Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA BENKI MPYA YA UBL JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua Benki mpya ya UBL, iliyopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Sept 4, 2013. Kushoto na kulia kwa Makamu wa ni baadhi ya viongozi wa juu wa benki hiyo, Anwar Pervez na Atif Bakhari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa benki ya UBL iliyozinduliwa leo Sept 4, 2013 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBL, Zamees Ghudrey, akizungumza wakati alitoa shukrani baada ya uzinduzi huo, uliofanyika leo Sept 4, 2013.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa benki hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais , wakati alipokuwa akiwahutubia kwenye uzinduzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata Keki maalum iliyoandaliwa kuashiria uzinduzi wa benki hiyo mpya ya UBL, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika leo Sept 4, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa benki mpya ya UBL, baada ya uzinduzi wa benki hiyo uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.

MASHINDANO YA SAFARI POOL NGAZI YA MKOA YAZINDULIWA LEO MKOANI IRINGA

0
0
 Diwani wa Kata ya Kitanzini Mkoani Iringa,Madam Jesca Msavatangu(wa pili kushoto) akiwa kwenye maadamano na wachezaji wa Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa wakelekea katika Hospitali ya Rufaa ya Manispaa ya Iringa  kutoa msaada wa vitu mbalimbali kabla ya kuanza mashindano hayo leo.
Diwani wa Kata ya Kitanzini Mkoani Iringa,Madam Jesca Msavatangu(kushoto) akimkabidhi Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Iringa, Rustila Tung’ombe  baadhi ya vitu walivyotoa msaada  katika Hospitali hiyo ambavyo ni pamoja na Sindano,Cloves,Sabuni na Machungwa kabla ya kuanza kwa mashindano ya  Safari Pool Taifa ngazi ya mkoa leo.
Diwani wa Kata ya Kitanzini Mkoani Iringa,Madam Jesca Msavatangu(katikati) akicheza pool kuashilia uzinduzi wa fainali za mashindano ya Safari Pool ngazi ya mkoa  yanayofanyika katika Ukumbi wa Olfare mkoani humo  leo.
Mchezaji wa kike wa Pool wa mkoa wa Iringa, akimkabidhi mama na moto zawadi ya Sabuni na machungwa kama pole wakati vilabu vya mkoa wa iringa vilipokwenda kutoa pole  na vifaa mbalimbali kwa wagongwa kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya Safari Pool ngazi ya mkoa yalioanza jana mkoani humo.

wakili israel magesa afariki dunia leo

0
0


Wakili Israel Magesa  (pichani) amefariki dunia ghafla leo asubuhi.
Wakili Magesa, ambaye  ni mmiliki wa kampuni ya Mawakili ya Magesa &Co. Advocates, ni baba  mzazi wa Phares Magesa(MNEC), Kalimba Magesa, Makongo Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na baba Mkwe wa Haika Lawere.
Wakili Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu, Msajili wa Mahakama kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International - Tanzania Chapter, pia ni mmoja wa wanasiasa waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini.
Enzi za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, na alikuwa ni miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na shughuli rasmi ya kuaga itafanyika ijumaa tarehe 6/9/2013 kuanzia Saa 5 asubuhi Dares Salaam na mazishi yatafanyika siku ya jumapili 8/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete washiriki mazishi ya askofu Mkuu wa kanisa la EAGT marehemu Dkt. Moses Kulola

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho na kuweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Muasisi na askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT Marehemu Dkt. Moses Kulola wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa huko Bugando Mwanza leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bibi.Elizabeth Kulola mjane wa Marehemu Askofu Dkt.Moses Kulola,aliyekuwa muasisi na Askofu Mkuu wa Kanisa laEAG(T) wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika viwanja vya kanisa huko Bugando Mwanza leo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

NDUGU KINANA AKUTANA NA BALOZI WA SUDAN

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali,kabla ya mazungumzo naye, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Saloaam. Picha na Bashir Nkoromo.

