Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

WAWEKEZAJI RANCHI ZA TAIFA WATAKIWA KUSAINI MIKATABA MIPYA

0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
WAWEKEZAJI wa vitalu vya ufugaji katika ranchi ya taifa watakiwa kusaini mikataba mipya kwaajili ya kuendelea na ufugaji wa kibiashara katika ranchi za taifa hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura wakati wa kusaini mikataba mipya ya uwekezaji katika lanchi ya taifa jijini Dar es Salaam leo.

Wambura amesema kuwa mikataba hiyo mipya itaanza kutumika mara moja hivyo mwekezaji ambaye atakuwa hajasaini mkataba  mpya atahesabika kuwa hana nia tena ya kuendelea na uwekezaji kaika ranchi za taifa.

"Mikataba mipya itaanza kutumika mara moja hivyo mwekezaji ambaye atakuwa hajasaini mkataba  huu mpya atahesabika kuwa hana nia tena ya kuendelea na uwekezaji katika ranchi za taifa na hivyo ataondolewa". amesema Wambura

Amesema kuwa utaratibu wa kuwaondoa wawekezaji ambao hawana mikataba mipya katika ranchi za taifa utaanza kutekelezwa mara moja.

 Kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) iliingia mkataba na wawekezaji kwenye vitalu katika ranchi za taifa na wafugaji wadogo toka 2007 kwa nia ya kuwawezesha wafugaji wa asili kufuga kibiashara.

Hivyo kampuni hiyo imefanya tathimini ya uwekezaji kwa miaka kumi na kubaini kuwa baadhi ya vifungu vya mkataba havina tija kwa kampuni na uwekezaji.
  Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO), Philemon Wambura akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba mipya ya wawekezaji katika ranchi za taifa hapa nchini, kushoto ni Kaimu meneja wa fedha Ranchi za Taifa (NARCO) Nesta Kuza na kulia ni wakili wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Alfred Shanyanga.
 Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura akisaini mikataba mipya ya uwekezaji katika ranchi za taifa jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu meneja wa fedha Ranchi za Taifa (NARCO) Nesta Kuza na kulia ni wakili wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Alfred Shanyanga.
 Baadhi ya wawekezaji wakimsikiliza Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya ranchi za Taifa(NARCO) Philemon Wambura mara baada ya kusaini mikataba mipya ya uwekezaji katika ranchi za taifa.
Baadhi ya wawekezaji wakisaini mikataba mipya ya uwekezaji katika ranchi za taifa. Mikataba hiyo imesainiwa leo Oktoba 10 ambapo ni mwisho wa kusaini mikataba hiyo.

ASILIMIA 86 YA WANAWAKE NA ASILIMIA 100 YA WANAUME WA MKOA WA SHINYANGA WASEMA UMASIKINI NDIO SABABU KUBWA YA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

0
0
Asilimia 86 ya Wanawake na Asilimia 100 ya Wanaume mkoani Shinyanga wanasema kuwa umaskini wa familia ndio chanzo kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira alipokuwa akitoa mada katika Mdahalo wa Kitaifa unaoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu namana bora ya kupambana na ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.

Bi Neema ameongeza kuwa waliamua kufanya utafiti huu mdogo ili kupata kujua uelewa wa jamii ya mkoa wa Shinyanga katika suala la mimba na ndoa za utotoni.

Ameongeza kuwa utafiti huo umefanyika katika Wilaya za Kishapu, Kahama na Shinyanga Mjini ambapo umebaini  kuwa jamii bado haina uelewa kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni na bado vitendo hivi vimekumbatiwa kwenye mwamvuli wa mila na desturi.

“Kwa mujibu wa utafiti huu mdogo tulioufanya tumebaini kuwa umasikini na uelewa mdogo wa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni” alisisitiza Bi. Neema.

Bi Neema ameeleza kuwa Asilimia 11 ya wavulana na  Asilimia 9 ya wasichana  wanaamini kjuwa ni haki kwa mwanaume kumpiga mke wake na wanaamini kuwa mke anapomkosea mume ana haki ya kukubali kupigwa na mume na anakubaliana na hilo  ili kuifanya familia iendelee kukaa pamoja.
 Mwenyekiti wa Mdahalo ambaye pia ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na watoto Dkt. John Jingu (kulia) akiongoza Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Bi Mwajuma Mwagwiza na kushoto ni Muongozaji wa Mdahalo kutoka Shirika la UNFPA Zanzibar Bi. Amina Kheri .
  Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira  akitoa mada katika Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mzee wa Mila kutoka Dodoma Chief Lazaro Masuma akitoa ushuhuda katika eneo analotoka kuhusu suala la ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni katika Mdahalo wa kitaifa unajadilia namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Ngariba Mstaafu Bi.Rahel Masagara akitoa ushuhuda akisisitiza wazazi kutimiza wajibu na majukumyu yao kwa watoto hasa wa kike kuhusu suala la ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni katika Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa Maendeleo na Ustawi wa mtoto nchini wakifuatilia Mdahalo wa kitaifa unaojadili namna bora za mapambano dhidi ya Vitendo vya Ukatili hasa ukeketaji, Mimba na Ndoa za utotoni uliozinduliwa jana  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAFANYAKAZI BENKI YA TIB CORPORATE WAMTEMBELEA MKURUGENZI WA TTCL

0
0
WAFANYAKAZI benki ya TIB Corporate leo wamemtembelea mteja wake ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Waziri Waziri Kindamba.

