Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110117 articles
Browse latest View live

TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION WAIOMBA SERIKALI KUWAPA KIBALI CHA KUANZA KULEA WAZEE KATIKA NYUMBA YA WAZEE ILIYOPO KWEMBE

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
ASASI ya kiraia ya Tushikamane pamoja  foundation imeiomba serikali kuwapa kibali cha kuwaruhusu kuanza kuwatunza wazee katika nyumba ya asasi hiyo iliyopo Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya wazee duniani, Mwanzilishi wa asasi ya kiraia ya Tushikamane pamoja, Rose Mwapachu  amesema kuwa kwa sasa wameshatuma  maombi ya kupata kibali kwaajili ya wazee kukaa katika nyumba waliyoijenga.

"Kwa sasa tumeshatuma maombi serikalini ya kuomba kibali kwaajili ya wazee wasio na ndugu na wasiojiweza kukaa katika nyuma hii tuliyoiandaa kwaajili ya wazee hawa."

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea siku ya wazee, Rose Mwapachu amesema kuwa siku hii ni mhimu kwaajili ya wazee wasiokuwa na ndugu na wasio na sehemu za kuishi ndio watakao kuja kukaa hapa. 

"Hivyo kwa wazee na wasio na ndugu wala watoto ndio wataishi katika nyumba hii ili kuepusha watu wa madai au kuja kudai mirathi hapa." Amesema Rose Mwapachu.

Kwa upande wa serikali mwakilishi wa  Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo,  Zainabu Mwafilamba amesema kuwa Maombi ya Tushikamane pamoja Foundation tumeyaona na yanafanyiwa kazi.

Na kwa upande wa wazee wasio na makazi na wasio na ndugu jijini Dar es salaam wamewashukuru tushikamane pamoja foundation kwa kuwajali kama wazazi wao.

"Sisi wazee wa Dar es Salam tunawashukuru sana Tushikamane pamoja foundation kwa kutujali sisi wazee Mungua awajalie kila lenye heri watu wote wanaowajali wazee kama sisi".

Pia wamesema kuwa pale tulikuwa na upweke sasa tunajiona kama watuwalio na ndugu kwa mchango wa Tushikamane pamoja  foundation wanavyojitoa kwetu.


 Tushikamane pamoja Foundation wamungana pamoja na wazee wasio na makazi jijini Dar es Salaam katika kusheherekea siku ya wazee duniani ambayo  hufanyika duniani kote ifikapo Oktoba 1 kila mwaka.
 Baadhi ya wazee wakielekea katika nyumba ambayo imejengwa na wana tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya kulea wazee wasio na ndugu wala watoto jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wazee wakielekea katika nyumba ambayo imejengwa na wana tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya kulea wazee wasio na ndugu wala watoto jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Tushikamane pamoja Foundationi, Rose Mwapachu akizungumza na wazee wakati wa kusheherekea siku ya wazee duniani walipokusanyika leo  katika nyumba iliyojengwa na Tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya wazee.
Baadhi ya wageni waliohudhulia siku ya wazee duniani iliyoandaliwa na Tushukamane pamoja Foundation jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waliofanyikisha jengo la Tushikama pamoja foundation kufikia hii leo.


Baadhi ya wazee.
Baadhi ya wazee wakiwa ndani ya chumba mojawapo katika nyumba ya kulelea waze ya kwembe  manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

ULEGA AAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUANZISHA VYAMA VYA USHIRIKA ILI KUIMARISHA UVUVI NCHINI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Uvuvi na Mifugo na Mbunge wa Mkuranga Mh. Abdallah Ulega ameziagiza halmashauri zote nchini kuanzisha vyama vya ushirika vya wavuvi ili kuwapa uwezo wa kukopa fedha na kununua zana za kisasa kwa ajili ya shughuli zao za uvuvi.

Ulega ameyasema hayo akiwa katika ziara Wilayani Chato Mkoani Geita ambako alitembelea vituo vya uzalishaji wa vifaranga vya samaki na kutembelea soko la kimataifa la samaki Kasenda pamoja na shamba la kunenepesha ng'ombe la Alpha Choice na kukagua namna utendaji na shughuli za uvuvi zinavyoendeshwa.

Akiwa Mkoani humo Naibu Waziri amesema kuwa wavuvi pamoja na wananchi wa kijiji cha Kikumbaitare Wilayani Chato lazima wawe na chama cha ushirika ambacho kitawasaidia hasa katika kukopa fedha na kununua zana uvuvi zenye tija zaidi na kuwa mfano kwa kuiunga serikali katika kupiga vita uvuvi haramu.

