Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI NA DAGAA KASENDA

0
0
Wakazi wa kata ya Mganza wilayani Chato mkoani Geita wameipongeza Serikali kwa kujenga soko la kimataifa la samaki, dagaa la kasenda  limesaidia kuzalisha Ajira mpya kwa baadhi ya wakazi mkoa huo.

Wakizungumza na na Michuzi Blog  wamesema  wamesema  kabla ya kujengwa kwa soko hilo hawakuwa na uhakika kupata  kipato kwa siku tofauti na sasa ambapo wameanza kunufaika.

Kupata vibarua vya kupakia na kuchambua dagaa.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya mganza Bw.Emanuel Mwita amesema  kupitia soko hilo wananchi ambao hawakuwa na kazi maalum sasa wamepata kazi  sokoni hapo ambazo zinawaingizia kipato cha kuendesha maisha ya familia zao. Baadhi ya wananchi  wakiwa bize kuwachambua Dagaa wasiofaa na wanaofaa kwa matumizi mbalimbali.
Baadhi ya wananchi  wakiwa bize kuwachambua Dagaa wasiofaa na wanaofaa kwa matumizi mbalimbali.
 Sehemu ya Magunia ya Dagaa yakiwa yamepangwa vyema ndani ya soko hilo tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa matumizi ya binadamu na mifugo.

 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mganza wilaya ya Chato mkoa wa Geita wakipanga magunia ya dangaa kwenye gari.(picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Wanaume kazini

TANGA UWASA YANUFAIKA NA RUZUKU YA ZAIDI YA BILIONI 1.2

0
0
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imenufaika na ruzuku ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 baada ya kutimiza masharti ya mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 3 toka katika benki ya CRDB ya utekelezaji wa huduma ya Maji safi Jijini Tanga.

Ruzuku hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani (KFW) kutokana na Mamlaka husika kutimiza vema masharti ya mkopo huo ikiwa pamoja na zoezi zima la marejesho huku likizingatiwa suala la utekelzaji wa mradi uliopewa fedha hizo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.

Alisema mkopo huo umewasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa maji hasa katika maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu yaliyochangiwa na udogo wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.“Kama nilivyoonyesha kwamba tumeongeza bomba kubwa la nchi 8 kwa ajili ya kuongeza mgawanyo wa maji kwenye eneo la Neema na kwengineko na kuwepo kwa usambazaji mkubwa kwenye maeneo hayo lakini pia tumejenga mtandao wa km 60 kwa kutumia mkopo huo na ruzuku tuliyopewa”Alisema
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akielezea mipango ya mamlaka hiyo wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly katikati akionyesha kitu ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.kulia ni Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly .

SPORTPESA WAMKABIDHI BAJAJI YAKE MAGITA MBWEGA WA KAHAMA SHINYANGA

0
0

HAKUNA kuchelewesha pale mtu anapotupia ubashiri wake na SportPesa anaingia kwenye Droo ya bajaj Re na unapopigiwa simu ya ushindi kuwa umeshinda bajaj utapelekewa mpaka ulipo bila kutoa hata shilingi.
Ni kwa wakati Mwingine Tena SportPesa inamkabidhi mshindi wa Droo ya saba ya Shinda zaidi na SportPesa bajaj yake huyu ni Magita Mbwega kutoka Kahama aliipokea timu ya ushindi ikiwa na Mzigo wake mpya wa bajaj ilioupeleka mpaka nyumbani kwake.
Mbwega anasema aliweka ubashiri wa shilingi elfu moja pekee na baada ya mechi akashinda shilingi elfu tano lakini habari njema kwake ilikuwa kupokea simu kutoka SportPesa kuwa ameshinda bajaj, Anadai kuwa wakati ameambiwa ameshinda hakuamini kabisa mpaka alipoona timu imefika nyumbani kwake.
Mshindi huyu wa droo ya Saba ambaye ni mjasiriamali wa kuuza nafaka anaeleza kuwa ili kubashiri sio lazima uwe maskini wala Tajiri bali hii ni Fursa kwa kila mtanzania.
"Unajua jambo ambalo nimejifunza tangu nimeanza kucheza na SportPesa ni kwamba mchezo huu hauchagui maskini wala tajiri mimi nina biashara yangu lakini bado kupitia ubashiri na Sportpesa ninaongeza kila siku mtaji wangu pale naposhinda ubashiri lakini mbali ya hilo leo nimeshinda bajaji naenda kuongeza tena mtaji wangu na pesa nyingine ntakayopata kupitia bajaj hii itaingia kwenye matumizi ya ujenzi wa nyumba yangu nyingine". Alisema Mbwega. 
Kwa upande wake mke wa Bwna Mbwega alisema kwake anaona kama neema Ya Mungu imewashukia kutokana na ushindi huo mkubwa kutoka SportPesa huku akiamini baadhi ya changamoto ambazo walishindwa kuzitatua kutokana labda na wingi wa majukumu zitatatuliwa na kipato kitachotokana na bajaj hiyo.
Huu ndio Mchongo wa Maana hivi sasa kwa watanzania kwani kwa kutumia simu Yeyote ya Mkononi unaweza piga *150*87# ukajisajili na SportPesa na kuanza kucheza , au unaweza kucheza kupitia tovuti yani www.sportpesa.co.tz kumbuka kuweka pesa kuanzia buku au zaidi ili uanze kucheza namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888 kumbuka kucheza mara nyingi ndio kuongeza nafasi ya kushinda bajaj.

