Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109588 articles
Browse latest View live

Vijana waliopitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria kambi ya Ruvu JKT Oparesheni Kambarage 1990/91

0
0
Pichani ni baadhi ya vijana wa zamani waliopitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria kambi ya Ruvu JKT (832KJ) Oparesheni Kambarage 1990/91 wakiwa pamoja baada ya kuhudhuria sherehe za kumaliza jeshi vijana kwa mujibu wa Sheria Oparesheni Mererani Ijumaa Septemba 14 kambini Ruvu.

Hii ni miaka 27 tangu vijana hao wa zamani kupitia mafunzo kambini hapo. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa wa zamani aka makuruta wa zamani  Be Ameir Juma Nondo, umoja huo una mpango wa kurudisha fadhila kambini hapo kwa kutoa mchango katika kambi na kijiji Jirani na kamba hiyo kwa kuwa eneo hilo lina kumbu kumbu kubwa katika ujenzi wa maisha ya vijana hao waliopita hapo . 
 Be. Nondo ametaja miongoni mwa mambo waliyojifunza kambini hapo ni pamoja na uzalendo kwa nchi yao, ujasiri katika maisha, upendo na mshikamano katika jamii pamoja na kujituma, kuchapa kazi kwa bidii, utiifu na umakini katika kazi na maisha kwa ujumla. 
 Mgeni rasmi katika sherehe za ufungaji mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Joketi Mwegelo amewataka vijana hao kuepuka kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwani kuna Sheria ya Makosa ya mtandao inaweza kuchukuliwa dhidi yao. 
 Aidha, mgeni rasmi hiyo amewataka vijana waliomaliza mafunzo hayo kuwa wazalendo , watiifu, wachapakazi, waadilifu na mabalozi wazuri popote watakapokwenda kuitumikia nchi.

HUMPHREY POLEPOLE AHITIMISHA KAMPENI VINGUNGUTI KWA KUSEMA KUMBILAMOTO NA VINGUNGUTI MPYA

CCM WAFUNGA KAMPENI KIBABE JIMBO LA UKONGA,DK. BASHIRU ATOA MSIMAMO KWA WANANCHI,AELEZA NAMNA WALIVYOJIPANGA

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimehitimisha kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa kuwahakikishia wananchi yote yaliyoahidiwa yatatekelezwa na hakuna wa kuwarudisha nyuma.

Wakati wa kuhitimisha kampeni hizo leo mamia ya wananchi wa Jimbo la Ukonga wamejitokeza kwa wingi huku Katibu Mkuu wa CCM  Dk.Bashiru Alli akiweka wazi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Dk.John Magufuli amefanikiwa kudhibiti ugonjwa uliokuwepo wa baadhi ya wanachama  kutumia rushwa ili kupata uongozi

Akizungumza mbele ya maelfu ya  wananchi wa jimbo hilo Dk.Bashiru amewaomba wamchague mgombea ubunge wa CCM Mwita Waitara kwani ndio mtu sahihi huku akieleza namna ambavyo Chama hicho kimejipanga katika kuwatumikia wananchi hasa katika kuwaletea maendeleo. Ameeleza miradi  namna mikubwa ya maendeleo inavyoendelea kutekelezwa na kwamba anawashangaa wanaodai uchumi umedorora.

Hivyo Dk.Bashiru amewaomba wananchi hao kumchagua Waitara kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika suala la maendeleo. Pia amewahakikishia waliohamia CCM kwamba wote  wana haki zote za uwanachama na hakuna ubaguzi na kuwahakikishia kwa namna ambavyo wamejipanga waliohamia na watakaoendelea kuhamia hawataondoka tena.

Amewaambia wananchi kwa sasa CCM kuna mambo kadhaa yanayofanyika ili kiendelee kuwa imara zaidi.Ametaja baadhi ya mambo hayo ni  kuwa na sauti moja kati ya Serikali na Chama.Pia wanaimarisha umoja ndani ya chama hicho.

"Moja ya changamoto ya kufa kwa upinzani ni kukosekana kwa umoja na CCM tumegundua hilo na ndio maana tumeamua kuimarisha umoja na mshikamano," amefafanua.

Pia amesema CCM imebadilika tofauti na hapo nyuma ambapo kulikuwa na tabia ya kupanga safu na vyeo lakini sasa ugonjwa huo umepona na aliyeutibu ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk.John Magufuli.

Dk.Bashiru ametoa onyo kwa watendaji wenye tabia ya kuwa na wagombea wao na atakayebainika atamfukuza na kwamba huu si wakati wa kubeba wagombea wala kupanga safu kwani wanachama wote ni sawa.

"Muda wa kutafuta vyeo haujafika na kwamba hatutaki yaliyotokea mwaka 2015 wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu yarudie.Wanaotembea na wagombea wao nitawachukulia hatua kwani hilo lipo ndani ya uwezo wangu," amesema.

Wakati huo huo amesema wapo wanaodai kwamba CCM hawakufuata utaratibu kumpata mgombea wake lakini ukweli taratibu zote zimefuatwa ambapo ikiwa pamoja na mgombea kuchukua fomu kwa Katibu wa Wilaya na kisha mchakato wote kuendelea kwa utaratibu uliopo. Hivyo amewaomba wananchi katika uchaguzi wa kesho wahakikishe wanamchagua mgombea wa CCM.
Kwa upande wake Waitara amewaomba wananchi wa Ukonga wampigie kura na lengo lake ni kuwa mbunge ambaye atakuwa na jukumu la kuzungumzia maendeleo ya jimbo hilo na atakuwa na nafasi sahihi ya kuzungumza maendeleo.
Pia amesema wapo wanaosema amenunuliwa,hivyo anataka kuwathibitishia Chadema kwamba hajanunuliwa huku akieleza namna ambavyo CCM ilivyokuwa na mpangilio wa kutekeleza mambo yake.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akimnadi  mgombea wa  ubunge  CCM,Mwita Waitara ambapo amewaomba wananchi aajitokeze kwa wingi na kumpigia kula mgombea wa CCM.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongizi wa chama hicho na wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za uchanguzi jimbo la Ukonga ambapo  amewaomba wa wananchi wamchague mgombea wa ubunge wa CCM,Mwita Waitara.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza leo na wananchi wa Ukonga katika ufungaji wa kampeni za uchaguzi ambapo amewaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura  na kumchngua kiongozi anao ataowaletea maendeleo.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwapokea wanancha waliotoka vyama vya upinzani






MHADHIRI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM DK.MISANYA BINGI AFARIKI DUNIA AKIPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MUHIMBILI

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

NI pigo!Ndivyo unavyoweza kuelezea taarifa za kufariki dunia kwa Mhadhiri wa  Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),Dk.Misanya Dismas Bingi.

