Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 251 | 252 | (Page 253) | 254 | 255 | .... | 3282 | newer

  0 0

    Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu eneo la  Ilungu karibu na mji wa Magu.  Jengo hilo litagharimu shilingi bilioni 6 na milioni 700 litakapokamilika. 
   Rais  Jakaya Kikwete ngoma ya utamaduni wilaya ya Magu kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu
  Rais  Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Magu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu. Kwa picha zaidi  na John Lukuwi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Dkt Noorali T. Jiwaji
  Leo Jumapili tarehe 8 Septemba, upande wa magharibi karibu na upeo, utauona Mwezi ukiosogea nafasi yake angani mbele ya macho yako, ukiuangalia kwa saa moja hivi kuanzia baada tu ya machweo, hadi baada ya saa mbili hivi. (angalia picha chini)


  Nyota ya Spika inayoonekana kushoto wa Mwezi mwandamo ipo juu kidogo tu ya Mwezi, lakini baada tu ya saa moja hivi utaona nyota ya Spika iko chini kidogo ya Mwezi mwandamo.


  Kilichotokea kihalisi ni kwamba kwa vile Mwezi unatembea kwa kasi kubwa katika mzunguko wake wakati nyota hasizogei, kihalisi, ni Mwezi uliosogea kupanda juu.


  Sayari zote, pamoja na Mwezi, husogea kutoka magharibi kwenda mashariki ukilinganisha na nyota, ambazo hazisogei angani kwa vile zipo mbali mno na sisi.


  Nyota angavu sana inayoonekana juu ya Mwezi si nyingine ila 'nyota ya jioni' ambayo ni sayari ya Zuhura.  Mwezi mwandamo na nyota angavu ya Zuhura inatoa mandhari ya kuvutia sana angani.


  0 0
 • 09/07/13--17:35: --none--


 • 0 0
 • 09/07/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Si rahisi kumsahau Marhum Issa Matona na ngoma yake ya Harusi