MSICHANA INITIATIVE YAHADHIMISHA SIKU YA MSICHNA DUNIANI KWA KUWAKUTANISHA WADADA NA WAVULANA

0
0
 Muwakilishi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Eugine Shao, akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa kuhadhimisha siku ya Msichana Duniani na Malengo ya Tasisi yao katika kumlinda Mtoto wa Kike hili aweze kufikia malengo sanjari na kupata elimu.
 Mourine Richard Kutoka Tasisi ya Her Initiative akkizungumza umuhimu wa Mtoto wa kike kujiamini na kuwataka wanaume kuondoa dhana ya kuwanyanyapaa Wanawake kwa umri.
 Dada Viola akitoa mada kwa wasichana waliohudhuria kongamano katika kuhadhimisha siku ya Msichana Duniani kwa kuwataka waweze kujiamini.
 Mmoja wa wadau walioshiriki katika Kongamano la siku ya Msichana Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Nafasi Art Space jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wasichana walioshiriki katika Kongamano siku ya Msichna Duniani katika Ukumbi wa Nafasi Arts Space.
--

kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed ametaka kutungwa kwa sharia Maalum kwa watu watakaobeza Muungano kutajwa kuwa ni wahaini.
Ahmed Amesema hay oleo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akichangia Mada katika kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililobebwa na Mada ya ‘Falsafa ya Mwalimu Nyerere juu ya Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda Tanzania’.
“Mimi ninachoomba tuvutane tu ila tuwandalie mstakabali mzuri hao wanakuja nyuma yetu na tuwajenge hawa kwa mazuri nimeguswa kidogo na katibu wa baba wa Taifa pale alipouliza nyie vipi huko katika vyama vya siasa nimekuwa nashangaa sana wanasiasa awajui kupambanua kipi cha kubeza na kipi sio cha kubeza”
Ahmed amesema kuwa kuna tatizo la kisheria katika mfumo wa kuongoza hivi vyama kwani wanasiasa ndio wamekuwa kipaumbele kuhoji muungano jambo ambalo linafanywa kwa utashi wa kulenga kupata kura tu.


Amesema ifike wakati wakusema kuwa mtu akigusa Muungano ni uhaini sio kwa kumgusa Rais Peke yake kwani wanfanya hivi kwa kutaka kupata umaharufu wa kisiasa.


Amesema ifike mahali ni sharia kufata fikra za Mwalimu kwani anayekiuka hizo atakuwa ametenda kosa kubwa la jinai kwani tukiacha uhuru tutaendelea kudanganyana siku hadi siku.

Alimaliza kwa kusema kuwa leo amekuja Rais Dk John Magufuli anasimamia haya lakini ipo siku atakuja kiongozi atayaaopuuza haya anayofanya kisha taifa hili litapromoka kwa kiwango cha ajabu nakupoteza nguvu yote hii.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa mada ya Umuhimu wa Taifa huru na uhuru wa Wananchi katika kukuza uchumi wa Viwanda.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigambboni Sarah Msafiri akizungumza kuhitimishaKongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere
 CAG Mstaafu, Ludovick Utouh akichangia mada katika Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Watoa mada na Wajumbe wa Meza kuu wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Viongozi wastaafu na wadau mbalimbali wakifatilia kwa karibu Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
 Baadhi ya Washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
Picha ya Washiriki wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam
--

