Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live

OSHA yafanikiwa kupunguza ajali na magonjwa mahala pa kazi


MWASELELA AFUNGUA FURSA YA AJIRA MKOA WA MBEYA

TRC Yaungana na DC Jokate kampeni ya Tokomeza Ziro Kisarawe , Kujenga Madarasa na Kutoa Chakula

GSENGO TV: FUNDI ALIYEOKOLEWA HII HAPA SABABU YAKE KUBAKI HAI

MFALME WA ROOTS ROCK REGGAE WA TANZANIA JAH KIMBUTE AZIKWA JIJINI TANGA JUMAPILI

$
0
0
 Jeneza lenye mwili wa Mfalme wa Reggae nchini Marehemu Jah Kimbute ukitelemshwa kwenye nyumba yake ya milele wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji
 Wazazi wa Jah Kimbute, Mzee Mrinde Samuel Kimbute na Mama Judith Kimbute baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji 

 Mjane wa marehemu Jah Kimbute akiweka shada la maua kwenye kaburi wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji
Watoto na mjukuu  wa marehemu Jah Kimbute wakiweka shada la maua kwenye kaburi la baba yao wakati wa mazishi ya mwanamuziki huyo aliyefariki Alhamisi iliyopita nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yamefanyika Dunga na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji. Sikiliza moja ya kazi za Jah Kimbute enzi za uhai wake aliyoitoa miaka ya 1980 akiwa mwanamuziki aliyekuwa mstari wa mbele katika kupigania amani na demokrasia barani Afrika.
Picha kwa hisani ya GOTTA IRIE

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU AWAOMBA WANANCHI WAWE WATULIVU KIPINDI HIKI CHA MSIBA

UP DATES AJALI YA KIVUKO MV. NYERERE: mpaka sasa miili 209 imeopolewa majini, 172 imetambuliwa na 112 imeshachukulia na ndugu zao

$
0
0

 Sehemu ya waokoaji wakiwa katika pemezoni mwa kivuko cha Mv. Nyerere kilichopinduka na kupelekea idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na wengine kujerukiwa, katika eneo la Ukara, Kisiwa cha Ukerewe jijini Mwanza, wakiangalia maeneo mbalimbali kutafuta miili au watu waliohai waliozama kwenye maji. ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka juzi Alhamisi (Septemba 20, 2018) kikikadiriwa kubeba idadi kubwa ya abiria kuzidi uwezo wake. Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mpaka wakati huu miili ya waliopolewa majini imefikia 209, huku kati yao miili  172 imetambuliwa huku 112 ikiwa imechukulia na ndugu zao.
 Picha zote na Steve Magombea.k.a Kasampaida.
 Vivuko vya Mv. Clarias na Mv. Nyehunge vikiwa tayari kwa msaada wowote wa hata.
 Baadhi ya vijana wa Skaut wakiwa wamebeba moja ya miili iliyoopolewa kwenye maji baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka.
Zoezi la Ukoaji likiendelea.

WATANZANIA WA DIASPORA UINGEREZA WAOMBOLEZA, WATUMA RAMBIRAMBI


BAKWATA WAFANYA DUA MAALUM KUOMBOLEZA MSIBA WA TAIFA

TIMU YA UONGOZI WA CCM TAYARI YAWASILI KWENYE TUKIO LA MAZISHI YA WAHANGA MV. NYERERE MKOANI MWANZA

$
0
0


Timu ya Uongozi wa CCM yenye wajumbe sita inayoongozwa na Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Ndg. Humphrey Polepole ambao ni Wakuu wa Idara CCM Makao Makuu, tayari imewasili na kuweka Kambi Mkoani Mwanza Wilaya Ya Ukerewe katika kisiwa Cha Ukara ili kuhakikisha mambo yote yanayoendelea kusimamiwa na Serikali yanakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Majeruhi wanapatiwa matibabu ya haraka pamoja na wale wote ambao wamepoteza maisha kuhakikisha kuna kuwepo na utaratibu mzuri wa kuwasitiri na kuwahifadhi.

