Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Yanga wafanya mkutano wao wa mwaka kwa mafanikio makubwa jijini dar leo.

$
0
0
 Wanachama wa timu ya Yanga kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu hiyo ya Yanga kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini  katika mechi yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao 3-2.
 Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo,maendeleo yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la katiba yao,masuala mbalimbali ya yanayohusiana na wanachama wao,ustawi wa wanachama wao,mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mbalimbali.
 Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
 Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Pichani kulia ni mchezaji wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa shukurani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.
 Pichani ni baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo. 
 Msanii mahiri wa kizazi kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.Picha zaidi bofya Jiachie Blog.

OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR YAWASILISHA MAONI KATIBA MPYA LEO

$
0
0
Katibu Mkuu Mstaafu Bw. Vincent Mrisho akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Jospeh Warioba na kushoto ni Mjumbe wa Tume Prof. Mwesiga Baregu.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Khalid Mohamed akiongea katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Katibu Mkuu huyo aliwasilisha maoni ya watumishi wa ofisi yake kuhusu Katiba Mpya.
Mkurugenzi wa Uratibu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Bw. Ahmad Kassim Haji akiongea katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Ofisi hiyo ya ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar iliwasilisha maoni ya watumishi wake kuhusu Katiba Mpya. kwa Tume.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Said akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume na ujumbe wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar uliowasilisha maoni ya watumishi wa ofisi hiyo kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi – Zitto Kabwe

New Arrivals! Wahi dukani Vazi

MASHINDANO YA KOMBE LA MEYA KINONDONI YAFUNGULIWA RASMI, MIKOCHENI WALALA 3-1 DHIDI YA KAWE

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akiwakagua wachezaji wa timu ya Mikocheni Warriors na wachezaji wa timu ya Kawe Kombaini wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Meya, Manispaa ya Kinondoni,jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meya wa Manispaa hiyo,Mh. Yusuph Mwenda.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yusuph Mwenda (kushoto) akimwongoza Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara (katikati), Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Fortunatus Fwema na viongozi wengine mara baada ya ukaguzi wa timu.
Golikipa wa Kawe Kombaini Simon Adamu akiudaka mpira huku wachezaji wa timu ya Mikochezni Warriors wakijiandaa kupiga goli. Kawe ilishinda magoli 3-1.
Mshambuliaji wa Kawe Kombaini, Hassan Ngonyani (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka beki Ally Ramadhan wa Mikocheni Warriors wakati wa mechi ya ufunguzi ya Kombe la Meya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kawe walishinda kwa magoli 3-1.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara akihutubia wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo. Kulia kwake ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordna Rugimbana (kuhoto kwake) na Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Mnyonge (kushoto).
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la Meya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na vyombo vya habari wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo.

Article 2

Kibonzo cha KP

BREAKING NYUUZZZZ.....: UKUTA WA STENDI YA MABASI UBUNGO WAANGUKIA MAGARI LEO

$
0
0
TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII ASUBUHI HII,INAELEZA KUWA SEHEMU YA UKUTA WA MAEGESHO YA MAGARI YA WATU WANAOSINDIKIZA ABIRIA KWENYE STENDI KUU YA MABASI YAENDAYO MIKOANI UBUNGO JIJINI DAR UMEANGUKA NA KUANGUKIA BAADHI YA MAGARI YA WATU YALIYOKUWA YAMEEGESHWA KATIKA SEHEMU HIYO.

HAIJAFAHAMIKA MARA MOJA CHANZO CHA KUANGUKA KWA UKUTA HUO NA HAKUNA MTU YEYOTE ALIEDHULIKA NA AJALI HIYO ZAIDI YA MAGARI HAYO KUHARIBIKA VIBAYA.

GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA ZAIDI HAPO BAADAE.


Sauti za Busara kicks off with Busara Xtra

$
0
0
Sauti za Busara music festival is taking a step back on the first day of the festival, February 14, in order to let Stone Town to shine. This is the first day of ‘Busara Xtra’ - a day where Stone Town businesses throw open their doors to display shows of art, drumming and dance classes, music, and a sunset reggae party.

