Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwa kutembelea Butiama

0
0
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walioko Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara wameungana na Watanzania kuazimisha kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama mkoani Mara.
 Wataalam hao wametembelea Kijiji cha Mwitongo ambako mwili wa Mwalimu Nyerere omehifadhiwa na kupatiwa maelezo mbalimbali kuhusu histoaria yake.
Katika maadhimisho hayo wananchi mbalimbali wamejitokeza wakiwamo wanafunzi, watalam wa afya Muhimbili na kufanyika kwa ibaada ya kumuombea Baba wa Taifa. 
 Baada ya wataalam hao kushiriki kwenye kumbukizi ya Hayati Mwalimu Nyerere leo, kesho Jumatatu (tarehe 15, 2018) wanaendelea kutoa huduma mbalimbali matibabu kwa wakazi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma. 
 Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza ambako alikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Madaktari walieleza kwamba kifo chake kilisababishwa na ugonjwa wa saratani ya damu. 
 Oktoba 14 kila mwaka imefanywa kuwa siku maalam ya kitaifa ili kutoa nafasi ya kumkumbuka na kutafakari mema na mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake.
 Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Rufaa ya Musoma wakiwa katika kaburi la Baba wa Taifa baada ya kumuombea leo ikiwa ni siku ya kumbikizi yake ambayo hufanyika Oktoba 14 kila mwaka.
 Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Rufaa Musoma na Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuelekea kwenye nyumba ambako Baba wa Taifa alikuwa akipumzika enzi za uhai wake na wakati mwingine kukutana na wageni wake.

 Wataalam wakiwa katika sebule ambako Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa akipumzika na Mama Nyerere.
Jengo la Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere.
Dkt. Brighton Mushengezi akipitia historia katika Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere yaliopo kwenye Kijiji cha Mwitongo, Butiama mkoani Mara.

Naibu Waziri Biteko Amaliza Mgogoro Mgodi wa Mable Mkoani Morogoro

Michuzi TV: ZAIDI YA WASANII 169 WAJIANDIKISHA BIMA YA AFYA YA NSSF...

WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE

0
0
WAGONJWA wa macho 379 wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wamepatiwa huduma ya vipimo na matibabu ya macho bure kwenye maadhimisho ya siku ya macho duniani.

Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu wa afya kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ‘Kilimanjaro Center for Community Opthmology ( KCCO) kupitia mradi wa (TRACHOMA SAFE) wametoa huduma ya kupima macho, ushauri, kutoa dawa sambamba na kuwapangia tarehe ya kurudi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na upasuaji wagojwa ambao wameonekana kwamba matatizo yao ya macho yanahitaji upasuaji.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt Malkiadi Paschal Mbota alisema ugonjwa wa Trakoma ni tatizo kubwa na idara ya Afya kwa kushirikiana na KCCO wamekuwa wakienda katika maeneo yote ya vijijini kutoa hudumaza ushauri, dawa, upasuaji, kutoa elimu juu ya umuhimu wa kusafisha uso kwa maji safi pamoja na usafi wa mazingira kwa ujumla kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo.

Dkt Mbota alitoa wito kwa jamii, hususani jamii ya kifugaji kujenga tabia ya kunawa uso kwa maji safi mara kwa mara ili kuepuka ugonjwa wa Trakoma. “Mikakati ya wilaya katika kukabiliana na ugojwa huo, kwa kushirikiana na KCCO tumekuwa tukienda kijiji hadi Kijiji kuwatambua wagonjwa na tukishawatambua, madaktari wetu na manesi wamejengewa uwezo wa kutosha kuwapatia huduma zote zinazotakiwa ikiwemo upasuaji, wanaweka mahema hukohuko vijijini wanawafanyia upasuaji,” alisema.
Mkazi wa eneo la Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, akipatiwa maelezo ya matibabu bure ya ugonjwa wa macho. 
Mganga wa macho wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, akimpima macho mkazi wa mtaa wa Kaloleni, Juma Ally. 
Mganga wa macho wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, Dk Enock Awary akimpima macho mkazi wa Kibaya, Khadija Hamis ambapo watu 379 walipatiwa vipimo na matibabu bure
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, walio na matatizo ya macho wakipewa maelezo ya namna ya kupata matibabu. 