Dk.Misanya ambaye pia amewahi kuwa mtangazaji maarufu nchini  wa Radio One na ITV amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuz Blog Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbii Aminiel Aligaeshi amesema Dk.Misanya amefia MOI ila mwili wake umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti Muhimbili.

 Dk.Misanya Bingi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.Alifikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili  baada ya kupata ugonjwa wa kupooza(stroke) na kupelekwa katika chumba cha Uangalizi maalum (ICU).

Kwa sasa msiba upo eneo la Makongo Juu jijini Dar es Salaam wakati taratibu nyingine zikiendelea.Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea kuhusu msiba huo.

Pia Michuzi Blog inaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na msiba huo mzito wa kuondokewa na mendwa wao Dk.Misanya Bingi.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN.

WAZAZI WATAKIWA KUONDOKANA NA DHANA POTOFU.

0
0

Na Frankius Cleophace Tarime.

Wazazi na walezi Wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kuondokana na dhama potofu kwa kupotosha jamii pale seriklai inapopeleka huduma ya afya huku wakitakiwa kukujenga tabia za kupima afya zao mara kwa mara bila kusahua watoto wa kike ili kuondona na vifo vya ghafla ambavyo vimekuwa vikijitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara Mchungaji Abel Obura kipindi akifunga tamasha la kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ukiwemo Ukeketaji lililoandaliwa na Shirika la RIGHT TO PLAY nakufanyika katika Shule ya Msingi Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Mchungaji amesema kuwa jamii imekuwa ikipotoshwa pale serikali inapopeleka madawa mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya za watoto nakusababisha baadhi ya watoto wengine kokosa huduma hiyo.“Serikali inaleta dawa za minyoo lakini jamii inapotoshwa kuwa wakimeza dawa hizo hawatazaa jambo ambalo siyo kweli na serikali inaleta dawa ambazo tayari zimethibitishwa hivyo sasa jamii iondokane na dhana potofu” alisema Mchungaji.

Pia Mchungjai amewataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kuwapima watoto wao kwani ni haki zao za msingi ikiwemo kupatiwa pia elimu ya msingi mpaka sekondari.

Kwa upande wake Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la RIGH TO PLAY ambao wanatoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijinsia kupitia matamasha ambayo yanahusisha michezo mbalimbali yakiwemo maigizo, Nyimbo, Ngoma, Mpira wa miguu kwa wasichana, kuvuta kamba na Mashariri, michezo hiyo imebeba ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia.

“Michezo inakusanya watu wengi hivyo sisi kama shirika tumeamua kutumia michezo kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa katika jamii ya Mkoa wa Mara ili kulinda na kutetea haki za watoto ikiwemo kupata elimu” alisema Leah.

Aidha wananchi na wakazi wa kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti mkoni Mara wanazidi kupongeza uwepo wa matamasha hayo ya kutoa elimu katika jamii huku wasema kuwa suala la ukeketaji linazidi kupungua kila kukicha bali elimu ienndelee kutolewa katika jamii ili kuondoa usiri uliopo kwa sasa.

“Baada ya serikali kutilia mkazo suala la kupinga ukeketaji kuna usiri mkubwa unafanyia sasa elimi izidi kutolewa katika maeneo ya vijijini” walisema Wananachi hao.
Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkiani Mara Mchungaji Abel Obura akifunga tamasha hilo la kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia ukiwemo ukeketaji lililoandaliwa na shirika la RIGTH TO PLAY.
Leah Kimaroambaye ni mwezeshaji kutika Shirika la RIGHT TO PLAY akitoa Elimu ya kupinga Ukatili katika jamii kwenye tamamsha liloandaliwa na shirika hilo na kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Maburi kata ya Nyambureti wilayani Serengeti Mkoani Mara.
mgeni rasmi ambaye ni Mchungaji wa kanisa la Anglikana lililopo Kijiji cha Maburi kata ya Nyambureti Wilayani Serengeti Mkoani Mara, Mchungaji Abel Obura akisalimiana na wachezaji baina ya timu ya Nyambureti Sekondari FC na Kerukerege FC. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

MABONDIA 18 LEO KUONESHA UMWAMBA KATIKA ULINGO WA CCM MWINJUMA DAR

0
0

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii


MABONDIA 18 leo wanatarajia kupanda ulingoni katika ukumbi wa ulingo wa CCM Mwinjuma uliopo Mwananyamala kuwania mataji mbalimbali katika mchezo wa ngumi likiongozwa na pambano la raundi 10 kati ya Bushiri Kulwa na Seba.

Mapambano hyao yaliyoandaliwa na Kampuni ya ‘Golden Boy Africa’ yanawakutaniosha mabondia hao wanaowania mkanda wa Dunia katika uzito wa kilo 84 ‘Cruiser weights’ linatajwa kuwa la kipekee na hasa kutokanana na viwango walivyonavyo mabondia wote wawili katika medani ya ‘masumbwi’

Mbali na pambano hilo ,.michezo mingine inatarajiwa kuwakutanisha mabondia Simba na Allen, Chidi Mbishi dhidi ya Moro Best,Mkalekwa Junior dhidi ya Abdala Luwanje, Hamisi Maya dhidi ya Karage Suba itakayochezwa kwa raundi nane kila mmoja.

