Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

0
0
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Idara ya Udhibiti hali hatarishi, Anderson Mlabwa akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Benki hiyo juu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea, yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji nchini, Kamshna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto, Bakari Mrisho na kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kitengo cha Uendelezaji wa Biashara, Eng. Misana Mutani
 Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji nchini, Kamshna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto, Bakari Mrisho akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Benki hiyo juu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea, yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Pendo Assey (kulia) pamoja na Meneje wa Benki ya CRDB Tawi la Viva Premier Club, Naomi Mwamfupe (kushoto) wakishirikiana kuzima moto wakati wa mafunzo ya vitendo ya uzimaji moto, yaliyokuwa yakitolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi akionyesha namna ya kuzima moto kwa kutumia kifaa maalum cha kuzimia moto kwa majumbani.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango akizima moto wakati wa mafunzo ya vitendo ya uzimaji moto, yaliyokuwa yakitolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam. 


BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 19.09.2018

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI SEPTEMBA 20, 2018

YANGA YAVUNA POINTI 3, MAKAMBO AFUNGA GOLI LA USHINDI

0
0
Na Agnes Francis, Globu ya Jamii.

Mabingwa wa kihistoria ligi kuu Tanzania Bara Yanga Sc wametoka kifua mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wagosi wa kaya Coastal Union katika dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 


Kipindi cha kwanza cha Mpira dakika 45 kilianza kwa kasi huku kila timu ikiitaji alama 3 kwa kulisakama lango la mwenzake. 

Katika kipindi cha kwanza dakika 11 mshambuliaji wa Yanga raia wa Kongo Heritie Makambo akaiandikia timu yake bao la kuongoza akipokea kwa pasi mujarabu iliyotolewa na Ibrahim Ajibu,na mpaka kipindi cha kwanza kimemalizika Coastal hawakupata goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila upande kulisakama lango la mwenzake na kushambuliana kwa zamu huku Coastal Union wakilishambulia lango la Yanga kutafuta goli la kusawazisha,ambapo Yanga walionekana kuridhizika na matokeo hayo. 

Lakini Dakika za lala salama mchezo uligeuka kwa Yanga ambapo walionyesha kuamka kwa kuwashambia wapinzani wao kwa kulenga mashuti yasiokuwa na madhara kwa Coastal na mpaka Dakika 90 za mchezo matokeo ni 1-0. 

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mazoezi ndio siri inayowafanya kushinda mechi zote mfululizo bila kupoteza mchezo hata mmoja. 

"Tatizo la wachezaji wangu wakishafunga goli huwa wanapotea mchezoni na hawafanyi vizuri kila mmoja anafanya anavyojua yeye"amesema kocha Zahera. 

Kocha wa Coastal Union Juma mgunda amezungumza na waandishi wa habari amesema kuwa watayafanyia kazi makosa waliyoyafanya mpaka kupelekea kikosi cha Yanga watumie nafasi hiyo kupata goli la kuongoza. 

Mgunda amelizungumzia swala la kuhusu kucheza kwa mchezaji wao Ali Kiba ambaye pia ni mwanamuziki wa bongo fleva hapa nchini kutokucheza tangu kuanza kwa ligi hiyo. 

"Ali ni mchezaji wetu Kama wechezaji wengine ikifikia muda wake nitamchezesha na kuitumikia timu yake". 

Yanga anaongoza ligi kuu Tanzania bara kwa alama 9 akiwa na magoli 7 ambapo amecheza michezo 3,atashuka tena dimbani septemba 23 kuwakaribisha Singida United uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Coastal Union kilichopambana na Yanga.

Kikosi cha Yanga kilichopambana na Coastal Union,
Kiungo wa Coastal Union Hassan Hamis akijaribu kumtoka Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa goli 1-0 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. 
Kiungo wa Yanga Pappy Tshishimbi akimtoka beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa goli 1-0 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. 
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Kongo Heritie Makambo akishangilia goli baada ya kufunga dakika ya 11 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa goli 1-0 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. 

Jalada la kesi ya Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa TAZAMA lipo kwa DPP

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya  Uhujumu Uchumi dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama), Samwel Nyakirang'ani na wenzake, umeieleza mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo lipo kwa (DPP), kwa ajili ya kulipitia na kulifanyia uchambuzi.

Imedaiwa, DPP analichambua kwa ajili ya kuangalia washtakiwa gani washtakiwe na washtakiwa gani waachiwe huru.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Patrick Mwita, ameeleza hayo leo Septemba 19, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai, amewasiliana na wenzake na  wamemueleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uchambuzi, akaiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi tarehe nyingine

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote , aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha zoezi la uchambuzi ili haki iweze kupatikana.

kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 3, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa na kuangalia kama uchambuzi huo umekamilika.

washtakiwa  wengine katika kesi  hiyo ni Nyangi Mataro mwalimu wa shule ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Mfanyabaishara, Farijia Ahmed mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias, mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus, mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko, mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick, mkazi wa Tungi Kigamboni.

