Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

benki ya CRDB imekuja na bidhaa tatu mpya kwa wateja wake

0
0
Kufuatia matukio ya kukosekana kwa uaminifu kwa wanavikundi wanaowekeza pesa ili kujikwamua kiuchumi, benki ya CRDB imekuja na bidhaa tatu mpya kwa wateja wake ikiwamo  wenye vikundi vya vikoba kupata akaunti kupitia simu zao za mkononi ili kuondokana na changamoto ambazo zinawakabili.

Meneja wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao wa benki hiyo, Edith Metta, ameyasema hayo wakati akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusiana na huduma hizo mpya kwa wateja.
Alizitaja huduma hizo kuwa ni akaunti ya kikundi, akaunti ya akiba na akaunti ya malipo.

Metta alisema kumekuwa na changamoto katika baadhi ya vikundi vya fedha ikiwamo vikoba za kupotea kwa fedha au mmoja kukimbia nazo hivyo wameamua kuja na suluhisho kwa vikundi ili fedha zao ziwe salama.
Alisema wanachama wanauwezo wa kufungua akaunti ya pamoja kupitia simu zao za mkononi na kisha kusajili jina la kikundi na kuanza kuweka fedha pamoja na kutoa bila kuwepo na makato.

“Mwanachama wa kikundi ana uwezo wa kuangalia kiasi cha salio kilichopo katika akaunti ya kikundi na endapo kuna fedha imetolewa kinyemela wanajua kwa wakati na kuepusha mwanachama kukimbia na fedha ama kuambiwa fedha imeibiwa,” alisema
Alisema akuanti ya kikundi  ni nzuri kwani fedha zao zinakuwa salama na endapo kunakuwa na udanganyifu wanajua mapema na kuanza kuchukua hatua.

Pia alisema fedha za wanachama zinakuwa salama na hakutakuwa na matukio ya kuibiwa kwa fedha za kikundi kama ilivyo katika maeneo mengine kumekuwa na malalamiko ya kuibiwa fedha za vikoba ama kupotea.
Aidha, alisema kuwa akaunti inaanza kwa kikundi cha watu watatu hadi na 3,000 na kiwango cha mwisho cha kuweka fedha ni Sh milioni 50 kwa kila kikundi.

Alisema kwa kikundi ambacho kitakuwa vizuri katika uwekaji wa fedha huwafuatilia na baada ya muda wanaweza kuwapatia mkopo ili wajijenge vizuri kiuchumi.

Alisema kaunti hiyo sio kwa vikundi tu hata kwa vikao vya harusi wanaweza kujisajili na kufanya malipo kupitia akaunti ya kikundi na fedha zao zikawa salama kuliko kumuachia mweka hazina kwenda nazo nyumbani.

“Kuliko mtu aende benki kutoa fedha ya mchango ama mweka hazina kupata shida ya kuandaa taarifa ya fedha ni kwamba ukishaingia katika hiyo akaunti utakuwa unahamisha fedha na kuona salio bila kuandaa taarifa ya fedha,” alisema Metta.

Aidha, alisema ili mteja aweza kupata akaunti kupitia simu yake ya mkononi atatakiwa kubonyeza *150*62 na kufuata maelezo ambapo atajisajili kupitia kitambusho cha kura ama cha utaifa na akaunti kuipata ndani ya dakika mbili.

Metta alisema lengo la huduma hiyo ni kuwafikia wateja wake hususani katika maeneo ya vijijini ambao wamekuwa wakihifadhi fedha zao katika mfumo usio rasmi jambo ambalo wanahatarisha usalama wa fedha zao.

MAJALIWA ASHUHUDIA MECHI KATI YA NAMUNGO FC NA DODOMA FC - UWANJA WA JAMHURI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kushuhudi mechi ya kirafiki kati ya Namungo FC ya Ruangwa na Dodoma FC, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rashidi Mpemba  (kushoto) wa Dodoma FC  na  Bruno John wa Namungo FC   wakiwania mpira katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu. 
Rashidi Mpemba (kushoto) wa Dodoma FC akimiliki mpira huku akizongwa na Bruno John wa Namungo FC katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu.
Zahoro Pazi wa timu ya Dodoma FC (kulia) akimtoka Luka Kikoti wa Namungo FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu.
Rashidi Mpemba  (kushoto) wa Dodoma FC  na  Bruno John wa Namungo FC   wakiwania mpira katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya mpira wa miguu  ya Namungo FC ya  Ruangwa na Dodoma FC baada ya mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Septemba 16, 2018. Timu hizo zilitoka suluhu.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAANZA KUTOA MSAMAHA WA KODI KWA MIRADI YA MAENDELEO

0
0
Serikali imesema imeshaanza kutoa misamaha ya kodi kwa mikataba ya ujenzi na matengenezo ya miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, viwanja vya ndege na madaraja ambayo ilitakiwa kusamehewa kulipa kodi ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikagua hatua za ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station), wilayani Manyoni mkoani Singida, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa mradi huo umechelewa kukamilika kutokana na mkandarasi kutopata msamaha wa kodi kama jinsi ilivyopangwa na hivyo kuathiri mtiririko wa fedha katika utekelezaji wa wake. 

