Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

TAKUKURU JIRIDHISHENI NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI-MAJALIWA

0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa TAKUKURU wajiridhishe huduma zinatolewa kwa wananchi bila ya rushwa, watakapobaini rushwa wachukue hatua.

Pia, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wajiepushe na vitendo vya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za Serikali katika utendajikazi wao.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa JWTZ.

“Msiwalazimishe au kutengenezea mazingira ya kuomba rushwa kwa wananchi. Wananchi mkiona mnazungushwa katika kupatiwa huduma katoeni taarifa TAKUKURU.”

Waziri Mkuu amesema “tabia ya njoo kesho njoo kesho haikubaliki katika Serikali hii. Serikali haitaki mtumishi mzembe anayedharau wananchi, fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zenu.”

Amesema Rais Dkt. John Magufuli anataka kila Mtanzania afikiwe na huduma za jamii bila ya ubaguzi wa aina yoyote, mtumshi atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake hatakuwa na nafasi Serikalini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo, Bi. Wende Ng’ahara awahamishe maafisa kilimo na kuwapeleka vijijini ili wakawahudumie wananchi.

Amesema maafisa kilimo wanaotakiwa kuwepo wilayani ni wawili tu, Afisa Kilimo wa wilaya pamoja na afisa kilimo anayeshughulikia mazao ya mbogamboga, wengine wanatakiwa kupelekwa vijijini kwa ajili ya kuhudumia wananchi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Bibi Saada Malunde na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Wende wahakikishe wakuu wa idara wanakwenda vijijini kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Wanatakiwa kwenda siku nne kwa wiki.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 8, 2018.

MTANGAZAJI NGULI WA REDIO TANZANIA (RTD) AHMED JONGO AZIKWA LEO MAKABURI YA MBAGALA CHARAMBE DAR

0
0
 Maziko ya Mtangazaji wa RTD Ahmed Jongo  yamefanyika leo  makaburi ya Mbagala Charambee Dar es Salaam
 Baadhi ya Ndugu,Jamaa na marafiki wakiwa wamejumuika nyumbani leo mchana kwenye mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake  kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Ndugu,Jamaa na marafiki wakijadiliana jambo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar Es Salaam.
 Sehemu ya waombolezaji wakiwamo ndugu,jamaa na marafiki wakijadiliana jambo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa mtangazaji nguli wa  Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar Es Salaam.
  Miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani ambaye amefarikia dunia jana.
 Baadhi ya  ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
  Waombolezaji wakijadiliana jambo katika msibani  wa marehemu aliyekuwa Mtangazaji nguli wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya  ndugu, jamaa na marafiki wakipata chakula cha mchana nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
 Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani Dar es Salaam.

CASTLE LAGER YAMLETA SAMUEL ETO'O NCHINI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KAMPUNI ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle lager imemualika mmoja ya wachezaji bora barani Afrika Samuel Eto'o kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-side utakaojengwa Oysterbay jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa bia hiyo Pamela Kikuli amesema kuwa nyota huyo atashiriki katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oysterbay  mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na ufukwe wa Coco.
 
Aidha ameeleza kuwa lengo la kumleta nguli huyo wa soka barani Afrika ni kuongeza hamasa ya soka kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika kabumbu.

Pia amesema kuwa kama kampuni wataendelea kushiriki katika shughuli za kijamii katika kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake msemaji ya klabu ya Simba  amesema kuwa urafiki unasimama hasa katika wakati wa kuliwakilisha taifa na amewataka mashabiki wa klabu za Simba na Yanga kujitokeza kwa wingi.

Dismas Ten msemaji wa klabu ya Yanga amesema kuwa ujio wa Eto'o nchini ni heshima kubwa kwa nchi na soka kwa ujumla hivyo wananchi hasa wapenda soka ni bora wakajitokeza ili kuweza kumfahamu nguli huyo wa mpira wa miguu.

