Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SUKOS yakabidhi vifaa vya zima moto kwa Idara ya Uratibu wa Maafa Nchini

$
0
0

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji - SUKOS, Suleiman Kova akimkabidhi vifaa vya zima moto Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto katika maeneo ya kazi.
 Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Utafiti Idara ya Uratibu wa Maafa Bw.Bashiru Taratibu akiangalia vifaa vya zima moto vilivyokabidhiwa na Taasisi ya Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji –SUKOS Oktoba 15, 2018 kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Oparesheni Bi.Rahma Kova wakati wa kukabidhi cheti cha Shukrani ya ushirikiano uliopo kati ya SUKOS  na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akikabidhi Hati ya Shukrani kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe walipomtembelea kukabidhi vifaa vya zima moto Ofisini kwake Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa SUKOS Foundation walipotembelea Idara hiyo ili kukabidhi Vifaa vya Zima Moto pamoja na hati ya shukrani kwa namna Taasisi yake inavyoshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Suleiman Kova. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Tazama Karakana Kuu ya Reli iliyofunguliwa na Baba wa Taifa inavyofanya kazi Morogoro

RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ameagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.
Vigogo walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani Mara moja. RC Makonda ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa utatuzi wa kero za wafanyabiashara Soko la Kariakoo ambapo pia ametoa siku tano kwa watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru mdogomdogo baada ya kubaini uwepo wa ushuru mkubwa unaoumiza na kuwarudisha nyuma wafanyabiashara. 
"Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani" Alisema RC Makonda. 
 Aidha RC Makonda ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina ya mbia na soko na badala yake ameagiza kazi ya ukusanyaji wa ushuru ifanywe na uongozi wa soko.
Pamoja na hayo RC Makonda ameagiza soko kuu la Kariakoo kurejeshwa kwenye hadhi ya kimataifa na sio kuendeshwa kiholela kama ilivyo sasa ambapo linapokea bidhaa za rejareja kutoka mitaani badala ya kuwa soko la kuuza bidhaa za jumla. 
 Miongoni mwa kero zilizolalamikiwa na wafanyabiashara ni uhusiano mbovu baina ya viongozi na wafanyabiashara, kodi ya pango, vyanzo vingi vya ushuru, mikataba, mikopo, soko kupoteza mwelekeo, mkanganyiko kwenye viwango vya vipimo, kadi ya kizimba na ukamataji ambapo RC Makonda ameahidi kuzifanyia kazi.

Uongozi Institute Yaandaa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO
Maboresho yanayofanyika ndani ya Jeshi la Polisi yametajwa kuongeza tija katika huduma zinazotolewa kwa wananchi hali inayochangia kupungua kwa vitendo vya uhalifu nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Ngimba amesma mafunzo ya uongozi kwa makamanda wa polisi wa mikoa na wale wa makao makuu yatasaidia kuongeza weledi kwa watendaji hao wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka na yatasaidia kutatua changamoto zilizopo katika utendaji wenu katika mikoa mkiwa kama Makamanda wa Polisi”, alisisitiza Ngimba.
Akifafanua, Ngimba amesema mafunzo hayo yanayoratbiwa na Taasisi ya Uongozi yana lengo la kuwaongezea ujuzi maafisa hao waaandamizi wa polisi na yatajikita katika maeneo ya muundo wa Jeshi la Polisi, Usalama wa nchi, maadili na rushwa, uongozi na utendaji binafsi, mahusiano yenye tija na akili hisia.
Mkurugenzi Ngimba pia aliwakumbusha makamanda  wa Jeshi hilo kuzingatia maadili na nidhamu kwa sababu ni moja ya nguzo muhimu za utendaji. Aidha, amewaagiza maafisa hao kuakikisha  wanawachukulia hatua stahiki maafisa na maaskari walio chini yao pale wanapojihusisha na vitendo vyenye kulichafua jeshi la Polisi kama vile rushwa na utovu wa nidhamu.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.  Joseph Semboja  amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikina na Jeshi hilo na  kufanyika kwake ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuimarisha utawala bora hapa nchini.
Aliongeza kuwa analipongeza Jeshi hilo kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo yanayolenga kuimarisha utendaji wake.
“Utendaji mzuri wa Jeshi la Polisi unajenga sifa nzuri kwa Serikali kutoka kwa wananchi wanaopata huduma kila siku kwani hili ndilo eneo ambalo taswira ya Serikali inaonekana kwa haraka”. Alisisitiza Prof. Semboja.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Saimon  Siro, Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, Kamishna wa Polisi, Albert Nyamhanga amesema kuwa nchi iko shwari na makosa ya jinai yamepungua kufikia asilimia 13.7 kwa sasa kutokana na utendaji  mzuri na ushirikiano uliopo kati ya Jeshi hilo na wananchi.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kufanya tathmini ya utendaji wa Jeshi hilo kujua llipotoka, lilipo na linapoelekea hali itakayosaidia kuboresha utendaji wake.
Naye Mkuu wa  Mfunzo na Operesheni wa Jeshi hilo, Kamishna wa Polisi, Nsato Marijani ameishukuru Taasisi ya Uongozi kwa kutenga muda na rasilimali fedha kufanikisha mafunzo hayo yanayotarajiwa kuboresha ufanisi kwenye taasisi hiyo muhimu nchini.
 Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.  Joseph Semboja akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo  kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.
 Sehemu ya makamanda wa Polisi wakifuatilia mafunzo  kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.
 Sehemu ya makamanda wa Polisi wakifuatilia mafunzo  kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.
 Sehemu ya Makamanda wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo maalum wa Jeshi hilo wakati wa mafunzo  kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na Makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma  Kamishna mwandamizi wa Jeshi la Polisi Giles   Muroto akizungumza wakati wa mafunzo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakiwemo kutoka makao makuu ya Jeshi hilo na makamanda wa Polisi wa Mikoa yanayofanyika Jijini Dodoma kwa siku tano.

