Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA 11 WAWASILI MBARALI KUTAFUTA SULUHU YA GN 28 YA MWAKA 2008

0
0



Makatibu Wakuu kutoka Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili wamewasili Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuanzia Oktoba 4 hadi 6, 2018 ikiwa ni ziara ya kikazi kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na vijiji vya Wilaya ya Mbarali.

Makatibu wakuu hao ni kutoka Wizara mbalimbali zikiwemo; Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Nishati, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Lengo la ziara hiyo ni Kuona na kujiridhisha mambo ambayo yanalalamikiwa kuhusiana na tangazo la Serikali namba 28 la mwaka 2008 (GN. 28 ya 2008.), kupata suruhu ya kudumu ya uchepushaji wa maji katika mto Ruaha pamoja uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mito na mito.

Maeneo yaliyotembelewa na Makatibu Wakuu hao ni pamoja na eneo chepechepe la Ihefu lililopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mashamba ya mpunga ya madibira (MAMCOS), Banio la maji lililopo eneo la Mnazi kijiji cha Warumba kata ya Ubaruku pamoja na mashamba ya Mpunga ya mnazi katika kijiji cha Mwanavala Kata ya Imalilosongwe.

Ziara hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera na Uratibu Prof. Faustin Kamuzora na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Makatibu wakuu wa Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili walipokutana Wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kutembelea maeneo ya shamba la Madibira, Eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu na eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha tarehe O5 Oktoba, 2018.

Baadhi ya Makatibu wakuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) walipohudhuria Kikao kazi hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Makatibu Wakuu walipokutana Wilayani Mbarali ili kutembelea shamba la Madibira, Eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu na eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha tarehe O5 Oktoba, 2018 Mkoani Mbeya.


TCCIA YAJIVUNIA UWEPO WAKE NA MCHANGO WALIOUTOA KWA MIAKA 30 KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KWA KUSAIDIANA NA SERIKALI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo kinajiandaa kusheherekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake huku kikijivunia mafanikio ambayo yamepatikana katika sekta ya kilimo,biashara na viwanda kutokana na uwepo wao nchini.

Kimeeleza namna ambavyo kimeshiriki kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini n katika kipindi hiki cha kusheherekea miaka 30 ya uwepo wao kabla ya kufikia siku ya kilele Novemba mwaka huu watafanya shughuli mbalimbali katika wilaya na mikoa yote nchini.

Akizungumza Dar es Salaam Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu amesema uwepo wao na mchango wake kwa Taifa mbali na kuwaunganisha vyombo mbalimbali vinavyojihusisha na kilimo,viwanda na biashara wamefanikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji.

Amesema kimsingi huko nyuma watanzania walikuwa hawashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi lakini kupitia TCCIA watanzania wameweza kushiriki kwa kuanzisha viwanda na kampuni na hivyo kuwa sehemu ya wawekezaji nchini."Kuna mengi ya kujivunia kama TCCIA ,kadri muda unavyokwenda kuelekea kwenye sherehe ya kutimiza miaka 30 tangua kuanzishwa kw TCCIA mengi tutazungumza kupitia viongozi mbalimbali.

" Baadhi ya viongozi hao wameshastaafu baada ya kuitumikia TCCIA na kutoa mchango wao mkubwa nao watapata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao,tulikotoka,tulipo na tunakokwenda,"amesema Mshiu.Kuhusu TCCIA na mchango wake kwa jamii anasema watanzania wengi wanamiliki viwanda ndani na nje ya nje ya nchi na TCCIA imetoa mchango mkubwa nchini Tanzania.
 Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu(kushoto) akiwa na aliyewahi kuwa Rais wa TCCIA David Mwaibula wakiwa wameshika cheti
Rais mstaafu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA)David Mwaibula akifafanua jambo kuhusu Chama hicho ambacho kinatarajia kusheherekea kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1988.

WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

0
0
Kutokua makini katika uratibu, usimamizi na ujenzi wa mradi wa maji mkoani Njombe kumewaweka matatani baadhi ya watendaji wa serikali na wakandarasi waliopewa dhamana ya kujenga na kufikisha majisafi na salama kwa wananchi.

Mradi uliotiliwa shaka wa Ukalawa na Kitole umesubiriwa na wananchi kwa zaidi ya miaka mitano na bado umekua butu kukidhi kiu ya wakazi wa vijiji vya Ukalawa na Kitole. Mradi huo umejengwa na kampuni ya Kihanga Farm International iliyolipwa kiasi cha Shilingi Milioni 532 kati ya Shilingi Milioni 562.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza wahusika walioshiriki katika mradi huo wakiwamo Watalaam wa maji wa Serikali popote walipo, Mhandisi Mshauri wa mradi na Mkandarasi wa mradi wasaidie Jeshi la Polisi kupata undani wa taarifa zinazohusu mradi, ikiwamo malipo yaliyofanyika wakati wananchi hawapati maji.

