Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

KWESE IFLIX KURUSHA MICHUANO MIKALI YA NDONDI, WATEJA KUSHUHUDIA KUPITIA SIMU ZA MKONONI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

KUELEKEA michuano mikali ya ndondi kati ya Anthony Joshua raia wa Nigeria na mshindi wa mataji 3 yakiwemo ya WBA dhidi ya Alexander Povetkin kutoka Urusi watakao zichapa Septemba 22 Kwese Iflix kupitia application yao watarusha mpambano huo moja kwa moja kutoka katika viwanja vya Wembley kwa gharama nafuu ya shilingi 1300 pekee.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mkuu wa Kwese Iflix Mayur  Patel ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Kwese Iflix miezi mitatu iliyopita malengo yao ya kuendelea kutimiza haja ya burudani kwa wateja wao imezidi kuimarika kwani wateja wao hutizama masuala ya burudani za kila namna kupitia simu zao za mkononi na upeperushaji huo huwa ni wa moja kwa moja ukienda sambamba na uchambuzi wa kina hasa katika kabumbu.

Ameeleza kuwa pamoja na ndondi pia mashabiki wa mpira watafurahia michuano ya kimataifa ya UEFA Nations League inayoendelea moja kwa moja sambamba na uchambuzi kutoka kwa wabobezi wa masuala la mpira.

Aidha imeelezwa kuwa kwese Iflix ina huduma pana ya maktaba ya vipindi na filamu kutoka ndani na nje ya bara la Afrika kwa kushirikiana na zaidi ya studio 240 na wasambazaji wa filamu ulimwenguni, na hupatikana kwa  kujinunulia VIP pass itakayodumu kwa muda wa siku 1, 3, 7 hadi siku 30 na kwa kukamilisha hii ni kwa kupakua bure application ya Kwese Iflix kupitia Google na apple app store.

Fursa ya kurusha michuano hiyo imekuja baada ya Kwese Iflix kufanikisha urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya kombe la dunia mwaka 2018 kwa ufanisi zaidi.

Pia katika kuelekea pambano hilo la ndondi Kwese Iflix itatoa vidokezo na marudio ya makabiliano manne ya mwisho bure kabisa bila malipo na hasa yale ya ushindi kwa wateja wao.

RC MAKONDA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA BARABARA KIGAMBONI, AWAHIMIZA TANROAD NA TARURA KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI

0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Madaraja inayotekelezwa na Serikali kwenye Wilaya ya Kigamboni ambapo kukamilika kwake kutafanya mji wa kigamboni kuwa wa kisasa zaidi.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na RC Makonda ni ujenzi wa Barabara ya njia sita za magari kuelekea Daraja la Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Kilomita 2 pamoja Mzunguko wa Magari (Round about) yenye ukubwa wa Mita 250 kuelekea Feri Mita 250 kuelekea Kibada ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika October 31 mwaka huu.

Aidha RC Makonda ametembelea ujenzi wa Barabara ya KKKT na mitaro ya maji yenye urefu wa Mita 275, Barabara ya Hospital ya Vijibweni Mita 800 kutoka Kibada,Barabara ya Kijaka-Mwasonga Km 8, Mwasonga-Kibada Km 16 Kimbiji-Pembamnazi, Daraja la Puna eneo la Buyuni na Daraja la Kibugumo Kata ya Gezaulole ambapo miradi hiyo ipo hatua za mwisho kukamilika. 

RC Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo na kuwahimiza TANROAD na TARURA kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waendelee kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema wamejidhatiti kuhakikisha Kigamboni inakuwa na Barabara za Lami, Maji ya kutosha na Umeme kwaajili ya Viwanda, Makazi na Showroom kubwa Africa Mashariki na Kati.
TULIAHIDI NA TUNATEKELEZA.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza leo na waandishi wa habari juu ya kuwahimiza Tanroad na Tarura kukamisha miradi kwa wakati katika wilaya ya Kigamboni.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambata na viongizi mbalimbali wakikagua miradi mbalimbali  katika  wilaya  ya Kigamboni.
Muonekano wa maadhi ya madaraja yanayojengwa katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

HAPPY BIRTHDAY KAMANDA RAS MAKUNJA WA NGOMA AFRICA BAND..