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set Bungalows iliyoko katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Abdullsamab Ahed Said akikagua athari iliyosababishwa na moto mkubwa uliyoyakumba baadhi ya majengo ya Hoteli hiyo juzi jioni. Pembeni yao aliyevaa kofia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A” Machano Fadhil Machano { Babla }  na Nyuma yao aliyevaa suti za Bahari ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
   Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  Pembe Juma Khamis akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hali halisi ya moto ulivyoikumba  Hoteli ya White Sand iliyoko Kendwa Nungwi Mkoani humo juzi jioni.
  Baadhi ya Majengo ya Hoteli ya White Sand iliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Kendwa Nungwi ikiwa ni miongoni mwa majengo 10 ya hoteli hiyo yaliyoteketea kwa moto mapaa yake juzi jioni.
  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
  -----------------------------------------------
  Hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni Moja Nukta 2 imepatikana kufuatia kuungua kwa moto hoteli mbili za Kitalii za  White Sand na Sun Set Bungalows ziliopo katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Wilaya ya Kaskazini “ A” Mkoa wa Kaskazini Unguja juzi majira ya saa 11.00 za jioni.
  Hoteli ya Sun Set Bungalows inakadiriwa kupata hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 400 wakati ile ya White Sand  iliyoungua zaidi kutokana na moto huo inakadiriwa hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 800.
  Moto huo ulisababishwa na hitilafu za umeme katika moja ya majengo ya Hoteli ya Sun Set Bungalows iliyoezekwa makuti na kutoa cheche za moto zilizosambaa kwa haraka katika baadhi ya  majengo mengine kutokana na upepo mkali uliokuwa ukivuma katika eneo hilo.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi akitokea Bungeni Mjini Dodoma alifika eneo hilo la tokeo ili kuwafariji Wamiliki, Wafanyakazi wa Hoteli hizo pamoja na Wananachi wanaozizunguuka Hoteli hizo kutokana na maafa hayo makubwa kwa uchumi wa Taifa.
  Akitoa ufafanuzi wa  mkasa halizi wa tukio hilo  Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set Bungalows Abdullsamad Ahmed Said alimueleza Balozi Seif kwamba Moto huo umevikumba vyumba Vinane vya  kulala wageni, Stoo pamoja na jiko la kupikia.
  Abdullsamad alisema Wageni wapatao sabini waliokuwemo kwenye vyumba vya Hoteli hiyo waliweza kuokolewa kwa ushirikiano kati ya Wafanyakazi wa Hoteli hiyo na Wananchi walioizunguka Hoteli hiyo jambo ambalo lilileta faraja kwa Uongozi pamoja na wafanyakazi wake.
  Mmiliki huyo wa Hoteli ya Sun Set Bungalows aliwashukuru wananchi hao, Viongozi wa Serikali Wilaya na Mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na Maafisa wa Kamisheni ya Utalii kwa msaada wao ulichangia kupunguza machungu ya janga hilo.
  Balozi Seif Ali Iddi akikagua hali ya tukio  la moto huo ambao pia uliathiri Hoteli nyengine ya jirani ya White Sand ambapo Mmoja miongoni mwa  Viongozi wa Hoteli hiyo Ramadhan Msanif  alimfahamisha Balozi Seif kwamba  wakati wakijiandaa kutoa msaada kwa wenzao jirani wa Sun Set cheche za moto huo pia zikaanza kuvamia Hoteli yao na kulazimika kukabiliana nalo.