VOA SWAHILI: Duniani Leo October 15, 2018

TAARIFA YA HABARI YA ITV SAA MBILI USIKU 15 OKTOBA 2018

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

SHIRIKA LA DAWA ASILIA NA ULINZI WA MAZINGIRA WAWAASA WATANZANIA KUWAENZI WAASISI WA TAIFA LA TANZANIA

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

Katika kumbukizi ya miaka 19 ya Muasisi wa Taifa la Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage nyerere   ambae alifanikisha kupatikana kwa uhuru mnamo mwaka 1960 wadau pamoja na  Shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira (TRAMEPRO) wamefanya dua katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Aidha Mkurugenzi wa shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira  (TRAMEPRO) Simba simba ameeleza lengo la kudhuru makaburi hayo ni kumuenzi marehemu Kingunge Ngombale Mwiru ambae walishirikiana na hayati nyerere katika kujikomboa Kwenye utumwa na kufanikisha kupatikana kwa uhuru na kuifanya nchi ya Tanzania kuwa ya mshikamano na Umoja.

Aidha , Simba amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Mapinduzi ya awamu ya nne chini ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ameweza kuiga mifano,uchapakazi na ushupavu  ambao alikua akifanya Muasisi huyo.

Hivyo basi vijana pamoja na viongozi hawana budi kuwaenzi waasisi ambao wametoa mchango mkubwa katika kulijenga,kulitetea na kuimarisha Muungano kwa ajili ya Mustakabali wa Taifa letu kwa ujumla.

Pia. Ametoa rai kwa viongozi wengine kuwaenzi waasisi hao ambao walileta uhuru na kuifanya nchi iwe ya amani hivo basi tujitahidi kulinda amani hiyo ambayo ikipotea ni madhara kwetu sote.

Katibu Mkuu wa Shirika la dawa asilia na ulinzi wa mazingira  (TRAMEPRO) Bonaventura Mwarongo ameeleza mchango wa Kingunge Ngombale Mwiru  aliteuliwa kwenda London uingereza kuuchukua mwili wa hayati Kambarage nyerere   na Kuuleta Tanzania.

Mwarongo ameeleza licha ya kushirikiana Kwenye jitihada za kulitetea Taifa pia ngombali  alikua mlezi kwa chama cha dawa asilia na kuhakikisha wanapewa vipaumbele katika kuleta chachu Pamoja kuwawekea mikakati sahihi ya kutoa huduma zao na kueka sheria za utoaji wake.

