Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 250 | 251 | (Page 252) | 253 | 254 | .... | 3285 | newer

  0 0
 • 09/06/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Hii ngoma ya Kihindi ya 'Kuch Kuch Hota Hai' inatupeleka mbaaaaali...
  Kupata tafsiri ya ngoma hii BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0


  Mkali wa muziki wa asili ya Kihaya, Saida Karoli,atafanya  matamasha makubwa mawili la kwanza ni usiku wa saida karoli, litafanyika tarehe,7.9.2013 leo jumamosi kuanzia saa 2 usiku kiigilio V.I.P ni Tsh.15000/= tu na kawaida ni Tsh.10,000/= tu kwenye ukumbi  wa LINA'S CLUB BUKOBA MJINI na Tarehe 8.9.2013 Jumapili ni katika uwanja wa Kaitaba Kiingilio ni Tsh.2500/= tu. Saida Karoli atasindikizwa na Jopo la wasanii lukuki waliowahi kurekodia nyimbo zao ndani ya Tivol Studio wakiwemo wasanii wa nchi Jirani na wa hapa nyumbani Bukoba.

  0 0

  Katibu wa Taswa Jijini Arusha,Mussa Juma akiongea na waandishi wa habari kuhusiana Tamasha la Taswa linalotarajiwa kufanyika kesho katika kiwanja cha general tyre,jijini humo.Kushoto ni Afisa wa Kinywaji cha Vita Malt ambao ni sehemu ya wadhamini wa Tamasha hilo,Deogratius Katambi.

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Tamasha la michezo la waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA) linatarajiwa kufanyika kesho September 8 katika viwanja vya general tyre vilivyopo njiro jijini hapa.

  Akiongelea tamasha hilo katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoani wa Arusha,Musa Juma alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki katika tamasha hilo.

  Alisema kuwa michezo mbali mbali itachezwa katika tamasha hili ikiwa ni pamoja na kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu ,mpira wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali sambamba na burudani mbalimbali za muzikikutoka katika sehemu na bendi mbalimbali.

  Alisema kuwa hili nitamasha la nane kufanyika na kwa mara hii wameboresha zaidi kwani zawadi zimeongezeka tofauti na kipindi kingine.

  Amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hili kwani tamasha hili ni lakihistoria kutoka na waandishi mbalimbali kushiriki kutoka katika mikoa mbalimbali.

  Alitaja baadhi ya timu zitakazo shiriki katika tamasha hili kuwa ni pamoja na timu ya taswa ya jijini dar es salaamu ambapo inatarajiwa kuwasili leo timu ya taswa arusha ambao ni wenyeji wa bonanza hili,timu ya taswa manyara ,timu ya triple a fm ,sunrise fm,radio five pamoja na timu nyingine nyingi ikiwemo timu ya tbl ambao ni wathamini wakuu pamoja na timu ya wazee klabu.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mshauri wa Mambo ya Afya,Wizara ya Afya ya Oman,Dr.Sayeed Sultan Bin Yarub Bin Qaatan Al- Busaid,wakikata utepe kama ishara ya ya uzinduzi wa jengo la madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,lililogharamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman,huko Mbweni Nje ya Mji wa Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa ushauri wakati alipotembelea moja ya madarasa ya Chuo cha Taaluma za Sayansi ya Afya,huko mbweni baada ya kuyazindua rasmi leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili ya Serikali ya Oman kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


  0 0

  Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewateua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN) baada ya bodi ya awali kumaliza muda wake mwishoni mwa mwezi Machi, 2013.

