Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Tony Elumelu Foundation to Launch World’s Largest Digital Platform for African Entrepreneurs at TEF Forum 2018

$
0
0
Africa’s leading entrepreneurship focused philanthropy, The Tony Elumelu Foundation, is launching the world’s largest digital platform for African entrepreneurs and the African entrepreneurship ecosystem –  TEFConnect.

TEFConnect will officially be unveiled at this year’s TEF Forum, taking place on October 25, 2018, at Federal Palace Hotel, Lagos, Nigeria.

Harnessing and building on the success of Africa’s largest entrepreneurship catalyst, the Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme, which has attracted over 300,000 African entrepreneurs as applicants and trained and funded 4,460 to date, the Foundation is further democratising access to opportunity. TEFConnect is an open source platform, which will provide bespoke tools and content to catalyse business development for millions across the continent, through technology and directly applicable content.

Positioned as the “Facebook for African Entrepreneurs”, the TEFConnect platform is a contemporary, intuitive, informative and user-friendly go-to entrepreneurship space, that provides five specific benefits to its users, among others:

  • The one-stop digital home for entrepreneurship ecosystem players, including entrepreneurs, incubators, investors, academia and the private sector, providing news, informative resources, entrepreneurship events and opportunities.

  • Creating the space to allow African entrepreneurs to transact across countries and regions in Africa's largest digital marketplace, with traffic reaching millions of consumers.

  • Access to free business tools such as financial planning calculators, business plan generators and marketing templates.

  • Access to the Foundation’s Entrepreneurship Programme Application Form, Enterprise Toolkit and business mentoring by global business leaders.

  • Enabling entrepreneurs to promote their businesses to potential investors and other entrepreneurs for cross-border collaboration.

Speaking on the launch of TEFConnect, the CEO of the Foundation, Parminder Vir OBE said: “The Tony Elumelu Foundation is simply about empowering African entrepreneurs. First, we launched the TEF Entrepreneurship Programme, to provde 10,000 African entrepreneurs, over a period of 10 years with seed capital, mentorship and training. Next, we convened the full entrepreneurial ecosystem at the TEF Forum to forment engagement and deliberate discussions to change the narrative of Africa. Now, we are scaling our impact by connecting African entrepreneurship ecosystem on a single platform.”

The Founder of the Tony Elumelu Foundation, Tony O. Elumelu, CON also said: “In the four years, since the launch of the TEF Entrepreneurship Programme, we have shown that entrepreneurship can change a continent – we have invested in people and processes. We have already helped create business successes and brought policy makers into the entrepreneurial dynamic.  But in many ways, we are scratching the surface. This year we are broadening our scope, taking the conversation to where interaction is increasingly occurring – the digital realm. By connecting African entrepreneurs globally on TEFConnect, we are further unleashing the true potential of our entrepreneurs and transforming the continent”.

The 4th TEF Forum will convene Africa’s entrepreneurial ecosystem, including the broad investor community, government and policymakers, leading developmental organisations, private sector representatives, the media and partners.

This year’s Forum will also feature an interactive dialogue between the President of Ghana, HE Nana Akufo-Addo and President of Kenya, HE Uhuru Kenyatta, moderated by TEF Founder, Tony Elumelu.

To attend the TEF Forum or watch the unveil of TEFConnect live, click here:www.tonyelumelufoundation.org/tef-forum2018


MARUFUKU KAMPUNI ZA UPIMAJI ARDHI BINAFSI KUPIMA ARDHI ZA WANANCHI BILA WAKUU WA WILAYA KUJUA

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Tabora katika viwanja vya Chipukizi kabla ya kuanza kutatua igogoro ya ardhi zao jana.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Bosco Nduguru akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi(hayupo katika picha)  wakati wa  ziara ya siku moja ya kiongozi huyo ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo jana.
 Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora ambao wana matatizo katika ardhi wakisubiri kukutana na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (hayupo katika picha ) ili asikilize shida zao wakati wa  ziara ya siku moja ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo jana.
picha na Tiganya Vincent


NA TIGANYA VINCENT- RS TABORA
SERIKALI imepiga marufuku kampuni binafisi za upimaji ardhi  ambazo zimekuwa zikiingia makubaliano ya upimaji ardhi za wananachi bila hata uongozi wa Wilaya husika kuwa na taarifa juu ya uwepo wa zoezi hili hali ambayo imesababisha baadhi ya wananchi kuwadhulumu fedha zao.

