Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

DAWASA, TIC, TTCL WAMPONGEZA MHANDISI MFUGALE

0
0

Na Mwandishi Wetu.Globu ya Jamii
VIONGOZI wa wanachama wa Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Serikali Tanzania waliamua kwa pamoja kumpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale kwa kutambuliwa na Serikali hususani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa umahiri na utumishi uliotukuka. 

Akizindua flyover ya Tazara ambayo imepewa jina la Mfugale, Rais alisema anajua uzalendo, uaminifu na ubunifu wa mhandisi huyo amabaye siku zote amesimama imara na kuchapa kazi mpaka kufanikisha ujenzi wa Flyober hiyo.

Wakiwa  katika kikao chao cha kawaida cha mwezi, viongozi hao wa Taasisi za umma walisema kila mwananchi anatambua mchango wa mhandisi Mfugale katika kujenga uchumi wa nchi kupitia uimarishwaji wa sekta ya usafiri wa barabara. 

Viongozi hawa wa taasisi hukutana kila mwezi wakiwa na lengo la kujadili njia bora za kuharakisha maendeleo ya nchi kupitia sekta wanazoziongoza. Aidha katika vikao hivyo hubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kupambana changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Jukwaa hilo lina jumla ya wanachama 70 kutoka taasisi mbalimbali za kiserikali.
 Mhandisi Cyprian Luhemeja akimpongeza mtendaji mkuu wa TANROADS mhandisi Partick Mfugale baada ya kufanikisha kwa ujenzi wa Flyover ya Tazara iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  jana Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Simu TTCL Waziri Kindamba  akimpa zawadi  ya pongezi Mtendaji mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale baada ya kufanikisha kwa ujenzi wa Flyover ya Tazara iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  jana Jijini Dar es salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Uwekwzaji TIC Geoffray Mwambe akimpongeza  Mhandisi Mfugale baada ya kufanikisha kwa ujenzi wa Flyover ya Tazara iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  jana Jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja.

NAFASI ART SPACE KUSHEHEREKEA MIAKA 10 TANGU KUANZISHWA KWAKE, KUFANYA TAMASHA KUBWA LEO JIJINI DAR

0
0
 *Ni leo Septemba 29 ,kufanyika katika ukumbi wao uliopo Mikocheni B kuanzia saa tisa alasiri
*Wasanii maarufu ndani na nje ya nchi kutoa burudani

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
 NAFASI Art Space katika kusheherekea miaka 10 tangu kuanzisha kwake wanatarajia kufanya tamasha kubwa na la aina yake leo kuanzia saa tisa alasiri ambapo wasanii maarufu katika uchoraji, uimbaji na waimbaji wa muziki wa dansi wafanya show kwa mashabiki na wapenzi wa Sanaa ndani na nje ya nchi.
Tamasha hilo linatafanyika katika Ukumbi wa Nafasi Art Space uliopo Michokeni B jijini Dar es Salaam na kwamba hakutakuwa na kiingilio chochote na lengo la kufanya hivyo ni kutoa nafasi kwa mashabiki na wapenzi wa sanaa kufika kwa wingi.
 Akizungumza na Michuzi Blog jana kuhusu Tamasha hilo ambalo limepewa jina la Sanaa Yetu Festival, Ofisa Maendeleo Biashara na Masoko wa Nafasi Art Space Agnes-Senga Tupper amesema katika kusheherekea miaka 10 ya Nafasi Art Space wanatarajia kufanya show hiyo matata ambayo itagusa sanaa za aina zote nchini Tanzania.
Amesema zaidi ya wasanii 19 wa uchoraji, uimbaji , wanamuziki wa dansi ni miongoni mwa watakaotoa burudani kwa mashabiki wao ambao kwa kipindi cha miaka 10 wamekuwa wakiwaunga mkono.
Tupper amefafanua kwamba “Mwaka 2008 kikundi kidogo cha wasanii wa Tanzania walijikusanya na kuanzisha Nafasi Art Space kwa ajili ya wasanii nchini kuwa na sehemu ya kufanya kazi zao, pamoja na msaada kutoka Denmark Embassy, Nafasi Art Space ilianzishwa.Tangu wakati huo, Nafasi imeweza kusaidia wasanii zaidi ya 100 nchini Tanzania kuendeleza na kukuza vipaji vyao .
 “Hii imewapatia wapenzi wa sanaa fursa ya kuona, kujifunza na kufahamu sanaa na utamaduni jijini Dar es Salaam pamoja na nje ya nchi. Hivyo kwa mwezi huu wa Septemba, Nafasi Art Space imekuwa ikisherehekea miaka 10 kwa kufanya matukio mbalimbali ya kisanaa kwa ajili ya umma,”amesema Senga.
 Ametaja baadhi ya matukio ambayo wameyafanya kama sehemu ya kusheherekea miaka 10 ambayo kesho ndio kilele chake ni pamoja na kufanya mkutano na waandishi wa vyombo vya habari, uzinduzi kwa kuchora live soko la Karume, kutembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wameshiriki kwenye kipindi cha Jukwaa la Sanaa pamoja na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).
Baadhi ya matukio ambayo wameyafanya kama sehemu ya kusheherekea miaka 10 ambayo leo ndio kilele chake ni pamoja na kufanya mkutano na waandishi wa vyombo vya habari, uzinduzi kwa kuchora live soko la Karume, kutembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wameshiriki kwenye kipindi cha Jukwaa la Sanaa pamoja na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).
 Michoro mbalimbali ilichorwa na vijana wenye vipaji ikiwa ni sehemu ya maandalizi
 Vikundi mbalimbali vilishiriki kuelekea kilele cha  NAFASI Art Space ambapo leo inatimiza miaka 10 tangu kuanzisha kwake.

