Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

VIGOGO SITA WA KAMPUNI YA CHAI YA MPONDE WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tanga jana imewafikisha mahakamani vigogo sita wa Kampuni ya Chai ya Mponde Tea Estate Limited kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya dola za kimarekani 15,050,254.00 sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 30.

Kosa hilo linadaiwa lilitendeka kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2000 na 2013 ambapo watuhumiwa hao baada ya kukosa dhamana wamepelekwa kwenye Gerezani wakisubiri kesi yao itakapotajwa tena.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Takururu mkoani Tanga Christopher Mariba alisema kosa hilo ni kunyume na aya ya kumi ya Jedwali la kwanza la kifungu cha 57(1) na kifungu cha 60(2) cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 pitio la mwaka 2002,iliyofanyiwa marekebisho kwa sheria namba 3 ya mwaka 2016.

Aliwataja waliofikishwa mahakamani kuwa ni Nawab Abdulrahim Mulla, Shahdad Nawab Mulla,William Shelukindo,Richard Abraham Mbughuni, Richard Madadi Semroki na Rajabu Ali Msagati ambao ni wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Mponde Tea Estate Company na kusomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa mkoa wa Tanga Desdery Kamugisha.

Alisema baada ya kusomewa mashitaka hayo washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo huku pia mahakama hiyo ikizuia kusikiliza maombi ya dhamana ya washtakiwa kwa sababu zilezile kwamba haina mamlaka ya kisheria yakusikiliza shauri hilo.

Akitolea ufafanuzi wa mashtaka hayo Mkuu huyo wa Takukuru mkoani Tanga alisema vigogo hao ni wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya MPONDE TEA ESTATE LIMITED ambayo awali ilikuwa inajulikana kama MPONDE TEA FACTORY kampuni ambayo kabla ya ubinafsishaji ilikuwa ni mali ya serikali.

“Uchunguzi wa Takukuru umebaini kwamba vigogo hawa kwa nyakati tofauti walifanya udanganyifu kwa kuagiza mizigo na malighafi mbalimbali kwa niaba ya wakulima wadogo wadogo wa chai waliopo wilayani Lushoto mkoani Tanga wakati si kweli… Vigogo hao wamekuwa wakifanya vitendo hivi na kisha kufanikiwa kuingiza vifaa vya thamani ya zaidi ya sh.bilioni 135.

Alisema kwa udanganyifu huo,vigogo hao waliomba na kupata msamaha wa kodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wa zaidi ya sh. Bilioni 35 wakati wakijua kwamba mizigo na malighafi hizo hazikuwa ni kwa ajili ya walengwa ambao ni wakulima wadogo wadogo wa chai.

Alieleza kwamba kwa mantiki hiyo vigogo hao wameisababishia serikali hasara ya sh.Bilioni 30 ambazo zingelipwa na kuingia katika mfuko wa serikali.“Lakini kwa hesabu za haraka haraka sh.bilioni 30 zingeweza kujenga kilometa 30 za barabara ya lami,Zahanati 60,Madarasa 1500,Visima vya maji 1000 au viwanda vidogo vidogo 60 kwa wakazi wa mkoa wa Tanga “Alisema.

Hata hivyo alisema Takukuru mkoani Tanga inatoa wito kwa watanzania wote hususani wakazi wa Jiji la Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo katika kufichua walarushwa wenye lengo la kuzorotesha maendeleo ya watanzania.

Mkutano mkuu wa kwanza wa MDIN wafanyika Sweden

$
0
0

Picha ya pamoja ya wana MDIN baada ya mkutano mkuu wa kwanza uliofanyika mjini Stockholm, Sweden katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania. Kutoka kushoto Balozi Dkt. Wilbroad Slaa, Bi. Josephine Slaa, Bi. Joyce Kimwaga Lundin, Katibu Mkuu Ahmed Salum Ahmed na wanachama wengine wa MDIN.

Jumamosi ya tarehe 15 Septemba taasisi isiyo ya kiserikali ya Muheza Diaspora International Network (MDIN) ilifanya mkutano wake mkuu wa kwanza kwa wanachama wote. Taasisi ya MDIN iliyosajiliwa rasmi mwaka 2017 ina malengo ya kuchangia maendeleo ya Watanzania, hasa wale wenye kipato cha chini waweze kujiendeleza kupitia viwanda vidogo vya miradi ya kilimo na ufugaji.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden, ulimualika Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuwa mgeni rasmi. Mheshimiwa Balozi Dkt. Slaa aliambatana na mkewe, Bi. Josephine Slaa, ili kusikiliza mipango na changamoto za taasisi hii tangu kuanzishwa kwake rasmi. Pamoja nao, alialikwa pia Mwenyekiti wa Baraza la Diaspora la watanzania Duniani au TDC-Global, Norman Jasson.
Kutoka kushoto, Bi. Elizabeth Lugendo, Bwana Matiku Kimenya na mke wa Balozi Dkt. Slaa, Bi. Josephine Slaa  wakifuatilia kwa makini hoja katika mkutano mkuu cha MDIN. 

