Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

LUGOLA AMELIAGIZA JESHI LA POLISI KIGOMA KUWAKAMATA WAUAJI WA WATU

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, kuhakikisha wamewakamata wahusika wa mauaji ya watu wanane yaliotokea mwezi mmoja uliopita katika Kata ya Kitanga yaliosababishwa na mgogoro wa wakulima na wafugaji kijijini humo.


Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Kitanga wilayani humo, jana, Waziri Lugola alitoa siku mbili kwa Jeshi hilo kukamilisha kazi hiyo kwa kufanya operesheni maalum ili kuondoa taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.


“Lazima tupendane, kwanini tunauana, wasukuma na waha wote ni ndugu, tushirikiane, tupendane ili tuweze kuishi kwa Amani, hizi chuki nataka ziishe, mkuu wa wilaya shirikiana na polisi ili hili tatizo liweze kuisha haraka iwezekananavyo.,” alisema Lugola.


Waziri Lugola aliongeza kua, katika siku mbili alizotoa anataka watuhumiwa wote wawe wamekamatwa na kushtaki kwa mauaji ya watu wanane.

Huku akiwa anashangiliwa na wananchi hao, Lugola alisema Serikali itaendelea kuwalinda wananchi wake kwasababu Tanzania ni nchi ya Amani na pia watu wake wana upendo.


Lugola pia alimtaka Mkuu wa Wilaya wa Kasulu…..kupitia Kamati yake ya Ulinzi na usalama ihakikishe wanatoa maeneo ya wafugaji na pia marufuku kwa wafugaji hao kuingiza mifugo mashambani.


“Mkulima haupaswi kwenda kulima sehermu ya malisho ya mifugo, halikadhalika wafugaji marufuku kuingiza mifugo yenu katika eneo la wakulima, huo ni utaratibu mzuri, tuufuate na tuzingatie ili kuimarisha Amani katika eneo hili,” alisema Lugola.


Aidha,  katika hatua nyingine Waziri Lugola alizungumza na wananchi wa mji wa Kasulu na kusema Serikali inaangalia uwezekano wa kuandaa vibali maalum vitakavyoruhusu wakulima wa wilaya hiyo kuwatumia vibarua kutoka nchi za Burundi na Kongo ili kupunguza wahamiaji haramu wanaokuja mkoani Kigoma kufanya kazi za kilimo ambao baadhi yao si waamini.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kata ya Kitanga, Wilaya ya Kasulu, Mkoani Kigoma wakati alipofanya ziara katika kata hiyo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi baada ya kutokea mauaji katika eneo hilo yaliyotokana na vurugu ya wakulima na wafugaji mwezi uliopita. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza mwananchi wa mjini Kasulu alipokua aamuuliza maswali, baada ya Waziri huyo kuwataka wakazi wa mji huo kutoa kero mbalimbali zinawakabili wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Kijiji cha Kitanga, Shabani Funyenge, alipokua anamfafanulia jinsi ugomvi wa wakulima na wafugaji ulivyoanza katika Kijiji hicho, Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma, uliosababisha watu wanane kuuawa. Lugola alitoa siku mbili kwa watuhumiwa wa mauaji hayo wawe wamekamatwa.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KIKOSI KAZI CHA KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIUMBE WAGENI/VWAMIZI NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ni vema kama nchi tukajipanga mapema kuhakikisha kwamba viumbe vamizi hawaendelei kushamiri ili kuepusha Taifa kuingia kwenye gharama kubwa za kukabiliana na janga hilo hapo baadaye.
Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa uzinduzi wa Kikosi Kazi cha Kutatua Changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Pamoja na kwamba viumbe hawa ni janga la kiuchumi, kimazingira na kiafya  lakini bado halijashughulikiwa kikamilifu hususani katika elimu ya kuzuia viumbe hawa na kuwa na mipango madhubuti ya kukabiliana nalo” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Janga hili si la sekta moja. Kama tulifanya makosa huko nyuma kushughulikia jambo hili kila sekta kivyake tangu sasa TUACHE.  
Amezitaka Sekta zote na Taasisi zifanye kazi kwa pamoja kwa kupeana taarifa na mikakati ya kukabiliana na changamoto hii. Na kutaka ushirikishwaji wa wadau wote wakiwemo, Halmashauri za wilaya ,Wizara za kisekta, Serikali za Mitaa, Asasi za Serikali na zisizo za Serikali, Sekta binafsi pamoja na wananchi pamoja na vyombo vya habari.
Akitoa rai kwa waliochaguliwa kuunda Kikosi Kazi cha Kitaifa, Makamu wa Rais alisema “Tambueni kuwa mmepewa jukumu kubwa la kulisimamia suala hili kikamilifu. Kafanyeni kazi kulingana na Hadidu za Rejea tutakazo wakabidhi ili mwisho wa yote kuwe na matokeo chanya ya kazi mliyopewa na Taifa”.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano wa Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa aligundua tatizo hili mara baada ya kufanya ziara yake ambapo amekuta athari za mimea na viumbe vamizi zimekuwa kubwa na tishio kwa wananchi hivyo kuona kuna kila sababu ya kuanza kulishughulikia.
Kikosi kazi hicho chenye wajumbe 18 kilichozinduliwa leo kitaongozwa nchi ya Mwenyekiti Dkt. Ezekiel Mwakalukwa.
Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Awesu, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega pamoja na wadau mbali mbali wa mazingira.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kikosi kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa  Uzinduzi wa Kikosi cha kutatua changamoto za Viumbe Wageni/ Vamizi nchini uliofanyika kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi john Malongo akiwatambulisha Wajumbe 18 wa Kikosi Kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi hicho kilichozinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kikosi kazi cha kutatua changamoto za viumbe wageni/ vamizi nchini mara baada ya uzinduzi wa Kikosi kazi hicho uliofanyika kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine Pichani ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Juma Awesu, Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