TTB YAMTEUA BI. JUDITH KUWA BALOZI WA HIARI WA UTALII INCHINI ITALIA.

0
0
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekabidhi rasmi majukumu kwa Balozi wa Hiari wa Utalii Bi Bi Judith Raymond Mushi aliyepewa jukumu la kufanya kazi na TTB ya kuvitangaza vivutio vya Tanzania katika nchi ya Italia. Bi. Judith ambaye ni Mtanzania ambaye anafanya kazi ya kufundisha Lugha ya Kiswahili nchini Italia. 

Wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Septemba 27, 2018 katika ofisi za TTB jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TTB Bi. Devota Mdachi amemkabidhi rasmi sharia na taratibu zinatakiwa kufuatwa wakati anatekeleza jukumu hilo kupitia matukio mbalimbali atakayokuwa anahudhuria akiwa italia. 
Pamoja na msaafu huo Bi . Judy alikabidhiwa majarida yenye taarifa za utalii wa Tanzania yanayotumiwa kama nyenzo ya kutangazia utalii wa Tanzania katika masoko mbalimbali ya Utalii Duniani. 

TTB imeweka utaratibu maalumu wa kuwapata mabalozi wa hiari wa Utalii. 

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AWAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA .IKULU CHAMWINO

VODACOM WASAINI MKATABA KUTUMIA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILINO

0
0
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania imesaini mkataba wa kibiashara na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) wa kutumia Huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) utakaowezesha mkongo kusambaza huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini.

Hafla ya makubaliano hayo ya kibiashara imefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo TTCL Corporation imewakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Ndugu Waziri Kindamba na Vodacom ikiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Hisham Hendi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kindamba alisema Vodacom amekuwa mteja wa Mkongo wa Taifa tangu Mei Mosi, 2013 na hadi sasa anatumia huduma za ukubwa wa STM-4 (Jumla 7) na STM-16 (Jumla 9), huku akiongeza kuwa Mkataba mpya uliosainiwa unaongeza viwango vya matumizi ya Mkongo kwa Vodacom kwa STM-16 (Jumla 2) na STM-64 (Jumla 1) wenye thamani ya Shilingi bilioni 25.6 bila VAT.

“..Mkataba wa leo unatufanya sisi NICTBB na TTCL kutambua uzito wa majukumu tuliyokabidhiwa na Serikali ya kuhakikisha kuwa huduma za Mkongo zinaimarishwa ili watoa huduma za Mawasiliano hapa nchini waboreshe huduma zao na kuwafikia wananchi wengi zaidi,” alisema.