Wengine ni Audai Ismail ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa  kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.

Inadaiwa, kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 huko Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja walijiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Bandari nchini(TPA).

Pia wanadaiwa  kutoboa  bomba  hilo ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta,  mali ya (TPA).

Aidha wanadaiwa kuharibu  bomba la mafuta mazito lenye upana wa Inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya (TPA).

NHIF TABORA YALIPA BILIONI 3.8 KWA WATOA HUDUMA KATIKA MWAKA WA FEDHA ULIOPITA

0
0
Na Tiganya Vincent
 
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Mkoa wa Tabora umelipa jumla ya bilioni 3.8 kwa watoa huduma mbalimbali mkoani humo katika mwaka wa fedha uliopita.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Jacob Mwailubi wakati wa mkutano wa wadau wa afya wa Mkoa huo.

Alisema vituo vya Serikali vimelipwa bilioni 1.021 , watoa huduma wa binafsi bilioni 1.246 na Vituo vya Taasisi za dini vimelipwa kiasi bilioni 1.566.

Aidha Mwailubi alisema NHIF mkoani humo imefanikiwa kusajili wanachama wapya 3,063 katika mwaka wa fedha uliopita na kuufanya ufikishe wanachama  20,400.

Mwailubi alisema kati yao watumishi wa umma ni 16,938, Mashirika binafsi 307, wastaafu 175, Vyuo vya Elimu ya juu 2,131, Madiwani 268,Viongozi madhehebu ya dini 125, Wanachama binafsi 6 na Watoto chini ya miaka 18 ni  450.

Aidha alisema katika kipindi hicho Ofisi ya Mkoa ya NHIF iliweza kukusanya jumla ya milioni 645.9 kama michango ya wanachama  ambapo kati yake  milioni 325.3 ni michango toka taasisi za umma wakati milioni 320.6 ilikusanywa kutoka mashirika binafsi.

Hata hivyo alisema Halmashauri za Wilaya ya Tabora –Uyui, Igunga na Urambo hazijalipa malimbikizo ya michango ya Watumishi wanaolipwa kupitia mapato ya ndani ya jumla milioni 39.5.

Mwailubi alisema Halmashauri ya wilaya Tabora  inadaiwa shilingi milioni 1.6, Igunga milioni 28.2 na Urambo milioni 8.6.

Aliwahimiza michango hiyo ilipwe ili watumishi husika wapate huduma za matibabu.

Wakati huo huo Mwailubi alisema NHIF imesajili jumla ya Vituo vya Huduma za Afya  302 ambapo kati ya hivyo  vituo 243  vinavyomilikiwa na serikali, vituo 24 ni Taasisi na mashirika yasio ya serikali na  vituo 35 vinavyomilikiwa na watu binafsi yakiwemo maduka ya dawa.

WANAWAKE 46,158 WAMEJIFUNGUA TOKA JANUARI HADI SASA MKOANI TABORA

0
0
Na Tiganya Vincent
JUMLA ya wanawake 46,158 mkoani Tabora wamejifungua katika kipindi cha kuanzia Januari hadi kufikia Septemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu wa Afya wa Mkoa wa Tabora Tausi Yunge wakati wa mkutano wa wadau wa faya wa Mkoa huo.

Alisema walijifungua chini ya umri wa miaka 20 walikuwa 11,332 ambao ni sawa na asilimia 24.5 na wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya ishirini waliojifungua walikuwa 34,826 sawa na asilimia 75.4.

Tausi alisema watoto waliozaliwa wakiwa hai walikuwa 45,336 sawa na asilimia 98.7 na wasio hai walikuwa 563 sawa na asilimia 1.2.

Kaimu Katibu Afya Mkoa huyo alisema jumla ya wanawake waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma walikuwa ni 43,991 sawa na asilimia 95.3.

Wakati huo huo Kaimu Katibu huyo wa  Afya Mkoa amesema kuwa hadi hivi sasa ni Wazee 32,470 sawa na asilima 50 ya wazee 71,116 ya waliotambuliwa ndio wameshapewa vitambulisho kwa ajili ya matibabu mkoani humo.