  Uteuzi wa Mhe. Waziri unafuatia uteuzi alioufanya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa Profesa Moses Wariobi kuwa wa Mwenyekiti wa Bodi ya TSN. Wajumbe wa Bodi ni kama Ifuatavyo:

  1. Dkt. Consolata Ishebabi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara
  2. Everlyn Richard kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam
  3. Alfred Nchimbi, Chuo cha Utumishi wa Umma
  4. Glorious Luoga, Mwanasheria

  Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 6 Septemba, 2013

  0 0

  Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jana alikutana na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje mjini Dar es Salaam.  Katika mazungumzo yake, Mhe. Waziri Membe alielezea yaliyojiri katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika mjini Kampala, Uganda hivi karibuni.  
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe wakati wa mazungumzo nao jana.
  Mhe. Waziri Membe akiongea na waandishi wa habari.Picha zote na Tagie Daisy Mwakawago 

  Na Zainabu Abdallah
  Wakuu wa Nchi wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR) wamemaliza kikao chao kilichofanyika Jijini Kampala, Uganda 05/9/2013. Kikao hicho  kilijadili hali ya kuzorota kwa amani Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na M23 katika mji wa Goma.
  Akioengea na Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam 06 Septemba, 2013, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa  Bernard Membe (Mb) alisema kuwa Wakuu wa Nchi walifikia maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulaani vikali mashambulizi  ya M23 katika mji wa Goma yaliyosababibisha vifo na majeruhi kwa raia na askari wa kulinda amani.
   Aidha, Wakuu wa Nchi na Serikali walitoa pole kwa Umoja wa Mataifa na Tanzania kutokana na kifo cha Meja  Khatibu Mshindo, mwanajeshi wa Tanzania aliyeuwawa katika shambulio lililofanywa na Kikundi cha Waasi cha M23. Katika shambulio hilo pia wanajeshi watano walijeruhiwa na hali zao zinaendelea vizuri.
  Vile vile, Mhe. Membe alisema kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukiongozwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nchi za Maziwa Makuu, Mhe. Marry Robinson upo Goma kuangalia hali ya usalama
  Katika hatua nyingine, Wakuu wa Nchi waliagiza Serikali ya DRC na M23 kufanya mazungumzo ili kumaliza mgogoro huo kwa amani na kutoa siku 17 kukamilisha zoezi hilo.   Siku tatu kati ya hizo ni kwa ajili ya maandalizi na siku kumi na nne ni kwa ajili ya majadiliano na makubaliano ya kufikia muafaka wa kumaliza mgogoro huo.
  Kando ya mkutano huo, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipata fursa ya kuongea na  Rais Paul Kagame wa Rwanda. Katika mazungumzo hayo, Viongozi hao waliazimia kudumisha na kukuza uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Rwanda.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Presidential Bureau Oamar Issa (katikati) na Mkuu wa Chuo cha Uongozi, Profesa Joseph Semboja katika mkutano aliouitisha wa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wa kujadili utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa, kwenye hoteli ya Dodoma Septemba 7, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Baada ya muda mrefu kupita bila kuwa na tamasha lolote la wanafunzi hasa wa shule za Sekondari, uongozi wa Mtakuja Secondary School ua Kunduchi kwa kushirikiana na mtangazaji maarufu Allan Lucky 'Rais wa Wanafunzi' wa kipindi maarufu cha Skonga ambacho hurushwa kupitia televisheni ya vijana ya EATV umeandaa tamasha la wanafunzi linalotarajiwa kuhudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 3000 kutoka katika shule zaidi ya 20 za jijini Dar-es-salaam.

  Tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa shule mbali mbali za Dar-es-salaam kwa pamoja na kupata changamoto kimawazo na kiburudani, pia kuwakutanisha wadau mbali mbali wa elimu katika kufanikisha uboreshwaji wa elimu na kusaidia katika kutekeleza mpango wa 'Matokeo Makubwa Sasa', linatarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo tarehe 14/09/2013 katika viwanja vya shule hiyo.

  Miongoni mwa shule ambazo zitashiriki ni: Mtakuja, Kondo, Jordan, St. Gasper, Mbezi Beach, Boko, Goba, Twiga, Maendeleo, Mwambao, Kisauke, Kinzudi, londa, Makongo, Kawe Ukwamani, Tegeta, Mbweni, Teta, Hananasif na Mtongani, zote ni za sekondari.

  Tamasha hilo linatarajiwa kuhusisha wadau mbali mbali wa elimu watakaokutana katika kubadilishana mawazo na kupata burudani kwa kushuhudia vipaji lukuki walivyo navyo wanafunzi kutoka shule mbali mbali.