Mhe. Aweso (Mb) katika kikao kilichodumu kwa saa sita kilichowakutanisha watalaam wa maji, na baadhi ya walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa maji Ukalawa-Kitole, amesema miradi ya maji sio kichaka cha kupitisha fedha na kusisitiza endapo mhusika yoyote atabainika kushiriki kuhujumu mradi huo, hata kama amestaafu utumishi wa umma, atatafutwa popote alipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Baada ya kikao kumalizika baadhi ya wahusika kutoka kampuni iliyopewa kandarasi ya Kihanga Farm na wataalam wa maji wa serikali walioshiriki walikabidhiwa kwa vyombo husika ili kusaidia zaidi kwa taarifa muhimu.

Mhe. Aweso (Mb) amesema hakuna faida ya kuwa na mtalaam wa maji anayekabidhiwa mradi bila kujiridhisha na ubora wake kama taratibu zinavyotaka, ambapo imebainika moja ya udhaifu katika mradi wa maji Ukalawa-Kitole ni kwenda kinyume na mkataba, na kutozingatia ushauri wa Mhandisi Mshauri wa mradi na kubadili mfumo wa kusukuma maji kutoka wa kutumia jenereta, kwenda mfumo wa kutumia nishati ya jua (solar) wakati mazingira ya mradi sio rafiki kwa mfumo wa nishati ya jua.

Mhe. Aweso (Mb) ameagiza kutokana na udhaifu ulioonekana katika mradi huo ameagiza timu aliyoiunda akiwa mkoani Mbeya mwezi Oktoba 2018, ipite katika mradi wa maji Ukalawa na mradi wa Lugenge ambao madakio ya maji mawili yamekamilika lakini mradi bado hauridhishi na ukiwa katika asilimia 60 ya kazi pamoja na Mkandarasi kuongezewa muda.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maji na Umwagiliaji 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na watalaam wa maji, pamoja na baadhi ya wahusika walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa maji Ukalawa-Kitole katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka (kulia). 
1. Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwasikiliza baadhi ya wananchi watakaofaidika na mradi wa maji Lugenge mkoani Njombe. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb ) akipewa maelezo kuhusu kazi iliyoanza ya utandikaji wa mabomba kutoka katika dakio la maji kwenda katika tanki katika mradi wa maji Lugenge,pichani kati ni MKuu wa Mkoa wa Njombe Mh  Christopher Ole Sendeka 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipokea mrejesho wa wananchi kuhusu kero ya maji kando ya tanki la maji lililokamilika la mradi wa maji Lugenge. Mkandarasi kapewa mwezi mmoja kuhakikisha maji yanafika katika tanki hilo. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia mitambo katika mradi wa maji Kibena. 

TANZIA: Msiba Ujerumani Wa KONDO MOHAMED MSUMI a.k.a Mguu Mtupu

0
0


 Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU e.V) kwa masikitiko makubwa tunawataarifu kifo cha Mtanzania mwenzetu   Kondo mohamed Msumi  ambaye alikuwa akiishi  Bochum,nchini ujerumani.
 Marehemu Kondo Mohamed Msumi amefariki usiku wa 2.kuamikia 3 Oktoba 2018 akiwa hospitalini akipatiwa matibabu,  kamati ya Umoja  wa Watanzania Ujerumani UTU e.V imewasiliana na ndugu wa marehemu waliopo Ujerumani na Tanzania  Tumeazimia kupitisha michango  ili  kutuwezesha kufanikisha  mazishi ya ndugu yetu, bado hatujajua kwamba tutazika hapa Ujerumani au tutasafirisha, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tunavyozipata.
 Kamati imechagua Rafiki  wa karibu na familia ya Kondo ili kupokea michango hiyo. Michango yote ipitishwe kwenye acc ifuatayo.

Gls Bank,Jafari Juma Mazangwi. IBAN:DE15 4306 0967 4046 5996 00.Bic: GENODEM1GLS.

Tunawaomba watanzania wote  kutoa michango kwa wingi ili kumuhifadhi ndugu yetu marehemu Kondo Mohamed MsumiAsanteni

MAJALIWA: VIWANDA VIMEPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA

0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba.Alisema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa.

