Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MJUKUU WA MALKIA ELIZABETH II WA UINGEREZA PRINCE WILLIAM IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William aliyeambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William picha ya wanyama wanaopatikana katika mbuga mbalimbali nchini mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Kamusi ya Kiswahili mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Picha kutoka kwa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha hiyo inamuonesha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa anazungumza na Malkia wa Uingereza Elizabeth II.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

RC NDIKILO -AUNDA TUME NDOGO KUFUATILIA SAKATA LA MWENYEKITI WA DUTUMI KUKATALIWA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ameunda tume ndogo kufuatilia malalamiko ya baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Dutumi ,Kibaha, kumtaka mwenyekiti wao Mkali Kanusu ajiuzulu kwa kukiuka taratibu za uongozi.

Mwenyekiti huyo anadaiwa kufanya ubadhirifu wa fedha,kuuza maeneo ya kijiji,kugawa ardhi bila ya utaratibu,vitabu tisa kuibiwa,kugomea mkutano na kutosoma mapato na matumizi.

Ndikilo,  alifikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza pande zote mbili za mwenyekiti na wajumbe wa kijiji ambao walimpinga  kwenye kikao cha ndani na kikao cha nje cha wananchi.

"Tume hii itaenda kufanya kazi kwa muda wa wiki moja kisha itatupa majibu kama ajiuzulu ama aendelee na nafasi yake ili shughuli za maendeleo ziendelee ".

"Shughuli za maendeleo zimesimama kwa muda mrefu sasa ambapo barua za malalamiko zimefika hadi kwa Rais hivyo lazima suala hili lifikie mwisho," alisema Ndikilo.

Alisema baada ya barua ya walalamikaji iliandikwa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha ambaye alimwambia mtendaji amwandikie mwenyekiti ili ajibu tuhuma zinazomkabili ndani ya siku tisa kuanzia tarehe 19 hadi 29 awe amejibu.

"Hata hivyo hakujibu lakini vyombo mbalimbali vilianza kufuatilia suala hilo ambao ni Takukuru,ofisa utumishi,kamati ya ulinzi na usalama na mkaguzi wa ndani hata hivyo hakukubali wala kukanusha," alisema Ndikilo.

Mwenyekiti huyo ambae pia ni diwani wa Dutumi,  Mkali Kanusu alisema , tuhuma zote anazopewa hazina ukweli.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alielezea suala hilo linaenda kisiasa kwani hata watu waliomkubali walikuwa wengi.
 MKUU wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza huko kijiji cha Dutumi ,Kibaha.(
Baadhi ya wananchi Dutumi, Kibaha Vijijini, wakimsikiliza, mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi).

RAIS MAGUFULI AAGANA NA BALOZI WA JAPANI ANAYEMALIZA MUDA WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa wa Japan Masaharu Yoshida anayetarajia kumaliza muda wake wa kuiwakilisha Nchi ya Japan hapa Nchini mwisho wa mwezi Septemba 2018.Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa wa Japan Masaharu Yoshida anayetarajia kumaliza muda wake wa kuiwakilisha Nchi ya Japan hapa Nchini mwisho wa mwezi Septemba 2018.Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 

WANANCHI WA SOGA WAPO KIHALALI WASIBUGHUDHIWE NA MTU AMA MWEKEZAJI-MABULA

0
0
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula ,ameweka bayana kuwa wananchi wa kijiji cha Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani, wapo kihalali hivyo asitokee mtu kuwanyanyasa.

Alilazimika kutoa ufafanuzi huo, baada ya mwekezaji kudai wananchi hao wamevamia eneo hilo. 

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi hao ambapo walitoa malalamiko yao juu ya kunyanyaswa kwa madai ya kwamba eneo hilo wamelivamia.

Angeline  alisema , kijiji hicho kiko kihalali na kina usajili wa Pw/Kij/442 wa mwaka 1975 .

"Kijiji cha Soga kiko kihalali kinatambulika hivyo hatuwezi kuwahamisha kwakuwa na kama huyo mwekezaji Mohammed Enterprises amekikuta kijiji," alisema Angeline.

Aidha alisema tayari serikali imetangaza kwenye gazeti lake kwa namba 213 la tarehe 11/5/2018 kuwa eneo hilo ni la mipango miji.

Aliwataka wananchi kufuata utaratibu kwa mujibu wa sheria namba 8 ya 2007 ya mipango miji.

"Serikali iko kwenye mchakato wa kulifutia hati shamba hilo la (Mohamed Enterprises) ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu hivyo utaratibu utafuata ili kuligawa sehemu ibaki kwa kijiji na sehemu ya shamba," alifafanua.

Angeline alieleza, mwekezaji alianza kumiliki shamba hilo mwaka 1999 toka kwa mwekezaji mwingine na ikibainika mwekezaji kakiuka masharti litafutwa na kama hajakiuka apeleke utetezi wake.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alisema ,kwa mujibu wa taarifa wananchi hao wako katika eneo hilo kwa muda mrefu.