Wafanyakazi hao wamemtembelea kwajili ya kujitathmini juu ya huduma zao katika wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba kila mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Waziri Waziri Kindamba akizungumza na MICHUZI BLOG amewashukuru benki ya TIB kwa kufanya kazi kwa ufanisi pamoja na uaminifu.

Pia amewapongeza kwa kufika ofisini kwake na ka kufanya kazi kwa vitendo sio kukaa ofisini na kuwashukuru wateja wake.
Mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate, Grace Wilbard akimpa ua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Waziri Waziri Kindamba wakati alipotembelewa na wafanyakazi wa wa benki ya Tib Corporate jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni njia moja wapo ya kusheherekea wiki ya huduma kwa mtaja ambayo hufanyika kila oktoba.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Waziri Waziri Kindamba akizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate jijini Dar es Salaam leo na kuwashukuru kwa kazi wanayoifanya benki hiyo.

Mkurugenzi wa idara ya sheria benki ya TIB Corporate Edward Lyimo  akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Waziri Waziri Kindamba kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya biashara wa benki ya TIB Corporate Mwallu Mwachin'ga Kushoto ni Mkurugenzi idara ya uendeshaji wa benki ya TIB Corporate.
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) Waziri Waziri Kindamba jijini Dar es Salaam leo walipomtembelea ofisini kwake ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mtendaji Mpya Benki ya CRDB abainisha vipaombele vyake

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea mipango na mikakati ya Benki hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela amewahakikishia Wateja, Wanahisa  na Wadau wote wa Benki ya CRDB kuwa Benki hiyo ipo kwenye mikono salama na itaendelea kukua pamoja na kuzalisha faida kama ilivyotarajiwa. Bwana Nsekela aliyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari wenye lengo la kumtambulisha rasmi uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu vipaumbele vyake, Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela alisema kuwa kwa kushirikiana na viongozi na wafanyakazi wa Benki hiyo, amedhamiria kufanya maboresho makubwa katika utoaji huduma kwa wateja kwa kutilia mkazo katika maeneo matano muhimu, ambayo ni uboreshaji wa mifumo na taratibu za  utoaji huduma, ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko, kuongeza weledi na umahiri wa wafanyakazi, kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa, kukuza biashara katika nyanja zote ili kuendana na kasi ya serekali ya awamu ya tano. Atahakikisha Benki inafanya vizuri na kupata faida zaidi ili kutoa gawiwo nono kwa wanahisa.   “Tutakuwa tukiboresha mara kwa mara taratibu za jinsi ya kupata na  kutumia huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki CRDB  uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu” alisema Ndugu Nsekela.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kuzungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Akifafanua zaidi juu ya uboreshwaji wa huduma na mikakati ya Benki ya CRDB  katika eneo hilo muhimu, Ndugu Nsekela alisema kwa kipindi kifupi kijacho Benki ya CRDB  itajikita zaidi kwenye uwekezaji wa mifumo ya kidigitali (innovative products and services)  itakayowezesha kuwafikia wateja wengi zaidi, kwa urahisi zaidi, mahali popote walipo na hivyo kuwaondolea wateja wao ulazima wa kutembelea matawi ya Benki ya CRDB pindi wanapohitaji huduma. “Tutatumia fursa ya kuwa zaidi ya watanzania milioni 19.3 wanatumia simu za mikononi  kufanya miamala yao na kuwashawishi kutumia bidhaa zetu za SimBanking na SIMAccount ambazo nazo  hutoa huduma kama hizo” alisema.

Akiongelea kuhusu mikakati ya kusogeza huduma kwa wateja, Ndugu Nsekela alisema Benki ya CRDB imejiwekea malengo ya kufikisha huduma katika wilaya zote nchini ifikapo mwaka 2022. Na wamejiwekea lengo la kuongeza Mawakala wake wa FahariHuduma katika kila kona ya nchi. Ndugu Nsekela alisema pia Benki hiyo pia ina mpango wa kuendelea kupanua wigo wa huduma zake nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza jambo wakati akiongoza mkutano baida ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Akielezea kuhusu mahusiano baina ya Benki hiyo na Serikali na wadau wengine, Ndugu Nsekela alisema  kuwa  Benki ya CRDB inaitambua Serikali kama Mwanahisha wake na mdau mkubwa wa biashara. “Benki ya CRDB itaendela kuthamini mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na Serikali na taasisi zake na tutaendelea  kubuni huduma na bidhaa mbalimbali mahususi kwa ajili ya kufikia mahitaji ya Serikali pamoja na wafanyakazi wake mmoja mmoja.

Tunajivunia kuwa mmoja wa wadau wakubwa wa Serikali ili kwa pamoja tuweze kujenga uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika kujenga uchumi wa kati wa Viwanda,” alisisitiza Ndugu Nsekela.

