Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KWA MADAKTARI KUWAANDIKIA WAGONJWA DAWA KWA MAJINA YA KIBIASHARA

$
0
0

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
 
Serikali imepiga marufuku kwa madaktari kuwaandikia wagonjwa dawa kwa majina ya kibiashara badala yake watumie majina ya asili (Generic name). Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. 
 
Dkt. Ndugulile amesema imefika wakati serikali imebidi kutoa tamko hilo kwasababu Madaktari wengi wamekuwa wakikiuka miongozo wa utoaji matibabu uliotolewa na wizara ya afya. "Katika mfumo wa utoaji wa huduma za afya, tunamtaka daktari aandike kwa jina la asili ili mfamasia akatafsiri aina ile ya dawa tulizonazo kwenye akiba yetu za dawa tulizonazo, ubora wa dawa za Tanzania ni za kiwango cha juu kabisa, tuwaambie wa Tanzania waache zile dhana potofu akisikia zile zinazotoka," amesema. 
 
Amesema kinachotokea kwasasa katika hospitali nyingi unakuta madawa ni mengi ila hayatumiki wanaishia kwenda kununua nje wakati angeandika kwa jina halisi angepatiwa. Amewataka wafamasia na waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini kuhakikisha wanatoa orodha ya dawa zote walizonazo kila mwanzo wa wiki ili kuwawezesha watoa dawa kufahamu dawa walizonazo ili kuondoa adha kwa wananchi kuandikiwa dawa ambazo hazipo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai akizungumza machache wakati akitoa neno la utangulizi katika Ufunguzi wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa -Tanzania linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula akitoa shukrani zake za pekee kwa waandaaji wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na Mwenyekiti wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) Bw. Mavere Tukai. 

Washiriki wa Kongamano la Wadau wa Mnyororo wa Ugavi wa Dawa- Tanzania (Tanzania Health Supply Chain Summit 2018) .


MABASI YA MWENDOKASI KARAHA TUPU DAR, RC MAKONDA AKASIRIKA, WENYEWE WAJITETEA

$
0
0

*Yaelezwa kuna madereva wamekimbia na funguo za mabasi kusikojulikana

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BADALA ya raha sasa karaha!Ndivyo unavyoweza kuuzungumzia usafiri wa mabasi ya mwendo kasi katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi wa Jiji hilo wamelalamikia unyanyasaji unaofanywa na watoa huduma wa usafiri huo.

Wakati watumiaji wa usafiri huo wakioneshwa kuchoshwa na usafir inavyoendesha, kwa upande wa uongozi wa DART umedai mradi huo unahujumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema kwao.

Hata hivyo kutokana na changamoto za usafiri huo leo asubuhi wananchi wa Kimara waliamua kuonesha hisia zao kwa kufunga barabara huku wakidai wamechoshwa na namna ambavyo huduma hiyo inatolewa.Wameiomba Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kuingilia kati kumaliza changamoto na adha ya usafiri wanayoipata huku wengine wakesema usafiri huo ni mateso kwao.

Wameiambia Michuzi Blog kuwa mabasi hayo yamekuwa yakiwapita watu vituoni na hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo na matokeo yake kusababisha watu kujazana na hiyo ni hatari kwani inaweza kusababisha maafa.

WATENDAJI UDART WAJITETEA 

Kwa upande wa Watendaji wanaosimamia Usafiri wa Mabasi ya Mwendo wa haraka(UDART) kupitia Meneja Mawasiliano wao Deus Bugaiywa amesema kinachotokea kwenye mradi huo 
wanahisi kuna hujuma zinazonywa kwa lengo la kukwamisha huduma ya usafiri kwa wananchi.

Amesema kutokana na hali hiyo kwa sasa kuna uchunguzi maalumu unafanywa kwa lengo la kubaini ukweli.Kuhusu kilichotokea leo asubuhi na kusababisha adha kubwa ya usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam na hasa wa Kimara amesema imetokana na kitendo cha madereva wawili kuchukua funguo za mabasi mawili ya mita 18 na kukimbia kusikojulikana."Kawaida mabasi huanza kutolewa saa 10 alfajiri ili kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya kusafirisha wananchi.Lakini leo asubuhi muda huo ulipofika walikuja madereva wawili na kisha kuchukua mabasi mawili na kisha kwenda kuziba njia.

