Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

MHAGAMA APONGEZA MIRADI KAMBI YA MLALE

$
0
0
NA MWANDISHI WETU:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amepongeza kazi za uzalishaji mali katika kambi ya Mlale.

Aliyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi kwenye kambi hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) iliyopo Mlale kwa lengo la kuzungumza na kuangalia miradi mbalimbali ya uzalishaji mali kambini hapo.

Waziri Mhagama alisema kuwa dira ya taifa kufikia 2025 ni kuongeza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii kufikia hadhi ya uchumi wa pato la kati kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati hapa nchini inayolenga kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa.  

“Miradi hii iliyoanzishwa hapa imekuwa na tija kubwa kwa jamii iliyokaribu katika kufanikisha upatikanaji wa ajira kwa vijana na kukuza uchumi na maendeleo ya wanamlale na watanzania kwa ujumla” alisema Mhe. Mhagama

Aliongeza kuwa, mageuzi ya kikosi cha JKT Mlale 842 yamekuwa ni makubwa sana hususan katika kuunga mkono maagizo ya Mhe. Rais, Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kiwanda cha kuchakata sembe kwa uwezo mkubwa na kuzalisha tani 440 kwa mwezi.

Aidha, Mheshimiwa Mhagama alihamasisha kikosi hicho kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana ikiwa ni njia moja wapo ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwezesha vijana kupata mafunzo ya stadi za kazi yatakayowawezesha kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuajiri.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Kikosi 842 cha Jeshi Kujenga Taifa (JKT) Mlale, alipofanya ziara ya kikazi kuona shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosi hiko.
 Mkuu wa Kikosi Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale, Luteni Kanali Al Solomon Shausi akielezea miradi ya  uzalishaji mali iliyopo kwenye kambi hiyo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kuona shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosi hiko.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mwendesha Mitambo ya Kiwanda SG. Vereranda Kihali jinsi shughuli ya uchakataji sembe inavyofanyika katika kiwanda hiko, alipotembelea kambi ya JKT Mlale 842 kujionea shughuli za uzalishaji mali katika kambi hiyo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimjulia hali mtoto Hawa Mapunda, aliyelazwa (kulia) ni mama wa mtoto Bi. Christer Ndomba alipotembelea wodi ya watoto katika kituo cha afya cha JKT Mlale, Peramiho, akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi mashuka kwa viongozi wa kambi ya JKT Mlale, alipofanya ziara kwenye kambi hiyo kujionea shughuli za uzalishaji mali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo kwenye ukumbi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Oktoba 8, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

 Watumishi  wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo wakimsikiliza Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Oktoba 8, 2018. 

Waziri akusanya sh mil 280 akizindua mashindano ya mbio za baiskeli kusaidia sekta ya elimu

$
0
0
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda amezindua mpango wa mashindano ya mbio za baiskeli na kufanikisha kukusanya Sh milioni 280 kati ya Sh milioni 340 zinazotarajiwa kukusanywa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la 'Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge', yameandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini nchini -Acacia kwa kushirikiana na Tasisi binafsi kutoka nchini Canada - CanEducate.

Akizungumza katika uzinduzi wa uchangiaji wa mashindano juzi jijini Dar es Salaam, Kakunda alitoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuchangia mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 3, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kakunda ambaye alimwakilisha Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alisema malengo ya mashindano hayo yanaenda sambamba na malengo ya serikali katika kurahisisha mazingira ya utoaji elimu nchini. "Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani na kufuta ada za shule pamoja na ada za ziada, hadi mwaka jana kumekuwapo na ongezeko la asilimia 44 la uandikishaji wanafunzi wapya wa elimu ya awali, ongezeko la asilimia 33 la uandikishaji wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na wanafunzi wapya wanaojiunga na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 366,396 mwaka 2015 hadi 483,216 mwaka 2017", alisema.

Alisema hatua hizo zinahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali kama wanavyofanya Acacia katika kufikia malengo ya serikali.Aidha, Mkurugenzi wa Acacia nchini, Asa Mwaipopo alisema kwa mwaka jana pekee kampuni hiyo imejenga madarasa na kukarabati mabweni yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 100 wa kike katika Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo wilayani Kahama.

Pia imefanikisha ujenzi wa maktaba sita katika shule zinazozunguka migodi ya kampuni hiyo."Tangu tuanze kushirikiana na CaEducate mwaka 2011 katika kuboresha sekta ya elimu nchini, Acacia imetumia zaidi ya sh milioni 450 zilizofikia shule 20 na wanafunzi zaidi ya 5000.