Alisema ni Halmashauri  ya Wilaya ya Igunga ndio inaoongoza kwa kutoa kwa wazee 6,700  kati ya 9,766, kufuatiwa na Kaliua iliyotoa kwa wazee 3,700 kati ya 6,019, Uyui 4,000 kati ya 6,840  na Urambo imetoa kwa wazee 5,120 kati ya 9,387.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kushoto) akifungua mkutano wa wadau wa afya hivi karibuni mkoani humo. Wengine ni  Katibu Tawala Mkoa huo Msalika Makungu( kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala(wa pili kutoka kulia) na  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba(kulia)
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba akitoa mada kuhusu hali ya huduma ya afya mkoani humo  hivi karibuni wakati wa mkutano wa wadau wa afya.
 Kaimu Katibu wa Afya Mkoa wa Tabora Tausi Yunge akitoa takwimu za wanawake waliojifungua tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa wakati wa mkutano wa wadau wa afya mkoani humo. 
 Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa wadau wa afya mkoani Tabora wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha ) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo hivi karibuni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

POLISI ARUSHA WAFANIKIWA KUPATA GARI AINA YA TOYOTA SURF ILIYOIBIWA SEPTEMBA 17

0
0
Na Seif Mangwangi, Arusha
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kupata gari aina ya Toyota surf namba T996AGK, lililokuwa limeibiwa  Septemba 17, mwaka huu katika eneo la stand ndogo lilipokuwa limepakiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhan Ng'azi alisema dereva wa gari hilo Susan Cornel mwalimu wa shule ya msingi Maviluni Akeri alikuwa amepaki gari hilo na kuingia stand kwa ajili ya kufanya manunuzi.

Anasema aliporejea alikuta gari lake halipo ndipo akatoa taarifa polisi na wao kuanza harakati za kulisaka gari hilo kwa kuweka vizuizi maeneo mbalimbali na baadae kupata taarifa kuwa gari hilo limetelekezwa eneo la kituo cha afya Kaloleni.

Kamanda Ng'azi amesema jeshi hilo linaendelea kuchukua alama mbalimbali ili kuweza kubaini wezi walioliiba na kulitelekeza.

Katika taarifa yake ya pili Kamanda N'gazi alisema jeshi hilo limefanikiwa kukamata bastola moja aina ya browning  na risasi nane ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha mkazi mmoja katika eneo la Kimnyak ambapo mtuhumiwa huyo ambae jina lake halijaweza kupatikana  alitoroka baada ya kupata taarifa anatafutwa.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mali mbalimbali zilizokamatwa na kuwataka wakazi wa Arusha kufika ofisini kwake kwa ajili ya kutambua mali walizoibiwa.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng'azi akionyesha mali mbalimbali zilizokamatwa na kuwataka wakazi wa Arusha kufika ofisini kwake kwaajili ya kutambua mali walizoibiwa.
Mwalimu Susan Cornel mkazi wa Olasiti Arusha akizungumza na waandishi wa habari nje ya Makao makuu ya Polisi Arusha akieleza namna gari lake liliibiwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CRDB BANK PLC announcing the new CEO, Mr. Abdulmajid Musa Nsekela

WAZIRI KALEMANI AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MATUMIZI YA UMEME WA REA

0
0
Na Veronica Simba – Mara
Wananchi wametakiwa kuondoa hofu kuwa umeme unaosambazwa vijijini kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) ni mdogo usioweza kutumika kwa shughuli kubwa za kibiashara kwani si kweli, kwakuwa umeme huo una nguvu sawa na umeme mwingine na unaweza kutumika kwa matumizi yote ikiwemo viwanda.
Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, wakati akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali katika Wilaya za Bunda na Serengeti mkoani Mara, pamoja na Bariadi mkoani Simiyu, Septemba 19, 2018 akiwa katika ziara ya kazi.
Waziri Kalemani alisema kuwa, baadhi ya watu wamekuwa na hofu kuwa huenda umeme huo ambao Serikali inausambaza vijijini  ni mdogo usioweza kuendesha shughuli kubwa za kibiashara zinazohitaji umeme mkubwa.
“Naomba niwahakikishie kwamba, umeme wa REA hautumiki kwa ajili ya kuwashia taa tu, bali ni umeme kama ulivyo umeme mwingine na una uwezo wa kutumika katika shughuli zote hata kuendeshea viwanda vikubwa.”
Akieleza zaidi, Waziri alifafanua kuwa, lengo la Serikali kupeleka umeme vijijini kupitia Mradi wa REA ni kuhakikisha umeme huo mbali na kutumika kwa matumizi madogomadogo ya kawaida, utumike zaidi kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo viwanda vidogo na hata vikubwa, ili kuinua kipato cha wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Alisema kuwa, katika kuwezesha uchumi wa viwanda, Serikali imedhamiria viwanda hivyo vianzishwe vijijini ambako ndiko kwenye rasilimali nyingi, na kwamba Serikali inatambua kuwa umeme ndiyo ‘injini’ ya uchumi wa viwanda; hivyo ni lazima upelekwe umeme unaoweza kukidhi matakwa hayo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Bukama, wilayani Bunda, Septemba 19, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bukama wilayani Bunda, wakati wa hafla ya uwashaji rasmi wa umeme katika eneo hilo iliyofanyika katika Shule ya Msingi Busore, Septemba 19, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwalimu Lydia Bupilipili akizungumza wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kushoto) na wananchi wa kijiji cha Salama ‘A’ (hawapo pichani), akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili-kushoto) akipokea fimbo maalum inayoashiria uongozi mahiri kutoka kwa wazee wa kijiji cha Bukama wilayani Bunda; wakati wa hafla ya uwashaji rasmi umeme katika eneo hilo iliyofanyika Septemba 19, 2018. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bunda, Boniphace Getere na wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwalimu Lydia Bupilipili.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akizungumza, wakati Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa kwanza kulia), alipofika ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kazi wilayani humo kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme. Ziara hiyo ilifanyika Septemba 19, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WALIOKUFA KWA AJALI YA BOTI NYAMINYWILI WATAMBULIWA - LYANGA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI

WATU watatu kati yao akiwemo mtoto wa miaka kumi, wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria wakitokea mashambani kupinduka wakati walipokuwa wakielekea msibani katika kijiji cha Nyaminywili ,kata ya Kipugira, Rufiji mkoani Pwani. Ajali hiyo imetokea baada ya boti hiyo kugonga gogo kwa chini na kusababisha kishindo  hali iliyosababisha taharuki kwa abiria  na kukimbilia upande mmoja hivyo boti ilipinduka na kuwafunika .

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Rufiji,Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 2 asubuhi septemba 19 mwaka huu. Alisema boti ambayo usajili wake bado haujajulikana mali ya serikali ya kijiji cha Nyaminywili ikiendeshwa na nahodha Jumanne Bumbo (20) mkazi wa Nyaminywili ikitokea Nyaminywili mashambani kuelekea kijijini ikiwa na watu 21 wakiwemo watoto watatu ilipinduka.

Alitaja waliofariki dunia kuwa ni pamoja na Mwajuma Libeneke (26), mkazi wa Nyaminywili  na mtoto wake Mwajuae Diola (10). Mwingine ni Wastara Tumbo (24) mkazi wa Nyaminywili ambapo watu 18 waliopolewa wakiwa wapo hai.

Hata hivyo,majeruhi wote walipelekwa kituo cha afya Nyaminywili kwa matibabu zaidi ambapo baadae waliruhusiwa. Boti hiyo imeshaopolewa majini ,miili imekabidhiwa kwa ndugu zao kwa taratibu za mazishi.

Lyanga aliwaasa ,watumiaji wa vyombo vya majini kuwa makini na kuwapa maelekezo maalum wasafiri wa vyombo hivyo ili kujiepusha na majanga  yanayoweza kujitokeza.

Nae mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ,wilayani Rufiji ambae pia ni mkuu wa wilaya hiyo ,Juma Njwayo alitoa rai kwa wamiliki wa boti na mitumbwi kuwa waangalifu na kubeba abiria kulingana na idadi inayotakiwa.

Alisema yeye alipata taarifa hiyo asubuhi kutoka kwa mtendaji wa kijiji hicho na ametoa pole kwa waliofikwa na misiba hiyo.

Kwa upande wake katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM ,Dk.Bashiru Ally alitoa pole kwa ndugu waliofikwa na mkasa huo. Alieleza chama kipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha msiba .

VIJANA 4200 NCHINI KUNUFAIKA MRADI WA KILIMO KUPITIA KITALU NYUMBA

0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akimwagilia bustani ya kijana Matogolo Samwel wa Kijiji cha Mwamanyili wilayani Busega, wakati wa Ziara ya kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vitalu nyumba mkoani Simiyu.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Vijana takribani 4200 hapa nchini wanatarajia kunuafaika na kilimo kupitia mradi wa kitalu nyumba(green house), ambao utaanza kutekelezwa katika mikoa sita ambayo imekuwa kinara kwa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana, ukiwemo mkoa wa Simiyu na Halmashauri zake zote sita. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu,  Sera, Bunge,  Kazi ,Vijana Ajira  na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua maeneo ya ujenzi wa vitalu nyumba na uwepo wa maji yatakayotumika katika  kilimo cha umwagiliaji.

Mvunde amesema katika kutekeleza mradi huo vijana watawezeshwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili iwe sehemu ya ajira yao, ambapo vijana watafundishwa kulima kwa tija kupitia kitalu nyumba na kujua namna ya kutengeneza vitalu nyumba na wananchi wengine wanapohitaji kujifunza namna ya kutengeneza vitalu nyumba wajifunze kwao.