MIAKA 19 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA, WASOMI WATOA NENO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

KATIKA kuadhimisha   miaka 19 tangu baba wa taifa afariki tarehe  14, Oktoba mwaka 1999 viongozi na wananchi kupitia majukwaa wamemuenzi kwa kuweka mijadala mbalimbali iliyolenga kujikumbusha yale tuliyohusiwa na baba wa taifa.

Akizungumza na Blogu ya jamii msomi na mwanahistoria Francis Daudi ameielezea sikuuu hii ya kumbikizi ya Mwalimu Nyerere hasa katika uongozi wake na uwezo wa kuunganisha makabila 120, bila vita.

 "Nafikiri kila mtanzania anaweza ongea kitu juu ya Baba wa Taifa letu, swali kama Taifa ‘tumemis’  nini toka kwa Mwalimu,
jibu linaweza lisiwe sahihi kwani Mwalimu hayupo; Na kusema angelikuwepo angelifanya hivi au vile sio sawa. Lakini ilipaswa lijibiwe tu" ameeleza.

Akieleza kuhusu mambo ambayo taifa linatamani kutoka kwa Mwalimu ni pamoja na Mwalimu kuwa  mwandishi mzuri sana wa vitabu ambapo aliandika vitabu vingi na pia alitafsiri vitabu vingine.

" Nafikiri Taifa hasa hiki kizazi chetu cha Vijana ‘ tumemis’ vitabu vipya vilivyoandikwa na Mwalimu Mwenyewe" amesema

Aidha amesema kuwa;  "Taifa limemis ile Sauti ya Ukali ya Baba wa Taifa, Ikionya na kukemea mambo yasipokwenda vizuri. Leo sauti ile tunaisikia ikikemea kupitia vyombo vya habari lakini hatunaye na
 baadhi ya mambo alionya siku nyingi yamebaki kuwa na uhalisia hadi leo. Maneno ya Mwalimu yamebaki na ‘Ukali’ wake ule ule bila kusukumwa kando na nguvu ya historia" ameeleza

Pia amesema kuwa taifa limekumbuka uadilifu wa mwalimu, kwani angekemea vikali viongozi ambao wanajisahau kuwa cheo ni dhamana. Wasiojua kuwa Uongozi ni huduma. Wasiosimamia haki na kupinga rushwa na ubadhirifu
sauti nzito ya Kibaba ingekemea vikali uvaaji mbovu wa vijana, Ungekemea mno vijana wasiopenda kufanya kazi na wanaouza mali za nyumbani ili ‘kubeti’. Nafikiri angekemea miziki isiyo na adabu!" Amefafanua zaidi.

Pia amesema kuwa Mwalimu angekemea matumizi mabovu ya Kiswahili pamoja na mazongezonge yote ya uchafuzi wa lugha.

Amesema kuwa Mwalimu atakumbukwa kwa kuwa mwana wa Afrika, Mtatuzi wa migogoro na mpenda Amani kindakindaki. Bila shaka Umoja wa Afrika na Mashirika makubwa yangemtumia zaidi katika kutatua migogoro mingi ndani ya Afrika.

Kiufupi Mwalimu angeweza kututangaza na kuitetea vizuri ile heshima nje ya mipaka ya Taifa letu.

Na ameeleza kuwa Mwalimu alipendwa na watu wa dini zote, kabila zote na rika zote. Alikuwa sio mtu wa kusita. akifanya maamuzi, Anasonga mbele na kuacha historia ihukumu. Pale alipogundua amekosea alikiri hadharani na kusema wazi ilikuwa ni KOSA.

Kuhusiana na  Misimamo na Matendo yake Mwanahistoria huyo amesema kuwa, ingekuwa ni kielelezo tosha kwa viongozi vijana ambao hatujui moja kwa moja alivyokuwa nje ya hotuba na maandishi tunayosoma
wakati Fulani, Mwaka 1994 aliombwa kuwa mgeni rasmi kwenye Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi kitaifa. Mwalimu alikataa mwaliko huo, aliwaeleza wazi kuwa hayo majukumu ya kitaifa ni ya Rais aliye madarakani, hivyo aliyestahili heshima hiyo si yeye bali ni Rais Ali Hassan Mwinyi.