Ndugu Nsekela alimalizia kwa kusema hali ya uchumi nchini inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa mabenki nchini huku akibainisha kuwa Benki ya CRDB itaendelea kutia mkazo katika kuhudumia wateja  Wakubwa, Wadogo na wa Kati pamoja na Biashara ya kilimo pamoja na kuwawezesha wawekezaji kwenye sekta ya viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Ndugu Ally Laay alisema Bodi hiyo ina amini kuwa Ndugu Nsekela ni mtu sahihi kabisa wa kuongoza Benki ya CRDB na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha.
Ndugu Laay pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru Dkt. Kimei kwa mchango wake kwa Benki ya CRDB kwa kipindi cha miaka 20 aliyoiongoza. “Ni kazi ngumu sana, lakini Dokta Kimei ameifanya kwa kujitoa na weledi wa hali ya juu sana,” alisema Ndugu Laay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela pamoja na Naibu Wakurugenzi wa Benki hiyo Dorah Ngariga wa Huduma Shirikishi (wa pili kulia) na Kushoto ni Esther Kitoka anayesimamia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.  

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Mkurugenzi Mtendaji Mpya Benki ya CRDB abainisha vipaombele vyake

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea mipango na mikakati ya Benki hiyo katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela amewahakikishia Wateja, Wanahisa  na Wadau wote wa Benki ya CRDB kuwa Benki hiyo ipo kwenye mikono salama na itaendelea kukua pamoja na kuzalisha faida kama ilivyotarajiwa. Bwana Nsekela aliyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari wenye lengo la kumtambulisha rasmi uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu vipaumbele vyake, Ndugu Abdulmajid Mussa Nsekela alisema kuwa kwa kushirikiana na viongozi na wafanyakazi wa Benki hiyo, amedhamiria kufanya maboresho makubwa katika utoaji huduma kwa wateja kwa kutilia mkazo katika maeneo matano muhimu, ambayo ni uboreshaji wa mifumo na taratibu za  utoaji huduma, ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko, kuongeza weledi na umahiri wa wafanyakazi, kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa, kukuza biashara katika nyanja zote ili kuendana na kasi ya serekali ya awamu ya tano. Atahakikisha Benki inafanya vizuri na kupata faida zaidi ili kutoa gawiwo nono kwa wanahisa.   “Tutakuwa tukiboresha mara kwa mara taratibu za jinsi ya kupata na  kutumia huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki CRDB  uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu” alisema Ndugu Nsekela.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kuzungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Akifafanua zaidi juu ya uboreshwaji wa huduma na mikakati ya Benki ya CRDB  katika eneo hilo muhimu, Ndugu Nsekela alisema kwa kipindi kifupi kijacho Benki ya CRDB  itajikita zaidi kwenye uwekezaji wa mifumo ya kidigitali (innovative products and services)  itakayowezesha kuwafikia wateja wengi zaidi, kwa urahisi zaidi, mahali popote walipo na hivyo kuwaondolea wateja wao ulazima wa kutembelea matawi ya Benki ya CRDB pindi wanapohitaji huduma. “Tutatumia fursa ya kuwa zaidi ya watanzania milioni 19.3 wanatumia simu za mikononi  kufanya miamala yao na kuwashawishi kutumia bidhaa zetu za SimBanking na SIMAccount ambazo nazo  hutoa huduma kama hizo” alisema.

Akiongelea kuhusu mikakati ya kusogeza huduma kwa wateja, Ndugu Nsekela alisema Benki ya CRDB imejiwekea malengo ya kufikisha huduma katika wilaya zote nchini ifikapo mwaka 2022. Na wamejiwekea lengo la kuongeza Mawakala wake wa FahariHuduma katika kila kona ya nchi. Ndugu Nsekela alisema pia Benki hiyo pia ina mpango wa kuendelea kupanua wigo wa huduma zake nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza jambo wakati akiongoza mkutano baida ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Akielezea kuhusu mahusiano baina ya Benki hiyo na Serikali na wadau wengine, Ndugu Nsekela alisema  kuwa  Benki ya CRDB inaitambua Serikali kama Mwanahisha wake na mdau mkubwa wa biashara. “Benki ya CRDB itaendela kuthamini mahusiano mazuri yaliyopo baina yake na Serikali na taasisi zake na tutaendelea  kubuni huduma na bidhaa mbalimbali mahususi kwa ajili ya kufikia mahitaji ya Serikali pamoja na wafanyakazi wake mmoja mmoja.

Tunajivunia kuwa mmoja wa wadau wakubwa wa Serikali ili kwa pamoja tuweze kujenga uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika kujenga uchumi wa kati wa Viwanda,” alisisitiza Ndugu Nsekela.

Ndugu Nsekela alimalizia kwa kusema hali ya uchumi nchini inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa mabenki nchini huku akibainisha kuwa Benki ya CRDB itaendelea kutia mkazo katika kuhudumia wateja  Wakubwa, Wadogo na wa Kati pamoja na Biashara ya kilimo pamoja na kuwawezesha wawekezaji kwenye sekta ya viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB Ndugu Ally Laay alisema Bodi hiyo ina amini kuwa Ndugu Nsekela ni mtu sahihi kabisa wa kuongoza Benki ya CRDB na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha.
Ndugu Laay pia alitumia nafasi hiyo kumshukuru Dkt. Kimei kwa mchango wake kwa Benki ya CRDB kwa kipindi cha miaka 20 aliyoiongoza. “Ni kazi ngumu sana, lakini Dokta Kimei ameifanya kwa kujitoa na weledi wa hali ya juu sana,” alisema Ndugu Laay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela pamoja na Naibu Wakurugenzi wa Benki hiyo Dorah Ngariga wa Huduma Shirikishi (wa pili kulia) na Kushoto ni Esther Kitoka anayesimamia Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, Jijini Dar es salaam, Oktoba 10, 2018.  

