Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Serikali yatumia Bilioni 5.6 Kuiwezesha Taasisi ya MOI Kuwa na MRI,CT SCAN, X- ray na Ultra Sound

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile leo ametembelea na kukagua hali ya utoaji wa huduma katika baadhi ya vitengo katika Taasisi ya MOI na kukagua usimikaji wa mitambo ya kisasa katika kitengo cha radiolojia yenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 5.6 .

"Lengo la ziara yangu ni kukagua maendeleo ya usimikaji wa mitambo hii ya kisasa ya MRI, CT SCAN, X-ray, Ultra sound, nimeona na kujiridhisha imekamilika kwa asilimia 99% . Naomba niwaelekeze mkamilishe mambo machache yaliyobaki ndani ya wiki hii ili wiki ijayo wagonjwa waanze kupata huduma hapa". Alisema Dkt Ndugulile.

Pia, Dkt Ndugulule ametembelea vitengo vya mazoezi tiba pamoja na utengenezaji wa viungo bandia ambapo amekagua na kujiaonea hali ya utoaji huduma na kujiridhisha kwamba huduma zimeboreka katika kipindi cha miaka 3 ya Serikali ya awamu ya tano na kwa sasa watanzania wanapata huduma kwa wakati ijapokuwa kuna changamoto chache ambazo Serikali inazishughulikia.

Aidha, Dkt Ndugulile ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuhakikisha usimikaji wa Mitambao unafanyika kwa wakati na hali ya utoaji huduma ni nzuri na ya kuridhisha kwani wagonjwa wamekuwa wakipata changamoto ya kwenda nje ya MOI kufuata vipimo hivyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja ya machine mpya ya X-ray ya kisasa ambayo iko tayari kutumika. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akipata maelezo ya hatua iliyofikiwa katika usimikaji wa mashine ya CT Scan, wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt Respicious Boniface pamoja na viongozi waandamizi wa taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile Dkt Ndugulile akimjulia hali mtoto anayepata Huduma katika Taasisi ya MOI
Mtaalamu wa viungo bandia wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bw. Deus David akitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile kuhusu namna viungo bandia vinavyotengenezwa na kufanya kazi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na moja ya mgonjwa ambaye anatengenezewa kiungo bandia MOI ili kubainisha changamoto zilizopo zinazomkabili mgonjwa huyo.(Picha zote na MOI).


VIONGOZI WA KIJIJI WAFUNGA OFISI, WATIMKA. KISA OPERESHENI YA BHANGI

$
0
0
 Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha 
 Wananchi wa kijiji cha Kisimiri Juu Kilichopo tarafa ya King’ori wilayani Arumeru walikiacha kijiji chao kwa muda huku viongozi wao wakifunga ofisi zao na kukimbia kisa operesheni ya bhangi iliyofanywa na vikosi vya Jeshi la Polisi Alfajiri leo hii. 
 Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba walitapata taarifa kwamba kuna kiasi kikubwa cha bhangi kinatarajia kusafirishwa siku ya leo ndipo walipoandaa askari hao ambao walifanikiwa kufika eneo la tukio na kupata jumla ya magunia 27 yenye uzito wa Kilogramu 25 kila gunia shambani kwa mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa pamoja na Misokoto 583 ya Bhangi. 
Kamanda Ng’anzi alisema kwamba kwa sasa Jeshi la Polisi mkoani hapa linawatafuta viongozi wa kijiji cha Kisimiri Juu kwa kukiuka agizo la Serikali linalomtaka kila kiongozi katika eneo lake ahakikishe kwamba halilimwi bhangi. 
 “Tunaendelea kuwatafuta viongozi wa kijiji pamoja na kamati zake za ulinzi na usalama na mkondo wa sheria utachukua nafasi kwani wao kama viongozi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha katika eneo lao hakuna biashara yoyote ya Madawa ya kulevya inayofanyika”. Alifafanua Kamanda Ng’anzi. 
 Kamanda Ng’anzi alisema kwamba Jeshi hilo mkoani hapa lipo makini na litaendelea na mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali na kubainisha kwamba katika eneo la mpaka wa Namanga matukio ya uingizaji wa madawa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa. 
 Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni wa Jeshi hilo mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Elias Mwita alisema kwamba operesheni hiyo sio ya kwanza kufanyika katika eneo hilo na itakuwa endelevu kuhakikisha kwamba zao hilo haliendelei kulimwa. 
Pia si mara ya kwanza kwa viongozi pamoja na wananchi hao kutotoa ushirikiano kwa Jeshi hilo pamoja na vyombo vingine vya usalama pindi wanapofanya operesheni ya bhangi katika eneo hilo ambapo huwa wanaacha makazi yao na kukimbilia milimani.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng'anzi
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakihesabu misokoto ya Bhangi iliyopatikana katika moja ya nyumba ya wakazi wa kijiji hicho katika operesheni iliyofanyika katika kijiji cha Kisimiri Juu kilichopo tarafa ya King'ori wilayani Arumeru.
Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Elias Mwita akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto ya bhangi iliyopatikana katika operesheni hiyo