AMBASSADOR MODEST MERO PRESENTS HIS LETTERS OF CREDENCE IN GENEVA

0
0
His Excellency Mr. Modest Jonathan Mero, has today, 4 September 2013, presented to Mr. Kassym-Jomart Tokayev, Director General of the United Nations Office at Geneva, the Letters of Credence accrediting him as Ambassador and Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations office in Geneva.
Ambassador Modest Mero presenting his Letters of Credence to H.EMr. Kassym-Jomart Tokayev
From left, H.E Mr. Mr. Kassym-Jomart Tokayev, Mrs. Rose Mero and Ambassador Modest Mero

kesi ya bilionea wa madini aliyeuwawa Arusha yaanza

0
0
 Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
 Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani kusikiliza kesi hiyo.
 Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .

MKUTANO WA SADCOPAC WAENDELEA JIJINI ARUSHA

0
0
Mkutano wa 10 wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka Mabunge ya Nchi wananchama wa SADC ujulikanao kama (SADCOPAC) unaendelea jijini Arusha, ambapo kamati ya Bunge ya PAC ndio mwenyeji wa Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akiwasilisha Taarifa ya Tanzania ya utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 8 na 9 ikiwa ni matakwa ya Wajumbe wa Mkutano huo ambapo kila Nchi wanachama huwasilisha taarifa hiyo.
Mjumbe wa Mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC kutoka Tanzania Mhe. Asumpta Mshama akiuliza swali wakati wa majadiliano ya mkutano wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) unaoendelea Arusha. Tanzania imewasilisha utekelezaji wa maazimio ya mikutano ya 8 na 9 katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akimweleza jambo Mwenyekiti wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) ambaye pia ni mwenyekiti wa PAC kutoka Bunge la Afrika Kusini Mhe. Sipho Makama wakati wa mapumziko ya Mkutano wa 10 wa SADCOPAC unaendelea Arusha.

KAMATI YA USHAURI WA UGAWAJI VITALU YAZINDULIWA

0
0
Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii ikiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki  (mwenye kaunda suti) na Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ibrahim Mussa (wa kwanza kulia).


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki amezindua rasmi Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Utalii  nchini.
Kamati hiyo inaundwa na wajumbe 10 kutoka sekta mbalimbali  na inajukumu la kumshauri waziri katika masuala yote yalioainishwa  kwenye sheria na kanuni za Wanyamapori juu ya ugawaji vitalu. 
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Selous uliopo Wizara ya Maliasili na Utalii Makao Makuu, Dar es Salaam, Mhe. Kagasheki alisema anaimani kamati hiyo itamsaidia kwa kumpa ushauri utakaokuwa umefanyiwa utafiti wakina kutokana na kamati hiyo kuundwa na watu wenye uweledi na uzoefu mbalimbali katika masuala ya usimamizi wa raslimali na maliasili.

Aidha, Mhe. Kagasheki aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kutekeleza majukumu waliopewa kwa kushirikiana kikamilifu na kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu, Prof. Leticia Rutashobya alimshukuru Mhe. Waziri kwa kumpa jukumu la kuongoza kamati hiyo na kuahidi kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa uadilifu.


Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu inaundwa na Prof. Leticia Rutashobya (mwenyekiti) na wajumbe wake Mhe. Zakhia Hamdan Meghji, Bw. Alli Mufuruki, Bw. Mohamed Abdukadir, Bw. Raymond Mbilinyi, Dkt. Simon Mduma, Bw. Allan Kijazi, Dkt. Fred Manongi, Prof. Alexander N. Songorwa na Bi. Agnes Ndumati; na itahudumu hadi tarehe 15 Julai, 2016.

