Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

OLE NASHA ATOA AGIZO KALI KWA VIONGOZI NA WAZAZI MKOANI MANYARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kote kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba, kwani kufanya hivyo kunawaondolea fursa ya kuendelea na masomo pindi wanapofaulu.

Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Hakikisheni watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha kuwa wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo “alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

Kiongozi huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa, ikizingatiwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipokelewa na Watendaji wa Mkoa wa Manyara wakati alipowasili mkoani hapo kwa ajili ya kupata taarifa ya Elimu ya Mkoa huo. Naibu waziri huyo yuko Mkoani Manyara kwa ziara ya siku tatu ikiwa ni muendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuangalia hali ya Elimu katika mkoa husika.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa maelekezo kwa Viongozi na watendaji wa VETA Manyara wakati wa kukagua karakana inayotumika na wanafunzi wanaosoma kozi ya ufundi wa zana za kilimo (Agro Mechanics).

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa karakana itakayotumiwa na wanafunzi wanaosoma kozi ya ufundi uwashi katika Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Manyara. 



SERIKALI KUANZISHA KURUGENZI YA KUSIMAMIA FUKWE KWA AJILI YA UTALII

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inatarajia kuanzisha Kurugenzi ya kusimamia fukwe za bahari kwa ajili ya kupanua wigo wa mapato yatokanayo na sekta ya  utalii .

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ameyasema hayo leo  wakati alipotembelea makao makuu ya Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) jijini Dar es Salaam ambapo amezungumza na watumishi wa bodi hiyo na kuwataka wawe wabunifu katika kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi.

Amesema licha ya kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na fukwe nyingi lakini fukwe hizo zimekuwa hazitumiki ipasavyo katika kuliingizia taifa mapato kupitia utalii.

Amefafanua kuwa Kurugenzi hiyo itakayoundwa itakuwa na jukumu la kusimamia fukwe zote nchini ikiwa pamoja na  kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji ili waweze kuziboresha kwa ajili ya watalii wa ndani na nje ya nchi

Pia ametoa wito kwa Wawekezaji wenye nia ya kutaka  kuwekeza kwenye fukwe hizo ambazo zitakuwa zikisimamiwa na Kurugenzi hiyo  wakae tayari kwa ajili ya  kuchangamkia fursa hiyo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Hasunga   amewataka watumishi hao wawe wabunifu badala ya kuendelea kulalamika kuwa  bajeti ya kujitangaza haitoshi

Hata hivyo, Naibu Waziri Hasunga amesema  anatambua kuwa bajeti wanayopewa  haitoshi katika kujitangaza lakini  ni lazima waje na njia  mbadala ya kuhakikisha kuwa bajeti hiyo hiyo ndogo inaleta matokeo makubwa.

Aidha, Amewataka wasijikite pekee katika kusafiri kwenda katika  maonesho ya  kimataifa  badala yake watumie njia nyingine za kujitangaza kwa kuanza   kuhamasisha utalii wa ndani mashuleni na vyuoni.

Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano, TTB itumie fursa hiyo kujitangaza kwa gharama ndogo lakini matokeo yake yawe makubwa. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devotha Mdachi amemueleza Naibu Waziri Hasunga kuwa licha ya ufinyu wa bajeti wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutangaza vivutio vya utalii na watazidi kubuni njia nyingine za kutangaza kwa gharama ndogo zaidi.

Amesema kutokana na  umuhimu wa kutangaza vivutio vya utalii, TTB imeandaa Onesho la Swahili International Expo ambalo litaanza Oktoba 12 mwezi huu ambapo jumla ya Washiriki 170 kutoka nje za nchi watashiriki.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea makao makuu ya Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) jijini Dar es Salaam ambapo amezungumza na watumishi wa bodi hiyo na kuwataka wawe wabunifu katika kutangaza vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi.