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MTWARA KUVUNA VIBE KAMA LOTE MSIMU HUU WA TIGO FIESTA 2018

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {Katikati} akiongea na waandishi wa Habari {Hawapo Pichani} kuhusiana na fursa mbalimbali za biashara zinatazopatika katika mkoa huo kutokana na ujio wa tamasha la Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama Lote linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ya wiki katika viwanja vya Nangwanda Sijaona. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa na Mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta, Pancras Mayalla {almaarufu Askofu TZA}.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa {Kulia}akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {katikati}pamoja na Mratibu wa Tigo Fiesta 2918 , Pancras Mayalla almaarufu Askofu TZA katika Mkutano na waandishi wa habari kueleza maandalizi ya tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika uwanja wa Nang'wanda Jumapili hii pamoja na ofa mbali mbali za kampuni ya Tigo katika msimu huu ikiwemo mfumo wa malipo kwa wakulima wa korosho kupitia huduma za Tigo Pesa.

Huku msimu wa mavuno ya korosho ukiwa umewadia katika mikoa ya nyanda za juu kusini, wakaazi wa Mtwara na viunga vyake wanajiandaa kuvuna vibe kama lote kutoka kwa mastaa wa muziki wa bongo flava katika msimu unaoendelea wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote.

Waandaaji Clouds Media Group, kupitia Katibu Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi, Gardner Habash amewaalika wakaazi wa Mtwara waje kupumzika baada ya shughuli ngumu za kuvuna korosho kwa kusikiliza 100% vibe za nyumbani.

‘Kwa wafanya biashara, msimu waTigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ni fursa ya kujiongezea kipato kwa kutoa huduma za usafiri, malazi, vinywaji na chakula na huduma nyingenezo zinazohitajika na maelefu ya mashabiki watakaojitokeza kushuhudia tamasha hili,’ Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byanakwa alisema.

Kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota, wasanii wanaochipuka kutoka Mtwara watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao, na wale watakaofanya vizuri watapewa fursa ya kutumbuiza katika tamasha kuu la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kurindima siku ya Jumapili tarehe 14 Oktoba katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz . Watakaoshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Iringa. 

Wengine ni wasanii a bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva. TIketi za Tigo Fiesta 2018 – Mtwara zinapatikana kwa bei punguzo ya TSH 5,000 kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika cha TSH 5,000 kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888. Tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote tayari limezuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga na Iringa, na linatarajiwa kutembelea mikoa ya Singida, Songea, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku fainali ikiwa Dar es Salaam.

MULTICHOICE YAZINDUA RASMI KITUO CHA MAFUNZO YA UANDAAJI FILAMU AFRIKA MASHARIKI

0
0
MultiChoice Africa imezindua rasmi kituo cha mafunzo ya uandaaji wa filamu  katika ukanda wa Afrika Mashariki . Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika mjini Nairobi nchini Kenya katika makao makuu ya ofisi ya MultiChoice na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu pamoja na wawakilishi mbalimbali wa serikali  kutoka katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria katika uzinduzi huo mjinji Nairobi ni pamoja na Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasiliano Kenya, Mhe. Joe Mucheru, Katibu wa Wizara ya Habari na Mawasilano Kenya, Bi Fatma Hirsi, Mwenyekiti wa Baraza la Filamu nchini Kenya Chris Foot, Mwenyekiti wa bodi ya Filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua, Kaimu Mkurugenzi Mkuu KBC Paul Jilani, wajumbe wa kamati ya bunge ya ICT kutoka Kenya akiwemo mheshimiwa John Kiarie huku Tanzania ikiwakilishwa kwa heshima kubwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza.

Akizingumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Mkurugenzi wa MultiChoice Kanda ya Afrika Kaskazini.Maharage Chande alisema, “Tunaamini kuwa kuanzishwa kwa programu ya hii, kutatuhakikishia muendelezo wa utamaduni wetu waafrika wa kutoa hadithi zetu kwani huo umekuwa ni utamaduni wetu toka enzi na enzi. Ni katika utamaduni huu huu wa kiafrika, sasa tunapanda mbegu hii kwa vijana ili kuuendeleza utamaduni wetu huu adhimu kwa kizazi kipya na kijacho.

Tutambue kuwa uhai wa utamaduni huu unategemeana na kutengenezwa kwa fursa za kukuza weledi na umahiri katika uzalishaji wa kazi za kisanii zinazoakisi historia, mila, desturi na tamaduni zetu na kuhakikisha kuwa weledi na umahiri huo unaendelezwa. Naamini kuwa kwa kupitia programu hii ya MultiChoice Talent Factory ndoto yetu hii itatimia. “ alisema Maharage.