“Mkataba wa leo unatufanya sisi NICTBB na TTCL kutambua uzito wa majukumu tuliyokabidhiwa na Serikali ya kuhakikisha kuwa huduma za Mkongo zinaimarishwa ili watoa huduma za Mawasiliano hapa nchini waboreshe huduma zao na kuwafikia wananchi wengi zaidi,” aliongeza Kindamba.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa kibiashara leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo Vodacom watatumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika huduza za data na sauti maeneo mbalimbali kuboresha mawasiliano. Nyuma ni wanasheria wa makampuni hayo wakishuhudia. 

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (kulia) wakipongezana mara baada ya kubadilishana nakala za mkataba wa kibiashara leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Katika makubaliano hayo Vodacom watatumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika huduza za data na sauti maeneo mbalimbali kuboresha mawasiliano. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Jim James Yonazi akishuhudia tukio hilo pamoja na Ofisa Msimamizi wa Mkongo wa Taifa. 

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Jim James Yonazi (katikati) akizungumzia tukio hilo kwenye hafla hiyo ya kusaini mkataba wa kibiashara kati ya Vodacom na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Kushoto ni Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (kulia) kabla ya tukio la kusaini mkataba wa biashara na Vodacom ya kutumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba wakionesha mikataba hiyo mara baada ya kusainishana. 
Mh. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Jim James Yonazi (wa pili kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Ndugu Waziri Kindamba (wa pili kulia) mara baada ya kusaini mkataba wa biashara na Vodacom ya kutumia huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi nchini Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi. 

Mzee Mwinyi kuwa Mgeni rasmi Maadhimisho siku ya Wazee Kitaifa jijini Arusha ,

0
0
Na. VERO IGNATUS, ARUSHA

Wakati tukielekea kusherehekea siku ya wazee septemba 30 imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80% (takriban mil2)ya wazee hapa nchini wanaishi vijijini. 
Akizungumza na vyombo vya habari kamishna wa ustawi wa jamii kutoka wizara ya Afya jinsia wazee na watoto Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa juhudi  za ziada zinashitajika ili kuwafikia na kuweza kuhakikisha wanapata huduma stahiki kama ilivyo katika sera ya Taifa 
Ng'ondi amesema maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa yatafanyika jijini Arusha ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi

Aidha kwa mujibu wa shirika la Help Age International limeweka wazi kuwa hapa nchini asilimia 27%  ya wazee wote (677,043) wanaishi wenyewe bila msaada wa mtu yeyote.Amesema kuwa zaidi ya asilimia 83% ya wazee wote (2.1m) wanaishi katika familia na kupata angalau matunzo ya familia tofauti na wenzao ambao wanaisha wangali pekee yao

  Nchini Tanzania  kuna familia ambazo wazee wamekuwa wakibeba majukumu ya kuwalea watoto yatima kama takwimu zinavyoonyesha asilimia 40% ya watoto yatima wanalelewa na familia za wazee.Mara baada ya uzinduzi wake kesho wazee watapata fursa ya kupata huduma ya kupima afya kupata ushauri wa kitabibu pamoja na ufunguzi wa maonyesho ya kazi mbali mbali za mikono zinazofanywa na wazee.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Wazee ni Hazina ya Taifa: Tuenzi Juhudi za Kutetea Haki na Ustawi Wao’’. Kaulimbiu hii inahimiza Serikali na Jamii kwa ujumla kutambua na kuenzi jitihada za Wazee katika ujenzi wa Taifa letu.“Tarehe moja mwezi ujao itakuwa siku ya wazee nawaombeni nyote kujitokeza kwa wingi wakiwemo wazee wetu kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid”alisema Dkt.Ng’ondi
Mmoja ya wazee aliohojiwa mkazi wa jiji la Arusha Swalehe Allly amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuonyesha juhudi zake kwa kuwaandalia wazee wetu angalau pensheni kama takwimu zinavyoonyesha kuwa Tanzania Bara 96% ya wazee wote hawana pension ya uzeeni
Amesema kuwa tuige mfano na kuonyesha juhudi za serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa kuwapatia  Wazee 58,371 kati yao 27,000,(46 %) wanapata pesheni Wenye umri wa Miaka 70.“Hapa utaona jinsi maisha ya uzee yalivyo kuwa na mtihani kama juhudi za maksudi hazitachukuliwa na serikali zetu kote ulimwenguni kuhakikisha wazee wanapata matunzo stahiki kama tawimu hizi” alisema Ally
 Imeonyesha juhudi kama hazitachukuliwa na kufanyiwa kazi, asilimia Zaidi ya 50% ya familia za wazee wanaishi chini ya kiwango cha umaskini. kigezo- Benki ya Dunia.