TANZANIA KWANZA.... USA AMBASSADOR TELLS TANZANIANS

0
0
The USA Ambassador to Tanzania H.E Alfonso Lenhardt (centre) says goodbye to Tanzania as he accomplished his tour of duty after four years of service. The envoy speaking to the Deputy Speaker of the Parliament of Tanzania Hon. Job Ndugai PM ® urged the Members of Parliament to consider Tanzania First (Tanzania Kwanza) in whatsoever they do…. “be it working for new constitution, fighting corruption, fighting poverty, inviting investors to the country, working with partner states, strengthening Union and the like….. TANZANIA KWANZA should be your focus,“ he insisted. At left is Ms. Virginia Blaser, Deputy Chief of Mission.

Ambassador Lenhardt visited the House in Dodoma to bid farewell just before he leaves the country early in October. He assured the House to keep in touch as he confessed to “have left his heart” in Africa and in particular Tanzania. He asked the MPs and Tanzanians at large to accept and work diligently with the new envoy who is due by the middle of October 2013.

Farewell photos as the US Envoy paid a visit in Dodoma today

Balozi Kamala atembelea kampuni ya Afix Group

0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Kampuni ya Afix Group ya Ubelgiji baada ya kutembelea Kampuni hiyo. Kampuni hiyo inashughulika na uzalishaji wa vitendea kazi vya shughuli za ujenzi. Balozi Kamala anaendelea na ziara ya kikazi ya kuhamasisha makampuni ya Benelux kuwekeza Tanzania kwa kushirikiana na Makampuni ya Tanzania.