Samuel Eto'o  anayesakata kabumbu huko Qatar anatarajia kuwasili katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Oktoba 10 na siku ya Alhamisi atatembelea mradi huo wa ujenzi wa uwanja hicho na kushiriki mazoezi na vijana.

KESI YA KUTOA LUGHA CHAFU KWA RAIS INAYOMKABILI HALIMA MDEE YASHINDWA KUSIKILIZWA

0
0
 Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Oktoba 8 mwaka 2018 imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kutoa lugha chafu ya matusi dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee shahidi wa upande wa mashtaka aliyetarajiwa kutoa ushahidi hakufika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini shahidi hajafika leo.

Alidai shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo, walimtumia wito lakini kwa bahati mbaya yupo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, aliiomba mahakama kuipangia tarehe nyingine kesi hiyo.

Hakimu Simba ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 22, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwamo  mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Mdee anadaiwa,  Julai 3,2017  katika ofisi za Chadema alitamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.

KISANGA AWATAKA WAKAZI WA OYSTERBAY KUWA WALINZI KWENYE MAENEO YAO

0
0
 Na Khadija Seif,Globu  ya jamii
  MWENYEKITI Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) katika Tawi la Oysterbay Dar es Salaam  Donald Kisanga ameendesha uchaguzi wa chipukizi huku akiwaomba wazazi kuruhusu watoto kushirikia kikamilifua.

Amesema chipukizi wanafundishwa mambo mbalimbali yenye maslahi kwa nchi yao yakiwamo ya  uzalendo,uadilifu,kuwa imara na ukakamavu katika kulijenga ,kulitetea na kupigania  kwa maslahi ya Taifa la  Tanzania.

Kisanga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam ambapo pia amepongeza juhudi na mikakati inayofanywa na Serikali chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kuwatumikia Watanzania.

Pia Kisanga ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kutunza na kulinda mazingira na kutoa taarifa pindi wanapoona wahalifu wanaingia kwenye makazi kwani vitendo hivyo lazima vikomeshwe ili kuwepo na amani 

Kisanga pia amezungumzia jitihada zinazofanywa na Serikali ya CCM katika kutoa mikopo ambapo  imeweza kutoa mikopo kwa wananchi ambao wanatakiwa kuunda kikundi cha watu wa tano na kuwasilisha barua zenye maelezo kwa mjumbe wa nyumba 10.

Amezungumzia pia namna ambavyo vijana wengi wamekua wakijuhusisha na uhalifu katika fukwe za Coco Beach ambapo watu wengi hufanyiwa vitendo vibaya na wengine kusababisha kupoteza maisha .

Kisanga ameeleza namna ambavyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alivyotembelea eneo hilo la fukwe hizo wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Mashujaa nchini.

Ambapo alishirikiana na wananchi kufanya usafi na kutoa tamko kwa Serikali kuboresha mazingira hayo ili kuwa kivutio kizuri zaidi kwa watu ambao wanafika maeneo hayo kwa ajili ya kudarizi.

TAMASHA LA WAJASILIAMALI KUFANYIKA OKTOBA 13 KINONDONI

0
0
Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha mwanamke wilaya ya ubungo Hidaya Njaidi akizungumza jijini Dar es Salaam leo na MICHUZI BLOG wakati akihamasisha wanawake na wananchi kwa ujumla kwenda kwenye tamasha la wajasiliamali litakalofanyika Oktoba 13 mwaka huu kinondoni jijini Dar es Salaam.

CHAMA cha wajasiliamali Tanzania kinatarajia kufanya tamasha kubwa la wajasiliamali litakalofanyika Oktoba 13 mwaka huu kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutambulisha tamasha hilo Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka amesema kuwa tamasha hili litawasaidia wajasiliamali kuonyesha bidhaa zao za mikono.

Pia amesema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na wajasiliamali mbalimbali watakao toa ushuhuda kuhusiana na ujasiliamali pia kutakuwa live bendi kutoka kwa msanii wa taarabu Isha Mashauzi.