  Miongoni mwa shughuli zitakazoendeshwa ni pamoja na maswali na majibu, fashion show, uimbaji, ufokaji, na wanafunzi wenye vipaji mbali mbali maalum watapewa nafasi.

  Msemaji wa tamasha hilo ambaye pia ni mwalimu wa michezo wa Mtakuja Beach Sekondari Bw Misonji Charles amewataka wadau mbali mbali wa elimu kuhudhuria na kushuhudia vipaji vya wanafunzi mbali mbali na pia amewataka waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi katika kuchukua habari na matukio mbali mbali yatakayojitokeza. Pia amewaomba wadau mbali mbali wenye uwezo wa kuchangia katika kufanikisha tamasha hili wajitokeze, kwa kuwa linaandaliwa kwa nguvu za shule na kamati maalum ya maandalizi pekee.

  Kwa maelezo na kama unataka kushiriki, tafadhali wasiliana na Msemaji wa Tamsha Bw Misonji Charles kupitia 0714642442.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa eneo la Ruaha Buyuni waliokuja kumpokea tayari kwa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
   Wamama kutoka mkoa wa Iringa wakicheza ngoma ya kihehe wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera.
   Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia salaam walizokuwa wanapewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Sixtus Mapunda akisalimia wakazi wa Ruaha Buyuni wakati wa uzinduzi wa  wa Mbio za Bendera ya Chama mkoani Iringa
   Wananchi akifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa chama waliofika wakati wa uzinduzi wa Mbio za Bendera ya Chama mkoani Iringa.


  0 0

  Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini Banjul, Gambia jana (Ijumaa) usiku tayari kwa mechi ya leo dhidi ya Gambia itakayochezwa saa moja na nusu kwa saa za Afrika Mashariki na saa kumi na nusu kwa saa za Gambia.Taifa Stars inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania,kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
  Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars),Kim Poulsen akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi hayo.


  0 0

  STILL THE CHEAPEST AND SIMPLY THE BEST!
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  KUCHUKUA MZIGO WAKO DAR ES SALAAM 
  MPIGIE AGENT WETU DAR; TORNADO LUKOSI TEL; 0713607116
  MZIGO UNANDOKA KILA IJUMAA

  ONCE YOU PAY HERE IN UK YOU DONT PAY ANYTHING IN TANZANIA
  UKIISHA LIPA UK UNAKWENDA KUCHUKUA ILALA DAR BILA KULIPA TENA

  FLIGHTS EVERY WEEK

  KWA WALE WANAOTAKA KUNUNUA VITU UK TUTUMIE EMAIL AU TUPIGIE
  MINIMUM WEIGHT IS 40K HANDLING/ADMIN FEE £20
  KABLA HUJATULETEA MZIGO HAKIKISHA UMEANDAA ORODHA YA VITU UNAVYOTAKA TUKUSAFIRISHIE NA NI LAZIMA TUUFUNGUE MZIGO NA KUHAKIKISHA UNACHOSAFIRISHA . KAMA HAUNA PACKING LIST HATUTASAFIRISHA MZIGO.
  USITEGEMEE KUSAFIRISHA MBUZI HALAFU UPOKEE NG'OMBE!

  40' CONTAINER TO DAR/MOMBASA NOW £1,800
  SALOON CARS TO DAR 750
  4X4 VEHICLES 850
  OUR AGENT IN DAR; TORNADO TEL; +255 713607116
  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0


  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a Congratulatory Message to the Australian Prime Minister Elect, Rt. Honourable Tony Abbott (MP).

  The message reads as follows

  “Rt. Honourable Tony Abbott (MP)
  Prime Minister Elect,
  Sidney,
  AUSTRALIA.

           I have received with great joy the news of your election as the 28th Prime Minister of Australia.

           On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and, indeed, on my own behalf, I wish to extend to you and through you to the Australian Liberal Party our profound congratulations on your momentous victory.  Your coalitions' election to lead your great country and its people is a clear testimony of confidence and trust that the people of Australia have to your Party and its coalition partners.
           As you prepare to assume office in your new mandate, I wish to assure you of my personal commitment as well as that of the Government of the United Republic of Tanzania, to continue to work closely with you and your Government to further strengthen the excellent bilateral relations that so happily exist between our two countries.
           While wishing you a very successful term and continued personal good health, please accept the assurances of my highest consideration and esteem.