ITV: TAARIFA YA HABARI YA SAA MBILI KAMILI USIKU OKTOBA 14, 2018

Article 7

KAMPUNI YA MZALENDO KUJENGA KIWANDA CHA PIKIPIKI ARUSHA

0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Kampuni ya kichina ya Kutengeneza vifaa vya pikipiki ililyopo Njiro Jijini Arusha hapa Nchini kimeahidi kuanza kutengeneza Pikipiki ifikapo mwaka 2020.

Akiongea wakati alipotembelewa na Kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi kata ya Themi Mkurugenzi wa kiwanda hicho,Zhang You Chin amesema mapango huo upo mbioni kukamilika kutokana na umuhimu wa mahitaji hapa nchini baada ya kuonesha mafanikio makubwa katika utengenezaji wa vifaa vya pikipiki hususani kofia Ngumu.
Amesema kiwanda hicho tangu kianzishwe mapema mwaka huu,kimeweza kuajiri Wafanyakazi wapatao 60 na wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia ajira za Wafanyakazi 200 pindi watakapofunga machine za kuunda pikipiki. Tunatengeneza kofia ngumu ambazo hazipasuki hata ikidondoka na tunauza nchi mbalimbali za Afrika zikitoka nchini Tanzania”Amesema 
Amesema hadi sasa kiwanda hicho kinazalisha kofia ngumu za pikipiki zipatazo 5000 kwa Siku na vifaa vingine vya pikipiki na baada ya miaka mitatu wanatarajia kutengeneza pikipiki zitakazouzwa jwa bei nafuu na hivyo kupunguza gharama ya kuagiza pikipiki kutoka Nje ya nchi. 
Awali mwenyekiti wa ccm kata ya Themi,Thomas Munis amekipongeza kiwanda hicho kwa kuanza kutengeneza kofia ngumu ambazo hazipasuki zitakazosaidia kupunguza vifo kwa ajali za pikipiki

TANESCO YAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA KUPANDA MITI ELFU KUMI (10,000)

0
0
NA SAMIA CHANDE, KILIMANJARO

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeungana na Watanzania katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kupanda miti elfu kumi (10,000) mkoani Kilimanjaro.

Sambamba na upandaji huo wa miti, TANESCO pia imetoa elimu ya uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutunza miundombinu ya Shirika hilo ambayo imekuwa ikiathiriwa mara kwa mara na Miti inayopandwa jirani na miundombinu ya umeme.

Kampeni hiyo ya upandaji miti ilizinduliwa rasmi leo Oktoba 14, 2018.na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kippi Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi katika shule ya Msingi Muungano katika Manispaa ya Mji wa Moshi.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupanda miti, Mhe.Warioba aliipongeza TANESCO kwa jitihada zake za dhati za kuungana na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro katika kutunza mazingira kwa kupanda miti katika wilaya za Moshi, Rombo, Same, Mwanga, Hai na Siha lakini pia kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba, Naibu Meya wa Manispaa ya Mji wa Moshi, Mhe. Jombo Koyi, (watatu kushoto), na Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu), Mhe. Esther Mmasi. (wane kushoto), wakiwa wamebeba miche ya miti na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Meneja wao Mhandisi Mahawa Mkaka (wasita kushoto), wakati wa zoezi la upandaji miti Mkoani humo leo Oktoba 14, 2018 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba, akifanya maandalizi ya kupanda mti leo Oktoba 14, 2018.
Meneja wa TANESCO Mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akimkabidhi zawadi ya mche wa Matunda Kaimu Mkuu wa Mkoa Kippi Warioba.


KAMARADI BASHIRU ALLY KATIBU MKUU WA CCM AONGOZA UJUMBE WA VIONGOZI WA CCM KATIKA ZIARA YA KIMKAKATI NCHINI CHINA

0
0

Ujumbe wa Viongozi wa CCM umeondoka leo kuelekea nchini China kwa ziara ya kimkakati inayolenga kuongeza mahusiano kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China (CPC), Kamaradi Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM anaongoza ujumbe huo.