Mkazi wa Soga,  Subira Juma alisema, wamekuwa wakinyanyaswa huku wakiambiwa wao ni wavamizi na wanatakiwa kuondoka.
Naibu Waziri wa  wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula akizungumza ,huko Soga wakati alipokuwa kwenye ziara yake mjini Kibaha. 
(Picha na Mwamvua Mwinyi)

JUMLA YA VIWANDA 1,596 VIMEJENGWA NCHINI-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia Juni, 2018 jumla ya viwanda 1,596 vimejengwa ambapo ni sawa na asilimia 61.4 ya lengo la kujenga viwanda 2,600 hadi Desemba 31, 2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la ujenzi wa viwanda 100 katika kila mkoa.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 27, 2018) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete, jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu amesema kuwa viwanda hivyo vimejengwa kupitia agizo la Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI kwamba kila Mkoa ujenge viwanda 100.

Amesema tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa Serikali kuelekea uchumi wa viwanda, inaonesha kwamba mpaka sasa jumla ya hekta 367,077 zimetengwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya viwanda vikubwa, viwanda vya kati na viwanda vidogo. 

“Nitoe wito kwenu kwamba mwendelee kupiga hatua nyingine mbele zaidi katika hili, tujue katika hekta hizo zilizotajwa ni kiasi gani kimerasimishwa kwa viwanda vipi, bidhaa zipi zinazalishwa, hali ya miundombinu ikoje na kuna mikakati gani ya kuiendeleza. Pia tufahamu ni ajira ngapi zilizozalishwa kutokana na uanzishwaji wa viwanda hivyo.” 

Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi na wasimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika kubuni na kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua fursa za uwekezaji.

Pia kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vikubwa ili Tanzania iweze kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. “Tumieni asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia vikundi vyao ili wawekeze katika viwanda vidogo vidogo vyenye kuleta tija na kuongeza pato la kaya ili kuutokomeza umaskini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali katika Dira ya Maendeleo ya 2025 ni kuhakikisha Halmashauri zinakuwa na uwezo wa kujitegemea kimapato kwa zaidi ya asilimia 80 ifikapo 2025. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAWATAKA WATAFITI KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA NA KUBORESHA SERA YA MAENDELEO

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (ambaye alikuwa mgeni rasmi) akizungumza  katika Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na kufanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna- Kajunason/MMG.
Wageni waalikwa na  Wanafunzi wa MUHAS waliohudhulia kongamano hilo.
 Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha MUHAS Prof. Andrew Pembe akitoa maneno ya kutambulisha Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Serikali imewataka watafiti kote nchini kufanya tafiti katika maeneo ya vipaumbele vya serikali, badala ya kufuata matakwa ya wafadhili.

Amesema kufanya hivyo kutasaidia kuboresha sera na mipango ya maendeleo itakayowezesha kufikia malengo katika sekta mbali mbali ikiwemo afya na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025

Akizungumza katika Kongamano la kuwasilisha tafiti za dawa za kulevya lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewataka watafiti kufanya tafiti zitakazozingatia takwimu sahihi ambazo zinachangia katika kuboresha sera na programu za afya.

"Natoa rai msifanye utafiti kwa sababu tu kuwa wafadhili wanatupatia fedha na msifanye tafiti na mkaridhika kwa vile tafiti zenu zimechapishwa kwenye majarida, bali mje na zile zitakazofanya mabadiliko ya sera mbali mbali hususani kuboresha upande wa afya," amesema.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha MUHAS Prof. Andrew Pembe amesema matokeo ya utafiti yanaonyesha tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya bado ni kubwa na waathirika wa madawa ya kulevya hawawezi kushiriki katika shughuli za kuzalisha.

Ameongeza kuwa watumiaji wengi wa madawa ya kulevya wanajishughulisha katika vitendo vya uharifu, na wanauwezo mkubwa wa kupata magonjwa mbali mbali likiwemo UKIMWI.

Upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS  anayeshughulikia Taaluma, Tafiti na Ushauri Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema kuwa chuo kimejipanga kutoa taarifa inayotokana na matokeo ya tafiti ambayo itakuwa imeandikwa kwa lugha nyepesi na kuwapelekea wizara ya afya ambao badae wanaweza kuangalia ni mambo gani yanaweza kuwasaidia katika kuborsha sekta ya afya.

30 WAITWA STARS MKUDE,KAPOMBE,BOCCO NDANI

0
0
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa stars', Emmanuel Amunike akizungumza na waandishi wa habari jijni Dar es Salaam leo. katikati kushoto ni Afisa habari habari na mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Criford Ndimbo kulia ni Kocha  msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa stars'.

Na Agness Francis,Globu ya jamii.
KATIKA kuelekea mtanange wa kufuzu Afcon 2019  dhidi ya cape Verde Oktoba 12 na 16 mwaka huu,kocha mkuu wa Taifa stars Emanuel Amuike ametangaza rasmi kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini.

Wachezaji watakao ikingia kambini itakayoanza septemba 30 mwaka huu ni  walinda Mlango  namba 1 Aishi Manula wa kikosi cha Simba, 2 Beno kakolanya  Yanga pamoja na Mohamed Abdalah wa JKT Tanzania.