Waziri Mkuu alisema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800. “Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisisitiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kopo la kahawa wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika kahawa cha TANICA kilichopo mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama paketi ya kahawa wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika kahawa cha TANICA mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo kusindika kahawa wakati alipotembelea kwanda cha kusindika kahawa cha TANICA mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP baada ya kutembelea kiwanda chao kilichopo mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP, Theobad Mushashu (katikati) kuhusu ukoboaji kahawa wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 6, 2018. 

MOJA BETI YAUTAMBULISHA MCHEZO WA BOOM PESA JIJINI MBEYA .

0
0
KAMPUNI ya moja Beti inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha imeutambulisha mchezo mpya wa kubahatisha Jijini Mbeya, unaofahamika kwa jina la ‘BOOM PESA’, na kuwataka wakazi wa Mkoa huo kujitokeza na kununua tiketi ili waweze kujishindia fedha taslimu papo hapo.

Akizungumza leo Jijini Mbeya wakati wa kuutambulisha mchezo huo wa kubahatisha, Msimamizi wa kituo cha huduma kwa Wateja kutoka Moja Beti Florida Mwangosi, amesema mchezo huo ni mpya lakini ni rahisi sana kupata fedha tofauti na michezo mingine .

“ Huu mchezo wetu wa kubahatisha unaofahamika kwa jina la Boom Pesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea” Alisema Florida Mwangosi .

Naye Balozi wa Boom Pesa Sabrina Ibrahimu, alisema mwitikio kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye mchezo huo wa kubahatisha ni mkubwa sana , nakwamba wananchi zaidi ya 100 kwa siku moja walijitokeza na kushiriki mchezo huo .

“ Tunawashukuru sana wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuupokea huu mchezo wetu mpya wa kubahatisha , nawapongeza sana maana wamekuja na baadhi wameshinda tunawashukuru sana tunawaomba waendelee kuucheza mchezo huu” Alisema Sabrinma Ibrahimu .

Aidha Baadhi ya washindi wa Boom Pesa kutoka Jijini Mbeya ambao ni Yasinta Ndesabula na Taison John waliliambia gazeti hili kuwa ni mchezo ambao wao hawakutegemea kama wangecheza na kushinda, ambapo wamewahimiza watanzania wengine kucheza ili waweze kujishindia fedha taslimu

Balozi wa mchezo wa kubahatisha wa BOOM PESA kutoka kampuni ya MOJA BET Diana Thomas, akitoa maelekezo kwa moja ya wateja wa kampuni hiyo jinsi ya kushiriki na kucheza huo wakati wa uzinduzi wa BOOM PESA uliofanyika leo jijini Mbeya. Kwa BOOM PESA, washiriki wanajishindia pesa taslimu papo hapo kwa kuweka dau ya kuanzia TZS1000 kupitia simu za mkononi. 

VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI

0
0
Vijana nchini watakiwa kubadili mtazamo kwa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayowawezesha kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipofanya ziara hiyo Mkoa wa Iringa kwa lengo la Kuhamasisha na kukagua maeneo ya ujenzi wa Vitalu Nyumba (Green House) na uwepo wa miundombinu itakayotumika kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mhagama amesema sekta ya kilimo inaajiri na kuchangia katika pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 60%, hivyo vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wakatumie rasilimali ardhi kama mtaji wa kujiajiri na kuweza kuajiri wenzao.

“Lengo letu ni vijana kutumia sekta hii ya umahiri kwa ajili ya kuwaondoa kwenye mitazamo finyu na kuwa na mitazamo chanya ili waweze kunufaika na miradi itakayo buniwa na kutumika kama mfano kwa vijana nchi nzima.” Alisema Waziri Mhagama

Aliongeza kuwa vijana watafundishwa kilimo cha Kitalu nyumba ambavyo vitawawezesha kuongeza thamani kwenye mazao watakayozalisha na mradi huo ukawe sehemu ya ajira zao.Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi zao ili kutimiza adhima ya vijana wote.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kuwasili ofisini hapo kwa ajili ya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yaliyotengwa kujenga vitalu nyumba mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara mkoani humo ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bw. Fikira Kisimba. 
Baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu waliombatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika ziara ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba. (Kulia ni) Afisa Vijana Mwandamizi Bw. Gedfrey Massawe na Afisa Kazi Bi. Neema Moshi. (Kushoto ni) Afisa Elimu wa Mkoa Bw. Richard Mfugale. 

RIDHIWANI KIKWETE AWAPONGEZA BENK YA NMB.

0
0

Na Shushu Joel,Chalinze.
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani pwani Ridhiwani Kikwete ameipongeza Benk ya Nmb kwa juhudi zao za kutoa misaada kwa jamii ili kutatua changamoto mbalimbali zinazokuwa zikiwakabili wanajamii.