"Serikali imeanza kutekeleza misamaha ya kodi iliyokwama katika miradi inayoendelea na inayotarajiwa kuanza hapa nchini ikiwemo huu mradi na mingine mingi", amesema Waziri Mhandisi Kamwelwe. Mhandisi Kamwelwe amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Impresa di Construction Ing E. Mantovani S. p. A con socio unico Via Belgio anayejenga kituo hicho kuhakikisha anakamilisha mradi huo ndani ya muda aliyoomba kuongezewa kwani hataongezewa muda mwingine. 

"Nahitaji kituo hichi kikamilike ifikapo mwezi Februari mwakani, kwani haya ni maazimio ya pamoja ya nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kupunguza ucheleweshwaji wa usafirishaji wa mizigo kupitia barabara ya kati kuelekea nchi jirani", amesisitiza Mhandisi Kamwelwe. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo (wa pili kushoto), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja katika kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni, mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Leonard Kapongo (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja kilichopo wilayani Manyoni, mkoani Singida.
Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya NIMETA Consult anayesimamia ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wilayani Manyoni, Mhandisi Patrick Lujinya (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kulia), kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa kituo hicho ambao ujenzi wake umefikia asilimia 60 mpaka sasa, mkoani Singida.
Muonekano wa baadhi ya nyumba za watumishi watakaoishi mara baada ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja kukamilika katika kijiji cha Muhalala, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida. Ujenzi wa kituo hicho utakamilika mwezi Februari mwakani.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


WANANCHI WAELEZA FURAHA YAO YA BARABARA YA JUU (FLYOVER) YA TAZARA

MULTICHOICE YAZINDUA KAMBI MAALUM YA RIADHA MBULU

0
0
MultiChoice Tanzania ikishirikiana na klabu ya riadha ya Rift Valley ya Karatu imefungua kambi maalum ya raidha wilayani Mbulu ambapo wanariadha 16 watakuwa wakipatiwa mafunzo kwa mwaka mzima. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na mwanariadha mwenye sifa ya kipekee duniani John Stephen Akhwari, katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gidabuday na Naibu Rais wa Shirikisho hilo Dk. Hamad Ndee

Kambi hiyo ina wanariadha wengi wenye umri mdogo akiwemo Francis Damiano Damas ambaye ni balozi maalum wa DStv na mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas mwaka jana.
Wanariadha wakongwe na maarufu hapa nchini Mzee John Stephen Akhwari (wa pili kulia), ambaye pia aliweka rikodi ya aina yake katika mashindano ya Olyimpic Mexico mwaka 1968, Dr. Hamad Ndee (kulia) - Makamu wa Rais Shirikisho la Riadha Tanzania na Wilhelm Gidabuday (wa pili kushoto)- Katibu Mkuu Shirikisho la Riadha Tanzania wakiwa na Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana, wakiwasili katika uwanja wa CCM Mbulu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kambi maalum ya riadha ya DStv iliyopo Mbulu mkoani manyara. Kambi hiyo yenye wanariadha 16 imzinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mawasiliano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana, amesema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha kuwa riadha inakuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa, kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.

“Tunataka Tanzania ijulikane ulimwenguni kote kama chimbuko la mabingwa. Tumedhamiria kikamilifu kukuza mchezo huu na kufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo, burudani na ni sekta nyeti kiuchumi kama ikiendelezwa”

“Tunataka kuusikia wimbo wetu wa taifa katika mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa, tunataka kuiona bendera yetu ikipepea juu katika kila mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa , tunataka mamia ya vijana wetu wenye uwezo mkubwa katika riadha washiriki kwenye mashindano makubwa , waweze kujipatia kipato na kuwa chanzo cha maelfu ya ajira na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu” amesema Mshana.
Mwanariadha mkongwe na maarufu hapa nchini Mzee John Stephen Akhwari akizumgumza wakati wa uzinduzi wa kambi maalum ya riadha ya DStv mjini Mbulu mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni mwanariadha mstaafu na Mwenyekiti wa klabu ya riadha ya Frift Valley ya Karatu inayoshirikiana na DStv kuendesha kambi hiyo Meta Petro Bare, Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania na Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana. Kambi hiyo yenye wanariadha 16 inatarajiwa kuendelea kwa mwaka mzima.

Kambi hii ilianza rasmi tarehe 1 Septemba 2018 na itasimamiwa na klabu ya Riadha ya Rift Valley kwa ufadhili wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, kwa mujibu wa makubaliano kati ya pande hizo mbili. Kwa kuanzia kambi hiyo ina jumla ya wanariadha 16 ambapo awamu ya kwanza ya mafunzo itakuwa kwa miezi mitatu (Septemba – Novemba 2018) na  awamu ya pili (Januari- Machi 2019).