MADAKTARI BINGWA 14 KUTOKA SAUDI ARABIA KUWASILI NA KUWEKA KAMBI TIBA ZANZIBAR

0
0
 Na Mwandishi Maalumu, Riyadh- Saudi Arabia 
 Kundi la madaktari bingwa 14 wa hiyari kutoka nchini Saudi Arabia linatarajiwa kuwasili Zanzibar tarehe 12 Oktoba ambapo wataweka kambi ya tiba (medical camp) kwa muda wa siku 10. Madaktari hao wanatarajiwa kufanya matibabu na upasuaji katika hospitali za kisiwa cha Pemba. 
 Akizungumza katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Riyadh wakati wa hafla ya kuagana na madaktari hao, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Hemedi Mgaza, alisema kambi tiba hii ni ya tatu kufanyika Zanzibar. 
Mwezi Novemba mwaka 2016 madaktari hao walifika Zanzibar na kuweka kambi ya kwanza katika kisiwa cha Pemba Iliyojulikana kama (Surgical Caravan 1) kwa mara ya kwanza kwa mafanikio makubwa. Mwezi Oktoba 2017 pia walifanya kambi ya pili iliyojulikana (Surgical Caravan 2) katika hospitali za kisiwa cha Pemba. 
 Katika safari yao miaka miwili iliyopita madaktari hao walipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na madaktari wenyeji, ndio maana wamependelea kurejea tena mwaka huu kufanya kambi ya tatu (Surgical Caravan 3). 
 Pamoja na kutoa huduma za matibabu, madaktari hao watasafiri na dawa na vifaa tiba vya aina mbalimbali ambavyo Mwisho wa kambi watavitoa kama msaada kwenye hospitali hizo.
Viongozi wa Madaktari wa Saudi Arabia wakiwa na Balozi Hemedi Mgaza walipofika Ubalozi mjini Riyadh kuaga.

WATOTO WA KIUME WAHAMASISHWA KUWALINDA WATOTO WA KIKE

0
0
 Malikia wa Nguvu 2018,Bahati Mandoa  akizungumza na wanfunzi wa  shule ya sekondari Makumbusho  juu ya watoto wa kiume wahamasishwa kuwalinda watoto wa kike ili  kufikia malengo yao wakati wa taasisi ya Taesafo ilipokwenda shuleni hapo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Viongizo wa taasisi ya Faeso wakimkabidhi Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo,Augustino Joseph(kulia)vifaa mbalimbali kwaajili ya wanafunzu wa kidato cha nne leo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani..(picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

VOA SWAHILI: Duniani Leo October 11th, 2018


Taarifa ya Habari Kutoka TBC ONE Oktoba 11, 2018 Usiku)

CHANNEL TEN: Habari za Kitaifa 11.10.2018

Habari za UN Oktoba 11, 2018

ITV: TAARIFA YA HABARI SAA MBILI KAMILI USIKU LEO OKTOBA 11, 2018.

TOTAL KUMWAGA MAMILIONI KWA VIJANA WATAKAOSHINDA KATIKA MAWAZO YA BIASHARA

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 11.10.2018

washindi waendelea kuibuka promosheni ya “Shinda na SimAccount”

0
0
Meneja Masoko wa CRDB Micro Finance, Ariel Mkony (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufanya droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CRDB Micro Finance, Mikocheni jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini ,Abdallah Hamedi
Meneja Masoko wa CRDB Micro Finance, Ariel Mkony akiendesha droo ya tatu ya promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CRDB Micro Finance, Mikocheni jijini Dar es salaam leo.

MICHUZI TV: SHUHUDIA HAPA KILICHOMLETA SAMUEL ETO,O NCHINI

MICHUZI TV: RC MAKONDA kasema haya, utata wa mabasi ya mwendokasi (UDART)

RC MBEYA Mhe. Albert Chalamila Atembelea Gereza la kilimo Songwe na kutoa Maagizo

UZINDUZI WA MAONESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI-CHAMANANGWE KASKAZINI PEMBA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika leo katika kijiji cha  Chamanangwe Wilaya ya Wete Mkoa  wa Kaskazini Pemba (kulia) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Rashid Ali Juma
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe za uzinduzi wa maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika leo katika kijiji cha  Chamanangwe Wilaya ya Wete Mkoa  wa Kaskazini Pemba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) alipokuwa akimkabidhi zana za Kilimo kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Bw.Hamad Othman Sheik wa Koowe  katika sherehe za maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika leo katika kijiji cha  Chamanangwe Wilaya ya Wete Mkoa  wa Kaskazini Pemba
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akivuna mahindi katika shamba la mfano   katika sherehe za maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika leo katika kijiji cha  Chamanangwe Wilaya ya Wete Mkoa  wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (wa pili kushoto)akiwa na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Rashid Ali Juma (kushoto) pamoja na Viongozi mbali mbali  wakiangalia Viazi vitamu wakati alipotembelea aina ya Vilimo mbali mbali na Ufugaji katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika leo  katika viwanja vya Chamanangwe Wilaya ya Wete Mkoa  wa Kaskazini Pemba. Picha na Ikulu

MOTO HAUZIMWI: KAMA SIO DSTV POTEZEA

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images