Vijana hawa 20 wa Afrika ya Mashariki , 4 kati yao kutoka Tanzania akiwemo Sara Kimario (25) Chalinze, Jamali Kishuli (23) Arusha, Wilson Nkya (24) Kigoma na Jane Moshi (25) Kilimanjaro wataanza rasmi programu hii ya mafunzo ya miezi 12 mapema mwezi huu  ambapo wataunganishwa na wataalamu waliobobea tasnia hii sambamba na mitaala iliyokidhi viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Teknolojia na Mawasilano nchini Kenya Mhe. Joe Mucheru, ameipongeza Kampuni ya MultiChoice kwa jitihada zake  hususani katika kuwekeza na  kuwainua na kukuza vipaji vya vijana wa kiafrika  kupitia  tasnia hii ya filamu. Alisema , “Nina imani  kuwa program hii itakuwa ni chachu kubwa katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu katika kanda yetu ya Afrika Mashariki. 

Ninaamini kupitia ujuzi watakaopatiwa vijana hawa watakuwa na uwezo wa kutengeneza kazi zenye ubora wa hali ya juu, wataweza kujiajiri wao wenyewe na pia watakuwa waalimu wa wenzao ambao wanavipaji katika tasnia hii. Ni matumaini yangu kuwa  darasa hili la 2018 litakuwa mfano wa kuigwa  kwa vizazi vijavyo ambao wangependa kuwa katika tasnia hii”, alisema Joe Mucheru.

“Kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 tumekuwa tukitumia nguvu nyingi katika kuongeza ubora na viwango vya kazi zetu bila mafanikio tuliyokuwa tukiyatarajia. Huu ni wakati sahihi kwetu kujiuliza swali hili, Ni njia gani sahihi inayotupasa kutumia ili kuongeza ubora katika kazi zetu”, Alisema Njoki Muhoho Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo filamu cha MultiChoice Afrika ya Mashariki.

WAZIRI NDALICHAKO: SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAENZI YALE YOTE ALIYOISHI MWALIMU NYERERE

0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema falsafa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zimepata msukumo wa hali ya juu katika serikali ya awamu ya tano kwa kuwataka watanzania kufanya kazi kwa bidii.

Prof Ndalichako amesema hayo leo Mapema Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua kongamano la Siku mbili katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni  lililokuwa na Mada inayosema  'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa la Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'

"Mwalimu Nyerere alisisitiza kufanya kazi kwa bidii na udalifu na kusimamia msingi wa uzalendo kwani Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dk. John Magufuli ameweza kusimamia neno la hapa kazi tu ambalo ni moja ya Falsafa ya Mwalimu Nyerere iliyosema kuwa kufanya kazi kwa bidii , Kazi ni Uhai na Kazi ni Utu hivyo tunapaswa kujiuliza hii falsafa ina umuhimu gani katika kufanikisha kuelekea nchi ya uchumi wa Viwanda"

Prof Ndalichako amesema kuwa kuna mambo mengi yanafanywa na Serikali ya awamu ya tano  ambayo yalianzishwa na Baba wa Taifa wa Mwalimu Nyerere hivyo hii falsafa iweze kuangaliwa ni namna gani itaweza kuleta mchango wa Maendeleo ya Viwanda katika Taifa hili kwani mada iliyochaguliwa ina akisi msisitizo wa serikali yetu.

Alisema kuwa nia ya Serikali hii ni kuendeleza miradi Mikubwa ambayo ndio Msingi wa kufikia Maendeleo ya Haraka kama ujenzi wa mardi mkubwa wa umeme wa Stiglizers  Gorge ambao utasaidia kuzalisha umeme mkubwa katika nchi hii  ambayo ni Nishati Muhimu

Alimaliza kwa kuwataka watanzania kuunga mkono Juhudi za Rais wetu ambaye amekuwa kipaumbele katika kusimamia rasilimali za Taifa hili tuweze kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati hivyo waswahili usema 'penye nia pana njia'
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamno la Kumbukumbu la kuenzi kazi zilizofanywa na Mwalimu Nyerere lilolikuwa linahusu 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa la Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
 Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,Mashavu Fakih akizungumza kabla ya kumkalibisha mgeni rasmi
 Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof. Shadrack Mwakalila akizungumza na watu waliofika katika kongamno hilo.
 Baadhi ya Viongozi Wastaafu walioshiriki katika Kongamano hilo la 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dr .Bashiru Ally Bashiru akifatilia Mdahalo wa 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda' uliofanyika katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Magogoni Dar es Salaam
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la 'Falsafa ya Mwalimi Nyerere Juu ya Taifa Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda'

KAMATI YA UKUMWI YAKUTANA NA WIZARA YA UJENZI KUJADILI UINGIZWAJI WA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

0
0

 Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI ikiwa katika kikao Jijini Dodoma ambapo leo wamepokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu Udhibiti wa Uingizaji wa Dawa za Kulevya kwenye maeneo ya Bandari, Fukwe, Barabara Kuu na Viwanja vya Ndege.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Mhe. Oscer Mukasa akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye. Kamati hiyo leo ilipokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu Udhibiti wa Uingizaji wa Dawa za Kulevya kwenye maeneo ya Bandari, Fukwe, Barabara Kuu na Viwanja vya Ndege katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye akijibu hoja za Wajumbe wa  Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Oscer Mukasa na pembeni ni Katibu wa Kamati Ndg .Agnes Nkwera. Kamati ya Masuala ya UKIMWI  imepokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu Udhibiti wa Uingizaji wa Dawa za Kulevya kwenye maeneo ya Bandari, Fukwe, Barabara Kuu na Viwanja vya Ndege katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