0
0

LEO  19 SEPTEMBER 19.SIKU YA KUZALIWA KAMANDA RAS MAKUNJA..

Siku kama ya leo 19 Septemba ndio siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja a.k.a kamanda Ras Makunja a.k.a mkuu wa viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" alizaliwa mjini Dar-es-Salaam, akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi.Moza Hassan Seifu Mpili (Mama Makunja).

Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja mtunzi na mwimbaji  mahili wa muziki wa dansi leo ndio Happy Birthday !!!!! yake.

pia unaweza kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni at www.reverbnation.com/ngomaafricaband

WAFANYABIASHARA TANGA WAPEWA ELIMU YA MSAMAHA WA KODI

0
0
Na Veronica Kazimoto-Tanga
Wafanyabiashara mkoani Tanga wameelimishwa kuhusu Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 na Mfumo wa Maadili wa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara hao kujua kwa undani masuala yanayohusu kodi pamoja na kuwahi kuomba msamaha wa riba na adhabu ambapo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Novemba, 2018.

Akifungua semina ya wafanyabiashara hao mkoani hapa iliyoandaliwa na TRA, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Monica Kinara amesema kuwa, elimu hiyo imekuja wakati muafaka na siyo tu itawasaidia kujua masuala ya kodi bali wale wenye malimbikizo ya madeni ya kodi watanufaika na msamaha huo na hatimaye wataweza kulipa kodi kwa wakati.

"Ninawashukuru sana TRA kwa kuleta elimu hii hapa mkoani kwetu na ni matumaini yangu kuwa, wafanyabiashara mtatumia fursa hii vizuri ili iwasaidie kuelewa masuala mbalimbali yanayohusu kodi na hasa msamaha wa riba na adhabu ya kodi ili muweze kuomba msamaha huo ndani ya muda uliopangwa," alisema Kinara.

Naye, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla amewaeleza wafanyabiashara hao kwamba, ni jukumu la kila mwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kuomba msamaha wa riba na adhabu akiwa ameambatisha dodoso maalum la msamaha huo pamoja na ritani ya taarifa za Mlipakodi.
 Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Masawa Masatu akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara  iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinara akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
 Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akiwasilisha mada kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
 Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida Rweikiza kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili wa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Katibu Kiongozi awataka Makatibu wakuu na Makatibu Tawala kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati

madereva wanaosafirisha mizigo nje ya nchi watakiwa kuomba Pasipoti Mpya za Kielektroniki

TASWIRA YA FLYOVER YA TAZARA BAADA YA MAGARI KURUHUSIWA KUPITA

0
0

 Muonekano wa njia ya juu (flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela eneo la TAZARA jijini Dar es salaam baada ya magari kuruhusiwa kupita juu yake. Kufunguliwa kwa flyover hio kumepunguza adha ya foleni kwa kiwango kikubwa kiasi ya kwamba safari kutoka katikati ya jiji hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hivi sasa huchukua si zaidi ya nusu saa badala ya masaa mawili au matatu ya awali. Picha na Muhidin Issa Michuzi

TAWLA TANGA YAENDESHA MDAHALO WA WADAU WA MASUALA YA ARDHI MKOANI TANGA

0
0
 Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoani Tanga TAWLA Latifa Ayoub kulia akisisitiza jambo wakati wa mdahalo wa wadau wa masuala la ardhi mkoani Tanga leo mjini Tanga kuhusu changamoto zinazowakabili wanawake kwenye kumiliki ardhi kushoto ni Mwanasheria wa TAWLA Mkoani Tanga Mwanaidi Kombo ambapo mdahalo huo uliandaliwa na chama hicho.
 MWANASHERIA wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga katika Sigisbert Akwilini akiwa na wadau wengine wakifuatilia mdahalo huo ambao uliandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) mkoani Tanga.
Madiwani wa Kata za Chumbangeni Saida Gadafi CCM) kushoto akiwa na Diwani wa Kata ya Majengo (CUF) Suleimani Mbaruku wakifuatilia mdahalo huo.

