Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 249 | 250 | (Page 251) | 252 | 253 | .... | 3272 | newer

  0 0


  I.                      UTANGULIZI:

  a)            Maswali

                                                                                          

  1.            Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutekeleza na kukamilisha majukumu yetu katika muda uliopangwa. Katika Mkutano huu Maswali 120 ya Msingi na 305 ya Nyongeza ya Waheshimiwa Wabunge yalijibiwa na Serikali. Aidha, jumla ya Maswali 12 ya Msingi ya Papo kwa Papo na 11 ya Nyongeza yalijibiwa na Waziri Mkuu.

  b)           Miswada


  2.            Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu, Bunge lako Tukufu lilijadili na kupitisha Miswada Mitatu (3). Miswada hiyo ni:

  i)             Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa Mwaka 2013 [The National Irrigation Bill, 2013];


  ii)            Muswada wa Sheria wa Vyama vya Ushirika wa Mwaka 2013 [The Cooperative Societies Bill, 2013]; na


  iii)           Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013 [The Constitutional Review (Amendment) Bill, 2013].


  0 0

  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

   TAARIFA KWA UMMA
   Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Uongozi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadau wa tasnia ya utalii nchini wanayo furaha kuwakaribisha wananchi wote na wadau mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka 2013 ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoa wa Mwanza.
  Siku ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila nchi mwanachama wa Shirika la Utalii Duniani husheherekea siku hii. Kwa mwaka huu Kimataifa, maadhimisho haya yatafanyika katika Visiwa vya Maldives.

  Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Utalii na Maji – Kulinda Hatma Yetu (Tourism and Water – Protecting Our Common Future)”. Kwa kuzingatia kauli mbiu hii, tunawajulisha wadau wote katika nyanja mbalimbali za uhifadhi mazingira, matumizi ya teknolojia sanifu, wafanyabiashara wa tasnia ya utalii na maliasili, wadau wa sekta ya maji, taasisi za elimu, wanasiasa, viongozi na wataalamu mbalimbali kushiriki katika wiki ya maadhimisho ya utalii duniani.

  Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na tafsiri ya kauli mbiu katika Nyanja mbalimbali kama, mashindano ya uandishi wa insha mbalimbali kuhusiana na mada, michezo na burudani mbalimbali, maonesho ya utalii, malikale, misitu na masuala ya uhifadhi kwa ujumla,  teknolojia mbalimbali, pamoja na ziara ya kutembelea Hifadhi ya Saanane.

  Wananchi pamoja na wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki katika maadhimisho haya.

  “Kumbuka Utalii ni nyenzo ya kuhamasisha uhifadhi kwa uhai na ustawi wa Taifa”

  Imetolewa na:

  Katibu Mkuu,

  Wizara ya Maliasili na Utalii,

  S.L.P 9372,

  DAR ES SALAAM.


  Simu: 255-22-2864230

  Barua pepe: ps@mnrt.go.tz  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA UCHUKUZI

  MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA 

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua za masika (Machi - Mei) 2013 na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi  cha Oktoba hadi Disemba2013.

  1.0 TATHMINI YA MVUA KIPINDI CHA MACHI – MEI, 2013

  Katika msimu uliopita wa mvua za masika 2013, maeneo mengi ya  nchi yalipata mvua za wastani isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Tabora, Rukwa, Mara na Singida  ambayo ilipata mvua juu ya wastani. Wakati huo huo baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa, Ruvuma, Kilimanjaro na maeneo mengi ya mwambao wa pwani yalipata mvua chini ya  wastani.