  Jakaya Mrisho Kikwete
  PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”

  Issued by: 
  The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam.

  7TH SEPTEMBER, 2013

  0 0

   Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi (kulia), ambaye ni mwasisi wa shindano la kutuma ujumbe kwa njia ya Tweet kwenye akaunti yake ya tweeter@ regmengi, akimkabidhi zawadi ya sh.300,000 Ombeni Kaaya,baada ya kuwa mshindi wa tatu wa mwezi Agosti, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya IPP, 
   Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi (kulia), ambaye ni mwasisi wa shindano la kutuma ujumbe kwa njia ya Tweet kwenye akaunti yake ya tweeter@ regmengi, akimkabidhi zawadi ya sh. 500,000, Susana Senga  baada ya kuwa mshindi wa pili wa mwezi Agosti, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya IPP,

   Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi (kulia), ambaye ni mwasisi wa shindano la kutuma ujumbe kwa njia ya Tweet kwenye akaunti yake ya tweeter@ regmengi, akimkabidhi zawadi ya sh. milioni 1, Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam, Lilian Wilson baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mwezi Agosti, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya IPP. Wanaoshuhudia ni mshindi wa pili, Suzana Senga aliyepata sh. 500,000 na Ombeni Kaaya aliyeshika nafasi yatatu na kupata sh 300,000. 
   Mengi akifafanua jambo mbele ya wanahabari waliofika kuripoti tukio hilo. 
   Mengi akielezea umuhimu wa vijna kubuni wazo zuri la biashara.
  PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafurahia wasanii chipukizi Gosbert Bwere(4) anayepiga ngoma na mwenzake Nyambari Mganga(5) walipokuwa wanamtumbuiza muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nansio,Ukerewe, kwa ziara ya kikazi. 
  ----------------------------------------
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siyo kazi ya Serikali kuviokoa vyama vya ushirika kutoka kwenye madeni kwa sababu shughuli za ushirika ni za sekta binafsi na maliya wanachama wenyewe.

  Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa makosa ya ushirika na wezi wa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika hatimaye yanabebeshwa vyama vya siasa.

  Kama namna ya kuwasaidia wananchi, Rais Kikwete amewataka viongozi mbali mbali wa mikoa kuwasaidia wananchi ili kupata viongozi waadilifu na waaminifu na wala siyo wezi kama ilivyo sasa kwa vyama vingi vya ushirika.

  Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 7, 2013, wakati alipopokea Ripoti ya Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza kwenye Ikulu Ndogo mjini Mwanza kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.

  Rais Kikwete aliwaambia viongozi hao wa Mkoa wa Mwanza: “Tumewahi huko nyuma kulipa madeni yote ya vyama vya ushirika. Nia ilikuwa kuvisaidia vyama hivyo na wanachama wake kujipanga upya na kupata uhalali wa kuweza kukopa fedha za kjuendesha shughuli zao. Lakini sasa, vyama hivyo, vimerudi kule kule kwenye madeni.”

  Alitoa mfano wa Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani kama moja ya vyama vya ushirika ambavyo madeni yake yalilipwa na Serikali lakini sasa kina deni kubwa zaidi kuliko hata lile lililolipwa na Serikali.

  “Wale watu wa Pwani walikwenda kukopa na benki moja ikakubali kuwapa fedha. Wameshindwa kulipa na ule ushirika nadhani utakufa. Njia bora kwa vyama vya namna hiyo ni kuviachia vife tu kwa sababu havina faida yoyote kwa mkulima.”

  Aliongeza: “Vyama vya ushirika siyo maliya Serikali. Ni maliya wanaushirika na hivyo ushirika ni sekta binafsi. Lakini hakuna shaka kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanatesa wananchi. Wanakopa fedha kwenye mabenki lakini wanashindwa kuzirudisha fedha hizo na hilo linapotokea Serikali inalaumiwa kwa hali hiyo.”