Walinzi ni Hassani Kessy (Nkana),Shomari Kapombe (Simba),Salum Kimenya (Prisons),Gadiel Michael (Yanga), Paul Ngalema (Lipuli),Aggrey Morris (Azam),David Mwantika  (Azam),Abdalah Kheri (Azam),Kelvin Yondani (Yanga),Andre Vicent (Yanga) pamoja na Abdi Banda  wa Baroka fc.

Viungo wakiwa ni Himidi Mao (Petro Jet),Simon  Msuva (El Jadida),Mudathir Yahya (Azam),Frank Domayo (Azam),Jonas Mkude (Simba),Feisal Salum   (Yanga),Salum Kihimbwa (Mtibwa sugar) na Farid Mussa wa Tenerife.

Huku washambuliaji wa kikosi hicho atakuwa Mbwana  Samantha (KRC Gank),Tomas Ulimwengu (Al hilal),John Bcco (Simba),Yahya Zayd  (BDFXL),Kelvin Sabah (Mtibwa sugar) na Shaban Iddy Chilunda (TEXARIFE).

Mchezo huo utakaoanza kupigwa nchini Cape Verde  octoba 12 ambapo marudiano yatafanyika Jijini Dar as Salaam  katika uwanja wa taifa tarehe 16 mwezi huo.

Michezo iliopita  Taifa stats walilazimika kutoa sare ya bila kufungana na  timu ya taifa ya  Uganda Uganda the Cranes,vile vile pia walifungana mabao 1-1 dhidi  Lesotho katika dimba la Azam complex Chamazi.

Taifa stars  wakiwa nafasi ya 3  na pointi 2,akifatiwa na Cape Verde wenye alama 1,huku Uganda wakiwa vinara wao  kwa pointi 4 katika  kundi hilo L.

Mashindano hayo ya Afcon yanatarajia kufayika nchini Camerron mwakani.

RAIS MAGUFULI AZINDUA FLYOVER YA MFUGALE ENEO LA TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  wakati akizindua rasmi wa Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida akipena mikono na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa  baada ya kuzindua rasmi  Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa akimpongeza   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale  baada ya kuzindua rasmi  Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018. 
Mke wa Rais Dkt. Magufuli, Mama Janeth Magufuli, akiongozana na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na mwakilishi wa BAKWATA Sheikh Alhad Mussa Salum wakielekea kushuhudia uzinduzi rasmi wa Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida wakisalimia mamia ya wananchi waliofurika kushuhudia uzinduzi rasmi wa Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2018.   
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ukipita katika Daraja la Juu la Mfugale (Mfugale Flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela maeneo ya TAZARA jijini Dar es salaam baada ya uzinduzi rasmi leo Septemba 27, 2018.   

Pinda ajitosa kuinua lishe Kagera

0
0
Na Mwandishi Wetu, Pugu
WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Peter Pinda, amesema asasi zisizo za kiserikali zitachochea vikubwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini endapo zitahamasisha ushiriki wa vijana na wanawake kwenye sekta za kilimo, uvuvi na biashara.

Akizungumza na ujumbe wa Agri-Thamani Foundation ya Mkoa wa Kagera uliomtembelea nyumbani kwake Pugu, Dar es Salaam ili kumshukuru kwa kuwa mlezi wa asasi hiyo, Waziri Mkuu mstaafu ameeleza thamani na nguvu asasi zizizo za kiserikali duniani kote katika kusaidiana na serikali kuneemesha maendeleo ya wananchi na akaahidi kutumia asasi hiyo kuinua lishe katika Mkoa wa Kagera.

“Mimi pia ni mkulima na nina uzoefu wa muda mrefu katika kilimo. Kwa sababu hii naamini nitaweza kuchangia vyema katika kuiongoza taasisi hii kufikia malengo yake na kwa kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano kujenga uchumi wa kati na viwanda…Ni matumaini yangu ni kwamba tutashirikiana kuinua lishe Mkoa wa Kagera. La muhimu ni ushirikiano na uaminifu wa hali ya juu, ameasa Bw Pinda.

Ametumia fursa hiyo kuwaeleza Watanzania kwamba ili asasi zisizo za kiserikali zifikie malengo yake, ni lazima zihamasishe ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta za kilimo, uvuvi na biashara na kufafanua kwamba, ni muhimu kuthaminisha mazao ya wakulima ili waweze kunufaika. Uzalishaji wa mazao ukiongezeka, ameeleza, uhitaji wa viwanda kuchakata mazao hayo yataongezeka pia.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa tatizo la unyafuzi limesababishwa na kukosekana lishe bora, kwani lishe bora ni muhimu kwa afya njema na kumwezesha mtu kujikinga na magonjwa mbalimbali na kuahidi kwamba yeye binafsi atahakikisha asasisi hiyo inashirikiana na wizara ya afya na taasisi nyingine za afya ndani na nje ya nchi ili elimu ya lishe iwafikike walengwa kwa usahihi vijana na wanawake wa Mkoa wa Kagera kutambua umuhimu wa lishe na afya bora katika juhudi za kuleta maendeleo.
WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Peter Pinda(kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya kiserikali Agri Thamani Foundation kutoka Kagera, Bi. Neema Lugangira (kulia). Mzee panda ni mlezi wa asasi hiyo alielezea umuhimu wa kutoa elimu sambamba na uboreshaji wa upatikaji wa lishe bora pamoja na kuwaunganisha vijana na wanawake katika sekta zingine za kimkakati hapa nchini ili kutokomeza unyafuzi na umaskini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAASWA KUTOA ELIMU YA UOKOAJI KWA WANAOTUMIA USAFIRI WA MAJINI