Imetolewa na,
Idara ya Hamasa na Chipukizi
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)

Tarafa ya Ukara, Ukerewe Mwanza.

MIILI ILIYOPATIKANA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE SASA YAFIKIA 224

$
0
0
*Waziri asema uwezo wa kivuko ilikuwa kubeba watu 101 lakini siku ya tukio kilibeba watu 265

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema hadi sasa idadi ya miili ya watu waliokufa kutokana na kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere imefikia 224.

Pia amesema uwezo wa kivuko hicho ni kubeba watu 101 lakini kimebainika kuwa watu ambao walikuwa kwenye kivuko hicho walikuwa 265 ambayo ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kivuko hicho.

Waziri Kamwelwe amesema hayo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa maziko ya miili tisa ambayo imezikwa na Serikali kati ya miili 224 iliyopatikana baada ya tukio hilo.Amefafanua kati ya miili hiyo 224 ambayo imepatikana wanawake ni 126,wanaume 71.Pia watoto wa kike ni 17 na watoto wa kiume ni 10

Pia amesema miili ambayo imetambuliwa ni waliotambuliwa ni 219 na wote wamechukuliwa na ndugu na miili ambayo bado haijatambuliwa ni watu wanne ambao hao watazikwa na Serikali leo.Ameongeza kuna miili ya watu watano ambayo hiyo itazikwa pamoja na miili ya watu wanne na kufanya jumla ya miili ambayo itazikwa leo ni tisa.

Waziri Kamwelwe amesema miili ambayo haijatambuliwa imechukuliwa DNA na kisha kukabidhiwa kwa ndugu au vyovyote itakavyoamriwa.

Wakati huo huo amesema kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo watanzania wote wamonesha ushirikiano mkubwa na kwamba michango ambayo imepatikana ni Sh.Milioni 190 na tayari wamefungua akaunti maalum ya maafa inayofahamika Mv.Nyerere.
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya Marehemu waliofariki kufuatia kivuko  cha MV Nyerere kupinduka na kuzama

HUZUNI KUBWA KWA TAIFA,MIILI YA WATU ... RC MONGELA AELEZA NAMNA WANANCHI WALIVYOFANIKIWA KUOKOA WATU 40 WAKIWA HAI

$
0
0
* Ni katika tukio la kuzama kivuko cha MV.Nyerere, Mbunge wa Ukerewe aomba kivuko cha uhakika

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema msiba huo ni mkubwa na wa kitaifa huku akieleza kuwa wananchi wamefanya kazi kubwa kwani wao ndio wamefanikisha kupata kwa watu 40 walio hai.

Mongella amesema hayo leo mchana huu wakati akitambulisha viongozi mbalimbali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ameongoza maziko ya Watanzania waliopoteza maisha kutokana na tukio la kupinduka kwa kivuko cha Mv.Nyerere.

Mkuu huyo wa Mkoa amemwambia Waziri Mkuu kwamba Septemba 20 mwaka huu saa nane mchana walipata taarifa za kuwa kivuko hicho kinazama na wao wakafika eneo la tukio saa 11 jioni.

Amesema baada ya kufika walikuwa wananchi wa eneo hilo tayari wamefanikiwa kuokoa watu walio hai 40 na hakika wananchi hao wamefanya kazi kubwa."Watu 40 wameokolewa na wananchi wa maeneo haya.Sisi wengine wote tumeokoa mtu mmoja tu jana.Hivyo wananchi hawa wamethibitisha uwezo mkubwa na tunao watu wananchi wenye uwezo mkubwa," amesema.

Wakati huo huo Mongella amesema kwamba tukio hilo limeacha majonzi na masikitiko makubwa lakini wanashukuru ushiriki wa makundi mbalimbali kwa namna ambavyo wameshiriki katika tukio hilo.Pia wamesema  viongozi mbalimbali nao wamefika katika eneo la tukio hilo na uwepo wao umekuwa faraja kubwa.