Wachimbaji Wadogowadogo Watakiwa Kuzingatia Taratibu Upatikanaji wa Leseni

$
0
0
  Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko akizungumza na mamia ya wachimbaji wadogowadogo wa madini katika mgodi wa madini ya Rubi uliopo katika kijiji cha Kitwai A wilayani Simanjiro mkoani Manyara leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Zephania Chaula akizungumza wakati wa mkutano baina ya Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Wachimbaji wadogowadogo wa madini katika mgodi wa madini ya Rubi uliopo katika kijiji cha Kitwai A wilayani Simanjiro mkoani Manyara leo.
  Mhandisi Edward Joseph toka Tume ya Madini akijitambulisha  wakati wa mkutano baina ya Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Wachimbaji wadogowadogo wa madini katika mgodi wa madini ya Rubi uliopo katika kijiji cha Kitwai A wilayani Simanjiro mkoani Manyara leo.

 Baadhi ya wananchi pamoja na wachimbaji wadogowadogo wakifuatilia mkutano baina yao na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko (hayupo pichani) kilichofanyika jana katika eneo la machimbo ya madini aina ya Rubi katika eneo la Kitwai A wilayani Simanjiro mkoani Manyara leo.
 Mmoja ya wakazi wa kijiji cha Kitwai A, Alaiharwa Lenae akiwasilisha hoja kwa niaba ya jamii ya wafugaji mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko (hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara kufuatia ziara ya Naibu Waziri huyo kutembelea eneo la mgodi wa uchimbaji madini ya Rubi uliopo katika kijiji hicho wilayani Simanjiro mkoani Manyara jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Dkt Kalemani aendelea kuwasha umeme vijijini

$
0
0

Katika kuhakikisha kuwa  adhma ya Serikali ya kusambaza umeme katika vijiji vyote  nchini ifikapo mwaka 2021 inatekelezwa, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara  katika Wilaya ya Handeni na Lushoto mkoani Tanga ili kukagua kazi za usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji.
Akiwa wilayani Handeni, Waziri wa Nishati aliwasha umeme katika Kijiji cha Madebe, Nyasa  na Kwamnele na wilayani Lushoto aliwasha umeme katika Kijiji cha Mabugai na Nkelei.
Aidha alifanya ziara katika kata na Vijiji mbalimbali ambavyo bado havijasambaziwa umeme ikiwemo Kijiji cha Mahezangulu kilicho katika Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto ambapo aliagiza kuwa, kiwashiwe umeme ifikapo tarehe 12 mwezi huu.
Katika ziara yake wilayani Handeni, Viongozi wa Wilaya hiyo walimweleza kuwa, kuna vijiji 10 ambavyo vimepitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina nishati hiyo, hivyo kuleta malalamiko miongoni mwa wananchi kuwa walitoa maeneo yao kupisha miundombinu hiyo lakini hawapati umeme.
Kuhusu suala hilo, Dkt Kalemani aliagiza kuwa, kuanzia Jumatatu ya tarehe 8 Oktoba, 2018 wataalam wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) waanze utaratibu wa kupeleka umeme katika Vijiji hivyo kwani kinachohitajika ni kusambaza tu umeme kwa wananchi hao kwa kuwa miundombinu ipo.
Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani alitoa onyo kuwa, Meneja yeyote wa TANESCO atakayeonekana anatetea wakandarasi wanaochelewesha kazi kwa kisingizio cha kutokuwa na vifaa atakuwa amejihesabia kuwa kashindwa kazi.
“ Hawa wakandarasi tayari wameshalipwa fedha za kuwawezesha kuanza kazi ya usambazaji umeme vijijini, hivyo wanatakiwa kuwa na vifaa vyote vinavyohitajika katika kazi hii,” alisema Dkt Kalemani.
Vilevile aliwataka watumishi kuwa na lugha ya staha pale wanapohudumia wananchi na kueleza kuwa atakayeshindwa kufanya hivyo ataondolewa katika nafasi yake.
Ziara ya Dkt Kalemani wilayani Handeni na Lushoto ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya hizo, Wabunge, Madiwani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Pili kushoto) akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Madebe wilayani Handeni mkoani Tanga. Wa Pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi kifaa cha UMETA, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Waziri wa Nishati alitoa vifaa vya Umeta 30 kwa Mbunge huyo ili kuwawezesha wananchi kuunganishwa na huduma ya umeme bila kutandaza nyaya ndani ya nyumba.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwasalimia wananchi katika Kijiji cha Mahezangulu katika Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mara baada ya kufika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nkelei  wilayani Lushoto ambapo pia alizindua huduma ya umeme katika Kijiji hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizidua rasmi huduma ya upatikanaji wa umeme katika Kijiji cha Mabugai wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga.