 Amesema kuwa; "Nafikiri angekuwepo angeonesha kwa vitendo kiongozi jinsi kiongozi anapaswa kuenenda na ni aibu kubwa kujiita Mwanafunzi au Muumini wa Mwalimu kama matendo yako hayaakisi Fikra zake" ameeleza Francis.

Na ameshauri kuhusu kujitafakari, na kuenenda vizuri katika njia nzuri ambazo Mwalimu, Mjezi makini wa Taifa alipenda tupite kwa ustawi wetu tukikengeuka, Historia itatung’ong’a na kutuhukumu daima.

Aliyekuwa Miss Ubungo asherekea siku ya kunawa mikono na wanafunzi wa shule ya msingi Umoja

$
0
0
Aliyekuwa Miss Ubungo 2014-2016 Diana Kato amesherehekea siku ya Kunawa mikono duniani na wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja.

Siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka

Mlimbwende huyo amekuwa anajihushisha na shughuli za kijamii katika swala zima la Upatikanaji wa Maji Safi na Salama na katika shule za Msingi amesherekea siku hii ya Kunawa mikono kwa kuwafundisha watoto Jinsi ya kunawa mikono na faida za kunawa mikono.

Pia Miss Diana Kato amekutana na changamoto mbalimbali katika shule ya Msingi Umoja iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam zikiwemo ubovu wa vyoo vya Wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja pia na kutokuwa na Maji  Salama kwa kunywa shuleni hapo.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa wamedhika mabango yanayohamasisha usafi wa mazingira katika eneo la shule wakati wa siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Umoja wakinawa mikono ili kujilinda ma magonjwa mbalimbali wa wakati wa siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka.
Aliyekuwa Miss Ubungo 2014-2016 Diana Kato akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Umojaalipowatembelea  ili kahamasisha usafi hasa kunawa mikono kwa kutumia maji safi wakati wa siku ya kunawa mikono Duniani inaadhimishwa kila ifikapo Oktoba 15 kila mwaka.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 16,2018

JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI

$
0
0
Na Lydia Churi- Mahakama, Mwanza 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka watumishi wa Mahakama katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza hususan Mahakimu kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa kuhakikisha wanamaliza kesi ili wananchi waweze kupata haki kwa wakati. 

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nansio-Ukerewe pamoja na Mahakama za Mwanzo za Ilangala na Nansio mjini, Jaji Mkuu pia amewakumbusha Mahakimu kuhakikisha hukumu zinatolewa ndani ya siku 90 baada ya shauri kusikilizwa na endapo siku zitazidi basi zisizidi siku ishirini na moja. 

Alisema Mahakama ya Tanzania inafanya kila jitihada ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati huku akitolea mfano wa nakala za hukumu kutolewa bure. Alisema Mahakama imeingia mkataba na shirika la Posta ili kusambaza nakala za hukumu pamoja na nyaraka nyingine za mahakama. 

“Suala la hakimu kuchelewesha hukumu bila sababu za msingi halikubaliki na ni utovu wa nidhamu, jiwekeni kwenye nafasi ya wanaocheleweshewa hukumu ndipo mtaona ni kwa namna gani wanaumizwa na suala hili”, alisema Jaji Mkuu. Awali akizungumza na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukererwe Bwana Focus Majumbi, Jaji Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa serikali kusaidia kuwaelimisha wananchi taratibu za Mahakama ili wapate haki kwa wakati kwa kuwa haki ni kwa mujibu wa Sheria. 

Alisema wananchi wengi hawafahamu taratibu za Mahakama ambapo badala ya kudai haki zao Mahakamani huenda kwa watu wasiohusika na kusababisha haki zao kuchelewa. Naye Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe aliiomba Mahakama ya Tanzania kuanza kuitumia Mahakama ya Mwanzo ya Irugwa ambayo hivi sasa haijaanza kutumika kutokana na ukosefu watumishi. Mkuu huyo wa wilaya pia aliiomba Mahakama kusaidia ili wilaya yake isaidiwe kupata Mwenyekiti wa kudumu wa mabaraza ya kata. 