Akizungumza kabla ya kuanza safari Kamaradi Bashiru ameelezea safari hiyo kwamba ni ya kimkakati na inalenga kuimarisha mahusiano kati ya CCM na CPC. Aidha amesisitiza safari hiyo pamoja na mambo mengine ujumbe wa viongozi hao utakwenda kubadilisha uelewa, uzoefu na kujifunza mikakati ya kujitegemea kirasilimali ili kuendesha Chama, namna bora na bunifu ya kuendesha Miji na Majiji nchini na namna bora ya kujenga mahusiano kati ya Chama na Serikali katika kutoa maendeleo kwa watu.

Ujumbe wa Chama Cha Mapinduzi umejumuisha kwa uwakilishi viongozi wa Chama Taifa ikiwamo wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Jumuia za Chama, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Wajumbe wa Bodi za Kampuni za Chama na Maafisa wa Chama kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu. Chama Cha Mapinduzi katika ujumbe huu kimejumuisha maafisa wawili wa Serikali ili nao wakajifunze kama sehemu ya ujumbe huo.

Ujumbe wa CCM utakuwa Nchini China kwa siku 10 na utakuwa na fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali wakiangazia fursa za mashirikiano na uwekezaji kwa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Taifa.

Wakati uo huo Kamaradi Bashiru ametumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa dhati watanzania wakaazi wa Wilaya ya Liwale na Jimbo la Liwale kwa uchaguzi mzuri uliokamilika kwa Amani na usalama na kukiwa na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea wake Zuberi Kuchauka kimeibuka na ushindi wa kishindo.

Huu ni muendelezo wa mikakati ya kukuza mahusiano ya kimataifa, diplomasia ya siasa na uchumi kwa manufaa ya nchi yetu Tanzania.

Imeandaliwa na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Idara ya Itikadi na Uenezi na,

KIDUMU CHA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
 
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

RAIS DKT SHEIN AHITIMISHA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU JIJINI TANGA.

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein akipokea Mwenge wa Uhuru Kitaifa kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Nd,Charles Francis Kabeho katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika leo katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika leo katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akimsikiliza Nd,Sakum Issa Ameir katika Banda la Vijana kutoka Baraza la Vijana Zanzibar katika maonesho maalum ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika leo katika uwanja wa Tangamano Jijini Tanga,sambamba na sherehe za kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere zilizofanyika leo katika Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, [Picha na Ikulu.] 14/10/2018.
Baadhi ya wananchi wa Mkoani Tanga wakiwa katika Uwanja wa Mkwakwani katika sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika leo katika Jiji la Tanga,[Picha na Ikulu.] 14/10/2018. 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 15, 2018

KAMPUNI YA DAGE YAWANOA VIZURI WAHITIMU 200,BALOZI WA MAREKANI NCHINI ATOA UJUMBE

0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii

KAIMU balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Petterson amepongeza juhudi za wazazi ambao wamewaruhusu watoto wao kujiunga na kupata mafunzo ya ujasiriamali na kuhitimu. Ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuwa mustakabali wa maisha yao ni  juhudi zao binafsi na si Serikali, hivyo basi waione fursa na kuifanyia kazi kwani tayari wameshapata mafunzo ya kutosha.

Petterson ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema hayo jijini Dar es Salaam na kwamba changamoto zipo na ni sehemu ya maisha na kujiamini ndio silaha tosha katika kukabiliana na maisha ili kujijengea maendeleo kwa ajili ya maslahi yako binafsi na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam John Mbwana  amewatangazia rasmi wahitimu hao kuwa Serikali inashirikiana mao bega kwa bega na tayari wametoa vipaumbele vya mikopo ambayo itawasaidia kufungua miradi yao wenyewe.

Aidha, ameeleza wimbi kubwa linalowakuta wasichana wenye umri mdogo katika wilaya hiyo na kupelekea wingi wa vijana ambao hawana ajira nakua tegemezi kwa wazazi wao.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kampuni ya Dage, Genoveva Kiliba ambayo inashughulika na kutoa mafunzo kwa vijana kwa ajili ya ujasiriamali imetoa vyeti kwa wasichana  200 jijini Dar es salaam ambao wamehitimu katika nyanja mbalimbali.

Kiliba amepongeza ushirikiano ulionyeshwa baina ya wahitimu hao pamoja na familia zao ambazo zilikubali kuingia Kwenye mafunzo hayo na kuiona fursa ya kutimiza ndoto zao .