"Kwa namna ambavyo watu wameshiriki katika tukio hilo ni vema tukashukuru makundi yote na si mtu mmoja mmoja," amesema Mongella.


MBUNGE WA UKEREWE

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi (Chadema) amemwambia Waziri Mkuu kwamba amejawa na simanzi kutokana na tukio hilo.Pia amesema katika maisha yake hakuwahi kushuhudia vifo vya idadi kubwa kwa mara moja kama ambavyo imetoke huku akieleza  na tukio hilo ni janga ambalo tayari limetokea.

Amesema kutokana na  janga hilo kuna jambo la kujifunza kuhakikisha halitokei tena tukio la aina hiyo huku akiomba Watanzania kushikamana kama Taifa."Faraja ambayo tunayoweza kuipata sisi wananchi wa Ukerewe na ukanda huu ni kupata chombo ambacho kitakuwa madhubuti na kuhakikisha wananchi wa eneo hili maisha yao kuwa salama.

" Tuwaombee marehemu wetu roho zao Mwenyezi Mungu azilaze mahala pema peponi.Amina,"amesema Mbunge huyo.

VIONGOZI WA DINI

Kabla ya kuipumzisha miili hiyo Katika nyumba zao za milele viongozi wa dini zote wameleza kusikitishwa na tukio hilo na kuomba dua na sala kwa Mwenyezi Mungu kutokana na tukio hilo.ia viongozi hao pamoja na kumuomba Mungu awape faraja wafiwa ambao wameondokewa na wapendwa wao wameeleza kwamba tukio limeleta masikitiko makubwa lakini wanaamini kila jambo jambo hupangwa na Mungu.

Wamefafanua watu wamekusanyika hapo ili kushuhudia tukio kubwa la kuwasitiri wapendwa wetu ambao leo wanarudi mavumbi.Pia wamuomba Mungu awape faraja viongozi wa ngazi mbalimbali katika kipindi hiki kigumu ambacho Taifa linapitia.

Viongozi hao wamesema wanawaombea wote walioaga dunia wasamehewe zambi zao.Wameomba Mungu aliupushe Taifa na majanga ambayo yanaweza kutokea.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU,AKUKUTANA NA BAADHI YA ASKARI USALAMA BARABARANI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri mkuu Mama Mary Majaliwa walipoungana na waumini wengine kusali Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa amani na mmoja wa  Masista wakati wa Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa mkono wa pole na Paroko msaidizi Padre Batholomeo Bachoo kwa niaba ya Waumini wa Parokia hiyo kufutia ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea katika Ziwa Victoria Septemba 20,2018.Wakati wa Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.

 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Janeth Magufuli akipewa mkono wa pole na Paroko msaidizi Padre Batholomeo Bachoo kwa niaba ya Waumini wa Parokia hiyo kufutia ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea katika Ziwa Victoria Septemba 20,2018.Wakati wa Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Paroko msaidizi Padre Asis Mendonca mara baada ya kushiriki Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Askari wa Usalama barabarani (Trafiki),alipopata nao chai ya asubuhi mara baada ya kutoka kushiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Osterybay Jijini Dar es salaam.Septemba 23,2018. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chai ya asubuhi na baadhi ya Askari wa Usalama barabarani (Trafiki) Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Osterybay Jijini Dar es salaam.Septemba 23,2018. 



PICHA NA IKULU.

NI MSIBA WA KITAIFA, VILIO VYATAWALA WAKATI WA MAZIKO YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA

$
0
0
*Serikali yaamua kutoa Sh.500,000 kwa kila mfiwa kusaidia mazishi,  Waziri Mkuu aongoza maziko ya pamoja

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NYUSO za majonzi,simanzi na huzuni ndizo zimetawala wakati wa mazishi ya pamoja ya makaburi ya watu tisa kati ya miili 224 ambayo imepatikana baada ya kivuko cha MV.Nyerere kupinduka.

Wakati wa maziko hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza Watanzania katika mazishi hayo ambapo pamoja na kutoa pole amesema hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa kwa maofisa na watendaji ambao kwa namna moja au nyingine ni chanzo cha kutokea kwa tukio la kuzama kwa kivuko hicho.