MKURUGENZI MKUU WA NSSF AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI TATU ZA KIBENKI NCHINI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio amefanya mazungumzo na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki hapa nchini ambazo ni NMB,CRDB na UBA kwa lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kibiashara. 

Katika mkutano huo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF. 

Wakurugenzi wakuu hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Charles Kimei,Bwana Usman Imam Isiaka Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker.
 Wa kwanza pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ,Bwana William Erio  akiwa kwenye mazungumzo na Menejimenti ya  Benki ya CRDB ofisini kwake makao makuu jijini DSM ambapo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali ya kuimairisha mahusiano baina yao.

 Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na viongozi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao  kwenye makao makuu ya NSSF ,katikati Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio na pembeni yake ni mkurugenzi mkuu wa CRDB Charles Kimei na pembeni ni viongozi mbalimbali  wa CRDB na NSSF.

 Mkurugenzi Mkuu  wa Benki ya UBA ,Bwana Usman Imam Isiaka akielezea jambo wakati wa mazungmzo yake na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  Bwana William Erio leo katika makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya NMB Bi.Ineke Bussemaker akipongezana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa  mazungumzo baina yao ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni  Bwana Miichael Mungure amabaye ni MKuu wa kitengo cha akaunti na malipo(NMB), wa kwanza kulia ni Richard Mtapa ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi za Serikali(NMB)

AZAM FC WAJIGAMBA KUIFUNGA BIASHARA UNITED KATIKA MCHEZO WAO WA LEO

0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii

UONGOZI wa Kikosi cha Azam chini ya  Kocha Mkuu wake Hans Van der Pluijm umesema kwa mazoezi waliyofanya sasa vijana  wapo tayari kupambana dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika  leo saa 10 jioni katika dimba la Karume mkoani Mara.

Hivyo Azam mchezo huo wa leo ni wa nne  kwao katika Ligi Kuu Tanzania Bara na wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama saba.

Wakati timu ya  Biashara ni  mzunguko wa tano na wanashika nafasi ya 12 ikiwa na alama nne.

Ambapo JKT Tanzania  wakiwa vinara wa ligi hiyo ambayo imeshacheza michezo 4 mpaka sasa na wakiwa na alama 8.

Katika mchezo uliopita Azam FC ilionesha kulazimisha sare  ya kufungana 1-1 dhidi  Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage huko mkoani Shinyanga.

Wakizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Biashara ,Uongozi wa Kikosi cha Azam umesema wachezaji wao wako vizuri na  hakuna majeruhi.

Wameongeza wachezaji wao kila mmoja akiwa na morali ya kuondoka na alama tatu  ugenini.

RELI YA KISASA (STANDARD GAUGE) YATANDIKWA RASMI...

VYAMA VYA SIASA HAPA NCHINI VIMETAKIWA KUDUMISHA NA KUIMARISHA DEMOKRASIA

0
0
VYAMA vya siasa hapa Nchini vimetakiwa kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi imara tofauti na mawazo ya walio wengi kuwa vyama hivyo sio imara kiasi cha kufananishwa na vikundi vidogo vidogo katika Jamii kama vile Saccos.



Hayo yalisemwa na Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa vyama vya siasa kinachoendelea leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvijengea vyama uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze kujiendesha kama taasisi.



Jaji Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati chafu kutoka Ofisi yaMdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.



‘’Mafunzo ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile mali za vyama ni muhimu kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni vyema mkatambua kuwa vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji wa ndio maana msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji Mtungi.



Aidha Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa kuwa elimu ya fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili linasaidia sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.