Kwa kipindi hiki, taasisi ya MDIN imejikita kwenye miradi ya majaribio katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga. Alipoulizwa kama taasisi hii inahusiana na Muheza peke yake, Mwenyekiti wa MDIN, Bi. Joyce Kimwaga Lundin, alisema "Jina la Muheza Diaspora International Network limetokana na sababu kuwa wengi kati ya waanzilishi, wametokea Muheza, lakini lengo ni kuleta maendeleo Tanzania nzima. Kutokana na sisi kuifahamu vizuri Muheza, tumeona tuanzie hapo ili tukishapata matokeo mazuri tuweze kusambaza hii miradi sehemu mbalimbali Tanzania. Lakini, sababu ya pili ni ubora wa ardhi ya Muheza ambayo ina uwezo wa kustawisha kila kitu bila tatizo. Hivyo, tunashirikiana na wataalamu wa viwanda, kilimo pamoja na mifugo katika kutafuta njia mbadala ili kuongeza faida kwa mkulima na kuinua kiwango chake cha maisha."

Mkutano huo ulijumuisha watanzania toka nchi mbali mbali duniani kama vile Norway, Ufaransa, na Sweden. Wana MDIN walitumia mkutano huu kutathmini safari yao tangu kuanzishwa kwake hadi walipofikia. Walitumia muda huo kuchambua mafanikio, changamoto na vikwazo walivyokutana navyo kabla ya kuanzisha MDIN hadi pale taasisi ilipotengemaa na kuanza kufanya miradi ya maendeleo katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga.


Kwa upande wake, Balozi Slaa aliwashukuru na kuwapongeza wana MDIN kwa kuwa na malengo na mipango endelevu kusaidia watanzania nyumbani, hasa kwa kugusa watu wa chini zaidi "Nishukuru sana kwa jitihada mlizozichukua, nimeelezwa aina ya shughuli mnazofanya. Nimeelezwa kuwa mnatafuta fedha zenu kisha mnanunua vitu na kuvisafirisha Tanzania kwa ajili ya kuwasaidia watanzania wenzenu. Sina maneno ya kuwashukuru, lakini ninasema Asante. Hii inaonyesha ni jinsi gani Watanzania walivyo wazalendo hata kama wamechukua uraia wa nchi nyingine."


Pamoja na hayo, Balozi Slaa aliwasihi wana MDIN kumshirikisha kama kutakuwa na changamoto ya aina yeyote itakayojitokeza katika kutimiza majukumu yao ya kuwekeza nchini Tanzania ili aweze kuchangia mawazo na hata kuwapa mwongozo sahihi pale inapohitajika.

Kwa kuongezea, Bi. Josephine Slaa aliwapa moyo wana MDIN na kuwasihi wasikate tamaa hata kama vikwazo vitazidi kuwa vingi, kwani mara nyingi mwanzo huwa mgumu. Aliongeza pia, ni vizuri kama wakipanga mipango ya muda mfupi na ya muda mrefu ili kuweza kuona juhudi zao zinazaa matunda mapema na kuwapa moyo ili kutokata tamaa mapema. Hii inatokana na ukweli kuwa mipango ya muda mrefu huchukua muda kuzaa matunda, na binadamu hukata tamaa pale anapoona juhudi zake hazizai matunda.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Salum Maulid Salum akitoa neno kwa wana MDIN alipohudhuria sherehe hizo kwa muda mfupi.


Taasisi ya MDIN inapatikana kwenye tovuti ya www.muhezadiaspora.org na pia ina ukurasa wa Facebook www.facebook.com/muhezadiaspora/.

PRINCE WILLIUM ATEMBELEA BANDARI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, kushoto, akimkaribisha Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William bandarini mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam jana. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu. Pembeni ya Mhandisi Kakoko ni Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, katikati, akitazama sanamu ya Twiga aliyomzawadia Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, kushoto, mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, katikati, akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Twiga Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, kulia, mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu. Kushoto ni Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi. 
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, katikati, akitambulisha watendaji wake kwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza, Prince William, kushoto, mara baada ya kufanya ziara ya kujionea utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Price William yupo nchini kwa ziara maalumu ya siku tatu. Nyuma ya Mhandisi Kakoko ni Waziri wa katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.