Amesema tayari baadhi ya maofisa wanaohusika na kivuko hicho wamekamatwa na kwamba uchunguzi utaanza mara baada kuundwa kwa chombo cha kuchunguza huku akieleza majina ya watu ambao wamefariki majina yao yatandikwa sehemu moja.Akizungumza kabla ya kupuumzisha miili hiyo leo katika eneo la Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ,Waziri Mkuu amesema ni msiba mzito na uliojaa majonzi kwa Taifa.

Amesema ni tukio la kusikitisha hasa kutokana na idadi ya watu waliofariki ambayo ni kubwa huku akielezea namna ambavyo Serikali imejipanga kuhakikisha kinapatikana kivuko cha muda ambacho kitatoa huduma ya kusafirisha abiria.Pia amesema pamoja tukio hilo ,Waziri Mkuu amesema kuna funzo ambalo wamelipata kutokana na tukio hilo na kwamba hatua mbalimbali zitachukuliwa.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Rais Dk.John Magufuli ametangaza siku nne za maombelezo kuanzia Septemba 21 mwaka huu ambapo amesema bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti.Waziri Mkuu amesema pamoja na hatua nyingine zikiendelea kuchukuliwa yeye hataondoka eneo hilo kwani anataka kuendelea kushuhudia namna ambavyo shughuli nyingine zinaendelea na atashiriki katika kupumzisha miili.

Pia amesema Serikali imeamia kutoa Sh.500,000 kwa wafiwa kwa ajili ya kusaidia katika shughuli za kupumzisha miili ya wapendwa wao ambao wamepoteza maisha kutokana na ajali ya kupinduka kwa kivuko hocho.Wakati wa mazishi hayo viongozi mbalimbali wamepata nafasi ya kuweka mashada ya maua ambapo Waziri Mkuu alikuwa wa kwanza kuweka shada la maua katika moja ya kaburi kati ya makaburi tisa
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya Marehemu waliofariki kufuatia kivuko  cha MV Nyerere kupinduka na kuzama

MAJAJI WASTAAFU MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM WAAGWA RASMI

$
0
0

Na Mary Gwera, Mahakama

JAJI Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewahakikishia Majaji Wastaafu kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.

Mhe. Jaji Feleshi aliyasema hayo, Septemba 22 jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya kuwaaga jumla ya Majaji Wastaafu tisa (9) kutoka Mahakama Kuu- Masjala Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Kazi.

“Napenda kuwapongeza kwa Utumishi wenu uliotukuka kwa Mahakama hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa Mahakama itaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kila hali, iwe kwa shida au raha,” alisema Jaji Kiongozi. Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwataka Majaji hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za Mahakama ili kuendeleza maboresho ambayo Mahakama inakusudia kufikia kupitia Mpango Mkakati wake.

Aliongeza kwa kuwasihi Majaji hao Wastaafu kutosita kutoa ujuzi wao kwa Majaji ambao bado wapo kwenye Utumishi wa Umma pindi wanapohitajika kutoa elimu katika Mafunzo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Mahakama. Kwa upande wake, Jaji Mstaafu, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Fredrica Mgaya ameushukuru Uongozi wa Mahakama kwa kuwaandalia hafla hiyo kwani wamefurahi na kujisikia kuwa wao bado ni sehemu ya Wanafamilia wa Mahakama.

Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo. 
Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo. 
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Sekieth Kihio akipokea zawadi kutoka kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, (katikati) ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Munisi. 
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Jaji Mstaafu Mhe. Laurence Kaduri ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kumaliza utumishi wa Mahakama salama. 



MICHUZI TV LIVE: MAZISHI YA MAREHEMU WA AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE

UPASUAJI WAANZA KUFANYIKA HOSPITALI ZA VIJIJINI MANONGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MBUNGE wa Manonga Seif Gulamali ameeleza hali ya afya katika jimbo la Manonga na hii ni baada ya mikakati ya kuboresha huduma za afya katika vijiji vyote  Jimboni  humo.