The Sober House will hold a daily art exhibition at Livingstone’s Restaurant, starting on 14 February and continuing throughout the festival. The artwork of recovering addicts and alcoholics will be displayed at the exhibit, starting at 10:00 am. The toughest choice visitors will have to make is not whether to come a day early, but which event to go to first! The sunset reggae cruise starts at 4:00 pm at Kae Funk Michamvi. Zanzibar’s popular Nadi Ikhwan Safaa will be performing at NIS Club House at 4:00 pm the same day. No matter if your music style is old Taarab or new Sinachuki Kidumbak or anywhere in between, Stone Town has something for you with Busara Xtra.

Festival Director Yusuf Mahmoud says that the festival has always made it a point to benefit Zanzibaris. Since the festival began in 2004 the number of visitors to Zanzibar in February has gone up by 500%.

By training and employing local people and drawing so many visitors to the island each year, Sauti za Busara helps the people of Zanzibar. Busara Xtra is another way the festival contributes to the economic and cultural life of the island.“Busara Xtra increases opportunities for regional artists to showcase their work, for visitors to see different parts of the island, meet local people and widen participation in the festival by local communities in Zanzibar,” said Mahmoud.


After warming up for the festival with Busara Xtra, Sauti za Busara’s main stage opens on 15 February and hosts performers until 17 February, 2013. The Busara Film Programme will show three films that complement the music on the main stage.


The amphitheatre of the Old Fort will be transformed into an open air cinema where popular music videos will be displayed as well as the three feature length films. For more information or to purchase tickets online, please visit www.busaramusic.org or purchase tickets at the door starting on 13 February, 2013. Tickets are Tsh 3,000/- for Tanzanians with special rates for East African residents.

With special thanks to Sauti za Busara sponsors: HIVOS, Goethe Institute, Grand Malt, Memories of Zanzibar, Diamond Trust Bank, ChemiCotex, Azam Marine, Ultimate Security, Zanzibar Unique Ltd., Southern Sun, Embassy of France, Alliance Française, SMOLE II and all of our sponsors and supporters.

KATIBU MKUU WA CCM AKUTANA NA MABALOZI WA RWANADA, CONGO DRC JIJINI DAR LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Juma Mpango aliyefika ofini kwa Karibu Mkuu leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Rwanda, Dk. Ben Rugangizi aliyemtembelea ofisini kwake, leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, (Picha zote na Bashir Nkoromo).

Makatibu wa Bunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola Afrika wakutana Kampala,Uganda

$
0
0
Makatibu wa Bunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika mwishoni mwa wiki wamekutana Kampala,Uganda kupitia Kanuni za vikao vyao pamoja na Mpango Mkakati wa Kundi lao ambalo ni moja ya vitengo vya Chama cha Wabunge wa Jmuiya ya Madola Kanda ya Afrika. Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Makatibu wa Mabunge ya Ghana, Botswana,Uganda,Nigeria, Kenya,Afrika Kusini na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Sekretarieti ya Chama hicho iliwakilishwa na Nd. Saidi Yakubu (kwanza kushoto waliosimama) na Nd. Demetrius Mgalami (wa tatu kushoto waliokaa) na Nd. Hassan Amour wa Baraza la Wawakilishi (wa tatu kushoto waliosimama). PICHA KWA HISANI YA SEKRETARIETI YA CPA KANDA YA AFRIKA.

Moto wazuka katika moja ya Nyumba,Mji Mkongwe Zanzibar leo

$
0
0
Moto mkubwa umezuka mchana wa leo katika moja ya nyumba zilizopo maeneo ya mji Mkongwe Zanzibar karibu maskani ya Lebanon na kusababisha hasara kubwa ambayo mpaka sasa bado tathimini yake haijafahamika.Pichani ni baadhi ya majirani wa nyumba hiyo wakionekana kusaidia kuuzima moto huo.
Baadhi ya wakazi nyumba hiyo wakiwa wamepanda juu ya paa la nyumba na kuifia kuangalia tu moto huo ukiendelea kuwaka mara baada ya zoezi la kuuzima kushindikana kutokana na namna miundombinu ilivyo katika eneo hilo.Picha na mdau Sabry Juma,Zanzibar.