  Bwana Msanif  alisema licha ya juhudi walizochukua kukabiliana na moto huo lakini kasi kubwa ya upepo uliokuwa ukivuma wakati huo ulisababisha kuathiri  mapaa ya nyumba  10  za hoteli hiyo katika kipindi kifupi kwa vile zilikuwa na mapaa ya makuti.
  Akizungumza na Viongozi, Wafanyakazi wa Hoateli hizo pamoja na Wananchi wa jirani na Hoteli hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alitoa wito kwa wananchi kuendelea kusaidia wawekezaji wakati yanapotokea majanga kwenye maeneo ya vitega uchumi.
  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inasisitiza na kutegemea sekta ya Utalii ambayo kwa sasa inasaidia kuongeza mapato ya Taifa sambamba na kutoa ajira kwa wananachi wanaovizunguuka vitega uchumi hivyo.
  Hata Hivyo Balozi Seif aliendelea kuwakumbusha wawekezaji vitega uchumi mbali mbali Nchini kujenga utamaduni wa kuiwekeza Bima Miradi yao ili wakati wanapopatwa na majanga au maafa Bima hizo ziweze kuwasaidia.
  Alisema inasikitisha kuona ipo miradi ya kiwango kikubwa cha fedha inayoendelea kuwekezwa Nchini lakini wamiliki wengi wa miradi hiyo wanashinda kuikatia bima na hatiame inakufa kabisa pale inapokumbwa na majanga kama ya moto.
  “ Wawekezaji na hata Wafanyabiasharawengi  bado wamekuwa wazito kuiwekea Bima miradi yao na kusahau kwa kuona ghali  mpango huo ambao kumbe huwa unawasaidia wakati wanapopatwa na majanga “. Alifafanua Balozi Seif.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi waliopo jirani na Hoteli hizo kwa juhudi kubwa waliyochukuwa na kusababisha  kupungua  kwa hasara kubwa iliyokuwa izikumbe hoteli hizo.
  Alisema juhudi hizo zilizowaongezea nguvu za uokozi wafanyakazi wa hoteli hizo zimesaidia kuokoa mali na vifaa vya hoteli pamoja na wageni waliokuwa wakipata huduma ndani ya Hoteli hizo.
  “ Nafarajika kusikia kwamba harakati za uokozi wa mali na vifaa katika Hoteli hizi mbili za White Sand na Sun Set Bungalows za Kendwa hakukuwa na ripoti za udokozi wa mali kama zilivyotokea Kwenye Hoteli ya Paradise Beach Resort iliyopo  Marumbi wakati ilipowaka moto wiki moja na nusu iliyopita.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri Uongozi wa Hoteli hizo kufikiria kubadilika  katika mfumo wa ujenzi wa mapaa ya makuti ili kujilinda na  majanga yanayoweza kuepukwa licha ya kwamba mfumo huo hutoa ajira kwa wananchi wanaouza makuti yao.
  Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliangalia eneo lililopembezoni mwa Bara bara mbele ya Skuli ya Msingi na Sekondari ya Mto Pepo ambalo liko katika hali mbaya kimazingira.
  Ziara hiyo ya ghafla ya Balozi Seif ilikuja kufutia baadhi ya wananchi kufanya Biashara katika eneo hilo linalotishia afya za Binaadamu kutokana na kutuwama kwa maji machafu yanayoweza kusababisha maradhi ya kuambukiza.
  Katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuagiza Sheha wa Shehia ya Mto Pepo pamoja na Diwani wa Wadi ya eneo hilo kufika Ofisini kwake Vuga Jumatatu  ya Tarehe  9 Septemba  asubuhi kulijadili suala hilo.
  Hali ya mazingira ya  eneo hilo mbali ya kutoa  sura mbaya kwa wapita njia na wageni lakini pia inaweza kusababisha mripuko wa maradhi  hasa kwa  wanafunzi wadogo wasiozingatia afya zao wa Skuli ya jirani na eneo hilo.


