Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

WAFANYABIASHARA HAPA NCHINI WAMECHANGAMKIA FURSA YA KWENDA KUSOMA NA KUTAFUTA MASOKO NCHINI CHINA.

$
0
0
Na Agness Francis,blogu ya Jamii.
Katika kuendeleza Tanzania ya viwanda wafanyabiashara wa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini   wamejitokeza kwa ajili ya kusafiri nchini China kwa lengo kujifunza mbinu za kufanya biashara  pamoja  kutafuta masoko.

Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki dkt Damas  Ndumbalo amezungumza na wafanyabiashara hao wakati wa mkutano Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwapongeza kwa kutaka kuleta maendeleo ya nchi kwa kujituma kutafuta masoko nchi za nje  pamoja na kujifunza namna ya kuanzisha  na  kuendesha viwanda kwa ujumla.

"Njia ya kujikwamua kiuchumi  hapa nchini ni kuwa na viwanda pamoja na kuwekeza nguvu  katika kilimo ambacho malighafi nyingi hupatikana humo,tukasake masoko, teknolojia ya viwanda ambazo zinatumia malighafi zetu za ndani"amesema dkt Ndumbalo.

Aidha mratibu wa safari ya china kushirikiana na BBIC Godwin Msigwa amewapongeza wafanyabiashara na wakulima hao wenye nia ya kutaka kujifunza pamoja na kutafuta masoko nchini humo ambayo ni nchi iliyoendelea kiuchumi hapa duniani.
 Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbalo akiwa anazungumza na wafanyabiashara na wakulima kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini wanaosafiri kuelekea nchini China kujifunza mbinu za kufanya biashara pamoja na kutafuta masoko,Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka kutokukata tamaa na waongeze nguvu katika kuleta naendeleo katika kuelekea Tanzania ya viwanda.
 Meneja Mkuu kampuni ya BBIC Zhu Huojian  akitoa mafunzo kwa wafanyabiasha na wakulima hao kuhusu mbinu za kufanya biashara  na kukuza viwanda,Jijini Dar es Salaam.
 Naibu waziri wizara ya mambo ya nje na ushirukiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbalo,akizungumza Jijini Dar es Salaam  na wafanyabiashara wanaosafiri kuelekea nchini China kujifunza namna jinsi uendeshwaji wa biashara unavyokuwa nchini humo pamoja na kutafuta masoko.
Naibu waziri wa wizara ya mambo ya nje na uhusiano wa Afrika Mashariki Damas Ndumbalo akiwa katika picha ya pamoja Jijini Dar es Salaam  na wafanyabiashara wanaosafiri kuelekea nchini China kwa ajili ya mafunzo zaidi ya kibaishara na kutafuta masoko ili kukuza uchumi wa nchi yetu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NEC YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Tarehe mbili Desemba (Desemba 2, 2018) kuwa siku ya Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Simanjiro, Serengeti na kata 21 za Tanzania Bara.

Akitoa taarifa kwa umma Jijini Dar es Salaam  leo (Jumatatu Oktoba 15, 2018), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage amesema fomu za Uteuzi  wa  Wagombea zitatolewa kati ya  tarehe 28 Oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.

“Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 03 Novemba mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 04 Novemba hadi tarehe 01 Desemba mwaka huu na siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 2 Desemba, mwaka huu,” Jaji Kaijage amesema.

Mwenyekiti huyo wa Tume amesema kwamba Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Majimbo mawili (2), Jimbo la Serengeti lililopo Halmashauri ya Serengeti Mkoani Mara na Jimbo la Simanjiro katika Halmashauri ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Jaji Kaijage alisema kwamba barua hiyo imepokelewa kufuatia Wabunge wa Majimbo hayo Waheshimiwa Marwa Ryoba Chacha,  na James Ole Millya kujiuzulu na kutoka  kwenye Chama vyama vyao vya awali.

Amesema Tume pia imepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 21 za Tanzania Bara.   Nafasi hizo wazi zimetokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kujiuzulu.

“Tunapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo,” alisema.

Kata zenye uchaguzi nah almashauri zao kwenye mabano ni pamoja na Ilboru, Mlanfarini na Oldonyosambu (Wilaya ya Arusha), Engutoto na Olasiti (Manispaa ya Arusha), Hazina (Manispaa ya Dodoma), Chinugulu (Wilaya ya Chamwino), Kasharu, Nyakimbili, Kishongo (Wilaya ya Bukoba), Chonyonyo, Ihanda (Wilaya ya Karagwe).

Nyingine ni pamoja na Muhindawa, Mnanila (Wilaya ya Buhigwe), Mnerongongo (Wilaya ya Nachingwea) Ngarenairobi (Wilaya ya Siha), Kyanyari (Wilaya ya Butiama), Namilembe (Wilaya ya Ukerewe), Lukanga, Beta (Wilaya ya Mkuranga) na Chikola (Wilaya ya Manyoni)

NEEC kuwawezesha kiuchumi walioacha matumizi dawa za kulevya

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA harakati za kutaka kuokoa nguvu kazi ya vijana walioathirika na madawa ya kulevya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kuchumi (NEEC) limepanga kuandaa program kabambe ya kuwawezesha kwa waliokubali kuachana na matumizi ya madawa hayo baada ya kupata tiba kutoka vituo vya tiba ili wakazalishe mali.

Mwenyekiti wa baraza hilo Dkt. Festus Limbu amesema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma wakati wa kikao na vijana waliokuwa wanatumia dawa hizo na ambao wanapata tiba katika vituo vya Hospitali ya Muhimbili, Temeke na Mwananyamala, kuwa baraza limejipanga kuwaletea program ya uwezeshaji ili waweze kujiletea maendeleo.

“Baraza limejipanga kuokoa kundi lenu hasa kwa wale waliokubali kuachana matumizi ya madawa ya kulevya na waopata tiba katika vituo mbalimbali nchini,” uwezeshaji unaolengwa ni wa kupata ardhi, mafunzo, mitaji na masoko, aliongeza kusema, Dkt Limbu.

Alisema uwezeshaji huo utawafikia baada ya kuwachambua kulingana na shughuli wanazoweza kufanya kupitia vikundi ambavyo vitaundwa ili kutoa fursa ya kuwawezesha kwa karibu zaidi.
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Dkt. Festus Limbu wa pili kushoto akisistiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na vijana wanaopata tiba ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya wa Vituo vya Hospitali ya Muhimbili, Temeke na Mwanyanyamala, wa tatu kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’I Issa, wa pili kulia ni Mjumbe wa baraza hilo, Bi. Dkt. Astronaut Bagile, kushoto Kamishina wa Kinga na Tiba Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya na kulia afisa toka baraza hilo, Bw. Jozaka Bukuku.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC),Dkt.Festus Limbu kushoto akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na vijana wanaopata tiba ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya katika Vituo vya Hospitali ya Muhimbili, Temeke na Mwananyamala wengine ni vijana hao.

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB AKUTANA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI

$
0
0
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kulia) akiukaribisha Ubalozini hapo ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nshekela (kushoto), Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa waliomtembelea Ofisini kwake, jijini Dar es salaam Oktoba 15, 2018. Ujumbe huo ulifika ubalozini hapo kwa utambulisho rasmi wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB baada ya kuchukua nafasi hiyo hivi karibuni. Denmark ni sehemu ya wanahisa wakubwa wa Benki ya CRDB.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (wa pili kushoto) akizungumza na ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nshekela (kushoto), Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa, walipokutana kwa mazungumzo kwenye Ofisi za Ubalozi, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nshekela (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati akizungumza na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (kulia), alipomtembelea Ofisini kwake, jijini Dar es salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa. kulia kwa Balozi ni Meneja Mipango kitengo cha Biashara wa Ubalozi huo, Ihunyo Boniface Nzogere.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nshekela, wakimsikiliza Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen, walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake, jijini Dar es salaam.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nshekela (kushoto) wakati walipokuwa wakizungumza baada ya kukutana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Denmark, jijini Dar es salaam Oktoba 15, 2018.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UGAWAJI VIWANJA 'PANDIKIZI'

$
0
0
Na Munir Shemweta, Musoma
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumbà na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amepiga marufuku ugawaji viwanja ambayo tayari vimemilikishwa huku wamiliki wake wa awali wakitafutiwa eneo lingine.