0
0
SERIKALI yaaswa kutoa elimu ya uokoaji kwa wananchi wanaotumia usafiri wa majini pamoja na matangazo kama ilivyo kwenye vyombo vya usafiri wa anga.

Hayo yamesemwa na mwanaharakati,Laulence Mabawa wakati akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema “Serikali itoe agizo la tangazo kwa wananchi wanaotumia usafiri wa majini ili waweze kujiokoa pale itokeapo dharura”

Amesema kuwa wakitoa matangazo yatakayo saidia watumiaji wa vyombo vya maji jinsi wanavyoweza kujioko ili kupunguza majeruhi pamoja na watu wanaofariki katika ajali zinazotokea kwenye bahari, ziwa na mito ambayo inatumia vyombo vya majini.

Mabawa amewaasa wananchi maneno ya upotoshaji kuhusu tukio la ajali ya MV Nyerere pamoja na wanaobeza  majeneza yaliyotumika katika mazishi ya waliofariki katika ajali ya kuzama kwa MV. Nyerere.

Pia Mabawa ameiomba serikali kuwaandalia vyeti vya heshima wananchi wote waliosaidia uokoaji na uopoaji wa wahanga wa MV.Nyerere na vyeti hivyo ameomba Rais ndio akabidhi wananchi hao waliojitole.

Pia amewaasa wananchi na wanasiasa kuacha kukosoa juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na kukosoa watendaji wake kutokana na historia za maisha yao ya awali.

Pia amewaasa wateuliwa wa Rais wafanye kazi kwa maarifa, busana na hekima.

JKCI KUTOA HUDUMA YA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO NA ELIMU YA AFYA YA MOYO KWA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI KESHO

0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha Wahariri na Waandishi wa Habari kwamba katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani itafanya uzinduzi wa upimaji wa afya ambao utaenda sambamba na upimaji na utoaji wa elimu ya afya ya moyo bila malipo kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wote pamoja na watoto wao. 

Upimaji huo utafanyika tarehe 28/09/2018 kuanzia saa nne (4) asubuhi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete. Usikose kuhudhuria nafasi hii muhimu ya upimaji wa afya.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya moyo Duniani inasema: “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya  Moyo Jakaya Kikwete
27/09/2018

VAN VICKER ATUA NCHINI KWA AJILI YA UZINDUZI WA FILAMU YA D.A.D

0
0
MUIGIZAJI wa Kimataifa wa Nchini Ghana Van Vicker ametua nchini kwa ajili ya uzinduzi wa filamu mpya ya D.A.D aliyoshirikishwa na muigizaji wa Tanzania Wema Sepetu utakaofanyika kesho Septemba 28  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Van Vicker ametua Tanzania alfajiri ya leo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyotakiwa izinduliwe miaka mitatu iliyopita, sasa inazinduliwa Septemba 28, 2018 siku ambayo Wema atakuwa akitimiza umri wa miaka 30.

Msanii huyo kutoka Ghana amepokelewa na mwenyeji wake  Wema Sepetu pamoja na wasanii wengine tayari kabisa kwa ajili ya kuzindua filamu hiyo baada ya kushindikana kufanyika Juni 30 kwa Van Vicker kushindwa kuwasili kusema hatahudhuria kutokana na kubanwa na shughuli nyingine.

Wema Sepetu amezungumza baada ya kuwasili kwa muigizaji huyo, amesema Van Vicker ni rafiki yake lakini kwa muda mrefu amekuwa akishindwa kufanikisha uzinduzi huu mara nyingi akidai yupo bize na kazi zingine,.

“Van Vicker ni rafiki yangu lakini hapo katikati tumekuwa tukikwaruzana mara kwa mara kwa sababu kila nikimwambia filamu inabidi iingie sokoni mara ataniambia hivi mara vile, lakini siku zote alikuwa ananiambia anataka tufanye kitu kizuri,” alisema.

Kukutana kwa Wema Sepetu na Van Vicker ilikuwa ni baada ya kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi katika mtandao wa Instagram akimuomba wafanye kazi pamoja na baada ya muda mfupi alimjibu hata yeye angefurahi kufanya kazi naye.


