Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 248 | 249 | (Page 250) | 251 | 252 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Timu za wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka 17 ambazo zitaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars zinaingia kambini jijini Dar es Salaam leo Alhamisi September 5 kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kukwea pipa kwenda nchini Nigeria kushiriki michuano hiyo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Jumatano Sept 4), Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wachezaji hao chipukizi watashughulikia na kukamilisha hati zao za kusafiria kati ya kesho, Alhamisi na Ijumaa. “Kwa upende wetu kila kitu kimekamilika kwa ajili ya safari kuelekea kwenye mashindano hayo ya kimataifa ambayo yatashirikisha timu kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika,” alisema.

  Jumla ya wavulana na wasichana 32 walifuzu kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Juni. Mashindano haya ya kimataifa yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu yakiwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa wachezaji chipukizi kuendeleza vipaji vyao.

  Kwa mara ya kwanza mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yalifanyika jijini Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wavulana pekee ambayo hata hivyo ilitolewa hatua za awali huku timu ya Nigeria ikitawazwa kuwa mabingwa.

  “Kulingana na kiwango cha kuridhisha cha wachezaji waliochaguliwa mwaka huu nina imani kwamba timu zetu za Tanzania – wasichana na wavulana – wana nafasi nzuri ya kufanya vizuri,” anasema Matinde ambaye ni mmoja wa maofisa wa Airtel Tanzania waliongoza na timu kwenye mashindano hayo.

  Airtel imeanzisha mashindano haya ya vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia upatikanaji wa vijana wenye vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya Taifa. Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa vijana kudhihirisha uwezo wao kwa makocha wa Taifa na kimataifa na kuweza kujiendeleza zaidi kisoka.

  Hivi sasa Airtel Rising Stars ni moja ya matukio muhimu ya kisoka kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF). Huanzia katika hatua ya usajili ikifuatiwa na mechi za mtoano ili kupata wachezaji nyota wa kuunda timu za mikoa ambazo huchuana katika ngazi ya Taifa.

  Airtel inaendesha muchuano hii kwa kushirikiana na klabu maarufu duniani ya Manchester United ambayo hutoa ushauri wa kiufundi na michuano hii imekuwa na hamasa kubwa katika nchi zote zinazoshiriki.

  0 0
 • 09/05/13--02:56: VIDEO WAFANYE WATABASAMU

 • 0 0


  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana septemba 10 anatarajiwa kuanza ziara ya kawaida katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
   
  Ziara hiyo itaanzia katika mkoa wa Shinyanga septemba 10 mpaka 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 mpaka septemba 19 kwa kutembelea wilaya zote tano Kabla ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea wilaya Sita za mkoa wa Mara kuanzia Septemba 20 Mpaka 25 mwaka huu.
   
  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
   
  Kwa mujibu wa Ratiba ya ziara hiyo, Wajumbe hao wa sekretarieti watakagua uhai wa Chama ikiwa ni pamoja na kupokea wanachama wapya sanjari na kuhamasisha wananchi kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha Yao na ya taifa kwa ujumla.
   
  Aidha watakagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara.
   
  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.
   
  Imetolewa na;
  Nape Moses Nnauye
  Katibu wa Itikadi na Uenezi
  05/09/2013

  0 0

  Mganga mkuu wa Serikali Dkt Donan Mmbando akizindua awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi Dkt Angela Ramadhan akitoa takwimu wakati wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwanamuziki wa bendi ya Fm Academia, ambaye ni rais wa Vijana, Nyoshi El Sadat akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  MSanii wa muziki wa bongofleva H.Baba akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! Inayosimamiwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi huo.


  Washiriki wa uzinduzi huo awamu ya pili ya kampeni ya tuko wangapi? tulizana! wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Hello Wanzania Wenzangu, 

  Nchi yetu ya Tanzania na sisi Watanzania wenyewe tuna msuli wa kutosha katika nyanja nyingi jamani, tuchukue fursa zilizopo, tusimame imara, tujipange vizuri. Sisi ni Taifa Kiongozi Afrika Mashariki. Twenzetu Jama na Kishwahili chetu Watatufuata Nyuma!!!!!!! Tusiogope Kiswahili chenyewe ni fursa!!!!!