Kwa upande wake mgeni maalum katika ufunguzi huo na mwanariadha nguli aliyewahi kuweka rekodi ya aina yake mashindano Olyimpic ya mwaka 1968 nchini Mexico, Mzee Stephen John Akhwari amesema kuwa huu ni uwekezaji mzuri uliofanywa na kampuni ya MultiChoice na ni mfano wa kuigwa na wadau wengine. “Ni kweli kabisa kuwa kwa muda mrefu kumekosekana uwekezaji katika riadha, mchezo ambao unaweza kuwa nguzo kubwa ya maendeleo ya jamii yetu nan chi yetu kwa ujumla. Huu ni uwekezaji wa maana sana na wenye tija kubwa” alisema Mzee Akhwari
Wanariadha mbalimbali wakiwa na viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Maafisa wa MultiChoice Tanzania na Makocha wa riadha wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya kambi maalum ya riadha ya DStv inayoendeshwa na Klabu ya Riadha ya Rift Valey. Kambi hiyo imeanza rasmi mwezi huu na uzinduzi wake ulifanyika mwishoni mwa wiki mjini Mbulu.

Amewaasa vijana wanaopata fursa ya mafunzo kambini hapo kuitumia vizuri. “Ni jukumu lenu nyinyi kama vijana mliopata fursa hii kuhakikisha kuwa mnaweka bidii kubwa na hatimaye muwe wanariadha wakubwa ulimwenguni na kuilieletea sifa nchi yetu kupitia mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa mtakayobahatika kushiriki.” Kwakuwa kambi ipo hapa karibu na nyumbani kwangu, nawaahidi kuwa karibu nanyi muda wote na nitashiriki kwa kwa hali na mali  katika kuwalea na kuwatia moyo” alisema Mzee Akhwari.

Naye Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gidabuday, amesema wamefarijika sana kuona kuwa MultiChoice inaendelea kudhamini riadha kwani wameanza jitihada hizo muda mrefu na matunda yake yameshaanza kuonekana.
Kitovu cha riadha!.. Baadhi ya watoto wa mji wa Mbulu wakionyesha umahiri wao katika riadha wakati wa hafla ya uzinduzi wa kambi ya riadha ya DStv mjini Mbulu mwishoni mwa wiki. Kambi hiyo itakuwa na wanariadha 16 na imeanza rasmi mwezi huu.

Amesema Shirikisho la Riadha la Tanzania litahakikisha kuwa ufadhili huo unakuwa na manufaa na unazaa matunda yaliyotarajiwa ya kuleta medali nyingi zaidi katika mashindano ya kimataifa. “Ufadhili wa aina hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa riadha . Tunaahidi ushirikiano wetu wa dhati ili kufanikisha malengo na tutahakikisha kuwa tunatoa ushikiano unaostahili kwa wafadhili wetu” alisema Gida. 


Mwaka ulipita, kampuni ya MultiChoice Tanzania ilidhamini kambi ya riadha ya timu ya taifa na pia ilimdhamini mwanariadha Alphonce Felix Simbu, ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wanariadha tegemeo kwa nchi hii. Hivi sasa MultiChoice Tanzania inamdhamini mwanariadha kinda Francis Damiano Damas ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas mwaka jana.

WAZIRI KAMWELWE AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA MAPEMA

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), anayejenga barabara ya Nyahua –Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kukamilisha barabara hiyo ifikapo mwezi Desemba 2020 badala ya Machi 2021.
Amezungumza hayo mkoani Tabora, wakati akikagua hatua za maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 117.9 na kuridhishwa na ubora wa kazi zilizoanza kutekelezwa.
Amemtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi ya ujenzi  ambao umefikia asilimia 12 ikiwa ni nyuma ya mpango kazi kwa asilimia 4.
Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (KFAED) na kukamilika kwake kutafungua mkoa wa Tabora na mikoa ya Katavi na Kigoma katika kukuza uchumi wa wananchi.
Waziri Mhandisi Kamwelwe, amefafanua kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu katika kukuza biashara na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani.
Aidha, Waziri Kamwele ameonesha kusikitishwa kwa vitendo vya baadhi ya wananchi kuhujumu miundombinu ya barabara ikiwemo alama za barabarani hasa katika mkoa huo na kuomba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kusaidia Serikali katika kudhibiti.
"Kuna watu huku Tabora waliokamatwa na vyuma vya alama za barabarani majumbani mwao wakitwangia mahindi, hili suala halikubaliki na yeyote atakayepatikana sheria kali zitachukuliwa dhidi yake na Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi zaidi ili kudhibiti suala hili", amefafanua Waziri Kamwelwe.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua moja ya boksi kalvati kati ya 32 yanayojengwa katika barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4  kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndibalinze (mwenye koti la kijivu), mara bada ya kukagua moja boksi kalvati katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akikagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisisitiza jambo kwa Mkandarasi kutoka kampuni ya China Henan International Cooperation (CHICO), Mhandisi Li, mara baada ya kukagua kokoto zitakazotumika katika ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
  Kaimu Mhandisi Mkazi, Mhandisi Regnard Kaganga, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara  ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati Waziri huyo alipokuwa akikagua mradi huo, mkoani Tabora.
Muonekano wa kazi zikiendelea za ujenzi wa tabaka la kifusi kiwango cha G7 katika barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora. Ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo itaunganisha mji wa Manyoni na wa Tabora.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa Kanda ya Afrika wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya wafanyika jijini dar