Mapambano mengine ambayo ni pamoja na bondia Mbunju Laga dhidi ya Iman Tavez, Nurdin Mohammed dhidi ya Issa Mbwana , Mlekwa dhidi ya Rama, pamoja na pambano kati ya Modest John dhidi ya Kassim Juma, yote yakichezwa kwa raundi 6.

Mratibu wa mapambano hayo Shomari Kimbau, alisema tayari maandalizi yote yamekwisha fanyika ikiwemo mabondia kupima afya zao kabla ya mchezo na kwamba kinachosubiriwa na kutimia kwa muda husika.

Alisema ‘mpambano’ huo unaotarajiwa kuanza saa 10 za jioni, unatarajiwa kuwa wa kuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mabondia wote, hasa kutokana na namna ambavyo kila kambi ya mabondia hao iolivyojipanga ili kupata ushindi.

Awataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia vipaji kutoka kwa mabondia mbalimbali wa hapa nchinim huku akisisitiza uwepo wa suala la ulinzi na usalama kwa mashabiki watakaojitokeza kutazama pambano hilo. 

DAWASA WAANZA KUDHIBITI UVUJAJI WA MAJI TABATA

0
0
* Yazindua siku tatu za kumaliza tatizo la uvujaji maji katika kata 11.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamezindua uzibaji wa mivujo ya mabomba inayomwaga maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakianzia katika maeneo ya Tabata zoezi litakalodumu kwa muda wa siku tatu ikiwa ni katika kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya siku 100. 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhaandisi Aron Joseph alipozindua mkakati huo wa kuhakikisha maeneo yote yanayotiririsha maji kutoka kwenye miundo mbinu ya Dawasa yanafanyiwa kazi kwa asilimia 90 na kisha kukabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata. 

Akielezea zoezi hilo lilioanza leo, Aron amesema kuwa watatembelea maeneo yote ya Tabata yenye kata 11 zinazopata huduma za maji na kupambana na mivujo na tayari wataalamu wameshaingia kazini kwa ajili ya kuyafanyia kazi. "Kuna timu zaidi ya watu 70 katika maeneo 20 tofauti ndani ya Tabata ambapo kuna kata 11 yenye maji na watalaamu hao wote wapo kuhakikisha mivujo yote inayojulikana na ile mipya wanafanyia marekebisho maeneo hayo yamefanyiwa kazi ndani ya siku tatu na iwe imeondoka,"amesema Aron. 

Amesema nia na madhumuni ya kufanya zoezi hili ni kuhakikisha eneo lote la Tabata lenye maeneo sugu na mapya yanayovuja kupatiwa ufumbuzi na iwe imeondoka kabisa na katika hilo na wamemtaka Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata kuhakikisha inapotokea mivujo anatakiwa kuidhibiti na kuziba ndani ya masaa 6. 

Aron amesema kuwa anatambua kuna baadhi ya maeneo ya Tabata na sehemu zingine miundo mbinu yake ni chakavu na hilo suala linajulikana, kama Dawasa mpya wameweka mikakati ya kuhakikisha ndani ya miaka mitatu miundo mbinu hiyo inabadilishwa na ili wananchi wasikose maji idara ya uzalishaji na usambazaji maji utahakikisha katika kipindi chote hicho watakuwa wanasimamia miundo mbinu hiyo ili kuondokana na uvujaji wa maji. 

Akiongezea, Aron amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona maji yanavuja kupitia namba yao ambayo haina malipo pia hata watakapowaona mafundi wa Dawasa wawape taarifa ili wakarekebishe eneo hilo. 

Meneja wa Usambazaji maji Mhandisi Paschael Fumbuka amesema zoezi hili ni kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ya maji kwa kuzuia upotevu wa maji kitu ambacho kinaathiri biashara ya maji maana kila tone la maji linahesabiwa. Fumbuka ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Dawasa kuwabaini watu wanaochafua miundo mbinu yao ikiwamo kutiririsha maji taka na hatua za kisheria zitachukuliwa juu yao. 

Dawasa wameanza kutekeleza moja ya mikakati yao siku 100 ya kumaliza miradi mbalimbali na changamoto ikiwemo uvujaji wa maji kutoka katika miundo mbinu yao. 
Baadhi ya mafundi waliokatika maeneo mbalimbali ya Tabata wakiziba uvujaji wa maji baada ya kuzinduliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) utakaofanyika kwa muda wa siku tatu.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Aron Joseph akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika baadhi ya maeneo yanayofanyiwa ukarabati wa uzibaji wa mabomba uliozinduliwa na utachukua siku tatu kukamilisha eneo la Tabata.

MAADHIMISHO YA SABA YA SIKU YA MARA (MARA DAY) YAFANYIKA NCHINI KENYA

0
0


Maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mara (Mara Day)

Bonde la mto Mara linalounganisha Tanzania na Kenya linashikilia uhai sio wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pekee, bali uhai wa nchi za Sudan, Ethiopia na Misri nazo kwa kiasi kikubwa unategemea bonde hilo.

Kauli hiyo ilitolewa na viongozi mbalimbali walioshiriki sherehe za maadhimisho ya saba ya Siku ya Mara (Mara Day) zilizofanyika katika Kaunti ya Narok, Kenya siku ya Jumamosi tarehe 15 Septemba 2018. Maadhimisho ya Siku ya Mara ambayo kwa mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu "Mto Mara unatuunganisha wote" hufanyika kwa kupokezana kati ya Tanzania na Kenya kila mwaka tarehe 15 Septemba kwa madhumuni ya kuhamasisha matumizi endelevu ya bonde la mto Mara.

“Siku ya Mara hailengi chochote, isipokuwa kutukumbusha jukumu letu la kutunza mazingira”, Gavana wa kaunti ya Narok, Mhe Samuel Oletunai alisema katika maadhimisho hayo.Mhe. Samuel Oletunai aliwaasa Wakenya kutunza msitu wa Mau ambao ndio chanzo kikuu cha maji yanayotiririka mto Mara na kuiomba Serikali ya Kenya kuhakikisha kuwa mgogoro katika msitu huo unapatiwa ufumbuzi haraka. 

