo kwa niaba ya wilaya za Rufia na Mafia
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akihutubia wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo wakati wa Uzinduzi rasmi wa zoezi la kutoa Huduma za Tiba Kutoka kwa Madaktari Bingwa kwa Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa Jamii ya Mkoa wa Pwani, wa pili kutoka kushoto ni mjumbe wa Bodi ya NHIF Charles Kajege,Mkurugenzi Rasmaili Watu na Utawala Beatus Chijumba na Meneja Mkuu wa NHIF mkoa wa Pwani Andrew Mwilunga.
  Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Charles Kajege akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza moja ya boksi lenye vifaa na Dawa wakati wa Uzinduzi rasmi wa zoezi la Huduma za Tiba kutoka kwa Madaktari Bingwa wa NHIF, kwa wanachama wa mfuko huo na jamii ya Mkoa wa Pwani .Uzinduzi huo ulifanyika katikaWilaya ya Bagamoyo kwa niaba ya wilaya za Mafia na Rufiji.

  0 0

  Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi nchini, Airtel imetajwa kuwa moja kati ya makampuni ambayo yamekuwa yakishirikiana na serikali kwa dhati katika harakati za kupambana na tatizo la ajali za barabarani.

  Akithibitisha madai hayo, Kamanda mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga amesema kuwa Airtel imeweza kutoa mchango katika kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa ikitoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na kikosi cha usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha ajali za barabarani.

  "Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani, kwa miaka mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Airtel pia imedhamini vipindi vya elimu ya usalama barabarani katika TV - kumekucha na Jambo Tanzania (ITV na TBC 1) na Radio one.

  Pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na jeshi la polisi usalama barabarani imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu = Kifo inayowaasa waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati wakiendesha magari, vile vile mwaka jana Airtel ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (Bodaboda) yaliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki ," alisema DCP Mpinga.

  Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania Bi Beatrice Singano Mallya, akizungumza juu ya suala hilo, amesema "Airtel imeamua kushirikiana na serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi la ajali za barabarani. Idadi ya vifo vinavyotokea barabarani ni kubwa mno na ndiyo maana Airtel imeamua kujikita katika kuokoa maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujuma. Tunapenda kuwakumbusha watanzania kuwa swala la kupunguza ajali za barabarani ni wajibu wa kila mwananchi hivyo tutii sheria bila shuruti".

  Airtel itaendelea kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika kuhakikisha lengo letu la kupunguza ajali linafanikiwa, tumeanza kuona mafanikio na kwa kiasi Fulani ajali za barabarani zinapungua kulinganisha na miaka iliyopita," alisema Beatrice.

  Tumepatiwa Takwimua kwa na ofisi inayoratibu wiki ya nenda kwa usalama barabarani zinabainisha ajali za barabarani zimeweza kupungua kwa kiasi kikubwa tokea mwaka 2011 ambapo Airtel imekuwa ikishirikiana nao katika programu mbalimbali mjini na vijijini, kabla ya hapo tokea mwaka 1995 ajali zilikuwa zikiongezeka kila mwaka kati ya ajali 2,000 na 4,000. Lakini Mwaka 2010 ukilinganisha na 2011 ajali zilipungua kwa 3% na 2011 na 2012 ajali zilipungua kwa 2%.

  Airtel Tanzania inaendelea na kudhamini wiki hii ambapo kwa mwaka huu imejitolea kuchapisha tena stika za usalama barabarani pamoja na kudhamini tena mashindano ya mpira wa miguu ya waendesha bodaboda yajulikanayo kama MPINGA CUP ambayo dhamira yake ni kuunga mkono juhudi za baraza linaloshughulikia usalama barabarani maalum kwa kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu barabara zote ili kuepusha ajali.

  0 0
 • 09/09/13--06:16: Article 13

 • 0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond 'Sukari ya Warembo' akiwapa ujumbe wa Tupo Wangapi??? Wananchi waliojotokeza katika tamasha la 'Tupo Wangapi' la kuhamasisha jamii kuachana na mitandao ya ngono lililoandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, H.Baba 'Mkali wa Mauno' akitoa burudani kwa Wananchi waliojotokeza katika tamasha la 'Tupo Wangapi' la kuhamasisha jamii kuachana na mitandao ya ngono lililoandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Snura 'Mama wa Manjanga' akiwapa ujumbe wa Tupo Wangapi??? Wananchi waliojotokeza katika tamasha la 'Tupo Wangapi' la kuhamasisha jamii kuachana na mitandao ya ngono lililoandaliwa na Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ndani ya viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia nyaraka za aina kumbukumbu mbalimbali kwenye maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Hifadhi ya kumbukumbu za Kitaifa za Oman Dk.t Hemed Mohammed Al-Dhawyani kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa maonesho ya kumbukumbu za nyaraka ya kitaifa za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)