PUNGUZO KABAMBE LA BEI YA TIKETI KWA WATAKAONUNUA KUPITIA TIGO PESA MASTERPASS QR

$
0
0
HUKU nchi nzima ikisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote, mdhamini mkuu Tigo Tanzania pamoja na waandaaji Clouds Media Group wameanza maandalizi rasmi ya tamasha hilo litakalorindima Jumamosi hii tarehe 29 Septemba katika viwanja vya Jamhuri, mjini Morogoro..

Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Viba Kama Lote, Gardner G. Habash aliwahakikishia wote watakaohudhuria tamasha hilo usalama na mapokezi mazuri. ‘Tunawakaribisha nyote kwenye shamrashamra za mwanzo wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote,’ Gardner alisema. 

‘Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Morogoro, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim,’ Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema. Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888. 

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia. 

‘Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Bali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,’ Gardner aliongeza. 

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu litashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam. 
Kuhusu Tigo Tanzania 

Tigo Tanzania ni kampuni ya simu yenye maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995. Kupitia bidhaa zake mbalimbali za kipekee kwenye sauti, ujumbe mfupi, internet yenye kasi na huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu za mikononi , Tigo imekuwa mwanzilishi katika ubunifu wa kidigitali kama vile simu ya kwanza ya smartphone kwa kiswahili, Huduma ya facebook kwenye lugha ya kiswahili, bure, huduma ya TigoPesa, Huduma ya simu ya Tigo pamoja na huduma ya kwanza Afrika Mashariki ya kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika. 
Kwa taarifa zaidi: woinde.shisael@tigo.co.tz
Msanii wa bongo flava Boniventure Kabogo – Stamina (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Pamoja naye ni (kuanzia kushoto), Mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Gardner Habash, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Morogoro, Stephen Kunambi, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Tigo – William Mpinga, Afisa Michezo wa Manispaa ya Morogoro - Asteria Mwang’ombe , msanii wa bongo flava Abednego Daniel – Belle 9, na mtangazi wa Clouds FM Kenneth Frank – Kennedy the Remedy.
Wasanii wa Bongo Flava (kuanzia kushoto) Z Anto, Mr Blue Kabayser na Ben Pol wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa uzinduzi wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote mjini Morogoro leo. Tigo imetangaza punguzo la bei kwa tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR pamoja na kuzindua shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo. Tamasha la kwanza la msimu huu wa Tigo Fiesta 2018l inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro siku ya Jumamosi.