Agizo hili lilitolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi baada ya wakazi wa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Tabora kuilalamikia Kampuni ya Ardhi Plan kuwachangisha fedha zao bila ya kupimia ardhi yao.

Alisema kuanzia sasa nchini kote hakuna Kampuni ya aina yoyote binafsi kwenda na kuingia moja kwa moja makubaliano na wananchi ya kuwapimia maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya husika.

Lukuvi alisema Kampuni za aina hiyo zimekuwa zikiwachangisha fedha na kugawana mapato bila hata ya kuwapimia wananchi huku uongozi wa Wilaya husika hauna hata taarifa.

Alisema haiwezekani upimaji wa ardhi za wanyonge ukageuza uchochoro wa kuwaibia na kuwadhulumu wananachi haki zao na kuongeza kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe katika upimaji wa ardhi za wananchi na taarifa ziwe kwa Wakuu wa Wilaya.

Aidha Waziri huyo alizitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia Chuo cha Ardhi Tabora na kuachana na Kampuni za nje kupima ardhi ili kuepuka matumizi makubwa ya gharama za zoezi hilo.

Alisema hakuna sababu ya Tabora kuendelea kuwa na maeneo ambayo yanajengwa kiholela holela wakati wanao wataalamu katika Chuo cha Ardhi ambao wameshindwa kuwatumia.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Lukuvi alizitaka Taasisi zote za Umma kuhakikisha maeneo yao wanayomiliki yamepima na wanazo hati kabla ya kumalizika kwa mwa mwaka huu.

Alisema baada ya kupima wanatakiwa kuweka alama katika mipaka ya maeneo yao ili kuepuka wananchi kuyavamia na kujenga na kusababisha migogoro ambayo inaweza kuzuilika.

Wakati huo huo Lukuvi ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanakamilisha uandaaji wa hati miliki za  viwanja 938 katika eneo la Malabi na kuwakabidhi wamiliki wake kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.
Alisema hatua ya kuendelea kukaa na viwanja hivyo bila kutoa hati kwa wahusika kwa miaka mitatu iliyopita kumesababishia hasara Serikali ya kukosa kodi ya ardhi kutoka kwa wahusika.

Waziri huyo aliwataka wakazi wa Malabi kuanzia Jumatatu ijayo ambao wameshipimiwa maeneo yao kwenda kuviripia ili hatimaye wapate hati.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alikuwa katika ziara ya siku moja ya kutatua migogoro ya ardhi ambapo alifanikiwa kusikiliza migogoro ardhi zaidi ya 540 na kuipatai majibu.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 21.09.2018

BURIANI MFALME WA ROOTS ROCK REGGAE WA TANZANIA JAH KIMBUTE

$
0
0

 Sehemu ya marafiki wa karibu wa Jah Kimbute wakiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Ijumaa jioni kuuaga mwili wa marehemu kabla ya kupelekwa Tanga kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Septemba 22, 2018
 Marafiki wakiaga mwili wa Jah Kimbute
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Jah Kimbute likiingizwa garini tayari kwa safari ya kwenda Tanga kwenye mazishi
 Marafiki wa karibu wa Jah Kimbute wakiomba dua katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Ijumaa jioni baada ya kuuaga mwili wa marehemu kabla ya kupelekwa Tanga kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Septemba 22, 2018
Gotta Irie, Dj Ebony Moualim na Carola Kinasha wakimfariji Ras Kimbute, mtoto wa Jah Kimbute,  kabla ya kuanza safari ya kwenda Tanga.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MSIKILIZE MFALME WA ROOTS ROCK REGGAE WA TANZANIA MAREHEMU JAH KIMBUTE