“Baada ya kumtumia ujumbe mfupi alinipa namba yake ya simu, tulizungumza namna tutakavyofanya kazi, kwa sababu nilitaka kufanya kazi kimataifa nilimwambia lazima niende Ghana akakubali. Nakumbuka nilikaa wiki mbili kule wakati wa kutengeneza filamu hii.”

Uzinduzi wa filamu hiyo iliyobatizwa jina la D.A.D unakuja miaka mitatu tangu walipoigiza huku Wema akisema Mghana huyo ndio chanzo cha kuichelewesha kuingia sokoni kwa kuwa amekuwa na mambo mengi kiasi cha kuwafanya wakwaruzane mara kwa mara.
Muigizaji wa Kimataifa wa Nchini Ghana Van Vicker  akizungumza  mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa JKNIA kwa ajili ya uzinduzi wa filamu mpya ya D.A.D aliyoshirikishwa na muigizaji wa Tanzania Wema Sepetu utakaofanyika kesho Septemba 28  katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

HUU NDIO UJUMBE WA CHIKI KWA WASANII WANAOCHIPUKIA

0
0
Khadija Seif, Globu ya jamii
STAA mwenye ubora wake katika tasnia ya filamu za kibongo a.k.a Bongo Muvie  Chiki Mchoma amewashauri  wasanii  wanaochipukia kuhakikisha wanaishi maisha yao halisi.

Amesema hata yeye pamoja waigizaji wengine wengi wakongwe wameishi maisha ya kawaida na kujenga heshima kwa wadau.

 Chiki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anapiga stori na Micbuzi Blog ambayo imekutana na Staa huyo na kuzungumza mambo kadhaa kuhusu sanaa ya uigizaji nchini.

Amesema changamoto inayowakumba kwa sasa wasanii chipukizi  ni kutopitia makundi mbalimbali ya filamu kama vile zamani wasanii ambavyo wamepitia na  kujifunza vingi kuhusu uigizaji.

Amefafanua kupitia makundi hayo waigizaji wengi wamepata  elimu, uzoefu pamoja na tabia  njema na matokeo yake wamejijengea heshima katika jamii na tasnia ya filamu kwa ujumla.

Pia Mchoma amesema kuna baadhi ya  wasanii kwa sasa wanaishi kwa kutegemea kiki wakiamini ndio zinaweza kuwapatia umaarufu badala ya kuweka jitihada kwa  kutengeneza kazi nzuri.

Ameongeza uzoefu wao ndio umeweza kuwajenga hivyo basi wajitahidi kujenga heshima ili waheshimike kwa watazamaji pamoja na wadau wa filamu.

"Kwa mataifa ya nje msanii akifanya jambo ambalo halipendezi kwa jamii anachukuliwa hatua kali tofauti na hapa kwetu linachukuliwa ni jambo la kawaida," amesema.
  
Amewataka  wanahabari waelekeze nguvu nyingi kwenye kutangaza kazi zao kuliko kuwatengenezea chuki baina ya msanii kwa msanii au kikundi fulani cha watu.

Ametoa mwito kwa wasanii  wanaotegemea Kiki kuwa  hazitawajengea chochote  badala yake zitafanya wanajamii kuiga mambo ambayo yatawapotosha kwani wasanii ni kioo cha jamii .

Na kwamba chochote watakachokifanya wapo watu ambao wanawatazamaa au  kuyafata.
Msanii wa filamu nchini, Chiki Mchoma akizungumza na Michuzi Blog kuhusu  wasanii chipukizi kusema jitihada    zao katika kazi ili watengeneze kazi nzuri na kufikia malengo waliyojiwekea.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

Wizara ya Madini na Taasisi zake yashiriki Maonesho ya aina yake mkoani Geita

0
0
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiwahutubia wananchi wa Mikoa ya Geita na Kagera tarehe 26 Septemba, 2018 katika Viwanja vya Kalangalala mkoani Geita.

Na Rhoda James, Geita

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka Mgodi wa Geita Gold Mine Ltd kuwalipa fidia wananchi waliopata madhara ya nyufa katika nyumba zao kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini wa kampuni hiyo. Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo tarehe 26 Septemba, 2018 wakati alipofungua Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu mkoani Geita kwa niaba ya Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.

Alitoa rai kwa Wachimbaji wadogo wa madini kote nchini kushiriki maonesho hayo yanayoendelea mkoani humo kwa kuwa yatawanufaisha kwa kupata fursa ya kujifunza kuhusu teknolojia mbalimbali na namna bora ya uchimbaji, uchenjuaji, ikiwemo kupata elimu ya kulinda mazingira na kuzalisha kwa tija.
Mjiolojia kutoka taasisi ya Jilojia na Utafiti wa Madini Tanzania  (GST) Hafsa Maulid akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Madini kuhusu huduma inayotolewa na taasisi hiyo (anayesaini kitabu cha wageni) alipotembelea banda la Madini katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.

Pia, aliwataka Wakuu wa mikoa yote nchini pamoja na Wakuu wa wilaya zote kujifunza kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi ili kuhakikisha kuwa wananchi wao wanafaidika na rasilimali pamoja na mazao yanayolimwa katika maeneo yao.