Hatua hiyo inafutia kushamiri kwa tabia iliyozueleka kwa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri kugawa maeneo ambayo tayari yana wamiliki wake kwa watu wengine wenye uwezo na baadaye kuwaahidi wamiliki halali kuwapatia kiwanja kingine.

Mhe Mabula alitoa kauli hiyo wilayani Musoma mkoa wa Mara mwishoni mwa wiki alipokutana na watendaji wa sekta ya ardhi katika Manispaa ya Musoma pamoja na halmashauri za wilaya za Musoma na Butiama wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya februari mwaka 2018.

"Kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri kugawa viwanja 'pandikizi' katika maeneo ambayo tayari yameshamilikishwa kwa mananchi kwani suala hili limekuwa likileta migogoro mikubwa katika sekta ya ardhi" alisema Mabila.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akikagua majalada katika ofisi ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akitoa maelekezo kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Simiyu Godwin Tumaini mara baada ya kukagua majalada na mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi katika halmashauri ya walaya ya Rorya mkoani Mara.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akizungumza na wanakikundi wa Boma la Masai katika wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wana kikundi wa Boma la Masai katika Wilaya ya Serengeti alipopita katika Boma hilo wakati wa ziara yake mkoani Mara mwishoni mwa wiki.
(PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

DKT TIZEBA AAGIZA WATAALAMU WA TUME YA UMWAGILIAJI KUZURU IRINGA KUKAGUA MFEREJI WA UMWAGILIAJI

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Iringa
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba amewaagiza wataalamu wa umwagiliaji kuzuru Tarafa ya Pawaga ili kutembelea na kukagua mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga ili kuanzisha skimu ya umwagiliaji.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo Jana tarehe 13 Octoba 2018 wakati alipotembela eneo la mashamba ya mpunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini.

Alisema kuwa mfereji huo unaohudumia wakulima wa mpunga katika vijiji vya mboliboli, Usolanga, Mbugani na Mkumbwani unapaswa kuwekewa mkakati wa haraka ili kujengwa skimu ya umwagiliaji kwa ajili ya mashamba ya wakulima yanayotajwa kuwa na ukubwa wa hekari 11,000.

"Kwa bahati nzuri Tume ya umwagiliaji sasa rasmi imehamishiwa kwangu haina hata siku tano nitawasimamia kweli kweli ili kuwa na matokeo makubwa na ya haraka kwenye kilimo ambacho ndicho mkombozi wa mkulima" Alikaririwa Dkt Tizeba

Aidha, aliwashauri wakulima katika Tarafa hiyo ya Pawaga kuingia katika kilimo cha pamoja ili pindi wanapovuna waweza kuuza kwa pamoja jambo litakalowafanya kuwa na maamuzi ya kupanga bei waitakayo ya Mazao.

Waziri Tizeba ameitaka Tume ya umwagiliaji kufanya uhakiki wa maeneo yote ya mashamba hayo ya wakulima kwa kuyapima kabla ya kuingia katika kilimo cha pamoja ikiwa ni pamoja na kuainisha gharama za ukamilifu wa mfereji huo wa Mkombozi na Mboliboli.

Alisema kuwa faida ya kulima kwa pamoja wakulima wanapata fursa ya kukopeshwa kirahisi na Mabenki kuliko kufanya kuomba mkopo kwa mkulima mmoja mmoja kwani masharti yake yanakuwa magumu zaidi. 