Na amesema wengi wa wasichana hao walishapoteza malengo na muelekeo wa maisha  kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa mashuleni,wazazi kukosa fedha za kuendelea na masomo pamoja na vifo vya walezi au wazazi.

Hivyo basi mafunzo waliyopatiwa ikiwemo elimu ya kujitambua,stadi za maisha,namna ya kufanya biashara zao itawasaidia kuendesha biashara zao kwa uweledi.

Aidha, mwalimu Makene ambae amehusika kwenye kutoa mafunzo amepongeza wasichana wote ambao wamethubutu na wameweza kunyanyuka upya na kuzikimbilia fursa hizo .

 Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Petterson akifungua rasmi mahafali ya wahitimu 200 ambao walimaliza mafunzo yao katika chuo cha Dage jijini Dar es salaam.
 kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Temeke JOHN MBWANA akitoa ufafanuzi juu ya serikali kuwapa kipaumbele wahitimu hao Kwenye mikopo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Dage, Geovina Kiliba akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Petterson alipotembelea baadhi ya kazi za wahitimu hao katika chuo cha Dage

TAARIFA ZA MIRADI YA MAENDELEO ZINAPASWA ZIWAFIKIE WANANCHI

0
0
Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA kuwa kuna umuhimu wa kutoa taarifa kwa wananchi zinazohusu utekekezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakizungumza katika mkutano wa kuandaa taarifa kwa wadau wa maji katika kata za Kwembe, Msigani na Kibamba, washiriki wamesema
sheria na taratibu zilizo wekwa taarifa ni muhimu ili wananchi wawe na mrejesho wa miradi inayowahusu.

Mwezeshaji wa mkutano huo ulioandaliwa na Asasi ya Pakacha na
kufadhiliwa na The Foundation For Civil Society, Bumija Moses amesema
wananchi wanaweza kuleta msukumo wa kiutendaji kwa viongozi kama
wakishirikishwa kupata taarifa za miradi inayojengwa na utekelezaji
wake.
Mkutano huo ulikutanisha wananchi na viongozi kutoka katika katika
kata tatu za Kwembe, Msigani na Kibamba.

Mkutano huo ulifanyika Ijumaa mjini Kibaha.
Diwani wa viti maalumu (Chadema) wa kata ya Msigani,mheshimiwa Vicky
Mchome amesema ushirikishwaji wa wananchi katika sehemu nyingi,
ikiwemo kata yake haupo akitoa wito kwa wananchi kupewa taarifa.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kwembe, Peter Chawala amesema wananchi
wasisubiri kushirikishwa, wana haki ya kuuliza viongozi wao ili kupata taarifa zinazowahusu.

Adam Kingu, mkazi wa Maramba Mawili amesema licha ya wananchi, wapo
pia baadhi ya viongozi ambao hawapati taarifa za utelekezaji wa miradi ya Maji.

“Unaweza kwenda kumuuliza mtendaji lakini cha kushangaza hajui bajeti
iliyotengwa au hata mradi unaotekelezwa”, amesema Kingu.
Kata za Kwembe, Msigani na Kibamba zina changamoto za upatikanaji wa
maji, hivyo kupelekea Pakacha kuunda kamati maalumu iliyowashirikisha
wananchi na kupita katika kata zote ili kujua kuna miradi ipi ya maji
iliyotengewa bajeti na hatua iliyofikia katika utekelezaji wake.

Mmoja wa mjumbe wa kamati hiyo, Almas Mohamed amesema wamepata
malalamiko mengi ya wananchi kutojua utekelezaji wa miradi ya maji
iliyopo katika kata zao.

Miongoni ya miradi hiyo ni ujenzi wa kisima cha maji cha Kibamba
kilichotengewa milioni 280 kwa utekelezaji wa kuanzia mwezi April
mwaka jana mpaka june mwaka huu na ujenzi wa tanki la maji lililopo
Kwembe Kingazi B uliotengewa milioni 55, ukiwa katika hatua za 
mwisho.

Katibu wa Pakacha, Haroun Jongo amesema serikali inafanya jitihada
kubwa kuleta maendeleo kwa wananchi, ndio maana asasi kama Pakacha
zinapata fursa ya kuelimisha wananchi.

“lengo la mkutano huo ni kuandaa taarifa kwa kuwashirikisha wananchi, baada ya kufanya upembuzi yakinifu ya miradi iliyopo.