Meneja Mkuu Uhusiano na Uwezeshaji wa Jamiii kutoka kampuni ya Acacia Bi Noleen Dube akiwashukuru wadau waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuchangia elimu nchini kupitia mashindano ya baiskeli yanayofahamika ' Acacia Pamoja Imara Cycle Challenge' yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza mwezi Novemba. Wengine ni pamoja na Naibu Waziri -Tamisemi, Joseph Kakunda (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Acacia, Asa Mwaipopo, (wa tatu kulia) na Rais wa taasisi ya CanEducate ambayo ndio inaratibu mpango huo kwa kushirikiana na Acacia Bw. Rishi Ghuldu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Peter Geleta (wa kwanza kushoto), kulia kwake ni Meneja Uhusiano na Uwezeshaji ya Jamii, Noleen Dube, Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo na Naibu Waziri - Tamisemi, Joseph Kakunda pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango wa mashindano ya mbio za baiskeli, "Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge" yenye lengo la kukusanya Sh milioni 340 kusaidia wanafunzi wasiomudu gharama za elimu nchini.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kusaidia wanafunzi wasiomudu gharama za elimu katika familia duni zinazonguka migodi ya Acacia, Yunista Marwa akizungumza katika hafla hiyo, namna mpango huo wa CanEducate ulivyomsaidia kuanzia kidato cha pili hadi alipohitimu kidato cha sita.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda akizungumza katika hafla ya kuzindua mpango wa kuchangia mashindano ya mbio za baiskeli yanayotarajiwa kufanyika Novemba 3, 2018 katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza kwa lengo la kuchangia huduma za elimu nchini.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUITEMBELEA HOSPITALI YA MAKUNDUCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA

$
0
0


Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kulia akifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja kuangalia Miradi na mafanikio mbalimbali yanayo patikana katika hospitali hiyo.
Daktari wa Hospitali ya Makunduchi Vuai Abdalla (MD) akimuelezea Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed maendeleo na changamoto zinazowakabili katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akisalimiana na Mzazi Asia Issa Hassan mkaazi wa Makunduchi aliyekuja kujifungua katika Hospitali hiyo na kumuelezea furaha yake ya kufuata uzazi wa Mpango.
Muonekano wa Jengo litakalotumika kama Makaazi ya Madaktari kwa ajili ya kuondoa usumbufu wa Madaktari waliokuwa hawana nyumba ya kuishi katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimsikiliza Mpishi wa kituo hicho Suleiman Mohammed Suleiman aliyekuwa akimuelezea changato wanazokabiliana nazo katika kutoa huduma ya chakula. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

DC MURO AENDELEA KUKABILIANA NA KERO ZA MAJI ARUMERU.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro ameendelea kutatua kero ya Maji katika kata ya Tarakwa Halmashauri ya ARUSHA iliyo Wilaya ya Arumeru, Kwa kuweka Ubunifu wa kuunganisha wadau mbalimbali wa Maendeleo Wilayani Arumeru na kuwaomba kuungana nae katika kuleta Suluhu ya muda mfupi itakayosaidia kupatikana Kwa Maji wakati Serikali inaendelea na Mpango wa ujenzi wa Miundombinu itakayoleta Maji ya kudumu katika kata ya Tarakwa.

Dc Muro amewaeleza wadau hao kuwa wananchi wanachotaka ni Maji yawe yanakuja Kwa mpango wa muda mfupi au mrefu wao haiwahusu cha Msingi ni kuhakikisha Maji yanapatikana Kwa Njia yoyote ili kusaidia kina Mama na wasichana pamoja na Vijana wanaozunguka umbali mrefu kutafuta Maji badala ya kuendelea na shughuli za kuwaletea Maendeleo 

Dc Muro amefanikiwa kuwashawishi wadau na kumuunga mkono Kwa kutoa Malori yenye maboza ya Maji na kisha kuwayapeleka Kwa wananchi wenye uhitaji katika kata ya Tarakwa.

Nao baadhi ya Wananchi Waliokuwa na Uhitaji wa Haraka wa Maji wamepongeza ubunifu wa Mhe Dc Muro na kuweza kuwashawishi wadau kupeleka Maji katika kata yao ambapo wamesema kitendo kilichofanywa na Dc Muro ni Cha Kizalendo na kinapaswa kupongezwa na kila mwananchi wa Arumeru pasipo kujali Itikadi ya vyama vya kisiasa, dini au ukabila ambalo wamemtaka Dc Muro aendelee kuchapa kazi Kwa kuweka Misingi ya kizalendo.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru

Halotel kuwazawadia wateja wake maadhimisho ya miaka 3

$
0
0
- Wateja kupata fursa kutoa mawazo kuboresha huduma.


Ikiwa katika shamrashamra ya kuadhimisha miaka 3 ya utoaji wa huduma kwa watanzania, Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imetangaza mpango wa kutoa huduma ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja.

Mpango huo uliopewa jina la “LONGA TUSONGE” pamoja na faida zingine una lengo la kuwashirikisha wateja wote pamoja na wafanyakazi wa Halotel katika kufanya maboresho ya utoaji huduma mbalimbali kupitia mawazo yao wakati huu ambapo kampuni hiyo inapoadhimisha miaka mitatu ya utoaji huduma zake za Mawasiliano hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, mkakati huo ni sehemu ya kuthamini mchango mkubwa wanaoutoa wateja wake tangu kuanza kutolewa kwa huduma kupitia mtandao huo hapa nchini .