“Tutaleta green house (Kitalu nyumba) ambayo itafungwa hapa na vijana wataelekezwa kulima kupitia huko, lakini pia tutawaunganisha na chama cha Wauza mboga Tanzania kwa ajili ya kutengeneza masoko ya uhakika ili green house (kitalu nyumba) hizo ziwe na tija” alisema Naibu Waziri Mavunde
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akikagua eneo litakalotumika kujenga vitalu nyumba Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi, wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo hayo mkoani Simiyu.

Akiwa katika ziara yake Naibu Waziri huyo amekutana na baadhi ya vijana ambao watatekeleza mradi huo na kuwapongeza kwa uamuzi waliochukua na akatoa rai kwa vijana wote nchini kuachana kukaa vijiweni na badala yake wajishughulishe na teknolojia hiyo ili waondokane na umasikini. Akiwa wilayani Busega, Bariadi na Itilima Mavunde ameeleza kuridhishwa kwake na maeneo yaliyotengwa na akatoa wito kwa viongozi wote kuwalea vijana wote watakaoanza kutekeleza mradi huo ili mradi huo uweze kuwa endelevu na uweze kuwaletea tija.

Mkuu wa Mkoa wa Mhe. Anthony Mtaka  ameishukuru Serikali kwa mpango huo ambao utawasaidia vijana kujiajiri kupitia vitalu nyumba na akamhakikishia Naibu Waziri kuwa mkoa wa Simiyu utahakikisha vijana wanafanya vizuri katika mradi huo

Mkuu wa wilaya ya Itilima amesema pamoja na vijana wilayani humo kujiandaa na mradi wa kilimo kwa kutumia kitalu nyumba Wilaya hiyo pia imeweka mpango wa kutoa mafunzo ya ujasiriamali na ufundi stadi yatakayowawezesha kupata maarifa ya namna ya kufanya shughuli za ujasiriamali na ufundi kama ajira zao.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mhandisi. Mohammed Ali akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde(mwenye miwani) juu ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kitalu nyumba lililopo Mwamanyili, wakati akiwa katika zi ara ya kukagua maeneo hayo mkoani Simiyu.

Kwa upande wao vijana watakaofaidika na mradi wa kitalu nyumba wamesema wanaupokea mradi huo kwa mikono miwili na wakaomba Serikali iwasaidie kupata mikopo ili waweze kununua vifaa vya kisasa hususani mashine na zana za kilimo zitakazowawezesha kutekeleza mradi huo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Mradi mpya wa utafiti kujenga uwezo kukabili mabadiliko tabia nchi wazinduliwa

0
0
Na Mwandishi wetu
MRADI mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania umezinduliwa jana.
Akizindua mradi huo ofisi za Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii –ESRF, Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba  alisema mradi huo unakuja wakati muhimu ambapo taifa linajikita katika kuelekea uchumi wa kati unaotegemea kilimo.
“Sekta ya kilimo imeendelea kuwa ni Sekta muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla hususan katika wakati huu Tanzania inapojizatiti kuelekea uchumi wa viwanda,” alisema Waziri Tizeba huku akisema kwamba sekta ya Kilimo iimekuwa ikiendelea kukua kwa kuchangia asilimia 30 ya fedha za kigeni na kuchangia malighafi za viwanda kwa asilimia 65.
Mradi huo umezinduliwa takaribani miezi mitatu baada ya wizara kuzindua rasmi Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II), yenye lengo la kuleta mageuzi ya Sekta ya kilimo (kilimo, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo.
Pamoja na kufanya uzinduzi huo aliipongeza ESRF na timu nzima ya mradi wa GCRF-AFRICAP kwa kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo kupitia tafiti na kujenga uwezo kwa lengo la kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kwa makundi ya jamii yaliyokua kwenye hatari zaidi.
Alisema Wizara yake itaendelea kukuza na kulinda maendeleo ya sekta ya kilimo yaliyo endelevu, kwa kuongeza uzalishaji, kuboresha mifumo ya kilimo inayokwenda sambamba na mabadiliko ya tabia nchi.
“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazingatia tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi kwa umakini mkubwa sana, na Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika ambazo zimefanikiwa kuendeleza Mpango Mkakati wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi,  ili kwenda sambamba na dira ya maendeleo ya taifa 2025.” Alisema Dk. Tizeba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (hayupo pichani) na washiriki wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akitoa hotuba kabla ya kuzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba (katikati) akizundua rasmi mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto), Msimamizi wa mradi wa AFRICAP kwa Tanzania na Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi –ESRF, Bi. Vivian Kazi (kushoto), Mwakilishi wa, FANRPAN – AFRICAP anayeshughulikia sera (kikanda), Bi. Sithembile Ndema Mwamakamba (wa pili kulia) pamoja na Dr. Susanna Sally (kulia) kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza wakishuhudia tukio hilo.
 Dr. Susanna Sally kutoka Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza akiwasilisha mada kuhusu mfumo wa kilimo cha kisasa kincahozingatia mabadiliko ya hali ya hewa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi ya taarifa za hali ya hewa TMA kutoka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa maoni wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya kilimo kutoka, vyuo vikuu, taasisi mbalimbali za serikali pamoja sekta binafsi walioshiriki hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Dk. Charles Tizeba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi mpya wa utafiti na wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa ushauri wa kisera katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAZISHI YA JOHN GUNINITA IFAKARA WILAYANI KOLOMBELO