Ufuatiliajia unafanywa kupitia Pets, amesema Jongo.
Pets ni mfumo unaowezesha ufuatiliaji matumizi ya rasilimali za umma
zinazotoka Serikali Kuu au halmashauri kwa maendeleo ya wananchi

kuanzia ngazi za mitaa hadi kata na kuendelea.
Washiriki wakiwa katika mkutano Wa kuandaa taarifa kwa wadau Wa maji

TFS YAWAKALIBISHA WATANZANIA KUTEMBELEA MISITU KUONA UMUHIMU WA IKOLOJIA

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania umetoa wito kwa watanzania kutmbelea Maeneo yaliyohifadhiwa hili kuweza kujionea namna Ekolojia na uhifadhi katika misitu hiyo ilivyo na faida kwa viumbe hai na Wanadamu.

akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog  katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam amesema kuwa watu wanpaswa kutemblea misitu hili waweze kujionea na kujifunza umuhimu wa ikolojia katika hifadhi.

"Ni vyema watu wakaja wakatembelea hifadhi ya misitu ya Amani waweze kujionea namna Misitu iliyopakana na makazi ya watu na maporoko ya maji yasikauka muda wote na kujionea maua ambayo yanaamika katika imani kuwa ndio yalitumika wakati wa kristo na watu uyafata kutoka maeneo ya mbali"amesema Mlog.

Kwa upande wakeMeneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo amewataka wadau mbalimbali kwa sasa kutembelea banda lao lililopo katika   Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam kujionea huduma zitolewazo na TFS na kujua wapi wanaweza kutmebelea kwa ajili ya mapumziko yao.

Mariamu amesema kuwa Misitu inayohifadhiwa na TFS ina mambomengi sana ambayo watu wanweza kupata  ikiwa na sehemu ya kufanyia tafiti, Mapumziko kwa wana ndoa pia wanaweza kwenda kutembelea na familia zao kwa ajili ya kuwafundisha watoto umuhimu wa uhifadhi.
 Afisa Misitu Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS),Arijanso Mlog akizungumza na Waandishi wa habari katika Maonesho ya Kimataifa ya Utalii Tanzania(SITE) Yanayoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Nchini, Mariam Kobelo akieleza huduma za kitalii zilizopo ndani ya Hifadhi za Misitu zilizo chini ya TFS.
 Wafanyakazi wa Huduma za Misitu nchini TFS, Wakiwaonyesha wadau Mazao Mbalimbali yatokanayo na misitu ambayo ni mazuri kwa ajili ya kuimarisha afya ya Mwanadamu.
Sehemu ya Mabanda ya Maonyesho yakiwa ynaonekana kwa juu katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

NAIBU KATIBU MKUU HAZINA:HAKUNA SABABU YA TASISI ZA UMMA KUFANYA VIBAYA KATIKA UNUNUZI NA UGAVI

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,Amina Khamis Shaban amesema hakuna sababu yoyote ya Tasisi za Umma kuendelea kufanya Vibaya  katika maeneo ya Ununuzi na Ugavi hili hali bodi ya usimamizi wa masula hayo ipo.

Naibu katibu Mkuu amesema hay oleo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa hotuba kwa wahitimu wa Mahafali ya tisa ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


“ninawaagiza kwa kushirikiana na tasisi zingine zinazosimamia ununuzi wa Umma kama  PPRA,GPSA,PPAA na zingine mlete mpango kazi namna mtakavyofikia tasisi za umma ili kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tuweze kutekeleza jambo hili mapema iwezekanavyo.Lengo ni kuhakikisha tunatumia rasilimali zilizopo ili kuleta Matokeo Makubwa kwa Wananchi” Amesema Naibu Katibu Mkuu.


Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi, Godfred Mbanyi  amesema bodi itaendelea na jitihada zake kuhakikisha wahitimu wa fani ya ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa stahiki ili kuweza kupenya na kuleta ushindani katika soko la ajira la ndani nan je ya nchi .


Mbanyi amesema bodi imeweza kuwatafutia fursa vijana wawili wa CPSP Na Wanafunzi bora wa somo la Procurement and Suply Audit nafasi ya ajira katika tasisi ya Kimataifa ya Nexia SJ Tanzania ambao ni Wataalamu wa Ukaguzi, Hesabu,Kodi, Ushauri wa Kibiashara nk.