Amesema tangu kuingia kwa huduma za Mtandao huo wa Halotel, wamekuwa wakipata matokeo mazuri ya wateja wake wanaondeelea kutumia huduma zake mbalimbali hadi wakati huu ambapo wanakuja na mpango huo mpya wa “LONGA TUISONGE”

Amesema kupitia mpango huo wa mwaka mmoja, wateja wa mtandao huo watapewa nafasi ya kutoa mawazo yao mbalimbali ya kuboresha huduma za Halotel ambayo baadae yatachujwa na kwa yale yatakayokidhi matakwa yatapitishwa na kuwa huduma rasmi ndani ya mtandao huo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda,(kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la Longa Tusonge. Kulia ni Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias.
Msaidizi wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias ( kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la “Longa Tusonge”. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda.

BENKI YA TIB CORPORATE YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTEMBELEA WATEJA WAKE

$
0
0
BENKI ya TIB Corporate waadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwatembelea wateja mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MICHUZI BLOG leo Mkuu wa masoko na mahusiano wa benki ya TIB, Theresia Soka
 amesema kuwa lengo la kutembelea wateja wao ni kujitathimini jinsi wanavyotoa huduma kwa wateja mbalimbali wa benki hiyo katika wiki ya huduma kwa wateja.

"Benki ya TIB Corporate katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja tunawatembelea wateja wetu ili kujitathimini ni wapi tunakosea ili tufanye marekebisho."

Pia amewakaribisha wateja mbalimbali kujiunga na benki hiyo kwani benki hiyo 
 
Nae Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Usimamiz wa Bandari (TPA), Nuru Mhando amewashukuru wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate kwa kuchagua kumtembelea na anajivunia kuwa mteja wa benki hiyo.

Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani wa benki ya TIB Corporate, Edwin Katanga akimkabidhi ua Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Usimamiz wa Bandari (TPA), Nuru Mhando mara baada ya kumtembelea ikiwa ni kuthamini mchango wa taasisi mbalimbali katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Usimamiz wa Bandari (TPA), Nuru Mhando kulia akizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi hao ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja.
Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Usimamiz wa Bandari (TPA), Nuru Mhando mara baada ya kutembelea ofisi ya TPA kwaajili ya kuadhimisha siku ya huduma kwa mteja ambayo hufanyika kila Oktoba.
Mkuu wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na wiki ya huduma kwa mteja ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba katika taasisi mbalimbali na mashirika mbalimbali duniani kote.

WAKANDARASI WA UMEME VIJIJINI WATAKIWA KUTOFICHA VIFAA VYA UMETA

$
0
0
WAZIRI wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kutoficha vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) wakati wa usajili wa wananchi wanaohitaji kuunganishwa na huduma hiyo. 

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, aliyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga ambapo alizindua huduma ya umeme katika kijiji cha Magaoni na Kibiboni vilivyopo wilayani Mkinga na Kijiji cha Tingeni na Kwabota vilivyoko wilayani Muheza. 

“ Ni marufuku kwa mkandarasi kuficha vifaa vya Umeta wakati wa usajili wa wananchi, hakikisheni vifaa hivi vinakuwepo na mwananchi awe huru kuchagua kama anahitaji kuunganishiwa umeme kwa kutumia UMETA au kuingia gharama ya kutandaza nyaya ndani ya nyumba yake,”alisema Dkt Kalemani. 

Alisema kuwa, kila mkandarasi amepewa vifaa vya Umeta 250 kwa kila eneo lake la mradi hivyo wana wajibu wa kuhakikisha kuwa, wananchi wanafahamu uwepo wa vifaa hivyo ili kuwapunguzia gharama za kutandaza nyaya ndani ya nyumba. 

Katika mikutano yake na wananchi, Dkt Kalemani aliwahamasisha kutumia vifaa hivyo kwani Mkandarasi anapomaliza idadi ya Umeta aliyokabidhiwa na Serikali, vifaa hivyo huuzwa kwa bei ya shilingi 36,000 . 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuanza kupatikana kwa umeme katika Kijiji cha Magaoni wilayani Mkinga mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mbunge wa Mkinga, Dunstan Kitandula. 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (mwenye kipaza sauti) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kibiboni wilayani Mkinga, Mkoa wa Tanga ambapo pia alizindua huduma ya umeme katika Kijiji hicho. 
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) na Mbunge wa Mkinga, Dunstan Kitandula wakipongezana mara baada ya Mbunge huyo kukabidhiwa vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) vitakavyotumika kuunganishia umeme wananchi wa Kijiji cha Magaoni wilayani Mkinga mkoani Tanga. 
Baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magaoni mkoani Tanga.

MAKATIBU KAMATI WAANDAA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
  Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Pamela Pallangyo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo mbele ya Makatibu Kamati katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
  Mkurugenzi Msaidizi kamati za Bunge Masuala ya Fedha na Uchumi, Ndg. Michael Chikokoto akizungumza jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati mbele ya Makatibu Kamati (hawapo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika leo Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kamati za Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Dickson Bisile
Mkurugenzi wa Kamati za Bunge, Ndg. Athuman Hussein (wa pili kushoto) akizungumza na Makatibu Kamati (hawapo kwenye picha) wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati mbele ya Makatibu Kamati katika kikao kilichofanyika leo Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ndg. Grace Bidya na kulia ni Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Pamela Pallangyo


(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.8 ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

$
0
0
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.65 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.32 na kuongeza kuwa ukusanyaji wa mapato hayo umekuwa ukiongezeka kila mwezi.