  Rais alikuwa anatoa maelekezo yake baada ya kuambiwa kuwa Chama cha Ushirika cha Nyanza cha Mkoa wa Mwanza kilikuwa kinakamilisha mpango wa kukopa kiasi cha sh bilioni saba kutoka Benki ya Raslimali Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununulia pamba.

  Lakini aliwaambia viongozi hao: “Uamuzi wa kukopa ama kutokukopa ni wa kwenu. Nyanza ni maliyenu, wezi waliopata kukibebesha madeni chama hicho mliwachagua nyie wenyewe. Fedha ni zenu lakini hatimaye athari za makosa yenu yanaiathiri Serikali na hata vyama vya siasa.”

  “Kuna wakati viongozi wa Chama cha Nyanza walipata kuuza godown ya thamani y ash milioni 600 kwa sh milioni 50 tu. Hawa ni wezi wa mchana wanaoiba kweupe. Wanaiba lakini wanataka Serikali iwasaidie. Kwa nini? Nadhani kazi yetu kamaviongozi ni kuwasaidia wananchi kupata viongozi adilifu na aminifu siyo wezi,” alisema Mheshimiwa Rais Kikwete na kuongeza:

  “Tatizo ni kwamba hata sisi viongozi tunakataa kuwashughulikia wezi kwa sababu hawa ni watu maarufu na wakati mwingine baadhi ya viongozi wanakula nao na jambo hilo limekuwa tatizo kubwa sana. Tunavifikisha vyama vya ushirika mahali ambako sina uhakika kama bado ni mali ya wakulima. Wakulima wanakutana na ushirika wakati wa kuchagua viongozi tu na baada ya hapo wakulima hawaonekani tena.”


                0 0

  Taifa Stars imemaliza vibaya mechi za mchujo za Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika baada ya kufungwa na Gambia huku Kocha Kim Poulsen akisema timu yake imefungwa mabao mepesi.

  Wenyeji Gambia wameshinda mabao 2-0 katika mechi hiyo iliyochezwa leo (Septemba 7 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Independence ulioko hapa jijini Banjul ukiwa ni ushindi wake wa kwanza katika kundi hilo la C ambapo imemaliza ikiwa ya mwisho ikiwa na pointi nne.

  Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Poulsen amesema Gambia ilistahili kushinda kwa vile ilitengeneza nafasi nyingi kuliko timu yake, na kuongeza kuwa mabao iliyopata Gambia yalikuwa mepesi.

  “Hatukutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini tukaruhusu mabao mapesi. Nawapongeza Gambia kwani walistahili ushindi. Unapofanya makosa unaadhibiwa. Gambia ilikuwa timu nzuri leo, kwani ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga, sisi tukatoa mabao mepesi,” amesema Kim.

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imemaliza katika nafasi ya tatu katika kundi hilo lililokuwa na timu nne ikiwa na pointi sita ilizozipata nyumbani kwa kuzifunga Morocco na Gambia.

  Hata hivyo, Kim amesema sababu nyingine ya kutofanya vizuri ni kuwakosa wachezaji wanaocheza nje ya nchi na wengine wa kikosi cha kwanza ambao ni majeruhi.

  Mabao yote ya Gambia katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Munyemana Hudu kutoka Rwanda yalifungwa na nahodha wa timu hiyo Mustapha Jarjue. Alifunga la kwanza dakika ya 44 na kupachika lingine dakika ya 51, mabao yaliyotokana na wachezaji wa Stars kutokuwa makini.
  Katika mechi hiyo Stars iliwakilishwa na Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni/David Luhende, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha/Juma Liuzio.