Mbanyi alimaliza kwa kutoa rai kwa wahitimu wote watakaotunukiwa shahada ya juu ya fani ya ununuzi na ugavi wafanye hima kujisajili na bodi ili waweze kufanya kazi za ununuzi na ugavi kihalali na kwa mujibu wa sheria .


 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akihutibia wakati wa mahafli ya tisa ya Bodi ya Wataalmu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi , Godfred Mbanyi akitoa hotuba yake kwenye Mahafali ya tisa ya bodi hiyo.
 Wahitimu wakila kiapo cha Uadilifu na Maadili mbele ya Mgeni rasmi mara baada ya  kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akiwa katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa bodi hiyo.

Ratiba ya Kumuaga mtoto wa Mwalimu Mwakasege

0
0
Ratiba ya Kumuaga mtoto  wa Mwalimu Mwakasege  aliyefariki Alhamisi October 11 :- Mwalimu atawasili Dar leo Jumatatu, Jumanne mwili utaagwa Mbezi Beach Lutheran Church, Jumatano alfajiri ni safari kuelekea Mbeya, na Alhamisi ni mazishi Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya

Mahali ulipo msiba Msiba uko Dar kwa mdogo wake Mwalimu Mwakasege anaitwa Eng. Mwakasingila (Mzee wa kanisa wa KKKT Mbezi Beach)  Jinsi ya kufika msibani Fika hadi  Mbezi Beach Jogoo, unaingia barabara ya Karibu Art Gallery kuelekea TAG Mbezi beach kisha utaona vibao vinavyoelekeza msiba ulipo.  

Ratiba ya Jumatatu Kutakuwa na sara ya pamoja na Mwalimu Mwakasege na familia yeke yote itakayofanyikia hapa msibani itakayoanza saa moja jioni, 7pm itakayoongozwa na Askofu , Mchungaji kiongozi na watumishi wengine  Kuaga  Mwili wa marehemu utaagwa Jumanne 16 Oct kanisani KKKT Mbezi Beach Dar, kuanzia saa nane mchana (2pm)  Baada ya kuaga mwili utapelekwa airport kwa ajili ya maandalizi ya safari.  

Kusafirisha: Mwili utasafirishwa Jumatano 17 Oct kwa ndege  Mazishi:  Yatafanyika alhamisi, Tukuyu, Mbeya 18 Oktoba,2018.  

Muhtasari: Joshua amefariki ghafla baada ya  kudondoka  alhamisi tarehe 11 Oct 2018 akiwa kazini kwake World Bank Dar. Alikimbizwa Aga Khan hospital ila alifariki siku hiyo hiyo.
Mwalimu Mwakasege pichani kulia akiwa na Mtoto wake Joshua ambaye kwa sasa ni Marehemu.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

Mesen Selekta na Gutta wapagawisha Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote Mtwara

0
0
Msanii Jerry Boniface maarufu kama Mesen  Selekta akishirikiana na mdogo wake Gutta waliweza kuwapagawisha mashabiki kwa mtindo wao Singeli. Msanii huyo alidhihirisha ubora wake uliopelekea uwanja kutimka vumbi kwa nyimbo zake za Kinanda, Kanyaboya, Dab Singeli na nk.
Mji wa Mtwara ulikuwa tofauti na miji mingine kutokana na wasanii kuimba pamoja na mashabiki.

Akizungumza na waandishi wa habari Mesen Selekta alisema " Hii inanipa mzuka kwa mashabiki kuukubali muziki wangu, nimeona jinsi shangwe la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote walivyolipokea wana Mtwara".
Msanii mwingine aliyeiteka Mtwara alikuwa Farid Kubanda Fid Q aliwaamsha kwa wimbo wake Fresh, ambao aliurudia mara mbili kutokana na kiu ya mashabiki.
Kivutio kingine kilikuwa kwa MaDj  Zero na Mafuvu waliweza kupiga mziki kwa zamu kama kwa kushindana hii iliweza kuleta ladha na Vibe la aina yake kwa mashabiki.
Kila Tamasha linapopita utafutwa msanii Chipukizi kupitia shindano la kusaka vipaji vya wasanii maarufu Kama Tigo Fiesta Supa Nyota, na kwa mkoa huo msanii, Siraji Mbuta kwa jina la kisanii Mbuta The Swagx aliibuka kidedea kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali mwezi ujao.