0
0
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa 28 wa Umoja wa  Mataifa Kanda ya Afrika wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya, wakimsikiliza Kamishna wa Mamlaka ya Kuzia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini,Rogers William Sianga alipokuwa akizungumza katika mkutano huo, unaofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa BOT, jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa. 

BREAKING NYUZZZZ....: TFF YASIMAMISHA UCHAGUZI WA SIMBA

0
0
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeusimamisha mchakato wa uchaguzi katika klabu ya Simba kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu stahiki.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi (TFF), Revocatus Kuuli, amesema mchakato wa uchaguzi huo umegubikwa na mambo mengi ambayo hayajafuata taratibu rasmi.

Mbali na hilo migogoro mbalimbali ya wanachama nayo imepelekea kusimamishwa kwa uchaguzi huo

WAKUFUNZI VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII WAASWA KUZALISHA WATAALAMU WENYE VIWANGO

0
0
Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi nchini wameaswa kutoa wataalamu wa maendeleo ya Jamii wenye viwango vya juu ili kuendana na ushindani uliopo na katika kufikiamuchumi wa kati na wa viwanda.

Hayo yamesemwa leo Mjini Singida na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni na utakaoanza kutumika kwa mwaka wamasomo 2018/2019 mpaka mwaka 2022/2023.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Bw. Golwike amewapongeza wakuu wa vyuo na wakufunzi hao kwa kazi nzuri wanaoendelea kufanya katika kutoa wataalamu wenye viwango katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.

 Ameongeza kuwa wakufunzi hao wanatakiwa kuongeza nguvu katika kutengeneza wataalamu wengi wenye viwango zaidi ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia na ushindani katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.

“Tutengeneza wataalamu wenye viwango ili tuendane na mabadiliko hasa kuelekea uchumi wa viwanda” alisisitiza Bw. Golwike
 Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa Vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
 Mkurugenzi Msaidizi upande wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka akielezea lengo na umuhimu wa mafunzo wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Mandeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii Bw. Paschal Mahinyila akitoa salamu za Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Patrick Golwike wakati wa uzinduzi wa mafunzo wa wakuu kwa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katika Mtaala mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
 Mwakilishi kutoka NACTE Bw. Gidion Karuguru akitoa muongozo wa matumizi ya Mtaaka Mpya kwa Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakuu wa vyuo na wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na ufundi yenye lengo la kupitishwa katiia Mtaala mpya wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii uliopitishwa na NACTE hivi karibuni.
Wakuu wa Vyuo na Wakufunzi kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakifuatilia mafunzo ya Mtaala mpya kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ufundi nchini  uliopitishwa na NACTE hivi karibuni utakaoanza kutumika kwa mwaka wa masomo 2018/2019. Picha zote na Kitengo cha Mawasilino WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DK.SHEIN AKUATANA NA BALOZI WA KENYA NCHINI

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar akifuatana na ujumbe wake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Kenya na Zanzibar zinauhusiano wa kihistoria hivyo ushirikiano katika sekta ya biashara kati ya pande mbili hizo utakuza uchumi na kuuendeleza udugu wa damu uliopo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi mpya wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dan Kazungu aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha. Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Kazungu kuwa Zanzibar na Kenya zina uhusiano na ushirikiano wa kihistoria hasa katika sekta ya biashara ambapo Zanzibar ilikuwa ndio kitovu kikuu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki tokea karne ya 19.

Dk. Shein alieleza kuwa kuna kila sababu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Zanzibar na Kenya katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ambapo kwa upande wa sekta ya biashara ndio sekta pekee yenye historia kati ya pande mbili hizo. Alisema kuwa wananchi wa Kenya na Zanzibar wana udugu wa damu na kutokana na matukio kadhaa ya kihistoria yakiwemo Watawala waliozitawala nchi hizo yamejenga ukaribu mkubwa na kumpelekea Dk. Shein kusisitiza haja ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambilisha akiwa na ujumbe wake (hawapo pichani).

Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein aliunga mkono wazo la Balozi huyo wa Kenya la kuwekwa utaratibu maalum wa kuzidisha ushirikiano huo katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya biashara kati ya Kenya na Zanzibar kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua ustawi wa maisha ya wananchi wa pande mbili hizo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAHER ALBARWANI, ALIYESAFIRI NA PIKIPIKI TOKA OMAN MPAKA TANZANIA KUSHUHUDIA TAMASHA LA URITHI JIJINI DODOMA

0
0
Maher Albarwani (aliyevaa kofia) akiwa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Urithi Festival.
Hii ndio Pikipiki aliyosafiri nayo Maher Albarwani kutoka Oman mpaka Tanzania akipita nchi mbalimbali Duniani.
Balozi wa Heshima kutangaza Pori la Akiba-Selous Miss Journalism Tanzania Witness Kavumo(kushoto) akiwa na Maher Albarwani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi jijini Dodoma.
Mdau wa mambo ya Utalii, Festo Mazuguni (Kushoto) akiwa na Maher Albarwani uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Heshima kutangaza Pori la Akiba-Selous Miss Journalism Tanzania Witness Kavumo, Maher Albarwani aliye safiri na pikipiki kutoka Oman mpaka Tanzania na Naomi Mbilinyi ambaye ni Afisa Utalii kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakiwa katika Banda la Utalii. Picha na Fredy Njeje

Halmashauri ya Kishapu yajipanga kufanya vizuri ukusanyaji mapato

0
0
Na Robert Hokororo, Kishapu.

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imejipanga kufanya vizuri katika ukusanyaji mapato ili kufikia malengo ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 14, 2018 na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka 2017/2018.

Alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia kwa wataalamu wake imeweka mikakati thabiti kuhakikisha inafika maeneo yote na kukusanya mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali.

“Zipo dalili za kufanya vizuri katika ukusanyaji katika mwaka huu mpya wa fedha ingawa bado kuna changamoto nyingi zinatukabili nawaomba wataalamu msikate tamaa tuendelee kuchapa kazi ili tuwahudumie wananchi,” alisisitiza.

Mhe. Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo zikiwemo ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iliweza kukusanya kiasi cha sh. Bilioni 25.1 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Bonophace Butondo akifungua kikao cha Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Wajumbe wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

TRA YATOA ELIMU YA MAADILI, MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI KWA WATUMISHI WAKE TANGA

0
0
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akiwasilisha mada kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi wa TRA mkoani Tanga kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.

Na Veronica Kazimoto, Tanga

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu ya maadili na mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi wake mkoani Tanga kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kufuata maadili ya kazi ipasavyo.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada ya Mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mwaka 2018, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka TRA Makao Makuu amesema kuwa, kila mtumishi wa TRA anapaswa kujua sheria za kodi na mabadiliko yake kwa undani ili aweze kutoa huduma stahiki kwa wateja.

"Kila mwaka wa fedha unapoingia, Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanya mabadiliko mbalimbali ya sheria na kanuni za ukusanyaji wa kodi, hivyo ni muhimu kila mtumishi wa TRA kujua mabadiliko na kanuni hizo kwa lengo la kutoa huduma stahiki kwa wateja wetu,"  alisema Masalla.

Aidha, Meneja huyo wa Elimu kwa Mlipakodi amewataka watumishi hao kufuata sheria na kuepuka upendeleo wakati wote wanapotoa huduma kwa wateja wanaotembelea ofisi za TRA.

Naye, Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida Rweikiza kutoka TRA Makao Makuu, amewaambia watumishi hao kuwa, ni muhimu kuzingatia maadili kila wanapotimiza wajibu wao ili kuondoa malalamiko ambayo yanaharibu taswira nzuri ya TRA.

"Kila mmoja wetu ana jukumu la kuilinda taswira ya mamlaka yetu, hivyo ni wajibu wetu kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kutumia lugha nzuri kila tunapowahudumia wateja," alisema Rweikiza.

Timu ya Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa elimu ya maadili na mabadiliko ya Sheria za Kodi ikiwa ni pamoja na Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi kwa watumishi wa TRA na wafanyabiashara wa Mikoa ya Kanda ya Kasikazini.
Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida Rweikiza kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akizungumza na watumishi wa TRA mkoani Tanga wakati wa utoaji elimu ya Maadili na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi hao kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga Masawa Masatu akizungumza wakati wa utoaji elimu ya Maadili na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi TRA mkoani hapo kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.
Afisa Kodi Mwandamizi Gelas Kinabo wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Tanga akichangia hoja wakati wa utoaji elimu ya Maadili na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa watumishi TRA mkoani hapo kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kutekeleza na kusimamia sheria za kodi kwa ufanisi na kutoa huduma stahiki kwa wateja.

MANISPAA YA TABORA YAAGIZWA KUJENGA BANDA LA ABIRA KATIKA STENDI MPYA

0
0
Na Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanajenga banda kwa ajili ya abiria kupumzikia wakati wakisubiri usafiri au wanapowasili.

Alisema baadhi ya wasafiri wamekuwa na watoto wadogo na wazee ambao wamekuwa wakipata shida ya sehemu ya kujikinga na jua au mvua wakati wa masika.

Mwanri alitoa kauli hiyo jana kufuatia malalamiko kutoka kwa wasafiri wakati akiwa katika maadhimisho ya Siku ya usafi Duniani ambapo Kimkoa yalifanyika katika eneo la Stendi mpya ya Manispaa ya Tabora.