  Na Mdau.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya pili ya mshindi wa nyumba wa promosheni ya Airtel yatosha Jishindie nyumba 3 ambapo bi Anna Gustav Lyimo (29) Afisa wa benki kuu na mkazi wa Dar es salaamu ameibuka kuwa mshindi wa nyumba ya kisasa iliyopo kigamboni jijini Dar es salaam , akishuhudia ni Meneja Msoko wa Airtel Aneth Muga ( kulia) na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na mshindi wa nyumba ya pili wa promosheni ya Airtel yatosha Jishindie nyumba 3 mara baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa katika ofisi za Airtel na kushuhudiwa na waandishi wa habari. bi Anna Gustav Lyimo (29) Afisa wa benki kuu na mkazi wa Dar es salaamu ameibuka kuwa mshindi wa nyumba ya kisasa iliyopo kigamboni jijini Dar es salaam , akishuhudia ni Meneja Msoko wa Airtel Aneth Muga ( kulia) na mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Emmanuel Ndaki.

  0 0


  Mwili wa Wakili Israel Magesa  (pichani) aliefariki dunia jana  asubuhi,unatarajiwa kuagagwa siku ya Jumamosi tarehe 07/09/2013 kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam,kuanzia Saa 5 asubuhi.

  Mwili unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili tarehe 08/09/2013 asubuhi,kuelekea kijijini kwao Chitare,Majita,Musoma kwa Mazishi.


  Wakili Magesa, ambaye  alikuwa ni mmiliki wa kampuni ya Mawakili ya Magesa &Co. Advocates, ni baba  mzazi wa Phares Magesa (MNEC), Kalimba Magesa, Makongo Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na baba Mkwe wa Haika Lawere.

  Wakili Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu, Msajili wa Mahakama kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International - Tanzania Chapter, pia ni mmoja wa wanasiasa waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini.


  Enzi za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, na alikuwa ni miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.


  Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na shughuli rasmi ya kuaga itafanyika ijumaa tarehe 6/9/2013 kuanzia Saa 5 asubuhi Dares Salaam na mazishi yatafanyika siku ya jumapili 8/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dk. Aloyce Nzuki (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya African Future Forum (AFF) Heunsu Kim (wa pili kushoto) wakitia saini makubaliano ya kuisaidia Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi ya Korea ya Kusini na kufungua ofisi ya utangazaji kwa ajili ya utalii katika mji wa Seoul. Wanaoshuhudia zoezi hilo ni wafanyakazi kutoka ofisi ya TTB na AFF, wakwanza kulia waliokaa ni George Kizeba ambaye ni Mkurugenzi wa AFF upande wa Tanzania na wa nne ni Chris Chae ambaye ni Katibu Mkuu wa AFF Afrika.
  Katibu Mkuu wa Taasisi ya African Future Forum (AFF) upande wa Afrika Chris Chae (kushoto) akimuelekeza kitu Mkurugenzi Mtendaji wa AFF Heunsu Kim (kulia) ili aweze kutia saini makubaliano baina yao na Bodi ya Utalii nchini (TTB) ya kuisaidia Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi ya Korea ya Kusini na kufungua ofisi ya utangazaji kwa ajili ya utalii katika mji wa Seoul. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dk. Aloyce Nzuki (kulia) akibadilishana na Heunsu Kim ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya African Future Forum (AFF) nakala za makubaliano ya kuisaidia Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi ya Korea ya Kusini na kufungua ofisi ya utangazaji kwa ajili ya utalii katika mji wa Seoul. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba yake katika Ufungaji wa Mafunzo Maalum ya kutuliza Ghasia Magerezani leo Septemba 05, 2013 yaliyofanyika Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani.
  Askari wa Kike pekee aliyemudu Kuhitimu Mafunzo Maalum ya kutuliza Ghasia Magerezani, Wdrs. Diana Nyaluta akionesha Ukakamavu wake pamoja na Ujasiri alionao alipoweza kuitumia kikwazo cha kamba kutambaa nayo huku akiwa amebeba silaha yake mgongoni aina ya Sub Machine gun(SMG) kama anavyoonekana.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) akiangalia baadhi ya Vifaa ambavyo hutumiwa na Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani wanapokuwa katika Operesheni mbalimbali za Kijeshi ikiwemo kutuliza Ghasia Magerezani zinapotokea (pembeni kushoto) ni Askari wa Kikosi Maalum akiwa amevalia Vifaa hivyo tayari kukabiliaa na ghasia yoyote.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha kibaka cha rangi ya kijani Askari Wdr. Sostenes Mwacha kwa niaba ya Wahitimu wenzake kutokana na kufanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo Maalum ya Kutuliza Ghasia Magerezani leo Septemba 05, 2013 katika Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Jijini Dar es Salaam.