Akitoa pongezi hizo jana, katika kata ya kiwangwa alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya hospital vilivyotolewa na benk hiyo,Ridhiwani alisema kuwa awali hospital hiyo ilikuwa na changamoto ya vitanda kwa ajili ya kinamama kuweza kujifungulia lakini kutokana na msaada huo tatizo hilo limebaki kuwa ni historia .

“Naipongeza benk ya Nmb kwa kutambua thamni ya kinamama wa chalinze ingawa katika nchi yetu kuna changamoto nyingi sehemu zingine lakini nyie mmeamua kutuletea misaada huu katika halmashauli yetu ya chalinze”Alisema Ridhiwani

“Mimi nawatia moyo tu kwa niaba ya wananchi wa chalinze msichoke kutusaidia kwani mahitaji yetu bado ni mengi ingawa nasi kama serikali tunapambana ili kuihakikisha kinamama wanajifungua bila matatizo ya aina yeyote hile ndio maana hata vifo vya kinamama chalinze wakiwa wanajifungua vinazidi kubaki kuwa historia”

Aliongeza kuwa awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa viwanda kwa ajili ya kinamama kujifungulia katika hospital hiyo lakini Nmb imewapatia vitanda 10 kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo hivyo amewataka wananchi wa kata hiyokwa kushirikiana na watumishi wa hospital hiyo kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia kwa kipindi kirefu.
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete  akipokea vifaa vya wagonjwa kwa ajili ya hospital ya kiwangwa vilivyotolewa na benk ya Nmb
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete  akipokea vifaa vya wagonjwa kwa ajili ya hospital ya kiwangwa vilivyotolewa na benk ya NMB.



SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA

0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM – Hydom,Manyara. 

Serikali imejipanga kuanzisha programu ya kukusanya na kuhifadhi taarifa jamii za kitanzania ambazo asili ya utamaduni wake upo hatarini kupotea. 

Kauli hiyo imetolewa leo katika Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini, Mkoani Manyara na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi alipokuwa akifunga Tamasha la Saba la Utamaduni wa Pembe Nne (7th Four Corner Cultural Festival) kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ambaye ndiye alikuwa afunge tamasha hilo. 

Bi.Mlawi alitoa pongezi kwa waandaaji wa tamasha hilo linahusisha makundi manne ya lugha yanayopatikana barani Afrika ila kwa Tanzania yanapatikana mkoani Manyara na jirani ambapo kwa sasa yameanza kupoteza asili yao na utamaduni wake ambayo ni Wahdzabe-Khoisan,Iraqw-Cushits,Datooga-Nilotic na Wabantu-Wanyiramba/ Wanyisanzu. 

“Kupitia Idara ya Utamaduni iliyo chini ya Wizara hii nitaunda Kitengo kitakacho kuwa kinashughulikia suala la ukufanyaji wa taarifa za makabila mbalimbali nchini katika mfumo wa picha jongefu pamoja na uandishi wa historia fupi makabila hayo kwa lengo la kuweza kuhifadhi taarifa hizo kwa maslai ya vizazi vijavyo”alisema Bi.Mlawi. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi akipongeza uongozi wa Four Corner Cultural Programme (4CCP) kwa kuendesha lenye kuenzi Utamaduni,Mila na Desturi za makabila manne yanayopatikana barani Afrika ambayo niyakujivunia leo katika sherehe za kufunga tamasha hilo lililofanyika katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi akimkabidhi cheti cha ushiriki muwakilishi wa Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw.Gibson Ngolongolo leo katika sherehe za kufunga tamasha la saba la 4CCP lililofanyika katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini .
Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe.Flatei Massey na Mratibu wa Kituo cha Four Cultural Programme Bi.Eliminata Awet wakiwa wamejiwekea nyoka mabegani anayetumika kuchezea ngoma ya kikiundi cha wasukuma kutoka Mwanza wakati wa Sherehe za Kufunga Tamasha la Four Corner Cultural Festival liloandaliwa na 4CCP na kufanyika leo katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini,wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi.
Baadhi ya Vijana kutoka Jamii ya Kidatooga wakicheza ngoma ya asili ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi(hayupo pichani) katika himaya ya nyumba yao iliyopo katika kituo cha makumbusho ya Four Corner Cultural Programme (4CCP) leo katika sherehe za kufunga tamasha la saba la Four Corner Cultural Festival lililofanyika Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini.

OCD KYERWA ATUHUMIWA KUSINDIKIZA KAHAWA YA MAGENDO

0
0
*Waziri Mkuu aagizwa achukuliwe hatua

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi awachukulie hatua askari polisi wote wa wilaya ya Kyerwa wanaotuhumiwa kusindikiza kahawa ya magendo inayouzwa nchi jirani akiwemo Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Justin Joseph.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 7, 2018) baada ya kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Nkwenda wilaya Kyerwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.