 Msajili wa vyama vya siasa,Jaji Francis Mutungi akizungumza  na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
 Msajili msaidizi Sisty  Nyahoza akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa katika semina ya siku mbili leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mkandala akizungumza na viongizi wa vyama vya siasa  kuhusu jinsi ya kujiendesha chama kama taasisi.
Sehemu ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika sema iliyofanyika lao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SEKTA YA UVUVI YAIMARIKA, BOTI YA DORIA YAHITAJIKA KUIMARISHA ULINZI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UVUVI na uuzaji wa samaki katika soko la Feri jijini Dar es salaam umezidi kuimarika katika mchakato mzima wa uvuvi wa samaki wenye viwango vinavyotakiwa na uuzwaji wake sokoni umekuwa na tija.

Akizungumza na blogu ya jamii Kaimu Afisa Uvuvi wa soko la Feri Ahmed Mbarouk ameeleza kuwa upatikanaji wa samaki kwa sasa ni mzuri hasa kwa samaki wakubwa  na hata mauzo yamekuwa mazuri pia kutokana na ubora wa samaki wanaovuliwa kuwa na viwango.

Kuhusiana na kutokomeza uvuvi haramu Abdallah ameeleza kuwa kwa sasa hakuna matukio hayo ya wavuvi kutumia baruti kuvua samaki na hii ni baada ya kampeni waliyoiendesha na kufanikisha kukamatwa kwa nyavu haramu kubwa 14 aina ya kokoro ambazo ziliteketezwa.

Akieleza changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji Afisa uvuvi huyo amesema kuwa vifaa vya kazi hasa boti la doria limekosekana hali inayowapelekea kufanya doria kwa miguu licha ya kuwa na askari wa Suma JKT wanaosaidia na kueleza kuwa boti hilo likipatikana litawarahisishia kazi ya kufanya doria nyakati zote na kwa uhuru zaidi.

Aidha ametoa wito kwa  kwa wavuvi kwa kuvua samaki wenye viwango vinavyofaa na doria hizo ni endelevu hivyo wavuvi wafuate kanuni na taratibu.

Mmoja wa wavuvi hao Jumanne Ramadhani amesema kuwa wanaushukuru uongozi wa soko hilo hasa maafisa uvuvi kwa kuwapa elimu na kuwasimamia kwani hadi sasa wanajua viwango vya samaki wanaotakiwa kuvuliwa na kupelekwa sokoni na kwa sasa biashara ni nzuri kwani upatikaji wa samaki hasa wakubwa umekuwa mkubwa na soko kwa ujumla limesimama imara.
 . Afisa uvuvi  Msaidizi katika soko la samaki Feri Ahmed Mbarouk akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na hali ya uvuvi na biashara ya samaki sokoni hapo.
 Samaki wakiwa tayari kwa mauzo ambapo samaki mmoja huuzwa kati ya shilingi 45,000 hadi 50,000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mnada wa samaki ukiendelea katika soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam.
Mwandishi kutoka Michuzi blog akiangalia samaki aina ya kaa mara baada ya kuvuliwa na mmoja wa wavuvi.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

MAHAKAMA KISUTU KUANZA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI MENEJA BENKI YA BACLAYS

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kuanza kusikiliza  kesi ya wizi wa zaidi ya milioni 390,2 na USD 55,000 na Euro 2,150 inayomkabili aliyekuwa Meneja wa Benki ya Baclays, Alune Kasililika na wenzake 11 kwa siku tatu mfululizo.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanzia Oktoba 3,4 na 5 mwaka huu.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa mashtaka leo Septemba 19 mwaka 2018 kukamilisha upelelezi na washtakiwa hao kusomewa Maelezo ya awali (PH).

Akiwasomea PH , Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai kuwa aliyekuwa Meneja  wa Benki ya Barclays Tawi la Kinondoni, Alune Kasilika,  aliwasiliana na watuhumiwa wa tukio la ujambazi katika benki hiyo wakiandaa utekelezaji wake.

 Kombakono alidai kuwa Aprili 15,  mwaka 2014 asubuhi, mshtakiwa Alune  Kasililika na Neema Batchu ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo, walifika kazini na shughuli za kibenki ziliendelea pamoja na wafanyakazi wengine.