  Na Inspekta Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amewaasa Askari wa Jeshi la Magereza nchini kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kujituma wakati wote wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku.

  Kamanda Jenerali Minja ameyasema hayo leo wakati wa Ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Kutuliza Ghasia Magerezani ya Kozi No.09 ya mwaka 2013 yaliyofanyika katika Kikosi Maalum cha kutuliza Ghasia Magerezani, Kilichopo Ukonga Jijini Dar es Salaam.

  "Zingatieni maadili ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kujituma kwani ndiyo chachu ya mafanikio yoyote yale ya kazini au mafanikio yenu binafsi". Alisisitiza Kamanda Minja.

  Aidha, akijibu hoja za changamoto mbalimbali zilizowasilishwa katika risala ya Wahitimu wa Mafunzo hayo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja alisema kuwa tayari Ofisi yake imeanza kuchukua hatua ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo za upungufu wa vitendea kazi, makazi duni na upungufu wa Vyombo vya Usafiri kadri hali ya kifedha inavyoruhusu.

  "Niwahakikishie kuwa kila jitihada zimekuwa zikifanyika na zitaendelea kufanyika kwa lengo la kuyatafutia ufumbuzi hatua kwa hatua matatizo haya kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu". Alisema Kamanda Minja.

  Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange amesema kuwa Mafunzo hayo Maalum ya Kutuliza Ghasia Magerezani yamechukua muda wa takribani miezi minane(08) na yalifunguliwa rasmi tangu Januari 04, 2013 ambapo Wahitimu hao wamejifunza mbinu za Medani za kivita, Magwaride ya aina mbalimbali, kutuliza Ghasia Magerezani, Upekuzi Maalum, Escort za aina mbalimbali.

  Vile vile Wahitimu hao wamejifunza Haki za Binadamu, Sheria na Ustawi wa Jamii, Ukakamavu na Ujasiri, Utafutaji wa Wafungwa waliotorokea kwenye misitu minene, Utafutaji wa Mifugo pamoja na Matumizi ya Vifaa vya kuzuia moto.

  Jumla ya Wahitimu 51 wa Kozi hiyo Maalum ya Kutuliza Ghasia Magerezani wamehitimu Mafunzo hayo ambapo kati yao Askari wa Kiume ni 50 na Askari wa kike 1 ambapo walijiunga na Mafunzo hayo mara tu baada ya kumaliza Mafunzo ya Awali ya Uaskari Magereza Kozi Na.26 Chuo Kiwira, Mbeya mwaka 2012.

  0 0

  Kampuni ya Delina Group na Chama Cha soka cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimeipiga tafu klabu cha waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC) kiasi cha sh milioni 4.2 ili kuwawezesha kushiriki katika mashindano ya wana-habari yaliyopangwa kufanyika Jumapili ijayo mkoani Arusha.

  Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye mgahawa maarufu wa City Sports Lounge uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Katika makabidhiano hayo, mjumbe wa DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka alikabidhi kiasi cha sh 1.2 huku Mkurugenzi wa kampuni ya Delina ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini, Davis Mosha alikabidhi shs milioni 3 kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto “Ronaldo De Lima” Omary.

  Kisaka alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini kwa mkoa wa Dar es salaam kwani ni wadau wao wakubwa.