TRC yarejesha eneo lake baada ya wananchi kuvamia kinyume na Sheria.

WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

$
0
0
IMEELEZWA kuwa kukamilika mapema kwa barabara za lami na madaraja ya kisasa katika mkoa wa Ruvuma kutauunganisha kirahisi na mikoa ya nyanda za juu kusini na nchi za jirani na hivyo kuhuisha uchumi wa wakazi wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema hayo alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 na kumtaka mkandarasi china Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO), anayejenga barabara hiyo kuikamilisha kwa wakati.
Amesema fursa za kilimo, uvuvi, usafirishaji na uchukuzi wa mazao na makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma zinahitaji barabara za lami na zenye uwezo wa kupitika wakati wote na kwa urahisi hivyo kukamilika kwa barabara za lami kwa wakati kutaleta ukombozi kwa wananchi wa mkoa huo.
“Viwanda vingi sasa vinatumia makaa ya mawe tena kwa kiwango kikubwa hivyo tunahakikisha usafiri katika mkoa huu unakuwa wa uhakika ili kuufungua na kuunganisha na mikoa mingine kwa njia fupi  na  hivyo kuongeza biashara ya ndani kuvutia biashara na nchi za jirani”, amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesisitiza kuwa  Serikali imejipanga kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara za Ikuyufusi –Mkenda,  Kitae-Lituhi KM 84.5, Lituhi –Mbamba Bay KM 112.5 na kukamilisha kwa wakati daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia Ludewa ili kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi mkoani Ruvuma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), mara baada ya kukagua kivuko cha Mv. Ruhuhu kinachotoa huduma kwa wakazi wa Wilaya za Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma na Ludewa mkoani Njombe.
 Muonekano wa makaa ya mawe katika kijiji cha Ikuyufusi, Serikali imeamua kujenga barabara ya lami kati ya Ikuyufusi na Mkenda ili kuwezesha shughuli za uchukuzi wa rasilimali hiyo mkoani Ruvuma kutekelezeka kikamilifu. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Ruvuma.
Muonekano wa mtambo wa kusaga kokoto kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 66 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Ruvuma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AWAONYA WALIMU KUTOJIHUSISHA NA WIZI WA MITIHANI

$
0
0
*Asisitiza kwamba vitendo hivyo vinawadharirisha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya maafisa elimu na walimu kutojihusisha na vitendo vya wizi wa mitihani vinavyofanywa kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kwa sababu vinawadharirisha.

“Kama kweli umemuandaa mtoto huna sababu ya kuiba mitihani na mtoto hawezi kufikiria kuiba mitihani kwa sababu yuko nje ya mfumo. Walimu heshimuni maadili ya kazi ya ualimu.”

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumanne, Oktoba 9, 2018) baada ya kukabidhiwa vyumba vya madarasa vya shule za msingi Nyakato na Kashozi, wilayani Bukoba.

Vyumba hivyo vilivyojengwa kwa msaada wa Serikali ya Japan baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka 2016.

Waziri Mkuu amesema tathmini ya elimu katika shule za msingi na sekondari hufanyika kwa kufanya mitihani, dosari ya udanganyifu wa mitihani iliyojitokeza katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu isijirudie tena.

Wiki iliyopitaBaraza la Mitihani la Taifa (NECTA) lilifuta matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa shule za msingi zote za Halmashauri ya Chemba na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuvujisha mitihani.

Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imechukua hatua kali kwa watu wote walioshiriki katika kitendo hicho kwa sababu kinadumaza uelewa na ufikiri kwa wanafunzi, hivyo kuwaandaa watoto kuwa wategemezi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe ikiwa ni ishara ya kupokea madarasa mapya yaliyojengwa kwa Masada wa serikali ya Japan katika Shule ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 8, 2018. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini,    Katsutoshi Takeda. Majengo ya shule hiyo yaliharibiwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikata utepe ikiwa ni ishara ya kufungua madaras mapya yaliyojengwa kwa Masada wa serikali ya Japan katika Shule ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 8, 2018. Kushoto ni Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini,    Katsutoshi Takeda (kushoto). Majengo ya shule hiyo yaliharibiwa na tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.(
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Bw. Katsutoshi Takeda wakiwa kwenye moja ya madarasa yaliyojengwa kwa ufadhili wa serikali ya Japan katika shule ya msingi ya Nyakato wilayani Bukoba ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi. Madarasa hayo yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Oktoba 9, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea funguo kutoka kwa Mwakilishi wa Balozi wa Japan Nchini, Katsutoshi Takeda  ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa madarasa yaliyojengwa na serikali ya Japan katika Shule ya Msingi ya Nyakato wilayani Bukoba, Oktoba 9, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi baada ya kupokea madarasa yaliyojengwa kwa masada wa serikali ya Japan katika shule ya msingi ya Nyakato wilayani Bukoba ambayo iliharibiwa na tetemeko la ardhi la Kagera. Madarasa hayo yalikabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini, Bw. Katsutoshi Takeda, Oktoba 9, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BINTI WA GEORGE W. BUSH AOLEWA NA CRAIG COYNE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
BINTI wa kwanza wa aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, Barbara Pierce Bush (36) amefunga pingu za maisha na Craig Louis Coyne (37) ambaye ni mwandishi na mtunzi  wa filamu katika harusi ya siri iliyohusisha familia siku ya jumapili huko Maine.

Barbara aliongozwa na baba yake George W. Bush  wakati akiolewa na Craig katika harusi ndogo iliyofanyika nyumbani kwao Kennebunkport Maine, Bush alieleza furaha yao (yeye na mkewe Laura) baada ya binti  yao kufunga ndoa na kumtakia kila la heri.

Wawili hao hawakuweka mahusiano yao wazi na imekuwa harusi ya kuduwaza wengi kwani walionekana kama marafiki wa muda mrefu.

Barbara ameeleza kuwa angetamani uwepo wa bibi yake na hiyo ilikuwa  zawadi kwa bibi yake na wajina wake Barbara Bush aliyefariki mwezi Aprili mwaka huu akiwa na umri wa miaka 92.

Katika ukurasa wake wa instagram bi. Laura Bush ameandika kuwa "Ilikuwa siku ya furaha kwa bintiye Barbara kufunga ndoa na mpenzi wake Craig na wamemfurahia kuwa sehemu ya familia yao" ameandika Laura kwenye picha ya familia.
 Aliyekuwa Rais wa Marekan George W. Bush akimuongoza bintiye Barbara kwenda kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Craig Coyne.
 Barbara Pierce Bush akiwa na mumewe Crag Louis Coyne mara baada ya kufunga ndoa siku ya jumapili huko Maine
 Picha ya familia 