Kongamano la Kimataifa la Utamaduni wa utaarabu wa Kiislamu lafanyika zanzibar

0
0
Na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Jamii ya Kiislamu popote pale Duniani inalazima kufanya jitihada za makusudi katika kuona inaendelea kutumia utamaduni wa Kiislam katika muelekeo zaidi wa elimu, mawazo ya maendeleo, biashara, uchumi, siasa, sayansi na utawala kwa lengo la kuuongezea nguvu ya ziada. 
 Hatua hiyo itawapa muono wa kweli watu wengi wasiokuwa waumini wa Dini hiyo kuwaondolea shaka kwamba Uislam si kundi la waumini ambao sera zao ni vurugu, ugaidi na uuwaji mawazo ambayo hata baadhi ya Waislam wanachangia bila kuelewa. 
 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Moh’d Gharib Bilal wakati akilifunga Kongamano la Kimataifa kuhusu Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika ukanda wa Afrika Mashariki Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya La Gemma Del Est Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
Alisema misikitini mingi siku hizi imekuwa na hotuba za hamasa, jazba , uchochezi na kugeuzwa kama majukwaa ya kisiasa badala ya kutolewa hotuba za ibada na mafunzo ya Kiislam yanayohusu kumuabudu Mwenyezi Mungu na mafundisho yake ya kupenda kufanya mazuri aliyoyaamrisha na kukataa mabaya aliyoyakataza. 
Aliwataka wana jamii wa Utamaduni wa kiislamu kutafakari kwa makini athari hii iliyojichomoza ambapo isipozingatiwa na kupatiwa dawa maalum inaweza kumong’onyoa maadili na usaarabu huo wa Kiislamu. Alieleza kwamba ipo haja kwa wakati huu kurejeshwa mfumo wa zamani wa kuifanya Misikiti kuwa ni chimbuko la elimu ambapo ilikuwa mwalimu hukutwa amezunguukwa na vitabu mbali mbali akiendelea kutoa elimu ambapo nyumba zao zikijaa baraza kwa kuwa ni sehemu ya Madrassa. 
 Alifahamisha kwamba elimu ya dini ilipewa umuhimu wa kipekee ambapo kila mtoto alijengewa mazingira ya kupata taaluma ya dini kwanza ikifuatiwa na ile ya elimu ya dunia 
“ Hakukuwa na mtoto ambaye hakuweza kupata elimu. Vyuo (Madrassa) vilienea kila pembe. Vijijini ilikuwa wazazi wakenda kulima mtoto mdogo anapelekwa chuoni kulelewa na wakubwa zake. Kwa hiyo alianza kupata hisia za elimu akiwa tangu mdogo “.Alifafanua Makamu wa Raiswa Serikali ya Jmuhuri ya muungano wa Tanzania. 
Dr. Bilal alisema kwamba Utamaduni wa Kiislam umepata nguvu kubwa kutokana na msingi wake wa kurithisha vizazi kwa njia ya mashairi, maandiko na tungo tofauti, hivyo si kosa kueleweka kuwa utamaduni huo umejengwa chini ya msingi wa elimu kwa vile chimbuko lake linatokana na Qur’aan na Sira za Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad (SAW). 
“ Mbali na athari zilizojichomoza lakini bado utamaduni wa Kiislam unabaki kuwa ni utamaduni wa Kiislam. Una miko yake, una sifa zake na una matumizi yake. Utamaduni wa Kiislam unaweza kujisifu kuwa umeweza kusaidia ukuaji wa tamaduni nyingi hasa za Ulaya “. Alifafanua Dr. Moh’d Gharib Bilal. 
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alisisitiza kwamba Ukuaji wa lugha ya kiarabu kuwa ya Kimataifa ya sayansi na uendeshaji Serikali umesaidia kuufanya Uislam uwe kiungo cha maendeleo chini ya msingi wa Quran inayowaagiza waumini kutafuta elimu popote pale na muda wote wa umri wao. 
Amewapongeza waliowaza kufanya kongamano kama hili hapa Zanzibar na hasa wakati huu ambao Uislam unapita katika mitihani mikubwa na kuelezea matumaini yake kutokana na ushiriki mkubwa wa wajumbe utakaotoa maazimio mazuri yatakayosaidia kupeleka mbele Uislam na ustaarabu wake. 
 Akisoma maazimio ya wana kongamano hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kongamano hilo Dr. Juma Halifa Juma alisema wana kongamano hilo wamependekeza kuendelezwa kwa makongamano hayo kila mara. Dr Juma alisema wana kongamano hao walisisitiza umuhimu wa kuandikwa kwa Historia ya Uislamu wa Afrika ya Mashariki na baadaye kuingizwa katika mitaala itakayozingatia mfumo wa sasa wa Sayansi na Teknolojia. Walisema umuhimu wa kubadilishana utafiti kati ya waislamu wa Afrika na wenzao wa mabara mengine Duniani unafaa kuzingatiwa vyema ili usaidie kuimarisha kasi ya utamaduni na Dini ya Kiislamu popote duniani. 
Wana kongamano hao wamemshukuru Mfalme Qaboos Bin Said wa Oman kwa uamuzi wa Serikali yake kupitia Taasisi zake kuandaa kongamo hilo lililotoa fura kwa wanafalsafa, wasomi na waumini wa dini ya kiislam kupata kubadilishana mawazo. 
Naye Mwenyekiti wa mamlaka ya kutunza nyaraka na kumbu kumbu ya Qasri Nchini Oman Dr. Hamad Moh’d Al – Dhawian Bin Balqas alielezea faraja yake kutokana na michango mikubwa ya washiriki wa Kongamano hilo hasa wale wenyeji Zanzibar. 
Dr. Hamad alisema utafiti unaonyesha wazi kwamba Afrika Mashariki ni markaz ya kuleta mabadiliko ya butamaduni wa ustaarabu wa Kiislamu hapa ulimwenguni. Akimaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna alisema Zanzibar imepata heshima na bahati kubwa ya kuteuliwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo jambo ambalo litaijengea historia ndefu katika masuala ya utamaduni wa ustaarabu wa kiislamu Duniani. 
Jumla ya nyaraka 60 zilijadiliwa katika kongamano hilo lililosheheni wataalamu, wasomi, watafiti na hata wanavyuoni wa dini ya Kiislamu kutoka pembe mbali mbali za Dunia. 
Kongamano hilo la pili la Kimataifa la ustaarabu wa Kiislamu likitanguliwa na lile llililofanyika Uganda mwaka 2012 na limeshirikisha Mataifa kumi na saba mbali mbali Duniani likiwa na lengo la kujitanga za Zanzibar katika Nyanja za Utafiti na Taaluma Kimataifa. 
Serikali ya Oman kupitia ushirikiano wa mamlaka ya kumbu kumbu na nyara ya Nchi hiyo ndio iliyoandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar { SUZA }.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akielekea kwenye ukumbi wa Kongamano la Kimataifa la Utamaduni wa utaarabu wa Kiislamu lililofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya La Gemma De est Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja akiwa na wenyeji wake Mkuu wa Mkoa huo Pemba Juma Khamis Kati kati na Waziri wa Habari wa Omar Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al-Hasani.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Juma Shamuhuna akitoa hotuba ya kukaribisha mgeni rasmi Balozi Seif kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Moh’d Gharib Bilal kulifunga Kongamano la Kimataifa la Ustaarab wa Utamaduni Afrika Mashariki.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifunga Kongamano la Kimataifa la Ustaarabu wa Utamaduni wa Kiislamu Afrika Mashariki kwenye hoteli ya La Gemma De Est Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano la Kongamano la Kimataifa la Ustaarab wa Utamaduni wa Kiislamu afrika mashariki kwenye hoteli ya La Gemma De Est Nungwi wakifuiatilia hotuba ya ufungaji wa kongamano hilo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Waziri Mkuu na Katibu Mkuu  Umoja wa Afrika mstaafu Dr. Salim Ahmed Salim ambaye naye alikuwa mshiriki wa kongamano la Kimataifa la Ustaarab wa Utamaduni wa Kiislamu afrika mashariki.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na wajumbe wa kongamano la Kimataifa la Ustaarab wa Utamaduni wa Kiislamu afrika mashariki kutoka Oman wakiongozwa na sheikhamauhannak Hairus nje ya ukumbi wa Hoteli ya La Gemma De Est Nungwi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