0
0
Waombolezaji wakiandamana kutangulia mbele wakati mwili wa Marehemu John Guninita ulipokuwa ukipelekwa eneo la kusaliwa wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana, Ifakara wilayani Kilombero.
Waombolezaji Wakilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya marehemu John Guninita.
Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu John Guninita kulipeleka kwenye eneo la kusaliwa wakati wa mazishi hayo.

 Mwili wa Marehemu ukiwa umepakizwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa eneo la ibada.

Naibu Waziri Biteko atatua mgogoro uchimbaji madini Tarime

0
0
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara katika machimbo ya dhahabu ya Msege yaliyopo wilayani Tarime mkoani Mara.

Na Greyson Mwase, Tarime

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametatua mgogoro kwenye machimbo ya madini ya dhahabu ya Msege yaliyopo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kuitaka kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini hayo ya Everson Limited kuhakikisha inasaini mikataba kati yake na wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini na kushirikiana kwa karibu zaidi. Naibu Waziri Biteko ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea machimbo hayo leo tarehe 19 Septemba, 2018 na kusikiliza kero za wachimbai wadogo wa madini ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya Mara na Geita yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini.

Katika hatua nyingine, Biteko alimtaka mmiliki wa kampuni ya Everson Limited, Mwita Wambura kuhakikisha anasimamia makubaliano aliyojiwekea kati ya wachimbaji wadogo wa madini na kampuni yake huku akihakikisha sheria na kanuni za uchimbaji wa madini zinafuatwa.

Alisema kuwa mara baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kampuni na wachimbaji hao alibaini kuwa kampuni husika ilikataa kusaini mikataba kati yake na wachimbaji wadogo wa madini kinyume na makubaliano hali iliyopelekea mgogoro kutokuisha.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akiangalia sehemu ya nyaraka mbalimbali za uchimbaji madini katika machimbo ya dhahabu ya Msege yaliyopo wilayani Tarime mkoani Mara.

“Haiwezekani kama kampuni mnakaa katika vikao kwa kushirikisha viongozi wa serikali na kukubaliana kuandaa mikataba ili kusaini halafu baadaye mnashindwa kutekeleza makubaliano, kama Serikali tunataka kuhakikisha kila upande unanufaika, huku Serikali ikipata mapato yanayostahili,” alisisitiza Biteko.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali ina haki ya kuchukua leseni ya kampuni yoyote pale inapoonekana makubaliano kati yake na wachimbaji wadogo hayafuatwi hali inayosimamisha kukwama kwa shughuli za uchimbaji madini na kukosa mapato yake.

Wakati huo huo wananchi kutoka sehemu mbalimbali katika Wilaya ya Tarime walimpongeza Naibu Waziri Biteko kwa kuhakikisha kuwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu pasipo kupatikana suluhu unatatuliwa ndani ya kipindi kifupi na kusisitiza kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Madini kwa kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni za madini huku wakilipa kodi zote serikalini.
Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika machimbo ya dhahabu ya Msege yaliyopo wilayani Tarime mkoani Mara akiwasilisha kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wa madini, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Mara, Stephan Msseti alimpongeza Biteko kwa kuhakikisha amefika kwenye machimbo hayo na kutatua mgogoro na kufafanua kuwa sasa wachimbaji wadogo wataanza kuchimba katika mazingira ya amani na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Msseti alimtaka mmiliki wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Everson Limited, Mwita Wambura kuhakikisha anaheshimu mamlaka za serikali kwa kuhakikisha anatekeleza makubaliano yote wanayojiwekea.

Awali akizungumzia mgogoro huo, mmiliki wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Everson Limited, Mwita Wambura alisema kuwa mara baada ya kufanya utafiti na kuanza uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo, wananchi walianza kuvamia eneo hilo hali iliyopelekea mgororo.

Alisema kuwa aliwaruhusu wachimbaji wadogo kuchimba madini katika mashimo matano lakini wachimbaji hao wamekuwa wakidhuru wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kuwapiga kwa kuwa si wakazi wa kijiji husika kauli ambayo ilipingwa na Diwani wa Kata wa Nyarukoba kupitia CHADEMA, Matiko Marwa.
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Msege kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara wakisikiliza ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).