  0 0

   Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface akipozi kwa picha mara baada ya kushinda taji hilo jana na kuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2013 baada ya kuwashinda warembo wenzake 29. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika Hoteli ya Snow View Arusha na kuwashirikisha warembo 30.
  Mshindi wa taji la Redd’s Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface (katikati) akipozi kwa picha na mshindi wa pili Elizabeth Pert (wapili kushoto), mshindi wa tatu Svetlana Nyameyo (wapili kulia), mshindi wan ne Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Tanzania Photogenic 2013 na Mshindo wa tano Latifa Mohamed, mara baada ya kushinda taji hilo jana ambapo Narietha amekuwa mrembo wa pili kuingia katika nusu fainali za Miss Tanania 2013 baada ya Miss Photogenic. Shindano la Miss Tanzania Top Mode lilifanyika katika Hoteli ya Snow View Arusha na kuwashirikisha warembo 30.

  0 0

  Ikikadiriwa kuwa na wateja zaidi ya Milioni Kumi na Moja kampuni ya simu ya Vodacom imesema itaendelea kuchukua juhudi za makusudi kuweka huduma zake karibu na wananchi ili kuendana na kasi ya ongezeko la wateja sanjari na kupanuka kwa miji. 
  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo anaeshughulikia usimamizi wa maduka ya Vodacom Upendo Richard wakati wa hafla ya ufunguzi wa duka jipya la Vodacom lilipo eneo la Kimara Stop Over nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. 
  Upendo amesema kuwa Vodacom imeendelea kushuhudia ongezeko la kasi la wateja ambao wamekuwa wakiishi maeneo mbalimbali wengi wao nje ya miji hatua ambayo amesema inaipa kampuni yake changamoto ya kuhakikisha huduma zake zinapatikana karibu zaidi bila kuathiri ubora. 
  "Tunafuraha kubwa leo hii kuzindua duka la 69 kwa nchi nzima likiwa ni la 19 kwa mkoa wa Dar es salaam, Jambo zuri kwa duka hili ni kwamba lipo nje ya mji na hivyo kuwahakikishia wateja wetu kupata kila wanachokihitaji karibbu na makazi yao na maeneo ya shughuli zao za kila siku.
  "Miji yetu nayo inapanuka na hatuwezi kuwafanya wateja wetu kuendelea kutegemea maduka yaliyopo ameneo ya katikati ya mji ama karibu na mijini lazima tuwafikishie huduma mahali walipo hata kama ni nje ya miji ili kuwpaunguzia gharama ya muda na fedha kwa kusafirei kufuata huduma hizo umbali mrefu."Aliongeza Upendo 
  Upendo amewataka wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani kulitumia duka hilo ili waweze kuendana na shabaha ya Vodacom ya kuwapunguzia wateja wake gharama huku akiwahakikishia wateja kuwa ubora wa huduama za Vodacom kwenye duka hilo unakidhi vigezo vya ubora wa maduka mengine. 
  "Tunaleta huduma karibu na wananchi ili kuwapunguzia gharama na kero za kusafiri umbali mrefu nataka niwahakikishe wateja wetu kwamba ubora wa huduma kwenye duka hili ni sawa na za kwenye maduka yetu mengine kama la Oysterbay, Mlinai City na Samora hivyo kwani linapokuja sula la kumhudumia mteja kwetu sisi hakuna tofauti."Alisisitiza 
  Kwa upande wake Meneja wa duka hilo Eunice Lulinga amesema duka hilo litakuwa likitoa huduma zote za Vodacom ikiwemo usjili wa nambari, Swim Swap, M-pesa. 
  "Tunawakaribisha wakazi wa Kimara kulitumia duka hili kwa mahitaji yao ya Vodacom, tunatambua umuhimu wa huduma bora na kuweka tabasamu kwenye uso wa mteja wetu muda wote ambao Vodacom inawahudumia wateja wake."Alisema Eunice 
  Akizungumzia umuhimu wa duka hilo kwa wateja, Mkazi wa eneo la Kimara Stop Over ambae pia ni mteja wa Vodacom Mohamed Salim amesema ni ukombozi mkubwa kwao kwa kuwa awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hasa kwenye duka la Mlimani City. 
  "Nikiwa mteja wa Vodacom najisikia furaha kubwa kuona Vodacom imetujali na kutuletea huduma karibu yetu, tunalipokoea kwa furaha sana kutokana na ukweli kwamba litatupunguzia gharama amabzo tulikuwa tukilamika kuingia kwenda hadi Mlimani City."Alisema Salim
   Salim amesema anatambua kuwa eneo la Kimara kama yalivyo maeneo mengine ya nchi yana uhitaji mkubwa wa huduma za Vodacom hasa M-pesa, usajili na huduma za kupatiwa laini mpya ya simu kutokana na sabbau mbalimbali ikiwemo kupoteza. 
  Vodacom imekuwa mstari wa mbele kuongeza mtandao wa maduka yake hatua ambayo imekuwa ikipongezwa na wananchi na wadau wengine hasa kutokana na jinsi jamii inavyoitegemea M-pesa katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiibiashara.
   Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania,Upendo Richard akishirikiana na meneja wa duka jipya la Vodacom lilillopo eneo la Kimara Stop over  jijini Dar es Salaam, Eunice Lulinga (kushoto) kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka hilo,akishuhudia Katikati ni meneja Uhusiano wa nje wa kampuni hiyo Salum Mwalim.
   Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania,Upendo Richard (katikati ) na mmoja wa  wateja waliofika kupata huduma katika duka jipya la Vodacom lililopo Kimara stop over  jijini Dar es Salaam, Mohammed Salim (kulia) wakimsikiliza kwa makini Meneja mauzo wa duka hilo Lenazitha Joel wakati alivyokuwa  akiwaelezea jinsi ya kutumia moja ya simu zinazopatikana dukani hapo mara baada ya kuzinduliwa rasmi.
   Meneja  Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akimkabidhi fulana mteja wa kwanza kupata huduma katika duka jipya la Vodacom lililopo eneo la Kimara  jijini Dar es  Salaam, Bi. Bahati Kahaya  baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Elihuruma Ngowi, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa kampuni hiyo,Upendo Richard na Meneja wa duka  hilo Eunice Lulinga.
  Duka jipya la Vodacom  lililopo eneo la Kimara Stop over jijini  Dar es Salaam likiwa  katika muonekano halisi baada ya kuzinduliwa  leo , wakazi wamaeneo hayo watapata fursa ya kupata huduma zote zinazotolewa na Vodacom  Tanzania.