Waziri Mkuu Majaliwa Awasili Eneo la ajali ya kivuko cha MV Nyerere

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA ENEO LA AJALI YA KIVUKO KATIKA KISIWA CHA UKARA, MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (katikati) na Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kuelekea katika eneo kilipozama Kivuko cha MV Nyerere katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 21, 2018. Kivuko hicho kinatoa huduma kati ya Kisiwa cha Ukara ba JKisiwa cha Bugorola. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo kilipozama Kivuko cha Mv Nyerere kinachotoa huduma kati ya kisiwa cha Ukara na Bugorola wilayani Ukerewe wakati alipowasili kwenye kisiwa cha Ukara kujionea shughuli za uokoaji Septemba 21, 2018.

MV Nyerere -LupaHero Kijana Wa Kitamaduni -Makeke African Brand


MKANDARASI WA MRADI WA MAJI PANGANI ATAKIWA KUUMALIZA KWA WAKATI

$
0
0

 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani[CCM akizungumza katika mkutano wa hadhara eneo sokoni wilayani Pangani kabla ya kushuhudia utiliaji wa saini ya mkataba wa maji kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo baina ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) wilayani hapo.
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) Phares Aram kushoto akisaini  hati za mkataba wa maji na Mkandarasi a Mkurugenzi wa Kampuni ya Macarious Hotel and Co.Ltd Filbert Mmassy kulia ambaye atatekeleza mradi wa maji wilayani Pangani wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

$
0
0
Uongozi na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ( Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) tunaungana na ndugu, jamaa na Watanzania wote katika kuombeleza msiba mzito kwa Taifa baada ya ndugu zetu wapendwa kupoteza maisha katika ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea katika Ziwa Victoria, tarehe 20 Septemba, 2018.

Tunatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu na tunawaombea majeruhi wote wapone haraka.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
22/09/2018

TRC YAAHIDI KUSAIDIA MAENDELEO YA ELIMU WILAYA YA KISARAWE MKOANI PWANI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jockate Mwegelo (wa nne kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (wa tatu kulia), wafanyakazi wa Wilaya ya Kisarawe, TRC pamoja na wawakilishi kutoka Mkandarasi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR Yapi Merkezi wakijadili namna ambavyo wanaweza kusaidia maendeleo ya Elimu wilayani Kisarawe katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Septemba 22. 2018. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kadogosa (kulia) kwa niaba ya TRC akimuahidi mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (kushoto) kujenga Madarasa na kuchangia Vyakula ikiwemo Maharage, Mchele na Mafuta ya kupikia kwa wanafunzi walio kambini wakati wa Harambee ya kuchangia maendeleo ya Elimu katika Kampeni ya 'Tokomeza Ziro' iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Septemba 22, 2018.
 Picha ya pamoja baada ya mazungumzo

MWENGE WAZINDUA MRADI WA MAJI AYAMOHE

$
0
0


Zaidi ya asilimia 50 ya wakazi 8,000 wa Kata ya Ayamohe Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, waliokuwa hawapati maji safi na salama kutokana na kutokuwa na miundombinu ya usambazaji wa maji ya uhakika wamefanikiwa kuondokana na adha hiyo baada ya mradi wa maji kuzinduliwa. Akisoma taarifa ya mradi huo wa maji jana kwenye mbio za mwenge wa uhuru, ofisa mtendaji wa kata ya Ayamohe John Tluway alisema mradi huo umegharimu sh388 milioni. 
 