"Baada ya hapo wakakimbia kusikojulikana na wakati wanachukua funguo hizo walikuwa wamevaa makoti marefu na kufunika sura zao.Hivyo bado wanaendelea kufuatiliwa ili kuwabaini na ndio maana tunahisi kuna hujuma zinaendelea,"amesema Bugaiywa.Ameongeza hata madai ya kuwa wamegoma kwasababu ya kutolipwa mshahara nalo halina ukweli kwani wamekuwa wakilipwa mshahara kama kawaida.

MAKONDA KUTINGA KITUO CHA KIMARA 

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaagiza watendaji wote wanaosimamia Usafiri wa Mabasi ya Mwendo wa haraka (UDART) kukutana nae kesho saa 12:30  asubuhi eneo la kituo cha Mabasi (Kimara Bus Terminal) .Makonda amesema lengo anataka kufahamu kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukuwa kumaliza kero za wananchi na  hafurahishwi hata kidogo na namna mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka unavyoendeshwa .

Amesema hata matarajio ya Rais Dk. John Magufuli yalikuwa ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri inageuzwa kuwa historia kupitia mradi huo lakini imekuwa tofauti na matarajio hayo."Hatuwezi kuvumilia kuona wananchi wanateseka wakati Serikali yao ipo kwaajili yao, kesho lazima hili liishe ili wananchi wasafiri pasipo usumbufu kama Serikali yao inavyotaka". amesema Makonda

TAASISI YA AGRI THAMANI FOUNDATION YASAINI MKTABA WA MAKUBALIANO NA OFISI YA MKUU WA MKOA KUTOKOMEZA CHANGAMOTO YA LISHE KAGERA

$
0
0
Na: Sylvester Raphael

Taasisi mpya ya Agri Thamani Foundation iliyoanzishwa kwa lengo kuu la kuboresha lishe Mkoani Kagera na kuongeza ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kuongeza Mnyororo wa thamani kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetiliana saini na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Mkataba wa Makubaliano ili kuanza utekelezaji wa shughuli zake ifikapo Novemba Mosi, 2018.

Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation ambaye ni mzawa wa Mkoa wa Kagera Bi Neema Lugangira mara baada ya kutiliana saini kwenye Mkataba wa Makubaliano na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory Bwana alisema kuwa aliamua kuanzisha Taasisi hiyo kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu na utapiamlo kutokana na kutopata lishe bora na stahiki.

“Nimeamua nianzishe Taasisi ambayo itausaidia Mkoa wetu wa Kagera hasa kuondoa udumavu kwa watoto kwani ukiangalia haraka utaona kuwa Mkoa wa Kagera kila zao linakubali kustawi lakini watoto hawapati lishe bora jambo ambalo linapelekea kudumaa kwao na mtoto akiwa na udamavu hawezi kuwa na kiwango kizuri cha akili hata kukua kwake kunaathirika.” Alieleza Bi Neema.

Bi Neema alieleza kuwa ili kufanikisha suala la kuondoa udumavu Kagera kwanza ni kuongeza ushiriki wa Wanawake na Vijana katika kuongeza Mnyororo wa Thamani katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo alitolea mfano katika kwenye kilimo kuwa Kagera kuna Mazao mengi lakini huenda akina mama hawajui namna bora ya kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao hayo lakini pia hawajui maana ya kufanya kilimo baishara ili kuingiza kipato na kuongeza ajira kwa vijana.

“Tutajikita katika Kilimo Biashara kwa kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao mfano mama anayelima viazi lishe afundishwe namna ya kukausha viazi hivyo na kuchanganya na mazao mengine na kutengeneza unga bora wa lishe, kwanza mama huyo watoto wake hawawezi kupata udumavu, pili atakuwa amejua namna bora ya kutunza unga wa viazi lishe badala ya kutunza viazi vyenyewe ambavyo mwisho wa siku vinaharibika.” Alifafanua Bi Neema

Bi Neema anasema kuwa Mkoa wa Kagera umebarikiwa kila zao kukubalika na wananchi wa Kagera wanalima mazao yote, masoko ya mazao hayo yapo lakini tatizo mazao hayo hayalimwi katika mfumo wa kuyaongezea Mnyororo wa Thamani yanapelekwa sokoni hivyo hivyo jambo ambalo linapelekea Mkulima kunyonywa lakini wakulima hanufaiki na mazao hayo kwani watoto wao utawakuta na udumavu kutokana na kutopata lishe bora.
 Bi Neema Rugangira Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation na Kaimu  Katibu Tawala Mkoa Bw. Nesphory Bwana Wakipeana Mikono Baada ya Kusaini Mkataba 
 Kabla ya Kusaini Mkataba wa Makubaliano.
 Kaimu  Katibu Tawala Mkoa Bw. Nesphory Bwana  akisaini Mkataba wa Makubaliano Pamoja Bw. Isaya Tendega Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji.
Picha ya Pamoja.