Kiingilio cha tamasha hilo kwa viti maalumu VIP ni shilingi 40,000/= na viti vya kawaida ni shilingi 20,000/=

Nae Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha mwanamke wilaya ya ubungo Hidaya Njaidi amewaomba akinamama, akinababa pamoja na wanafunzi wa shule zote jijini Dar es Salaam kufika kwaajili ya kupata kile wajasiliamali wa jiji la Dar es Salaam walichowaandalia.

Mawasiliano kwaajili ya kujipatia kadi za kiingilio katika tamasha hilo wasiliana na Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka namba o716589737 tigo au 0687935927 airtel.
Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka akizungumza na MICHUZI BLOG wakati akitambulisha tamasha la wajasiliamali litakalofanyika Kinondoni jijini Dar es Salaam Oktoba 13 mwaka huu.
Mwenyekiti wa chama cha malkia wa nguvu, Grace Mpanduka akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha mwanamke wilaya ya ubungo Hidaya Njaidi jijini Dar es Salaam leo wakati walipotambulisha tamasha la wajasiliamali litakalofanyika Oktoba 13 Kinondoni jijini Dar es Salaam.

BODI YA UTALII YAANDAA MAONESHO YA UTALII NCHINI YATAKAYOANZA OKTOBA 12

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BODI ya Utalii Nchini (TTB) imeandaa maonesho ya kimataifa ya utalii yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo (SITE) ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam.

Lengo la maonesho hayo ni kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo na wakati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabiashara kutoka masoko makuu ya Utalii.

Akizungumza na waandishiw a haari kuelekea maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza Oktoba 12 hadi 14, Mwenyekiti wa bodi wa TTB Jaji Mstaafu Maiko Miayo amesema kuwa, onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na makampuni ya uoneshaji 170 kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika na Ukanda wa bahari ya Hindi pamoja na wafanyabiashara wa kimataifa na vyombo vya habari 300.

Jaji Miayo amesema mara ya kwanza maonesho hayo yalifanyika mwaka 2014 na yalihudhuriwa na waoneshaji kutoka makampuni 40 pamoja na wafanyabiashara na vyombo vya habari va kimataifa kutoka nchi 24.

Alisema, hawakuishia hapo mwaka 2015 maonesho hayo yalizidi kuvutia na wakapokea makampuni ya utalii 110 pamoja na wafanyabiashara na vyombo vya habari 39 kutoka nchi mbalimbali duniani.Kwa mwaka jana, onesho la SITE liliweza kuhudhuriwa na waoneshaji kutoka makampuni 145 na kufanikiwa kupata jumla ya wafanyabishara wa kimataifa na waandishi wa habari 241.

Jaji Miayo amesema kuwa, kwa mwaka huu maonesho  hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Mikutano  kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) yatakuwa yamezidi kuimariki pamoja na kuwapeleka baadhi ya washiriki katika mafunzo sehemu mbalimbali za kitalii nchini.

Wana maonesho hao wanatarajiwa kwenda katika hifadhi za Mkoani Arusha kama Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za Serengeti, huku kwa mkoa wa Iringa wakitembelea utalii wa kilimo na ardhi yoeru ya Mufindi pamoja na vivutio vingine vya kiutamaduni na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Katika maeneo mengine ni Tanga, Mafia ambapo watatembelea utalii wa bahari kivuko kikuu Papa Potwe(Whale Shark), Morogoro  kwenye milima ya Udzungwa na Hifadhi ya TAifa ya Mikumi pamoja na  Zanzibar.

Maonesho hayo yatazidi kuboresha katika sekta ya utalii ambapo lengo kuu ikiwa ni kuongeza watalii kutoka  nje ya nchi na ndani ya nchi.
Mwenyekiti wa bodi wa  Utalii Nchini (TTB) Jaji Mstaafu Maiko Miayo  akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana maonesho ya kimataifa ya utalii yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo (SITE) ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam.