Kadhalika, Waziri Tizeba amemuagiza Mshauri wa Kilimo wa Mkoa wa Iringa Bi Grace Macha kuanisha uhitaji wa mbegu katika Mkoa huo ili taarifa zitolewe haraka kwa Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA) ili waweze kutoa mbegu punde msimu unapoanza.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa kwa ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya mpunga katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini Jana tarehe 12 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashamba ya mpunga alipotembelea Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini jana tarehe 12 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea kuelekea msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019.

UMUHIMU WA MBOLEA NI PALE INAPOMFIKIA MKULIMA SHAMBANI SIO KUWA GHALANI-DKT TIZEBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Iringa
SERIKALI imesema itahakikisha mbolea inawafikia wakulima kwa wakati kabla ya kuanza msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19 kwani umuhimu wa mbolea ni pale inapowafikia wakulima shambani sio kuhifadhiwa ghalani.

Katika msimu ujao Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbolea na pembejeo nyingine katika maeneo yao wakati wote wanapohitaji ili kuondoa adha ya muda mrefu ya mbolea kuchelewa kuwafikia wakulima kwa wakati.

Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Octoba 2018 wakati akizungumza na wanachama wa chama cha Tuungane wakulima Interpises akiwa katika ziara ya kikazi kata ya Itunundu Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini.

Dkt. Tizeba amesema kuwa ili kuboresha usambazaji wa pembejeo kwa wakulima katika msimu wa mwaka 2017/2018 mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system- BPS) umeongeza upatikanaji wa mbolea kwa wingi, bei nafuu na wakati.

Aidha, kwa kutumia utaratibu huo bei za mbolea aina ya DAP na UREA zimepungua kwa wastani wa asilimia 30.

Akifafanua zaidi, Dkt Tizeba alisema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na pindi ukiukwaji wa bei elekezi unapobainika hatua stahiki zinachukuliwa kwa wahusika.

” Endapo kama kuna mtu atapandisha gharama za mbolea kwa kupandisha bei maradufu zaidi ya bei elekezi serikali itamchukulia hatua haraka za kisheria atakayebainika ” Alikaririwa Dkt Tizeba

Katika kuimarisha sekta ya kilimo serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuimarisha kilimo kwa kuwekeza katika pembejeo, mbolea na zana zinazoweza kuikuza sekta ya kilimo ili iweze kuchochea uchumi wa viwanda.

Kadhalika, Waziri Tizeba amewatoa hofu wakulima nchini kuwa kuna akiba ya mboleaya awali isiyopungua Tani 80,000 kwa ajili ya kupandia.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua Ghala la kuhifadhi mpunga la Tuungane Wakulima Inteprises wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashine ya kukoboa mpunga ya Chama cha Tuungane Wakulima Inteprises wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini leo tarehe 12 Octoba 2018.

NAIBU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA ATAK WANAOPINGA MUUNGANO WASHTAKIWE KAMA WAHAINI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed ametaka kutungwa kwa sharia Maalum kwa watu watakaobeza Muungano kutajwa kuwa ni wahaini.


Ahmed Amesema hay oleo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akichangia Mada katika kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililobebwa na Mada ya ‘Falsafa ya Mwalimu Nyerere juu ya Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda Tanzania’.

“mimi ninachoomba tuvutane tu ila tuwandalie mstakabali mzuri hao wanakuja nyuma yetu na tuwajenge hawa kwa mazuri nimeguswa kidogo na katibu wa baba wa Taifa pale alipouliza nyie vipi huko katika vyama vya siasa nimekuwa nashangaa sana wanasiasa awajui kupambanua kipi cha kubeza na kipi sio cha kubeza”


Ahmed amesema kuwa kuna tatizo la kisheria katika mfumo wa kuongoza hivi vyama kwani wanasiasa ndio wamekuwa kipaumbele kuhoji muungano jambo ambalo linafanywa kwa utashi wa kulenga kupata kura tu.