  0 0
 • 09/08/13--03:41: JAHAZI YAFUNIKA DAR LIVE
 • Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo
  Mashabiki wakiwa wamembeba juujuu mlemavu ambaye alipagawa na burudani za Jahazi.
  Khadija Yusuf akijinafasi stejini.
  Jukwaa likiwa juu wakati Leila Rashid akiwapa raha mashabiki.
  Mzee Yusuf (kushoto) akiwa na Dude 'Yahaya' wakiimba kwa pamoja.
  Mzee Yusuf akiendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live.
  Mcharaza gitaa wa Jahazi, Musa Musa akiwa kazini. Pembeni ni mabango ya wadhamini.
  Wanamuziki wa Jahazi wakiimba kwa pamoja.
  Leila Rashid akiwapagawisha mashabiki.
  Baadhi ya wasanii wa filamu wakiwa jukwaani kusalimia mashabiki.
  Baadhi ya mashabiki waliofurika wakiserebuka.
  Mzee Yusuf akiserebuka na mpiga gitaa wa bendi hiyo, Mauji.
  Hata sehemu ya kutema mate haikuwepo kwa jinsi mashabiki walivyofurika.
  BENDI ya Jahazi Modern Taarab usiku wa kuamkia leo imefunika vilivyo katika onyesho lao la nguvu lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf na kundi lake ilizikonga nyoyo za mashabiki na kuwaacha roho safi.
  (PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  Sekta ya pamba nchini ina uwezo wa kuwakwamua wakulima wa pamba katika dimbwi la umaskini endapo serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wataweza kusaidia uwepo kilimo cha mkataba nchini.

  Akiongea na vyombo vya habari hivi karibu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Gabriel Mwalo, alisema kuna faida nyingi katika kilimo cha mkataba lakini kukosekana kwa usimamiaji mzuri pamoja na ukosefu wa uungwaji mkono wa kutosha kutoka Serikalini kunawafanya wawekezaji kutochangia fedha nyingi zinazohitajika katika mfumo.

  Sasa wakati umefika kwa Serikali kuyaangalia matatizo yanayokwamisha kilimo cha mkataba na mkazo uwekwe kwenye uzalishaji wa pamba pasiwepo ucheleweshaji wa utekelezaji wa sera ya Serikali,” Bw. Mwalo alisema.


  0 0


   Mwili wa Marehemu Yusta Mkali ukiwa tayari kwa kuagwa Hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam,na kuanza kwa safari ya mazishi yatakayofanyika kijiji cha Nzasa  Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma. 
   Mtoto wa Marehemu Baraka Simon(12)akimuaga mama yake mzazi kabla ya safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi kuanza aliemshikilia ni mama yake mkubwa Lucy Ngorido.

   Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Yusta Mkali likiwa kwenye gari tayari kwa kuanza safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yatakayofanyika hapo kesho.
  Wakinamama wakilia kwa uchungu
  Mtuhumiwa Musa Senkando ambaye bado anatafutwa na Polisi kwa mahojiano akiwa mtuhumiwa wa mauaji hayo. Wananchi tunaomba msaada wenu kwani huyu mtu ni hatari sana katika jamii yetu.

  0 0

  Burudani ya ngoma ikiendelea katika Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika Ndani ya Tamasha la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya (wa pili kulia) akiwa na wageni wake pamoja na wanachama wa TGNPBaadhi ya wageni waalikwa ndani ya Usiku wa Mwanamke wa Kiafrika kwenye maadhimisho ya Tamasha la Jinsia Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye semina ya kamata fursa twenzetu.ASAS amejitolea kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia vikundi vitakavyoamua kutumia fursa ya kulima vitunguu na kuendelea kuwa wajasiliamali katika fursa mbalimbali. 
    Mfanyabiashara mkubwa wa mjini Iringa,Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akionesha baadhi ya fursa zilizopo mkoani Iringa kwa kuonesha kitunguu cheupe kama moja ya bidhaa za thamani zinazopatikana mkoani humo,ASAS ameeleza kuwa vitunguu hivyo vinauzwa kwa kilo kwenye SuperMarket nyingi,anasema kuwa vitunguu hivyo vinadaiwa kutoka nje ya nchi,lakini vitunguu hivi inawezekana kuvipanda hapa mkoani Iringa na vijana wakanufaika kupitia mradi wa vitunguu hivyo.