WAZIRI MKUU MAJALIWA: WANAJIOSAYANSI MNA WAJIBU WA KULINDA MADINI YETU

$
0
0
*Ataka waisaidie Serikali kubaini vyanzo vya maji vya uhakika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wanajiosayansi nchini wawe walinzi wa kwanza wa rasilmali za madini, maji na mafuta bila kujali wako serikalini au kwenye sekta binafsi.

“Katika utendaji wenu wa kazi, mnapaswa kuwa wa kwanza kujua kinachoendelea katika sekta zote mnazohusiana nazo, yaani madini, maji na mafuta. Haijalishi unafanya kazi serikalini au shirika binafsi, wewe ni Mtanzania na una jukumu la kulinda rasilimali za nchi yako.” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Septemba 27, 2018), wakati akifungua warsha ya siku sita ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania iliyoanza leo kwenye hoteli ya New Dodoma, jijini Dodoma.

Waziri Mkuu ambaye amefungua warsha hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka wanajiosayansi hao kutoka Serikalini, taasisi binafsi na vyuo vya elimu ya juu wasishiriki kulihujumu Taifa kwani kwa kufanya hivyo, watakuwa wasaliti namba moja.

“Msijihusishe au kushiriki kulihujumu Taifa lenu kwani kwa kufanya hivyo, mtakuwa wasaliti namba moja. Hakikisheni mnakuwa mabalozi wa Serikali katika mashirika haya kwa kutoa elimu juu ya sheria zinazosimamia sekta hizi huku mkisisitiza umuhimu wa kufuata sheria za nchi zenye kusimamia rasilimali zetu adhimu,” amesema.

Amesema mbali ya kilimo, rasilmali miamba na madini ndivyo vyenye mchango mkubwa wa kukuza viwanda kote duniani na kwamba utaalamu wa jiosayansi una mchango mkubwa kwenye malighafi za viwandani, upatikanaji wa maji ya kutosha nchini, mafuta, gesi asilia na uzalishaji wa nishati kupitia jotoardhi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wanajiosayansi hao waisaidie Serikali kutafuta vyanzo vya maji vya uhakika ili itumie kihalali fedha zinazotengwa kwenye uchimbaji visima vya maji na kuepuka upotevu wa fedha.

“Ni jukumu la wanajiolojia la kutuambia wapi maji yapatikana. Muandae utaratibu mzuri wa kutunza takwimu kuhusu kiwango cha maji, ni wapi maji yalipo na ujazo wake. Kwenye eneo hili tumepoteza fedha nyingi sana, tumepeleka fedha nyingi kwenye halmashauri ili tutoe huduma za maji wananchi lakini kwa sababu hatukuwashirikisha wanajiosayansi, wachimbaji wameenda kuchimba visima na wakakosa maji, yakabaki mashimo tu bila maji. Mna jukumu kubwa la kuisadia Serikali ili itumie vizuri fedha inazozitenga kwa ajili ya maji kwa kubainisha wapi kuna maji, yako kiasi gani na yako umbali gani,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri wa Madini, Bibi Angella Kairuki amesema wizara hiyo inakusudia kuanzisha chombo maalum cha usajili cha kuwatambua wanajiosayansi kisheria kupitia Bodi ya Usajili wa Wanajiosayansi nchini (Geoscientists Registration Board -GRB) kama ilivyo kwa wahasibu, wahandisi na mabaraza ya wasajili mbalimbali ili kukabiliana na wataalamu feki wa fani hiyo.