Amesema ifike wakati wakusema kuwa mtu akigusa Muungano ni uhaini sio kwa kumgusa Rais Peke yake kwani wanfanya hivi kwa kutaka kupata umaharufu wa kisiasa.


Amesema ifike mahali ni sharia kufata fikra za Mwalimu kwani anayekiuka hizo atakuwa ametenda kosa kubwa la jinai kwani tukiacha uhuru tutaendelea kudanganyana siku hadi siku.

Alimaliza kwa kusema kuwa leo amekuja Rais Dk John Magufuli anasimamia haya lakini ipo siku atakuja kiongozi atayaaopuuza haya anayofanya kisha taifa hili litapromoka kwa kiwango cha ajabu nakupoteza nguvu yote hii.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa mada ya Umuhimu wa Taifa huru na uhuru wa Wananchi katika kukuza uchumi wa Viwanda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigambboni Sarah Msafiri akizungumza kuhitimishaKongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.
Picha ya Washiriki wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.

MSIMU MPYA WA VICHEKESHO VYA MWANTUMU KUANZA KESHO

$
0
0
Msimu mpya wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo huonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo unaanza rasmi Jumanne Oktoba 16, huku vikiwa vimeongezewa manjonjo ili kuwahakikishia watazamaji na mashabiki wake burudani isiyo na upinzani.

Vichekesho hivyo vinavyoongozwa na mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile maarufu kwa jina la kisanii JOTI ambaye kwenye vichekesho hiviamevaa uhusika wa watu watatu tofauti; Mzee Mrisho, Kaboba na Mwantumu Sahare, vimekuwa ni moja wa vipindi vinavyotazamwa sana nakupendwa na maelfu ya watu hapa nchini ambapo huonyeshwa kupitia chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo – DStv 160. Majina maarufu pia katikatasnia ya uigizaji na uchekeshaji yatakuwepo msimu huu akiwemo Mzee Fungafunga (Mzee Mwalubadu), Mama Abduli (Mwantumu Mcharuko), AlexWasponga(Kayombo) na wengineo wengi


Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa vichekesho hivyo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwatangu kuanza kwa msimu wa kwanza wa vichekesho vya Mwantumu mnamo Oktoba 2017, vichekesho hivyo vimekuwa na msisimko wa aina yake navimepokelewa vizuri sana na watazamaji na hivyo kuvifanya kuwa na mashabiki wengi sana.

Amesema msimu huu wa pili watazamaji wa Maisha magic Bongo na mashabiki wa Mwantumu watashuhudia mikasa ya aina yake ambapo baada ya Bahati kupata ujauzito, baba yake mzee Mwalubadu anaamua kumpeleka Kaboba katika vyombo vya sheria kwa kosa la kumpa Bahati ujauzito. Hatahivyo suala hilo linafika kwa Babu yake Kaboba mzee Mrisho, ambaye wakati huohuo hataki Kaboba apate matatizo yoyote. Kinachotokea hapo nidrama ya aina yake itakayowaacha watanzamaji wakivunjika mbavu kwa kucheka.


Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo vitakuwa vinaonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo.
Mzalishaji wa vipindi Rakim Mohamed akizungumza jinsi walivyoweza kuzalisha vipindi hivyo vya kuchekesha vya Mwantumu wakati wa uzinduzi mpya wa Vichekesho hivyo.
Mchekeshaji maarufu nchini Lucas Mhuvile "JOTI" akizungumza wakati wa uzinduzi wa vichekesho vyao vya Mwantumu ambavyo vitakuwa vinaonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ASASI ZA KIRAIA WAFUNDWA KUHUSU MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imezitaka Asasi za Kiraia (Azaki) kuwa mabalozi wa maadili ya viongozi wa umma na utawala bora ili kujenga jamii yenye maadili.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa mafunzo kwa Asasi za Kiraia (Azaki) Katibu wa Usimamizi wa Maadili wa Sekretarieti hiyo, John Kaole, amesema lengo la mafunzo hayo ni kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu na kazi zinazofanywa na sekretarieti hiyo pamoja na masharti ya maadili ambayo viongozi wa umma wanapaswa kiyazingatia.