“Katika mwezi Julai, 2018, TRA ilikusanya jumla ya shillingi trillioni 1.20 sawa na ukuaji wa asilimia 9.20, mwezi Agosti, 2018 jumla ya shilingi trillioni 1.27 zilikusanywa ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.86 wakati mwezi Septemba, 2018 mamlaka ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.36 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.65,” alisema Kayombo.

Kayombo amewashukuru walipakodi wanaoendelea kulipa kodi zao kwa hiari na wakati na amewahimiza wale wote ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo na wale wenye changamoto mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za TRA mikoani na wilayani ili kuonana na mameneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Aidha, Kayombo amesema TRA inaendelea na zoezi la kupokea maombi ya misamaha ya riba na adhabu katika malimbikizo ya madeni ya kodi za nyuma ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa jumla ya walipakodi 1,950 wamewasilisha maombi ya kusamehewa riba na adhabu ambayo yanafikia jumla ya shilingi bilioni 185.4.

“Mwitikio wa walipakodi kuomba msamaha wa wa riba na adhabu ni mkubwa na unaridhisha na kuna baadhi ya walipakodi waliowasilisha maombi ambao wameshapewa majibu na wengine wako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa maombi yao. Hivyo, nachukua fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara ambao hawajawasilisha maombi wawahi kuwasilisha maombi hayo kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

Mkurugenzi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kuwaasa wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya kugushi risiti za kielektroniki za EFD nchi nzima hasa maeneo ya Kariakoo, kuacha mara moja kwa sababu wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu makusanyo ya kodi kwa kipindi cha miezi mitatu kwa mwaka wa feda 2018/2019. Kulia ni Meneja wa huduma na elimu kwa mlipakodi Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Gabriel Mwangozi.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kulia ni Meneja wa huduma na elimu kwa mlipakodi Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Gabriel Mwangozi na kushoto Meneja wa huduma na elimu kwa mlipakodi Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA).
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

OCD Kyerwa ashushwa cheo,ahamisishwa

$
0
0
Timu ya Uchunguzi ya wasindikizaji wa Kahawa ya magendo yaundwa
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Nchini limetuma kikosi cha uchunguzi kufatilia tuhuma za askari waliokuwa wakisindika Kahawa ya Magendo wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Uchunguzi huo unatokana na kauli ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya kutaka kufanyika uchunguzi kwa askari hao waliohusika kusindikiza Kahawa ya magendo.

Akizungumza na waandishi habari Jijini Dar es Salaam Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa amesema katika uchunguzi huo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kyerwa (OCD) Justine Joseph ameshushwa cheo pamoja na kuhamishwa katika Kituo cha kazi.

Amesema aliyekuwa OCD wa Wilaya Kyerwa Justine Joseph amehamishiwa mkoani Iringa na kuwa chini ya uangalizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa.

Amesema uchunguzi huo ukikamilika watatoa  majibu kwa wale  waliohusika na tuhuma za usindikizaji wa Kahawa ya magendo.

Aidha amesema kuwa wakati Polisi  wanafanya operesheni wananchi wanatakiwa kutii amri hiyo.

Mwakalukwa amesema tukio lilotokea mkoani Songwe la Mtu kupigwa risasi ilitokana na wananchi kutotii amri ya polisi wakati wakifanya operesheni ya waganga wa jadi lambalamba.

"Amri ya Polisi inatakiwa wananchi watii ili kuweza kuepuka na madhara yatayotokea mara baada ya kusaidia"amesema Mwakalukwa.Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

ZAIDI YA WATOTO 1,300 KUSHIRIKI KAMPENI YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO WA MIKOANI

$
0
0
 Baadhi ya vijana ambao wanashiriki kampeni hiyo ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani Iringa zoezi ambalo linaenda sambamba na utoaji elimu ujasiriamali kupitia michezo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
ZAIDI ya watoto 1,300 wamejuishwa katika kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani 


Iringa zoezi ambalo linaenda sambamba na utoaji elimu ujasiriamali kupitia michezo.

Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wasichana kiuchumi uliochini ya shirika la BRAC Anna David amewaambia waandishi wa Habari katika viwanja vya chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE)  

kuwa lengo la kufanya michezo hiyo kuwaleta pamoja watoto kutoka pande mbalimbali na kuwapa elimu juu ya kupinga ukatili kwa wasichana siku chache kabla ya kufikia maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike yatakayofanyika baadae Octoba 11 mwaka huu katika viwanja vya mwembetogwa mjini Iringa.

Bi David alisema katika maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Salum Hapi anatarajia kuwa mgeni rasmi, maamisho ambayo siku ambayo vilevile ulimwengu unaadhimisha.