MISA-TANZANIA YATOA TUZO YA UTOAJI WA TAARIFA KWA WIZARA, MASHIRIKA YA UMMA

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii
TAASISI ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) imetoa tuzo kwa mashirika mawili hapa nchini wakati wa kuadhimisha siku ya  kupata taarifa duniani kwa alieonesha ushirikiano wa kutoa taarifa na kwa aliebana  taarifa zake kwa umma mwaka 2018.

Ambapo tuzo ya ufunguo wa dhahabu ilikwenda Mfuko wa wahifadhi ya watumishi wa umma (PSPF) kwa kuonesha ushirikiano wa kutoa taarifa,ambapo zawadi ya kufuli la dhahabu imekwenda kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kubana sana taarifa zao kwa mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam  Mjumbe wa MISA-Tanzania Rose Mwalimu
amesema tuzo hizo hutolewa Kila mwaka hapa nchini ambapo leo zimetoleo baada ya uzinduzi wa utafiti wa upatikanaji wa taarifa katika ofisi mbalimbali za umma.

Aidha Mwalimu amesema kwa mwaka huu utafiti huo umehusisha taasisi nane za umma kati ya hizo kuna Wizara nne, na taasisi ya wakala  wa Serikali nne.

Amezitaja  wizara hizo ni Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Viwanda na Uwekezaji.

Kwa upande wa taasisi ni Mfuko wa fedha kwa wafanyakazi (WCF),Mfuko wa Hifadhi wa Watumishi wa Umma (PSPF) ,Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

"Lengo la utafiti huu ni kuona jinsi gani wananchi wa kawaida wanapata taarifa zinazohusu maendeleo yao ama ya nchi  ili waweze kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maisha yao binafsi na taarifa kwa ujumla"amesema Mwalimu.

Hata hivyo taasisi ya MISA Tanzania imetoa mapendekezo kuwa mafunzo yatolewe mara kwa mara kwa watumishi hasa kwa wale ambao wanatumika moja kwa moja na utoaji taarifa kwa umma  ili kujenga imani na wale wanaofika kwenye taasisi hizo kwa wenye nia ya kupata huduma mbali mbali,hasa mafisa habari,maofisa wa mapokezi na wale wa masjala.

Mwalimu amesema taasisi  hiyo ya MISA iliyoanzishwa 2002 Septemba 28 ikijumuisha nchi 11 za Kusini mwa Afrika (SADC) inayohusika na kufanya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye ofisi za  umma,ikiwa na lengo la kutetea na kuhakikisha uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.

SPIKA NDUGAI AFUNGA RASMI MKUTANO MKUU WA ALAT JIJINI DODOMA

$
0
0


V25A8972
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) pamoja na wadhamini wa Mkutano huo, wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 34 wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
V25A8949
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tawala za Mitaa Tanzania pamoja na wadhamini wa Mkutano huo (hawapo kwenye picha) wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 34 wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
7. TFDA
Mwakilishi wa TFDA, akipokea cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi Job Ndugai kufuatia ushiriki wa mamlaka hiyo kuwezesha kutano wa 34 ALAT jijini Dodoma.
V25A9048
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimpatia cheti mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa, Ndg. Tuntufye Mwambusi  mmoja wa wadhamani waliofanikisha Mkutano Mkuu wa 34 wa Tawala za Mitaa Tanzania, wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” kabla ya kufunga Mkutano huo katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.
V25A8925
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Tawala za Mitaa Tanzania, wadhamini wakiwa kwenye Mkutano wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma. 
V25A8964
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 34 wa Tawala za Mitaa Tanzania, wadhamini wakiwa kwenye Mkutano wenye kauli mbiu “Umuhimu na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa ushiriki wa wananchi kupitia fursa na vikwazo kuelekea uchumi wa Viwanda” Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dodoma.

MGALU AWASHA UMEME KIJIJI CHA KISANGA

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KISARAWE

NAIBU Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu amelitaka shirika la umeme (Tanesco) lizingatie kufikisha umeme katika taasisi za umma ikiwemo shule na zahanati ili ziondokane na changamoto hiyo. Aliyasema hayo ,kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe ,mkoani Pwani wakati alipokwenda kuwasha umeme kijijini hapo .

Subira alisema, kwanza shirika hilo lihakikishe linaipatia umma shule ya msingi Kisanga ili waondokane na adha hiyo.“Tanesco wakati wa kuunganisha umeme mhakikishe taasisi hizo ikiwemo zahanati,shule na ofisi za serikali zinapata umeme ili kurahisisha utoaji huduma kupitia miradi ya umeme vijijini (REA)” alisema.