RAIS KIKWETE APOKELEWA RASMI NCHINI UFARANSA NA RAIS FRANCOIS HOLLANDE

$
0
0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
 Gari iliyomchukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiondoka Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika maongezi rasmi na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa na ujumbe wake  katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.PICHA NA IKULU

wachimbaji wadogo wa madini wilayani ruangwa wapewa somo

$
0
0
Kaimu Kamishina Msaidizi wa Uendelezaji Uchimbaji Mdogo Bw.Julius Sarota akitoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu elimu ya biashara na ujasiriamali iliyofanyika wilayani Ruangwa,Mkoani Lindi leo.
Mhandisi Migodi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Jones Mushi akitoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu utunzaji kumbukumbu, uwasilishaji wa taarifa na ulipaji kodi na tozo mbalimbali kwa wachimbaji wadogo.

Mmoja wa wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo akionesha cheti cha ushiriki wa mafunzo kuhusu sekta ya Madini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wilayani Ruangwa wakisikiliza moja ya mada zilizokuwa zikitolewa.

Changamoto za uendeshaji wa meli MV. Victoria ziwa Victoria

$
0
0
Ankal, Wawekee wadau waweze kuiona meli hii ambayo ni Mojawapo ya meli kongwe hapa nchini,Hii ni Meli ya MV. Victoria inayosafiri kati ya jiji la Mwanza na mji wa Bukoba, MV. Victoria ambayo ilianzarasmi kufanya kazi mwaka 1962 na bado inadunda mpaka leo pamoja na changamoto nyingi, tuangalie video ya hali halisi ya uendeshaji wake.

Article 17

January Night Skies over Tanzania

MH. SAMUEL SITTA, OFISI YA MWANASHERIA MKUU, TUME YA KUREKEBISHA SHERIA NA WAZEE WATOA MAONI KATIBA MPYA LEO

$
0
0
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Kushoto ni Mjumbe wa Tume Bi. Maria Kashonda.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Samwel Sitta (katikati) akiagana na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) na Bw. Nassoro Mohammed (kulia) mara baada kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Mashtaka Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (jumatatu januari 21, 2013) jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju na Wajumbe wa Tume Bw. Humphery Polepole na Bw. Awadhi Said.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo cha utafiti cha Tume kwa ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) ulioongozwa na Makamishina wa Tume hiyo, Jaji Ernest Mwipopo (wa tatu kulia) na Bi. Esther Manyesha (wa nne kulia). LRCT imewasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya kwa Tume leo
Kamishina wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) Jaji Ernest Mwipopo akikabidhi maoni ya LRCT hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Katikani ni Mjumbe wa Tume Bw. Simai Mohammed.
Mjumbe wa Mtandao wa Kinga Jamii (TPSN - Tanzania Social Protection Network) Bi. Clotilda Isdor akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko uliofanyika leo (jumatatu janauari, 21, 2013). Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume, Bi. Mwatumu Malale.

BALOZI KAGASHEKI APOKEA UJUMBE KUTOKA TAASISI YA JANE GOODALL

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (kushoto) akipata ufafanuzi kutoka kwa Bi. Jane Goodall mwanzilishi wa Taasisi ya Jane Goodall inayotambulika duniani kwa mchango wake wa kuhifadhi wanyama aina ya Sokwe katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe. Kulia ni mmoja wa wataalam wa Taasisi hiyo, Bw. David Shear.
Mhe Balozi Khamis Kagasheki akiagana na mgeni wake Bi. Jane Goodall.

Hatimae Bi Arafa Afanyiwa Upasuaji na anaendelea vema katika hospital ya Muhimbili

$
0
0
Kwa Niaba ya Familia ya Bi Arafa (Pichani) Napenda kutoa shukrani za Dhati kwa wale wote ambao waliguswa na hali ya Mgonjwa huyu na kuridhia kumchangia ili kumtoa wilayani Ruangwa na kuwezesha kumfikisha katika Hospital ya Muhimbili Mwezi Nov 2012 na juzi kufanyiwa Upasuaji.

Hali ya Mgonjwa huyu inaendelea vema katika hospital ya Muhimbili akisubiria kutoa Nyuzi

Mungu aliwawezesha na kumsaidia mpaka hali ilivyofikia sasa na Kubwa Nawaomba Muendelee kumuombea Dua ili aweze kupona na kuendelea kujitafutia riziki ya kila siku

Ahsanteni sana.
Ni Mimi Abdulaziz Ahmeid Video

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images