"Matarajio yetu kuwa mafunzo haya yatawawezesha kushiriki vyema katika kutoa elimu ya maadili na utawala bora kwa wadau wenu na wananchi katika kujenga jamii yenye maadili na ambayo haivumilii kamwe vitendo vya utovu wa maadili miongoni mwetu.

Amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa asasi za kiraia katika kuchangia maendeleo endelevu na kukiri kuwa kupitia mwongozo kuhusu ushirikishwaji wenye ufanisi kati ya Serikali na Azaki wa mwaka 2010, ambao umejikita katika kukuza uelewa na kubadilishana uzoefu kama tunavyofanya katika mafunzo haya.

"Ni matumaini yangu kuwa tutatumia maudhui ya mwongozo huo kutoa maoni na ushauri wenye tija kuhusu namna bora ya kukuza na kusimamia maadili ya viongozi nchini" amesema Kaole.

Ameongoza kuwa uadilifu ni nyenzo muhimu ya kukuza utawala bora nchini licha ya kazi ya usimamizi wa uadilifu na kukuza maadili miongoni mwa jamii ni ngumu na yenye changamoto nyingi.

"Lakini iwapo sisi asote tutashirikiana kwa pamoja tunaweza kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye kupunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya mmomonyoko wa maadili nchini" amesema Kaole.
Katibu idara ya ukuzaji wa maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Waziri Kipacha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua semina ya kuwajengea uelewa wafanyakazi wa asasi za kiraia hapa nchini kuhusu ukuzaji na usimamiaji maadili ya viongozi wa umma ili waweze kujihuwisha na masuala yanayohusisha na maadili ya uongozi kwenye kwenye programu za kutoa elimu kwa wadau wao na wananchi kwa ujumla.
John Kaole akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunguliwa semina ya maadili ya kuwajengea uelewa kwa wafanyakazi wa sekta za kiraia jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wa asasi za kiraia wakiwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa asasi za kiraia jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa asasi za kiraia mara baada ya kufungua semina ya mafunzo kwa wafanyakazi wa asasi za kiraia jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

Kanye West ampa zawadi Rais Museveni alipomtembelea Ikulu

$
0
0
Mapema leo hii rapa Kanye West na Mkewe Kim Kardashian walipomtembelea Ikulu ya Uganda katika jiji la Entebbe ambapo walikutana na Rais Yoweri Museveni na kufanya mazungumzo ya masuala kadhaa kuhusiana na sanaa pamoja na utalii
Rapa  wa Marekani Kanye West(kushoto) akisaini viatu aina ya Yeezy alivyopewa rais wa UgandaYoweri Museveni(kulia) alipomtembelea Ikulu jijini Entebbe leo.
 Rais wa UgandaYoweri Museveni(kulia) akipeana mikono na Rapa wa Marekani Kanye West(kushoto)mara baada ya kupewa zawadi ya viatu vya Yeezy alipomtembelea Ikulu jijini Entebbe leo.
Rais wa UgandaYoweri Museveni(kulia) akimsindikiza mgeni wake Rapa wa Marekani Kanye West(katikati) pamoja na mke wake Kim Kardashian (kushoto) mara baada ya kutembelewa  Ikulu jijini Entebbe leo.