KUZINDULIWA KWA SHINDANO JIPYA LA TANZANIA TOP MODEL.

0
0


Jackson M. Kalikumtima

Mwenyekiti Mtendaji
Shindano la Tanzania Top Model limeanzishwa ili kuziba ombwe lililoko la kuwatafuta,  kuwatayarisha na kuwatafutia mikataba wanamitindo wa kitanzania ambao ndoto zao zimekuwa ni kufanikiwa na kuwa wanamitindo wa Kitaifa na Kimataifa. Ni shindano litakalo wajenga na kuwafanya wajiamini na waaminiwe kwa kazi mbalimbali. Hiki kitakuwa ni kichocheo kingine cha kuitangaza nchi yetu katika mavazi na sanaa nyingine kimataifa na kuwa chimbuko la nyota nyingine katika dunia ya Wanamitindo hapa nchini.
Mashindano ya kumtafuta Tanzania Top Model si mashindano ya kawaida kama tulivyo zoea mashindano ya kuwakutanisha Washiriki na kupima Mshiriki aliye bora tu kuliko wenzake, bali ni Mashindano ya kumtafuta Mwanamitindo bora tena wa Mfano hapa nchini. Haya ni mashindano yatakayo ruhusu Jamii/ Wananchi/ Wadau kushiriki kuchagua mshindi kwa kiwango Fulani. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

cheka unenepa: alamba alamba aaaaaaH!