   Mdau mkubwa wa michezo nchini Fredrick Mwakalebela naye alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakaoweza kutumia fursa ya rasilimali zilizopo mkoani hapo.
   sehemu ya meza kuu. 
   Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu Dominic  mjini Iringa,ambapo watu mbalimbali wamepata fursa ya kujua namna ya kutumia sasilimali zilizopo mkoni humo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
   Mwakilishi kutoka NSSF Makao Makuu Salim Khalfan, akizungumzia Fursa kwa upande wa NSSF wanavyoweza kuitumia wakazi wa Iringa katika kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.
   Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Kamata fursa twenzetu mepema leo mchana ndani ya mkoa wa Iringa.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0   Mmoja wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta  linafanyika usiku huu.
    Pichani ni sehemu ya wakazi wa Mkoa Iringa na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linaloendelea kufanyika hivi sasa katika uwanja wa Samora.

  Moja ya kikundi mahiri kutoka jijini Dar,chenye maskani yake Kinondoni,KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza moja ya wimbo wa Michael Jackson,mbele ya wakazi wa Iringa wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
   Msanii aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba jukwaani usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora. 
  Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.
   Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
    Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
   Ni noma saana
  Anaitwa Linah,moja ya wasanii wanaofanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva akiimba kwa hisia jukwaani,huku shangwe za mashabiki zikivuma kila kona ya uwanja.
  Anaitwa Shilole na Skwadi lake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.PICHA ZAIDI LIVE HAMIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0


  0 0

  Drug smugglers have set fire to a ship carrying more than £50m worth of hashish after they were spotted by customs officials.
  Plumes of smoke billowed from the bridge of the Gold Star freighter minutes after it was "buzzed" by a helicopter from the Italian coastguard.
  Nine people on board the Tanzanian-registered ship jumped overboard and had to be rescued.
  Smugglers torch £50m of hashish on board a ship
  Customs officials received a tip off that the Gold Star had drugs on board
  Italian customs officials intercepted the Gold Star as it sailed off the coast of Sicily in the Mediterranean following a tip-off that it was carrying a huge consignment of drugs.
  The vessel had been followed for several days before the operation was launched.
  Fast patrol boats were used in the "raid" and a search of the ship's hold revealed 30 tonnes of hashish which had been loaded on board in Turkey.
  Officials said the crew were Syrian and Egyptian, but before they could board the 82-metre ship they had to obtain permission from Tanzania where it was registered.
  Smugglers torch £50m of hashish on board a ship
  Nine crew on the ship have been arrested
  Firefighting boats had to be called in to put out the flames and the ship was being towed to the Sicilian port of Syracuse where the crew members were arrested.
  A spokesman for Italian customs said: "The ship was intercepted after intelligence was received that it was carrying drugs - but we never expected such a huge consignment and for the crew to set her on fire.
  "The idea was no doubt to try and destroy the evidence so that we could have no case against them, but their plan failed and the fire was put out and the drugs were found during the search.
  "Nine people onboard jumped into the sea, but they couldn't get very far as they were several miles from shore and they had to be rescued by Italian customs officers.
  "The fire is now under control and the ship is being taken to a port where it will be thoroughly searched again and the nine crew members will be questioned by prosecutors."

  0 0

   Maelfu ya wakazi wa Mwanza na miji ya jirani wakimsikiliza Rais Kikwete katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo jioni.

   Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na miji ya jirani katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo jioni.Rais Kikwete yupo Mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo Picha na Freddy Maro
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa na kubonyeza kitufe kuashiria kuzindua mradi wa kufua umeme wa megawati 60 huko Nyakato,Mwanza leo asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo.Uzinduzi wa mitambo hiyo ni sehemu ya ufumbuzi wa tatizo la umeme uliokuwa unaikabili kanda ya ziwa.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo ya kufua umeme wa megawati 60 muda mfupi baada ya kuzindua mitambo hiyo huko Nyakato Mwanza leo. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia akiwa na mavazi maalumu) akikagua jengo la upasuaji katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana,Mkoani mwanza leo mchana.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Septemba 8, 2013, amezindua mtambo wa kufua umeme kiasi cha megawati 60 katika eneo la Nyakato mjini Mwanza, umeme ambao utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza shida ya umeme katika Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.