MTAYARISHAJI WA MUZIKI NCHINI PANCHO LATINO KUZIKWA KWAO GAIRO MKOANI MOROGORO.

$
0
0
Muandaaji wa Muziki nchini Tanzania, Producer Pancho Latino almaarufu Mafia ambae alifanya kazi kwenye studio mbalimbali  aliyefariki jana kwa  kuzama kwenye maji kwenye kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam anatarajia kuzikwa Wilayani Gairo, Morogoro. 

 Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Msanii Fid Q katika ukurasa wake wa Twitter imesema kuwa Marehemu  Pancho Latino itahitimishwa siku ya Jumamosi nyumbani kwao. Ibada itaanza saa 4 asubuhi, na baadae wataaga mwili wa marehemu na maziko yatafanyika saa nane mchana. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo kwa uchunguzi zaidi.

WAZIRI JAFO AMUONYA MTENDAJI MKUU WAKALA MABASI YAENDAYO KASI DAR , AMTAKA ATOE MAELEZO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam(DART) Mhandisi Ronald Lwakatare amepewa onyo kwa kile kinachoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Onyo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Suleiman Jafo ambapo pia amemtaka Mhandisi Lwakatare kujieleza kwanini ameshidwa kumsimamia mtoa huduma Udart.

Waziri Jafo mbali ya kutoa onyo hilo ametoa maagizo kwa Naibu Waziri wake Joseph Kakunda kufanya kikao ambacho kitamjumuisha Mtendaji mkuu wa Dart pamoja na mtoa huduma Udart ili kubaini changamoto zilizopo ambazo zinasababisha usafiri huo kuonekana kero kwa wananchi.

Amefafanua usafiri wa mabasi ya mwendo kasi ni usafiri uliokuwa wa nema kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao wengi wao walikuwa wanatumia zaidi ya saa tatu kutoka Posta hadi Kimara.

"Leo hii kupitia usafiri huu wanatumia takribani dakika 40 hadi 45, hivyo hatuwezi kuacha huduma ziendele kudorola kwa kiasi hichi.Lazima ufumbuzi upatikane ili wananchi wafurahie huduma za usafiri huo,"amesisitiza Jafo.

Wakati huo huo Waziri Jafo amemtaka Katibu Mkuu wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhandisi Mussa Iyombe kufanya uchunguzi katika ofisi ya Dart ili kuona kama wapo watendaji ambao wanakwamisha huduma hiyo.

TCRA Kanda ya Ziwa yatoa wasilisho la Chaneli za Maudhui kwa Madiwani Halmashauri ya Chato

LIVE: Taarifa ya Habari Kutoka TBC 1 Oktoba 10, 2018- Usiku

BALAAA..! DC KILOLO AWASHA MOTO UJENZI WA MADARASA


WAWEKEZAJI SWEDEN WATUA NCHINI KUJADILI UWEKEZAJI, TCCIA WATOA NENO...

WAZIRI NDALICHAKO SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENZI YALE ALIYOISHI MWALIMU NYERERE

MC PILIPILI ALIVYOKIWASHA MBELE YA MWASELELA MKOANI MBEYA

WAWEKEZAJI SWEDEN WATUA NCHINI KUJADILI UWEKEZAJI, TCCIA WATOA NENO...

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 10.10.2018

MICHUZI TV: MWENDOKASI WAJITETEA, WADAI WANAHUJUMIWA...MADEREVA WAO WAKIMBIA NA FUNGUO

BREAKING NEWS....ACACIA MINING PLC IN CORRUPTION SCANDAL INVOLVING SENIOR OFFICIAL AT NORTH MARA GOLD MINE IN TANZANIA

$
0
0
Two Acacia mine, North Mara Gold Mine in Tanzania, has been hit with a serious corruption scandal involving its two senior officials at North Mara Gold Mine in Tanzania. The officials are accused to bribe Government official and politicians in Tanzania so as to induce them to obtain favour against the interests of villagers and the Government in Mara Region.  