MTANDAO WA ELIMU WA TESEApp WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Muanzilishi wa mtandao wa Elimu wa Tesea Abdul Mombokaleo amesema kuwa msingi wa kuanzishwa kwa mtandao wa Tesea ni kurahisisha upatikanaji wa marejeo(notes) kwa wanafunzi kujifunza na kupata elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Amesema mtandao huu utakuwa na marejeo(notes) zote za kutosha na ambayo yame hakikiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania ili kusaidia wanafunzi kupata marejeo yanayotakiwa katika masomo yao.“mtandao huu hauchukui nafasi ya mwalimu bali utamsaidia mwalimu kuandaa masomo kwa urahisi kwani notes hizo zinafata mtaala wa serikali kwa kuwa na silabasi zote zinazotakiwa kwa mwanafunzi kujifunza awapo shuleni”. amesema Mombokaleo

Amesema mtandao huo unaopatika kupitia simu za smartphone,laptop,tablet na computer za mezani na unaweza kupakuliwa kiurahisi na mwanafunzi kijisali na kuanza kutumia mtandao kwa gharama nafuu,na kupata masomo yote ya biashara,sayansi na elimu za dini ya kiislamu na kikristo pamoja na mitihani iliyopita (pastpapers).

Kwa upande Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa taifa wa wamiliki wa shule binafsi nchini Charles Totera, amesema kuwa elimu inatakiwa kumsaidia mtu kuweza kutatua matatizo yake bila kusubiri msaada kutoka kwa mtu mwingine kwa uwezo wake wa kufikiri kutokana na elimu aliyonayo.
  Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 – 4) na (kidato 5 – 6) akiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp. 
Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 – 4) na (kidato 5 – 6) akiwa na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.

Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo wa kulia akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.

MKUU WA MAJESHI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA

0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo  akizungumza mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gaurge kutoka kituo cha Ilala hadi kituo cha Soga.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akimsikiliza maelezo kutoka kwa Wafanyakazi wa kampuni iliyojenga reli ya mwendokasi ya Yapi Markez jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli hiyo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo  pamoja na baadhi ya wanajeshi wakiangalia jinsi mataaluma yanavyotengenezwa katika kituo cha Soga.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo  akizungumza na waandishi wa habari  katika kituo cha soga mara baada ya kutembelea na kukagua jinsi mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa standard george.
Baadhi ya mataaluma kushoto yakiwa tayari kwa kutandikwa reli ya kisasa ya standard gaurge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa  akitoa maelezo kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance  Mabeyo wakati alipoembelea ujenzi wa reli ya kisasa ya standarge gaurge.
Sehemu ya reli ambayo imekamilika.
Picha na Avila kakingo,Globu ya Jamii

Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana

0
0
Serikali imejipanga kuboresha upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa (Green house).  

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoa wa Songea na Iringa ili kuhamasisha na kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujenga vitalu nyumba (Green house) kwenye Mikoa hiyo.

Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali imeamua kuanzisha mradi huo ili kuhakikisha vijana wanafikiwa kwa idadi kubwa na kuwawezesha kupata ujuzi na ajira kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa itakayowawezesha kujipatia kipato.

“Teknolojia hii itawawezesha vijana kulima katika eneo dogo, kupata mazao kwa wingi na kuweza kuyauza, vilevile kutumia eneo hilo kuweza kuajiri vijana wengine kwani asilimia zaidi ya 60% ya watu wanaojiajiri na kujishughulisha inatokana na na mashamba.” alisema Mhagama

Ameongeza kuwa vijana watafundishwa teknolojia hiyo ya kilimo cha kitalu nyumba ili iwawezeshe kuongeza thamani ya mazao watakayozalisha.

Aidha, Waziri Mhagama aliziagiza halmashauri zote kujipanga haraka katika utayarishaji wa miundombinu kwenye maeneo hayo na kuhakikisha vijana wanaandaliwa mapema pamoja na kuanzishiwa Vyama vya Ushirika (AMCOS) kwani  wananchi wapo tayari kuona mradi huo unaanza kufanya kazi mapema.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na viongozi na watendaji (hawapo pichani) alipowasili Halmashauri ya Mufindi, Mkoani Iringa kwa ajili ya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Vijana na Wananchi wa Songea, alipofanya Ziara ya kikazi mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara  Mkoa wa Iringa kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
 Baadhi ya Viongozi na Watendaji kutoka Halmashauri ya Mufindi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa Wilayani hapo kwa ziara ya kikazi kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba. (Kulia ni) Afisa Kazi, Bi. Neema Moshi na Katibu wa Waziri Bw. Raymond Kaseko, wote kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA MKOANI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kibakwe wilayani Mpwampwa, akiwa kwenye ziara mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Binilith Mahenge, akizungumza na wananchi wa Kibakwe wilayani Mpwampwa, kwenye ziara ya Waziri Mkuu mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
 Mke wa Waziri Mkuu Marry Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Kibakwe wilayani Mpwampwa mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018.
 Wananchi wa Kata ya Kibakwe wilayani Mpwampwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati  akiwahutubia wananchi hao, akiwa kwenye ziara mkoani Dodoma, Oktoba 10, 2018. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Maonesho ya kimataifa ya Utalii ya  Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14.