MTOTO WA MIAKA TISA APOTEA DAR, NI BAADA YA KWENDA SHULENI HAKURUDI TENA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
MTOTO  anayetambulika kwa jina la Thomas Rwembiza Renatus(9)  anayesoma darasa la pili  Shule ya Msingi Kilungule jijini Dar es Salaam amepotea na hajarudi nyumbani tangu juzi.

Imeelezwa kuwa mtoto huyo anaishi Kimara Bonyokwa mtaa wa Mavurunza na kwamba amepotea  Septemba 26 alivyotoka asubuhi saa nne kuelekea shule.

 Tayari familia ya mtoto huyo imetoa ripoti Polisi na kupewa  RB.

Baba wa  mtoto huyo amesema kwa atakayemuona atoe taarifa kituo chochote cha Polisi au awasiliane naye kwa namba ya simu 0652066366

Dkt. Mwakyembe: Viongozi wa Kimila Nchini Himizeni Uzalendo na Utaifa

$
0
0
Na Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.
Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa rai kwa Viongozi na Wazee wa Kimila nchini , kuhakikisha wanatumia nafasi walizonazo kuhimiza  uzalendo na utaifa kwa kuikumbusha jamii dhawabu ya kudumisha Utamaduni.
Hayo amesema leo Jijini Arusha katika Mkutano na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Wamasai,ambao hukutana mara kwa mara kujadili  mila na desturi za kabila hilo .
 Aidha Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa viongozi wa kimila wana nafasi kubwa ya kujenga na kudumisha mila na desturi kwa kurithisha tamaduni hizo kwa kizazi kilichopo ili kutokupoteza tamaduni hizo muhimu.
“Kumbukeni kuwa mnanafasi kubwa ya kulea jamii yetu kwa misingi ya mila na desturi  nzuri ,kwa kuwa jamii inawasikiliza, inawaelewa na kuwaheshimu ” amesema Dkt. Mwakyembe.
Anazidi kufafanua kuwa kwa kutumia mila na desturi nzuri itasaidia kurejesha vijana ambao kwa asilimia kubwa wameadhiriwa na maendeleo ya Teknolojia na Utandawazi,hivyo kuupuza utamaduni wa mtanzania .
Vilevile Dkt. Mwakyembe amewaahidi viongozi hao kufanyia kazi changamoto wanayokumbana nayo   kuhusu eneo la kukutania lililopo ndani ya Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Amani Lukumay (Kulia) baada ya kuwasili katika Chuo cha Ufundi  cha Arusha (Arusha Technical College) kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Kimila wa Wazee hao leo Jijini Arusha.
 Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiongozana na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai kuelekea mahali ambapo mkutano wa kimila unafanyika.
Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai  Bw. Isack Lekisongo (kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati)  njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na Ukoo wa Mollel kuingia  katika eneo  ambalo  hutumika kufanya mila mbalimbali za kabila hilo, eneo hilo limo ndani ya nyumba za Waalimu wa Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).
Waziri wa Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(Katikati) akijadiliana jambo na Viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Maasai , alipohudhuria mkutano wa kimila wa viongozi hao leo Jijini Arusha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TADB yaendelea kuchagiza mapinduzi ya kilimo katika Skimu ya Umwagiliaji Mombo Tanga

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) imeahidi kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuwapatia mitaji itayowawezesha kununua zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP 2).

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa skimu hiyo, Katibu wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo, Bwana Sufian Mohamed aliishukuru serikali kupitia Benki ya Maaendeleo ya kilimo kwa kuwapatia mkopo wa gharama nafuu ambao umeweza kuwanufaisha jumla ya wakulima 429 kati yao wanawake wakiwa asilimia 54, mkopo ambao umeboresha miundo mbinu ya skimu hiyo hali iliyowezesha kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 1.9 hadi kufikia tani 6 kwa hekta moja.

Skimu hiyo ya Mombo mpaka sasa imenufaika na mkopo wa mbolea, mbegu bora pamoja na trekta, mashine ya kuvunia na sasa Benki ya Kilimo ipo katika hatua ya mwisho ya kuwapatia mashine ya kukobolea mchele ili waweze kuongeza thamani ya zao la mpunga katika skimu hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, wakati wa yeye na timu yake walipofanya ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji unaotekelezwa na skimu hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (aliyenyanyua mkono) akipata maelezo ya maendeleo ya matrekta na mashine ya kuvunia walizozitoa kama mkopo kwa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akichukua kumbukumbu ya mandhari ya shamba lenye ukubwa wa hekta 220 linalolimwa kwa ufadhili wa mkopo kutoka TADB.
 Timu ya Ukaguzi ikiangalia mandhari ya mifereji inayotumia kumwagilia shamba hilo.
 Timu ya Ukaguzi ikiangalia namna uongezaji wa thamani wa zao la mpunga unavyofanyika,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akioneshwa mfuko utakaotumika kufungashia mchele unaozalishwa na Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo. Skimu hii imeweshwa kwa mkopo unaotolewa na TADB.