  Aidha, Rais Kikwete ameiangiza Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanza mara moja maandalizi ya kupeleka umeme kwenye machimbo ya madini ya nikeli yaliyoko Kabanga, Ngara, Mkoa wa Kagera.

  Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake itaharakisha mipango ya kujenga reli hadi kwenye eneo hilo kama maandalizi ya kuanza kuchimbwa kwa madini hayo ambayo ni mazito na kuyasafirisha kwa barabara kwenda bandarini Dar Es Salaam kutaharibu kwa haraka barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa nchini.

  Akizungumza kabla ya kuzindua mtambo huo, Rais Kikwete  ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuharakisha mipango ya kuunganisha eneo la Kabanga, Ngara, Mkoani Kagera kwenye Gridi ya Taifa ili uzalishaji wa madini ya nikeli usije kukwamishwa na ukosefu wa umeme. Amesema kuwa mgodi huo utahitaji umeme mwingi kiasi cha megawati 40.

  Rais amesema kuwa Serikali yake itahakikisha inafikisha reli kwenye eneo la Kabanga mapema ili kuhakikisha kuwa nikeli inayozalishwa inasafirishwa kwa reli badala ya barabara. Amesema kuwa madini hayo ni mazito mno na kuyasafirishwa kwa barabara kutaharibu kabisa na katika muda mfupi barabara ambazo zinajengwa nchini kwa gharama kubwa.

  Mtambo wa Umeme wa Nyakato wenye uwezo wa kuzalisha megawati 60 ulianza kujengwa mwaka jana, 2012, baada ya Serikali ya Tanzania kutiliana mkataba wa ujenzi na Kampuni ya Semco and Rolls Royce ya Norway mwaka 2011 wakati maandalizi ya ujenzi huo yalipoanza.

  Gharama za ujenzi wa mtambo huo ambazo ni sh bilioni 130 (Euro milioni 48.7 na dola za Marekani 15.9) zimelipwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Tanzania.

  Akizungumza na wananchi kwenye sherehe ya uzinduzi huo, Rais Kikwete amesema kuwa umeme siyo anasa bali ni moja ya vigezo vya msingi na muhimu kabisa vya maendeleo.

  “Vipo vigezo vingi vya maendeleo ya nchi na binadamu, lakini moja ya vigezo hiyo ni umeme. Na ukiangalia matumizi ya umeme kwa kila nchi yanaonyesha kiwango cha maendeleo cha nchi hiyo. Katika Marekani, kwa mfano, kila mwananchi anatumia kiasi cha kilowati 12,000 kwa wastani. Sisi katika Tanzania ni kilowati 89 tu na wastani wa Bara la Afrika ni kilowati 150,”  amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  “Nc hi yetu ya Tanzania ina umeme kiasi cha megwati 1,450 tu wakati katika Afrika Kusini ni megawati 45,000 na unaweza kuona tofauti ya maendeleo. Hivyo, ni muhimu sana kwetu kuongeza kiwango cha kuzalisha umeme katika nchi yetu.”

  Katika siku ya tatu ya ziara yake kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mwanza, Rais Kiwete pia amefungua Kituo cha Polisi cha Nyakato ambacho kimegharimu sh milioni 450, Serikali ikiwa imechangia kiasi cha asilimia 20 cha gharama hizo.

  Kituo hicho cha kisasa kilianza kujengwa mwaka 2003 lakini ujenzi wake ukawa unakwamakwama kutokana na ukosefu wa bajeti hadi uongozi wa polisi wa Mkoa wa Mwanza ulipoamua  kukijenga kituo hicho kwa njia ya kuishirikisha jamii na ikaundwa Kamati ya Ujenzi chini ya uenyekiti wa Bwana Alfred Wambiura.