Maonesho hayo yameandaliwa na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) yatafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC yakiwa na lengo la kuwaunganisha wafanyabishara wadogo na wa kati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabishara kutoka masoko makuu ya utalii duniani yameweza kudhaminiwa na wadhamini kadhaa wakiongozwa na Tanzania Ocean Cruisng and Safaris Ltd.

Akizungumzia maandalizi kueleka maonesho ya mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa maandalizi yamekaamilika kwa asilimia kubwa na mgeni rasmi akitaraiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Amesema kuwa, maonesho hayo yatakuwa yanafunguliwa kuanzia saa nne asubuhi nna kufungwa saa 12 jioni na huduma mbalimbali zitakuwa zinafanyika ikiwemo bidhaa za utalii, semina zitakazokuwa zinaendelea ambapo jumla ya mada 24 zitawasilishwa na watalaamu waliobobea kwenye masuala ya utalii.

Devotha amesema kuwa,maonesho  yatajumuisha jumla ya mataifa  27 kutoka nje ya Afrika na mataifa 15 ya ndani ya Afrika  na zote zitaleta bidhaa zao za utalii na pia kuhudhuriwa na vyombo vya habari 300 duniani.

"Maonesho haya yatahudhuriwa na mataifa 42, mataifa 15 yakiwa ni kutoka Afrika kama vile Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Congo, Malawi, Namibia, Zimbabwe, Ghana, Cote D'ivoire, Nigeria, Malawi, Tunisia, Misri na Afrika Kusini huku mataifa mengie 27 kutoka  nje ya Afrika nayo yatashiriki  wakiwemo Marekani, Canada, Sweden, Italy, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Ubelgiji, Australia, India na nchi zingine"amesema Devotha.

 Amesema kuwa  katika maonesho hayo pia kutakuwa na vyakula vya kiasili vitakavyopikwa hapo hapo na wanafunzi  kutoka vyuo vya utalii nchini
ili washiriki na wageni wawezse kufahamu vyakula vya kiutamaduni nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akizungumza na waandishi wa habari maandalizi ya kuelekea maonesho ya kimataifa ya Utalii ya  Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14. Kulia ni Meneja Mauzo na Masoko  wa Tanzania Ocean Cruising Safaris Christine Jengo na kushoto ni Meneja wa Ukumbi wa Kimataifa wa JNICC Assah Mwambene.


 Maandalizi ya mabanda ya maonesho ya Maonesho ya kimataifa ya Utalii ya  Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14  kwenye ukumbi wa kimataifa wa JNICC

WAWEKEZAJI WA RANCHI YA TAIFA WATAKIWA KUSAINI MIKATABA MIPYA


MAWAZIRI WA SEKTA YA KILIMO WATUAMA JIJINI DODOMA KUJADILI UTEKELEZAJI WA ASDP AWAMU YA PILI

0
0
Na Mathias Canal, WK-Dodoma
Mawaziri wa wizara za sekta ya kilimo leo tarehe 10 Octoba 2018 wametuama kwa masaa kadhaa Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kujadili kwa kina kuhusu maandalizi ya utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Wizara washirika katika kutekeleza ASDP II ni pamoja na Wizara ya kilimo, Wizara ya mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Utekelezaji wake utachagizwa pia na Wabia wa maendeleo, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima, Wafugaji na Wavuvi.Mawaziri hao wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) wameridhia kwa pamoja kuanza haraka utekelezaji wa mradi huo wa ASDP II ambao utakuwa chachu ya ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo.

Majadiliano hayo yalijikita zaidi kujadili mapendekezo ya kikao cha makatibu wakuu wa wizara za sekta ya kilimo kilichofanyika tarehe 30 Agosti 2018 pia kujadili namna bora ya Uratibu wa ASDP II, na Mikakati ya kutafuta fedha za kugharamia utekelezaji wa ASDP II.

Katika Mkutano huo Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) aliitaka timu ya ASDP II Taifa kueleza kwa kina mikakati ya kuboresha masoko ya mazao ya kipaumbele yaliyoainishwa katika utekelezaji wa ASDP awamu ya pili.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Kutoka kushoto ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Willium Lukuvu (Mb), Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) na Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji wakifatilia kwa umakini kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akieleza umuhimu wa kuanza haraka utekelezaji wa ASDP II wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Willium Lukuvu (Mb), akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018. Mwingine ni Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba.

Total kuwatunuku vijana katika ubunifu wa mawazo ya Biashara

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya Mafuta ya Total imeazisha shindano la  Startupper of the Year Challenge kwa ajili  wabunifu wa mawazo ya biashara na kupata  fursa ya ya mtaji pamoja na mafunzo maalumu kwaajili ya uendeshaji wa biashara hizo. 