“Wizara ya Madini inategemea wanajiosayansi wawe wazalendo kwa Taifa kwa kutoa taarifa za kitaalamu zinazoendama na uhalisia ili kuondoa malalamiko yanayotokana na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu hasa wale wanaojifanya wataalamu ilhali wakijua wazi hawana utaalamu wa fani hii,” amesema.

Amesema azma ya Serikali ni kumaliza changamoto zinazoikabili sekta hiyo ya madini zikiwemo ukiritimba uliokuwa ukifanyika katika mlolongo mzima wa utoaji leseni, utafutaji na uzalishaji wa rasilmali madini.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa mwananjiolojia, Batwenge Chakutema kuhusu vifaa mbaIimbali vinavyotumika katika utafiti na upimaji madini wakati alipofungua Warsha  ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akifungua Warsha   ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia zawadi ya kinyago cha njiwa wawili kilichotokana na jiwe  wakati  alifungua  Warsha  ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . Kushoto ni Waziri wa Nishati, Angela Kairuki na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas  Katambi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Warsha  ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania  (Tanzania  Geological Society - TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CCM YARIDHISHWA NA MAENDELEO UJENZI WA RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE)

tzegovernment: Serikali Mtandao ndani ya HESLB

HABARI KUTOKA UMOJA WA MATAIFA JIJINI NEW YORK, MAREKANI

Habari kamili ya Utandikaji wa Reli ya SGR wafikia zaidi ya kilomita 3

AIRTEL YAWEKEZA KATIKA MADUKA YA KUTOA HUDUMA NCHI NZIMA

$
0
0
KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Airtel, inaendelea na mpango wake wa kuboresha huduma zake, ambapo kwa sasa imekuja na mipango ya kufungua maduka yanayotoa huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni hatua ya kusogeza huduma hizo kwa wananchi.

Katika kutekeleza mpango huo, tayari Airtel imefungua maduka zaidi ya 400 katika maeneo mbalimbali Nchini na hivyo kusogezakaribu na wateja wake huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuma na kupokea pesa, kurudisha namba iliyopote, kuswap Sim Card na kununua vifurushi mbalimbali vya Airtel.

Akizungumzia mpango huo wa kufungua maduka na kutoa huduma kwa Mkoa wa dare s Salaam, Meneja wa Biashara Airtel Mkoa wa Dar es Salaam, Brighton Majwala amesema, miongoni mwa maduka yoa ya mkoa wa Dar es Salaam yamewezesha wateja wao kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi zaidi.

“Sisi Airtel, tumeamua kuanzisha maduka haya ili kusogeza karibu huduma zetu kwa lengo la kuwawezesha wananchi na wateja wetu kupata huduma hizo kwa urahisi na pia karibu na maeneo yao,”.amesema Majwala.

“Hata hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa mawakala wetu kuweza kupata huduma za Airtel Money na huduma nyingine bila kutembea umbali mrefu kuzifuata kama ilivyokuwa hapo awali”. ameongeza.Kwa upande wao baadhi ya wateja na mawakala wa wa Kampuni hiyo, wameeleza namna ambavyo wananufaika na huduma zinazotolewa na maduka hayo ya Airtel katika maeneo yao.

“sisi wateja, tunafurahia huduma hizi kusogezwa karibu na maeneo yetu kwani inaturahisishia kupata huduma na kuokoa muda ambao tungeutumia kufuata huduma hizo maeneo mengine ya mbali na hapa” walieleza wateja hao.“Mawakala wengi wa hapa maeneo ya Tangi Bovu tunanufaika sana na uwepo wa Duka hili la Airtel katika maeneo yetu kwani kwa sasa tuweza kumuhudumia mteja kiasi chochote cha Airtel Money bila kuhangaika kufuata floti maneo ya mbali” aliongeza wakala Elizabeth Madeje

Kufunguliwa kwa maduka hayo katika maeneo ya karibu na wananchi, kumeelezwa kuwasaidia wananchi na wateja wa Airtel kupata huduma za kampuni hiyo kwa urahisi na hivyo kuokoa fedha na muda wa kufuata huduma hizo maeneo ya mbali.