  “Waandishi wa habari za Michezo wametoa mchango mkubwa wa maendeleo ya michezo nchini, sit u kwa DRFA, bali kwa vyama vyote vya michezo, sisi DRFA tumekuwa wa kwanza kuonyesha mfano mfano na tunaamini wengine watatuunga mkono ili kufanikisha jambo hili,” alisema Kisaka.

  Mosha alisema kuwa amesukumwa sana na mwamko wa waandishi wa habari ambao wameamua kuonyesha kwa mfano kwa kucheza soka na mpira wa pete (netiboli).

  Alisema kuwa kampuni ya Delina Group imeamua kutoa mchango huo ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Ms Unique kwa kushirikiana na Taswa Arusha na kudhaminiwa na TBL, Tanapa, Mega Trade, Pepsi, AICC na Wazee Klabu.

  “Huu ni mchango wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo, nimefarijika sana na tunaamini kuwa mtafanya vizuri katika mashindano hayo ambapo nimeambiwa Taswa SC ni mabingwa mara mbili mfululizo,” alisema Mosha.

  Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wadau hao kwa msaada huo mkubwa. “Mbali ya DRFA na Davis Mosha, pia Azam imetupiga tafu safari hii ambapo mbali ya fedha pia wametoa jezi mbili,” alisema Majuto.

  Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Bodi ya Ligi (TPL Board) na Kassim Dewji ambao wamechangia kufanikisha ziara hiyo. “Bado tunahitaji msaada wa hali na mali ili kuweza kufikia bajeti yetu, kwa ajili ya safari hiyo,” alisema Majuto.
  Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,juu ya mashindano yao dhidi ya Taswa FC ya jijini Arusha.
   mjumbe wa DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka akizungumza machache kabla ya kukabidhi mchango wao kwa timu hiyo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),Juma Pinto akitoa shukrani kwa wadau mbali mbali walioweza kudhamini mashindano hayo.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani. 
  Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda. 
  Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili. 
  Viongozi hao wawili wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR)” unaofanyika leo Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort. 
  Viongozi wengine ambao wanahudhuria Mkutano huo ni pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU). 
  Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili Kampala asubuhi ya leo akitokea mjini Dodoma ambako aliwasili jana jioni kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuuu wawili iliyofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma. 
   Rais Kikwete aliwasili Dodoma akitokea Mwanza ambako alihudhuria mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Dkt. Moses Samwel Kulola yaliyofanyika kwenye Kanisa la Bugando Calvary Temple, mjini Mwanza. 
   Imetolewa na;
   Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
  Ikulu, 
  DAR ES SALAAM. 
   05 Septemba, 2013
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana faragha sambamba na mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala,Uganda, leo
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mazungumzo na Marais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto), Rais Salva Kiir wa Sudan ya kusini na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda 
   Baadhi ya viongozi wan chi za jumuiya ya Maziwa Makuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi hizo uliofanyika jijini Kampala Uganda leo.Kutoka kushoto ni Rais Salva Kiir wa Sudani ya Kusini,Rais Joseph Kabila wa DRC,Rais Dkt.Jakaya Kikwete,Rais Yoweri Museveni wa Uganda,Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Dkt.Nkosazana Dlamini Zuma na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana na kufanya mazungumzo ya faragha, katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala, Uganda.Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

  0 0


  Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .
  MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI PROFESA MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI
  Mbunge Wa Same Mashariki, Anne Kilango  katikati akiwa  na bingwa wa unia wa wbf fransic Cheka kulia kwake na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia na wadau wengine wa mchezo wa masumbwi nchini walipotembelea Bunge la Jamuhuri ya Muhungano wa Tanzania 

  Baadhi ya wadau wa mchezo wa masumbwi nchini wakiongozwa na Mohamed Bawazir Katikati wakiwa katika picha ya pamoja kabla awajaingia ndani ya bunge kusikiliza bunge la Tanzani Super d Wa nne kulia nae akiungana nao pamoja
  Bondia fransic Cheka akiwa na wabunge mbalimbali pamoja na mwanaseria mkuu wa Selikari le alipotembelea bungeni