WATANZANIA WATAKIWA KUENZI VITU VYA KIASILI KUVUTIA WATALII

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WATANZANIA wameombwa kuenzi vitu vya asili ili kudumisha utamaduni na kuvutia watalii wengi kuja nchini.



Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga alipokua anazungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Nchini baada ya kuwatembelea ofisini Kwao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri amesema kuwa moja ya vitu ambayo watanzania wanatakiwa kuvidumisha ni utalii wetu ili kuweza kuongeza pato la Taifa.

Amesema, kwenye baadhi ya sehemu ambazo zimesahaulika ni Utalii wa Utamaduni kitu kinachopelekea kupotea kwa tamaduni zetu ikiwemo vyakula, mavazi, sanaa za mkono na michoro, michezo pamoja na lugha ya Kiswahili.

Amesema, kuanzia mwaka huu wameweka mwezi Septemba kuwa mwezi wa Utamaduni utakaokuwa unajulikana kama Urithi Festival ambapo kutakuwa na maonesho mbalimbali ya vitu vya utamaduni ili kuvutia watu wa nje waje kujionea namna utamaduni wa watanzania ulivyo.

Hasunga amesema kuwa, lengo kuu la maonesho hayo ni kuongeza watalii nchini  ikiwemo na kuongeza mapato ya ntaifa kutoka Dola Bilioni 1.2 kwa mwaka na kuwa zaidi ya hiyo.


'Tanzania ina vivutio vingi vua utalii ila vimekuwa vikiharibiwa na watanzania wenyewe na kusababisha Tanzania kushuka kutoka nafasi ya pili hadi ya nane kwenye vivutio vya utalii duniani unaotokana na uvamizi wa wakulima na uvamizi wa mifugo kwenye hifadhi za taifa," amesema

" Kwa sasa serikali inataka kuondoa mfumo wote na kurudisha hadhi ya hifadhi zote ili kuboresha utalii ikiwemo wa ndani kutokana na kushuka kutoka watalii laki nane  (800,000) kwa mwaka na kufikia watalii  laki sita na elfu ishirini na nne (602,400)," amesema Hasunga.

Hasunga amesema kuwa kumekuwa na utofauti mkubwa sana kulinganisha na nchi zingine katika kutembelewa na watalii ambapo kwa nchi kama Misri wamekuwa wanapokea watalii Milioni 10 kwa mwaka, Morroco wakipata watalii Milioni 13 huku Afrika Kusini wakipata watalii Milioni 1,500,000.

Akisisitiza zaidi, Naibu Waziri amewataka TTB kujitangaza zaidi kwa kila kivutio kilichopo kwenye mkoa, , kutumia Digital Market,  kutengeneza makala (video) zinazohusu vivutio, kuweka mabango barabarani ikiwezekana baadhi ya barabara wakabidhiwa kabisa Bodi hiyo.

Akijibu hoja za Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa  katika upande wa makala wapo katika hatua za kukamilisha na wanatarajia kuzindua mwakani mwezi Machi na utazinduliwa nchini Ujerumani.

Amesema kuwa, makala hizo zitaelezea zaidi kuhusu utalii wa ndani, hata hivyo matarajo ya kuongeza watalii wa ndani kwa kuongeza mabalozi ambapo wka sasa wana mabalozi tisa kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Aidha, ameweka wazi msimamo wa TTB kwenye kutangaza utalii ikiwemo kutumia baadhi ya mashirika ya ndee kama Qatar, ligi kuu ya Uingereza na tayari makampuni mengine kama Emirates wapo kwenye mazungumzo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea bodi ya Utalii Nchini (TTB) na kuzungumza na menejimenti nzima na kuwataka kutanaza vivutio vya hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa na
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga na kumuahidi kutekeleza yale aaliyowaagiza.