Mkuu Wa mauzo wa Airtel Dar es salaam, Bryton Majwala akiongea na baadhi ya wateja wakati wa kuzindua moja kati ya maduka madogo madogo ya Airtel maarufu kama Airtel Money Branch mkoani Dar es salaam Mbezi Tangi bovu ambapo zaidi ya maduka 400 yameshafunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini. Anaehudumia wateja ni Afisa huduma kwa wateja wa duka hilo la Airtel Money Branch Tangi Bovu Bw, Thobias Bango. Duka hilo la Airtel limezindualia rasmi jana na Airtel ambapo litatoa huduma zote za Airtel kama vile kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea na kuharibika, pamoja na kusajili laini mpya kwa wateja wapya
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Branch ya Mbezi Tangi Bovu bw, Thobiasi Bango akitoa huduma ya kusajili laini mpya kwa wateja wa kwanza kwenye duka hilo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo, Duka hilo la Airtel Money Branch Mbezi Tangibovu ni moja kati ya maduka 400 yaliyofunguliwa nchini na Airtel ikiwa ni mkakati wake wa kufikisha huduma zao kila mahali, huduma zinazotolewa ni pamoja na le kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea na kuharibika, pamoja na kusajili laini mpya kwa wateja wapya

Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando ( wakwanza kulia) pamoja na msimamizi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel Money Branch la Mbezi Tangi Bovu Thobias Bango wakisajili laini ya mteja wa kwanza Bi Elizabeth Gundula mara baada ya uzinduzi wa duka hilo jana. Duka la Airtel Money Branch Mbezi Tangibovu ni moja kati ni ya mikakati wa Airtel wa kufikisha huduma kila mahali, katika maduka hayo mteja ataweza kuweka na kutoa pesa –Airtel Money, kurejesha laini iliopotea au kuharibika au kusajili laini mpya kwa wateja wapya.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 18 YA KIFO CHA MAREHEMU JOHN MGEJA

$
0
0
Leo ni miaka 18 tangu ulipotuacha ghafla Mpendwa Baba yetu....
Unakumbukwa kwa upendo wako wa dhati na Mke Wako Mpendwa RUTH NKIYA MGEJA, Wanao LOUIS MANGALA MGEJA, MUSSA MWANDU MGEJA, FRANK JOHN MGEJA, MARC MIPAWA MGEJA pamoja na EDGER NKONOKI MGEJA.
 Unakumbukwa pia na Kaka, Dada pamoja na Ndugu na jamaa zako wote uliopata kuwa karibu nao katika  uhai wako. 
Upumzike kwa Amani Baba Yetu. Bado unaishi ndani ya mioyo yetu hata sasa.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 27.08.2018

Introducing "KATIKA" by Navy Kenzo feat. Diamond Platnumz (Official video)

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 28, 2018

Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018

$
0
0
Na. VERO IGNATUS, ARUSHA

Ni septemba 29/2018 ni siku ua  kuanza rasmi ligi daraja la kwanza msimu wa kwanza  wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya Mkoa huo ya Arusha United Wanautalii siku ya tarehe 29 wakati timu hiyo itakapomenyana na Rhino Rangers Fc ya Tabora.

Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar akizungumza na waandishi wa habari  katika uwanja wa Shekh Amri Abeid  amesema anatarajia wana Arusha watajitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuishangilia timu hiyo ambayo kwa sasa inarudisha Mkoa huo  katika ramani ya soka nchini ambayo imepotea kwa muda mrefu.

Jamillah amesema kikosi cha timu ya Arusha United  wanautalii kimedhamiria  kuingia ligi kuu mwakani kutokana na kuwa na kikosi imara chini ya kocha mkuu Felix Minziro  ambae anahistoria safi katika soka nchini.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji  wa timu ya Arusha United wana utalii Fikiri Elias amesema timu yake imejiandaa vyema kukabiliana na timu ya Rhino Rangers Fc kutoka Tabora na wauhakika na ushindi wa point tatu.

Kwa mara ya kwanza tangu ipate usajili timu ya Arusha United wana utalii itajitupa uwanjani rasmi kuanza kushiriki ligi daraja la kwanza mwaka huu ikiwa katika safari yake ya kuelekea ligi kuu mwakani.
 Kikosi cha timu ya Arusha United  wanautalii kama wanavyoonekana pichani. 
Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar

KIVUKO CHA MV.NYERERE KILICHOUA WATU 226 BAADA YA KUPINDUKA KIMEWEKWA SAWA,SASA KUVUTWA MWALONI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI WA Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema wamefanikiwa kukipindua kivuko cha MV.Nyerere na kukiweka sawa.