MFAHAMU DKT. JOSEPH JACKSON, MWAFRIKA ALIYEGUNDUA RIMOTI TELEVISIONI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
IDADI kubwa ya watu hupenda kuangalia televisheni katika kufuatilia masuala mbalimbali kama vile mpira, muziki na hata tamthiliya, tumekuwa tukitumia kifaa maarufu kama rimoti katika kubadili chaneli mbalimbali Dkt. Joseph N. Jackson ni mwafrika aliyegundua kifaa hicho.

Imeelezwa kuwa kablanya kutokuwepo na kifaa hicho televisheni ilitumika kama rimoti pia hali iliyoleta adha katika kubadilisha chaneli hasa za redio na televisheni.

Jackson alianza kujihusisha na masuala ya ugunduzi  tangu alipokuwa mtoto na katika mahojiano katika vipindi mbalimbali vya redio na televisheni alieleza kuwa akiwa na miaka 8 alifungua redio ili kuweza kuona watu wanaozungumza na hapo ndipo alipoanza kudadisi kuhusiana na teknolojia hiyo.

Akiwa na miaka 17 alikuwa  katika harakati za kutafuta maisha, aliwahi kuhudumu kama msaidizi wa utengenezaji wa vifaa vya mafuta na baadaye alijiunga na jeshi huko Marekani na hii ni kati ya miaka 1956 hadi 1968.

Akiwa anahudumu katika jeshi alianza kuhudhuria shule kwa masomo ya jioni ambako alijifunza namna kufanya matengenezo televisheni na baadaye kumiliki duka lake la matengenezo kwa miaka 7.

Ugunduzi wake wa kwanza ulikuwa ni V chip kifaa ambacho kililenga kufunga maudhui yasiyofaa kwa watoto na hii ilimsaidia sana katika kutengeneza rimoti ambayo imeelezwa aliigundua katika miaka ya 1961.

Dkt. Jackson ni mtoto wa 4 kati ya 8 akiwa na shahada ya uzamivu katika masuala ya fedha na utawala akiwa amehudumu nafasi mbalimbali hasa jeshi kwa miaka 12, uhandisi (nchini Korea) na ametunukiwa tuzo mbalimbali za heshima katika televisheni zikiwemo zilizotolewa na Hollywood na vyuo mbalimbali.

BUNGE LA EALA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WATOA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI YA MV NYERERE

$
0
0
Spika wa Bunge Job Y. Ndugai (Mb), (kushoto) akimsilikiliza Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Alhaji Adam Kimbisa wakati wa makabidhiano ya kiasi cha Shillingi Milioni 8,550,000 kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere. Kulia ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), akipokea shilingi Milioni 8,550,000 kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa kwa niaba ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere. Bunge la Jamahuri ya Muungano pia limetoa rambirambi yake kiasi cha Sh. milioni 86

Spika wa Bunge akisisitiza jambo mbele ya wanahabari baada ya kupokea rambirambi kutoka kwa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Shillingi Milioni 8,550,000 ikiwa ni rambirambi kufuatia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere zilizowasilishwa na Mheshimiwa Alhaji Adam Kimbisa (kushoto) .Bunge la Jamahuri ya Muungano pia limetoa rambirambi yake kiasi cha Sh. milioni 86.

MICHUZI TV LIVE: SHEREHE ZA KUMUAGA KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA MAGEREZA TANZANIA

JUKWAA LA MAARIFA NA TAARIFA ZA AFYA LAZINDULIWA NCHINI

$
0
0

Na Avila Kakingo,Globu ya jamii
JUKWAA la maarifa na taarifa za afya lazinduliwa na TanzMED jijini Dar es Salaam leo.

Jukwaa hilo litakuwa kwa mfumo wa application (programu ya simu) ya simu ya mkononi inayopatikana kwenye toleo la Android pekee pamoja na tovuti ya www.tanzmed.co.tz yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa na maarifa ya afya Tanzania na nchi mbalimbali wanaotumia lugha ya Kiswahili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwanzilishi mwenza wa Tanz MED Mkata Nyoni amesema lengo kuu la kuanzishwa programu hiyo ni kuhakikisha jamii inanufaika na ukuaji wa teknolojia na mtandao wa matumizi ya huduma ya simu kwa upatikanaji wa taarifa za afya popote walipo.