“Mkifanya maonesho ya aina hii katika mikoa yenu kulingana na mazao au rasilimali mlizonazo katika mikoa yenu wananchi wenu watafaidika,” alisema Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.

Vilevile, Naibu Waziri Nyongo, aliwataka wananchi wa  mkoa wa Geita na Kagera pamoja na wadau wa madini ya dhahabu kujipanga ili kuhakikisha kuwa maonesho hayo yanafanyika kila mwaka. Pia, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana na uongozi kutoka Mkoa wa Geita kuhakikisha kuwa wanayatangaza maonesho hayo kwa kiasi kikubwa ili yaweze kufahamika duniani kote hatimaye wadau wa madini waweze washiriki kwa wingi.

“Wateja wengi wa madini wanatoka nje ya nchi na ni vyema pia wakajua chanzo cha madini hayo kiko wapi,” alisema Nyongo.
Mhandisi kutoka Wizara ya Madini Johnbosco Karungamye akimwelezea jambo Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ( kati kati) alipotembelea banda la Wizara ya Madini mkoani Geita.

Akizungumzia mchango wa Sekta ya madini katika pato la taifa, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, mchango wa Sekta ya Madini bado ni kidogo na kuongeza kuwa, malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, mchango wake unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

“Mwaka 2016 na 2017 sekta ya madini imechangia kwenye pato la taifa asilimia 4.8 lakini tunatarajia ifikapo 2025 sekta ya madini itachangia zaidi ya asilimia10,” alisema Nyongo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Nyongo ametoa onyo kwa wachimbaji wadogo kuachana na tabia ya kutorosha madini na kueleza kuwa, atakayekamatwa akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Vipande vitatu vya madini katika gram tofauti baada ya kuzalishwa na kampuni ya Wachimbaji Wadogo mkoani Geita.

Pia, Naibu Waziri Nyongo alitumia fursa hiyo kuupongeza Mkoa wa Geita na wadau mbalimbali akiwemo Mamlaka ya Maendeleo ya Bishara Tanzania (TanTrade) pamoja na Wizara ya Madini kwa kuandaa maonesho ya madini ya dhahabu mkoani Geita.

Pia, amewapongeza umoja wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu (GEREMA) kwa kuhakikisha kuwa Maonesho hayo yanafanyika kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi alisema kuwa, ni matarajio yake kuwa maonesho hayo yatakuwa ya kitaifa na hatimaye ya dunia nzima na kuongeza kuwa, anataka maonesho hayo ya madini ya dhahabu kufanyika kila mwaka mkoani kwake.

Pia, alisema alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya madini kwa ushirikiano inayotoa kwa wachimbaji wadogo kupitia taasisi za GST na STAMICO.

WAZIRI MEDARD AZINDUA MATUMIZI YA GAS DANGOTE-MTWARA

0
0
JOSEPH MPANGALA -MTWARA

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kaleman amezindua Mradi wa matumizi ya Nishati ya Gasi awam ya kwanza katika kiwanda cha Saruji cha Dangote kwa lengo la kuzalisha umeme wa megawatts 45 unaozalishwa na mashine tatu zenye uwezo wa Kuzalisha Megawats 15 kila moja.

Uunganishwaji wa Nishati ya gas katika kiwanda Utaongeza uzalishaji wa Saruji katika Kiwanda cha dangote pamoja na Kupunguza matumizi ya gaharama za uendeshaji kwa asilimia 40 ambapo kwa sasa Dangote anazalisha Saruji kwa kutumia mafuta ya dizeli ambayo yanagharimu shilingi Milion315 kwa siku Gharama ambazo ni kubwa ukilinganisha na gharama za Umeme wa Nishati ya Gas.

Akiongea mara baada ya Kuzindua matumizi ya Gas kutumika katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara Waziri wa Nishati Dr Medard kaleman amesema dhamira ya serikali kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wote ili waweze kuvutika kuwekeza hapa Nchini ili kuongeza Ajira kwa wananchii.

“Punguzo la asilimia 40 katika Gaharama za Uzalishaji katika Kiwanda cha Dangote ni Tija kwa kampuni lakini ni Tija kwa serikali,kwa sasa Kiwanda Kinaweza Kuajiri wafanyakazi watu elf moja hadi elfmoja na miatano lakini wanafanya hivyo kwa sababu gharama za uendeshaji zilikuwa ni kubwa lakin kwa Kutumia Gas ambayo inawapunguzia gharama kubwa za uendeshaji wameniambia wanaweza kuongeza ajira kwa Watanzania”Amesema Dr.Medard.

Akiongea kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Avod Mmanda amesema uzalishaji wa Saruji utakapoongezeka utaleta maendeleo ya Mtu Mmoja mmoja pamoja na ajira kwa wingi zaidi.