Mratibu wa mradi huo alisema waliamua kuijumuisha mkoa wa Iringa baada ya kuona unakabiliwa na visa vya ukatili na hadi sasa wamekwisha kuunda klabu zipatazo 50 ambazo zimekuwa zikitumika kutoa elimu ya kupingana vitendo vya ukatili, ujasiriamali ,kuibua vipaji vya watoto ,kuwafundisha namna ya kuweka fedha na kujiajiri.

Mashindano hayo yameshirikisha watoto wa shule za msingi,sekondari na baadhi ya watoto ambao wameshindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu tofauti.

Alisema kuwa kupitia michezo chini ya mwavuli wa shirika lisilo la kiserikali la BRAC wamepeleka zaidi ya watoto 160 chuo cha veta kwa ajaili ya kujifunza ujasiriamali.

Nao baadhi ya washiriki wa michezo hiyo Sarafina Mwinuka alisema kuwa amepata elimu ambayo itamsaidia kuepuka na mambo yasiyofaa ikiwamo usinzi,ndoa na mimba za utotoni.

Naye agetine Joseph na Neema Pius walisema kuwa wanajifunza stadi mbalimbali za maisha ikiwamo kuweka akiba,kujitambua na michezo hiyo imefanyika ikiwa wanaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili kwa watoto.


TRA YAKUSANYA TRILIONI 3.8 ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA 2018/19

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.65 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.32 na kuongeza kuwa ukusanyaji wa mapato hayo umekuwa ukiongezeka kila mwezi.

“Katika mwezi Julai, 2018, TRA ilikusanya jumla ya shillingi trillioni 1.20 sawa na ukuaji wa asilimia 9.20, mwezi Agosti, 2018 jumla ya shilingi trillioni 1.27 zilikusanywa ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.86 wakati mwezi Septemba, 2018 mamlaka ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.36 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.65,” alisema Kayombo.

Kayombo amewashukuru walipakodi wanaoendelea kulipa kodi zao kwa hiari na wakati na amewahimiza wale wote ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo na wale wenye changamoto mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za TRA mikoani na wilayani ili kuonana na mameneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Aidha, Kayombo amesema TRA inaendelea na zoezi la kupokea maombi ya misamaha ya riba na adhabu katika malimbikizo ya madeni ya kodi za nyuma ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa jumla ya walipakodi 1,950 wamewasilisha maombi ya kusamehewa riba na adhabu ambayo yanafikia jumla ya shilingi bilioni 185.4.

“Mwitikio wa walipakodi kuomba msamaha wa wa riba na adhabu ni mkubwa na unaridhisha na kuna baadhi ya walipakodi waliowasilisha maombi ambao wameshapewa majibu na wengine wako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa maombi yao. Hivyo, nachukua fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara ambao hawajawasilisha maombi wawahi kuwasilisha maombi hayo kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

Mkurugenzi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kuwaasa wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya kugushi risiti za kielektroniki za EFD nchi nzima hasa maeneo ya Kariakoo, kuacha mara moja kwa sababu wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza makusanyo ya robo mwaka ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ambapo TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84. Kulia kwake ni Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla na kushoto kwake ni Meneja Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Grabriel Mwangosi.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano ambao Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (hayupo pichani) ametangaza makusanyo ya robo mwaka ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ambapo TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84.

“VITENDO VYA UKEKETAJI KWA WATOTO WADOGO NCHINI VICHUNGUZWE”- DKT. NDUGULILE.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam.
Serikali imeagiza kuchunguzwa kwa vitendo vya ukatili hasa ukeketaji kwa watoto wachanga unaondelea kufanyika nchini kwa baadhi ya makabila yenye mila za ukeketaji wamebadili mbinu na kuanza kukeketa watoto wachanga kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo wakati akiongea na vyombo vya habari katika mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana masuala ya ukeketaji,mimba na ndoa za utotoni.

Naibu Waziri Ndugulile amesema kufuatia jamii hizo kubadili mwenendo wa ukeketaji na Serikali kubaini mbinu hizo amesisitiza agizo lake alilolitoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika Mkoani Arusha la kuwataka madaktari wote nchini kufanya uchunguzi kwa watoto wote wachanga ili kubaini kama watoto hao wamefanyiwa ukatili kwa kukeketwa ili wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa utafiti unaonesha kuwa takwimu za mimba za utotoni bado ziko juu Nchini nakutaja mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni kuwa ni Katavi 45%, Tabora%, Morogoro 39%,Dodoma 39%, na Shinyanga 34%.