“Tumeamua kuanzisha mtandao huu ili kuhakikisha jamii wanakuwa na uelewa mpana wa maswala ya afya pamoja na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za afya hii ni juhudi za kuunga mkono Serikali ya viwanda kwa kuhakikisha kuwa na jamii ya watu wenye afya,"amesema.

Nyoni amesema katika Application hiyo ya jukwaa la TanzMED linawmwezesha mtumiaji kusoma makala za afya zilizoandikwa na madaktari bingwa, kusikiliza simulizi za makala za afya na kupata orodha ya vituo vya afya kama hospitali, maduka ya dawa na maabara kulingana na umbali ulipo.

 Pia amesema kuwa taarifa za chanjo kwa watoto, taarifa za kriniki na taarifa za watu wanaotumia bima za afya.

Ameongeza wanawezesha mwanamke na wasichana kufatilia taarifa za mwenendo wa siku zao za hedhi kwa kupokea ujumbe kwenye simu zao pale wanapokaribia siku zao

Huku ikimpa nafasi ya kumuunga mweza wake ambaye naye ataweza kufatilia siku za hedhi ili kuchukua maamuzi sahihi.

Ameeleza kuwa pia Application wanajamii hawataweza tena kusahau muda wa kunywa dawa na kwenda kriniki kwani TanzMED itawawakumbusha kwa kuwatumia ujumbe kwenye simu zao za mkononi.
 Moja ya wavumbuzi wa Application ya jukwaa la maarifa na afya, Mkata Nyoni akizungumza na waandishi wa habari leo alipotambulisha aplication ya TanzMED jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Saansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu.
Moja ya wavumbuzi wa Application ya jukwaa la maarifa na afya, Mkata Nyoni akionesha application ya TanzMED inavyopatikana kwenye simu ya mkononi leo katika uzinduzi jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Tume ya Saansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu (wapili Kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na vijana wavumbuzi waliovumbua Application ya Afya kwa jamii inayotumia simu za mkononi. kulia ni Moja ya wavumbuzi wa Application ya jukwaa la maarifa na afya, Mkata Nyoni, na kushoto ni Mkuu wa fedha na uendeshaji DTBi Makange Mramba.

MTENDAJI MKUU TIC ,BALOZI WA DENMARK NCHINI TANZANIA WAFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU UWEKEZAJI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)Geophrey Mwambe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Einar Jensen.

Miongoni mwa mambo ambayo wameyazungumza ni pamoja na wawekezaji wa nchini Denmak kuja kuwekeza Tanzania kwani kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Mwambe amesema Balozi Jensen amekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kufanyabiashara.

"Balozi Jensen ni rafiki mkubwa wa biashara na amekuwa akishiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya kiabiashara.Tumekuwa tukishirikiana na Balozi Jensen kuratibu za kuwezesha wafanyabiashara," amesema Mwambe.

Pia amesema Balozi Jensen katika kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanakuwa na soko la uhakika huku akieleza kwamba balozi amekuwa akihamasisha wawekezaji wa Denmark kuwekeza nchini Tanzania.

Mwambe amesema siku za karibuni amefanya mazungumzo na Balozi huyo na moja ya jambo ambalo wamelizungumza ni namna ya kusaidia katika mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea kufanywa na TIC.

"Balozi amekubali kuisaidia TIC katika mabadiliko ya kimfumo koutendaji.Kama nchi tumedhamiria kushindana kidunia.Tunakuza uwezo wa kuongeza ajira kwa Watanzania," amesema.

Pia wamekubaliana na Balozi Jensen katika kuandaa maeneo ya yaliyopimwa kwa ajili ya uwekezaji."Nchini kwetu hatuna tatizo la ardhi kwani ipo ya kutosha ila changamoto ipo kupata eneo ambalo limepimwa.

"Hivyo moja ya mipango yetu ni kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapimwa na mwekezaji anapohitaji eneo inakuwa rahisi kupata.Bolozi amekubali kisaidia katika upimaji wa maeneo," amefafanua.

Mwambe amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Denmark kuna kampuni kubwa za nchi hiyo ambazo zimejenga viwanda.

Pia amesema kupitia Balozi huyo Denmark kwa sasa kuna mchakato wa  mradi wa umeme wa upepo unaoendelea mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Balozi Jensen amesema nchi hizo mbili zimekuwa kwenye ushirikiano mkubwa kwa miaka 50 na kwamba nchi ya Denmark imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geophrey (kushoto) akizingumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelewa na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Einar Jensen. Balozi wa Denmark nchini Tanzania Einar Jensen akiwa ameshika kitabu kinachozungumzia uwekezaji akiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)Geophrey Mwambe leo jijini Dar es Salaam.