Kivuko hicho kilipinduka na kuzama katika ziwa Victoria  Septemba 20 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 226 huku watu 41 wakipatikana wakiwa hai.

Akizungumza jioni hii kuhusu kivuko hicho Waziri Kamwelwe amesema hatimaye leo wamefanikiwa kukiweka sawa na kazi ambayo imebakia ni kukovuta ili kiwe mwaloni kwa ajili ya kuendelea na hatua iliyobakia."Tunashukuru makundi yote kwa namna ambavyo wamefanikisha kukiweka sawa kivuko hiki ambacho kilipinduka na kusababisha maafa ya Watanzania wenzetu.

"Zaidi ya watu 570 wameshiriki katika kufanikisha kivuko hicho tunakipindua baada ya kupinduka.Tunawashukuru wananchi wa Ukara kwa namna ambavyo wameshiriki katika kuokoa maisha ya watu 40,"amesema Waziri Kamwelwe.

Ameongeza kuwa kivuko hicho ambacho kimewekwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa TanzaniaVenance Mabeyo ataelezea hatua ambayo inafuata baada ya kukamilisha hatua ya kwanza.Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Venance Mabeyo amesema baada ya hatua ya kukisimamisha kivuko hicho kwa asilimia 85, kazi iliyobaki sasa ni kuondoa maji ambayo yamejaa ndani ya kivuko hicho.

" Kwa sasa tumefanikiwa kwa asilimia 85 kwani bado kuna hatua ambayo inafuata ya kuondoa maji,"amesema.Amefafanua baada ya kukipindua kivuko hicho na kisha kutoa maji watakivuta  Mwaloni kwa ajili ya kuanza kufanyiwa matengenezo.Amesema pia watahakikisha wanasafisha eneo hilo ili kuangalia kama kuna chochote ambacho kimebakia na lengo ni kuacha eneo hilo likiwa salama."Tunataka wananchi Ukara wasiwe na hofu baada ya kukamilisha shughuli za kuondoa kivuko hicho kilipo na kukiweka Mwaloni," amesema Mabeyo.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  John Mongella amesema msiba huo ulikuwa ni wa kitaifa licha ya kwamba limetokea mkoani Mwanza katika Wilaya ya Ukerewe katika eneo la Ukara.Amesema kuwa baada kikupindua kivuko hicho kwa sasa ni kuendelea kutoa maji yaliyomo.Amesema kuwa baada ya kutokea ajali hiyo Rais Dk.John Magufuli alikuwa akiwasiliana naye kwani alihakikisha anapata taarifa kwa kila kinachoendelea.

"Saa moja baada ya ajali hiyo kutokea Rais Magufuli alinipigia simu na kutoa maelekezo, pia nikapigiwa simu na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa." Tunashukuru kwa ushirikiano ambao umeoneshwa baada ya kutokea ajali hii kwani Watanzania wote wameonesha kuguswa na ajali hii mbaya.Tuendelee kishikamana na ukweli tukio hili limetufundisha jambo kubwa,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.

Ametoa shukrani kwa makundi mbalimbali ambayo yameshiriki kikamilifu katika msiba huo ambapo pongezi hizo amezielekeza pia kwa vyombo vya habari kwa namna ambavyo wametoa taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea.

RC HAPI ABAINI MADUDU MANISPAA YA IRINGA

$
0
0

Udhaifu, upigaji kwenye miradi inayosimamiwa na manispaa vyabainika,
Migogoro ya ardhi Kihesa yateka mkutano.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amefichua madudu katika miradi ya machinjio mapya ya Ngelewala yaliyojengwa na fedha za serikali kwa milioni 900 takribani miaka 9 bila kukamilika huku manispaa wakihitaji shilingi bilioni 1.3 ili kukamilisha.

Tukio hilo limetokea jana wakati alipotembelea machinjio hayo ambapo kwenye taarifa iliyosomwa na afisa mifugo imetoa maombi kwa serikali kuwaongezea shilingi bilioni 1.3 kukamilisha machinjio hayo huku fedha za awali shilingi milioni 928 zimetumika machinjioni hapo bila kukamilika mpaka sasa.