Jaji Mkuu wa Tanzania anaendelea na ziara yake ya siku nne mkoani Mwanza ambapo atakagua utekelezaji wa shughuli za Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwasili katika kisiwa cha Ukerewe kuanza ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama katika Mkoa wa Mwanza. Leo Jaji Mkuu alitembelea Mahakama ya wilaya ya Nansio- Ukerewe, Mahakama za Mwanzo za Nansio mjini na Ilangala pamoja na Ofisi ya Mkuu wa wilaya. Katikati ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Mary Moyo. 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama baada ya kumkabidhi kitabu cha Mpango huo Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya (DAS) Bwana Focus Majumbi. 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ilangala mara baada ya kuzungumza nao.wakati Jaji Mkuu alipotembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Mkewe mama Anna Abdalah alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe. Wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania. 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Mkewe mama Anna Abdalah alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe 

MSIBA WA KISASA NDANI YA DIRA YA KITAA..

MICHUZI TV: MKOA WA NJOMBE NA RUVUMA WATOA FURSA KWA WAJASILIAMALI WA KITANZANIA NCHINI CHINA

Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro awa mgeni rasmi maadhimisho ya Taifa la Hispania

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro akihutubia wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya Taifa la Hispania iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi. Katika hotuba yake Mhe. Naibu Waziri ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uhispania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mabalozi na wageni mbalimbali.
Kaimu Balozi wa Hispania Bibi. Teresa Martin naye akihutubia kwenye hafla hiyo 
Sehemu ya Mabalozi na Wageni mbalimbali walio hudhuria hafla hiyo


Sehemu ya Mabalozi na Wageni mbalimbali walio hudhuria hafla hiyo.

TANROADS TABORA YAAGIZWA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUWEKA TAA ZA BARABARANI ZINAZOTUMIA MWANGA WA JUU

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano imeiagiza Wakala wa Barabara wa Tanzania mkoani Tabora kuangalia uwezekano wa kubadilisha mfumo wa taa za barabarani mkoani humo kutoka matumizi ya umeme wa TANESCO na kuanza kutumia umeme wa jua ili kupunguza gharama za uendeshaji kila mwezi.

Kauli hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Elias John Kwandikwa jana mkoani Tabora apokutana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Shinyanga.

Alisema kuwa pamoja na gharama za kubadilisha taa hizo kutoka matumizi ya umeme wa TANESCO kwenda matumizi  kuwa kubwa mwanzo lakini manufaa yake ni makubwa.

Naibu Waziri huyo alisema za barabarani muhumu katika kuimarisha usalama na ulinzi wa raia na mali zao katika mitaa mbalimbali nyakati za usiku.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kwa muda mrefu taa hizo zimekuwa haziwaki kwa sababu ya kuwepo na mvutano juu ya nani kati Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na TANROADS Mkoa huo anayepaswa kulipia ankra za matumizi ya umeme katika barabara kuu.

Alimwomba Naibu Waziri huyo kusaidia kutatua tatizo hilo kwa kuwaagiza TANROADS wawasaidie kubadilisha taa hizo ili ziweze kusaidia katika kuimarisha usalama mitaani.

Kwa upande wa Meneja wa Tanroads mkoa wa Tabora  Damian Ndabalinze alisema kuwa barabra hiyo ina jumla ya nguzo 97

na gharama za uendeshaji wa taa kwa mwezi mmoja hivi sasa kwa kutumia umeme wa TANESCO ni milioni 2 .

Barabara za kutoka Tabora kwenda Urambo imewekwa taa za barabarani lakini zimekuwa haziwaki kwa sababu ya gharama kubwa za ankra zinaletwa na TANESCO.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Aggrey Mwanri(katikati)  ili naye amkaribishe Naibu Waziri wa Ujenzi Elias John Kwandikwa(kushoto) kwa ajili ya kuzungumza na Menejimenti ya Mkoa huo alipopita Tabora akiwa safarini kwenda Mkoani Shinyanga jana.
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakifuatilia hotuba fupi ya Naibu Waziri wa Ujenzi Elias John Kwandikwa(hayupo katika picha) wakati alipopita Mkoani humo akiwa safarini kwenda Shinyanga jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(katikati) akiotoa salamu za Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Elias John Kwandikwa(kushoto) aliyepita Mkoani humo wakati akielekea Mkoani Shiinyanga jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu.  
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa (kushoto) akibadilisha mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kushoto), Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu( wa pili kutoka kulia) na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Tabora Damiani Ndabalinze(kulia) wakati alipopita mkoani humo jana akiwa safarini kuelekea Shinyanga.