TUNA UMEME WA KUTOSHA KUWAHUDUMIA WATANZANIA – WAZIRI KALEMANI

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kwamba, kwa sasa umeme unaozalishwa nchini unatosheleza mahitaji ya wananchi; bali jitihada za kuzalisha umeme mwingi zaidi zinazoendelea kufanywa na Serikali, ni kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Ameyasema hayo leo, Oktoba 9, 2018 wakati akizungumza na Mwekezaji kutoka Kampuni ya Jos’ Hansen ya Ujerumani, Michael Kabourek, aliyemtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma, kwa ajili ya majadiliano kuhusu uwekezaji katika sekta ya umeme.
“Mathalani, leo hii tunavyozungumza, tuna ziada ya takribani megawati 213 za umeme. Hii inadhihirisha kuwa umeme tulionao kwa sasa unatosheleza kabisa mahitaji ya nchi; isipokuwa tunaendelea na jitihada za kuzalisha umeme mwingi zaidi kwa ajili ya matumizi ya baadaye,” amefafanua.
Akifafanua zaidi, Dkt. Kalemani amesema kuwa, Serikali, kwa kutambua kuwa mahitaji ya umeme yanaongezeka siku hadi siku; sambamba na malengo ya kuingia kwenye uchumi wa kati kupitia uanzishwaji viwanda; ndiyo sababu inaendeleza jitihada kuhakikisha kunakuwa na umeme mwingi zaidi unaofikia megawati 5000 ifikapo mwaka 2025 kutoka takribani megawati 1500 zinazozalishwa sasa.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto), akifafanua jambo kwa Mwekezaji kutoka Kampuni ya Jos’Hansen ya Ujerumani, Michael Kabourek (kulia), aliyemtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma, Oktoba 9, 2018 kwa ajili ya majadiliano kuhusu uwekezaji katika sekta ya umeme nchini. Katikati ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Hassani Mwamweta.
 Mwekezaji kutoka Kampuni ya Jos’ Hansen ya Ujerumani, Michael Kabourek (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa pili-kushoto), wakati wa kikao kilichofanyika Oktoba 9, 2018, ofisini kwa Waziri jijini Dodoma, kujadili kuhusu nia yake kuwekeza katika sekta ya umeme nchini. Wengine pichani (kutoka kulia) ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Edward Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Hassani Mwamweta na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Christopher Bitesigirwe.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto), akiagana na Mwekezaji kutoka Kampuni ya Jos’ Hansen ya Ujerumani, Michael Kabourek, aliyemtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma, Oktoba 9, 2018 kwa ajili ya majadiliano kuhusu nia yake ya kuwekeza katika sekta ya umeme nchini.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKULIMA WA MBAAZI NA CHOROKO KUNEEMEKA NA SOKO LA UHAKIKA LA MAZAO HAYO

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Kondoa
WAKULIMA wa Mbaazi na Choroko hapa nchini wanatarajia kuondokana na adha ya mazao yao kukosa soko baada ya wawekezaji kadhaa kujitokeza kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao hayo katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro.

Kauli hiyo ya matumaini kwa wakulima hao imetolewa wilayani Kondoa mkoani Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, wakati akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

" Kilimo kinategemewa na zaidi ya asilimia 65 ya watanzania, lakini zao la mbaazi limekuwa na matatizo ya soko ndio maana Serikali imeamua kuchukua hatua kwa kuwahamasisha wawekezaji kujenga viwanda vya kusindika mazao hayo hapa hapa nchini, jambo ambalo limeanza kutekelezwa" alisema Mhe. Mgumba

Alisema hivi sasa viwanda vitatu vya  kuchakata mbaazi vinajengwa mkoani Arusha, Dar es Salaam na Morogoro katika eneo la Mtego wa Simba, huku kiwanda kimoja na kusindika choroko kikijengwa mkoani Dodoma.

Alisema kuwa lengo la hatua hizo ni kujibu kero ya muda mrefu ya wakulima wa mazao hayo katika mikoa ya Manyara, Arusha, Dodoma na maeneo mengine yanayolimwa mazao hayo  kukosa soko la uhakika kwa kuongeza thamani ya mazao hayo hapa hapa nchini.

"Ukiongeza thamani ya hizi mbaazi unapanua soko katika dunia badala ya kutegemea soko moja tu la nchini India, ambapo sasa mbaazi zitauzwa nchi mbalimbali zikiwemo nchi za kiarabu, Ulaya na Marekani" Alisisitiza Mgumba.