Mkuu huyo wa mkoa akanusa harufu ya upigaji baada ya kuomba BOQ kutoka kwa mhandisi wa halmashauri manispaa ya Iringa Michael Sakala na kuikosa hivyo kuagiza uchunguzi kufanyika kwa mradi huo wa machinjio na endapo itabainika yeyote amehusika kwenye upugaji wa mradi huo basi achukuliwe hatua.

Aidha mkurugenzi Mpya wa manispaa Iringa ameeleza mbele ya RC kuwa naye alishtushwa na Fedha hizo zinazoombwa wakati kwa tathmini Mpya waliyofanya wamebaini kuwa ikipatikana shilingi milioni 300 hadi 400 tu machinjio hayo yataanza kufanya kazi na kuingiza mapato.

Katika hospitali ya Frelimo, mkuu wa mkoa amezindua jengo la kufulia nguo na kukausha pamoja na mashine mbili za kufulia kwenye hospitali ya Frelimo lililojengwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Iringa lenye thamani ya shilingi milioni 32 na kuwapongeza kwa hatua hiyo ya kuisaidia jamii yake hivyo kujenga mahusiano mazuri.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akizungumza na wananchi wa mkoa huo jana tarehe 27 Septemba 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akihutubia mamia ya wananchi wa Kihesa waliojitokeza katika mkutano wa hadhara hapo jana. 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara katika Machinjio ya Ngelewala wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wake jana tarehe 27 Septemba 2018. 



WABUNGE WAALIKWA NA BUNGE LA CHINA KUSHIRIKI SEMINA YAKUJENGEWA UWEZO

$
0
0

Kushoto katika picha ni Mheshimiwa Maida Abdallah, akifuatiwa na Mheshimiwa Munira Khatib, Mheshimiwa Kiza Mayeye, Mheshimiwa Joram Hongoli na mwisho kulia ni Mheshimiwa Fredy Mwakibete.
Mheshimiwa Kiza Mayeye akichangia mada katika semina hiyo. Semina hiyo iliwakilishwa na nchi saba za bara la Afrika na Asia.
Mheshimiwa Fredy Mwakibete ambaye ndiye Mwenyekiti wa Msafara huo wa wabunge akitoa neon la shukrani baada ya kumalizika kwa semina hiyo. Semina ilikuwa inahusu kupeana mikakati mbalimbali ya kuweza kufanikisha malengo 17 ya millennia. Wabunge walipata kujifunza kutoka China ambao wamekuwa mara zote walitimiza malengo ya millennia kwa wakati.

MASHIRIKA YATAKIWA KUHUDUMIA JAMII KWA KURUDISHA FAIDA WANAYOPATA

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud ,Arusha

Taasisi na mashirika mbali mbali hapa nchini yametakiwa kurudisha sehemu ya faida wanayo ipata ili kuhudumia Huduma za kijamii zikiwemo Mausala ya afya elimu na watoto wasiojiweza Sanjari na maafa mbali mbali

Akizungumza wakati akitoa msaada kwenye shule ya Msingi na ufundi Sing’isi wilayani Arumeru mkoani Arusha mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani amesema kwamba katika faida wanayo ipata watakikisha wanaendelea kusaidia sekta ya elimu nchini

Aidha ameyataka mashirika mbali mbali kuona namna ya kurudisha faida wanayopta katika kuhudumia masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo kusaidiana na serikali katika hatua mbali mbali za kuwaleta maendeleo wananchi hususani benki hiyo ilipokuwa ikikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 4 katika shule ya msingi na ufundi ya Sing’isi 

Amezitaka taasisi mbali mbali kujitokeza katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya ,kutoa elimu bure na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya awali bila kuwepo na changamoto ya madarasa pamoja na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya kusoma na kufundishia

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Singisi Safira Ndelwa ametaja changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya majengo katika shule hiyo ikiwemo uhaba wa vyumba vya kusomea na uzio wa shule.‘’Shule hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uzio uhaba wa vyumba vya madarasa mashine ya kuchapisha mitihani pamoja na nyumba za walimu ‘’alisema mwalimu Ndelwa