Tluway alisema serikali kuu imechangia sh322 milioni, halmashauri ya mji sh19 milioni na serikali ya mtaa imechangia sh46 milioni kwa kutoa ardhi na kushiriki kwenye uchimbaji mtaro na ulazaji mabomba ya kilomita 15.
Alisema baada ya kukamilika kwa mradi huo wananchi wa eneo hilo hivi sasa watapata huduma ya maji tofauti na awali walikuwa wanatembea umbali wa kilomita mbili kufuata huduma hiyo. 
 
“Lengo la mradi ni kusogeza huduma ya maji karibu na na wananchi wa kata ya Ayamohe na mitaa ya jirani inayowazunguka ili kuondoa upungufu mkubwa wa maji unaosababishwa na ongezeko la wakazi,” alisema Tluway. 
Awali, mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akisoma taarifa ya halmashauri ya mji wa Mbulu alisema mwenge wa uhuru utatembea miradi sita ya thamani ya sh1.1 bilioni. 
 
Mofuga alisema mwenge utafungua mradi wa maji Ayamohe, uzinduzi wa kikundi cha wanawake cha unenepeshaji ng’ombe na uzinduzi wa kiwanda cha usindikaji wa mikate na biskuti. Alisema pia utakagua shughuli za klabu ya wapinga rushwa shule ya sekondari Daudi, kuweka jiwe la msingi kituo cha afya Daudi ufunguzi wa vyumba vinne vya madarasa na choo cha wanafunzi na uzinduzi wa daraja la Endamaksi. 
 
Mmoja kati ya wakazi wa Ayamohe Jane Bayo alisema mradi huo wa maji utawanufaisha wananchi wa eneo hilo waliokuwa wanatembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma hiyo. Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2018 Charles Kabeho aliipongeza halmashauri ya mji huo kwa kutekeleza mradi huo kwani wamefanikiwa kumtwika mama ndo ya maji. 
 Askari upelelezi wa kituo cha polisi Mbulu, Gloria Nasson akielezea madhara ya matumizi ya dawa za kulevya huku akiwa ameshikilia bangi wakati mwenge wa uhuru ulipotembelea banda la polisi, kushoto ni Mkuu wa kituo cha polisi Mbulu, Amiry Mlemba.
IMG-20180920-WA0171
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Charles Kabeho akitambulishwa kwa Mkurugenzi wa Mji wa Mbulu, Anna Mbogo na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga. 
IMG-20180920-WA0069
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Charles Kabeho akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha usindikaji wa mikate na biskuti kwenye mtaa wa Gwandumehi Halmashauri ya Mji wa Mbulu. 
IMG-20180920-WA0163
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho akizindua kituo cha afya Daudi Halmashauri ya Mji wa Mbulu. 

WAJUMBE WA BODI YA ZABUNI WIZARA YA MADINI WATAKIWA KUEPUSHA HOJA ZA MANUNUZI

$
0
0


Na Asteria Muhozya, Morogoro

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini kuhakikisha kwamba wizara hiyo haipati hoja kutokana na kukikukwa kwa taratibu za manunuzi baada ya wajumbe hao kupatiwa mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

Pia, wajumbe hao wametakiwa kuhakikisha wanafamu kwa weledi Sheria na Kanuni za manunuzi ili waweze kutoa maamuzi sahihi.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika ofisi za Madini Mkoa Morogoro tarehe 21 Septemba,2018.

Naibu Waziri Nyongo alisema hitaji la kuwapatia mafunzo wajumbe hao linafuatia upya wa wizara hiyo ikiwemo wajumbe wa bodi hiyo ambao wengine wametoka katika sekta mbalimbali hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi zilizoanishwa.