TAASISI YA HDIECA YAFANYA MAONESHO YA WAJASILIAMALI WADOGO KUONESHA KAZI ZA MIKONO YAO JIJINI DAR

0
0
Taasisi ya isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na maswala ya Mazingira pamoja na Utu (HDIECA) , iliandaa maonesho maalum ambayo yaliwakutanisha wajasiliamali mbalimbali ambao wanafanya shughuli zao kwa kutumia mikono yao kwa lengo la kurudisha shukurani zao kwa  jamii kutokana na wananchi kupokea na kushirikiana nao vyema katika kazi zao mbalimbali wanazozifanya kila siku.

Maonesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Azura Kawe Jijini Dar es Salaam na hakukuwa na kiingilio chochote kwa wananchi na wajasiliamali hawakulipia kitu ilikuwa ni Bure kabisa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajasiliamali wengi waliishukuru taasisi hivyo kwa kuwapa fursa hiyo hata ya kuonesha kazi zao na kufahamiana na watumbalimbali na pia kuongeza wigo wa kibiashara kwa kupata wateja wapya.
 Katika maonesho hayo kulikuwa na wajasiliamali wanaotengeneza vitu mbalimbali kwa mikono yao ambapo pamoja na yote waliomba ikiwezekana watengewe sehemu ambayo watakuwa wanapeleka bidhaa zao na kuziuza hata mara moja kwa mwezi.
Wananchi wakiendelea kutazama Bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watanzania .
 Wajasiliamali mbalimbali pamoja na waandaaji wa maonesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja
 Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Batiki
  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetumia chupa chakavu zilizotupwa anaokota na kuziongezea thamani kwa kuviwekea marembo kwa kutumia nyuzi vitambaa na nakshi nakshi zengine
  Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza bidhaa zao kwa kutumia mishumaa na maua ya asili

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>

JIMBO LA KONDOA LAPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO MIAKA MITATU YA JPM

0
0
Na Mwandishi wetu, Kondoa

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa mkoani Dodoma, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, maji, afya, miundombinu ya barabara na huduma nyingine za kijamii zimeimarika zaidi katika Jimbo la Kondoa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Kijaji ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Jimbo lake katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa uliowashirikisha zaidi ya wajumbe 1,200, uliofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa.

Ameyataja baadhi ya mafanikio makubwa kuwa ni kuchimba na kukarabati visima virefu na vifupi vya maji vipatavyo 56 pamoja na kukarabati visima vingine 4 vilivyoharibika zaidi ya miaka 15 iliyopita ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.8 zimetumika, hatua iliyochangia wananchi zaidi ya laki moja katika Jimbo la Kondoa kuanza kupata huduma ya uhakika ya maji.

Kuhusu Sekta ya Elimu, Dkt. Kijaji ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mbili mpya za Sekondari katika Kata za Hondomairo na Bumbuta kwa gharama ya sh. milioni 140.5, ambazo zitaanza kuchukua wanafunzi kuanzia mwezi Januari, 2019 pamoja na kujenga na kukarabati vyumba ya madarasa, mabweni na nyumba za walimu, kwenye shule mbalimbali za Sekondari na msingi.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi-CCM, katika kipindi cha miaka 3, katika Jimbo la Kondoa, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa uliofanyika katika Kata ya Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dodoma, Comrade Godwin Mkanwa, akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa, baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo hilo, iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Amina Mollel, akifuatilia kwa makini matukio ya uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa. Walioketi karibu naye ni wazazi wa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mzee Abdallah Kijaji na mkewe Aziza Selemani, katika Kata ya Pahi, Kondoa, Dodoma

Sehemu ya umati wa wajumbe 1,200 wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, wakipokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa, iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, katika Kata ya Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