Awali, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji alimweleza Naibu Waziri huyo wa Kilimo kwamba Wilaya ya Kondoa ina wakulima wengi ambao wanahitaji kuboreshewa mazingira yao ya kilimo ili waweze kujikwamua kiuchumi

"Watu wanasema Kondoa ni vijijini kwa asilimia 100 lakini kwa kasi tunayokwenda nayo, baada ya miaka 5 Jimbo hili litakuwa miji mitupu katika kata zote 21 na kitakacho tuvusha kwenda kwenye miji hiyo ni kilimo" alisisitiza Dkt. Kijaji

Mbaazi imekosa soko katika miaka mitatu mfululizo ambapo bei hiyo ilishuka kutoka  shilingi 2,500 na 3,000 kwa kilo mwaka 2015 na kufikia bei ya shilingi 250 hadi 300 kwa kilo jambo linalowakatisha tamaa wakulima huku wafanyabiashara na baadhi ya wakulima wakiwa na shehena ya zao hilo kwenye maghala wakisubiri kupanda kwa bei.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omari Mgumba, akitoa salaam kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, ambapo Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa kipindi cha miaka 3 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, katika Jimbo la Kondoa, uliofanyika katika Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa.

TAMISEMI yapokea magari mawili kutoka USAID Boresha Afya

$
0
0
Na Mathew Kwembe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepokea magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 na kusema kuwa magari hayo yataongeza thamani katika juhudi za serikali za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akiongea katika hafla ya makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania David Thompson aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa dhamira yake ya kuboresha viwango vya afya kwa watanzania wote.
“Kupitia msaada huu, Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watu wote, katika jamii za watu wa Lindi na Mtwara, mkazo zaidi ukiwa kwa wanawake na vijana,” alisema.
Kabla ya kuyapokea magari hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) David Thompson, Waziri Jafo alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya kusini.
Alisema kuwa kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na mradi wa Boresha Afya katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara na Ruvuma anayo furaha kubwa kushiriki katika hafla hiyo ya kupokea magari hayo yenye thamani ya Tsh.219, 372,136.
“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania ningependa kuwafikishia shukrani zetu za dhat kwa Serikali ya Marekani na wote walio katika mradi huu wa USAID Boresha Afya Kanda ya kusini,” alisema.
Waziri Jafo aliongeza kuwa serikali inajivunia kushirikiana na washirika ambao kweli wanajali hali za raia wa Tanzania.
Alisema kuwa kupitia msaada huo USAID Boresha Afya Kanda ya kusini imeonyesha kweli iko pamoja na watanzania katika kusimamia changamoto za afya nchini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akizungumza wakati wa kupokea msaada wa magari mawili katika wizara hiyo yatakayotumika katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia mradi wa USAIDS Boresha Afya Kanda ya Kusini.
 Kaimu Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania David Thompson akizungumza kuhusu wanavosimamia miradi mbalimbali ya USAID hapa nchini Tanzania wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mkurugenzi wa Deloitte Consulting LTD, Carlton Jones akizungumza kuhusu wanavyosimamia mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya Kusini unaotekelezwa katika halmashauri 43 kwenye mikoa ya Iringa, Njombe, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma wakati wa kutoa msaada wa magari mawili kwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 Kaimu Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania David Thompson (wa tatu kushoto) akimkabidhi mfano wa funguo wa gari Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(katikati) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa Wizara hiyo leo Jijini Dar Es Salaam. Wa kwanza kulia ni Dk. Marina Njelekela, Wa Tatu kulia ni Mkurugenzi wa Deloitte Consulting LTD, Carlton Jones na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI Dkt Zainabu Chaula.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwasha moja ya gari mara baada ya kukabidhiwa magari hayo mawili yatakayotumika  kwenye kuimarisha usimamizi wa Shuguli zinazohusiana na masuala ya Afya katika mikoa ya Lindi na Mtwara kupitia mradi wa USAID Boresha Afya Kanda ya Kusini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(kulia) akimkabidhi mfano wa funguo ya gari  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Wedson Sichalwe(kushoto) ili kusaidia na kuimarisha usimamizi wa Shughuli zinazohusianana na VVU, Uzazi wa mpango. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania David Thompson 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo(kulia) akimkabidhi mfano wa funguo ya gari  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dk. Genchwele Makenge(kushoto) ili kusaidia na kuimarisha usimamizi wa Shughuli zinazohusianana na VVU, Uzazi wa mpango. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi mkazi wa USAID Tanzania David Thompson 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa magari mawili na USAID kupitia mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya Kusini unaotekelezwa katika halmashauri 43 katika mikoa ya Iringa, Njombe, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MIMBA ZA UTOTONI NI CHANGAMOTO KUBWA NCHINI-MTENGETI

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA BI.BELLA BIRD NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini Bella Bird na ujumbe wake walipokutana na kufanya nao mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini Bella Bird na ujumbe wake walipokutana na kuzungumza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 9, 2018.