“Askari polisi wa wilaya ya Kyerwa pamoja na OCD wao wanatuhumiwa kusindikiza kahawa inayosafirishwa kwa njia ya magendo kwenda nchi ya jirani kupitia njia mbalimbali zisizo rasmi zikiwemo za Kumisongo, Kashaijo na Omukatoma.”

Waziri Mkuu amesema ni jambo la hatari kama askari Polisi wanasindikiza kahawa inayouzwa kwa magendo, hivyo ameagiza jambo hilo lidhibitiwe haraka.”Marufuku kupeleka kahawa nje ya nchi kwa njia ya magendo na polisi msishiriki katika butura.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amesema kuanzia msimu ujao wa kahawa, minada yote ya kahawa inayozalishwa mkoani Kagera itafanyika ndani ya mkoa huo badala ya kufanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Kaderes kilichopo eneo la Nyakatuntu wilayani Karagwe Oktoba 7, 2018.  Kulia ni Mkewe Mary na kushoto ni Mkurugenzi  wa kiwanda, Leonard Kachobonaho. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco  Elisha Gaguti. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakimfariji mtoto , Mathews Martin aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Kayanga wilayani Karagwe, Oktoba 7, 2018. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Joyce Martin.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia mti alioupanda baada ya kutembelea Kituo cha Afya cha Kayanga kilichopo Karagwe, Oktoba 7, 2018. Wapili kulia ni mkewe Mary.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kayanga Changarawe, Karagwe kuhukutubia mkutano wa hadhara, Oktoba 7, 2018.

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA MKOBA ILI KUJENGA UWEZO HOSPITALI ZA RUFAA

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imeanza programu ya kutoa huduma kwa njia ya mkoba ili kujenga uwezo wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini hasa katika maeneo yenye upungufu wa watalaam au maeneo yenye watalaam lakini wanahitaji kuongezewa ujuzi zaidi katika fani mbalimbali. 

Hayo yameswa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha wakati anazungumzia huduma hiyo.

Amesema kuwa utoaji wa huduma hiyo ni sehemu ya mpango mkakati wa Hospitali iliojiwekea kuhakikisha inatembelea Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma kwa wananchi ambao wangepewa rufaa kwenda Muhimbili kupata matibabu wakati huohuo ikijenga uwezo wa watalaam."Hospitali ya Taifa Muhimbili ina majukumu makuu matatu ambayo ni kutoa huduma za ubingwa wa juu, kufundisha na kufanya utafiti hivyo huduma kwa njia ya mkoba ni kiungo kikubwa cha jukumu letu hapa nchini," amesema Aligaesha. 

Ameongeza katika kutekekeleza majukumu hayo walifanya mawasiliano na hospitali kadhaa nchini na wenzao Hospitali ya Rufaa ya Musoma wamekuwa wa kwanza kuitikia mwito na kuwaomba wawatembelee."Hivyo tumepeleka timu ya watalaam 14 ili kutoa huduma kwa pamoja na kuwajengea uwezo katika maeneo ya upasuaji wa watoto na watu wazima, kina mama, njia ya mkojo, huduma za macho, huduma za upasuaji wa pua, koo na masikio." Aidha tumepeleka pia watalaam wa tiba ya dawa za usingizi na mtalaam wa patholojia katika timu hiyo. Timu hiyo itatoa huduma kwa muda wa siku tano mfululizo,"amesema.

Pia amesema wananatoa mwito kwa wananchi walioko Mkoa wa Mara na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo zitakazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma.

" Utaratibu wa kupata huduma ni uleule unaotumika katika Hospitali husika,"amesisitiza.Ameongeza wanatoa mwito kwa wananchi na wadau kujitokeza kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kutoa huduma mikoani hususani katika kuchangia huduma za usafiri, gharama za vifaa vinavyotumika kutoa huduma husika na matumizi mengine ili kufanikisha azma yao ya kuwafikia wananchi wengi zaidi na hatimaye kupunguza rufaa.