 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Alhaji Ally Hassan Mwinyi (picha kutoka Maktaba) 

Dkt. Abbasi, TAGCO Watembelea Kituo cha Radio cha Storm Mkoani Geita

0
0


Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo aliwasisitiza umuhimu wa kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kuzingatia weledi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akishiriki Kipindi cha Moja kwa moja katika kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo aliongelea masuala mbalimbali ikiwamo miradi mikubwa inayotekelezwa na iliyotekelezwa na Serikali katika kipindi cha Miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita
Mwenyekiti Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akishiriki Kipindi cha Moja kwa moja katika kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo alisistiza kuwa wataendelea kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano Serikalini na kuendelea kurahisisha uhusiano kati ya waandishi wa habari na Maafisa Habari wa Serikalini.
Katibu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Abdul Njaidi akiongea na watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita ambapo ambapo aliwasisitiza kuhusu umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo katika mkoa wa Geita.

Watumishi wa kituo cha Redio cha Storm FM Mkoani Geita wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi alipokutana nao.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafanya upimaji afya na kutoa elimu kwa Wahariri na Waandishi wa Habari

0
0




Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpima shinikizo la damu mwandishi wa habari kutoka Gazeti la Mtanzania Veronica Romwald kuashiria uzinduzi wa upimaji afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.
upimaji 2
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nancy Mallya akimpima sukari kwenye damu Mwandishi wa Habari Mkongwe Allan Lawa wakati wa uzinduzi wa upimaji afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.
upimaji 3
Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Theophylly Mushi akitoa ushauri wa afya ya moyo kwa  Mhariri wa gazeti la Habari Leo Mgaya Kingoba mara baada ya kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa uzinduzi wa upimaji wa afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka  tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.
upimaji 4
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipata ushauri kabla ya kufanyiwa  vipimo vya magonjwa ya moyo wakati wa uzinduzi wa upimaji afya ikiwa ni moja ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Septemba. Uzinduzi huo ulienda  sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya magonjwa ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari ikiwemo kiharusi, madhara ya mafuta katika mishipa ya damu ya moyo, lishe bora kwa afya ya moyo na tezi dume.Picha na JKCI

WANANCHI 40,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA SALASALA

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) imeunda kikosi maalum cha kufanya kazi ya maunganisho mapya ili kuongeza wateja wa maji. 



Kazi hii imeanza leo rasmi katika eneo la Salasala ikiwa inaongozwa na Mhandisi Mtindasi chini ya Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Ritamary Lwabulinda. 


Mradi huo wa Salasala utawanufaisha wananchi 40,000 wa maeneo hayo ikiwa ni katika kutekeleza siku 100 za DAWASA mpya.
Katika kuhakikisha kuwa kazi inafanywa kwa weledi na usimamizi wa kutosha mhandisi Mtindasi atasaidiwa na wahandisi wengine 3 na mafundi 3 na vijana 150 kutoka Veta.
Mradi huo utakuwa na awamu tofauti na katika awamu ya kwanza imeweza kuhusisha vijana 50 ambao tayari wamemaliza mafunzo na leo hii tayari wapo kazini. 
Wananchi wanaoishi eneo la Salasala watafaidika moja kwa moja na mradi huo na ndio wataanza kufanyiwa maunganisho kwani tayari kuna mtandao na maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini yataunganishwa hivi karibuni.

Aidha katika mikoa mingine ya kazi ya DAWASA kuna miradi midogo midogo ya kusogeza huduma kwa wateja inayoendelea. Miradi hii yote inagharamiwa na DAWASA na wateja wataunganishiwa maji kwa mkopo.
 