Amedai kuwa  Alune, siku hiyo ya tukio alikuwa na mawasiliano na mshtakiwa wa tatu hadi wa tisa ili kuandaa tukio la wizi wa fedha za benki hiyo na hatimaye lilifanyika. 

Amedai wizi ulifanikiwa baada ya washtakiwa hao ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo kutoa taarifa za kina kuhusu benki kwa mshtakiwa wa tatu hadi wa tisa.

Akiendelea kusoma PH, Wakili Kombakono amedai askari E 9660 D/SSGT  Iddy, P407 D/CPL Bundala na Sezary Massawe wakati upelelezi wa kina ukifanyika huku wakijua mshtakiwa wa kwanza hadi wa tisa wanatafutwa kwa wizi, waliwapa taarifa za kiupelelezi ili kuwasaidia wajifiche wasikamatwe na walikimbia kukwepa mkono wa sheria.

Pia mshtakiwa Ruth Macha yeye anadaiwa kuwa alimsaidia mshtakiwa Maulid Seif kutoroka ili kukwepa mkono wa sheria.

Baada ya kumaliza kusomewa PH hizo, Hakimu Shaidi alimtaka kila mshtakiwa kujibu anayokubali na anayokataa ambapo washtakiwa wote walikubali maelezo yao binafsi ikiwamo majina  na walikana maelezo yote yanayohusu wizi huo.

 Katika kesi hiyo,  mshtakiwa wa kwanza hadi wa tisa, wanashtakiwa kwa kula njama kutenda kosa la wizi wa fedha za Benki ya Barclays.

Inadaiwa Aprili 15 mwaka 2014  kwa unyang’anyi wa kutumia silaha,  washtakiwa hao waliiba Sh. 390,220,000, Dola za Marekani 55,000 na Euro 2,150 mali ya benki hiyo.

Katika shtaka  linalowahusu maofisa wa polisi, Iddy na Bundara, wao wanadaiwa kuwasaidia washtakiwa kutoroka ili wasikamatwe na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Ambapo walikana mashtaka yote.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni mameneja wawili wa benki hiyo, Alune Kasilika (28), Neema Batchu (26), mfanyabiashara Hamis Shabani au Carlos (34), mkazi wa Magomeni na dereva Manase Genyeka au Mjeshi (35), mkazi wa Tabata.

Wengine ni wafanyabiashara Kakamie Julius (32), Iddy Khamis  (32), Sezary Massawe (31), Boniphace Muumba (29), Ruth Macha (30) na maofisa wawili wa polisi, Iddy (33) na Bundala (37). Washtakiwa hao wanatetewa na wakili Nehemiah Nkoko.

WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU WATUMISHI WIZARA YAKE KUNYANYASWA, AFUNGUA MILANGO KULETA KERO ZAO OFISINI KWAKE

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi na watumishi mbalimbali wa wizara yake wafanye kazi kwa kushirikiana na kuacha tabia ya kunyanyasana wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.

Lugola pia amesema kila mtumishi wa wizara yake ana umuhimu mkubwa kwa kufanikisha mafanikio ya wizara hiyo kwakuwa watumishi hao wanafanya kazi kwa kutegemeana. Akizungumza na watumishi wa makao makuu wa wizara hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma jana, Lugola alisema kikao hicho alikiitisha kwa lengo la kujuana na watumishi hao pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi.

“Mambo muhimu ambayo yatatuletea mafanikio ndani ya wizara yetu ni kufanya kazi kwa bidii, kufanya kazi kwa kushirikiana na tukifanya hivyo hakika tutapendana na kuzidi kufanikiwa,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, hapendi kuona mtumishi yeyote ananyanyaswa kwa kutopewa haki zake au kucheleweshewa pasipo kuwa na sababu za msingi ikiwemo malipo mbalimbali ya watumishi wanayodai, na endapo yatatokea hayo watumishi hao wamletee kero zinazowakabili ofisini kwake na kwa kushirikiana na katibu mkuu wa wizara hiyo watazitatua.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na watumishi wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi. Pia Lugola aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kuwataka baadhi ya viongozi wa wizara hiyo kuacha tabia ya kuwanyanyasa watumishi wao. Lugola alikutana na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Veta, jijini Dodoma, leo jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu alipokua anawasili katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Veta, jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo, leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhan Kailima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Makatibu Wakuu, MaRas Watakiwa Kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria kwa Maendeleo Wananchi.