Akiwa kwenye soko la kimataifa la samaki la Kasenda na kuzungumza na wavuvi walimuomba Naibu Waziri kuimarishiwa miundombinu hasa barabara kwa kuwekwa lami ili kuwarahisishia usafiri wa bidhaa zao.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Mtemi Msafiri amemwomba Naibu waziri kuzuia baadhi ya mialo inayoendesha shughuli za uvuvi kwa kuwa inakosesha serikali mapato na sehemu maalumu ya mauzo yawe ni soko la Kasenda.

Baadhi wa wavuvi wamemshukuru Naibu waziri kwa kuwatembelea mara kwa mara na kusikiliza kero zao na wamehadi kuwa walinzi dhidi ya uvuvi haramu na wameziomba halmashauri kutilia maanani suala la kuanzishwa kwa vyama vya ushirika ili waweze kunufaika na kuongeza mapato kwa serikali.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza leo na  wafanyabiashara, wavuvi katika mwalo wa Kikumba Itare wilaya ya Chato mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia akiwa ameambatana na watendaji wa Wilaya ya Chato akingalia mifugo inayo nenepeshwa katika shamba la Alpha Choice leo mkoa wa Geita.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Geita)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Chato,Mhandisi Mtemi Msafiri (kulia)wakikangua mwalo wa Kikumba Itare.

MAFANIKIO TUNAYOYAPATA NI MABORESHO NA MAONI YA WATEJA - NMB

$
0
0

BENKI ya NMB imesema maboresho makubwa iliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wake. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga alipokuwa akizungumza na Baadhi ya wateja wa Benki hiyo Tawi la Ilala ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.

"...Maboresho makubwa tuliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wetu ambayo tumeyapokea siku za nyuma. Siku zote tunatambua na kushukuru kwa michango na maoni ya wateja wetu, ndio sababu ya kuendelea kuwa nao bega kwa bega," alisema Bw. Mtiga.

Aliongeza kuwa NMB inatambua ushindani mkubwa uliopo na itaendelea kukabiliana nao kwa kadri unavyo kua siku hadi siku. Alisema kwao ushindani wanaupenda na wanachukulia kama fursa ya kufanya vizuri zaidi. "...Ushindani ni fursa nzuri maana inatufanya kubuni bidhaa bora kulingana na mahitaji ya wateja na kufanya vizuri zaidi kwa wateja wetu."

Alisema wiki ya huduma kwa wateja tangu ilipoanza NMB imepata fursa ya kujumuika na wateja wake maeneo mbalimbali na kupata mrejesho kwa masuala mbalimbali juu ya huduma zao na ndio maana inachukulia uzito mkubwa kuzungumza na wateja na kutupa mrejesho ili kuweza kuifanyia kazi.

"...Sisi kwetu tunaiona kama fursa ya pekee kukutana na wateja na kupata maoni yao lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma zetu. Lakini tumekuwa tukifarijika zaidi kwani mbali na mrejesho kuna maeneo ambayo wametutia moyo kwamba tunafanya vizuri hivyo tunawaahidi kuongeza juhudi ili kusonga mbele zaidi."

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga akimkabidhi cheti maalum Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco ambaye ni mteja aliyetukuka wa Benki ya NMB kwa muda mrefu sasa. Mteja huyo amepata mafanikio katika biashara yake baada ya kukuwa na huduma za kibenki za NMB, alianza kukopa shilingi 300,000 na sasa anapata mkopo wa zaidi ya milioni 100 kuendesha biashara zake. 



Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga pamoja na baadhi ya wateja Benki ya NMB waliojumuika kwenye hafla ndogo ya kuwasikiliza wateja katika tawi hilo wakikata keki maalum ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Meneja wa NMB Tawi la Ilala jijini Dar es Salaam, Kidawa Masoud akiandaa keki maalum ya wateja kabla ya kuanza kuwalisha wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MAONESHO YA SIDO KITAIFA SIMIYU

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vidogo (SIDO) ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika kikao cha maandalizi ya maonesho hayo kilichowashirikisha baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na mameneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) kutoka mikoa ya Simiyu, Dodoma ,Mwanza, Kagera ,Mara, Shinyanga na Arusha.

Mtaka amewakaribisha wananchi wa mkoa mwenyeji Simiyu Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho ya SIDO yatakayobebwa na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” na kubainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaamini kuwa maonesho hayo yatakuwa ni maonesho darasa, mahali ambapo watu watajifunza na kufanya biashara.