Wataalam kutoka Mamlaka ya Maji wanaendelea kufanya 'survey' kwenye maeneo mbalimbali ya mradi kuweza kubaini maeneo ya maunganisho mapya kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji kwa kila mwananchi.


Jumla ya wateja wapya 40,000 wanatarajiwa kuunganishwa na huduma katika eneo la Salasala.

Mafundi wakiendelea kuchimba mifereji kwa ajili ya utandikaji mabomba ya maji katika mradi wa eneo la Salasala,utakaounganisha wateja wapya 40,000 baada ya mradi huo kukamilika.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT.JOHN MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU MAALUM YA HALMSHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI JIJINI DAR LEO

0
0

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akipiga makofi na wajumbe wengine kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli pamoja na wajumbe wengine wakiwa wamesimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka na kuwaombea Majeruhi na waliopoteza maisha katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea Septemba 20,2018 katika ziwa Victoria kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halimashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akiongoza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018

TAMBO NA MAJIGAMBO YA WASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUELEKEA MTANANGE WA KESHO

Wema Sepetu ashindwa kuzuia hisia,Mapenzi ya Diamond na mrembo Irene yawekwa wazi.

DIWANI WA CHADEMA DAR ATANGAZA KUJIUNGA CCM,AFURAHIA KUKAMILIKA KWA FLYOVER

0
0

Na Khadija Seif,Globu ya jamii

KIMBUNGA cha Chama Cha Mapinduzi(CCM)kimeendelea kuvuma na kusomba wanasiasa wa upinzani ambapo leo kimemsomba Diwani wa Kata ya Mtongani wilayani Temeke Bernard Mwakyembe.

Mwakyembe aliyekuwa Chadema ametangaza leo jijini Dar es Salaam kwamba ameamua kuondoka Chadema na sasa amehamia CCM.Ametaja baadhi ya sababu ambazo zimemfanya ahamie CCM ikiwemo ya kuitwa msaliti kwa sababu tu ya kusifu juhudi za Serikali ya Awamu ya tano katika kuwatumikia Watanzania.

"Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Magufuli ni vyema kuonesha ushirikiano ili kujenga Tanzania iliyo imara," amesema.Pia amesema Rais amefanya jitihada za kuhakikisha msongamano wa foleni barabarani unamalizika na juzi tu amefungua flyover .Pia amesema Serikali imekuwa mstari wa mbele kuboresha huduma za wananchi ikiwemo sekta ya elimu.Aidha Mwakyembe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amefanya mabadiliko mengi kwenye mji huo ikiwemo suala la usafi katika kila kata.

Pia kuwapa nafasi wanawake wajane na waliotelekezwa na wanaume zao na kuwapa nafasi walemavu waliosoma Kupata ajira serikalini.Hivyo ameona ni jambo la kuungwa mkono kwani hakuna wanaoweza kuleta mabadiliko yote haya lakini wapinzani wamekaa kubeza jitihada za Serikali ya Awamu ya tano

Amesema sababu nyingine ambazo zimempeleka CCM ni serq nzuri za Chama hicho kwani kuna ujamaa na kushirikiana."Hakuna anayeama chama kwenda CCM kwa kununuliwa kama inavotafsiriwa na wengi," mesema.Ametoa rai kwa vyama vya upinzani kuunga mkono juhudi hizo kwani maendeleo yote hayo ni kwa faida ya Watanzania wote si kwa Rais, Mkuu wa Mkoa au kwa CCM peke yake.