Aidha ameamuagiza Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushirikiana na Idara Kuu ya Afya kuona namna bora ya kupamba na vitendo hivyo na kuhakikisha vitendo vya ukeketaji kwa watoto wachanga vinakomeshwa nchini.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kutoka  vyombo mbalimbali vya habari wakati wa mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
 Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto John Jingu akielezea jitihada za Wizara katika kukabiliana na vitendo vya uaktili kwa watoto wa kike kwa vyombo vya habari wakati wa mdahalo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
 Baadhi ya Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari na wadau wa mtoto wa kike wakifuatilia mdahalo wa Kitaifa kuliofanyika jijini Dar es Salaam   kuhusu namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa mtoto wa Kike kuelekea Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto John Jingu akiwa katika picha na viongozi nz wajumbe wa Baraza la watoto la taifa na wadau wa maendeleo na ustwi wa Mtoto mara baada ya kumalizika kwa mafunzo kwa watoto kuhusu mimba na ndoa za utotoni yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kitengo cha Mawasilianio WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DED BAGAMOYO APANGA VIKOSI KAZI KUFUATILIA VYANZO VYA MAPATO ILI KUONGEZA MAPATO YA NDANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

HALMASHAURI ya wilaya ya Bagamoyo, imeanza kusambaza vikosi kazi vya wataalamu ambao watatembelea na kufuatilia vyanzo vya mapato yake ya ndani kujua changamoto zinavyovikabili ili kufikia asilimia 25 ya makusanyo kwa kila robo ya mwaka .

Aidha halmashauri hiyo, imetumia milioni 20 ya mapato yake na nguvu za wananchi ,kujenga makalavati makubwa matatu kata ya Kilomo ,hatua iliyosaidia kupitika kwa barabara na kuongeza mapato ya chanzo cha machimbo ya mchango .

Akielezea walivyojipanga katika eneo la ukusanyaji wa mapato ,mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ,Fatuma Latu ,alisema ,wamekubaliana kuwe na vikosi kazi kufuatilia japokuwa wapo wakusanya mapato ,kodi kwenye kata .

Alisema, itawezesha kwenda pamoja na mpango mkakati wa kimkoa wa Pwani ,kuwa kila robo ya mwaka kukusanya asilimia 25 na kama usipofikia utoe changamoto halisi iliyosababisha kutofikia lengo hilo .

Latu alieleza ,moja ya majukumu yao ni kuhakikisha halmashauri inakusanya mapato kwa kiasi kikubwa kulingana na vyanzo vya mapato .

"Mwaka Jana tuliunda kikosi kazi cha kutambua vyanzo baada ya kugawanyika Bagamoyo na Chalinze "

"Kilichofuata sasa ni kununua mashine za kutosha (posi )kwa ajili ya ukusanyaji mapato ,kutoa elimu kwenye mikutano ya maeneo na madiwani na wenyeviti wa vitongoji kushirikiana kusimamia ukusanyaji wa mapato na kodi,"alibainisha Latu .

Alifafanua kwa asilimia kubwa wanategemea chanzo cha mchanga katika kata ya Kilomo ambayo ndio yenye vibali hivyo.

Alieleza kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 walipata changamoto kubwa ya mapato madogo kwenye eneo hilo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kutoa makalavati makubwa matatu .

"Tunalitegemea sana eneo hilo kuinua mapato yetu ,mwaka jana tuliyumba ,na bahati mbaya hakukuwa na fedha iliyoelekezwa kutengeneza barabara hiyo kupitia TARURA "alieleza Latu

"Kwahiyo tuliamua na kujitahidi kutoa fedha za mapato ya ndani na nguvu za wananchi ,hivyo tunatarajia mapato yatapanda na kurudi kwenye hali yake kwenye chanzo hicho "alisema .

Kwa mujibu wa Latu , vyanzo vingine wanavyovitegemea kuongeza mapato ya ndani ni soko la samaki huko feri ya Bagamoyo na stendi .

Diwani wa kata ya Kilomo Hassan Wembe ,alisema chanzo kikuu kinachoongoza cha mapato ni ushuru wa mchanga na kata inayoongoza kwenye chanzo hicho ni Kilomo na Yombo .

Alisema kawaida kwa mwezi makusanyo  hayo hufikia sh .mil 80 kwa mwezi ambapo kwenye robo ya mwaka hupatikana hadi sh.milioni 280 lakini kwa mwaka jana kilishuka kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu kutokana na mvua .

Nae diwani wa kata ya Yombo Mohammed Usinga alisema ,watashirikiana na halmashauri kuhakikisha wanaimarisha na kuboresha mapato .

Usinga, alisema watasimamia na miradi ya maendeleo na fedha za umma ndio maana wamepata hati safi .

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Kawawa alitoa rai kwa wataalamu ,madiwani na watendaji wa halmashauri hiyo kuwa wamoja na kushirikiana ili kuleta maendeleo chanja.

UFUNGUZI WA MDAHALO WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUELEKEA SIKU YA MTOTO WA KIKE 2018

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya kusini amewataka Viongozi wa Majimbo kusikiliza kero za Vijana ili kuweza kuzipatia ufumbuzi

$
0
0
Na Takdir Ali-Maelezo Zanzibar
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Abdul-aziz Hamad Ibrahim amewataka Viongozi wa Majimbo kusikiliza kero za Vijana ili kuweza  kuzipatia ufumbuzi.

Amesema vijana wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo hivyo iwapo Viongozi wanapita na kuwatatulia matatizo yanayowakabili wataweza kuongeza juhudi za kukipatia ushindi chama cha Mapinduzi ifikapo 2020.