MICHUZI TV: SHUHUDIA CHECHE ZA HAJI MANARA

UJUMBE MZITO WA DIAMOND, KHERI YA BETHIDEI KWA KIKWETE

Balozi Dr. Abdallah Possi, awasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dr. Abdallah Possi, aliwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder hivi karibuni. Pamoja na Ujerumani, Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin pia unahudumia maeneo mengine tisa tisa ya uwakilishi, ikiwemo nchi ya Hungary. 
 Baada ya kuwasilisha hati, Balozi alipata fursa ya mazungumzo mafupi na Rais wa Hungary, mazungumzo ambayo yalilenga zaidi katika masuala ya kilimo, elimu na maji. 
Balozi Dkt. Possi alimueleza Rais wa Hungary kwamba Tanzania inawakaribisha wawekezaji katika maeneo mbalimbali, yakijumuisha pia viwanda vinavyojihusisha na mazao ya kilimo. Dkt. Possi alifafanua kwamba, kilimo ni sekta ambayo bado inategemewa na watanzania walio wengi, na kwamba kuna fursa nyingi zaidi katika sekta ya kilimo siyo tu kutokana na uwepo wa ardhi nzuri yenye rutuba, bali pia uwepo wa idadi kubwa ya watu ndani ya Tanzania na nchhi zinazoizunguka, hali ambayo inahakikisha uwepo wa soko la uhakika katika bidhaa za kilimo. 
Dkt. Possi aliongeza kwamba, uwekezaji wa kilimo siyo tu utapunguza upotevu wa mazao unaojitokeza baada ya mavuno, bali pia utasaidia uongezaji thamani ya mazao ya kilimo, na hivyo kuchagiza zaidi biashara ya mazao ya kilimo, na kuongeza ajira kwa idadi kubwa ya watanzania ambao wanategemea kilimo.
 Balozi Dkt. Possi pia aliishukuru serikali ya Hungari kufuatia mpango unaowapa fursa watanzania kupata elimu ya juu nchini Hungary. 
Rais wa Hungary Bw. János Áder alimueleza Balozi Dkt. Possi kuhusu mkutano mkubwa kuhusiana na masuala ya maji unaotarajiwa kufanyika nchini Hungary mwaka 2019, mkutano ambao utawakutanisha wataalamu wa maji kutoka nchi mbalimbali duniani. 
Rais Áder alisema mkutano huo ni fursa nyingine ya kufahamu aina mbalimbali za teknolojia zinazoweza kutumika kutatua changamoto kubwa ya upotevu wa maji. 
 Balozi Dkt. Possi pia aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Hungary. Mnara huu ulijengwa kwa heshima ya askari wote wa Hungary waliofariki katika vita, na ambao miili yao haikupatikana au kutambuliwa. 
Siku moja kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dkt. Possi alikutana na jumuia ya Watanzania wanaoishi nchini Hungary. Dkt. Possi aliwapongeza watanzania hao kwani, licha ya idadi yao ndogo, wameonyesha moyo wa mshikamano, jambo ambalo ni muhimu kwa mshikamano thabiti wa jumuia za watanzania wanaoishi nje ya nchi. 
Pia Dkt. Possi aliwaeleza watanzania hao kwamba bado wana nafasi ya kupeleka maendeleo nyumbani, na kwamba milango ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Berlin iko wazi kwa kila mtanzania anayeishi katika eneo linalohudumiwa na Ubalozi huo. Watanzania hao pia walipata fursa ya kuuliza masuali ambayo yalipatiwa majibu.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Possi, akiwasili katika kasri la Budapest tayari wasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder hivi karibuni.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Possi, akitambulishwa  katika kasri la Budapest  kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Hungary Bw. János Áder hivi karibuni.
 Baada ya kuwasilisha hati, Balozi alipata fursa ya mazungumzo mafupi na Rais wa Hungary, mazungumzo ambayo yalilenga zaidi katika masuala ya kilimo, elimu na maji.
Balozi Dkt. Possi pia akiweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Hungary. Mnara huu ulijengwa kwa heshima ya askari wote wa Hungary waliofariki katika vita, na ambao miili yao haikupatikana au kutambuliwa. 
Balozi Dkt. Possi na mkewe na afisa wa ubalozi wakipozi baaada ya yeye kuweka  shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Hungary. 