Picha na IKULU

TAMASHA LA URITHI FESTIVAL LAMEZINDULIWA RASMI MKOANI ARUSHA

$
0
0

Na.Vero Ignatus ,Arusha

Kila mwaka mkoa unatakiwa kutenga fungu kwaajili ya kuandaa tamasha la urithi na utamaduni itakayochangia kuzaa zao jipya la utalii na kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini.

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi katika uzinduzi wa Tamasha la Urithi lililozinduliwa Jijini Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid na kushirikisha makabila mbalimbali mkoani hapo.Ameeleza kuwa Taifa lisilo na utamaduni ni taifa lililokufa, sambamba na kupoteza rasilimaliza husika kwani utamaduni ni kuvutio kibwa cha utalii.

"Tusipoenzi na kuzitunza tamaduni hizo utu wetu rasilimali zetu zitapotea, kwani utamaduni wetu ni kivutio kikubwa cha utalii"alisema Katibu Suzan Kwa upande wake Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema asilima 80%wageni wanaoingia nchini wanatembelea Mkoani hapo kutokana na vivutio vilivyopo mkoani Arusha kupitia vya utalii Maonyesho hayo yamehusisha wadau kuonyesha mambo burudani,ngoma za asili,vyakula vya asili,mavazi ya asili ,utalii na tamaduni za Mtanzania bila kuvunja sheria .

Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha katika Tamasha la Urithi Festival lililozinduliwa mkoani Arusha. Picha na Vero Ignatus
Katibu mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi akiwa katika moja ya banda wanalotengeneza vitu vya asili. Picha na Vero Ignatus. 
Kutoka katikati ni Katibu mkuu wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi, kulia kwake ni Mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya Taif a Profesa Audix Mabula ambaye pia ni Mwenyekiti wa maandalizi ya Tamasha la Urithi, akifuatiwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega.
Hawa nao wakinamama kutoka kabila la Kimaasai walipamba Tamasha hilo la Urithi na utamaduni mkoani Arusha katika uwanja wa Shekh Amri Abeid. Picha na Vero Ignatus.

MICHUZI TV: RELI YA KISASA ITASAIDIA SANA SHUGHULI ZA KIJESHI - CDF MABEYO


MICHUZI TV: TIB CORPORATE BANK YAJA KIVINGINE KWA KUWATEMBELEA WATEJA WAKE

WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA WILAYA YA KYERWA WAJIPIME

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechukizwa na biashara za magendo zinazoendelea katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, hivyo amewataka viongozi wa wilaya hiyo wajipime wenyewe. 
 Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera Bw. Adam Ntogha kumsimamisha kazi Afisa wa Forodha katika mpaka wa Mulongo Bw. Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo. 
 Ametoa agizo hilo Jumanne, Oktoba 9, 2018 wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani hapa kilichofanyika mjini Bukoba. 
 “Biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika. Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na butura.” 
 Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo ulipo kwenye eneo ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za magendo na butura zinafanyika na hakuna kiongozi wanaochukua hatua.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwenye ukumbi wa ELCT, mjini Bukoba, Oktoba 9, 2018.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti, Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
Baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwenye ukumbi wa ELCT, mjini Bukoba. Oktoba 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CHANNEL TEN: Habari za Kitaifa 09.10.2018

WASAFI TV: MANENO YA MWISHO YA PANCHO LATINO KWA DULLY SYKES

WASAFI TV: RATIBA NZIMA YA MAZISHI YA PANCHO LATINO/ BAADA YA KIKAO CHA FAMILIA

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images