  Akizungumza kwenye sherehe ya ufunguzi wa kituo hicho, Rais Kikwete ameahidi kuwa atajenga nyuma moja kwa ajili ya mkazi ya polisi. Kituo hicho kina jumla ya askari polisi 65.  0 0


  0 0


  0 0

  Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania kiwanda cha Mbeya wamehitimisha shamrashamra za kupokea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona zilizodumu kwa mwezi mmoja nchi nzima. Kama ilivyokuwa maeneo mengine, maelfu ya mashabiki wa soka jijini Mbeya pia wamepata fursa ya kuwa sehemu ya shamrashamra hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki na kuvutia maelfu ya mashabiki wa kandanda.

  Shamrashamra hizo zilihusisha maandamano makubwa ya wafanyakazi wa Kampuni Bia Tanzania (TBL) pamoja na vikundi vya sanaa vya Magereza Brass Band na Bombeso waliokatiza katika mitaa ya jiji la Mbeya wakitoa burudani ya muziki, matarumbeta na manjonjo ya kucheza kandanda.

  Wakati wa maandamano hayo mashabiki wengi wa mpira wa miguu walijitokeza barabarani kushuhudia utambulisho huo, baadhi yao wakiwa wamevalia jezi za Barcelona.

  Maandamano hayo yaliyowahusisha wafanyakazi wa TBL yalianzia katikati ya jiji la Mbeya na kupita katika mitaa kadhaa ya katikati ya jiji la Mbeya na kuishia Iyunga kilipo kiwanda cha TBL yakiwa na lengo la kuutambulisha ubia wa Castle Lager na Barcelona kwa wafanyakazi wa TBL pamoja na wadau wa michezo wa Mbeya.

  Pia maandamano hayo yalikuwa na lengo la kuonyesha sapoti ya wafanyakazi hao kwa ubia wa Castle Lager na FC Barcelona, ambayo inatajwa kuwa ni klabu ya karne kutokana na mafanikio makubwa na kuwa na wapenzi wengi zaidi duniani kuliko timu nyingine yoyote.

  Wakati wa maandamano hayo mashabiki wengi wa mpira wa miguu walijitokeza barabarani kushuhudia utambulisho huo, baadhi yao wakiwa wamevalia jezi za Barcelona.

  Akizungumza na wafanyakazi wa TBL katika hafla iliyofanyika kwenye kiwanda cha TBL Mbeya kuhusu ubia wao na Barcelona, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa TBL, James Kavuma amesema wafanyakazi wa TBL Mbeya na wananchi wa Mbeya wameupokea udhamini huo kwa furaha kwani anaamini kuwa udhamini huo utaweka karibu mashabiki wa Barcelona na klabu yao waipendayo kupitia bia ya Castle Lager.

  ‘’Udhamini huu umelenga mambo mengi, moja ikiwa ni kuwaweka karibu wapenzi wa klabu hiyo waliopo Tanzania na Barcelona. Lakini si hilo tu, yapo mambo mengi yenye manufaa kwa jamii yatakayopatikana kutokana na udhamini huo wa miaka mitatu.’’

  Naye Meneja Mauzo wa Kanda hiyo, Michael Myinga alisema kuwa kutokana na historia ya zaidi ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa FC Barcelona na Castle Lager basi ubia huu unaleta maana kubwa na ni muafaka ukizingatia kuwa Castle Lager ni kinywaji cha bara zima la Afrika.

  Meneja wa Castle Lager Kabula Nshimo alisema kwamba sherehe hizo zilizofanyika Mbeya ndio za mwisho katika mlolongo wa kuzindua mahali pote ambapo TBL ina viwanda. Aliongeza kuwa sasa shughuli nyingine mbalimbali zinazohusisha wadau wa soka na jamii kwa ujumla ndio zitakazofuatia kupitia shughuli mbalimbali zilizopangwa kufanyika nchi nzima katika.
  Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakicheza kwaito kusherekea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.
  Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakicheza foosball kusherekea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.
  Wananchi wa jiji la Mbeya wakitazama maandamano ya wafanyakazi wa TBL Mbeya kupokea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.
  Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakicheza mduara kusherekea udhamini wa Castle Lager kwa FC Barcelona.

older | 1 | .... | 251 | 252 | (Page 253) | 254 | 255 | .... | 3282 | newer