FUSO LINAUZWA

0
0
Gari hii aina ya Fuso engine 6D16, usajiri T 251 BSG. imetumika muda mfupi na ipo ktk hali nzuri bei 40m. mazungumzo yapo. 
contact 0787 202075 au 0655202075 




ngoma azipendazo ankal

0
0
Ngoma ya The Brothers Johnson ya 'Stomp!' ni balaa enzi zetu

Article 18

SEHEMU YA PILI YA MAHOJIANO YA MWANDISHI WA KISWAHILI- PROF. SAID A MOHAMMED

0
0
 Na Freddy Macha
 Kwa wasomaji wapya. Mwandishi Said A Mohammed keshaandika zaidi ya vitabu thelathini ikiwemo michezo ya kuigiza (tamthiliya), riwaya, mashairi na vitabu ya watoto. Riwaya yake maarufu, Asali Chungu, ilichapwa mara ya kwanza, 1976. Mwandishi aliyetopea, Adam Shafi, aliwahi kusema katika mahojiano na mhadhiri wa Kiswahili Ujerumani, Lutz Diegner, kwamba Asali Chungu ni miongoni mwa hazina kuu za Kiswahili na hupenda sana, kukisoma... KUENDELEA BOFYA HAPA
Said A Mohammed 
Profesa Said A Mohammed, alistahafu kazi ya kufundisha Kiswahili vyuo vikuu mbalimbali duniani, mwaka jana. Soma sehemu ya kwanza ya mahojiano hapa: http://www.kitoto.wordpress.com

Article 16

0
0
20130904_115112_resized
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes kuelekea kwenye chumba cha mikutano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwenye Hospitali hiyo.
20130904_115838_resized
Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili Bi. Agnes Jonathan Mtawa akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uotaji huduma kwa wananchi mbele ya mgeni rasmi Mstahihiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa katika hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali hiyo.
20130904_120709_resized
Katibu wa Neema Womans Power Mgeni Ottow akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
20130904_121628_resized
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
20130904_122836_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi Magodoro 50 kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
20130904_122738_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akimshukuru Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes (mwenye hijabu nyekundu) mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo.
20130904_123027_resized
Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes katika picha ya pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakinamama wa Kikundi cha Neema Womans Power.
Na. Mwandishi wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala MH.JERRY SILAA amekabidhi magodoro 50 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kikundi cha wakimama "NEEMA WOMANS POWER".
Neema Womens Power ni kikundi cha wakina mama kilichoanzishwa mwaka 2005 kwa kuanza na Madrasa mbili ya akinamama na wasichana akiwa na wanafunzi 18 tu. Madrasa hizo zipo Kinondoni na Buguruni chini ya Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Maryam Dedes. Jumuiya hii pamoja na kuwa na Elimu ya dini, husaidia jamii kwa michango mbalimbali ikiwemo kulipia ada za shule kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo, kusaidia Walemavu na Wajane pamoja na familia duni.
Katika hafla hiyo fupi Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitoa kwa kusaidia jamii kwani mzigo uliopo kwa Serikali peke yake haiwezi, na ukizingatia ya kwamba hakuna mtu asiyeijua Hospitali kama si Muhimbili basi Amana, Temeke au Mwananyamala na Hospitali nyingine nyingi zinahitaji msaada vifaa mbalimbali na endapo kila mwananchi angeweza kuchangia japo kifaa kimoja sasa tungekuwa mbali sana na inawezekana kabisa tusingekuwa na matatizo sugu katika Hospitali zetu.
Mh.Jerry ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa ndani ya Halmashauri yake na anayesifika kwa uchapakazi wake na umakini aliwashukuru kwa dhati kabisa uongozi wa Neema Womans Power pamoja na wanachama wao kwa kuliona tatizo hilo na kwa uwezo walionao leo hii wameweza kutoa magodoro hayo 50 na kuwaasa waendelee kujitoa zaidi na wasife moyo maana kazi ya jamii haina malipo zaidi ya fadhira mbele za Mungu.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi Magodoro imehudhuriwa na Bi.Maryam Dedes ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Agnes Jonathan Mtawa- Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili, Mgeni Ottow Katibu wa Neema Womans Power pamoja na Khadija Mwita Makamu mwenyekiti na wajumbe wao 30 na Uongozi wa Hospitali ya muhimbili.

Article 15

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images