TAARIFA

MRADI WA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM WAFIKIA ASILIMIA 42

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam 
Nditiye amesema kuwa ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya mradi huo kwa kufikia kiwango cha asilimia 42 ya mradi huo ambapo mradi huo ulitegemewa ukabidhiwe mwezi Oktoba mwaka huu 2018. Amefafanua kuwa ilibidi  mradi huo ufanyiwe maboresho ili kuendana na matakwa ya mradi ili uweze kubeba mizigo mizito na utakamilika mwezi Juni mwakani, 2019. 
Pia, ameongeza kuwa, ili kuweza kwenda sambasamba na muda wa mkataba wa mradi huo, ujenzi wa gati namba moja ulikuwa unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu, 2018 badala ya mwezi Aprili mwakani 2019, “hivyo tuko ndani ya muda wa mkataba,” amesema Nditiye.
Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Karim Mataka amemweleza Nditiye kuwa maendeleo ya mradi ni mazuri japo walikumbana na changamoto ya kukukutana na udongo laini baharini kwenye eneo la ujenzi wa mradi huo ambapo iliwalazimu kuimarisha eneo hilo ili bandari iweze kubeba mzigo wa kontena mpaka tano zikiwa zimepandana kutokea chini kwenye eneo la kupakia na kupakua mizigo
Mataka ameongeza kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania imejipanga ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ndani ya kipindi cha miezi 36 kuendana na matakwa ya mkataba wa mradi huo ambao ulianza rasmi tarehe moja Julai mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020. Mataka amesema kuwa mradi huo unagharimu jumla ya shilingi bilioni 336 na unajengwa na mkandarasi wa kampuni ya kutoka China ya CHEC (LYU wei)
Amefafanua kuwa mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo, utaiwezesha bandari kuhudumia meli kubwa zaidi ambapo hivi sasa hamna kina cha mita 12 ambapo inazifanya meli nyingi kuwa kwenye foleni na kulazimika kusogeza meli moja moja ambapo mradi huu ukikamilika, bandari itakuwa na uwezo wa kushusha mizigo ya kutoka kweye meli kubwa saba kwa wakati mmoja
 Naibu Waziri wa Uchukzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha sehemu ya kupakia na kupakua mizigo wakati wa ziara yake kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Karim Mataka.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Karim Mataka (aliyenyoosha mkono) kuhusu maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo wakati wa ziara yake kwenye bandari ya Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Karim Mataka (wa kwanza kulia) kuhusu utengenezaji wa zege maalumu kwa ajili ya kujengea magati ya bandari wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Picha ya muonekano wa maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo bandarini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani)  kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

DC Uyui Atoa Mkono wa Pole kwa wananchi waliathiriwa na Uvamizi wa Tembo

$
0
0
Na Mwandishi wetu- Uyui
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya amewatembealea na kuwapa pole wananchi walioathirika na uvamizi wa Tembo katika Kijiji cha SawMill Kata ya Migiri.
Akizungumza  na wananchi hao mara baada ya kuwatembelea na kuwafariji amesema kuwa ameshawaagiza Askari wanyamapori kufika katika kijiji hicho na kuwaondosha tembo hao ili wasiendele kuleta madhara katika eneo hilo ikiwemo kuharibu mali na kudhuru wananchi .
“Jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama na wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kama kawaida ndio maana nimewaagiza askari wanyamapori kufika hapa mara moja na kuwaondosha tembo hawa” ; Alisisitiza Msuya
Akifafanua amesema kuwa tembo hao ambao idadi yao haikufahamika waliingia katika kijiji hicho na kuanza kuharibu mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao katika vihenge.
Pia aliwataka wananchi katika maeneo hayo kuishi kwa tahadhari kwa kutoa taarifa haraka pale watakapoona wanyama hao wameingia katika makazi yao ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa  haraka kuepusha maafa.
Tembo hao ambao idadi yao haikufahamika mara moja walivamia makazi ya watu usiku wa kumakia tarehe 15 Oktoba na kusababisha uharibifu wa wa mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift  Msuya  akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa wananchi walioathirika na uvamizi wa tembo katika kijiji  SawMill Kata ya Migiri Wilayani humo.  (Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui)

VITUKO, MALUMBANO VYAKWAMISHA UCHAGUZI NAIBU MEYA JIJI LA DAR

$
0
0

Na Said Mwishehe, Glogu ya jamii

UCHAGUZI wa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam umeshindwa kufanyika kutokana na sabababu mbalimbali ikiwemo ya mvutano wa pande mbili kati ya wajumbe wanaoshiriki uchaguzi huo wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na wa vyama vya upinzani.