The Acacia official working with North Mara Mining in Tanzania  (NMML) (Marteen Van Der, Johanness Jensen) were on 10 October, 2018 brought before Tarime Resident Magistrate’s Court  being charged for serious corruption offences under the Prevention and Combating of Corruption Act, No. 11 of 2007. The accused in the case are MARTEEN VAN DER (Finance Superintendent, North Mara Gold Mine), JOHANNESS JENSEN (Land Manager, North Mara Gold Mine) JOSEPH THOMAS KLERUU, BOMBOGA CHIKACHAKE, TANZANIA OMTIMA AND ABEL Kinyimari
 The accused taken into the Tarime Resident Magistrate’s Court

The accused at the  Tarime Resident Magistrate’s Court

 The accused at the  Tarime Resident Magistrate’s Court
Copy of charge sheet 
 Copy of charge sheet 
Copy of charge sheet.

TAMASHA LA KIMATAIFA LA 37 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO.

MAKATIBU KAMATI WAANDAA TAARIFA YA USIMAMIZI WA SDGs KATIKA BUNGE

$
0
0
Mwenyekiti wa Kikao cha cha kuandaa Taarifa kuhusu Usimamizi wa Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) katika Bunge Ndg. Athuman Hussen akiongoza kikao hicho  kilichowahusisha Makatibu Kamati kutoka Ofisi ya Bunge kilichofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Makatibu Kamati wa Ofisi ya Bunge wakiwa katika kikao cha kuandaa Taarifa kuhusu Usimamizi wa Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) katika Bunge.Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. 

NHC YAKABIDHI KITUO CHA POLISI KWA JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limekabidhi Kituo chá Polisi kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam klichojengwa kwa thamani ya zaidi ya 
sh.milioni 75 ili kiweze kutoa huduma kwa jamii inayozunguka eneo la Changanyikeni Kibada jijini Dar es Salaam.Ujenzi wa kituo hicho kwa NHC sera ya utekelezaji wa huduma kwa jamii katika sehemu mbalimbali zilizokuwa na miradi na hata sehemu zingine ambapo miradi haifayiki.. 

Akizungumza kabla ya ufunguzi na makabidhiano, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi, amesema kuwa kabla ya ujenzi wa nyumba 248 za shirika hilo katika eneo la Kibada, walipanga kujenga kituo hicho ambacho sasa kimesha kamilika ikiwa kuhakikisha wakazi wanaoishi katika nyumba hizo wanakuwa na ulinzi wao na mali zao.

Amesema kituo hicho chenye vyumba viwili vya mahabusu (wakiume na wakike), ofisi ya mkuu wa kituo, vyoo viwili vya maofisa na vya mahabusu.
"Kumekuwa na mawasiliano na Jeshi la Polisi kukifanyika kwa maboresho kabla ya kukikabidhi kwa kuhakikisha kituo kimekidhi viwango vya ubora vya mahitaji ya polisi na kitawahudumia wakazi wengi wa eneo hili, "amesema Maagi.

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Awadhi Haji, alilishukuru shirika hilo kwa kuonesha uzalendo na kueleza kuwa, usalama ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi kwa amani na kujiletea maendeleo."Sasa ni jukumu letu kukitunza kituo hiki na kuwalinda wananchi na mali zao. Hata hivyo kwa asilimia mia moja hatutaweza peke yetu bila wananchi kushirikiana nasi kufichua uhalifu na wahalifu, "alisema Kaimu Kamanda Haji. 

Haji ambaye pia alimwakilisha Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa, amesema kituo hicho kwa sasa kitatoa huduma kwa saa 12 kutokana na kuwa ni kidogo na NHC wamekubali kukiongeza ili kiongeze huduma kwa kufanya masaa 24 na kuhimiza kuunda kikundi cha ulinzi shirikishi ili kushifikiana na polisi kuimarisha ulinzi zaidi. 

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Gwalugano Mwakatobe, aliishukuru NHC na kuekeza kuwa, awali walilazimika kutembea zaidi ya kilometa tisa kufuata huduma na uwepo wa kituo hicho utaimarisha usalama na kuondoa ubambikizaji wa kesi kwa raia.

Aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Kituo hicho, Jacob Daqaro, aliwaomba wananchi ushirikiano na kuahidi kusimamia sheria, haki na usalama. Kituo hicho kipo katika eneo lá mradi wa nyumba 208 za NHC Kibada, Kigamboni na Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Nyumba hizo, Juvenil Mwambi, alishukuru Polisi kwa kuanza kazi jana mara baada ya makabidiano na kusisitiza ushirikiano.
 .Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadh Haji akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha Polisi 
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadh Haji akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Kibada na . Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi
Muonekano wa Kituo cha Polisi cha NHC Changanyikeni .