MKUU WA MKOA WA SONGWE AWASIHI WANANCHI KUJITOKEZA KUPIMA AFYA ZAO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela anaawalika wananchi wote katika uzinduzi wa Kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia ARV ijulikanayo kama "Furaha yangu Pima, Jitambue, Ishi, itakayofanyika kuanza Jumamosi tarehe 29 Septemba 2018, katika eneo la Shule ya Sekondari Nalyelye, Mji ndogo wa Mlowo mkoani Songwe..

Kampeni hii inaendeshwa na mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia mpango wa kitaifa wa kudhibiti UKIMWI NACP Kwa kushirikiana na shirika la MHRP - HJRMRI.

Kampeni inalenga kuhamasisha wananchi hususan wanaume kupima afya zao. Kwa sasa huduma za upimaji wa afya zinatolewa bure katika iliwa ni upimaji wa VVU, presha, kisukari, uzito na uchangiaji wa damu wa hiyari.

Wote mnakaribishwa.

TANZANIA YAPEWA TUZO YA KIMATAIFA YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA (NCD) DUNIANI.

$
0
0
SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepata Tuzo ya Kimataifa ya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) kama vile Kisukari, Shinikizo la Damu, Magonjwa ya Moyo na Saratani.

Tuzo hiyo ya Kimataifa, imekabidhiwa leo tarehe 27 Septemba, 2018 kwa Waziri ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu na Kikosi kazi maalumu cha Umoja wa Mataifa mahususi kwa kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (UN Interagency Task Force on the Prevention & Control of NCDs- UNIATF). Hii ni kutokana na juhudi za Wizara ya Afya za kupambana dhidi ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD), hususan kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.

Tuzo hiyo ya kimataifa ya mwaka 2018, imekabidhiwa kwenye mkutano wa wa viongozi wa juu wa Umoja wa Mataifa (United Nations High Level Meeting on NCDs) unaofanyika Mjini New York, Marekani.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tisa Duniani ambazo zimefanikiwa kupata tuzo hiyo ambayo imetolewa kwa mara ya kwanza katika ngazi ya Kiserikali Dunianii, na ilichaguliwa kupata tuzo hiyo baada ya mapendekezo yaliyoandikwa na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza vya Tanzania (TANCDA). Hii ni kutokana na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata habari ya namna ya kujikinga na magonjwa haya.

Timu ya UNIATF imeipongeza Tanzania kwa kuanzisha programu ya kuhamashisha jamii kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku.

“Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (NCD) ndiyo yanayoongoza duniani kwa sasa kwa kusababisha ulemavu na vifo vingi. Nchini Tanzania asilimia 34 ya Vifo vilivyorekodiwa Hospitali mwaka 2017 zimesababishwa na magonjwa haya. Isitoshe kupambana na NCD ni miongoni mwa mikakakati ya Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu (SDG) ya kupunguza kwa theluthi moja vifo vya mapema vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ifikapo mwaka 2030. Amesema Waziri Ummy.

Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ni magonjwa sugu au ya muda mrefu, ambayo hayawezi kuambukizwa kwa maana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Magonjwa haya yapo mengi nayo ni kama vile kisukari, saratani, shinikizo la damu na mishipa ya fahamu, magonjwa sugu ya mfumo wa hewa, magonjwa sugu ya figo, macho na meno, selimundu (siko seli) na mengineyo.

Waziri Ummy amelishukuru Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza la Tanzania (TANCDA) baada ya kuandika andiko la kuitambulisha Dunia kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, na dunia kuona umuhimu wa juhudi hizo.

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na TANCDA na wadau wengine inaamini mikakati madhubuti, Sera mbalimbali za afya zikiwekwa, kutekelezwa na kuhakikisha Watanzania wanakuwa na elimu sahihi ya kujikinga na kuyadhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, itaboresha afya ya wananchi.

Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Afya).
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akipokea tuzo ya Kimataifa ya kupambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Duniani toka kwa Makamu Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Dkt.Soumya Swaminatha Mjini New York,Marekani

TTCL YATOA POLE YA MILIONI 25 MAAFA YA KIVUKO CHA MV NYERERE

$
0
0


Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) limetoa mchango wa pole ya shilingi Milioni 25 kusaidia katika maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea wiki iliyopita Kisiwani Ukerewe, Mkoa wa Mwanza. Pichani kulia ni Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Bw. Jalili Bakari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Tanzania, Ndugu Waziri Kindamba akikabidhi nakala ya hundi ya malipo hayo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akishuhudia.
Meneja wa TTCL Mkoa wa Mwanza, Bw. Jalili Bakari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Tanzania, Ndugu Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya kukabidhi nakala ya hundi ya malipo ya mchango wa pole ya shilingi Milioni 25 iliyotolewa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) ikiwa ni pole yao kwa maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere iliyotokea hivi karibuni kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela katikati akishukuru mara baada ya kupokea pole hiyo ya shilingi Milioni 25 kusaidia katika maafa ya ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere.