“Masuala ya manunuzi yanalalamikiwa sana kutokana na ucheleweshaji wa maamuzi. Lakini pia, manunuzi ya umma yamekuwa na matatizo kutokana na kuwepo Mikataba mibovu kwa hiyo baada ya ninyi kupatiwa mafunzo haya, sitarajii vitu kama hivi kujitokeza. Pia, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wajumbe wa bodi kuhakikisha kuwa, mafunzo waliyoyapata yanawasaidia kuepukana na vitendo vya rushwa wakati wa kusimamia shughuli za manunuzi ya wizara.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi 

NAIBU WAZIRI NDITIYE APOKEA MAONI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA UTUNGAJI KANUNI ZA MIUNDOMBINU YA KIMKAKATI YA MAWASILIANO

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amepokea maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo 

Nditiye amewaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeona ni vema iwasilishe rasimu ya kanuni hizo ili ziweze kupata maoni ya wajumbe hao kwa kuwa mawasiliano ni suala la muungano. 

Aidha, amefafanua kuwa wajumbe walishiriki na kutoa maoni yao wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walishirikiana kutunga Sheria iliyoanzisha Shirika la Mawasiliano Tanzania na kufuta Kampuni ya Simu Tanzani ili kuiwezesha Serikali kumiliki Shirika hilo kwa asilimia 100 na liweze kujiendesha kwa faida kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa letu na ulinzi na usalama ambapo Shirika limeweza kutoa gawio kwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa Serikali.

Mhandisi Nditiye amewashukuru wajumbe wa Baraza hilo kwa ushirikiano wao wakati wa utungaji wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo Serikali imezingatia na kutekeleza maoni waliyoyatoa wakati wa utungaji wa sheria hiyo ikiwemo suala la uwakilishi wa Zanzibar kwenye Bodi ya Shirika na Ofisi Zanzibar

Amefafanua kuwa katika kifungu cha 7 (2) (b) cha sheria ya Shirika hilo, sheria imeelekeza wazi kuwa lazima wajumbe wawili wa Bodi ya Shirika watoke Zanzibar na muundo wa Shirika umezingatia uwepo wa Ofisi ya Shirika Zanzibar badala ya kuwa na tawi tu.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akifafanua jambo kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza hilo ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. 
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Ahmed Salum wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma (wa kwanza kushoto) akitoa maoni yake wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza hilo ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe. Mgeni Hassan Juma. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisikiliza kwa makini wasilisho na maoni ya wajumbe wa Baraza hilo wakati wa kikao cha kupokea maoni yao ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakisikiliza kwa makini maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar ya rasimu ya Kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo. 


Waziri Ummy avipongeza viwanja vya ndege kudhibiti Ebola

$
0
0


WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kuchukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, imeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu katika hotuba yake kwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini yaliyoanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo imesharipotiwa ugonjwa huo umeingia nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Mhe. Mwalimu amesema TAA inafanya jambo jema kwa kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege wanafanyiwa ukaguzi na kutoa taarifa za afya zao kwa wale ambao watabainika kuwa na joto la mwili lisilokuwa la kawaida.

“Nawapongeza sana tena sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama bila kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa Ebola, imeripotiwa sasa huu ugonjwa upo Kivu Kaskazini, ambapo ni karibu na nchini na Wavuvi wanakuwa na muingiliano kwa kutoka huko na kuja nchini,” amesema Mhe. Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akiongea na wananchi walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
DSC_0783Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akikata utepe kuzindua kitabu cha mpango mkakati wa udhibiti wa ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, baada ya kufanya Matembezi ya Hiyari yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa Ebola.
DSC_2006Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela akiongea na wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa kuanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Viwanja vya Karimjee.
DSC_0608Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (watatu kulia) leo akiongoza Matembezi ya Hiyari kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mohamed Kambi.
DSC_1935Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa miongoni mwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


MUME AMUUWA MKEWE NA KUMFUKIA HUKO MKURANGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

KATIKA hali ya kustaajabisha mkazi mmoja katika kijiji cha Magoza Wilayani Mkuranga amemuua mkewe na kumfukia.

