Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: KALALA JUNIOR NA MUZIKI WA DANSI


SHUGHULI MBALIMBALI ZA WIKI YA TRC BADO ZINAENDELEA

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI ATEMBELEWA NA MKURUGENZI MKUU TAKUKURU

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye atembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman jana katika Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam. Lengo ni kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili.
Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, alitumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) na kumuahidi ushirikiano katika kulijenga Taifa. 
Vilevile Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman amepata fursa ya kujifunza jinsi gani Jeshi hilo linavyoendesha shughuli zake pamoja na kufanya mazungumzo ya kina na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
 “Nimejifunza mengi lakini pia nashukuru kwa kupata fursa ya kutembelea na kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana” alisema Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimtambulisha Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, Billy Mwakatage (kulia), kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman (kushoto), baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam jana tarehe 14/09/2018.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) akimkabidhi zawadi ya Kalamu yenye namba ya dharura 114, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman (kushoto), alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam jana tarehe 14/09/2018. Wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Diwani Athuman, akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyopo jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi barabara ya ohio jijini Dar es Salaam jana tarehe 14/09/2018. Wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kukuza mahusiano kati ya vyombo hivyo viwili. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

SERIKALI INATAMBUA NA KUHESHIMU MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA-WAZIRI UMMY MWALIMU

$
0
0
SERIKALI inatambua na kuthamini juhudi za wadau mbali mbali zinazofanywa zenye lengo la kuhakikisha maendeleo ya Watanzania yanawezeshwa kikamilifu, hasa zinazochochewa na asasi za kiraia. 

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Watoto wa wizara hiyo, Margaret Mussai alipokuwa akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii ulioandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation.

Akizungumza katika mkutano huo ulioshirikisha asasi mbalimbali za kiraia, alisema Serikali inafarijika kuona wadau wakiungana na kupanga mikakati ya kufikia malengo ya mafanikio ya utendaji kwa pamoja kuihudumia jamii.

“...Asasi za kiraia mmekuwa muhimili muhimu kwenye kuhimiza maendeleo ya jamii, mmekuwa mnabuni miradi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha vijana na wanawake kiuchumi na kutoa huduma za maendeleo ya Jamii kwa kutumia gharama nafuu na hata muda mwingine kwa kutumia rasilimali za wanaojitolea,”

“...Tunatambua mchango wa asasi nyingi za kiraia zinazotoa elimu juu ya mapambano ya magonjwa yanayoambukizwa, mila na desturi zenye madhara kwa vijana wakiwemo watoto wa kike na wanawake. Lakini pia kuna asasi zinazowezesha vijana kuwekeza kiuchumi katika miradi midogomidogo ya uzalishaji mali,” alisema Ummy katika hotuba hiyo.

Aidha alisema licha ya Serikali kutambua mchango mkubwa wa asasi za kijamii, alizitaka kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na ushirikishwaji wa rika zote, huku zikizingatia sheria na katiba ya nchi ili kufikia malengo yao.
Mkurugenzi wa Watoto toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii kwaniaba ya waziri wa wizara hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na taasisi ya NAMA Foundation kwa kushirikiana na asasi ya An Nahl Trust.
Mwenyekiti wa Asasi ya An Nahl Trust, Mhandisi Alliy Kilima akizungumza kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na asasi yake kwa kushirikiana na NAMA Foundation leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Uwezeshaji wa Asasi za Kijamii nchini Tanzania ulioandaliwa na NAMA Foundation kwa ushirikiano na Asasi ya An Nahl Trust wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC Chongolo aomba taarifa uharibifu wa Mto Tegeta