Diwani wa Kata ya Mtongani wilaya ya Temeke Bernard Mwakyembe akizungumzana na wanahabari sababu zilimzopelekea kuhamia chama cha Mapinduzi

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUAGANA NA BALOZI WA MISRI NCHINI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf aliyefika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf aliyefika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Dkt. Damas daniel Ndumbaro kwa Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Yasser Ahmed Al Eldin Elshawaf aliyefika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018

LUGOLA ATANGAZA OPERESHENI KUWAONDOA WAHAMIAJI HARAMU MKOANI KIGOMA, AWATAKA UHAMIAJI, POLISI WASHIRIKIANE

0
0

Na Felix Mwagara, MOHA-Buhigwe

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma ishirikiane na Jeshi la Polisi kufanya operesheni maalum ya kuwaondoa wahamiaji haramu mkoani humo.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika uwanja wa Mnanila mjini Manyovu wilayani Buhigwe, leo, Lugola alisema anataarifa za kutosha kuhusu wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani wapo mkoani humo, hivyo lazima waondolewe kwa mujibu wa sheria.

Lugola ambaye alikua akishangiliwa na wananchi baada ya kutoa agizo hilo, pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaohifadhi raia hao wa kigeni ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.

“Sasa natoa agizo hili na litekelezwe, Uhamiaji mkoa washirikiane na polisi kuwaondoa raia hawa wa kigeni ambao wameingia nchini kwa njia zisizo halali, nataka operesheni hii ianze mara moja,” alisema Lugola.

Lugola pia aliirudia kauli hiyo ya kuondolewa kwa wahamiaji hao haramu alipokua anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi, Wilaya ya Kigoma Vijijini, na kuongeza kuwa anashangaa wahamiaji hao wanaendelea kuwepo mitaani huku maafisa uhamiaji wakiwepo mkoani humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi, Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati Waziri huyo alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali  za wananchi wilayani humo. Waziri Lugola alitangaza operesheni kuanza kwa operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga. Kulia ni Mwanasheria wa Sekretaireti ya Mkoa wa huo, Said Kamugisha. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiyaangalia majina ya watuhumiwa waliopo mahabusu katika Kituo cha Polisi Manyovu, wilayani Buhigwe, Mkoa wa Kigoma, alipokua anaonyeshwa na Askari Polisi wa zamu  kituoni hapo, Peter Charles. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwahoji watuhumiwa (hawapo pichani) ndani ya mahabusu ya kituo cha Polisi Manyovu wilayani Buhigwe, Mkoa wa Kigoma, alipofanya ziara katika kituo hicho kujua utendaji kazi wa Polisi wa kituo hicho kilichopo mpakani na nchi ya Burundi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Luteni Kanali, Michael Ngayalina, na nyuma yake ni Mkuu wa Kituo hicho, Nickobay Mwakajinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUFANYA TATHMINI YA ELIMU NCHINI

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO 

Wadau wa Elimu wametakiwa kuendelea kufanya tathmini ya elimu kwa kujadili mafanikio na changamoto za sekta hiyo ili kuboresha na kukuza elimu nchini.

Hayo yamebainishwa jana jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Selemani Jafo alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Elimu.

Waziri Jafo amesema kuwa nchi nyingi ambazo hazina rasilimali za madini wala vivutio vya utalii zinaendelea kuwekeza katika rasilimali elimu ambapo baadae nchi hizo huwa tajiri na kutoa misaada kwa nchi masikini.

“Taifa linalowekeza vizuri katika sekta ya elimu ndilo Taifa lenye nafasi kubwa ya kukomboa wananchi wake na taifa kiujumla hivyo kutathmini juu ya elimu inayotolewa nchini kwetu ni jambo la muhimu sana”, alisema Jafo.

Waziri Jafo amewasisitiza wadau wa elimu walioshiriki katika mafunzo hayo kutekeleza maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ili kuendelea kutoa matokeo chanya katika sekta hiyo.

Vile vile ametoa rai kwa wadau wa elimu kuendelea kutoa michango yao ya hali na mali katika kuinyanyua sekta ya elimu nchini ili kwa pamoja taifa la Tanzania liweze kujinasua katika umasikini kupitia elimu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Selemani Jafo akifunga Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akitoa neno la Utangulizi wakati wa ufungaji wa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu. 
Baadhi ya wadau wa elimu walioshiriki katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.

Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi  walioshiriki kama Wadau wa Elimu katika Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu. 
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Lydia Wilberd akitoa salamu za asasi hiyo kabla ya kufungwa kwa Mkutano wa pamoja wa Wadau wa Elimu nchini uliofanyika kwa siku nne Jijini Dodoma. Mkutano huo ulijadili kuhusu mafanikio na changamoto za sekta ya elimu.