Akifanya mahojiano na blogu ya jamii Gulamali amesema kuwa: "Ni furaha yetu kuona Upasuaji unafanyika katika vijiji vyetu na tuna washukuru Afrikan Dev Bank kwa kufanikisha hili. Kituo cha afya cha Choma  Chankola tayari kimeshafanya  upasuaji 69 na kati ya 69 ni 1 tu ndio iliyofeli na  hiyo ni kutokana na  mzazi kuchelewa kufika Kituoni hali iliyopelekea Upasuaji wake kufanikisha mtoto mmoja na mama kuwa hai na mtoto mwingine kupoteza maisha, lakini zilizobaki zote 68 zilienda Vizuri" ameeleza Gulamali.

Kuhusiana na huduma za upasuaji zinazopatikana katika Kituo hicho cha Afya Gulamali amesema ; "Upasuaji wa kutoa mawe tumboni, kujifungua, na upasuaji kwa  watoto na huduma zote hizo zinafanyika katika kituo chetu cha afya Choma" ameeleza.

Aidha ameeleza kuwa hayo ni maendeleo makubwa sana, kilichobaki ni kuongeza majengo hasa ya mama na mtoto, jengo la kuhifadhia  maiti, maabara, jengo la Ufuaji na Nyumba za Watumishi na hiyo ni  Sambamba na kuongeza madaktari na wauguzi.Hata hivyo anamshukuru Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake kwa kutoa Fedha za Kuboresha Kituo hicho cha Afya cha Choma Chankola.

 Pia amesema kuwa; "Ni matumaini yetu Tutaweza pata hela kwa ajili ya hayo majengo, na  nitumie nafasi hii kumpongeza Daktari Frank na wauguzi wote kituoni hapa kwa huduma zao wanazotoa" ameeleza.

Baadhi ya wananchi wamempongeza Mbunge huyo na kueleza kuwa amekuwa lulu kwa wana Manonga hasa kwa kutoa vipaumbele muhimu kwa Wananchi bila kujali itikadi zao na wamemtaka kuendelea na moyo na imani hiyo ya kuipeleka Manonga mbele zaidi.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akikagua baadhi ya majengo katika hospitali ya Choma Chonkola katika jimbo la Manonga.
Muonekano wa chumba cha upasuaji katika hospitali iliyopo katika kijiji cha Choma Chonkola.

KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) ZANZIBAR

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kichofanyika Leo katika ukumbi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 23/09/2018.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiteta na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kichofanyika Leo katika ukumbi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja,(kulia)Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Sadala na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan (kushoto)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kichofanyika Leo katika ukumbi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja,wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka Wananchi waliofariki katika ajali ya Meli MV Nyerere huko Mwanza,ilioyotokea tr 20 mwezi huu, (kushoto).

DC JOKATE APONGEZWA NA WADAU WA MAENDELEO KWA KUANZISHA KAMPENI YA TOKOMEZA ZIRO KWA WANAFUNZI WILAYANI KISARAWE

$
0
0
VICTOR MASANGU,KISARAWE 

WADAU mbali mbali wa maendeleo hapa nchini katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu wamempongeza na kumuunga mkono mkuu mpya wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa kuweza kuanzisha kampeni maalumu kwa ajili kutokomeza ziro kwa wanafunzi wa shule za sekondari kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu.

Pongezi hizo wamezitoa wakati wa halfa fupi ambayo iliandaliwa na mkuu huyo wa wilaya kwa lengo la kuweza kuchangia fedha katika sekta ya elimu ambazo zitaweza kuwa mkombozi mkumbwa katika kuwasaidia wanafunzi kuweza kufanya vizuri katika masomo yao husaani pindi wanapomaliza katika kidato cha nne.