Ameongeza kuwa maonesho ya SIDO yanabeba ajenda ya Serikali ya awamu ya tano na matamanio ya Mhe. Rais ya kuwa na Tanzania ya Viwanda na kuifikisha nchi katika Uchumi wa Kati, hivyo akaawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali kushiriki maonesho haya.

“Ninawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali waweze kushiriki maonesho haya , nayaalika makampuni, taasisi na mashirika yenye vitu vinavyoweza kuwafaa wajasiriamali na Watanzania ambao wangehitaji kuwekeza kwenye viwanda, waweze kuleta teknolojia zao” .

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018. 
Baadhi ya na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktob, 2018 . 
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi. 


KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA>>>>

IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewashuru wananchi kwa ushirikiano uliopelekea matukio ya uhalifu nchini kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwemo matukio ya matumizi ya silaha.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini hapa Siro amesema kuwa matukio mengi ya uhalifu hapa nchini yamepungua ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano utakaosaidia kuondoa uhalifu nchini. Amesema kuwa Dhamana ipo kisheria na kila mmoja na haki ya kuipatahivyo inategemea na kosa ulilofanya ndio linepelekea kupewa dhamanatena kwa siku yoyote na muda wowote.

“Swala la dhamana lipo kwa mujibu wa sheria na dhamana inatolewawakati wowote ila inategemea na makosa ya mtuhumiwa”alisema siro Amesema Hali ya ulinzi na usalama hapa nchi kwa sasa ni shwari kuanzia hapa Arusha na mikoa mengine isipokuwa kwa kigoma wameongeza askari kuendelea kudhibiti matukio kwa kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa ya mipakani ina ina muingiliano.

Aidha amesema kuwa matukio ya mauaji ya mapenzi yamekuwachangamoto kubwa na yanalisumbua jeshi hilo hususani masuala ya ubakaji lazima tuwe wastaarabu kuepuka matukio yatakayopelekea mauaji na familia kuteseka. “Suala la mauaji ya wapenzi kwa wapenzi ikiwemo kufumaniana limekuwa changamoto kwetu tumejipanga kuyashughulikia na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kulishughulikia hilo lipo kwenye uwezo wao”alitanabisha Sirro

Amesema kuwa ushamba ndio unaopelekea mtu kumuua mpenzi wake hivyo kuifanya familia kuteseka na kuwasihi watanzania kuweza kuepuka matukio hayo kwa kuwa wastaarabu na kuvumiliana. 

MAJAMBAZI SUGU WAWILI HATARI WANASWA MWANZA

$
0
0
· Mmoja anaswa na bastola,risasi 42 na magazine mbili, fedha tasilimu sh. milioni 1.3 za hongo barabarani, simu tatu na kadi nane za mitandao tofauti. 
· Mwingine anaswa na Bendera ya Taifa, king’amuzi cha Startimes

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MAJAMBAZI sugu wawili hatari wamenaswa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza waiwa na silaha na vitu mbalimbali baada ya kufanya uhalifu katika matukio mawili tofauti.

Majambazi hao Peter Thomas Nyanchiwa au Smart Boy mkazi wa jijini Dar Es Salaam, alikamatiwa eneo la Runzewe mkoani Geita huku Jackson Elias maarufu Longoko (20) mkazi wa Shamaliwa Igoma katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza akikamatwa Oktoba 3, majira ya saa 11:00 alfajiri akiwa nyumbani kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi (ACP) Jonathan Shanna alisema majambazi hao walikuwa wakiwatesa wananchi kutokana na uhalifu wa kutumia silaha wakiwavunjia nyumba na kuwapora mali na fedha .

Alisema tukio la kwanza jambazi Peter akiwa na wenzake wawili walikodisha gari hilo jijini Mwanza kutoka kwa mmiliki wake kwenda kuwachukua watalii wakidai wameharibikiwa gari lao katika mbuga ya wanyama Serengeti ili kuwawezesha kuendelea na safari ya kutalii kwenye mbuga hiyo.
Jambazi sugu Peter Thomas Nyanchiwa anayedaiwa kuiba gari na kumjeruhi dereva wa gari hilo kwa risasi akionyeshwa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) ACP Jonathan Shanna (kushoto). Picha na Baltazar Mashaka.