0
0
Na Frank Mvungi- MAELEZO
Katibu  Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano  kila wanapofanya maamuzi.
Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa  wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
“Nafasi zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.” Alisisitiza Mhandisi Kijazi.
Akifafanua, Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano yakuleta mageuzi makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Aliongeza kuwa Kikao kazi hicho kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila mwaka ili kuwapa fursa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala  kubadilishana uzoefu, kubaini changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa kuzitatua kwa maslahi ya wanachi.
  Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akifungua  Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Mtendaji Mkuuwa Taasisi ya Uongozi Prof.   Joseph  Semboja akisistiza jambo wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Sehemu ya Makatibu Wakuu wakifuatilia uwasilisjhaji wa mada mbalimbali  kwenye Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini  Bw.  James Syanga akiwasilisha mada kuhusu athari za madawa ya kulevya wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
  Manaibu Katibu Wakuu  na  Makatibu Tawala wakifuatilia mada wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma. (Picha zote na Frank  Shija- MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KALEMANI KUTOA MUELEKEO WA NCHI KATIKA KUTUMIA NISHATI YA MAFUTA NA GESI

0
0
*Ni kupitia Kongamano la pili la sekta ya mafuta, gesi litalokafanyika Septemba 24/25

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
SERIKALI kupitia Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani inatarajia kuzungumzia mwelekeo wa nchi katika kutumia nishati ya mafuta na gesi katika viwanda.

Waziri Kalemani atatoa muelekeo huo katika Kongamano la Pili la Sekta ya Mafuta na Gesi linalotarajia kufanyika kuanzia Septemba 24 hadi 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.Mbali ya Waziri kutoa mwelekeo, pia wadau muhimu wa sekta ya mafuta na gesi wakiwamo TPDC, PURA,EWURA, NEEC, ATOGS na TPSF watashiriki.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu kongamano hilo Abdulsamad Abdulrahim kutoka Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini amesema Serikali na wadau wa sekta ya mafuta na gesi wameunga mkono na watashiriki kikamilifu.

Amefafanua kongamano hilo limeandaliwa na Pietro Fiorentini Tanzania kwa kushirikiana na CWC Group ambapo pamoja na mambo mengine mradi wa bomba la mafuta ghafi utachambuliwa wakati wa kongamano hilo.

“Mradi huo wa bomba la mafuta unatarajiwa kuleta fursa mbalimbali katika mnyororo wa thamani.Pia kongamano hili litajadili hatua za uendelezaji wa miradi ya gesi iliyopo nchini .

“Miradi ambayo itaifanya Tanzania kuwa mzalishaji na msambazaji mkubwa wa gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki,”amefafanua.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba akifafanua jambo wakati anazungumzia Kongamano la Pili la sekta ya mafuta na gesi litakalofanyika Septemba 24 hadi 25 mwaka huu.
Kamishina Msaidizi wa Mendeleo ya Petroli kutoka Wizara ya Nishati akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa Kongamano la pili la sekta ya mafuta na gesi

 Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi nchini Abdulsamad Abdulrahim akizungumza leo kuhusu  Kongamano la Pili la Sekta ya Mafuta na Gesi ambalo litafanyika jijini Dar es Salaam Septemba 24 hadi 25.
Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watoa Huduma za Mafuta na Gesi akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kongamano litakalofanyika Septemba 24 hadi 25 mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DAWASA YADAIWA ZAIDI YA BILIONI MOJA NA BODI YA BONDE LA WAMI/RUVU

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Majisafi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) inadaiwa zaidi ya sh. Bilioni Moja na Bodi ya Bonde la Wami/ Ruvu ikiwa ni kusambaza maji bila kulipia bonde kwa ajili ya uendelezaji wa vyanzo vya maji. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa baadhi ya mamlaka za maji katika mikoa wanatumia bonde la Wami/ Ruvu wamekuwa wakilipa vizuri isipokuwa Dawasa. 