“Kiwanda Hichi kitakapo zailisha Simenti kwa wingi maana yake ni kwamba usambazaji utakuwa Mkubwa,Hapa katikati Kiwanda Kiliposimama Mji Ulitikisika kwenye swala zima la Ujenzi kwa hiyo Siment Inapokuwa nyingi na kwa bei nafuu Ujenzi utaongezeka na ajira zitakuwepo kwa wingi”Amesema Mmanda. Mradi huu ni wa Awamu ya Kwanza wa Megawats 45 na awamu ya pili itakuwa na Megawats 75 kuingia katika kiwanda cha dangote na unatarajia kukamilia mwezi October 2019.
 Waziri wa Nishati DR.Medard Kaleman akikata Utepe Kuashiria Uzinduzi wa Matumizi ya Nishati ya Gas tayari kwa uzalishaji wa Umeme wa Megawats 45 katika kiwanda cha Saruji kilichopo Mkoani Mtwara.
 .Mtendaji Mkuu wa Kiwanda Cha Sarauji Cha Dangote kilivhopo Mkoani Mtwata akimuonesha Wazirir wa Nishati dr.Medard Kaleman Mitambo ya Umeme ya Umeme ya Megawats 45 ambayo imeanza kutumika katika Kuzalisha Saruji ya Dangote.
 .Waziri wa Nishati Dr.Medard Kaleman akitazama baadhi ya Mitambo ya Umeme ya Megawats 45 inayomilikiwa na Kiwanda cha Dangote ambacho tayari kimeanza kupokea Nishati ya Gas tayari kwa Uzalishaji wa Saruji.

INDONESIA YAAHIDI USHIRIKIANO NA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

0
0
Na. VERO IGNATUS, ARUSHA. 

Ubalozi wa Indonesia umeridhika na kazi zinazofanywa na Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini katika kudhibiti matumizi ya nyuklia sanjari na kushirikiana katika kuhakikisha matumizi sahihi ya nyuklia yanakwenda katika sekta ya viwanda.

Akizungumza Balozi wa Indonesia Ratlan Pardede nchini Tanzania amesema upande kwa upande Indoneshia nyuklia wanaitumia katika viwanda na kilimo hivyo wanataka kuutumia uzoefu huo kwa kushirikiana na Tanzania ili kuinua uchumi kupitia teknolojia hiyo. 

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala amesema ujio wa Balozi wa Indonesia nchini a utaleta mafanikio katika sekta mbalimbali zinazotumia nguvu za nyuklia.Profesa Busagala amesema mbali na kutembelea katika Kituo hicho cha Nyulkia kilichopo Jijini Arusha pia aliweza kutembembelea mahabara ya kuzalishia nguvu za nyuklia na amesema kituo hicho kipo katika hatua nzuri kwani kazi za ndani zimeshamalizika kwa sasa wanamalizia za nje.

Sambamba na hayo Balozi huyo amesema Mhe Rais Magufuli alimweleza Kwamba atafute maeneo mbalimbali nchini ambayo ataleta viwanda Tanzania kwa kupitia wafanyabiashara mbalimbali na ndicho anachochokifanya kwa sasa.Uwezekano wa Indonesia kuleta viwanda vinavyotumia teknlojia ya nyuklia na madawa, uchumi wa Tanzania utaongezeka kwani unaendana na sera sahihi ya serikali wa kujenga Tanzania ya viwanda.

'' Tunapoongelea teknolojia ya nyuklia tunaongelea uwezekano wa kiwa na viwanda vingi zaidi uchumi wa nchi utaongezeka. "alisema Busagala. Licha ya nchi ya Indonesia kufanya vizuri katika viwanda, huku Tanzania nayo ikiweka mkazo na msisitizo katika uongezaji wa viwanja ameeleza ushirikiano huo wa Teknolojia mpya utasaidia nchi ya Tanzania kuondokana na upotevu wa asilimia 40 ya mazao ya kilimo na kuongeza mapato ya nchi kwa kiasi kikubwa
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Profesa Rtlan Pardede akizungumza na menejimenti ya Nguvu ya Atomiki iliyopo Njiro Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
Mkurugenzi mkuu wa Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala akizungumza mara baada ya kuwasili ugeni kutoka Ubalozi wa Indonesia katika Makao makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Njiro Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Kaimu Mkurugenzi - Kurugenzi ya matumizi ya Teknolojia ya Mionzi Yesaya Sungita akimuonyesha Balozi wa Indonesia mahali pa kufanya vipimo na kuangalia usalama wa vyakula, Mahali pa kufanyia utafiti wa vitu vinavyotoa mionzi.

UJENZI WA BARABARA KIWANGO CHA LAMI KINONDONI MKWAJUNI MPAKA MANGO KUPITIA POLISI UNAENDELEA KWA KASI

0
0
 Uchimbaji wa barabara hiyo inayotoka Kinondoni Mkwajuni nyuma ya Muslim ukiwa unaendelea
 Moja ya Greda likiendelea na kazi ya uchimbaji wa barabara wa eneo la Mkwajuni.
 Hili ni eneo ambalo Usawazishaji wa Barabara unaendelea, ambapo kifusi hicho mbele kinakaribia kuondolewa.
Baadhi ya wahusika wa ujenzi wa barabara hiyo wakiwa wanashauriana jambo wakati kazi inaendelea
 Huu ni uzio uliowekwa ili wananchi wapite huko na wasiharibu utaratibu wa ujenzi wa barabara hiyo.Picha zote na Fredy Njeje.