Aidha Subira alieleza ,wizara ina malengo ya kuhakikisha umeme unawaka kila kijiji ambapo kwa sasa miradi iko mingi lengo likiwa ni kufanikisha suala hilo.“Pia wananchi wanapaswa kutumia miradi hiyo kwani itakapokwisha bei haitakuwa hii ya 27,000 itaongezeka hivyo wachangamkie fursa hiyo,” alisisitiza Subira. Diwani wa kata ya Kisanga, Pili Chambuhi alisema,kijiji hicho kupata umeme ni mkombozi kwao kwani utasaidia kufanya shughuli ndogondogo za ujasiriamali. Alielezea hadi sasa jumla ya nyumba 60 zimeunganishiwa umeme.Pili, alisema kuwa shirika hilo linapaswa kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo ya ndani ndani na si maeneo ya barabarani peke yake.

Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu akionyesha ishara ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.


Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisanga wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani. 

TISA WAKAMATWA PWANI KWA MAKOSA YA KIUHALIFU -WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI

JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu Tisa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji, wizi na vitendo vingine vya kihalifu.

Ikumbukwe kwamba, septemba 18 majira ya saa 21:15 usiku katika kitongoji cha Kibosho ,Mapinga Wilaya ya Bagamoyo, watuhumiwa 15 wakiwa na gobore, mapanga, nondo na visu walivamia makazi ya Jaji mstaafu Salum Masati (69) na Flora Timoth (59) muuguzi hospitali ya Mwananyamala-Dar es salaam. 

Aidha baadhi ya nyumba za wananchi wa eneo hilo, waliwajeruhi na kuiba pesa taslim, simu wa mkononi aina mbalimbali, laptop, televisheni, ipad, saa za mkononi, spika za music system na vitu vingine vyenye thamani mbalimbali na kutokomea navyo. 

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa, alisema kufuatia matukio hayo jeshi hilo kwa kushirikiana na raia wema lilipokea taarifa za watuhumiwa wanaojihusisha na matukio hayo."Septemba 28 kati ya saa 6-8 usiku na tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa (majina yamehifadhiwa) "

"Baada ya kufanyiwa upekuzi tuliwakamata na gobore, televisheni 4,deki za video 5, amplifaya 3, ving'amuzi 4, redio za subwoofer 3, spika 5,simu za mkononi za aina mbalimbali 15, bangi ambayo haijasokotwa kifurushi kimoja ,misokoto/kete 169 na pakiti moja ya karatasi za kusokotea iitwayo lizla"alieleza Wankyo. 

Aliwataka ,wananchi wa Mapinga na maeneo ya jirani waliowahi kuvamiwa, kujeruhiwa na kuporwa kufika katika kituo cha polisi cha Mapinga wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutambua mali zilizokamatwa .

Wankyo alitoa rai kwa wananchi kuliamini Jeshi la Polisi na kuendelea kuwapatia taarifa za uhalifu na wahalifu pasipo kusita waweze kukamatwa na sheria ichukue mkondo wake.

Mchakeshaji Bill Cosby akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono, atupwa jela miaka mitatu hadi 10


AZAM TV: MFUGALE FLYOVER: Hii ndio CV ya Mhandisi Patrick Mfugale

INTRODUCING "BINUA" BY MOVANY

TEKU YAKILI KUFUNGIWA KUDAHILI WANAFUNZI, YATOA UFAFANUZI

Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Ufungaji Maonesho ya Teknolojia Bora ya Dhahabu Mkoani Geita

NGOs ZAPEWA SIKU 30 KUWASILISHA TAARIFA ZA MATUMIZI YA FEDHA KWA MSAJILI

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeyaagiza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuwasilisha kwa Msajili wa Mashirika hayo taarifa za fedha zilizokaguliwa za mwaka 2016 na 2017 ndani ya siku 30 kuanzia leo Septemba 28, 2018.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali yanayuhusu Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.Dkt. Ndugulile  ameyataka pia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuwasilisha taarifa inayoonesha miradi iliyotekelezwa kwa fedha iliyopatikana  kwa mwaka wa 2016 na 2017 na kutoa taarifa ya vyanzo vya mapato husika ikiambatana na hati za makubaliano za vyanzo husika kwa kipindi cha miaka hiyo.

Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameeleza kuwa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 inasisitiza misingi ya uwazi na uwajibikaji kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini.Amesisitiza  kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 29(a) na (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Na. 24 ya mwaka 2002, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yana wajibu wa kuwasilisha taarifa za kazi na fedha kila mwaka kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kwa Umma.

Ameongeza kuwa Kanuni za utendaji za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali za mwaka 2008 zinasisitiza uzingatiaji wa misingi ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi, masuala ya fedha na utawala hivyo wanufaika wa miradi yao, Halmashauri wanapofanya miradi na vyombo vya habari wana haki ya kupata taarifa hizo.Dkt. Ndugulile ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa miongozo hiyo bado Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mengi yamekuwa yakikiuka matakwa husika hivyo kuleta mkanganyiko katika jamii.

“Serikali itaendelea kufuatilia na haitosita kuchukua hatua kali za kisheria ikiwemo kuzifutia usajili NGOs ambazo zitashindwa kutekeleza agizo hili ndani ya muda uliopangwa” alisisitiza Dkt. Ndugulile.Pia Dkt.Ndugulile ameziagiza NGOs nchini zizingatie ushiriki wa wazawa wa ndani katika miradi wanayoitekeleza kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za NGOs hapa nchini.Aidha Dkt. Ndugulile ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutuma taarifa zao za fedha na za miradi kila mwaka kama ilivyoagizwa kupitia barua pepe ifuatayo dngo@communitydevelopment.go.tz .

Maagizo haya kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanakuja siku chache mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) Dkt. John Jingu kufuatilia utendaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini wakati alipokuwa akimuapisha kuwa Katibu Mkuu huyo katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.
Pix 1 (4)
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali yanayuhusu Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na ameziagiza NGOs kuleta taarifa za fedha za mwaka 2016 na 2017 na utekelzaji wa miradi yake kwa ofisi ya Msajili  ndani ya siku 30 . Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 28.09.2018

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW TORK, MAREKANI


VOA SWAHILI: Duniani Leo September 28, 2018

RAIS MSTAAFU JK ASHIRIKI MKUTANO WA TOKOMEZA MALARIA DUNIANI

$
0
0
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ameshiriki katika mkutano wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 26 Septemba, 2018 mjini New York Marekani.
Baraza la Kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri katika sekta ya umma na sekta binafsi chini uenyekiti wa Bill Gates. Lengo la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

MICHUZI TV: NYOSHI EL SAADAT ALIAMSHA DUDE LIVE

BREAKING NEWS: WAANDISHI WAGOMEWA KUCHUKUA MATUKIO KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YA WEMA SEPETU

$
0
0
Na Khadija Seif, 
Globu ya Jamii

Waandishi wa habari jioni hii wagomewa kuingia ndani Kwenye hafla ya uzinduzi wa filamu ya D.A.D ya Msanii wa kibongo nchini  Wema Sepetu maarufu kama ambayo amemshirikisha msanii kutoka nchi ya Ghana Van Vicker.

Akizungumza nje ya ukumbi Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amesema shughuli hiyo ilishanunuliwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini ambao wana mamlaka yote ya kurusha kwa matangazo ya moja kwa moja na kupiga Picha zote.

Mmoja wa wanahabari akiongea na Michuzi TV ameeleza kuwa ni vibaya kwani mpaka kuweza kuingia ndani ni lazima kulipa Dola elfu 20.
Hivyo basi kitendo hiko kilichofanywa na waandaji wa shughuli hiyo kimewanyima nafasi wanahabari ,na sio la haki kwani mpaka alipofikia nguvu nyingi zimetokana na kushirikiana na wanahabari.

Wanahabari wamesema kitendo hiko kinaweza kuibua matabaka, pamoja na chuki kutokana na ubaguzi huo uliofanyika katika hafla hiyo na watu kutafsiri vibaya kuwa imeonekana chombo hicho kuwa bora kuliko vingine.

Van Vicker aliwasii nchini jana kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyofanywa miaka mitatu iliyopita.

NDONDI OCTOBER 27, 2018 SI ZA KUKOSA!

Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images