Wajumbe wa uchaguzi huo ni madiwani na wabunge wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo baada ya mvutano mrefu ulioanza tangu ajenda ya uchaguzi ilipowasilishwa mezani na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Spora Liana.Mwenyekiti wa uchaguzi huo alikuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.

Mchakato wa uchaguzi huo ulianzaa saa nne asubuhi na kuendelea hadi saa nane mchana.Baada ya malumbano ya muda wote huo ilitolewa hoja ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo.Mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jisnia,Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile alitoa hoja ya kuahirishwa uchaguzi huo.

"Mheshimiwa Mwenyekiti na Mkurugenzi pamoja na wajumbe wengine naomba busara itumike...tuahirishe uchaguzi huu hadi siku nyingine.Kwa namna hali ilivyo leo hii hatutafanikiwa.Kila upande utataka kushinda na matokeo yake hatutafika mwisho.Hivyo tuahirishe," amesema 

Dk.Ndugulile wakati anatoa hoja hiyo.Baada ya kuiwasilisha wajumbe waliiunga mkono hoja hiyo.Hivyo uchaguzi huo umeahirishwa hadi hapo utajapotangazwa tena.

KABLA UCHAGUZI KUAHIRISHWA
Baada ya wajumbe wenye sifa ya kushiriki uchaguzi huo wapatao 23 kuingia ukumbini dalili za malumbano zilianza kuonekana mapema kutoka kwa baadhi ya wajumbe ambao ni madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Madiwani wa CCM na wa upinzani ambao ni Chadema na CUF walikuwa wakishindana kwa hoja.Kuna wakati utulivu uliotoweka na kusababisha kelele kuibuka mara kwa mara kiasi cha Mwenyekiti wa uchaguzi kutumia rungu lake kutuliza madiwani.

Mjadala mkali uliibuka baada ya Mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuwa uchaguzi huo kuna jina moja la mgombea wa nafasi ya Naibu Meya ambaye ni wa CCM Mariam Rulida.Mkurugenzi hiyo wa Jiji hilo alisema jina la mgombea wa CUF liliondolewa baada ya aliyekuwa anagombea nafasi hiyo kujiuzulu nafasi zake zote na kisha kujiunga CCM.

Hata hivyo baada ya majibizano ya muda mrefu walikubaliana haina tatizo uchaguzi ufanyike.Baada ya kukubaliana ikaibuka hoja nyingine iliyowasilishwa na madiwani wa upinzani kwa kutaka kuwe na kura ya ndio na kura ya hapana.

Eneo hilo nalo liliibua utata baada ya madiwani kutaka upigaji wa kura ufanyike mbele ya wajumbe na watakaopiga kura ya hapana wawe na wakala wao na wale watakaopiga kura ya ndio nao wawe na wakala.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Jiji ambaye ndio msimamizi wa uchaguzi huo alisema kura ni siri ya mpiga kura na hivyo lazima utaratibu 
ufuatwe.Hivyo kukaibuka malumbano yaliyochukua muda mrefu.

Madiwani wa upinzani wao walitaka kura isiwe siri kwani kwa idadi yao inatosha kupiga kura ya hapana.Pia hoja nyingine ni 
muongozo wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya uliodaiwa ni wa Wizara uliowasilishwa na ya wajumbe wa upinzani.Muongozo huo nao uliiibua utata mkubwa huku baadhi ya wajumbe wakionesha kutokuwa na imani nao kwa kuwa haukutolewa na Mkurugenzi wa Jiji

Hata hivyo kwa namna ambavyo malumbano hayo yalitawala na wapinzani kuonesha hawana imani na Mkurugenzi wa Jiji ,hali hiyo nayo iliyozidisha mjadala kwa pande zote mbili.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images