Amesema kuwa licha ya Dawasa kuwa na mikakati ya usambazaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam hivyo lazima walipe katika bonde kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji hivyo. 

Ngonyani amesema kuwa maji ambayo wananchi wanapata yanatokana na kuwepo vyanzo vya maji ambavyo vinahifadhiwa na mamlaka zilizopo kazi yake ni kusambaza tu. 

Amesema kufikia deni hilo kwa Dawasa ni kutokana na kila wakipelekewa Ankara zao wanazichukua na kuzihifadhi huku wakiendelea kutoa huduma za maji. 

Amesema kuwa wenye visima wote katika jiji la Dar es Salaam wafike katika ofisi za Bodi ya bonde la Wami/Ruvu kupata amelezo juu ya ulipaji wa Ankara za maji ndani ya mmoja baada ya hapo watapita kwa kila watu wenye visima. 

Aidha amesema kuwa kampuni za uchimbaji wa visima watakutana nao Oktoba mwaka huu kwa ajili ya kupeana maelezo katika uchimbaji wa kisima. 

Ngonyani amesema ada ya uchimbaji wa kisima ni sh.150,000 na baada hapo kupewa utaratibu wa ulipaji wa ada kwa kila mwaka kuendana na matumizi. 
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kazi za bonde la Wami/Ruvu pamoja na kuzikumbusha Mamlaka za Maji kulipa Ankara zao , jijini Dar es Salaam.

KAMWELWE: KADOGOSA ANAFANYA VIZURI KUANZA KUWARUDISHA WALIOSTAAFU TRC

KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTAPERI KWA KUTUMIA JINA LA RAIS MSTAAFU

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imepanga Octoba 11, 2018 kuanza kusikiliza kesi ya kujitambulisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kufungua vikoba vya kukopesha na kutumia jina la Rais mstaafu Jakaya Kikwete inayomkabili mtuhumiwa, Masse Uledi.

Masse anadaiwa kufungua akaunti ya vikoba kwa jina la Salma Kikwete vicoba Saccos na Ridhiwan Kikwete na kujifanya kuwa anakopesha hela kitendo kilichomwezesha kujipatia fedha kwa watu mbalimbali kwa njia ya udanganyifu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amedai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja leo Septemba 19,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa Maelezo ya awali. (PH)

Akisomewa PH,, Mwita mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Thomas Simba, imedaiwa, Novemba 9, mwaka jana, mshtakiwa alijipatia sh. 840,000 kutoka kwa Joyce Chitumbi kiasi hicho kama dhamana ya kupata mkopo.

Pia mshitakiwa inadaiwa siku hiyo, alijipatia sh. 600,000 na sh. 200,000, kutoka kwa Daniel Cedalia ikiwa ni dhamana ya kupata mkopo wa sh. milioni mbili.

Katika shtaka la tatu imedaiwa, kati ya Septemba 28 na Oktoba mosi  mwaka jana  mshitakiwa alijipatia sh. milioni 2,160,000, kutoka kwa Lucas Kiula kama dhamana ya kupewa mkopo wa sh. milioni 10.

Pia  inadaiwa Novemba mwaka jana alijivika uhusika ambao sio wake kwa kutengeneza peji kwenye mitandao ya kijamii kwa kujitambulisha majina ambayo sio yake ambayo ni Jakaya Kikwete,Salma Kikwete, Getrude Rwakatale na Reginald Mengi kwa ajiri ya kujipatia fedha hizo.

Baada ya kusomewa maelezo hayo mshitakiwa amekiri taarifa zake binafsi ambazo ni jina lake, kufikishwa polisi na mahakamani huku akikana kuhusika na tuhuma hizo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11, mwaka huu.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images