Wasanii Rukwa waomba uwekezaji kwenye utayarishaji wa “Audio” na “Video”

$
0
0
WASANII wa fani mbalimbali mjini Sumbawanga, Mkoani Rukwa wameeleza kilio chao juu ya utayarishaji mbovu wa sauti za muziki na picha za video unaofanywa na watayarishaji waliopo ndani ya mkoa na kuwaomba wadau wa sanaa kutoka katika mikoa iliyoendelea katika fani hiyo kuja kuwekeza ili waweze kuleta ushindani katika sanaa.
Kilio hicho kimetolewa baada ya Afisa utamaduni wa Manispaa ya Sumbawanga, Charles Kiheka, kuwaita wasanii hao wa fani mbalimbali ili kujua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo pamoja kuwaelimisha miongozo na taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa ili kutokiuka taratibu za kiserikali katika kufanya shughuli zao za sanaa.
Mmoja wa wasanii wa Hip-hop, Martin Gondwe amesema kuwa ‘studio’ zilizopo zimekosa vifaa vizuri vitakavyomwezesha msanii aliyerekodi nyimbo yake mjini Sumbawanga kuweza kuleta ushindani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
“Vile vile tukizungumzia upande wa “video”, wasanii wanakuwa wanafanya nyimbo inakuwa na “quality” (ubora) ndogo, “Audio” inakuwa ya kawaida, pamoja na “video” pia inakuwa ya kawaida yaani kila kitu kibovu, huwezi kuifikisha hiyo nyimbo yako sehemu yoyote,” Alisisitiza.
Nae Steven Stanley, msanii wa Hip-hop aliongeza kuwa kutokana na ubovu wa kazi zinazofanywa na watayarishaji wa muziki katika upande wa sauti na picha inapelekea wasanii wengi kushindwa kuwashawishi wadau wa sanaa na hatimae kukosa kusaidiwa ili kuweza kusonga mbele zaidi.
“”Video” zinakuwa ziko “local” kiasi kwamba huwezi ukamshawishi mtu anunue, kwasababu kila mtu anapenda kitu kizuri, kwahiyo mtu akiona “video” nzuri anasema hii nimeipenda na akiona kitu kibaya anasema piga chini, ila ukosefu wa “production” ndio “una-cost” kabisa, kwasababu siwezi nikarekodi nyimbo hapa ambayo “production” ipo “local” halafu nikatuma Dar,” Alibainisha.
Kwa upande wake Charles Kiheka alileza kuwa wasanii hawatakiwi kusubiri sherehe za kiserikali pekee kama fursa ya kujitangaza bali ni jukumu la msanii kuwa mbunifu katika kuandaa matamasha hayo na hatimae kuonana nae ili kuona namna ya kumsaidia katika kukamilisha mipango ya msanii aliyonayo ili kujiongezea kipato kwa kumpa vibali vyote stahiki pamoja na ushauri wa mikataba mbalimbali anayotaka kuingia na wadau wa burudani.
“Leo hii msanii anakwambia serikali iandae “event” aje “kuperform” wasanii wapo wangapi na matukio ya serikali sio ya kila siku, wewe kama mdau wa sanaa, kama msanii ni jukumu lako kuandaa matukio mbalimbali, unakuja na mipango yako ofisini tunaelekezana namna ya kufanya na kuzitafutia ufumbuzi changamoto unazoweza kukabiliana nazo,”Alisema Kiheka.
Katika juhudi za kuhakikisha wasanii hao wanajifunza namna ya kuandaa matamasha, Kiheka anatarajia kuzindua tamasha la “Amka Kijana, Onesha Kipaji Chako” litakalojumuisha mashindano ya sanaa za fani mbalimbali, kuanzia kuimba, kuigiza, ngoma za asili, pamoja na kucheza nyimbo za kisasa (ku-dance) kabla ya kuisha mwaka 2018.
 Baadhi ya wasanii mbalimbali waliokuwa wamehudhuria kwenye kikao kilichoitishwa na afisa utamaduni wa manispaa ya Sumbawanga ili kujua changamoto zinazowagusa wasanii hao pamoja na namna ya kutafuta ufumbuzi. 