  Vifuatavyo ni viwango vya mvua pamoja na asilimia ya mvua zilizonyesha ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu katika baadhi ya vituo nchini:

  0 0

   .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mwanzilishi na Mkurugenzi waShirika la Africa School House Bi.Ainee Bessire (watatu kushoto) pamoja naMbunge wa Misungwi Charles Kitwangwa(kushoto) na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo(kulia) wakikata utepe kuzindua rasmi shule ya msingi Ntulya katika kata ya Mondo wilayani Misungwi.Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Ntulya muda mfupi baada ya kuizindua katika kata ya Mondo wilayani Misungwi leo. Shule hiyo imejengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la kiserikali la Africa School House lenye makao yake nchini Marekani.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo. 
  Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0

  Afisa Msadizi wa uhamasishaji Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro, Lidya Mandara akiwaPA MAELEZO warembo wa Redds Miss Tanzania 2013 juu ya bwawa la viboko na mamba lililopo katika hifadhi hiyo wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
  Warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa wameketi katika moja ya sehemu za kupumzikia watalii katika hifadhi ya Taifa Mikumi wakati warembo hao walipo tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.

  Warembo wa Redds Miss Tanzania 2013 wakiangalia Mamba na Viboko waliokuwepo bwawani wakati walipotembelea hifadhi hiyo jana
  Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro, Tutendaga George akiwakawia warembo wa Redds Miss Tanzania 2013 walio tembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani kofia na CD zilizo na taarifa mbalimbali mbali za hifadhi hiyo ya taifa.
  Warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya taifa Mikumi jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.

  0 0

  Wachezaji wa Timu ya Taifa, Taifa Stars wakiwasili katika Hoteli ya Sea View iliyopo Banjul, Gambia, jana jioni tayari kwa mechi dhidi ya Gambia kesho Jumamosi. 
  Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama hapa Banjul, Gambia tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji itakayochezwa kesho (Septemba 7 mwaka huu).

  Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili hapa jana (Septemba 5 mwaka huu) saa 11 jioni ikitokea Dakar, Senegal ambapo ilichelewa kuunganisha ndege, hivyo kuamua kutumia usafiri wa barabara kwa vile ni karibu na baadaye kupanda kivuko kuingia Banjul badala ya kulala na kuchukua ndege nyingine siku inayofuata.

  Wachezaji wako katika hali nzuri na leo jioni wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Independence ulioko Bakau ambao utatumika kwa mechi ya kesho. Timu imefikia hoteli ya Seaview iliyoko kandokando ya Bahari ya Atlantic.

  Mechi hiyo itaanza saa 10.30 jioni kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 1.30 usiku, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda Munyemana Hudu. Waamuzi wasaidizi ni Theogene Ndagijimana, Honore Simba na Issa Kagabo. Kamishna ni Andy Quamie kutoka Liberia.

  Washabiki na vyombo vya habari vya hapa wanaizungumzia mechi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa pande zote, huku Gambia ikiwa imeita wachezaji tisa wanaocheza barani Ulaya na Marekani. Gambia ambayo imepata uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Gambia (GFA) imepania kuhakikisha haimalizi mechi za mchujo ikiwa na pointi moja tu.

  Kwa upande wa Tanzania, Kocha Kim Poulsen amesema nia ni kuona Stars yenye pointi sita inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ambayo tayari imechukua tiketi pekee ya kucheza raundi ya mwisho kutoka kundi hili la C.
  “Mechi hii ni muhimu kwetu kwa vile tunataka matokeo mazuri ugenini. Lakini kikubwa ni kuwa matokeo mazuri si tu yatatuweka katika nafasi ya kuwa wa pili, lakini vilevile yatatusaidia kuongeza pointi kwenye viwango vya ubora vya FIFA, na kikubwa zaidi hii ni sehemu ya maandalizi ya sisi kucheza Fainali za Afrika za 2015,” amesema Kim.

  Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
  +2207362384 Banjul

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akionyesha ngao aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi URA-SACCOS, Naibu Kamishna wa Polisi, Thobias Andengenye. Ngao hiyo alikabidhiwa jana kama ishara ya IGP kuwa balozi wa saccos hiyo katika viwanja vya kilwa road wakati wa uzinduzi wa Tawi la URA-SACCOS la Kilwa Road.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Kilwa Road la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi URA-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Saidi Mwema akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bahati nasibu ya kushindania pikipiki na cherehani itakayochezeshwa na Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, Ura Saccos tawi la kilwa road. Tawi hilo lilizinduliwa na IGP.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini , IGP Saidi Mwema akipasha na maofisa, wakaguzi na askari wa Jeshi la Polisi, wakati wa uzinduzi wa Tawi la Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi Kilwa Road, Ura-Saccos jana jijini Dar es Salaam.
  Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi, Advera Senso akionyesha ngao aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa bodi ya Chama cha Kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, URA-SACCOSS. Ngao hiyo ni ishara ya kuwa balozi wa SACCOS hiyo ambayo tawi lake la Kilwa Road lilizinduliwa jana na IGP.
  Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Jeshi la Polisi wakionyesha mahadhi ya makhirikhiri jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tawi la Kilwa Road la Chama cha kuweka na Kukopa cha Jeshi la Polisi, URA-SACCOS. (Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi).

  0 0
 • 09/06/13--09:56: TASWIRAZZZZ
 • Kamera ya Globu ya Jamii,Mchana wa leo imefanikiwa kuinasa Taswira hii ya wanafunzi waliokuwa wakiteka maji mcda wa masomo katika Bwawa moja lililopo kwenye Kijiji cha Kishapu,Mkoani Shinyanga.

  0 0

  Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw.Ramadhani Sululu akiongea mapema leo ofisini kwake kuhusu ufunguzi wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI itakayofanyika mjini Dodoma Septemba 21 mwaka huu.

  Timu za mpira wa miguu za Hazina na Ofisi ya Mkoa Dodoma zinatarajiwa kucheza mechi ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayohusisha watumishi wa umma katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) .

  Katibu Mkuu wa SHIMIWI Bw. Ramadhani Sululu alisema hayo mapema leo alipokuwa akiongea kuhusu ufunguzi wa mashindano hayo ambayo yanayotarajiwa kuanza Septemba 21 mkoani Dodoma.

  Alisema timu zote zinatakiwa kukamilisha usajili haraka iwezekanavyo na kuwahi kufika mjini Dodoma kabla ya tarehe 20 Septemba mwaka huu.

  “Timu zote zitakazoshiriki katika mashindano zinatakiwa kufika katika kituo cha mashindano siku moja kabla ya kuanza mashindano na timu itakayochelewa kufika katika kituo na kukuta michezo yake imepita itahesabika kuwa imepoteza michezo hiyo”alifafanua Bw.Sululu.

  Aidha,alizitaja timu nyingine zitakazofungua pazia la michuano hiyo kuwa ni Bunge na TAMISEMI kwa upande wa mpira wa pete, Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa upande wa timu za kamba wanawake na wanaume.

  Sambamba na ufunguzi huo Bw. Sululu alisisitiza juu ya wachezaji kupima afya zao kabla ya kuanza kwa mashindano ili waweze kushiriki kikamilifu na kujua kama wako fiti kwa michezo hiyo yenye ushindani mkubwa miongoni mwa watumishi.

  “Kila mchezaji anawajibika kupimwa afya yake na daktari wa michezo kabla ya kuanza michezo”alitahadharisha Bw. Sululu.

  Michezo ya Watumishi wa Serikali (SHIMIWI) imekuwa ikijizolea umaarufu siku hadi siku kutokana na ushindani wake na nidhamu inayoonyeshwa na washirikihivyo kutoa picha tofauti na mashindano mengine yanayoendeshwa hapa nchini.