Shindano hilo la pili kufanyika nchini linaloendeshwa na Kampuni ya Mafuta  ya Total Tanzania na limewalenga vijana wenye mawazo ya biashara na miradi inayoweza kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zao ikiwemo biashara hizo zilitokana na mawazo ziweze kukua.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa Shindano hilo, Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya  Total, Thomas Biyong amesema mbali na Tanzania shindano hilo litafanyika katika nchi 40 katika Bara la  Afrika ikiwa ni mpango wa kuinua kazi za ubunifu na kuwa endelevu katika mapinduzi ya biashara.

"Mawaz ya Miradi hiyo itapimwa kulingana na wazo la ubunifu wa asili, umuhimu kwa jamii pamoja na uwezekano wa mradi kuwa endelevu," amesema.

Naye, Mkurugenzi wa Sheria na  Mahusiano wa Kampuni hiyo, Marsha Kileo amesema wabunifu watakaoshiriki wanatakiwa kuwa na biashara ya isyozidi miaka miwili au chini pamoja na wale wenye mawazo mapya.

"Washiriki wetu wa shindano  watakaopatikana  watapata mafunzo maalumu juu ya uendeshaji, uangalizi  na namna ya kuboresha biashara zao,"amesema.

Ametaja masilahi ya washindi watatu watakaopatikana wa Kwanza atapata Kiasi cha Sh.Milioni 30,wa pili Sh. milioni 20 pamoja na mshindi wa tatu atapata Sh.milioni 15 kwaajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi watakayoibuni hapa nchini.
Amesema utaratibu wa kutuma katika tovuti ya Total ambayo imefunguliwa Oktoba Tisa na kuisha Novemba Mwaka huu.

Shindano la kwanza lilifanyika mwaka 2015 ambapo Iddi Kalembo kutoka Mtwara aliibuka mshindi kwa mradi wake wa upigaji picha kwa njia ya simu hasa vijijini.

Mshindi wa tatu Krantz Mwantepele ambaye ndiye mlezi wa shindano hilo amesema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu kwani kwa mawazo yao wanaweza kushinda na kupata mtaji wa kuendeleza Biashara zao.
Amesema aliposhinda nafasi ya tatu amepata fursa za kutosha ikiwa ni pamoja na kuendeleza biashara yake.
 Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Total Thomas Biyong akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa shindano la Start upper of the year Challenge uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa Total Marsha Kileo akizungumza kuhusiana jinsi uwasilishaji wa mawazo yao katika tovuti yao kwa muda uliowekwa.
Mlezi wa Shindano hilo Krantz Mwantepele akizungumza kuhusiana na ushindi wake wa awamu ya kwanza na namna akuvyonufaika.

IGP APOKEA KAMERA MAALUM KUSAIDIA MAPAMBANO YA UHALIFU

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea kamera maalum (Drons) kutoka kwa Mwakilishi wa kampuni ya Kifaru Ifigenia Anselmi walipokutana Makao Makuu ya Polisi ambapo kampuni hiyo imetoa kamera tatu kwa ajili ya kusaidia mapambano ya uhalifu hapa nchini (Picha na Jeshi la Polisi).

MWENDOKASI WAJITETEA, WADAI WANAHUJUMIWA...MADEREVA WAO WAKIMBIA NA FUNGUO

KADA CCM AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTUHUMA ZA KUISHI NCHINI BILA KIBALI

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Michael Mlowe maarufu kwa jina la Mayko Namlowe (44)  anayeishi Iringa eneo la Lugalo Kihesa leo Oktoba 10 2018 amefikishwa  Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu.

Kada huyo wa CCM anakabiliwa na mashtaka ya kuishi nchini bila kibali na kutoa maelezo ya uongo.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji, Novatus Mlay amedai, mshtakiwa Namlowe ambaye pia ni mfanyabiashara anadaiwa kuwa  Mei 31 mwaka 2018  katika Makao Makuu ya Ofisi ya Uhamiaji iliyopo wilayani Temeke akiwa raia  wa Uingereza alikutwa akiishi nchini bila ya kuwa na Visa(hati ya kusafiria) ama nyaraka yoyote inayomwezesha kufanya hivyo.

Katika shtaka la pili la kutoa maelezo ya uongo, ambapo imedaiwa Mei 31, mwaka huu katika ofisi hizo za uhamiaji mshtakiwa alitoa maelezo ya uongo kuhusiana na uraia wake raia na kufanikiwa kujipatia kitambulisho cha uraia namba 19741219_51108_00001_24 ambacho kina jina la Michael Juma Mlowe wakati akijua alichokifanya ni kosa.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo na hakimu Mmbando amemtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika wenye barua na vitambulisho.

Mshtakiwa huyo anayetetewa na Wakili Kashindye Thabiti amekamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa huru.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Kesi imeahirishwa hadi Novemba 11, mwaka huu.
 Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Michael Mlowe maarufu kwa jina la Mayko Namlowe (44) akiingia katika mahakama ya hakimu mkazi jijini Dar es Salaam leo.  
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Michael Mlowe maarufu kwa jina la Mayko Namlowe (44) akitoka katika mahakama ya hakimu mkazi jijini Dar es Salaam leo. Kada huyo wa CCM anakabiliwa na mashtaka ya kuishi nchini bila kibali na kutoa maelezo ya uongo.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images