Mwakilishi wa Serikali ya Tanzania katika maadhimisho hayo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso (Mb) alieleza kuwa maji hayana mbadala kama chakula ambapo ukikosa wali utakula ugali, hivyo aliwahakikishia wadau waliohudhuria sherehe hizo kuwa Serikali ya Tanzania haitakuwa kikwazo cha harakati za kuhifadhi ikolojia ya mto Mara.
Waziri wa Maji na Usafi wa Kenya, Mhe. Simon Chelugui ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya saba ya Siku ya Mara akitoa hotuba ya ufunguzi ambayo ilielezea mikakati mbalimbali inayochukuliwa ili kukabiliana na vihatarishi vya kutokomeza ikolojia ya Mto Mara. 
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Mara yaliyofanyika kaunti ya Narok nchini Kenya
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Chana akitoa salamu katika maadhimisho ya Siku ya Mara. 
Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana; Katibu Tawala wa mkoa wa Mara, Bibi Caroline Mthapula; Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso; Waziri wa Maji na Usafi wa Kenya, Mhe. Simon Chelugui wakipata maelezo kutoka moja ya banda la maonesho ya Siku ya Mara kuhusu utunzaji wa mazingira. 
Mmoja wa wanaharakati wa kutunza Mazingira akipokea cheti cha kutambua mchango wake kutoka kwa Gavana wa kaunti ya Narok, Mhe. Samuel Oletunai. katikati ni Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Dkt. Ally Said Matano. 


Ratiba ya RC Hapi katika tarafa mbalimbali wilaya ya Iringa mjini

WAZIRI LUKUVI KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI YA MIKOA NANE KWA WIKI MBILI

0
0

 Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anataraji kufanya ziara ya kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mikoa nane ya Tanzania bara katika wiki mbili kuanzia tarehe 17 hadi 30 Septemba 2018.

Ziara hii ni katika utekelezaji wa kampeni yake ya “Funguka kwa Waziri wa Ardhi” ambayo aliizindua rasmi mwezi Januari mwaka 2018 yenye lengo la kuzunguka nchi nzima kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi papo hapo.

Katika wiki mbili hizi za kutatua migogoro ya ardhi katika mikoa nane waziri Lukuvi ameeleza kuwa kuanzia tarehe 17 hadi 19 atakuwa katika mkoa wa Mara katika wilaya ya Bunda, Musoma na Tarime na baadae tarehe 20 hadi 30 atakuwa katika mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Njombe, Iringa na Morogoro.

“Nipo njiani kuelekea mkoa wa Mara ambapo siku ya jumatatu tarehe 17 Septemba ntaanzia wilayani Bunda ili kutatua mgogoro wa Bibi Nyasasi Masike na kukagua kiwanja chake kama nilivyomuahidi Mheshimiwa Rais wakati alipofanya ziara yake wilayani Bunda na kunipigia simu moja kwa moja” Amesema Waziri Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akicheza na Wakazi wa kijiji cha Lolkisale Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipotembelea na kutatua mgogoro mkubwa wa wakazi wa maeneo hayo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisoma mabango ya Wakazi wa kijiji cha Nafco Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipotembelea na kutatua migogoro mikubwa ya wakazi wa maeneo hayo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akivishwa mavazi ya heshima ya kimasai na Wakazi wa kijiji cha Eng’arooji Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipofika kuwatatulia mgogoro wa ardhi uliokuwa umewagawa wananchi hao katika makundi mawili ambapo Waziri Lukuvi aliweza kutatua mgogoro huo.


CEO MHANDISI LUHEMEJA NA SIKU 100 NDANI YA DAWASA MPYA

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa utambulisho wake kwa Menejimenti mpya iliyozinduliwa Septemba 09 Mwaka huu.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
HII KAZI ITAFANYIKA: Hiyo ni kauli ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa utambulisho wake baada ya kuteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo.

DAWASA mpya, iliundwa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutoa kauli na kutaka DAWASCO na DAWASA ziwe kitu kimoja, agizo ambalo Wizara ya Maji na Umwagiliaji kama wasimamizi wa mamlaka hiyo kuunda DAWASA mpya itakayokuwa na bodi ya wakurugenzi moja.

Uteuzi wa kwanza wa Rais Dkt Magufuli ni wa Mwenyekiti wa Bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na baadae kuteuliwa kwa bodi ya wakurugenzi iliyoundwa na wataalamu mbalimbali wa maji.

“Nimshukuru sana Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa uteuzi wake, ameniamini sana kwa kunipa majukumu haya makubwa kuongoza mkoa wa Dar es Saalaam na Pwani,” alianza kwa kusema.

Alisema, Mabadiliko haya ni mabadiliko ya kihistoria, kwa kuona hatua nyingine inapigwa kwa kutatua tatizo la umaskini, malazi na ujinga. Stadi mbalimbali zinaonesha huduma za maji zikiboreshwa kwa asilimia moja uchumi wa nchi huongezeka kwa asilimia nne na huduma zikizorota kwa asilimia moja uchumi hupungua kwa asilimia nne.

Ni kwelil; Kuna changamoto zinazowakabili DAWASA katika suala la upatikanaji wa maji pembezoni mwa mji, Kwa Mkoa wa Dar es Salaam ifikapo mwaka 2030 utakuwa ni moja ya majiji makubwa barani Afrika na ongezeko la watu litakuwa ni Milioni 11 na makadirio ya maji kwa siku yatakuwa ni n Lita Milioni Moja na Laki Moja (110,000).

Mhandisi Luhemeja ameweka mikakati mbalimbali ya DAWASA  baada ya kukabidhiwa dhamana ya kuiongoza Mamlaka hiyo na hatua ya kwanza ni kuhakikisha miradi iliyokuwa inasuasua inamalizika kwa wakati tena ndani ya siku 100.

Siku 100 za Mhandisi  Luhemeja ndani ya DAWASA, mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ameweza kumuahidi ndani ya siku 100 miradi ya maji iliyokuwa inasuasua na mingine kutokumalizika kwa wakati imepata dawa nayo ni uongozi mpya wa DAWASA.