Kwa upande wa wadhamini Kampuni ya Tigo, Meneja wa Kanda ya Pwani, John Tungaraza alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Tungaraza alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.

Walioshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Songea pia. Wengine ni wasanii wa bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.

TIketi za Tigo Fiesta 2018 – zitakuwa zinapatikana  kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika  kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Msanii Chege kutoka TMK Family akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang'wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu. 

Rock City Marathon yazidi kuwavutia washiriki wa kimataifa

0
0
Rock City Marathon yazidi kuwavutia washiriki wa kimataifa

Zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kufanyika kwa mbio za Rock City Marathon, idadi kubwa ya wanaridha wa kimataifa wameonyesha nia ya kuja nchini ili kushiriki katika mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo wanariadha walioonyesha nia ya kushiriki mbio hizo wengi wanatoka katika nchi za Ethiopia, Ghana, Afrika Kusini, Marekani, Canada, China, Rwanda, Burundi, DRC Congo huku Kenya ikiendelea kuongoza katika orodha ya mataifa ya nje yanaoleta washiriki zaidi katika mbio hizo.

“ Zikiwa zimebaki takribani wiki mbili kabla ya kufanyika kwa mbio hizo tayari zaidi wa washiriki 200 kutoka nje ya nchi wameonyesha nia ya kushiriki mbio hizi na kinachosubiriwa kwasasa ni wao tu kufuata taratibu kupitia Shirikisho la Riadha Taifa (RT). Lengo letu ni kupata washiriki zaidi ya 5000 katika msimu huu,’’ alisema Ngowi katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mapema leo.

“Ni taarifa njema kwetu kuona kwamba baada ya muda mrefu sasa si watanzania bali ulimwengu mzima umeanza kutuelewa nini tunakifanya Kanda ya Ziwa hususani katika jiji la Mwanza…ni ushindi pia kwa sekta ya utalii katika kanda hii.’’alibainisha

Kwa mujibu wa Ngowi, katika kuhakikisha kwamba mbio hizo zinalitangaza vyema jiji la Mwanza, njia ambazo zimekuwa zikitumika kwa wakimbiaji zinahusisha alama muhimu za jiji hilo ikiwemo jiwe la Bismarck lililopo kwenye fukwe ya Ziwa Victoria, makutano ya mzunguko wa samaki (The Vic Fish Roundabout), jengo la Rock City Mall pamoja na Daraja la Furahisha na hatimaye kuishia Uwanja wa CCM Kirumba.
Baadhi ya washiriki wa mbio za Rock City Marathon mwaka jana.

SHILINGI BILIONI 3/- ZATENGWA KWA AJILI YA UJENZI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

0
0

Na Mwandishi Wetu,Globu ya jamii

SHILINGI bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa  machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unatarajia kuanza  Novemba mwaka huu.

Uamuzi wa kutengwa kwa fedha hizo ni katika jitihada za kuondoa changamoto zinazoikabili machinjio hayo.

Hayo ameelezwa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam  mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega.

Ulega alifanya ziara fupi katika machinjio hiyo akiambata na viongozi wengine wa serikali wakiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Nyama, Dk wa Mifugo na Mkurugenzi Msaidizi wa  Masoko na uzalishaji toka Wizarani.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega alielezwa changamoto zinazoikabili machinjio hiyo ikiwa ni pamoja na  wafanyabiashara wa nyama kutozwa ushuru mkubwa kwa mazao ya mifugo, ukosekanaji wa  soko la uhakika la ngozi, ambapo Ulega amesema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mkakati  kabambe wa kukabiliana na changamoto hizo.

Ulega amefafanua  kwa kuanza na ujenzi wa machinjio mpya ya kisasa utakaofanyika kwa gharama hizo za fedha za Serikali.