WANANCHI WALALAMIKIA WAFANYABIASHARA WALIOPANGA BIDHAA ZAO PEMBENI MWA BARABARA YA MWENDOKASI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Wananchi Mkoani Dar es Salaam wanaotumia Barabara ya Msimbazi wamelalamikia wafanyabishara waliopanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara ya mwendokasi.

Wafanyabiashara hao walioweka bidhaa zao pembezoni mwa barabara hiyo wamekuwa kero kubwa kwa wananchi hao kutokana na kukaa kwenye maeneo yanayopaswa kupita kwa miguu.

Wakitoa madukuduku yao, wananchi hao wamesema kuwa kwa sasa inawalazimu wapite kwenye barabara ya magari au mwendokasi badala ya kutumia maeneo waliyotengewa baada ya wafanyabiashara hao kuweka bidhaa chini.Wamesema kuwa, kinachofanywa na wafanyabiashara hawa sio kitu cha haki na zaidi kinahatarisha usalama wao waenda kwa miguu kwani nara nyingi wamekuwa wanakoswa koswa na magari.

" kwanza wafanyabiashara hawa wamepanga bidhaa zao katika pande zote mbili, unakosa hata kwa kupita maana wamebana eneo lote inatulazimu kupita pembezoni mwa barabara ili kupita kwa urahisi ila napo pamekuwa na changamoto ya kunusurika kugongwa na magari na kuhatarisha maisha yetu," walisema.

Kika barabara hiyo ya Msimbazi, wafanyabiashara mbalimbali wameweka bidhaa zao pembezoni mwa njia ya wapita kwa miguu na imekuwa kero kubwa.

Ikumbukwe kuwa Wakati wa ufunguzi wa huduma ya mwendokasi, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alitoa agizo la wafanyabishara wadogo wadogo wasipange bidhaa zao pembezoni mwa barabara ya mwendokasi, agizo ambalo lilifanyiwa kazi kwa kushirikiana na kampuni ya Strabag na Halmashauri kuajiri askari ambao walisimamia kikamilifu.

Aidha katika miezi ya karibuni askari hao hawaonekani na kuwapa fursa wafanyabiashara hao kupanga bidhaa zao na kuleta usumbufu kwa wapita kwa miguu.
Wananchi wakipita katika barabara baada ya wafanyabiashara kupanga bidhaa zao kwenye njia ya wapita kwa miguu Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MDOGO WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU.

0
0
Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu katika jimbo la Liwale na kwenye Kata 37 za Tanzania Bara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni za uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi.

Jaji Mbarouk amewataka Wasimamizi hao kufanya kazi kwa ufanisi, uhuru, uwazi na bila kuegemea upande wowote ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu.Amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.

“ Tunakutana hapa ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi, natumaini mtatumia fursa hii kubadilishana uzoefu katika kutekeleza jukumu hili lililo mbele yenu” Amesema Jaji Mbarouk.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk akifungua mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani utakaofanyika katika jimbo la Liwale na kwenye kata 37 leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo wa Ubunge na udiwani utakaofanyika katika jimbo la Liwale na kwenye kata 37.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria wakati wa mafunzo ya siku 3 kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo yenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo, jijini Dodoma.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi washiriki wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mdogo, jijini Dodoma leo.


MAPINDUZI MAKUBWA SEKTA YA MADINI YAZIDI KUONGEZA MAPATO

0
0
Mageuzi makubwa katika sekta ya madini nchini yameifanya sekta hiyo kuendelea kuongeza mapato ya Serikali kutoka bilioni 194.6 ilizopanga kukusanya mwaka 2017/18 hadi kufikia shilingi bilioni 301.6 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 55. 

Hayo yameelezwa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mkoani Geita wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Serikali.

Dkt. Abbasi ameeleza kuwa ongezeko hilo la mapato katika sekta ya madini limechagizwa na mabadilikomkatika sheria za madini, kujengwa kwa ukuta wa Mirerani na kuzuia kwa usafirishaji wa mabaki (kaboni) ya dhahabu nje ya mkoa yanapochimbwa madini.