Mhandisi Luhemeja ameweka wazi , Mradi wa Chalinze tayari wakandarasi wa mradi huo wameshaitwa kujieleza kwenye bodi ,waeleze kwanini mradi huo umekuwa unasuasua kwa kipindi chote na kama tayari wameshatekeleza yale waliyoaizwa na Profesa Mbarawa.

Mradi wa pili ni wa usambazaji maji katika maeneo ya Goba, Salasala, Bunju, Bagamoyo na Kiluvya na mardi huu unatakiwa kukamilika mwisho wa mwezi Oktoba, huku mradi mwingine ukiwa ni Ruvu Juu na Rais Dkt Magufuli aliahidi mradi huo utapeleka maji maeneo ya Kisarawe na tayari serikali imeshalipia malipo ya awali na wapo katika mikakati ya kukamilisha Milioni  700 ili usambazaji huo uanze mara moja.

Mita za malipo ya awali (Prepaid Meter) zilizozinduliwa na Waziri Mbarawa, Mhandisi Luhemeja amesema Kuna changamoto kubwa sana ya madeni  na ndani ya siku 100 za DAWASA mpya atahakikisha mita hizo ambazo tayari zimeshaanza kufungwa kufanyika kwa zoezi hilo kwa taasisi zote kubwa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam. Mita hizi zitaweza kusaidia wizi wa maji unaofanyika na kusababisha hasara kubwa kwa Mamlaka.

Wakati wa uzinduzi wa mita hizi, Profesa Mbarawa aliweka wazi mkakati wa kukomesha wadaiwa sugu ambapo mtumiaji wa maji atatakiwa kulipia maji kabla ya matumizi na hela yake ikimalizika maji nayo yatakatika na pia itasaidia katika kupunguza madeni kwani pindi anapokuja kununua maji atalazimika kulipa kiasi Fulani cha deni.

Mita hizo tayari zimeshafungwa kwenye baadhu ya maeneo ikiwemo viwanda na wateja wa kubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam na Profesa Mbarawa aliagiza hilo zoezi liende kwa kasi sana, na baada ya uteuzi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA mpya ameahidi ndani ya siku 100 wateja wote wakubwa watakuwa wameshafumgiwa mita hizo za malipo ya kabla.

Muelekeo wa DAWASA mpya,Mhandisi Luhemeja amesema kwa sasa wana mikakati ya kupeleka maji Dar es Salaam ya Kusini na ameshakabidhi maradi wa maji wa Kiwalani  utaaokuwa na dizaini ya kusambaza maji katika maeneo ya Kitunda, Yombo, Mwanagati, Gongo la Mboto.

Kumekuwepo na malalamiko kuhusu mardi wa Kimbiji na Mpera, utakaozalisha maji Lita Milioni 260 kwa siku ulio chini ya Kampuni ya Serengeti ksuhindwa kukamilika kwa wakati Visima vya maji vikiwa tayari vimeshachimbwa kwa asilimia kubwa,  Mhandisi Luhemeja ameahidi kupitia upya usanifu wa Matanki yatakayotumika kuweka maji yanayotoka kwenye visima hivyo  na matanki hayo ni ya Gongo la Mboto, Chanika, Luanda na Pugu. Luhemeja amesema kuna wahandisi 12 wenye leseni na mihuri na kwa pamoja  Kamati ya wahandisi kwa pamoja wataanza kujenga matanki hayo kwa uwezo wa ndani.

Kukamilika kwa matanki hayo kutasaidia  upatikanaji wa maji katika maeneo ya Chamazi, Kitunda, Pugu, Ukonga, Kinyerezi na Uwanja wa Ndege. Mradi wa Kimbiji Mpera umekamilika ila umekuwa hauendelezwi ila mpaka kufikia Desemba 9 mwaka huu utakuwa umefikia hatua za mwisho.

Desemba 9 2018 DAWASA mpya inaazimia kutangaza Uhuru wa Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam , Mhandisi Luhemeja amesema kuwa siku ya uhuru maji miradi mingi itakuwa imekamilika na itakabidhiwa kwa Katibu Mkuu Profes Mkumbo ikiwemo na kukabidhi ripoti ya  mradi wa Benki ya Dunia wa Km 1426 ambao unatarajiwa ifikapo Septemba 15 mkandarasi atakuwa eneo la ujenzi.
Maji Taka, Mhandisi Luhemeja amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya huduma za maji taka toka kwa Mamlaka kutoka na uwekezzaji wake kuwa mkubwa ila tayari wameshapana bajeti kwa kutumia uwezo wa ndani kuwa ifikapo Desemba 9  wawe wanamiliki malori 20 ya kutoa huduma za maji taka nkwa wananchi, ila ameainisha changamoto nyingine katika mradi huo ni wamiliki binafsi kujipangia bei na zimekuwa kubwa sana na kuja kwa malori hayo kutasaidia kutoa huduma kwa watanzania kupata huduma kwa bei nafuu.

Ukarabati wa mabwawa, Mhandisi Luhemeja ameweka wazi mkakati wa DAWASA mpya kukarabati mabwawa yote ya maji taka yaliyoharibika na kutengenezwa yaliyopo maeneo ya Mikocheni, Mabibo, Airwing na Buguruni kwa ajili ya kuanza kupokea makazi malori kutoka makazi ya watu.

Akielezea changamoto ya upotevu wa maji, Mhandisi Luhemeja amesema DAWASA mpya imeacha yale yote yaliyofanywa na DAWASCO, upotevu wa maji umebaki historia, na kwa sasa watahakikisha wanapunguza upotevu mkubwa wa maji  na wametenga asilimia 35 ya mapato ya ndani ya kila mwezi kwa ajili ya upanuzi wa mtandao wa usafirishaji maji.

“Mtandao mdogo wa maji umekuwa unaleta changamoto kubwa katika upotevu wa maji, maji ni mengi yanapokuja kwa wingi yanasababisha kupasuka kwa mabomba na yanapelekea kupotea kwa maji na mapato yatakayotengwa yatasaidia kulaza mabomba na kutatengwa akaunti maalumu kwa ajili ya kuingiza makusanyo hayo ,” amesema Mhandisi Luhemeja.