Imeelezwa kuwa katika  kijiji cha magoza  Kata ya Kiparang'anda Wilayani Mkuranga  Selemani Juma amemuua mkewe Bi Selina Sulubu kwa madai ya mgogoro wa mapenzi uliodumu kwa muda mrefu na kisha kumfukia kwa siri katika shamba la jirani yake.

Tukio hilo limebainika leo baada ya siku kumi kupita tangu kufukiwa kwa mwili huo.

Michuzi blog ilifika eneo la tukio na kushuhudia jeshi la polisi kwa kushirikiana na wataalam wa afya  kutoka hospitali ya Wilaya na wananchi wakifukua mwili wa marehemu.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkuranga Dkt. Steven Mwandambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  kwa kuuona mwili wa marehemu na wamekabidhi jeshi la polisi ili waweze kuendelea na hatua nyingine.

Aidha kaka wa marehemu  bahati Mabubu amesema; baada ya kupata taarifa kwa shemeji yake kuhusu kutoroka kwa dada yake nyumbani aliamua kufunga safari kuja Mkuranga ili kumtafuta dada yake.

Mabubu ameongeza kuwa alipofika Mkuranga katika kijiji cha magoza alibaini shemeji ya kuwa na hali ya wasiwasi,ndipo alipompeleka kituo cha polisi na kukiri kufanya mauji ya mke wake.

Ikumbukwe kuwa ni miezi minne tu imepita tangu kutokea kwa mauaji ya nesi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga yaliyosabishwa na wivu wa mapenzi kutoka katika wilaya ya Mkuranga.
Polisi na wataalamu wa afya kwa kushirikiana na wananchi wakisaidiana kufukua mwili wa Selina Sulubu aliyeuwawa na mumewe katika kata ya Kiparang`anda Wilaya ya Mkuranga mkoa Pwani. (picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Polisi,wataalamu wa afya kwa kushirikiana na wananchi wakibeba mwili.

WAZIRI KANGI LUGOLA AAGIZA WANAOSAMBAZA PICHA ZA WATU WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA KIVUKO WASHUGHULIKIWE

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watu wanaosambaza picha za watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea juzi Septemba 20,2018.

Waziri Lugola ameviagiza vyombo vinavyohusika kufuatilia wanaosambaza picha hizo kwa ni kinyume cha sheria za makosa ya mtandao.

Tangu jana kumezuka tabia kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp,instagram na facebook wamekuwa wakisambaza picha za watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye magroup na wengine kupost kwenye kurasa zao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,utu na maadili.

WAFAMASIA WAOMBOLEZA MAAFA YA AJALI YA KIVUKO CHA MV. NYERERE

$
0
0
CHAMA CHA WAFAMASIA TANZANIA
Uongozi na wanachama wa Chama cha Wafamasia
Tanzania unatoa pole
kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa. Dkt. John Pombe
Magufuli, ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa
ujumla kwa msiba mkubwa
uliotokea kutokana na ajali ya kivuko cha Mv.
Nyerere katika ziwa
Victoria, tarehe 20.09.2018.
Tunawaombea majeruhi
wapone haraka na
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.
AMINA
Imetolewa na
Rais wa Chama cha Wafamasia Tanzania (PST)
Wafamasia: Wataalamu wako wa dawa

MV NYERERE BY DELTA MUSIC

$
0
0
ARTISTS: Delta Music_ft_ Chombaa, Fortune Bello, Akali, Mansizi, Mediking, Pradeta, Kodo
SONG: MV Nyerere
STUDIOS: Delta Music
PRODUCER: H Pol 
Contacts: +255 683 538 189 (Mbudu Theboss)
Studio Manager

African Court mourns loss of lives in tragic MV Nyerere ferry disaster

$
0
0
The African Court is mourning: The flag of Tanzania is flying half-mast at the African Union‘s Judicial Organ in Arusha to join Tanzanians in mourning the tragic loss of over 200 lives following the capsizing of MV Nyerere in Lake Victoria on Thursday (Picture a Correspondent).
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images