  Waziri wa Wizara ya Habari ,Vijana,utamauni na michezo, Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kushoto)  akiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdallah pamoja na mapromota Mohamedi Bawazir kulia na  Catherini Matili  


  Waziri Mkuu Mh,Mizengo Pinda katikati akiwa na mabondia Francis  Miyeyusho kushoto na Francis Cheka wakati walipo tembelea bungeni Dodoma kwa ajili ya kutambua mchango wao na kuwapongeza 

  0 0

   President Jakaya Kikwete (left) cuts a ribbon to open an exhibition shortly after opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
   President Jakaya Kikwete addresses health sector stakeholders during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
   The Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation (BMAF) Chief Executive Officer, Dr Ellen Mkondya Senkoro addresses participants during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
   Health sector stakeholders follow up the President’s speech during the opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.
   President Jakaya Kikwete (centre) poses for a group photo with health sector stakeholders shortly after opening of the three day National Human Resources for Health Conference held in Dar es Salaam this week.

  0 0

  Askari wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakimdhibiti Mhe mbunge wa Chadema jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ndani ya bunge wakati akitolewa ndani ya ukumbi wa bunge hilo mjini Dodoma leo.
  ---------------------------------------------------
  Vurugu kubwa zimetokea Bungeni leo  baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo. 
   Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge huyo wa Hai kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali. 
   Mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge. Mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi ulizuka na songombingo likaumuka
  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma. 

  0 0

   Mdau RICHARD MTAITA NA VICTORIA YONGOLO wakiwa amepozi na mwandani wake mara baada ya kumeremetA katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri usharika wa Makorola na kufuatiwa na mnuso wa nguvu kwenye hoteli ya Regal Naivera Jijini Tanga. Bwana harusi ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na Majitaka Tanga-Uwasa wakati bibi harusi ni mhitimu wa Chuo cha Mipango Dodoma. Picha na Mashaka Mhando


  0 0

  Miss Universe Tanzania chini ya kampuni ya Compass Communications inakamilisha jumamosi hii usaili wa warembo jijini Dar es Salaam.

  Timu ya Miss Universe Tanzania ilifanya mchakato wa usaili na picha (scouting) katika mikoa 8 ambayo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Dodoma, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.

  Miss Universe Tanzania msimu huu utafanya fainali zake mwezi Septemba taehe 27 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (NATIONAL MUSEUM), Shaban Robert street jijini Dar es Salaam.

  Mashindano ya mwaka huu umepata wafadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mohamed Enterprises na Fastjet. Wadhamini wengine watajulikana ndani ya siku chache. Wadhaimini wote watatambullishwa wiki ijayo.

  Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa kushika nafasi ya Sita kidunia.Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010.

  Baadae taji lilichukuliwa na Nelly Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic

  0 0

  Matukio ya picha baada waandishi na maafisa wabunge walivyonusurika katika ajali iliyotokea mjini Karatu leo. Maafisa wa Bunge na waandishi walikuwa katika msafara wa Wabunge toka nchi za Sadc waliokua wanaelekea Ngorongoro. Hakuna aliyepoteza maisha wakati wanahabari na maofisa wa Bunge kadhaa walipata majeraha
  Wanahabari, maafiosa wa Bunge na wasamaria wema wakiokoa majeruhi kutoka garini
  Mpiga picha wa mwananchi Edwin Mjwahuzi (mwenye kamera) akiangalia namna anavyopatiwa huduma ya kwanza mmoja wa wahanga wa ajali hiyo.
  Dereva wa gari hilo akiwa amepoteza fahamu
  Gari lilivyopinduka
  Afisa Habari wabunge Owen Mwandumbya akiwa amepumzishwa ili apate hewa kidogo baada ya ajali