  0 0

  Chifu wa Wasukuma Wilaya ya Kwimba Shimbi Martin Morgan akimabidhi silaha za jadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za kumtawaza kuwa Mtemi wa Sungusungu Kitaifa, zilizofanyika kijiji Ngudu, Wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza. 
  Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0

  Hatimae Mabingwa wa Mashindano ya Ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi na kufadhiliwa na Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni amepatikana.
  Hii ni baada ya mchezo wa Fainali ya mashindano hayo yaliyozikutanisha Timu za Soka za Kitamli ya Nungwi dhidi ya wapinzani wao Timu ya Soka ya Mwendo Mdundo ya Kidoti. 
   Pambano hilo la Fainali lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wapenzi wa soka wa Jimbo la Nungwi na Vitongoji vyake limeiwezesha Wenyeji wa mashindano hayo Timu ya Kitamli ya Nungwi kuibuka na ushindi kwa kuilaza Mwendo Mdundo ya Kidoti Goli 1-0. 
   Timu ya Kitamli ilijipatia goli lake la pekee na la ushindi lililofungwa na mchezaji Haji Wa Haji katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ambapo mgeni rasmi katika pambano hilo la Fainali ya Dr. Sheni Cup alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Mashindano hayo ya ujirani mwema yaliyoanza kutimua vumbi Tarehe 24/8/2013 yamejumuisha Timu Tisa kutoka katika vijiji tofauti vya Jimbo la Nungwi yakienda sambamba na yale ya mchezo wa Pete { Net Ball } kwa Wanawake yaliyojumuisha Timu Nne. 
   Akizungumza mara baada ya pambano hilo la Fainali Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwahimiza Vijana hao kujitahidi kujifunza zaidi michezo ili wajijengee njia rahisi ya kupata ajira kupitia sekta ya michezo ambayo wakati huu imekuwa na thamani kubwa Duniani. Balozi Seif alisema Ulimwengu hivi sasa umeshuhudia ongezeko kubwa la ajira kupitia Sekta ya michezo hasa Mchezo wa soka na Table Tennis ambayo imeonekana kutajirisha wanamichezo wengi wenye vipaji vikubwa vya michezo hiyo. 
   “ Tumeshuhudia wachezaji mbali mbali Duniani wakiwemo pia wale wanaotokea Bara letu la Afrika wakicheza mpira wa kulipwa katika timu mbali mbali za bara la Ulaya hasa ndani ya Uingereza. Huo ni Mfano halisi mmaopaswa kuutilia maanani ili na nyinyi siku moja mjikute mmetinga katika vilabu hivyo maarufu Duniani “. Alisisitiza Balozi Seif.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi Kipa Bora wa mashindano ya ujirani mwema ya Dr. Sheni Cup yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Jimbo la Nungwi.
   Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohamed Haji jezi na vifaa baada ya timu hiyo kuibuka bingwa wa  Dr. Sheni Cup huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
   Balozi Seif akimkabidhi Kikombe Kepteni ya Mabanati wa Timu ya Pete ya Tusitengane ya Nungwi Ndamu Makame Mussa baada ya kuibuka na ushindi wa Kombe la Mwanamwema Sheni dhidi ya Timu ya Pete ya Tuko Imara.
    Kepteni wa Timu ya Soka ya Kitamli ya Nungwi Makame Mohamed Haji akifuahia kikombe anachokabidhiwa na mgeni rasmi balozi Seif baada ya kutawadhwa kuwa mabingwa wa kombe hilo.Kati kati yao ni lezi wa Jimbo la Nungwi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa wa Idara Maalum Haji Omar Kheir
  Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Michezo Zanzibar { BTMZ } Sharifa Khamis akipokea mchango wa shilingi Milioni 2,000,000/- kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia ufufuaji wa michezo ya ndani inayoonekana kufifia hapa Nchini.