  0 0


  0 0

  Baadhi ya wachezaji wanaoshiriki fainali za mashndano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa, Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye maandamabo kuingia ukumbini wakati wa ufunguzi wa fainali hizo zinazofanyika Airport Pub mkoani humo.
  Meneja matukio wa TBL tawi la Mbeya, Godfrey Mwangugulu(kushoto) akizungumza na wachezaji wa Pool (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa yanayofanyika Airport Pub mkoani humo.Wengine kushoto kwake ni mratibu wa mashindano hayo, Peter Zacharia,Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima na Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Samweli Aron.
  Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima akizungumza na wachezaji wa Pool(hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa yanayofanyika Airport Pub mkoani humo.Kulia ni Meneja matukio wa TBL tawi la Mbeya, Godfrey Mwangugulu,mratibu wa mashindano Peter Zacharia na Mwenyekiti wa chama cha Pool Mkoa wa Mbeya, Samweli Aron.
  Afisa michezo wa Mkoa wa Mbeya, George Mbijima akicheza wakati wa ufunguzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa yanayofanyika Airport Pub mkoani humo.Wengine wanaoshuhudia kushoto kwake ni mratibu wa mashindano , Peter Zacharia na Meneja matukio wa TBL tawi la Mbeya, Godfrey Mwangugulu.

  0 0

  Mkazi wa Kawe Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Musa Senkando anatafutwa na polisi kwa mahojiano baada ya kutoweka akisadikika kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Yusta Mkali.

  Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo(jana)habari za kuaminika za mauaji hayo kutendeka zilizibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema kwa uchunguzi wa awali mauaji hayo yanasadikika kutokea usiku wa kuamkia leo.

  “Yusta ameuwawa na kitu chenye ncha kali kilichomchoma kwenye koromeo na inasadikika mume huyo ameshatoweka na jeshi la polisi linamtafuta kwa uchunguzi zaidi kwani yeye ndiye aliekuwa mtu wa mwisho kuwa nae ndani,” alisema.

  Wambura alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

  Naye Mtoto wa dada yake marehemu ambaye alikuwa anaishi naye, Joshua Zebedayo alisema yeye ameshtukizwa na mauaji hayo pale alipo amka asubuhi kuelekea kufanya usafi chumbani mwa mama yake mdogo kwani yeye huwa analala chumba kingine na ndipo alipoukuta mwili wa marehemu ukiwa na majeraha pamoja na damu.

  “Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi nilipoamka kufanya usafi chumbani kwa mama kama ilivyo kawaida yangu mama na baba waendapo kazini, ila cha kushangaza nilimkuta mama bado amelala wakati alitakiwa kuwepo kazini. Nilimwita mama bila mafanikio nikafunua shuka alilojifunika na kumkuta amekwisha fariki dunia,” alisema kijana huyo huku akibubujikwa na machozi.

  Marehemu Yusta wakati wa uhai wake,alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya umma Frontline Porter Novelli(PR COMPANY)
  Huyu ndiyo Mtuhumiwa Musa Senkando anaetafutwa na polisi.
  Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake.
  Wakazi wa Kawe wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa marehemu ukitolewa ndani kwenda kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

  0 0

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.

   Mkongwe wa Hip Hop,Afande Sele a.k.a Baba Tundaa.k.a Simba Mzee akiimba kwa hisia mbele ya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
  Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu.
   MKali wa kukamua mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwarusha maelfu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanaondelea kumiminika kwenye uwanja wa Sokoine usiku huu.
  Msanii aliyewahi kulwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu,pichani akitumbuiza mbele ya mashabiki wake.
  Baadhi ya watu wakifuatilia yanayojiri usiku huu kwenye tamasha la Seremgeto Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
   Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya

  PICHA ZAIDI HAMIA LIVE MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0

  Tanzania DMV
  Senegal DMV

  Timu ya Tanzania DMV Jumapili Sept 8, 2013 itajitupa tena uwanjani kwa mpambano wa kimataifa wa kirafiki kati yao na Senegal mechi inayotarajiwa kuanza saa 9:30 alasiri (3:30pm) kwenye uwanja uliopo 2013 Walker Mills, Capitol Heights, MD.
  Mechi nyingine itakuwa Sept 15, 2013 Jumapli ijayo dhidi ya timu ya Guinea.