MBUNGE MWINGINE WA CHADEMA JIMBO LA SIMANJIRO JAMES OLE MILLYA ATANGAZA KUACHIA NGAZI CHADEMA NA KUREJEA CCM

0
0
 
Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mhe. James Ole Millya leo ametangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuomba kurejea ndani ya chama chake cha zamani CCM


WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA

0
0
Na Felix Mwagara, Mwanza. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (pichani) , amefiwa na mdogo wake aitwae Josiah Chitage Lugola, aliyekua anaishi jijini Mwanza. Waziri Lugola ambaye ndiye Msemaji wa familia hiyo, alisema mdogo wake Josiah (51) alifariki dunia leo asubuhi Oktoba 7, 2018 na mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika Hospitali ya Sekour Toure, jijini Mwanza. 
Waziri Lugola aliongeza kuwa, msiba upo Kijiji cha Nyamitwebili, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Waziri Lugola alikua wilayani Bunda kikazi ndipo akapata taarifa hizo za kushtukiza za msiba wa mdogo wake. 
Waziri Lugola alisema msiba huo ni wa ghafla, umeshtua familia na hakika mdogo wake huyo ameacha pengo kubwa katika ukoo wao. 
"Msiba huu ni mkubwa, na pia umetikisa familia yetu, kifo kinapangwa na Mungu, hivyo tunamuombea Mungu, mdogo wangu apokelewe peponi, amina," alisema Waziri Lugola. 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, ametoa pole kwa Waziri Lugola pamoja na familia kwa ujumla. 
"Wizara inatoa pole kwa familia ya Waziri Lugola, ndugu wote, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo," alisema Kingu.
 Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, taarifa za mazishi zitatolewa baada ya kikao cha familia.

OCD KYERWA ATUHUMIWA KUSINDIKIZA KAHAWA YA MAGENDO, Waziri Mkuu aagizwa achukuliwe hatua

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi awachukulie hatua askari polisi wote wa wilaya ya Kyerwa wanaotuhumiwa kusindikiza kahawa ya magendo inayouzwa nchi jirani akiwemo Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Justin Joseph.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 7, 2018) baada ya kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Nkwenda wilaya Kyerwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.


“Askari polisi wa wilaya ya Kyerwa pamoja na OCD wao wanatuhumiwa kusindikiza kahawa inayosafirishwa kwa njia ya magendo kwenda nchi ya jirani kupitia njia mbalimbali zisizo rasmi zikiwemo za Kumisongo, Kashaijo na Omukatoma.”

Waziri Mkuu amesema ni jambo la hatari kama askari Polisi wanasindikiza kahawa inayouzwa kwa magendo, hivyo ameagiza jambo hilo lidhibitiwe haraka.”Marufuku kupeleka kahawa nje ya nchi kwa njia ya magendo na polisi msishiriki katika butura.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amesema kuanzia msimu ujao wa kahawa, minada yote ya kahawa inayozalishwa mkoani Kagera itafanyika ndani ya mkoa huo badala ya kufanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu amesema minada yote ya kahawa ikifanyika mkoani Kagera itawawezesha wakulima kulipwa fedha zao kwa muda mfupi na pia itapunguza makato  yasiyokuwa ya lazima ambayo ni kero kwa wakulima.

“Wanunuzi watafuata kahawa ilipo, utaratibu huu utawawezesha wakulima kulipwa fedha zake kwa wakati. Mnada ukifanyika katika maeneo ya uzalishaji utamuwezesha mkulima kujua bei, tofauti na unavyofanyika Moshi kwani ni rahisi mkulima kuibiwa.”

Waziri Mkuu amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali yao ambayo imedhamiria kuwaletea maendeleo na kwamba itahakikisha kila mmoja anapata haki yake wakiwemo wakulima ambao watasaidiwa katika kutafutiwa masoko ya mazao yao.

WATANZANIA WAASWA KUPIMA MACHO MARA KWA MARA

0
0


Na WAMJW-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, imewaasa Watanzania kujijengea tabia ya kupima macho mara kwa mara ili kuweza kuepuka aina mbalimbali za magonjwa ya macho ikiwemo vikope.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Eliud Eliakimu wakati wa kufungua hafla ya kuelekea siku ya Afya ya Macho Duniani ambayo huadhimishwa kila alhamisi ya Pili ya mwezi Octoba.“Asilimia kubwa ya magonjwa ya macho yanatibika ikiwemo upeo mdogo wa macho kuona  ambao yanazuilika kwa miwani  endapo mtu akiwahi katika kituo cha kutolea huduma za Afya na akigundulika ana tatizo la macho basi atapata matibabu mapema”alisema Dkt. Eliakimu.