Alisema wanacholalamikia wasafiri kiko sahihi Stendi hiyo haina sehemu ya wasafiri kumpuzika wakati wakisubiri usafiri wa kuendelea au wale wanaowasubiri ndugu zao wawapokee.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema ni vema wakatumia sehemu ya fedha wanazokusanya katika Stendi hiyoo kwa ajili ya kuwawekea mazingira mazuri na ambayo ni rafiki kwa wasafiri wote.

Mwanri alisema wakati wanasubiri kuanza ujenzi wa Stendi ya kisasa nje ya mji kwa kutumia fedha kutoka Benki ya Dunia ni vema wakarekebisha kasoro zilizopo katika Stendi ya sasa ili watumiaji wafurahie huduma zake.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora William Mpangala alisema watahakikisha wanafanyia marekebisho na kuongeza kuwa mpango wa muda mrefu ni kujenga Stendi ya kisasa nje ya mji ambayo itakuwa na huduma zote muhimu kwa ajili ya abiria. 
 Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya(kulia) akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Tabora jana wakati wa maadhimisho ya siku ya usafi duniani. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Manispaa ya Tabora William Mpangala
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora na wasafiri wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) jana wakati wa maadhimisho ya siku ya usafi duniani.

QNET: Kusaidia Maendeleo ya Michezo Afrika

0
0

Sekta ya michezo barani Afrika inakua kwa kasi sana. Iwe katika michezo ya riadha (ambayo Afrika ya Mashariki na pembe ya Afrika huwa wanaongoza katika bara zima na hata katika mashindano ya kiulimwengu kwa ujumla), au michezo mingine. Bara la Afrika linabadilika taratibu kuwa mabingwa katika shughuli mbalimbali za michezo ambayo mpaka hivi karibuni zimetawaliwa na nchi za ulaya na Asia.

Kwa ujumla katika mchezo wa mpira wa miguu Afrika imeonyesha viwango vikubwa kwa timu za kiafrika kufanya vizuri katika mashindano ya kidunia. Tunashukuru umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu miongoni mwa mashabiki ndani ya Afrika na wadhamini wapya wenye mapenzi mema wanaojitokeza, wapenzi wa michezo na wadau mwengine.

Miongoni mwa wale ambao wameingia katika ushirika na vyama vikubwa vitatu vya mpira wa miguu barani Afrika ni QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja yenye asili ya Asia ambayo biashara yake iko Afrika na ambayo kwa hakika dunia nzima inaichukulia kuwa ni miongoni mwa mashirika makubwa katika tasnia hiyo.

Mapema mwaka huu, QNET ilisaini mkataba wa ushirikiano wa muda wa miaka miwili na mabingwa wa ligi za vilabu vya Afrika: Ligi ya Mabingwa CAF, Ligi ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Kombe la Super Cup katika mpango wa udhamini unaolenga katika wigo mpana wa kidigitali na shughuli ambazo zinalenga kukuza ushirikiano wa mashabiki na wawakilishi wa QNEt (IRs) Afrika.

Akizungumzia kuhusu udhamini huo, CEO wa QNET bwana Trevor Kuna alisema kwamba ushirikiano huo na CAF ni uwekezaji muhimu sana kwa kampuni, ambayo unaendana na wateja wake na jamii ya Afrika kwa ujumla. Ikiwa inawianisha bidii za kimichezo na biashara ya QNET. Bwana Kuna alihamasisha: “Kama mpira wa miguu, QNET inaunganisha dunia na kuhamaisha ari ya kufanya kazi kwa pamoja kama timu miongoni mwa wawakilishi wake (IRS) na kila mmoja anayehusika katika biashara yetu. Kufanya kazi kama timu na utendaji thabini ni mambo ambayo yako sambamba katika mpira wa miguu na biashara ya masoko ya mtandao”

Udhamini huu pia ni kilemba kingine katika kofia ya QNET na inaonyesha tena jitihada za kampuni ya mauzo ya moja kwa moja katika kuthamini maadili ya michezo: Umakini, kufanya kazi kwa bidii na kuongeza bidii mpaka kiwango cha mwisho. Ushirikiano huu unakuja kama jukumu la QNET kama mshirika rasmi wa mauzo ya moja kwa moja wa Klabu ya Mpira wa Miguu wa Manchester City, shughuli ambayo imeiwezesha QNET kuunganisha msisimko wa mpira wa miguu na shauku ya mashabiki katika msisimko wa mauzo ya moja kwa moja na msukumo wa wawakilishi (IRs) wa QNET

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>>

WAZIRI MKUU ATAKA MIKAKATI ZAIDI KUKABILIANA NA DAWA ZA KULEVYA

0
0
*Azungumzia dawa za viwandani zinavyotumika kama dawa za kulevya

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 huku akieleza kuwepo kwa mbinu mpya ambapo dawa za viwandani zimeanza kutumiwa na baadhi ya watu kama sehemu dawa za kulevya.