Ameyasema hayo huko Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani alipokuwa akizungumza na Vijana wa Tawi la Mpendae juu katika ziara ya kubadilishana mawazo na Vijana wa Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani Wilaya ya Kusini.

Ameeleza kuwa Vijana wana matatizo mengi ikiwemo Ajira na elimu lakini baadhi ya Viongozi hawasaidii kitu chochote cha kuweza kujiendesha maisha  jambo ambalo linawavunja moyo na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

“Matatizo ya vijana ndani ya nchi  ni mengi ikiwemo ukosefu wa ajira hivyo viongozi wawasaidie vijana hao kwa kuwapa mitajiili waweze kujiendeleza katik maisha yao”. Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha amewataka Vijana hao kuwaacha woga na kuwafikisha katika sehemu husika Viongozi watakaowabaini kwenda kinyume na Ilani ya Chama hicho.

Hata hivyo amewataka kujiendeleza kielimu ili wapate Ajira na kuisimamia Serikali mara baada ya Viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao wa Utumishi.

Amewapongeza Vijana wa Mpendae juu kwa kufanya ziara hiyo na kusema wamepata kukaa na kujadili njia za kuwaletea maendeleo na kukipatia ushindi cha Chama Cha Mapinduzi 2020.

Amefahamisha kuwa  Serikali inatumia gharama kubwa kutafuta Wataalamu nje ya nchi lakini iwapo Vijana watajiendeleza wataziba kuziba upungufu uliopo.

Mapema akitoa maelezo katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mpendae Choum Fakih Muhudin amewapongeza Vijana wa Kizimkazi Dimbani kwa mapokezi mazuri na kuahidi kuendeleleza mashirikiano hayo yaliodumu kwa muda mrefu.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kuweza kubadilishana mawazo juu ya njia mbalimbali za kuleta maendeleo kwa Vijana na kuzidi kukiletea ushindi chama cha Mapinduzi katika Chaguzi zote zinazoshiriki hapa nchini.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI SOLAR POWER KWA ZAHANATI TATU ZA HALMASHAURI YA CHALINZE

$
0
0
Na Victor  Masangu, Chalinze
WANAWAKE  wa kijiji cha Mduma  kata Magindu  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani  kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na nishati ya umeme hivyo inawalazimu kupatiwa matibabu  kwa kutumia mwanga wa tochi au simu  pindi wanapokwenda kujifungua  katika zahanati ya Mduma  kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha yao.

Wakizungumza   kijijini hapo  kuhusiana na changamoto inayowakabili wanawake hao wamesema   kwamba kwa sasa  wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua hasa katika nyakati za usiku kutokana na kuwa na giza hivyo kuwapa wakati mgumu  wauguzi  pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Aidha walisema  kwamba kwa kipindi kirefu katika zahanati hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbali mbali za upatikanaji wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa hivyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuingilia kati suala hilo kwa lengo la kuweza kuwafikishia nishati ya umeme ambayo itakuwa ni mkombozi katika utoaji wa huduma hasa katika nyakati za usiku.

Kwa upande wake mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mduma Neema Muhagama amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya kutokuwa na nishati ya umeme hivyo inawapelekea  wakati mwingine kutumia mwanga wa tochi  za simu katika kuwapatia matibabu wagonjwa hasa kwa upande wa wakinamama wajawazito pindi wanapohitaji kujifungua.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wa katikati ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) kutoka Mkoa wa Pwani  akikabidhi msaada wa Solar Power  kwa baadhi ya wauguzi wa zahanati ya Mduma iliyopo kata ya Kibindu  katika halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo   kulia kwake ni muuguzi Neema Muhagama akipokea kwa niaba ya wenzake.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Naibu Waziri wa nishati Subila Mgalu wa kulia ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) kutoka Mkoa wa Pwani akimkabidhi msaada wa Solar Power  Martha Kilimba ambaye ni mmoja wa wauguzi  katika zahanati ya Kwamsanja iliyopo kata ya Kibindu katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa ambao wamekuwa wakipata adha ya kutibiwa kwa kutumia mwanga wa tochi za simu.
Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu kulia ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) kutoka Mkoani Pwani akimkabidhi msaada wa Solar Power mmoja wa wauguzi katika zahanati   ya Kibindu iliyopo kata ya Kibindu katika halmashauri ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BALOZI SEIF AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA KUWAHUDUMIA WALEMAVU

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Serikali Kuu kwa kushirikiana na Taasisi na Mashirika megine ya Kitaifa na Kimataifa kujenga Kituo cha Taifa kitakacholenga kuwahudumia Watu wenye ulemavu katika kuwajengea nguvu na maarifa ya kuendelea kujitegemea Kimaisha.

Alisema Ulimwengu wa sasa umebadilika kwa kubeba harakati nyingi zinazoibua matukio mbalimbali yanayosababisa Jamii kukumbwa na ajali tofauti  katokana na kasi ya maisha na hatimae kuzalisha Walemavu wanaohitaji huduma za matunzo na maarifa mengine ya Kimaisha.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuzindua rasmi Kituo cha Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo kiliopo pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni Mjini Zanzibar.