Mtuhumiwa wa Ujambazi Jackson Elias akitambulishwa wkwa waandishi habari jana baada ya kutiwa mbaroni na polisi kuhusiana na tukio la uhalifu.Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi wa polis (ACP) Jonathan Shanna. wengine ni maofisa na askari wa jeshi hilo. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Jonathan Shanna akiwasomea waandishi wa habari majina ya hati ya kusafiria ya mtuhumiwa wa ujambazi Peter Thomas Nyachiwa.

Kamanda Jonathan Shanna akiwaonyesha wana habari gari T 122 DLY lilioibwa na majambazi kabla ya kukamatwa huko Runzewe mkoani Geita. 


ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA 

DAKTARI Bingwa bandia wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) ya jijini Mwanza Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) anayedaiwa kujifanya daktari atafikisha mahakamani muda wowote.

Samweli aliangukia mikononi mwa jeshi la polisi jijini Mwanza akituhumiwa kujifanya daktari bandia ambapo alikamatwa Oktoba 3,mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni katika Hospitali ya BMC akiwa katika chumba cha upasuaji. Mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wagonjwa waliyotaoa kwa uongozi wa hospitali hiyo pamoja na jeshi la polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna akizungumza na waandihi wa habari jana alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na kunaswa akiwa kwenye chumba cha upasuaji atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema kabla ya kutiwa mbaroni mtuhumiwa huyo alikuwa akijifanya ni daktari bingwa na alifanikiwa kuwatapeli baadhi ya wagonjwa wanaotaka kupata huduma za upasuaji na matibabu kwa njia za mkato kwa kuwatoza kati ya sh. 100,000 na 200,000 ili awapangie tarehe za karibu wapate huduma hizo.

Kwa mujibu wa ACP Shanna mtuhumiwa huyo tapeli ni mkazi wa Mtaa wa Pasiansi katika Manispaa ya Ilemela ingawa awali alipohojiwa kwenye Hospitali ya BMC alidai ni mkazi wa wilayani Magu.

“Jeshi la polisi tulipokea malalamiko ya wagonjwa kutapeliwa na kuibiwa mara kwa mara wodini na hivyo tuliwaelekeza wayafikishwe kwa uongozi wa hospitali.Tuliweka mtego tukishirikiana na na uogozi wa hospitali hiyo ya rufaa BMC tukafanikiwa kumnasa akiwa kwenye chumba cha upasuaji akiwa amevalia sare zinazovaliwa na madaktari wakiwa theater,” alisema ACP Shanna.
Daktari bandia wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) akiwa kwenye kituo cha Polisi Kati Nyamagana, kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Jonathan Shanna wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa daktari huyo bandia. 

BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA

$
0
0


Na Stella Kalinga, Simiyu.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amesema angependa kuona  katika kipindi chake atakachokuwepo hapa nchini akiiwakilisha nchi ya Kenya ushirikiano wa kiabishara katika Kenya na Tanzania na unaimarika na takwimu za biashara, viwanda na uwekezaji kati ya nchi hizo zikiongezeka mara dufu.

Balozi Kazungu ameyasema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery LTD), kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Oktoba 05, 2018 katika ziara yake mkoani Simiyu.

Balozi Kazungu amesema ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hususani katika viwanda, kati ya Tanzania na Kenya ukiendelea kuimarika zaidi utachangia kuongeza ajira, kuwatoa wananchi katika umaskini pamoja na kuimarika kwa uchumi wa nchi hizo pia.

 “Baada ya miaka minne kazi yangu kama ikiisha hapa, naomba nione takwimu za viwanda, biashara, uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya zinaongezeka mara dufu, nafasi za kazi kwa watu wetu zinapatikana na watu wetu wanaondokana na umasikini; kukua kwa Tanzania kuwe ndiyo kukua kwa Kenya hilo ndiyo ombi letu” alisema Mhe. Balozi Kazungu. 
 Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kushoto) akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
PICHA D (2)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiangalia akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani humo, wakati ziara ya Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa nne kulia) kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.
PICHA E (1)
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa tatu kushoto) akiangalia pamba iliyochambuliwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018 (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na (wa pili kushoto) Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance 
PICHA I (1)
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) wakiwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.
PICHA K
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini kenya(kulia), akimuongoza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu, kuelekea katika moja ya majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


SERIKALI HAITALIPA MADENI YALIYOKOPWA NA USHIRIKA-MAJALIWA

$
0
0
*Awataka viongozi wa vyama vya ushirika wawe waaminifu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri rasimali za vyama hivyo na kwamba Serikali haitalipa deni lolote lililokopwa na vyama hivyo.
 