  0 0

  Taswira ya uwanja wa Maonyesho ya Biashara kwa  wafanyabiashara toka nchi tano za jumuia ya Africa Mashariki yaani Uganda, Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda yanayoendelea jijini Mwanza kama ilivyonaswa na kamera yetu leo

  0 0

  KWA KULA SAMAKI HUYU MWENYE GAMBA GUMU AINA YA OYSTER AU CHAZA KWA KIMATUMBI,  KUNA UWEZEKANO WA ASILIMIA 99 KUONGEZA  HESHIMA YA BOMA (NGUVU ZA KIUME)  NDANI YA DAKIKA 10 TU 
  UKIMLA HUYU CHAZA UTAKUA NA NGUVU ZA KAWAIDA TU KAMA BINADAMU WENGINE BILA MADHARA KWA MWILI WAKO AU MWILI WA MWENZI WAKO BADALA YA KUTUMIA DAWA ZENYE MADHARA NA MWILI WAKO NA KWA MWENZI WAKO.... 


  KAMA UNAONA KINYAA BASI MWAGIA CHUMVI NA LIMAO KISHA MLE TARATIBU


   PIA UNAWEZA MMWAGIA BALSAMIC VINEGAR AU SIKI KUONGEZA LADHA


  VIPANDE VIWILI AU VITATU VINATOSHA KABISA KWA DOZI UNASHAURIWA KULA MARA MOJA KWA WIKI, KAMA MBICHI INAKUSHINDA UNAWEZA KULA WALE WA KWENYE MAKOPO, AU WA KUCHEMSHWA LAKINI USILE WA BBQ AU WA KUKAANGA KABISA UKIMALIZA KULA TU BAADA YA DAKIKA 10 MAJIBU UTAYAONA.
  Kwa taarifa kamili tembelea libeneke la Chef Issa
  BOFYA HAPA

  0 0

  ???????????????????????????????
  Balozi mpya wa vijana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania Bi.Tamara Bertha Itanisa

  ???????????????????????????????

  Mabalozi wapya wa vijana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania Bi.Tamara Bertha Itanisa na kushoto ni naibu wake Alice Mseti. Kwa picha zaidi ungana na Sundayshomari.com

  0 0

   Zuberi Mussa  katika muonekano wa picha tofauti 
  tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.

  Zuberi Mussa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Dotto Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya (kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo na Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira mkoani Tanga, walipokwenda kumjulia hali kijjiini kwao.

  Na Dotto Mwaibale, Tanga

  Zuberi Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali.

  Kikubwa kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa ambao bado haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili na ya tatu wakati wa kuongea naye hautaelewana naye kutokana na matamshi yake ambayo hayafahamiki yanayoonesha  kama mtu aliyechanganyikiwa.

  Kutokana na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika matibabu hasa Hospitalini, Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake kwa waganga wa jadi.

  Wakati Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani Korogwe mkoani Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema Amir kwa kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es Salaam, hawezi kufanya chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika inaumiza na kusikitisha.

  Ndugu wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni tulionao wa kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

  Binafsi nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita nilishitushwa na hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.

  Zuberi alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali ambayo si ya kawaida zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea naye hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi pamoja na mke wake kipenzi  Rehema Amir anaweza kuwasiliana na Dotto Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na kaka yake.

  Ndugu wanahabari wenzangu  na mtu mmoja mmoja, Taasisi yoyote, shirika lolote, Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya, Wafanyabiashara, Makampuni mbalimbali na vyama vya michezo  hima tujitoe kimasomaso kumsaidia mpiga naji mwenzetu Zuberi Mussa na mke wake waondoke katika matibabu ya jadi wanayopata kwa waganga wa kienyeji badala yake wapelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya zao kwani kutoa ni moyo na si utajiri.

  0 0

  Adubo Mustafa Omer Enzi ya uhai wake

  Picha hapo juu ndiye marehemu Adudo Omer ambaye maiti yake ipo montuary Dallas Texas nchini Marekani tangia Aug 26, 2013 bado wanatafutwa ndugu, jamaa au watu wanaomfahamu marehemu popote pale walipo. Marehemu alizaliwa April 25, 1956.

  Marehemu alishawahi kuishi kwenye miji ifuatayo hapa Marekani  Lincoln na Omaha miji iliyopo Nebraska. pia alishawahiishi Des Moines naCedar Rapids miji iliyopo Iowa.

  Tafadhali tunaomba ndugu au mtu yeyote anayemfahamu  marehemu wajitokeze

  Tafadhali wasiliana na 
  Ben Kazora@ 269 873 0937
  Viola Mbise @ 405 613 3445
  Frank Maji@ 214 674 6666


older | 1 | .... | 252 | 253 | (Page 254) | 255 | 256 | .... | 3272 | newer