Hivyo amesema ipo haja ya kuhakikisha kunakuwa na mikakati mipya ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya huku akiomba wakuu wa vyombo vinavyohusika na kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika kuweka mikakati ya kuiabiliana na mbinu mbalimbali ambazo zinatumiwa na wanaofanya biashara hiyo.

Waziri Mkuu amesema hayo leo baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC),ambao unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza ipo haja kwa nchi hizo kuangalia kwa namna gani wanaweza kuweka mikakati ya kukomesha biashara ya dawa za kulevya.
Ameeleza namna ambavyo baada ya kufanikiwa kudhibitiwa kwa dawa za kulevya wapo baadhi ya watu wasiwaaminifu ambao wanachukua dawa zinazotengenezwa viwandani kama sehemu ya dawa za kulevya.


Ametoa mfano wa dawa hizo ni pamoja na dawa za usingizi ."Zipo dawa zinazotengenezwa viwandani watu wasiowaaminifu wanazichukua na kisha kuzibadilishia matumizi kuwa dawa za kulevya,"amesema.

Hivyo amesema lengo la  mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bibi Jo Dedeyne ambaye ni  Katibu Mkuu Kiongozi wa Taasisi za  Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia dawa za kulevya na uhalifu (United Nations Office on Drugs na Crime - UNODC)  baada ya kufungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTAMBO KUPIMA SAMPULI YA MAGONJWA YA SARATANI WAZINDULIWA

0
0
Na Khadija Seif , Globu ya jamii

WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na  Taasisi ya Madaktari nchini Marekani  inayoshughulika na magonjwa ya saratani (ASCP) wamezindua rasmi mitambo wa kupima sampuli ya vipimo  vitakavowezesha  kwa baadhi ya magonjwa kama saratani kufanyiwa ugunduzi wa haraka zaidi.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Mpoki Ulisubisya amesema leo jijini Dar es Salaam dhumuni la taasisi hiyo ni kupunguza mrundikano wa wagonjwa wengi kwa wakati mmoja.

Amefafanua kwani hapo awali vipimo hivyo vilikua vikichukua muda mrefu kupata majibu hivyo basi mtambo huo utawezesha kutoa majibu  ndani ya siku tatu na kumpatia tiba haraka mgonjwa atakaegundulika ana tatizo la saratani.

Dk.Ulisubiya ameongeza wataalam waliopo kwa sasa ni takribani 20 ambao wanataaluma ya Pathology ambao watasaidia wagonjwa wenye saratani  na hospital ambazo zimepewa vifaa hivyo ikiwamo Hospital ya Taifa Muhimbil, Ocean road na KCMC Moshi  itawasaidia wakufunzi kusoma kwa vitendo zaidi.

Kwa upande wa Daktari wa magonjwa ya saratan  Dk. Edda vuhahula ametoa shukrani za dhati kwa taasisi hiyo kwa kuleta vitendea kazi   na kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutoa tiba haraka na kunusuru kutokana na magonjwa hayo.

KAGERE ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA MWEZI WA NANE LIGI KUU TPL

0
0
Na Agness Francis, Blobu ya Jamii

MCHEZAJI wa Klabu ya Simba Middie Kagere amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Agosti wa Ligi kuu Tanzania bara (TPL) msimu huu 2018-19.

Mshambuliaji huyo anayevalia jezi namba 10 katika kikosi hicho ambacho maskani yake iko mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashida wenzake wawili.

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)limesema kuwa wachezaji hao waliokuwa wakiwania nafasi hiyo ni Joseph Mahundi ambaye ni mchezaji wa Azam FC pamoja na Omary Mponda wa Kagera Sugar alioingia nao fainali katika kinyanyang'anyiro hicho.

Hata hivyo raia huyo wa kigeni kutoka Rwanda alikuwa akiongoza kwa kufunga magoli  msimu huu ambapo katika mtanange wa kwanza  dhidi ya Tanzania Prison alifunga goli moja,

Ambapo pia alipata mabao mengine mawili walipocheza na vijana wa Mbeya city hapa Jijini Dar es Salaam katika dimba la Taifa,

Hata hivyo rekodi yake imevunjwa na mchezaji wa Stand United Hakizimana Kitenge ambaye ni raia wa Burundi aliefunga hat-trick rekodi ya kwanza msimu huu jana dhidi ya Yanga.

Kagere ambaye ndio mara ya kwanza anachezea Ligi Kuu ya Tanzania (TPL) akitokea katika kikosi cha  Gor Mahia nchini Kenya alikokuwa akikipiga kabubumbu.

Tanzania Remix watapeli bilioni 3.7 za serikali

0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TANZANIA Remix watapeli bilioni 3.7 fedha za serikali ambazo zilikuwa kwaajili ya fidia kwa wahanga wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Fedha hizo zilkuwa kwaajili ya kununua maeneo ya wananchi waliokuwa wananishi kipunguni A na Kipunguni Mashariki.