Bondia Amos Mwamakula kuzichapa na Mmalawi Oktoba 27

$
0
0
Pambano la kumaliza utata dhidi ya mabondia wawili nguli Africa, Amos Mwamakula wa Tanzania vs Ogdson Kayuni wa Maliwi la kuwania ubingwa wa UBO International, tarehe 27/10/2018 PTA saba saba. Mwamakula anaomba watanzania wengi wajitokeze kuweza kumshangilia kuweza kufanikisha kutwaa ubingwa wa dunia huo.

TADB yaendelea kuchagiza mapinduzi ya kilimo katika Skimu ya Umwagiliaji Mombo Tanga

$
0
0
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) imeahidi kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuwapatia mitaji itayowawezesha kununua zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP 2).

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa skimu hiyo, Katibu wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo, Bwana Sufian Mohamed aliishukuru serikali kupitia Benki ya Maaendeleo ya kilimo kwa kuwapatia mkopo wa gharama nafuu ambao umeweza kuwanufaisha jumla ya wakulima 429 kati yao wanawake wakiwa asilimia 54, mkopo ambao umeboresha miundo mbinu ya skimu hiyo hali iliyowezesha kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 1.9 hadi kufikia tani 6 kwa hekta moja.

Skimu hiyo ya Mombo mpaka sasa imenufaika na mkopo wa mbolea, mbegu bora pamoja na trekta, mashine ya kuvunia na sasa Benki ya Kilimo ipo katika hatua ya mwisho ya kuwapatia mashine ya kukobolea mchele ili waweze kuongeza thamani ya zao la mpunga katika skimu hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, wakati wa yeye na timu yake walipofanya ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji unaotekelezwa na skimu hiyo.

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akioneshwa mfuko utakaotumika kufungashia mchele unaozalishwa na Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo. Skimu hii imeweshwa kwa mkopo unaotolewa na TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (aliyenyanyua mkono) akipata maelezo ya maendeleo ya matrekta na mashine ya kuvunia walizozitoa kama mkopo kwa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga.

SEHEMU YA VIVUTIO KATIKA ZIWA VICTORIA

$
0
0


Mwalo wa kijiji cha Igombe wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umepambwa na mitumbwi ya wavuvi wa samaki katika ziwa Victoria hivi karibuni. Eneo hilo ni marufu kwa uvuvi na uuzaji samaki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kisiwa cha Makobe kilichopo kwenye ziwa Victoria kati ya wilaya ya Ilemela na Ukerewe mkoani Mwanza ni moja kati visiwa vingi vilivyopo katika ziawa hilo vyenye makazi ya wavuvi. Picha hii imepigwa hivi karibuni.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DIRA YA KITAA : IMEBAINIKA..!!, TOFAUTI YA CHOO NA TOILET..

SERIKALI YAANZA KULIPA MADAI YA MAREJESHO YA VAT YA WAFANYABIASHARA NCHINI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Tanga
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na wafanyabiashara mkoani Tanga na kuwaeleza kuwa Serikali imeanza kulipa  madai ya marejesho ya kodi ya Ongezeko la thamani (VAT Refund) kwa kampuni na wafanyabiashara mbalimbali nchini wakiwemo waagizaji wa sukari za viwandani ambao madai yao yamehakikiwa kuanzia mwezi huu wa Septemba, 2018.

Kauli hiyo ya Serikali inafuatia maombi ya wafanyabiashara wa mkoa huo walioitaka Serikali kuwalipa wafanyabiashara wanaodai kurejeshewa fedha zao zinazotokana na kufanya biashara zao nje ya nchi pamoja na  wazabuni mbalimbali.

Waziri Mpango amesema kuchelewa kulipwa kwa madai hayo kunatokana na kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu hivyo kutaka kuingizia Serikali hasara kwa kulipa madai hewa. ‘Kuna baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu, mfano tulipofanya uhakiki tuligundua madai hewa ya pembejeo ya zaidi ya Shilingi bilioni 87’, alisema Waziri Mpango.

Dkt. Mpango aliwahakikishia wafanyabiashara wote nchini kuwa serikali itahakikisha inaweka mazingira mazuri ili kila mwananchi mwenye nia njema aweze kufanya biashara halali itakayomletea faida na serikali iweze kukusanya kodi bila ya kumuonea mtu. 