  Taifa Stars inaondoka Banjul kesho (Septemba 8 mwaka huu) saa 6 mchana kwa ndege ya Arik hadi Dakar, Senegal ambapo itaunganisha kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi ambapo itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) keshokutwa (Septemba 9 mwaka huu) saa 8.05 mchana.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
  +2207362384 Banjul

  0 0

  Wakonge katika game la Muziki wa Bongo Fleva hapa nchini,Prof. Jay (kulia) na Mwanadada Lady Jay Dee a.k.a Binti Komando wakifanya yao stejini Usiku huu wakati wa Tamasha la Muendelezo la Kili Music Tour 2013,lilifanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Kahama.
  Mwanadada Lady Jay Dee akiwapagawisaha wakazi wa Kahama usiku huu waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa wa Kahama usiku huu.
  Binti anayetawala jukwaa la muziki wa kizazi kipya kwa sasa, Recho kutoka THT akicheza na madansa wake jukwaani.
  Izzo Biznes akiimba moja ya nyimbo zake mbele ya mashabiki lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa wa Kahama.
  Muite Ngosha the Swagger Don a.k.a Fid Q akifanya yake stejini.


  0 0

  Tamasha la Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli limefana usiku huu kwenye ukumbi wa Lina's Night Club Bukoba. Tamasha lililokuwa linaitwa "usiku wa Saida Kaoli" ambalo  watu wengi wakijitokeza kumuona kwa mara nyingine hapa Bukoba Tangu azushiwe na wadau kwamba alifariki Dunia katika ajali ya boti miezi michache iliyopita.Saida kajitokeza kuthibitisha kuwa  habari hiyo ilikuwa ya uzushi mtupu na ya uongo. Leo hii Jumamosi akiwa amesindikizwa na wasanii wa  Nyumbani kwao Bukoba Bk Sande, Papaa Kishaju, pamoja na wanamuziki wa VISION MUSIC AMBASSADOR wanaodhaminiwa na 100.0 Vision fm Radio BUKOBA na Kundi la Ka Jay Poda kutoka Kenya amabo wameusindikiza usiku wa SAIDA KAROLI vilivyo na kukamua kisawasawa.
  Saida Karoli akiimba baadhi ya nyimbo zake mpya
  Willy Kiroyera kulia akicheza na Saida Karoli

  0 0

   Ankal akipongezwa na blogger gwiji duniani kaka Ndesanjo Machas iku alipoanzisha rasmi Globu ya Jamii katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki, Finland, Septemba 8, 2005 (BOFYA HAPA)
   Ankal na mai waifu wake na toto tundu Sellah wakikata keki kuadhimisha miaka 9 ya Globu ya Jamii usiku huu
  Ankal na familia yake wakisherehekea kimya kimya hepi besdei ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii usiku huu.
  -----------------------------------------------------------
  Ilikuwa siku ya Alhamisi tarehe kama ya leo (Septemba 8,) miaka TISA iliyopita wakati Globu ya Jamii ilipozaliwa rasmi katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki Finland, kama utani tu. Kwa msemo mwingine, ni miaka TISA kamili leo toka Globu ya Jamii ianze Libeneke la kuhabarisha wadau kwa mapicha na habari kemkem bila kukosa hata siku moja

  Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kingependa kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote duniani kote kwa kampani mnayotupa kila saa, siku, wiki, miezi na hadi sasa ikiwa ni MIAKA TISA kamili.  Si jambo dogo, ukizingatia katika safari hii njiani tumekutana na kila aina ya changamoto, kubwa kuliko yote ikiwa ni kufanya kila tuwezalo kubakia hapa tulipo kwa kufuata weledi pamoja na sera ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI, pamoja na kauli mbiu kwa wadau watoa maoni ya kuwa waangalifu kutochafua hali ya hewa wala kujeruhi hisia ya mtu wakati wa kutoa maoni.

  Si rahisi kumridhisha kila mdau, na kwa mujibu wa usemi wa Kimombo wa “What’s good for the goose is bad for the hen” unaomaanisha hivyo. Yaani “Kilicho kizuri kwa bata mzinga, ni kibaya kwa kuku”.

  Katika kuadhimisha hii MIAKA TISA ya Libeneke, Globu ya Jamii haitofanya sherehe ya pamoja na wadau kama ilivyotarajiwa. Badala yake Ankal kajikakamua na kununua kajikeki na kukata na kula na familia kwa niaba ya wadau. Ila ahadi yetu ni kwamba, panapo majaaliwa, sherehe kubwa itaandaliwa mwakani wakati wa kuadhimisha MIAKA KUMI. Ni mapema mno kusema itakuwaje, ila panapo uhai itakuwa  SHEREHE KUBWA na inayostahili.