RAIA WA SUDANI KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA FEDHA DUBAI

$
0
0
Raia wa Sudan Nada Zaelnoon Ahmed Elbokhary(38) aliyejifunika kitambaa chekundu akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa shtaka moja la kukutwa na fedha za Dubai kiasi cha zaidi ya milioni 120 ambazo ameshindwa kuzitolea taarifa ya fedha.

Na Karama Kenyunko, Glogu ya Jamii
RAIA wa Sudan, Nada Zaelnoon Ahmed Elbokhary(38), anayeishi Masaki jijini Dar es salaam, Leo Oktoba 15/2018 amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kukutwa na fedha za Dubai kiasi cha zaidi ya milioni 120 ambazo ameshindwa kuzitolea taarifa ya fedha.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa, mshtakiwa ametenda kosa hilo Oktoba 9, 2018 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini.
Imedaiwa, siku hiyo, mshtakiwa Elbokhary wakati akiondoka katika nchi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Sudan, alikutwa akiwa na USD 60,000 ambazo ni zaidi ya sh. milioni 120 na Sudanese pound 3410 ambazo hakuzitolewa maelezo kwa mamlaka wa forodha.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh.milioni 20.

Pia mahakama imemtaka  kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahakamani hapo

 Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 22 Mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH) kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika.

BREAKING NEWZZZZ: FAMILIA YA MO DEWJI YATANGAZA DAU LA TSHS. BILIONI MOJA

$
0
0
FAMILIA ya Mohamed Dewj imetangaza dau ya shilingi  bilioni Moja kwa mtu atakayetoa taarifa ya kupatikana kwa bilionea huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwanafamilia Azim Dewj amesema kuwa familia inashukukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka serikalini kwa jitihada zinazoendelea za kumtafuta Mo Dewji.

Azim amesema taarifa zote zifike kwa Murtaza Dewji  kupitia namba za simu 0 755030014,0717208478, 0784783228 au kupitia barua pepe findmo@metl.net.

Amesema  familia inaahidi kwamba mtoa taarifa pamoja na taarifa zitaaki kuwa kubwa baina ya mtoa taarifa na familia.

Mtendaji Mkuu Wa Makampuni ya Metl Group Mohamed Dewji alipotea mnamo alfajiri ya saa 11:35 hadi 11:40 tarehe 11 Oktoba 2018 katika Hotel ya Collesseum Mtaa wa Haile Selasie Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Familia kwa ujumla wanatoa shukrani serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na taasisi zake kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuhakikisha kwamba motto wao anapatikana.

Pia wametoa shukurani kwa vyombo vya habari kwa kazi kubwa ya kuchukua jambo hili kwa uzito mkubwa na kuwataarifu umma, mbali na hilo taasisi za kidini na zisizo za kidini na kila mmoja wenu kwa maombi na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu familia inachopitia.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU MWAKA HUU WA 2018 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama walioongozana na wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu wa 2018 alipokutana na kufanya nao mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 15, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu wa 2018 alipokutana na kufanya nao mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 15, 2018
PICHA NA IKULU

INTRODUCING DJ Boniluv Master Mix 001

SIKU TATU ZA MAONESHO YA SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO 2018 (S!TE) UKUMBI WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

$
0
0

 Ulikuwa unapoingia tu katika Maonesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2018 unapokelewa na Burudani mbalimbali yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
 Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa (aliyevaa suti ya Blue) akiwa katika banda la Maliasili na Utalii wakati wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2018, yaliyo andaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) 
 Baadhi ya wadau mbalimbali wa Utalii wakiwa katika maonesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE) 2018, yaliyo andaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
 Wadau wa Utalii wakimsikiliza Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake  wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo (S!TE), yaliyo andaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

DC ILEJE ASHANGAZA WAUMINI KWA KUINGIA NA ILANI KANISANI.

INTRODUCING "WACHANIIMBE" BY JACO BEATZ X ONE SIX

MICHUZI TV: SERIKALI YAANZA KUSHUGHULIKA NA WAKWEPA KODI KWENYE MASOKO JIJINI MBEYA

Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images