  0 0

  Bharti Airtel imetangaza leo kwamba michuano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars itaanza kutimua vumbi katika jiji la Lagos nchini Nigeria kuanzia September 16 hadi 22 ambapo Tanzania itawakilishwa na timu za wasichana na wavulana. 
   Michuano hii inafanyika kwa mara ya pili mfululizo kwa lengo la kutoa fursa kwa vijana chipukizi kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika kuonyesha vipaji vyao na kuchochea maendeleo ya mpira wa miguu. 
   Akizungumzia mashindano hayo Mkurugenzi Mtendani wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesema: “Michuano ya Afrika ya Airtel Rising Stars itasaidia kuinua kiwango cha soka barani Afrika na Airtel inafarijika kupata fursa hii ya kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi”. 
  Huu ni mwaka wa tatu tangu kuanzishwa kwa programu hii ya Airtel Rising Stars barani Afrika ambapo maelfu ya vijana wamepata nafasi ya kushiriki katika nchi 16 kuanzia ngazi ya chini, mkoa hadi Taifa. 
   Wachezaji nyota kutoka katika kila nchi hizo sasa wanaelekea nchini Nigeria kuchuana kwa lengo kuonyesha vipaji vyao zaidi na kupata mshindi ambaye ndiye atakuwa kinara wa Airtel Rising Stars barani Afrika mwaka huu. Mshindi pia atajinyakulia kitita cha dola za Mimarekani 10,000 ambazo ni zaidi ya milioni kumi na sita za Tanzania. 
  Fedha hizi zitatumika kuwaendeleza vijana hao kielimu. Michuano hii ya Afrika mwaka jana ilifanyika jijini Nairobi ambapo timu ya wasichana kutoka Ghana ilinyakua taji huku timu ya wavulana kutoka Niger ikiukwaa ubingwa kwa upande wa wavulana. 
  Mchuano unatarajiwa kuwa mkali zaidi mwaka huu huku timu mwenyeji Nigeria ikiwa imejianda vilivyo kuhakikisha kwamba wanawapa raha mashabiki wao na hatimaye kutwaa ubingwa wa mashindano hayo. 
  Timu nyingine zinazotarajiwa kutoa upinzani mkali na hata kuiadhili Nigeria nyumbani kwao ni Ghana na Zambia. Kwa kuendesha mashindano haya ya vijana Airtel inaelekea kutimiza lengo lake ililojiwekea awali la kuwa mdhamini mkubwa wa mchezo wa soka kwa vijana barani Africa. Wachezaji bora kutoka katika mashindano hayo ya Afrika watapata fursa ya kushiriki kliniki mbili zitakazofanyika chini ya usimamizi wa klabu maarufu duniani: Arsenal na Manchester United. Kliniki hizo zitafanyika Lagos (Nigeria) na Lubumbashi (Democratic Republic of Congo) mwezi Aprili 2014 na kusimamiwa na makocha wa Manchester United na Arsenal. Akizungumzia umuhimu ya kliniki za Airtel Rising Stars Colaso amesema: 
  “Zitasaidiwa kuwaendeleza vijana kisoka na kuwapa hamasa ya kutaka kuwa wachezaji wa kulipwa”. Kliniki hizo ndizo zitakazozindua rasmi mwaka wa nne mwezi Aprili 2014. 
   Awali kliniki hizo zilipangwa kufanyika baada ya mashindano ya kimataifa lakini zimelazimika kusongezwa mbele ili kuwa na muda zaidi wa maandalizi ya kuziboresha.
  Mabingwa wa Airtel Rising Stars 2013 Mwanza wakisheherekea ushindi kwenye Uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Julai 6. 

  Wasichana walionyesha vipaji vya hali ya juu vya kusakata kabumbu wakati wa fainali za Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam mwaka huu.

  Vijana wakipambana vikali wakati wa fainali za Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam mwaka huu.