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Anjela Izack ameshukuru benki hiyo kwa msaada huo na kuomba kuongezewa madarasa mawili kwa lengo la kuondoa usumbufu wa wanafunzi wenzake kusoma kwa awamu mbili kwani wanachoka na masomo yao na kujikuta wakishindwa kushika masomo na maendeleo kushuka.
Sehemu ya Wanafunzi wa shule ya msingi na ufundi Sing'isi wakiwa na mfano wa hundi waliokabidhiwa na benki ya CBA jana wilayani Arumeru 
Pichani ni Mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani akiwa na mwalim mkuu wa shule ya ufundi na msingi Sing'isi Safira Ndelwa wakati wa makabidhiano ya Hundi kutoka Benki ya CBA picha zote na mahamoud ahamd Meru

NMB SASA KUSAIDIA KILIMO CHA MICHIKICHI MKOANI KIGOMA

$
0
0
BENKI ya NMB Plc imesema itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma.

Mpango huo ulielezwa jana na Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa mazungumzo mafupi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) unaoendelea jijini Dodoma.

Mponzi alisema kwa sasa NMB inawasaidia zaidi ya wakulima wadogo wadogo milioni moja nchi nzima, na kwamba benki itaendelea kutenga fedha za kutosha ili kusaidia wakulima wengi zaidi. “Kwa sasa, NMB imetenga zaidi ya shilingi billioni 500 kwa ajili ya kusaidia wakulima hapa nchini lengo likiwa kusaidia jitihada za serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda kupitia sekta ya kilimo.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu alisema kwa sasa Serikali inapeleka nguvu zake katika kukuza kilimo cha zao la mchikichi mkoani Kigoma, na hivyo akaitaka benki ya NMB kuisaidia Serikali katika kufanikisha azma hiyo kwa kuwasaidia wakulima wa michikichi mkoani humo.

“Tumekuwa tukiwashawishi wakulima mkoani Kigoma kujikita katika kilimo cha michikichi lakini kwa bahati mbaya wakulima wengi hawana mitaji ya kulima michikichi kwa wingi. Nitafurahi kama benki yenu kupitia mikakati yake itawawezesha wakulima wa michikichi,” alisema.

Aidha, Waziri Mkuu ameomba kukutana na uongozi wa benki ya NMB mapema wiki ijayo mkoani Kigoma ili kwa pamoja waweze kupanga mkakati kazi wa kuwasaidia wakulima mkoani humo kulima michikichi kwa ufanisi na wingi zaidi. 

Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB- Filbert Mponzi (kulia) akitoa maelezo ya huduma za kifedha zinazotolewa na benki hiyo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) alipotembelea Banda la Benki hiyo jana Jijini Dodoma kwenye monyesho ya Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT). Benki ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kufadhili mkutano huo, ikiwa ni kwa mwaka wa sita mfululizo sasa. Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi pamoja na Meneja Mwandamizi wa Biashara za Kilimo wa NMB -Isaac Masusu.
Mkuu wa Idara ya Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) wakati wa mkutano mkuu wa 34 wa jumuiya hiyo unaoendelea jijini Dodoma.KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

DKT NDUGULILE ATOA MWEZI MMOJA KWA UONGOZI TAASISI YA USTAWI WA JAMII KUTATUA CHANGAMOTO ZAKE

$
0
0
Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,Mh. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amefanya ziara katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikiwa ni miongoni mwa ziara ya kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake katika kuboresha utendaji kazi. 

Dkt Ndugulile jana Septemba 27,2018, pamoja na kufanya ziara  katika taasisi hiyo na kujionea mazingira halisi,pia alifanya mkutano na menejimenti, wafanyakazi pamoja na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii,ambapo pamoja na mambo mengine Mh Naibu Waziri alisomewa taarifa ya maendeleo ya taasisi na mipango ya baadae. 

“Nimeskia taarifa nzuri ya maendeleo na mafanikio pamoja na changamoto za Taasisi, nawaagiza viongozi kutatua changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wenu na sisi kama serikali tutazifanyia kazi zile zinazotuhusu. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa ubora na maslahi ya watumishi yanaboreshwa”. Alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Ndugulile ametoa maagizo kwa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii kufanyia kazi kwa muda mwezi mmoja tu,baadhi ya mambo ambayo ameona yanahitaji ufumbuzi wa mapema ili kuboresha mazingira ya utoaji huduma katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii. 