Awali Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Bw. Deogratias Ruhinda, alisema kuwa wafanyabiashara hasa wakulima wa zao la Mkonge wanakutana na changamoto kubwa kutokana na serikali kuruhusu na kutoa msamaha wa baadhi ya kodi kwa wafanyabiashara wanaoingiza Kamba za manila hapa nchini, hivyo kulifanya zao la mkonge kutokuwa na soko hapa nchini kutokana na bei ya Kamba hizo za nje kuwa chini ukilinganisha na Kamba zinazotokana na mkonge.

Aidha wafanyabiashara hao waliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza kina cha Bandari ya Tanga ili meli kubwa ziweze kuja katika bandari hiyo na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kwenda nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo bidhaa nyingi kutoka Tanga zinasafirishwa kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam au Mombasa jambo linalowaongezea gharama kubwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga.

Akijibu hoja mbalimbali za wafanyabiashara hao, Dkt. Philip Mpango, aliwahakikishia kuwa Serikali itazipitia na kuzitolea ufafanuzi kero zote zinazohusu kodi ili kurahisisha biashara na kuweka mahusiano mazuri kati ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania, hali ambayo itaongeza mapato kwa serikali. Pia amesema Serikali inalifanyia kazi suala la wingi wa kodi anazolipa mfanyabiashara kwa Taasisi mbalimbali za serikali ili kodi hizo ziweze kutozwa sehemu moja  na kupunguza adha wanazopata walipa kodi.

Waziri Mpango aliwataka wafanyabiashara hao kutosita kuishauri serikali njia bora ya kukusanya kodi na kutoa maoni yao jinsi ya tozo mbalimbali zinazotozwa na serikali kwa kuiandikia Mamalaka ya Mapato Tanzania au Wizara ya Fedha na Mipngo ili serikali iweze kuboresha maeneo yenye mapungufu kwa faida ya Taifa. Pia Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara kote nhini kushiriki katika mikutano ya sera za kodi inayondaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ambayo huanza mwezi Disemba hadi Januari kila Mwaka.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb), akiongea na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga alipokutana na wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kusikiliza maoni na changamoto zinazowakabili katika masuala ya kodi. 
 Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara hao Jijini Tanga kuhusu kuimarisha ushirikiano kati yao na Serikali ili kuliletea maendeleo Taifa.
 Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh.Thobias Mwilapwa akiwahutubia wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kabla ya Kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kuzungumza na wafanyabiashara hao  katika Mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
 Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), (waliokaa mbele) wakiwa katika mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

UTOAJI HATI MILIKI ZA ARDHI TANZANIA WAONGEZEKA KWA KASI- MABULA

$
0
0

Na Munir Shemweta, Dodoma 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema kasi ya utoaji hati za umiliki wa ardhi na makazi imeongezeka kwa kasi ambapo hadi kufikia septemba mwaka huu 2018 jumla ya hati 25,463 zimeandaliwa.


Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa uwasilishwaji matokeo ya utafiti kuhusu haki na usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi jijini Dar es salaam leo Mabula alisema jumla ya hati 17,680 zilikuwa zimewasilishwa ofisi za kanda kwa ajili ya usajili na hati 9,739 zimeshakamilika.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na Wizara yake katika kutoa hati lakini takwimu zinaonesha kuwa hati nyingine zimeandaliwa katika halmashauri lakini zilizowasilishwa kwenye ofisi za kanda husika ni chache kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuandalia hati.


Kwa mujibu wa Mabula, kuna hati nyingi zinaonekana kuwasilishwa ofisi za kanda lakini hati zilizokamilika ni chache kutokana na hati nyingi zilizowasilishwa katika ofisi za kanda kuwa na upungufu mbalimbali na hivyo kusababisha hati hizo kutokamilika kwa wakati.


Akigeukia suala la haki na usalama na umiliki wa rasilimali ardhi na makazi kwa wananchi waishio vijijini, Mabula alisema hadi kufikia Mei 2018 jumla ya vipande vya ardhi 96,257 vimepimwa katika vijiji 91 na hati za kimila 20,583 zimeandaliwa na vijiji 20 vimeandaliwa na mipango ya makazi ambapo jumla ya viwanja 18,224 vimepimwa kwa ajili ya kuandaliwa hati ya haki miliki ya kimila.


Kwa mwaka 2018/2019 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imejipanga kuandaa hati za kimila 120,000, mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 30 na mpango wa kina kupima viwanja 20,000 kwa lengo kumuwezesha mwananchi wa kawaida kuwa na uhakika na usalama ya miliki yake na kuepusha migogoro.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akionesha Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania mara baada ya kuizindua, kushoto ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula
akimkabidhi Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati Ezekiel Kitilya mara baada ya kuizindua ripoti hiyo.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akimkabidhi Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Frank Mvungi Ripoti ya Utafiti kuhusu Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania.

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images