 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Temeke, Awadhi Haji akizungumza katika halfa ya makabidhiano ya kituo cha polisi Kibada kilichojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Félix Maagi akizungumza kuhusiana na ujenzi wa kituo cha polisi ikiwa ni sera ya shirika hilo katika hafla makadhibiano ya kituo polisi yaliyofanyika Kibada jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Changanyikeni, Gwalugano Mwakatobe akieleza umuhimu wa kujengwa kwa kituo cha polisi katika eneo lake katika hafla ya makabidhiano ya kituo cha polisiliyofanyika kibada jijini Dar es Salaam.

MO DEWJI UPDATES: MSAKO MKALI UNAENDELEA WAKATI WAZUNGU WAWILI WAKITAJWA KUHUSIKA NA UTEKAJI

$
0
0
*Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar wafanya msako mkali kuhakikisha anapatikana

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuna Wazungu wawili wanasakwa kwa kuhusika kuratibu mpango wa kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji 'Mo'.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kwamba katika tukio hilo kuna wazungu wawili wanahusika kuratibu tukio la kutekwa kwa Mo Dewj.

"Tupo hapa kwa ajili ya kufuatilia tukio hili la kutekwa kwa Mo.Taarifa za awali ambazo tumezipata zinaonesha kuna Wazungu wawili wamehusika kuratibu tukio la Mo kutekwa."Tumeanza kufuatilia na wananchi wasiwe na wasiwasi,kikubwa watupe taarifa nasi tutazifanyia kazi," amesema Kamanda Mambosasa akiwa eneo la Hoteli ya Collessium  eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako tukio la kutekwa Mo linadaiwa kutokea.

KAULI YA MAKONDA
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema taarifa za kutekwa kwa Mo zimeshutua wengi lakini anaamini atapatikana kwani tayari vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake.

Makonda amesema kuwa kikubwa wananchi wa Dar es Salaam kutokuwa na wasiwasi na wawe watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea  kufuatilia.

HAJJ MANARA ATOA NENO
Wakati huo huo Msemaji wa Klabu ya Simba Hajj Manara amesema kikubwa ni kwa sasa ni utulivu na kuacha vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake.

Pia amesema kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ni kumuomba ili Mo apatikane akiwa salama na anaamini atapatikana."Mbali ya kuwa Mo ni shabiki wa soka bado tukio la kutekwa kwake limeshutua makundi mbalimbali," amesema Manara.

NMB WADHAMINI MASHINDANO YA GOLF YA MKUU WA MAJESHI, JWTZ

$
0
0


Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo zilizotolewa na NMB ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

BENKI ya NMB imedhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 na kushirikisha wachezaji wa gofu kutoka klabu mbalimbali nchini.

Udhamini uliotolewa ni wa shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zitakazo tumika katika mashindano hayo vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga katika viwanja vya Lugalo.Kukabidhiwa kwa udhamini huo ni mwendelezo wa Benki ya NMB kudhamini na kusaidia shughuli anuai za michezo hususani ya Jeshi la wananchi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kukabidhiwa kwa udhamini huo, Makamu Rais wa Umoja wa Klabu za Golf Tanzania, Luteni Canali David Luoga alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali vya golf Tanzania na makundi ya wachezaji wakiwemo watoto.Alisema mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa siku moja pekee na kufunguliwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo washindi watajipatia fedha taslimu pamoja na vikombe.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kile kushirikisha viongozi waandamizi mbalimbali kutoka Serikalini waliostaafu na awaliopo madarakani."Kama unavyofahamu klabu yetu ya mchezo wa golf inashirikisha pia viongozi mbalimbali waandamizi kutoka Serikalini waliostaafu na wengine bado wapo madarakani nao tunatarajia watashiriki katika mashindano haya...hivyo yatakuwa na mvuto wa kipekee," alisema Luteni Canali Luoga.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wa kati wa benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 26 Mwenyekiti wa klabu ya gofu Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo (katikati) zilizotolewa na NMB kudhamini Mashindano maalum ya Mchezo wa Golf ya Mkuu wa Majeshi nchini yanayotarajia kufanyika Oktoba 13 katika viwanja vya Lugalo Dar es Saalam.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images