Katika kuhitimisha mkutano wake na uongozi, wafanyakazi pamoja na serikali ya wanafunzi wa Taasisi, Mh. Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amepongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi na ameahidi wao kama Wizara kuendelea kushirikiana na Taasisi ya Ustawi wa jamii katika kutoa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wananchi.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akisikiliza ripoti ya utendaji kazi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Zena Mabeyo.
 Wajumbe wa menejimenti ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakimsikiliza Mh. Naibu waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana nao Jana.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akizungumza na Watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Taasisi Ya Ustawi wa Jamii  Dkt Zena Mabeyo alipofika kutembelea Taasisi hiyo jana,jijini Dar Es Salaam.

Ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Habari, Septemba 28, 2018

$
0
0
Mapinduzi ya kiteknolojia yanabadilika kwa kiasi kikubwa jinsi tunavyojulisha wenyewe. Katika miaka michache tu, vyanzo vya habari vimeongezeka, vinachukuliwa kwenye muundo mbalimbali na kuwa wa kimataifa. Sasa inawezekana kupata mara moja utajiri wa vifaa kwenye mada mbalimbali.
Hali hii mpya inatoa fursa kubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na kijamii. Hata hivyo, maendeleo kama hayo yanaweza tu kuchukua nafasi kama fursa hizo zinapatikana kwa wote. Katika jumuiya ya kimataifa inayoingiliana sana, ukosefu wa upatikanaji sawa wa habari ni njia ya uhakika ya kuongeza marginalization na kutengwa kwa haraka kutoka kwa dunia nzima. Kusudi la siku hii ya kimataifa ni kuwakumbusha serikali na wadau wote katika mashirika ya kiraia ya haja ya kuhakikisha ufikiaji wa habari wa ulimwengu wote.
Utekelezaji wa haja hii ni sehemu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) ya 20 Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, ambayo inahitaji hatua ya "kuhakikisha ufikiaji wa umma kwa habari na kulinda uhuru wa msingi".
Upatikanaji wa habari unahusishwa moja kwa moja na kufurahia haki za msingi na uhuru na huathiri kufikia Malengo yote ya Maendeleo ya kudumisha.
Kuwa raia mwenye ujuzi ni maana ya kuwa na ujuzi, kuwa na akili kubwa, na kuwa na uwezo wa kucheza sehemu ya maisha na jamii.
Ina maana kuwa na upatikanaji wa maarifa muhimu kwa afya na ustawi wa mtu.
Ina maana kuwa na rasilimali za elimu ambazo zinawezesha kufurahia kujifunza maisha yote na kukabiliana na mazingira ya kiuchumi ya kijamii.
Ina maana kufungua uwezo wa ubunifu na ubunifu.
Pia inamaanisha kuwa na ufahamu wa changamoto kuu zinazokabili mwanadamu - kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, kwa mfano - na kujua jinsi ya kujibu ili kupunguza madhara yake.
Kufanya upatikanaji wa habari kwa ukweli ukweli unahitaji hatua kwa mipaka mbalimbali. Mataifa lazima kuendeleza sheria ya kutosha na kuhakikisha upatikanaji wa wote wa mtandao. Wanapaswa kuhimiza multilingualism mtandaoni na nje ya mtandao ili jumuiya zote ziweze kufikia ujuzi muhimu katika lugha zao za asili. Wanapaswa pia kufanya kazi ya kuifungua kugawanyika kwa digital, ambayo huelekea kuendeleza usawa wa kijamii na jinsia. Kupitia programu zake mbalimbali na kwa kufanya kazi pamoja na serikali, UNESCO inasaidia kupambana na usawa huu.
Hatimaye, upatikanaji wa habari ni bila shaka shaka inayohusu uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi wa habari. UNESCO inafanya kazi kwa bidii ili kuondoa vikwazo kwa vyombo vya habari vingi na vya bure ili raia wote waweze kufaidika na habari za uhakika, kuthibitishwa na ubora.
Ufahamu na jamii ya habari ambayo kwa sasa inachukua sura ina ahadi mkali. Katika Siku hii ya Kimataifa ya Ufikiaji wa Ulimwengu wa Universal, hebu tufanye kazi pamoja ili kuhakikisha kuwa ahadi hii inazaa matunda kwa wote.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images