Akizungumza na wanachi wa kata ya Luhangwa Kata ya Msongola manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaamleo, Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye alipotembelea viwanja vya fidia vya Luhangwa amesema kuwa serikali inataka viwanja ambavyo havina mgogoro na vilivyolipiwa kwa kuwa serikali ishalipia fedha viwanja vyote 537 ambavyo vinadhamani ya shilingi bilioni 3.7.

" Tanzania Remix ninawapa wiki moja kupima na kuwalipwa wananchi fedha zao za viwanja kulingana na mkataba wao. Msipofanya hivyo Jumatatu ya Septemba 24,2018 hamtaru nyumbani mtaenda sehemu tofauti na nyumbani " Amesema Nditiye.

"Tanzania Remix imelipwa Fesha ya viwanja 537 ambavyo  vinatakiwa kuwapa  wananchi wa kipungunj A na Kipunguni Mashariki kama ya fidia kwaajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege na kwakuwa hawajawalipa wenyevinjwa leo tuhairishe shughuli ya ukaguzi wa viwanja na tuwape muda Tanzania Remix kuwalipa wenye viwanja kwa kadili ya walivyosaini mkataba".

Nditiye ameiagiza Tanzania Remix ifikapo Septemba 24 mwaka huu iwalipe fedha wananchi atakagua viwanja visivyo na mgogoro na wananchi vilivyopangiliwa vizuri kila kiwanja kikijitegemea na vyenye barabara zinazoeleweka.

Wananchi wa Luhangwa  wanena.
Mwenyekiti wa mtaa wa  Luhangwa, Salum Kipendo amesema kuwa yeye pamoja na anaowaongoza hatujalipwa fedha za viwanja kadiri ya mkataba unavyosema kwa asilimia 40 kwa Asilimia 60.

Nae Mrisho Hasimu miliki wa shamba amesema kuwa mimi na baadhi ya wenzangu hatujalipwa fedha za ununuzi wa viwanja kadili ya mkataba tuliosaini sisi na serikali kwaajili ya viwanja vya wananchi waliopisha  upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Tanzania Remix Ilipewa Mradi wa Kununua na Kupima viwanja vya wananchi waliopisha uapanuzi wa uwanja wa ndege Tangu Mwaka 2014 na haija tekeleza
 Naibu waziri wa uchukuzi Mhandisi Atashazita Nditiye akizungumza na wananchi wa Luhanga kata ya Msongola Manispaa ya Ilala jijni Dar es Salaam alipotembelea viwanja vya fidia za wananchi  waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege na kuwapa  Tanzania Remix wiki moja kwaajili ya kuwalipa wananchi stahiki zao kwani serikali imeshatoa fedha kwaajili ya ununuzi wa viwanja hivyo.
  aibu waziri wa uchukuzi Mhandisi Atashazita Nditiye akitembelea viwanja vya fidia kwa wananchi waliopisha upanuaji wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mmilikiwa shamba eneo la Luhangwa,Seif Mbonde  akizungumza na Naibu waziri wa uchukuzi Atashazita Nditiye wakati alipotembelea eneo la viwanja vya fidia za wananchi walipisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa malimu Julius Nyerere Luhanga kata ya Msongola manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja wa ndege (TAA) Richard Mayongela akizungumza na wanachi wa Luhangwa Kata ya  Msongola jijjnj Dar es Salaam na kuwaambia kuwa wao mamlaka ya viwanja vya ndege wameshalipa fedha zote kwaajili ya viwanja waliobakia ni Tanzania Remix ambao wanatakiwa kuwalipa fedha hizo.
Mmiliki wa shamba katika eneo la Luhangwa Mrisho Hashim akizungumza na waandishi wa habari katika eneo Luhangwa kata ya Msongola jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kutolipwa sitahiki yake kadili ya Mkataba wao kati ya Tanzania Remix na baadhu ya wananchi wenye mashamba eneo la Luhangwa kata ya Msingola  Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ikiwa bado hawajalipwa fedha za viwanja vyao kadili ya mkataba unavyosema.  


RC MAKONDA APONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUSIMAMIA AMANI NA UTULIVU UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ya kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kipindi chote cha kampeni za uchaguzi Jimbo la Ukonga hadi uchaguzi uliofanyika siku ya Jana na kumalizika salama pasipo uvunjifu wa amani.

RC Makonda ametoa pongezi hizo leo alipokutana na Makamanda na maafisa wa polisi ambapo amesema anajivunia kuona uchaguzi wa Ukonga umemalizika salama bila fujo wala uvunjifu wa amani.
Aidha RC Makonda amewapongeza wananchi kwa kulinda aman na kulifanya jiji la Dar es salaam kuzidi kuwa na amani masaa 24.

Pamoja na hayo RC Makonda amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na Kamanda wa Polis Kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kwa kuwa na vijana shupavu, wakakamavu na wenye morali ya kuwatumikia wananchi.
 Askari wa Jeshi la Polisi wakimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda. 

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images