Marwa mbali na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Madini alimtaka mwekezaji huyo kutii makubaliano kwa kusaini mikataba ili kumaliza mgogoro. Kabla ya kufanya ziara katika machimbo hayo, Naibu Waziri Biteko alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga na kuelezwa changamoto mbalimbali zinazoikabili Wilaya hiyo hususan kwenye uchimbaji wa madini.

Luoga alieleza changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukusanyaji wa maduhuli kuwa mdogo kutokana na wachimbaji wadogo wengi kuchimba madini pasipo kutambulika, baadhi ya wachimbaji wadogo kuwepo kwenye leseni zenye uwekezaji, utoroshwaji wa mawe yenye dhahabu na migogoro katika baadhi ya maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini.

KILIMO CHA MPUNGA CHA SHADIDI KIMEANZA KUWA MKOMBOZI KWA WAKULIMA ZANZIBAR

0
0
Na Fatma Abdallah, Maelezo - Zanzibar 

Wakulima wa Mpunga wa kilimo cha majaribio cha Shadidi wameongeza uzalishaji kutoka tani 4.3 msimu wa vuli kufikia tani 13.5 msimu wa mwaka baada ya kupatiwa mafunzo ya kilimo hicho.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari Ofisini kwake Darajani, Afisa elimu kwa wakulima wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Sada Seif Said alisema Wakulima wa kilimo hicho wa Kisiwa cha Unguja walivuna tani 7.3 za mpunga na Pemba tani 6.2. Aliyataja mabonde yanayolima kilimo cha Shadidi kwa Unguja kuwa ni Uzini, Cheju, Bumbwisudi na Kibokwa na Pemba ni Makombeni, Weni, Kibirinzi na Kinyapunzi.

Alisema baada ya wakulima wa kilimo cha Shadidi kuongeza uzalishaji wataendelea kuhamasisha wakulima wengine wanaolima mpunga wa umwagiliaji maji ili waweze kujiunga na kilimo hicho.

Afisa Elimu kwa Wakulima alielezea matarajio yake kuwa iwapo  wakulima watakubali kujinga kwa wingi na kilimo cha Shadidi, Zanzibar inaweza kupunguza kwa asilimia kubwa kuagiza mchele kutoka nje.

Aliongeza kuwa kilimo cha Shadidi, kinacholimwa kwa vipindi viwili kwa mwaka, kilianza mwaka 2016 na wakulima 85 waliopatiwa mafunzo Unguja na Pemba wanaendelea kulima kwa mafaniko makubwa.

“Tumeweza kutoa elimu kwa wakulima wa kilimo cha Shadidi Unguja na Pemba kwa lengo la kukiimarisha zaidi na tumeanza kupata mafanikio”, alisema Afisa huyo.

Sada Seif alieleza kuwa wakulima wa kilimo cha Shadidi wanatumia mbegu na maji kidogo na kinauwezo wa kutoa polo 60 za mpunga kwa eka moja wakati kilimo cha kawaida kinazalisha polo 32.

Aliongeza kuwa kilimo cha Shadidi kinachuka muda mfupi zaidi kuanzia wakati wa kupanda mbegu, ukuaji hadi kufikia wakati wa kuvuna tafauti na kilimo cha mpunga wa kawaida.

Aidha  alieleza kuwa tayari Wizara ya Kilimo, Mali Asili, Mifugo na Uvuvi imeshatoa mafunzo ya kilimo cha hicho kwa Jeshi la Kujenga Uchumi  Upenja ili kukiendeleza na kufikia lengo la kujitosheleza kwa mchele Zanzibar.

WAFANYABIASHARA SAME WAFURAHIA ELIMU YA KODI

0
0
Na Veronica Kazimoto
Wafanyabiashara Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wamefurahia elimu ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwa na lengo la kuwaongezea uelewa juu ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi kulingana na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 na Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA.

Wakizungumza mara baada ya kumaliza semina hiyo, wafanyabiashara hao wamesema kuwa, wamefurahishwa na elimu waliyoipata kutoka TRA na kwamba itawasaidia katika shughuli zao za kila siku.

"Binafsi nimefurahi sana kupata elimu ya kodi ambayo kwa hapa Same tuna takribani mwaka mzima bila kupatiwa elimu hii, kwa kweli ninaomba TRA watupatie semina hizi mara kwa mara ili tuweze kuendesha biashara zetu kwa ufanisi", alisema Regina Msuya ambaye ni Mfanyabiashara wa Vifaa vya Shule na Ofisi.

Msuya ameongeza kuwa, ni muhimu Mamlaka ya Mapato Tanzania iangalie namna ya kuongeza muda wa semina hizo ili waweze kuyapata kwa undani masuala yote yanayohusiana na kodi.