Wakizungumza katika hafla fupi ya uchangiaji wadau wa maendeleo akiwemo Mohameda Kilumbi ambaye pia ni diwani wa wa kata ya Kibuta pamoja na Hamisa Mobeto wamesema kwamba wameamua kuchangia kwa hali na mali katika sekta ya elimu kwa lengo la kuweza kuborsha sekta ya elimu kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya vibaya katika mitihani yao.

“Kwa kweli sisi kama wadau wa maendeleo tumeona umhumimu wa kushiriki katikam zoezi hili la kumuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuchangia sektaya elimu, na pia kwa pamoja tumeungana kumuunga mkono mkuu wa wilaya wetu ambaye ameteuliwa hivi karibuni lakini lengo letu kubwa ni kuhusina na hii kampeni ya kutokomeza Ziro katika wilaya ya Kisarawe,”waliwema wadau hao.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokete Mwegelo akizungumza jambo wakati wa halfa iliyoandaliwa kwa ajili ya uchagiaji katika sekta ya elimu yenye lengo la kutokomeza ziro kwa wanafunzi wa shule za sekondari. 
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akiwa na na wadau mbali mbali wa maendeleo katika halfa hiyo iliyofanyika katika shule ya Sekondari Minakaki. 
Diwani wa kata ya Kibuta Mohamed Kilumbi akizungumza jambo wakati wa halfa hiyo ya uchangiaji kwa ajili ya kutokomeza ziri katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe .PICHA NA VICTOR MASANGU .

SHEREHE ZA MIAKA 51 TANGU KUGUNDULIWA KWA MADINI YA KIPEKEE DUNIANI, TANZANITE, NCHINI TANZANIA

$
0
0
Na Asha Ngoma
Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma wameadhimisha  miaka 51 tangu madini hayo yagunduliwe mwaka 1967 katika hotel ya Serena Hotel jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2018.
Hata hivyo sherehe hizo hazikuwa na shamrashamra zilizoandaliwa na badala yake ukafanyika mkutano na wanahabari  baada ya kuahirisha sherehe hizo kutokana na maombolezo ya kitaifa ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere huko Ukara, Mkoani Mwanza.
Tanzanite Founder Foundation ni Taasisi isiyo ya kiserikali lilioanzishwa na kusajiliwa mwaka 2013 ikiwa na lengo kuu la kuwajengea uwezo vijana na watu wote waishio migodini na maeneo jirani ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku kutokana na madini haya. Tanzanite Founder Foundation na wadau leo
imeona iadhimishe miaka 51 tangu madini haya ya kipekee duniani kuvumbuliwa nchini Tanzania. 
Madini haya husheherekewa ulimwenguni na mashirika, taasisi na wafanya biashara Mbalimbali wa madini lakini hayajawahi kusherehekewa wala kuadhimishwa nchini Tanzania. Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation imeona iadhimishe siku hii kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu madini haya ikiwa ni pamoja na kutoa historia fupi ili kutoa tathmini ya tulipotoka na tulipo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kudhihirishia ulimwengu kuwa Tanzanite ni fahari yetu na urithi wetu watanzania. 
Madini ya Tanzanite yalivumbuliwa mwaka wa 1967 na Mzee Jumanne Mhero Ngoma ambaye ni Mtanzania, a iyaokota madini haya katika eneo la Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Arusha wakati huo na kuyapeleka kwa ofisi ya Madini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro ambayo nayo hawakuyatambua ni madini gani.
Bango la miaka 51 tangu madini hayo yagunduliwe mwaka 1967 huko Mirerani kwenya mkutano na wanahabari katika hotel ya Serena Hotel jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Bi. Asha Ngoma akiwa na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma (wa pili kushoto) na watendaji wa taasisi hiyo  katika mkutano na wanahabari katika kuadhimisha   miaka 51 tangu madini hayo yagunduliwe mwaka 1967 huko Mirerani. Mkutano huo umefanyika leo katika hotel ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Bi. Asha Ngoma akipongezana  na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tanzanite Founder Foundation Bi. Asha Ngoma akiwa na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma. Kusoma habari kamili BOFYA HAPA
Viewing all 110132 articles
Browse latest View live




Latest Images