Rais Magufuli akutana na Wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  katika kikao cha kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma kutoka kwa wataalamu mbalimbali wanaohusika na ujenzi huo. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 8, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax wapili kutoka kushoto mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji  Mnyepe wapili kutoka kulia akifatiwa na  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara hiyo Bw. Shio. Kushoto ni Msaidizi wa Rais Maswala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 125 kutoka kwa Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu  Kwa ajili ya Rambirambi ya nchi hiyo kwa Tanzania kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Mwanza mwezi uliopita. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BREAKING NEWZZZ: KAMANDA WA POLISI MKOA WA KAGERA NA MAKAMANDA WA WILAYA YA KYERWA WASIMAMISHWA KAZI


WAZIRI MKUU ATOA SIKU MBILI KWA AFISA ELIMU MULEBA

0
0

* Ifikapo Jumatano awe amepeleka walimu shule ya msingi Rwenzige
*Ina wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne bila mwalimu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Kaimu Afisa Elimu (Msingi) wa wilaya ya Muleba, mkoani Kagera Bw. Bukuru Malembo awe amepeleka walimu wawili katika shule ya msingi iliyoko kwenye kitongoji cha Rwenzige kwa kuwa haina mwalimu hata mmoja.

Shule hiyo yenye madarasa wawili na ofisi moja ya mwalimu ina jumla wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne, ilijengwa na wananchi ambapo wanafunzi wake wanafundishwa na mwananchi mmoja aliyemua kujitolea ili kuwapunguzia watoto kutembea umbali wa kilomita 16 kwenda kusoma katika shule ya kijiji cha Kiteme.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya bango wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha kituo cha afya Kimeya, baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

“Haiwezekani watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano wakatembea umbali wa kilomita 16 kwenda shule wakati katika kitongoji chao kuna shule yenye madarasa mawili na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu na Afisa Elimu hadi sasa hajapeleka walimu na kumuachia mwalimu Benson (kijana ambaye si mwalimu ila anajitolea kufundisha) akifundisha wanafunzi hao peke yake.”


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba, DKt. Modest Buchari (kulia) wakati walipokagau ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba (kulia), Oktoba 8, 2018.Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

aziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakimjulia hali, Consolata Marios na mwanae Revina Albert wakati walipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Bibi Saura Venant na aliyempakata mwanae, Anord Revocatus (kushoto) na Bibi Dorothea Fidel aliyempakata mwanane Redemta Deobey (wapiki kushoto) wakati awalipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018

Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa AnnaTibaijuka (mwenye gauni la bluu) wakicheza ngoma ya asili wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba kuhutubia mkutano wa hadhara, Oktoba 8, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI

0
0
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kuzuia na kudhibiti madhara yanayosababishwa na machafuko ya kisiasa katika jumuiya hiyo na Bara la Afrika kwa ujumla. Wawakilishi wa nchi hizo wamekusanyika nchini Malawi kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 17 Oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko

Wawakilishi wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi, Magereza na taasisi za kiraia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa watu 600 wanaoshiriki zoezi hilo lililopewa jina la EX UMODZI CPX 2018 na kaulimbiu ya Afrika ni Amani na Maendeleo (Africa for peace and prosperity).

Katika hafla ya ufunguzi wa mazoezi hayo iliyofanyika leo tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo mji wa Salima takriban kilomita 120 kutoka Lilongwe, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Mhe. Evaton Chemulirenji alisema mazoezi hayo ni utekelezaji wa maazimio ya SADC na Umoja wa Afrika (AU) wa kuandaa kikosi cha kukabiliana na machafuko barani Afrika (Standby Force-SF) ambacho kinatakiwa kiwe kimekamilika ifikapo Januari 2019.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Evaton Chimulirenji akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo na mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko iliyofanyika tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo katika mji wa Salima nje kidogo ya jiji la Lilongwe.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya SADC yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi ya ulinzi, askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani.