RAIS MAGUFULI AWANYOOSHEA KIDOLE WATALAAM WASIO WAZALENDO, ATOA MAAGIZO

0
0
Atuma salamu kwa watalaam wa mazingira..awaambia ole wao.

Na Said Mwishehe,Globu ya kijamii

RAIS Dk.John Magufuli amewataka watalaam nchini kuwa wazalendo kwa nchi yao huku akieleza kuwa baadhi ya watalaam ndio chanzo cha kukwamisha miradi na hasa ya maendeleo.

Pia ametoa onyo kwa wataalam wa mazingira ambao wametoa mapendekezo ambayo ameyaita ua hovyo na yenye lengo la kukwamisha mradi wa umeme wa maji wa Stiglers georg na amewataka kuyafuta mapendekezo yao mara moja na ole wao wakishindwa kuyabadilisha.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati anazindua rasmi flyover ya Mfugale katika makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi kueleza namna ambavyo baadhi ya watalaam nchini wamekuwa chanzo cha kukwamisha miradi."Ngoja nitoe mfano mmoja tu wa namna ambavyo baadhi ya watalaam wetu wanakwamisha miradi yenye tija kwa watanzania."Tena ni wataalam ambao wamezaliwa Tanzania na wamesomeshwa na Serikali,wengine ni weusi kuliko hata mimi lakini wanafanya maamuzi ya hovyo kabisa.

" Tunafahamu umeme wa maji ndio wenye bei nafuu kabisa kuliko umeme wowote .Mkakati wa Serikali ni kuhakikisha tunapata umeme wa maji kupitia mradi wa Stiegler's Gorge,"amesema.Ameongeza wakati Serikali inataka kuanza ujenzi huo na fedha zipo tayari lakini watalaam wa mazingira wametoa mapendekezo yao.

"Ukiisoma ile ripoti yao utakutana na mapendekezo mengi na baadhi ya mapendekezo yanasema watakaokuwa wanajenga eneo hilo wasijisaidie eneo hilo,waende umbali wa kilometa 10." Pendekezo lingine chochote ambacho kitapelekwa hapo kipimwe kwanza,yaani kama unataka kupeleka mchicha kwa ajili ya watu waliopo eneo la mradi basi lazima upimwe.Chochote ambacho utakipeleka eti wanataka kipimwe.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA WARSHA YA WANAJIOSAYANSI. JIJINI DODOMA.

0
0


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa mwananjiolojia, Batwenge Chakutema kuhusu vifaa mbaIimbali vinavyotumika katika utafiti na upimaji madini wakati alipofungua Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia zawadi ya kinyago cha njiwa wawili kilichotokana na jiwe wakati alifungua Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . Kushoto ni Waziri wa Nishati, Angela Kairuki na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Warsha ya Jumuiya ya Wanajiosayansi Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) kwenye hoteli ya New Dodoma, Septemba 27, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VIONGOZI WA KIJIJI WAFUNGA OFISI, “WATIMKA” KISA OPERESHENI YA BHANGI

0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha 

Wananchi wa kijiji cha Kisimiri Juu Kilichopo tarafa ya King’ori wilayani Arumeru walikiacha kijiji chao kwa muda huku viongozi wao wakifunga ofisi zao na kukimbia kisa operesheni ya bhangi iliyofanywa na vikosi vya Jeshi la Polisi Alfajiri leo hii.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi alisema kwamba walitapata taarifa kwamba kuna kiasi kikubwa cha bhangi kinatarajia kusafirishwa siku ya leo ndipo walipoandaa askari hao ambao walifanikiwa kufika eneo la tukio na kupata jumla ya magunia 27 yenye uzito wa Kilogramu 25 kila gunia shambani kwa mtuhumiwa mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa pamoja na Misokoto 583 ya Bhangi.

Kamanda Ng’anzi alisema kwamba kwa sasa Jeshi la Polisi mkoani hapa linawatafuta viongozi wa kijiji cha Kisimiri Juu kwa kukiuka agizo la Serikali linalomtaka kila kiongozi katika eneo lake ahakikishe kwamba halilimwi bhangi.

“Tunaendelea kuwatafuta viongozi wa kijiji pamoja na kamati zake za ulinzi na usalama na mkondo wa sheria utachukua nafasi kwani wao kama viongozi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha katika eneo lao hakuna biashara yoyote ya Madawa ya kulevya inayofanyika”. Alifafanua Kamanda Ng’anzi. 
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakihesabu misokoto ya Bhangi iliyopatikana katika moja ya nyumba ya wakazi wa kijiji hicho katika operesheni iliyofanyika katika kijiji cha Kisimiri Juu kilichopo tarafa ya King’ori wilayani Arumeru. 
Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Elias Mwita akiwaonyesha waandishi wa habari misokoto ya bhangi iliyopatikana katika operesheni hiyo

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images