Kwa upande wake Mfanyabiashara anayemiliki Baa wilayani hapa Tizinga Mbogo, mbali na kufurahishwa na elimu ya kodi aliyoipata, ameiomba TRA kushirikiana na ofisi ya Afisa Biashara ili kuondoa changamoto zinazowakabili ambazo utatuzi wake hutegemea ofisi hizo mbili.

"Kwanza kabisa naomba elimu hii iendelee maana tumejifunza mambo mengi mazuri kutoka kwa wenzetu wa TRA, aidha naomba Afisa Biashara ashirikiane na Mamlaka ya Mapato Tanzania hapa wilayani kwetu kwa ajili ya kututalia kero ambazo zinategemea maamuzi ya ofisi hizi mbili," alieleza Mbogo.

Awali akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyamle, amewahimiza wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni ya kodi yanayotokana na riba na adhabu kuwahi kutuma maombi ya msamaha pamoja na kuwataarifu wenzao wenye madeni kama hayo.

Elimu ya kodi inaendelea kutolewa katika Mikoa ya Kaskazini ambapo baada ya kumaliza Mkoa wa Tanga, sasa elimu hiyo inatolewa katika Mikoa ya kilimanjaro, Arusha na Manyara.
 Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyamle akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi. Semina hiyo imefanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
 Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akitoa elimu ya kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
  Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
 Afisa Kodi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Shaban Makumlo akiwasilisha mada kuhusu Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTSPESA YAZINDULIWA

0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya  kubashiri michezo nchini ya Sportspesa imezindua rasmi promosheni ya kuinua watu maisha yao hasa kiuchumi inayokwenda kwa jina la Shinda zaidi na Sportspesa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Tarimba Abbas amesema kampuni hiyo inaendesha shindano hilo kwa wateja wake ikiwa ni mara ya pili.

Ambapo kwa mwaka jana ilitoa takribani bajaj 100 kwa washindi kutoka mikoa mbalimbali nchini waliobuka washindi.

Pia Tarimba amesema  lengo la shindano hilo limejikita zaidi kwenye kubadilisha maisha ya Watanzania kwani washindi wamekua wakishinda zawadi mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingne zinawasaidia kujiongea kipato.

Ametoa rai kwa wateja kutumia fursa hiyo kubadilisha maisha yao kwani promosheni hiyo kila mmoja anayo nafasi ya kuwa mshindi na kufafanua shindano hilo linaambatana sana na wapenzi wa mpira wa miguu.

Kwa upande wa Submean Auto Limited Venkatesh Bussiness ambao ni wasambazaji wa Bajaji RE nchini  wametoa waranti kwa miezi 12 bajaj za watakaoshinda ili kuonesha imani kwa bidhaa hizo.

Pia wamewaomba watanzania kubashiri kupitia Sportpesa ili waweze kushinda hasa kwa kuzingatia kampuni hiyo inaongoza kwa  Afrika Mashariki.

 Wakati huohuo Meneja Uhusiano wa Sportspesa Sabrina Msuya  amefafanua jinsi ya kushiriki Kwenye promosheni ya Sindano hilo.

Msuya amesema kwa promosheni iliyopita ilifika mikoa 23 ya Tanzania na kwa kila aliyewekea ubashiri wake alipata nafasi ya kujishindia pesa taslimu,jezi na safari ya kwenda Uingereza ,Bajaji ni fursa peke kwa sasa kubashiri.
Meneja uhusiano wa shindano la shinda zaidi na Sportpesa, Sabrina Msuya (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habarini kushoto ni Mkurugenzi wa utawala na udhibiti Abass Tarimba pamoja na wawakilishi kutoka klabu za mpira wa miguu nchini

MICHUZI TV LIVE: KATIBU HAMASA UVCCM HASSAN BOMBOKO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI

AMANI CENTRE WAOKOA WATOTO 1200 WALIOKUWA WAKIISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kituocha Amani (Amani Center for Street Children ) Meindert Schaap akizungumza wakati wa mahafali ya 12 ya wanafunzi wa Darasa la Saba waliokolewa na kituo hicho kutoka mitaani.
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ,Mratibu wa Elimu kata ya Karanga,Mercy Mandia akikabidhi zawadi kwa baadhi ya Wanafunzi walihitimu Darasa la Saba waliooklewa kutoka Mitaani na kupata msaada wa Elimu kutoka katika kituo hicho.
Mzazi Mwakilishi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho ,Editha Cyril akitoa neon la shukrani kwa msaada mkubwa uliotolewa kwa watoto hao.
Mtoto Getrude Salutary ,mmoja wa Wahitimu wa Darasa la Saba waliokuwa wakilelewa katika kituo hicho akisoma Risalambele ya mgeni rasmi,kushoto kwake ni mwanafunzi mwenzake ,Michael Salutary.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images