Mratibu wa Program ya Mafunzo yanayofanyika nchini Malawi akieleza mpangilio wa program ya mafunzo hayo kwa ujumla

Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo Meja Jenerali A.B Mhone naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi Mhe. Evaton Chimulirenji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Generali Supini Phiri (kulia) pamoja na Mkuu wa Misheni ya mafunzo hayo, Mhe. Bi. Eunice Lumbia

Sehemu ya viongozi wa kijeshi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi huo .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

DIRA YA KITAA NA TOFAUTI YA MAWAIDHA NA MATANGAZO..!

AJALI YA KENTA YAUA MCHEZAJI WA TIMU YA IYUMBU FC NA KUJERUHI 38 WAKIENDA KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI NA TIMU YA MGUNGIRA

0
0
Na Jumbe Ismailly SINGIDA 

MCHEZAJI mmoja wa timu ya soka ya Kijiji cha Iyumbu,tarafa ya Sepuka,wilayani Ikungi,Mkoani Singida,Mussa Kikumbu (20) amepoteza maisha na wengine 38 wamejeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya kenta walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kata ta Mgungira kuacha njia na kupinduka.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji na washabiki waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida walisema ajali hiyo ilitokea Okt,07,mwaka huu saa tisa za alasiri wakati wakielekea kwenye mchezo wao wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira.

Mmoja wa majeruhi hao Emanueli Peter alisema waliondoka wakiwa watu 38 kwenye gari hilo na walipoanza safari askari mmoja wa kituo cha polisi Iyumbu alisema yeye hatapanda gari bali angekwenda na usafiri wake wa pikipiki.

Alifafanua majeruhi huyo alaiyelazwa katika wodi namba tatu katika Hospitali hiyo kwamba askari huyo alikuwa nyuma ya garai walilopanda akiendesha huku akionesha kila dalili za kuwa amekunywa kilevi huku dereva naye akiendesha mwendo kasi huku naye akiwa amelwa.
Kwa mujibu wa Peter inasemekana awali askari huyo alikuwa akitaka kumpita dereva wa gari ili aweze kutangulia lakini ilishindikana lakini baada ya muda alianza tena kuomba nafasi ili atangulie na alipopishwa ndipo ghafla alianguka chini.

Aidha majeruhi huyo aliweka bayana pia kwamba baada ya askari huyo kuanguka chini ndipo dereva wa gari walilopanda aliamua kumkwepaa ili asimkanyage na ndipo alipoingia kwenye korongo lililokuwa nje ya barabara na gari hilo kuanguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja kati ya watu 39 waliokuwepo kwenye gari hilo.
FATUMA JISHIMU(19) aliyelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida pamoja na mwanaye MAARIAMU RAMADHANI(2) kufuatia ajali ya gari aina ya kenta iliyokuwa imewabeba wachezaji na washabiki Iyumbu FC waliokuwa wakienda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya kata ya Mgungira FC.
PICHA Na.879 Ni MAGRETH SAWA (40) aliyelazwa katika wodi namba tatu hospitali ya Mkoa wa Singida akipatiwa matibabu kufuatia ajali ya gari aina ya kenta kucha njia na kupinduka katika Kijiji cha Iyumbu.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).

MAMA MARIA NYERERE:MAGEUZI YANAYOFANYWA NA RAIS MAGUFULI NI YA KUUNGWA MKONO

0
0
Maneno haya yamesemwa na Mama Maria Nyerere, Mke wa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere mwasisi wa Taifa letu alipotembelewa na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) TAIFA jana Oktoba 08/2018. 
Viongozi hao kutoka Makao Makuu ya UVCCM ni Wakuu wa Idara Ndugu Hassan Bomboko (Uhamasishaji na Chipukizi), Peter Kasera (Organaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa), Khamana Juma Simba (Vyuo na Vyuo Vikuu)
Mama Maria Nyerere ameipongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na amewaomba Viongozi wote nchini, Vijana na wananchi kumuunga mkono na kufanya juhudi kwenye maeneo yao ili kusaidia kuijenga Tanzania Mpya.
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images