Tatizo lingine la upotevu wa maji unatokana na mita za maji, kuna  mita elfu sitini na nane (68,000) kwa ajili ya kuwafungia wananchi  na ili kuhakikisha upotevu wa maji unaondoka, Pia Mhandisi Luhemeja amewaonya wezi wote wa maji kuwa tayari DAWASA mpya imeshasharikiana na kitengo cha Polisi  na kuwataka wananchi kushirikiana na Polisi kuwabaini wezi wa maji ili wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Ongezeko la Mapato ndani ya DAWASA mpya, Mikakati iliyopo ni pamoja na kuhakikisha mapato ya ndani yanaongezeka kutoka Bilioni 9.3 mwezi Agosti na kufikia Bilioni 12 na hili litafanikiwa kwa kudhiditi upotevu wa maji kwa asilimia 35 kufikia Desemba ikiwa ni ndani ya siku 100.

Hali ya watumishi ndani ya DAWASA mpya, Mhandisi Luhemeja ameweka wazi kuwa kunzia mwezi ujao mishahara ya wafanyakazi itakuwa na maslahi mazuri yatakayomuwezesha mtumishi maslahi mazuri

Mhandisi Luhemeja ameweka wazi kuwa DAWASA mpya  kushindwa sio sehemu yao bali watashirikiana kwa pamoja kuijenga ili ilete manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Malengo hayo ni mikakati madhubuti waliyojiwekea ya kuwa na DAWASA mpya yenye tija na itakayoiinua Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

DAWASA mpya rasmi imeanza kazi yake Septemba 9, baada ya kutambuklishwa kwa menejimenti mpya iliyo chini ya Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa sambamba na Mwenyekiti wa bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na amewahidi watanzania wote kuwa hususani wa Mkoa wa Dar es Saalaam na Pwani maji yatawafikia sehemu zote chini ya uongozi wake.

Hitimisho, kuundwa kwa DAWASA mpya kunakuja kujena taswira ya mapinduzi ya sekta ya maji iliyokuwa inasuasua kwa kipindi kirefu katik jiji la Dar es Salaam, ili nchi iweze kuinuka kiuchumi haina budi kuwa na maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu na hata katika viwanda mbalimbali vikiwemo vya Vinywaji ambao takribani lita laki moja (100,000) zinatumika kwa siku kwenye kiwanda kimoja, ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali nayo imekuwa inatumia maji kwa wingi ili kufanikisha shughuli zao za ujenzi wa maendeleo ya nchi.Napenda kuipongeza Serikali kwa kuunganisha DAWASCO na DAWASA kwa manufaa ya nchi

Kituo cha Afya PCMC kimetoa msaada katika Kituo cha Afya Vijibweni

0
0
 Kiongozi Mkuu wa Kituo cha Afya cha PCMC Richard Ulanga akizungumza na waandishi habari mara baada ya Kituo hicho kutoa msaada katika Kituo cha Afya Vijibweni,Kigamboni Jijini Dar es Salaam
 Kiongozi Mkuu wa Kituo cha Afya cha PCMC Richard Ulanga akikabidhi msaada katika mgonjwa aliyelazwa katika Kituo cha Afya Vijibweni.
Picha ya watumishi wakiwa wameshika vitu vya msaada kwa ajili ya wagonjwa waliopo katika Kituo cha Afya Vijibweni.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
KITUO cha Afya cha PCMC kimetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika kituo cha Afya Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Viongozi Mkuu wa Kituo hicho Richard Ulanga amesema msaada huo ulilengwa kwa wagonjwa katika kutuo cha Vijibweni ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitano ya kituo cha Afya cha PCMC.
Amesema kama watoaji wa huduma za afya wameona na umuhimu wa kutoa msaada katika kituo cha afya cha Serikali.
Ulanga amesema hawataishia hapo bali wataendelea kutoa msaada kila wanapoadhimisha miaka mingine
Aidha amesema katika kusherekea huko kila mtumishi amejitoa kwa nafasi yake kwa kutambua anawajibu ya kusaidia jamii inayomzunguka.

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAKABIDHIWA KUKU MKURANGA

0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

MWENYEKITI  wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga mkoani Pwani Mariam Ulega amekabidhi msaada wa kuku 4000 ambao watatolewa kwa wanawake wajasiriamali 400 ambao wamehudhuria mafunzo ya ujasiriamali.

 Akizungumza wakati akikabidhi kuku hao kwa wajasirimali ,amesema kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla na amewataka wawe na ushirikiano ili wafiikie malengo yao.

Kwa upande wa baadhi ya akina mama hao wameshukuru kwa  kupewa msaada huo na kuahidi kuwatunza kuku hao na kueleza kuwa kuku hao watakuwa chanzo cha miradi mikubwa zaidi
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na wanajasiriamali kuhusu kuwatunza kuku waliopewa ili kujiongezea kipato.
 Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga,Mariam  Ulega  akiwakangua kuku kabla ya kuwakabidh wananchi walilaya hiyo kwajili ya kufunga iliwaweze kujikwamua kiuchumi.
 Mwenyekiti wa jukwaa la la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam  Ulega akiwakabidhi wananchi kuku 3000 kwajili ya kufunga iliwaweze kujikwamua kiuchumi nakuongeza pato la Taifa. ambapo kila mwananchi alipewa kuku10 (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

NHIF Arusha yatembea minadani kusaka wanachama

0
0
Na Seif Mangwangi, Arusha

MFUKO wa bima ya afya (NHIF), mkoa wa Arusha umewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kusajili watoto wao kwenye mpango wa bima ya afya ya Toto kadi ili kuwaondolea usumbufu wa kupata matibabu na kuwapunguzia gharama.

Akizungumza katika mji wa Loliondo Ngorongoro Mkoani Arusha, jana katika zoezi la Uhamasishaji Wananchi na Jamii kwa ujumla juu ya Usajili wa Watoto kupitia Toto Afya Kadi na Usajili wa Wajasiliamali wadogo kupitia mpango wa KIKOA, afisa masoko wa mfuko huo Miradji Kisile alisema toto kadi ni mkombozi mkubwa kwa watanzania maskini.