Aidha, Dkt. Eliakimu alisema kuwa kwa Tanzania watu wasioona kabisa ni asilimia moja sawa na watu laki 5.7 huku watu wenye matatizo mbalimbali ya macho wanakadiriwa kuwa mara tatu ya wasioona kabisa sawasawa na mil.7.Kwa mujibu wa Dkt. Eliudi amesema kuwa takwimu zinaonesha kwamba ugonjwa wa macho umepungua kutoka asilimia 4.6 mwaka 1990 na kufikia asilimia 3.4 mwaka 2015 kutokana na hamasa ya juu ya upimaji toka kwa wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mpango wa Huduma za Macho Nchini kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Benadertha Chilio amesema kuwa tatizo la macho linaloongoza nchini ni mtoto wa jicho ambapo wagonjwa wanafikia kwa asilimia 50 na wengi wao ni wanawake.
 Kaimu mganga mkuu wa serikali Dkt. Eliud Eliakim (Kushoto) akimkabidhi Kaimu Meneja wa Mpango  wa Taifa wa huduma za macho Dkt. Bernadetha Chilio kitabu cha muongozo wa utoaji huduma za macho katika maadhimisho ya wiki ya afya ya macho yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere jijini Dodoma.
DSC_0615
Washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi wakiwa katika maandamano kuadhimisha wiki ya afya ya macho yaliyofanyika jijini Dodoma mapema leo.
DSC_0719
Kaimu Mganga Mkuu Wa Serikali Dkt. Eliud Eliakim akipata maelezo kutoka Titus Nyange jinsi mashine ya Perkins inavyochapa nukta nundu zinazosomwa na watu wenye ulemavu wa macho wakati wa maadhimisho ya wiki ya afya ya macho duniani yanayofanyika jijini Dodoma.


Wataalamu Muhimbili Wawasili Musoma Kutoa Huduma za Afya

0
0
Wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamewasili leo Musoma, mkoani Mara kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wakazi wa mkoa huo kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa hospitali za rufaa za mikoa nchini.

Lengo la ziara hii ni kuwaongezea ujuzi wataalamu wa hospitali za rufaa kupitia wataalamu wabobezi wa muhimbili ikiwa ni kutekeleza mpango mkakati wa MNH wa kuhakikisha inazitembelea hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi ambao pengine wangepewa rufaa kwenda kupata huduma za kibingwa Muhimbili.

Baada ya timu ya wataalamu 14 kuwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma mkoani Mara, ilipokelewa na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Joachim Eyembe na hakusita kueleza furaha yake kwa ujio wa watalaamu hao wabobezi ambao watawajengea uwezo wataalamu wenzao katika maeneo ya upasuaji wa pua, koo, masikio na usingizi na kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa wa Mara.

“Kwa kweli tuna furaha kubwa kwa ujio wenu kwani tunaamini tutanufaika katika ushirikiano wetu wa kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa wa Mara. Naamini tutafanya kazi ambayo itakidhi mahitaji ya wananchi wa mkoa huu,” amesema Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo. Dkt. Eyembe.



Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara, Dkt. Joachim Eyembe akiwakaribisha wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kuwasili leo Musoma kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa kushirikiana na wataalamu wenzao wa hospitali hiyo.
Wataalamu wa afya wa Muhimbili na wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakimsikiliza Mganga Mfawidhi, Dkt. Eyembe leo wakati akiwakaribisha wataalamu wa MNH.
Wataalamu wa Muhimbili na wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma wakijadiliana jambo baada ya kuwasili kwenye hospitali hiyo leo.
Baadhi ya wataalamu wa Muhimbili wakiwa safarini kuelekea Musoma mapema leo asubuhi.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

RUDI TTCL KUMENOGA-MWANRI

0
0

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuliunga mkono Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiunga na huduma mbalimbali wanazotoa ili liweze kuendelea kutoa gawio kubwa kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wote hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya rudi nyumbani kumenoga mkoani humo.

Alisema kuwa kupitia gawio ambalo Shirika hilo linatoa kwa Serikali kati ya fedha hizo zinakuja Mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, huduma za maji, shule , ununuzi wa dawa, ulipaji wa mishahara ya watumishi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Ndugu zangu TTCL kumenoga turudi…ukiongeza salio kwenye simu yako hata usipotumia mwezi salio lako liko salama…hivi sasa huduma zao hazihitaji kupanda kwenye mti ndio ufanye mawasiliano, bali popote unawasiliana…hakuna kusema sogea pembeni sikusikii ndio upige simu…hivi sasa hata ukiwa hata porini TTCL inapatikana” alisema.

Mwanri alisema kwa kuunga mkono huduma za TTCL watakuwa nao wajiwekea akiba ya kurudishiwa sehemu ya huduma walizochangia kwa njia ya Serikali kupata gawio na hatimaye kurejesha sehemu ya fedha hizo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba (kushoto) na viongozi wengine wa Shirika hilo wakiwa na bango lenye maneno ya lugha ya Kinyamwezi yenye maana RUDI NYUMBANI KUMENOGA wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jana mkoani humo. 
1
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(katikati) akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania juu ya huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
2
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwapungia mkono wakazi wa Manispaa ya Tabora wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ilifanyika mkoani humo jana .
4A
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
5A
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipata maelezo  wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo jana.picha na Tiganya Vincent RS TABORA .


MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 8,2018

TAMASHA LA URITHI NA SIKU YA MIKINDANI YAFUNGUA MILANGO YA UTALII KWA MIKOA YA KUSINI

0
0
 

Wizara ya Maliasili na Utalii imeagizwa ishirikiane na wadau wa utalii wenye nia ya kuwekeza kwenye majengo na maeneo ya kihistoria yaliyopo nchini kwa kuboresha hali ya majengo hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu zaidi na yaendelee kutumika kama kivutio cha Utalii.

Pia, Wizara hiyo imeagizwa ianze mara moja ukarabati wa jengo ambalo Mwl.Nyerere alifikia na kulala kwa muda wa siku mbili wakati wa harakati za kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni. Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati kisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika maadhimisho ya siku ya tamasha la urithi wa Mtanzania na siku ya Mikindani iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameutangaza mji Mkongwe wa Mikindani kuwa ni kivutio rasmi cha Urithi wa Utamaduni na Malikale hapa nchini kufuatia kuhifadhiwa kwake rasmi kisheria kwa tangazo la Serikali namba 308 la mwezi Julai mwaka huu. Kufutia juhudi hizo za Serikali za kutaka kuongeza idadi ya watalii,Waziri huyo amesema juhudi hizo zitasaidia kutangaza na kuhamasisha jamii kupenda na kuenzi utamaduni wao na hivyo kuulinda na kuutumia utamaduni kama fursa ya kukuza utalii kwa mikoa ya kusini.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima ambacho kiligunduliwa na Wajerumani mnamo karne ya 15 . Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima ambacho kiligunduliwa na Wajerumani mnamo karne ya 15 . Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni ,maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Mzee Mohamedi Kidume kuhusiana na Nyumba aliyofikia na kulala aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika nyumba hiyo ambayo kwa sasa imekuwa gofu. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini 
Baadhi ya maandishi yanayoonesha kuwa Mji Mkongwe wa Mikindani umetangzwa rasmi kwenye gazeti la serikali, Mji huo utafungua milango ya watlii kwa mikoa ya Kusini.
Baadhi wananchi wakimskiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizindua Mji Mkongwe wa Mikindani ambao umetangazwa kuwa ni kituo cha Urithi wa Taifa na kivutio cha Utalii 


Dkt Kalemani Aendelea Kuwasha Umeme Vijijini

0
0
Afanya ziara wilayani Handeni, Lushoto na kuwasha umeme katika Vijiji Vitano

Katika kuhakikisha kuwa adhma ya Serikali ya kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2021 inatekelezwa, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Handeni na Lushoto mkoani Tanga ili kukagua kazi za usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji.

Akiwa wilayani Handeni, Waziri wa Nishati aliwasha umeme katika Kijiji cha Madebe, Nyasa na Kwamnele na wilayani Lushoto aliwasha umeme katika Kijiji cha Mabugai na Nkelei. Aidha alifanya ziara katika kata na Vijiji mbalimbali ambavyo bado havijasambaziwa umeme ikiwemo Kijiji cha Mahezangulu kilicho katika Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto ambapo aliagiza kuwa, kiwashiwe umeme ifikapo tarehe 12 mwezi huu.

Katika ziara yake wilayani Handeni, Viongozi wa Wilaya hiyo walimweleza kuwa, kuna vijiji 10 ambavyo vimepitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina nishati hiyo, hivyo kuleta malalamiko miongoni mwa wananchi kuwa walitoa maeneo yao kupisha miundombinu hiyo lakini hawapati umeme. Kuhusu suala hilo, Dkt Kalemani aliagiza kuwa, kuanzia Jumatatu ya tarehe 8 Oktoba, 2018 wataalam wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) waanze utaratibu wa kupeleka umeme katika Vijiji hivyo kwani kinachohitajika ni kusambaza tu umeme kwa wananchi hao kwa kuwa miundombinu ipo.



Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Pili kushoto) akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Madebe wilayani Handeni mkoani Tanga. Wa Pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe. 


Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi kifaa cha UMETA, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Waziri wa Nishati alitoa vifaa vya Umeta 30 kwa Mbunge huyo ili kuwawezesha wananchi kuunganishwa na huduma ya umeme bila kutandaza nyaya ndani ya nyumba.  
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizidua rasmi huduma ya upatikanaji wa umeme katika Kijiji cha Mabugai wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga. 

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images