  0 0

  The CEO Round Table hosted an appreciation farewell dinner reception for the outgoing US ambassador to Tanzania, Ambassador Alfonso E. Lenhardt, whose tenure in Tanzania ends in October this year. 
   The ambassador through numerous initiatives of the US government has supported and promoted Tanzania’s economic growth by providing unique partnership opportunities for businesses in Tanzania. Ali Mufuruki Chairman, of the CEOrt appreciated the Ambassador for using his role to grow the relations between the United States and Tanzania and for the continued support in health and infrastructure sectors in Tanzania. 
   He said, “Tanzania has greatly benefitted from your efforts during the last four years that you have served your nation as Ambassador to Tanzania. You have reached out more than any of your predecessors as far as I know and in the process you have helped unlock new business opportunities for the private sector as well as provided much needed support through donor agencies and projects such as the Millennium Challenge Account Compact. Diplomatic and trade relations have tremendously grown in recent years thank to you.” 
   He added, “We are cognisant of the fact, that it is through your efforts that President Obama during his recent visit, chose Tanzania as a base from which he announced his now famous Energy-Africa and Trade-Africa initiatives that will form key planks of US engagement with the African continent going forward. 
  On behalf of all the members of the CEOrt and on behalf of the private sector of Tanzania, I thank you for your leadership and we the private sector of Tanzania will forever consider you a friend of our country and welcome you and your lovely wife Jackie to come back to Tanzania again”. 
   In his remarks, Ambassador Lenhardt said, “The US government has contributed more than 750 million dollars to various initiatives and programs in Tanzania. These initiatives have increased household incomes, raised the quality of life, targeted infrastructure investments in the transport, energy and water sectors and have contributed to economic growth. 
  This contribution, however only scratches the surface of what is needed to unlock the potential of this great country. The private sector has the power to drive economic growth as well as support infrastructure and social investment in Tanzania.” 
   He noted that the private sector will need to take a more central role in growing the middle-income bracket of the country’s economy as well as boost economic growth. 
  “If Tanzania is to grow and industrialize, the private sector will need to partner with government and other stakeholders to ensure infrastructure projects are implemented, especially in the energy sector, as emphasised by President Obama during his visit in Tanzania. In everything you do, always think about Tanzania Kwanza. 
  When I go back home, I will try to tell every corporate and organisation about Tanzania. It is upon you to utilize the opportunities” he said. 
   The US government is involved in numerous activities in an effort to boost Tanzania/US relations in different levels, in both public and private sectors. Among them is a pact signed to partner in power regulation capacity building, a step meant to solve energy problems through ‘power Africa project’ initiative and the Millennium Challenge Pact II that will support the development of infrastructure in the water and transport sectors as well as numerous initiatives in the health sector through its donor agencies. 
   The CEOrt is a leading private sector forum in Tanzania. The forum constructively engages the Government and other stakeholders in creating a more conducive environment for businesses to prosper and contribute to economic growth for the country. 
  The forum has over 80 leading companies who account for more than 40% of the total tax revenue collected by the government.
  Ambassador Mwanaidi Sinare Majaar of Rex Attorneys and member of the CEORT chats with US Ambassador Alfonso Lenhardt during the CEOrt farewell reception held recently. The CEORT thanked the ambassador, for his role in supporting and promoting Tanzania’s economic growth by providing unique partnership opportunities for businesses in Tanzania during his tenure.
  Leonard Mususa Country Representative of pwc Tanzania and board member of CEORT, Jackie Lenhardt and Ambassador Alfonso E. Lenhardt listen to Ali Mufuruki (not in picture) during the farewell reception for the US ambassador held recently. The CEORT thanked the ambassador, for his role in supporting and promoting Tanzania’s economic growth by providing unique partnership opportunities for businesses in Tanzania during his tenure.
  Ali  Mufuruki, Chairman, of the CEORT appreciates Ambassador Alfonso E. Lenhardt  for his role in supporting and promoting  Tanzania’s economic growth by providing unique partnership opportunities for businesses in Tanzania during the farewell reception held recently for the US ambassador.
  Members of the Board of the CEORT – Yogesh Manek of MAC Group, Ali Mufuruki Chairman CEORT and Ambassador Ami Mpungwe present the Nyamwezi harp to Ambassador Alfonso E. Lenhardt during the farewell reception dinner held recently. The CEORT thanked the ambassador, for his role in supporting and promoting Tanzania’s economic growth by providing unique partnership opportunities for businesses in Tanzania during his tenure.

  0 0
 • 09/06/13--08:54: Article 20


older | 1 | .... | 248 | 249 | (Page 250) | 251 | 252 | .... | 3270 | newer