Alisema gharama za Toto kadi ni ndogo kiasi ambacho kila mtanzania mwenye nia ataweza kuimudu na kumwezesha mtoto mdogo kupata huduma ya afya popote nchini.

Kisile alisema watendaji wa NHIF mkoa wa Arusha umeendelea kuhamasisha wakazi w mji huo kujiunga na mfuko huo na sasa wameanzisha zoezi la kuhamasisha wakazi wa Loliondo wilayani Ngorongoro kupitia Minada na Magulio yaliyopo Loliondo.

" Katika zoezi hili la hamasa tumeshapita kwenye minada ya Digodigo, Malambo, Piyaya na Wasso ambapo wananchi wamehamasika vizuri na kuahidi kujiunga," Alisema.

Kisile alisema katika zoezi hilo lililofanyika kwa siku nne kuanzia septemba 10 hadi 14 wananchi wamepata fursa ya Kuelimishwa Juu ya huduma za NHIF na jinsi ya kujisajili na mfuko wa Watoto na Wajasiliamali Wadogo Wadogo

Alisema zoezi hilo la kuhamisha litaendelea katika wilaya zingine za mkoa wa Arusha na kuhakikisha watu wengi wanajiunga na mfuko huo kwa lengo la kupata huduma bora za afya.
Afisa Masoko wa mfuko wa bima ya Afya NHIF mkoa wa Arusha Miradji Kisile akiwa katika mnada wa digodigo wilayani Ngorongoro akihamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujiunga na huduma za bima ya afya kupitia mpango wa Kikoa na toto afya kadi

Halmashauri Jiji la Arusha Kuanzisha Mahakama ya Jiji

0
0
Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji

Halmashauri ya Jiji la Arusha imetenga kiasi cha Shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuanzisha mahakama ya Jiji ifikapo Tarehe 20 mwezi Novemba mwaka huu.

Ujenzi wa mahakama hiyo ni kwa lengo la kushughulikia kesi mbalimbali za wafanyabiashara wataokaidi kulipa kodi ya Serikali au ushuru wa vibanda vya biashara zao kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza mwishoni mwa wiki  Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Madeni amesema kuwa kuanzishwa kwa mahakama hiyo kutasaidia kuongeza mapato katika Halmashauri kwa kuwa jiji tayari zipo sheria ndogo zitakazotusaidia kupitisha hukumu kwa watakaopatikana na hatia ya ukoseshaji wa mapato ya Halmashauri.

“Katika Mahakama itakayoanzishwa tutaweza kutoa hukumu kwa masaa machache ikiwa ni faini ama kifungo kwa wataopatikana na hatia ya kuinyima mapato halmashauri, itasaidia mapato ya jiji kuongezeka na itamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi zake kwa watanzania ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya na elimu kwa kupitia mapato yatakayopatika” alisema Dkt. Madeni.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalist Lazaro ameunga mkono juhudi za serikali ya awamu hii katika ukusanyaji wa mapato na ameahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Mkurugenzi katika operesheni yake ya ukusanyaji wa mapato.

“Kamwe asijitokeze wananchi yoyote kukwepa kulipa kodi ama ushuru kwa mwamvuli wa chama fulani cha siasa , katika suala la mapato tuondoe itikadi zetu za vyama ili Halmashauri iende mbele” alisema Mhe. Kalist.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato bado inaendelea ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa shilingi Bilioni 30 kwa mwaka badala ya bilioni 15 tunazokusanya sasa.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 17, 2018

JAFFO APONGEZA UJENZI WA BARABARA YA OLJORO - MURRIET JIJI LA ARUSHA.

0
0
Na Fatuma S. Ibrahimu – Arusha Jiji 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) amepongeza ujenzi wa barabara ya oljoro murriet inayojengwa kupitia mradi wa TSCP awamu ya tatu wenye gharama ya Shilingi Bilioni 22. 3 inayojengwa na mkandasi kutoka kampuni ya Sinohydro Co-Operation Ltd ya nchini China.

Mhe. Jaffo ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Jijini Arusha mapema leo hii alipotembela mradi huo wa ujenzi wa barabara unaosimamiwa na mhandisi wa barabara wa Jiji Eng. Agust Mbuya na kujionea hatua nzuri iliyofikia ujenzi huo ambapo kwa sasa upo kwenye hatua za awali na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 11 mwaka 2019 na kuanza kutumiwa na wananchi.

“Nichukue fursa hii kukupongeza mhandisi kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huu, pia nitoe rai kwa mshauri elekezi wa ujenzi wa mradi huu kufanya kazi kwa niaba ya halmashauri , kushauri kwa weledi na kuwa mtetezi mkuu kwa upande wa Serikali kwani atakapokuwa upande wa mkandarasi basi Halmashauri itashindwa kufikia malengo kwani itakosa mshauri mwenye kusimamia haki ” Alisema Mhe. Jaffo.

Sambamba na ziara yake hiyo kwenye mradi wa ujenzi wa barabara Mhe. Jaffo pia alitembelea kituo cha afya cha Kaloleni kilichopo Jijini hapa ili kujionea matumizi ya kiasi cha Fedha shilingi milioni 400 zilizotolewa na Serikali tagu tarehe 26 June, 2018 kwa ajili ya kukarabati majengo katika Kituo hicho pamoja na ujenzi wa wadi mbalimbali.

"Nimepokea barua nyingi kutoka hapa kutaka mbadilishe matumizi ya ujenzi wa majengo ya hospitali pamoja huduma za meno ,sitaki mbadilishe chochote hapa na jumatano kazi ianze na nitakuja kukagua mwenyewe ukamlishwaji wa jengo hili novemba 30 mwaka huu " alisema Mhe. Jafo.

Pia Waziri Jafo alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Fabian Daqqaro kufuatilia na kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unaanza Jumatano wiki ijayo. 

Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dk. Simon Chacha alimhakikishia Waziri Jaffo kuwa wataanza ujenzi wa majengo ya upasuaji na wodi ya wazazi, jengo la X Ray, sehemu ya Kusubiria wagonjwa (waiting bay),Jengo la kufulia na ukarabati wa chumba cha meno, dawa, Maabara na mfumo wa maji taka katika kituo hicho cha Kaloleni ili kuboresha huduma za afya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) (Kulia) akitoa maelekezo wakati wa ziara yake aliyoifanya jana Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jafo(MB) ( kushoto) akiwa katika moja ya chumba cha kutolea huduma za afya katika Kituo cha Afya Kaloleni

Vijana 3440 wanufaika na programu ya kukuza Ujuzi nchini.

MDAHALO WA WAZI WAKUPINGA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.

0
0
Khadija Khamis –Maelezo 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe, Riziki Pembe Juma aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano na Serikali kuhakikisha vitendo vya uzalilishaji vinaondoka nchini .

Hayo alisema leo huko katika kiwanja cha kufurahishia watoto kariakoo wakati wa mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya wananchi dhidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wanawake na watoto ulioandaliwa na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto..

Alisema serikali imetunga sheria kwa wale wote wanaofanya vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto lakini kila siku vitendo vinaendelea hivyo iko haja ya mashirikiano ya pamoja kati ya walezi wazazi na serikali ili kuvidhibiti vitendo hivyo .

Aidha alisema tupange mikakati madhubuti kwa pamoja jinsi ya kuondoa wimbi sugu la udhalilishaji wanawake na watoto na hata watu wazima na kuhakikisha kila mmoja anahusika katika mapambano ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia ..

Nae mshiriki wa mdahalo huu Shadida Machano alisema wazazi wawe karibu na watoto wao na kuwalea malezi ya kirafiki ambayo yanazingatia maadili ili kumjengea mtoto uwezo wa kusema kwa kila ambalo linamtokezea .Alisema skuli ziandaliwe masomo maalumu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa skuli za msingi na sekondari ili kuweza kujielewa na kujihami.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akizungumza na Washiriki katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni ya Wananchi zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar uliofanyika Viwanja vya Kariakoo kwa kuwataka Wazazi kuzidi kutoa mashirikiano juu ya vitendo vya udhalilishaji vinavyotokea ( kulia) Naibu waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na WatotoShadia Mohamed na Mshauri wa Rais wa Zanzibar masuala ya Wanawake Zainab Omar.
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Mhe,Maudline Castico Akielezea juu ya wazazi kuwalea watoto katika maadili mazuri wa Kwanza( kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto Fatma Gharib.Bilali na Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar Jaji Mshibe 
Mmoja wa wachangiaji katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar Shadida Machano akichangia kwa kusema kuna vyuo mbali mbali vya madrasa vilivojitokeza bila ya kusajiliwa.
Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi mbali mbali waliohudhuria katika mdahalo wa wazi wa kupokea maoni zidi ya mapambano ya ukatili na udhalilishaji wa Wanawake na watoto Zanzibar wakifuatilia kwa umakini mdahalo huo uliofanyika Viwanja vya Kariakoo Mjini Unguja.
Picha na Maryama Kidiko – Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

WAKANDARASI MIRADI YA UMEME WATAKIWA KUANZISHA YADI MAALUM

0
0

Na Veronica Simba – Chato

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka wakandarasi wote nchini wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini, kuwa na Yadi maalum za kuhifadhi vifaa katika maeneo wanakotekeleza miradi hiyo, ili kuondoa kisingizio cha kutowaunganishia wananchi umeme kutokana na kutokuwepo na vifaa.

Aliyasema hayo, jana Septemba 16, 2018 katika Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, akiwa katika ziara ya kazi, ambapo pia aliwasha umeme rasmi kijijini hapo. “Kuanzia sasa nawaelekeza muwe na Yadi zenu ambapo mtahifadhi vifaa vyote vya kazi na sisi Serikali tutazikagua. Maneneja wa TANESCO kagueni Yadi hizo.”

Waziri alitaja vifaa vya kazi vinavyotakiwa kuwepo katika Yadi hizo kuwa ni pamoja na nyaya za umeme, nguzo, transfoma pamoja na mita za Luku. Aidha, akiwa katika Kijiji cha Magiri wilayani humo, ambako pia aliwasha umeme rasmi, Waziri Kalemani aliwaasa wananchi kuepukana na vishoka wakati wanapotaka kutandaziwa mfumo wa nyaya za umeme katika makazi yao.

Aliwataka wananchi kujiridhisha na uhalali wa mafundi watakaowatumia kuwatandazia mfumo wa nyaya, katika Ofisi za TANESCO zilizopo katika maeneo yao. Akifafanua, alisema majina ya mafundi wenye sifa yatatundikwa katika Ofisi hizo ili kuwarahisishia wananchi kuwatambua hivyo kuepukana na vishoka. 

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Magiri wilayani Chato, Mkoa wa Geita akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, Septemba 16, 2018.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwasha umeme katika moja ya nyumba za wakazi wa Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, Mkoa wa Geita, kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme kijijini humo. Tukio hilo lilifanyika Septemba 16, 2018, wakati Waziri akiwa katika ziara ya kazi.
Wananchi wa Kijiji cha Kahumo wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wakimpokea kwa bashasha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu-kulia), alipowasili kijijini hapo jana, Septemba 16, 2018, kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo.

Waziri wa Nishati, Dkt, Medard Kalemani (kulia), akiwaonesha wananchi wa Kijiji cha Kasenga wilayani Chato, kifaa cha Umeme Tayari, kinachotumika kuunganisha umeme pasipo kutandaza mfumo wa nyaya (wiring). Waziri alikuwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi, jana Septemba 16, 2018. Pamoja naye pichani (kutoka kushoto) ni Meneja wa TANESCO Wilaya ya Chato, Nyabingiri Nyaonge na Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini katika eneo hilo, Ibrahim Saidi.

Viewing all 109588 articles
Browse latest View live




Latest Images