Alisema tabia ya kuwatenga Watu wenye Ulemavu haipendezi na nidhambi jambo ambalo halikubaliki katika Jamii yoyote ile. Hivyo aliwahimiza wahusika hao wasikubali kukata tamaa katika kupigania haki zao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushukuru Uongozi wa Kampuni ya Peny Royal na Kumpongeza Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo kwa jitihada zao zilizopelekea kujengwa kw kituo hicho muhimu kwa Watu wenye mahitaji Maalum.

Balozi Seif alifarajika kuona kwamba Ujenzi wa Kituo hicho umelenga kuwajengea Uwezo na maarifa Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo ili wawe Wajasiri Amali watakaokuwa na nguvu za kujiendesha wenyewe Kimaisha.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikizindua Rasmi Kituo cha Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo kilichojengwa pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni Mjini Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud.
 Balozi Seif akiangalia na kufurahia bidhaa zinazozalishwa na Watu wenye Ulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo ndani ya Kituo kipwa alichokizindua rasmi.
 Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa Kituo cha Watu wenye ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo Bibi Mrashi Mikidadi akiwasilisha Risala kwenye hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Shaurimoyo katika hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi hapo pembezoni mwa Skuli ya Sekondari ya Ufundi Mikunguni.
 Balozi Seif akimkabidhi Baskeli Mtoto mwenyeulemavu wa Jimbo la Shaurimoyo Feisal Mbarouk kwenye hafla ya uziduzi wa Kituo chao cha kazi za ujasiri amali pamoja na Ofisi hapo Mikunguni.
 - Mtoto Lutfia Mohamed ambae ni mlemavu akifurahia Baskeli mpya aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi zilizotolewa na Wafadhili mbali mbali.
 Fundi Seremala wa Kituo cha Watu wenye ulemavu cha Jimbo la Shaurimoyo Bwana Juma Abdulaah Juma akipokea Baskeli yake itakayomsaidia katika harakati zake za Kimaisha. Picha na – OMPR –ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI MABULA AMKABIDHI BIBI MASINGE HATI ZA VIWANJA VIWILI

$
0
0
Na Munir Shemweta,  Mara
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amemkabidhi Bibi Nyasasi Masige  Hati za viwanja viwili vilivyopo eneo la Bunda mkoa wa Mara na kutoa onyo kwa wataalamu wa ardhi kutotoa ushauri potofu kwa viongozi wa serikali  wakati wa utekelezaji wa majukumu ya sekta ya ardhi. 

Utoaji wa hati kwa bibi Masige unafuatia bibi huyo kuwasilisha malalamiko kwa mhe Rais John Pombe Magufuli  wakati wa ziara yake katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kutaka kudhulumiwa viwanja vyake. Hati za viwanja  alivyokabidhiwa bibi Masige ni za viwanja  Na 92 na  93/ Kitalu S/ Nyasula C vilivyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara. 

Mabula alikabidhi hati hizo pamoja na hati nyingine 92 kwa wananchi wa Bunda leo akiwa katika ziara ya siku tano katika mkoa wa Mara  kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyatoa katika ziara yake ya februari mwaka huu 2018 katika mkoa wa Mara. 

Alisema serikali inategemea wataalamu katika kuendesha shughuli zake na kitendo cha wataalamu kutoa ushauri potofu ikiwemo suala la viwanja vya bibi Masige siyo tu kunawapoteza viongozi katika kutekeleza majukumu yao  bali kunachangia kuwepo migogoro katika sekta ya ardhi. 

"haiwezekani kupima viwanja na kuchanganya viwanja vidogo, vikubwa na vya kati na kama mtaalamu ukienda kinyume utachukuliwa hatua kwa kutozingatia taaluma."" Alisema Mabula. 

Kauli hiyo ya Mabula inafuatia Kauli ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Mpilipili kueleza kuwa tatizo la viwanja vya bibi Masige lisingefikia hatua hiyo kama wataalam wa ardhi wangetoa ushauri sahihi kwa viongozi wa wilaya katika kushugulikia mgogoro wa bibi huyo.
 Bibi Nyasasi Masige akipelekwa na ndugu zake kwa ajili ya kukabidhiwa hati za viwanja vyake na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angeline Mabula leo wilayani Bunda mkoani Mara.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akimpa mkono Bibi  Nyasasi Masige mara baada ya kumkabidhi hati za viwanja vyake  wilayani Bunda mkoa wa Mara leo  ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais kushughulikia tatizo la bibi huyo.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akimkabidhi hati ya kiwanja mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Bunda mkoa wa Mara Joseph Matundilo  wakati wa ziara yake ya siku tano mkoani humo kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake  ya Februari 2018.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akizungumza na viongozi na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri mbili za wilaya ya Bunda mkoani Mara wakati wa ziara yake ya siku tano kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake aliyoyatoa wakati wa ziara ya Februari 2018. (Picha zote na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>