“Mheshimiwa Rais aliagiza kujengwa ukuta eneo la wachimbaji wadogo la Mirerani na April mwaka huu ukuta huo ulikamilika na kuwezesha kuongezeka kutoka kilo 164.6 za madini ya Tanzanite yenye thamani yas milioni 71.8 mwaka 2016 hadi kufikia kilo 449.6 zenye thamani ya shilingi milioni 893.8 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018”, ameeleza Msemaji Mkuu wa Serikali.

Ameeleza kuwa kutokana na usimamizi mzuri, makampuni ya uchimbaji madini yameendelea kutoa mchango wake kwa jamii ambapo Geita Gold Mine imetoa shilingi bilioni 9.2 kwa mkoa wa Geita kama mchango wa kampuni hiyo kwa maendeleo ya mkoa huo.

Aidha, Msemaji Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa zuio la kaboni zenye dhahabu kusafirishwa na kuchakatwa nje ya mkoa zinakozalishwa limesaidia kuongeza pato kwa Serikali kufikia shilingi milioni 850 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka shilingi milioni 400 kwa mwezi April. 
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi. 


ARUSHA YAZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA WAZEE NCHINI KWA MWAKA 2018

0
0
Wazee 576,370 wamenufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini nchini tangu februari mwaka 2018 chini ya TASAF na kati ya hao wanaume ni 217,947 na Wanawake 358,423 kwa pande zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema hayo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo mjini Arusha akitaja Siku hii kuwa inatukumbusha wajibu wetu katika kuwalinda, kuwatetea na upatikanaji wa huduma bora kwa wazee.

Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa serikali inatekeleza Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 kwa kuanzisha Mpango wa Utambuzi wa Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo wazee wote wasiojiweza hapa Nchini.

Aidha pamoja na utekelezaji Sera hiyo pia aserikali inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza mauaji ya wazee ambao utazinduliwa ifikapo Juni mwaka 2019 lakini pia serikali itapitia Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 ili iendane na hali halisi ya maisha ya Wazee.

‘’Kutokana na umuhimu wa uwepo wa wazee katika familia, jamii na Taifa letu hatuna budi kuitumia siku hii ya leo kuhamasishana, kuelimishina na kukumbushana wajibu wetu kwa wazee wetu ili kuwawezesha kuishi maisha bora yenye staha’’. Aliongeza Dkt. John Jingu.Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Fabian Daqaro ambaye amezindua rasmi maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee ya Mwaka 2018 amesema wazee wote watanufaika na msamaha wa kodi wa nyumba ambazo wanaishi lakini msamaha huo hautausika na nyumba zote za biashara kama vile vyumba vya maduka au nyumba za kupangisha.

‘’Naomba nieleweke vizuri kama nyumba yako ni kuishi na haitumiki kwa biashara itapata msamaha wa kodi lakini kama nyumba yako au nje ya nyumba yako yenye uzio ina sehemu za kufanyia biashara itatozwa kodi ya serikali nendeni ofisi za Mapato nakuweka takwimu zenu sahihi watawahudumia’’.Alisistiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Fabian Daqaro.Mkuu huyo wa Wilaya Arusha pia amewataka watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo kuweka kumbukumbu sahihi za Wazee mkoani humo ili wazee waendelee kutambuliwa ili kuwawezesha wazee hao kupata huduma muhimu ikiwemo Afya,malazi chakuala, ulinzi na hifadhi ya Jamii ya Uzeeni.

Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani huadhimishwa hapa Nchini kila tarehe 1 mwezi wa kumi kufuatia Azimio la Umoja wa Mataifa linalozitaka Nchi Wanachama kutenga Siku maalumu ya kutafakari mchango wa wazee katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akiongea wakati wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Bw. Fabian Daqaro akiongea wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.

 Mkuu wa Wilaya ya Arusha wakwanza kushoto Bw. Fabian Daqaro, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu katikati na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi wakikagua baadhai ya kazi za ujasiliamali za kikundi cha wazee walipotembelea mabanda ya Wazee kujionea shughuli zao.

 Wazee wa Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.

Wazee wa Jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images