“Biashara ya kununua madeni yaliyokopwa na vyama vya ushirika haipo kwenye Serikali hii ya awamu ya tano, badala yake itawachukulia hatua wote waliohusika na ubadhilifu huo.”

Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku wafanyabiashara kuwaibia wakulima kwa kununua kahawa mbichi ikiwa shambani maarufu kama butura.Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara pamoja na wadau wa zao la kahawa baada ya kuwasili mjini Bukoba kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Waziri Mkuu amesema Serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao si waaminifu na wabadhilifu wa mali za ushirika.”Tunahitaji wakulima wapate fedha.”Amesema Serikali itahakikisha wafanyabiashara wote, hususani wa mazao ya kilimo wanakuwa na mfumo sahihi wa ununuzi wa mazao utakao ongeza tija kwao na kwa wakulima.

Amesema kwa sasa Serikali inataka kuondoa mfumo uliopo wa vyama vya ushirika kufanya biashara na badala yake jukumu hilo libakie kwa wafanyabiashara.Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao waihakikishie Serikali kwamba watanunua kahawa yote iliyopo kwa wakulima pamoja na kwenye vyama vya ushirika. Wafanyabiashara wameridhia kununua kahawa yote.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, wanne kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijhage na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma bango lenye malalamiko ya mmoja wa wananchi wa Bukoba wakati alipowasalimia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuwasili kwa ziara ya siku nne mkoani humo, Oktoba , 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti na kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Baadhi ya wafanyabiashara wa zao la kahawa wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. 

DAWASA YAENDELEA KUTEKELEZA OPERESHENI YA KUZUI UVUJAJI WA MAJI

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imeanzisha Operesheni maalum ya kupambana na uvujaji wa maji katika Jiji hilo ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo , Dhamira ya Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa inaondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji kwa kuzuia maji yasivuje kutoka katika mabomba hali itakayoongeza tija katika huduma zinazotolewa kwa wananchi na kuongeza mapato ya Mamlaka hiyo.

“Kazi hii inahusisha mafundi zaidi ya 70 na lengo ni kupunguza tatizo la maji kuvuja kwa asilimia 90 katika maeneo yote DAWASA inayotoa huduma “; Inasisitiza sehemu ya taarifa hiyo .Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Kazi hiyo inayosimamiwa na Idara ya Uzalishaji na Usambazaji Maji itatekelezwa kwa weledi wa hali ya juu ili kufikia lengo la kuzuia upotevu wa maji kutokana na kuvuja.

Katika kuimarisha huduma zake kwa wananchi DAWASA imejidhatiti kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Mamlaka hiyo, yakiendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge.

Aidha, Mamlaka hiyo imekwishaendesha Operesheni ya kudhibiti uvujaji wa maji katika eneo la Tegeta na sasa zoezi hilo linaendelea kuanzia leo Oktoba 6, 2018 katika eneo la Magomeni na katika maeneo mengine Jijini Dar es Salaam na Pwani.

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam DAWASA imefanikiwa katika kuboresha huduma zake kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa upatikanaji wa maji ni wa uhakika na unaendana na mahitaji ya wananchi na dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.


Mafundi wa Mamlaka ya MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na Operesheni ya kuziba mabomba yanayovuja maji katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi. Operesheni ya kuzuia maji kuvuja tayari imefanyika Tegeta na leo inaendelea katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam. 
Mafundi wa Mamlaka ya MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na Operesheni ya kuziba mabomba yanayovuja maji katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi. Operesheni ya kuzuia maji kuvuja tayari imefanyika Tegeta na leo inaendelea katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam. 

UZINDUZI WA ACT WITH MONALISA 2018 MAKUMBUSHO YA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Balaa la Dulla Makabila ndani ya tamasha la URITHI WETU

Mgunga mwa Mnyenyelwa, Mratibu mkuu wa tamasha la Urithi wetu aelezea tukio zima

Mhe. Ali Abeid Karume azungumza haya kuhusu tamasha la Urithi wetu kufika visiwani Zanzibar.

Chatu katika tamasha la urithi wetu


Introducing "Iokote" Official Music Video by Maua Sama & Hanstone

Introducing "GO Gaga" Official Music Video by Lava Lava

Navy Kenzo feat. Diamond Platnumz - "Katika" (Official video)

ALIKIBA X Abdukiba X Cheed X K2ga X Killy - Mwambie Sina (Official Video)

Mtuhumiwa ujambazi 'Handsome' alivyoingia kwenye 18 za Polisi wa Mwanza

Viewing all 110117 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>