“Wasimamizi wote wa ujenzi wa machinjio hii  nawataka muhakikishe kuwa ujenzi huu unafanyika kwa haraka na ubora ili machinjio hii iweze kuchinja ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku kwa kuwa machinjio nyingi zilizojengwa hazijazingatia suala la uchinjaji wa kuku,” amesisitiza Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati)  akiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo jana jijini  Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akikagua eneo linalotumika kuuza nyama ya Ng`ombe na Mbuzi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi (wadau) wa machinjio ya Vingunguti  kuhusu kero zao mbalimbali wazipatazo kuhusu eneo hilo la Mchinjio.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi(wadau) wa machinjio ya Vingunguti ambapo amewahakikishi serikali ya awamu ya tano ipo pamoja nao na amewaomba kulipa kodi ili kuinua uchumi wa Taifa.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega jana  katika machinjio ya vingunguti  jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa machinjio ya Vingunguti wakiendelea na kazi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

A RECORD TURNOUT FOR THE ROTARY DAR MARATHON AS IT MARKS 10 YEARS

0
0

The Rotary Dar Marathon had one of its biggest turnouts this year as it marks ten years of its existence since it was started in 2009. An estimated total of 15,000 people participated in the event which included a full marathon of 42.2km, a half marathon 21.1km, including cyclists, and a 9km and 5km family walk. This year, the Rotary Marathon was also held in Bukoba and Karagwe where over 1,400 participants ran and walked.

The Rotary Dar Marathon, considered as one of the biggest marathons in the country and a prime event in the Country’s sporting and social calendars, had participants from all walks of life, different ages and a number of professional marathon runners Kenya, Rwanda, Uganda, and Malawi. This year’s event, as has been the case in the past 9 years, was generously sponsored by various companies such as Pepsi, Ashton Media, Toyota, ALAF, Minet, Zoom Tanzania, Resolution Insurance, Clouds Media Group, Azam, Plasco, Insignia, Knight Support, Ashers Industries, Exim Bank, KLM, CSI Construction and Soft Tech.

The event kicked off in the early morning hours of Sunday as the various runners were flagged off starting with the long-distance runners 42.2 km runners, followed by the half marathon 21.1 km runners and cyclists. The route which saw runners and cyclists go through the peninsula into the heart of the city had the first runners back at The Green around 8.30am where the full marathon was dominated by professional athletes and the male winners being Samson Ntandu from Tanzania for the full marathon, followed by Peter Sule from Tanzania for the second place and thirdly Dushimukiza Thomas from Rwanda.

Winners amongst the female runners were Sara Ramadhani from Tanzania seconded by Dorcas Chesano from Kenya and thirdly Doris Fisha from Malawi.The Tanzania winning runner in the full marathon is Samson Ntandu for the men and Sara Ramadhani for the women who have won a full sponsorship to represent Tanzania in the Beirut Marathon this year, courtesy of SBC Pepsi.
Rotary Dar Marathon Patron, His Excellency the former President Al-Haj, Ali Hassan Mwinyi hands over a fully paid ticket to Beruit Marathon to the winner of Men’s 42.2km full Marathon a Tanzanian resident, Samson Ntandu during the 2018 Rotary Dar Marathon which took place at the Green grounds Oysterbay in Dar es Salaam yesterday. The runner will have the opportunity to participate in the Beirut Marathon with everything fully sponsored by Pepsi. Through this initiative, Pepsi aims to raise the profile of Tanzanian runners on the global stage.
Winner of Women’s 42.2km full Marathon a Tanzanian resident, Sara Ramadhani poses for a photo with her counterparts Dorcas Chesano (left) who emerged second and Doris Fisha (right) who emerged third in the 2018 Rotary Dar Marathon which took place at the Green grounds Oysterbay in Dar es Salaam yesterday. PHOTO COURTESY OF ROTARY DAR MARATHON.


(From Left to right) The Rotary Dar Marathon 2018 committee chair, Ms. Catherinerose Barretto, The Rotary Dar Marathon Chair of the Board, Ms. Sharmila Bhatt and SBC Tanzania’s CEO Avinash Jha wave their flags to officially start the Rotary Dar Marathon 2018 which took place yesterday during the Nyerere Day at the Green grounds Oysterbay in Dar es salaam. PHOTO COURTESY OF ROTARY DAR MARATHON.
A cross section of runners take part in the 10th edition of the 2018 Rotary Dar Marathon which takes place annually in Dar es Salaam. More than 15,000 people have turned up to participate in this year’s Marathon where the event marked its 10th anniversary in a fashionable style in Dar es Salaam yesterday. PHOTO COURTESY OF ROTARY DAR MARATHON.

Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images