  0 0

  Mtangazaji wa kipindi cha burudani cha Funika Base kutoka Radio 5 ya Mjini Arusha , Julius Kamafa (kushoto) akifanya mahojiano na Washiriki wa Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2013 katika studio za redio hiyo jana.
   Baadhi ya warembo wakijieleza Live Redio 5 hii leo walipotebelea kituo hicho.

  Meneja Biashara wa TAN MEDIA, Angela Maina akizungumza na warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati warembo hao walipotembelea Kituo cha Redio cha Radio 5 cha mjini  Arusha leo kujionea shughuli mbalimbali na kufanya mahojiano maalum. Warembo wa Redd’s Miss Tanzania wapo mkoani Arusha kwa ziara ya kimafunzo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa TAN MEDIA wakisikiliza kwa makini mkutano huo baina ya warembo na Viongozi wa TAN MEDIA.
  Meneja Biashara wa TAN MEDIA, Angela Maina akizungumza na warembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati warembo hao walipotembelea Kituo cha Redio cha Radio 5 cha mjini  Arusha jana kujionea shughuli mbalimbali na kufanya mahojiano maalum.
   
   Walimbwende na Viongozi wa TAN MEDIA na watangazaji wa Radio 5 walipiga picha ya kumbukumbu.
  Warembo wakiondoka Radio 5

  0 0

  Mpendwa msomaji tunashukuru kwa mapendekezo kupitia kura zako, hatimaye blog hii yahttp://eddymoblaze.blogspot.com/ imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tuzo ya THE BEST DESIGN/GRAPHIC DESIGN BLOG, Tunakuomba hivi sasa uipigie kura blog hii ili iweze kuchukua tuzo hiyo. 

  Ili kupiga kura yako tafadhali bonyeza link ifuatayo na uchague palipoandikwa eddymoblaze.blogspot.com:-


  Asante kwa ushirikiano wako, piga mara nyingi uwezavyo

  0 0


  Na Edwin Moshi, Makete
  Serikali wilayani Makete mkoani Njombe imewataka wananchi kutoa ushirikiano wa pamoja kuwakamata ama kutoa taarifa kwa ngazi husika pindi wanapowaona watu wakijisaidia ovyo maeneo yasiyo rasmi

  Hayo yamesemwa na afisa afya wilaya ya Makete Bw Boniphace Sanga wakati akizungumza na mtandao huu na kuongeza kuwa kumekuwa na ongezako la magonjwa hasa ya kuhara ambayo yanatokana na watu wanaojisaidia ovyo na kuchafua mazingira

  Bw sanga amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja na si la bwana ama bibi afya pekee na kwa kuwa wananchi ndio wanaoshinda maeneo mbalimbali wanawaona wale wanaojisaidia hovyo na kuomba watoe taarifa kwenye ofisi yake ili wachukuliwe hatua za kisheria

  Amesema inashangaza kuona hadi sasa wapo watu ambao hawana vyoo na wanaongoza kwa kuchafua mazingira kutokana na kujisaidia ovyo, na kutoa wito kuwa msimu huu ni wa kiangazi hivyo wanatakiwa kujenga vyoo kabla mvua haijanyesha

  "Kwa kweli natoa wito nyumba bila choo haijakamilika, acheni kun***a(akimaaisha kujisaidia) maeneo ambayo si kwa ajili hiyo, unakuta mtu kavaa vizuri lakini ni namba moja kujisaidia maporini, huu si ustaarabu na watu wa namna hii ndio wanaoleta magonjwa kwenye wilaya yetu

  Katika hatua nyingine Bw. sanga amewaomba wananchi kuendelea kujijengea utaratibu wa kutupa taka maeneo yanayoruhusiwa( kwenye vizimba vya taka) na kuwaasa kuacha tabia ya kutupa chupa za soda na maji mitaani kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokamatwa

  0 0

  Description: cid:image001.png@01CEA58D.85562470
  EAST AFRICAN COMMUNITY
    
  East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania; 6 September 2013: As part of the process to deepen democracy in the region and following an invitation by the Government of Rwanda, the East African Community is preparing to deploy an Election Observer Mission (EOM) to the Parliamentary Elections in Rwanda scheduled to take place on 16th September 2013. The Mission will be on the ground from 10–19 September, 2013 and will be lead by the former Minister of EAC of the Republic of Kenya, Hon. Musa Sirma.

  The Mission’s mandate is to observe the preparations for the election, the polling, and the overall electoral environment. The mission will also assess the conduct of the process as a whole and, where appropriate, make recommendations for the future strengthening of the electoral framework in the Republic of Rwanda.

  EOM are expected to look out for best electoral practices that could be emulated in the region and generally to widen and deepen cooperation between Partner States in socio-economic and political Affairs. The Mission will ascertain whether the elections were free and fair and conform to principles of good governance and democracy in the region.

  According to Rwanda’s Electoral Calendar, the legislative elections are staggered over 3 days with 16th September 2013 being the polling day for direct election of members of the National Assembly, the 17th
  September 2013 for indirect elections of 24 female Members of Parliament; and finally on 18th September 2013 is slated for indirect election of youth and people with disabilities.

  The Mission,  will undergo a pre-election training session, undertake a consultative session with key stakeholders and accreditation from 10th - 12th September 2013 and be deployed to the field from 13thSeptember, 2013

  The EAC Observer Mission consists of 36 members, who include among others Members of EALA, officials from National Electoral Commissions and Human Rights Commissions from Partner States and the East African Community Secretariat.

  A Mission report with recommendations on how best to improve election management in Rwanda in particular and in the EA region in general will be produced and  submitted to, among others, the National Electoral Commission – Rwanda and the EAC Council of Ministers for consideration to inform future engagement and interaction during electoral processes in other Partner States

  The Mission will issue a launching statement to the media at a Press Conference scheduled for 10thSeptember  2013 at Lemigo Hotel, Kigali, Rwanda. All members of the  local and international media are invited to attend

  0 0

  DFF-DAR---LIFE 

  The Tanzanian Chefs Association (TCA) would like to welcome you to the first ever Food Fair in Dar-es-Salaam on Saturday, September 7, 2013 from 11:00am to 3:00pm (music till 5pm) at the Botanical Gardens, Garden Avenue.
  Discover a world of food! With over 30 different flavors for your taste buds, live cooking demonstrations by the chefs; face painting for the children; live music/band and food tasters for everyone. Come join us on a spectacular day for family and friends, young and old.
  Tickets: 35,000/- (Limited Tickets Available)
  Tickets available at: Epidor; Southern Sun; Waterfront, Slipway, Holiday inn and AK’s Café.
  For ticket information you can call: +255 767 500 380 or +255 788 234 100

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wakati alipowasili katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kuanza ziara ya kikazi 
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya kuzindua rasmi Shule ya msingi Ntulya,iliyopo kata ya Mondo, Wilayani Misungwi,Mkoa wa Mwanza.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na bvaadhi ya watoto waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa Shule ya Msingi Ntulya,katika kata ya Mondo,wilayani Misungwi
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba motto Paulo Muhangwa muda mfupi baada ya kuzindua shule ya Msingi Ntulya wilayani Misungwi,Mkoani Mwanza
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalmiana na baadhi ya wauguzi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo,
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezoi katika hospitali ya wilaya ya Misungwi wakati wa uzinduzi wa huduma ya X Ray katika hospitali hiyo,

older | 1 | .... | 249 | 250 | (Page 251) | 252 | 253 | .... | 3272 | newer