  Kwanza kabisa tunamshukuru Jalali Muumba wa vyote kwa tunu hii aliyoitupa. Tunatambua kuwa tuna bahati ya sisi kuwa sisi, na kamwe bahati hiyo uliyotupa, EWE MOLA, hatutoichezea...
  Globu ya Jamii pia inachukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wake, ikiwa ni pamoja na VODACOM, AIRTEL, UHURU ONE,  TTCL, NMB, NBC, AZANIA BANK, CRDB, NHC, PRECISION AIR, AIR UGANDA, NSSF, PSPF, DSTV, SKYLINK, SERENGETI FREIGHT FORWADERS  ‘WAZEE WA KAZI’, SWIFT FREIGHT, GIRAFFE OCEAN VIW HOTEL, DR MKOMBOZI,  na wengineo wote. Tunashukuru kwa kutuamini na kuendelea kuendeleza nasi Libeneke. 
  Shukrani zingine  za kipekee ziende kwa familia yangu kwa uvumilivu wanaoonesha kwangu, pia kwa wadau kadhaa ambao tukiamua kuwataja wote hapa itachukua ukurasa wote hu na tusiwe tumetaja japo robo yao. Kwa uchache tu, na ambao ni kwa niaba ya wale ambao hatutotaja kwa ufinyu wa nafasi na pia si  kwa ubora wao, shukrani hizo zimwendee kaka Ndesanjo Macha kwa kuwa wa kwanza kutufungulia na kutuongoza njia na kutupa maudhui ambao baada ya kuyafuata, tumeona faida yake.

  Washauri wakuu wetu pia hatuwasahau katika hili. Nao  ni Profesa Mark Mwandosya, Mhe. January Makamba, Freddy Macha, Balozi Peter Kallaghe, Othman Michuzi, Ahmad Michuzi, Christopher Makwaia MK, Steve Wassira jnr., Nathan Chiume, DJ Luke Joe wa Vijimambo, Waziri Ally, John Kitime, Alex Perullo, Muhidin Maalim Gurumo, kaka Jeff Msangi, Boniface Makene, Kirk Gills, Oscar Shelukindo, Ephraim Mafuru, Imani Kajula, Profesa Mbele, Da' Chemi Chemponda, Ankal Beda Msimbe, kaka Assah Mwambene, Da' Tagie Daisy Mwakawago, Shamim Zeze wa 8020 Fashions, Mama wa Mitindo Asia Idarous na mumewe Mzee Khamsin, Ainde, kaka Asimwe Kabuga, Abdallah Ezza na Fide Tungaraza wa Heslsinki na wengineo wengi tu. Ushauri wenu tunauthamini na kuuheshimu!
  Wengine ni viongozi wote wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Spika, Naibu Spika na maofisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano pamoja na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Viongozi  maofisa wote wa vyama vya siasa, Viongozi wote na watumishi  wa taasisi za umma na binafsi, Mablogger wote na mwisho ni wadau wote wanaotupa moyo kila kukicha. Asanteni sana, sana,  sana, sana. Hatuna cha kuwapa zaidi ya hizo SHUKURANI kutoka katika kilindi cha moyo wetu. MOLA AWE NANYI, NA AWAZIDISHIE PALE PALIPOPUNGUA.

  Hatuna la zaidi la kusema zaidi ya kuahidi kwamba tutaendeleza Libeneke kwa moyo wetu wote huku tukipiga magoti kuwaomba wapendwa wadau wetu duniani kote muendelee kutupa kampani, kwani bila ninyi sisi si lolote si chochote. Pia tunaomba radhi pale tunapoteleza kama binaadamu yeyote ambaye daima duni si mkamilifu, ambapo likitokea litalotokea si kwa makusudi ama nia mbaya bali ni kwa udhaifu huo huo wa kibinaadamu.


  Naomba kuwasilisha,

  Wenu Mnyenyekevu,

  Muhidin Issa Michuzi “Ankal”

older | 1 | .... | 250 | 251 | (Page 252) | 253 | 254 | .... | 3285 | newer