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Daniel Chongolo ameuagiza  uongozi wa bonde la Mto Wami/Ruvu kupeleka taarifa ya uchafuzi wa mto Tegeta lililoathiriwa na shughuli za Binadamu.
Chongolo aliyasema hayo wakati alipofanya ziara katika bonde la Mto Tegeta eneo la Salasala, amesema uharibifu ni mkubwa kwa shughuli za kibinadamu ambapo ni hatari kwa wananchi wa liopo kandokando ya Mto huo.
Amesema kuwa hakuna sababu ya kuacha uharibifu mazingira wakati vyombo vya kusimamia vipo.
Chongolo amesema wananchi lazima waheshimu sheria zilizowekwa katika bonde mabonde ya Mito.
"Hatuweza watu wakaendelea kuchimba mchanga huku wakiharibu mazingira na baadae serikali kuingia gharama ya kuhudumia wananchi waliohadhilika na mafuriko wakati shughuli za uchimbaji mchanga  walizifanya wenyewe"amesema Chongolo.
Nae Afisa wa Maji wa Bonde la Mto wa Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa watu kama wanachimba mchanga lazima wafuate utaratibu.
Amesema kuwa hakuna sababu ya kuacha uchimbaji wa mchanga wa holela na kama hawataki kufuata sheria waache kuchimba mchanga katika mabonde ya Mito.
Amesema kuwa kuna operesheni wataifanya hakuna mtu atabaki salama kwa wachimbaji wa mchanga.
Aidha amesema kuwa wachimbaji  wa mchanga lazima waheshimu sheria.

MAANDALIZI UCHAGUZI MDOGO MONDULI YAKAMILIKA WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIGA KURA

$
0
0

  Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Monduli, Stephen Ulaya amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kupiga Kura kesho (Jumapili, Septemba 16,2018) ili kumchagua Mbunge wa Jimbo hilo.

Akizungumza na NEC TV wilayani Monduli leo Bw. Stephen Ulaya ameeleza kuwa maandalizi ya kufanikisha kufanyika kwa uchaguzi huo yamekamilika ikiwemo usambazaji wa vifaa vya uchaguzi na Mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi

UCHAGUZI MONDULI, POLISI ARUSHA YAWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa limesema litaendelea kuimarisha ulinzi katika uchaguzi mdogo wa marudio wa kugombea kiti cha ubunge unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili wilayani Monduli kama jinsi ilivyokuwa kwenye kampeni.

Akitoa taarifa hiyo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi, alisema wananchi wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi katika vituo vya kupigia kura kwani Jeshi hilo limezidi kuimarisha ulinzi ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu.

“Kama ilivyo kwenye kampeni hali ilikuwa tulivu na wakati wa uchaguzi tutahakikisha kwamba hali hii inaendelea kuwa shwari, askari toka vikosi mbalimbali watakuwepo wilayani hapo kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya usalama.” Alilisitiza Kamanda Ng’anzi.

Aidha aliwataka wananchi wa jimbo la Monduli mara baada ya kutimiza haki yao msingi ya kupiga kura wasikae kwenye vituo kwani hali hiyo inaweza kusababisha vurugu.

Kamanda Ng’anzi aliwaonya baadhi ya watu wanaopanga kufanya fujo wakati wa uchaguzi au mara baada ya uchaguzi kumalizika watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kusisitiza kuwa yeye mwenyewe atakuwepo wilayani humo kwa ajili ya kujionea na kusimamia kwa karibu shughuli za Usalama katika kipindi chote cha kupiga kura hadi kutangaza matokeo.

“Ole wao watakaopanga kufanya vurugu, Jeshi la Polisi lipo imara na halitashindwa kumkamata yeyote atakayeshawishi au kufanya fujo katika uchaguzi huo ambao tunategemea utakuwa wa amani na utulivu”. Alimalizia kwa kuonya Kamanda Ng’anzi.

MAGARI YAANZA KUPITA BARABARA YA JUU (FLYOVER) ENEO LA TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 
Magari yakipita kwa ajili majaribio leo (Jumamosi Septemba 15, 2018) katika barabara za juu (flyover) ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la Tazara Jijini Dar es Saalam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

WAJUMBE, WADAU MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WAPATIWA SEMINA YA MABADILIKO YA SERA BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali, Ndg. Ismail Suleiman akizungumza na Wajumbe waliofika katika semina ya Mabadiliko ya Sera ya Mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Msajili wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali, Ndg. Marcel Katemba (wa pili kulia) akizungumza na Wajumbe (hawapo kwenye picha) waliofika katika semina ya Mabadiliko ya Sera ya Mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali, Ndg. Ismail Suleiman, kushoto ni Mwenyekiti anaeendesha semina hiyo Ndg. Justa Mwatoka Kiwohede na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali, Ndg. Nicholaus Zacharia
 Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Wakili Harold Sungusia akitoa maada katika semina ya Mabadiliko ya Sera ya Mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Katika semina hiyo iliwahusisha wadau na wajumbe mbali mbali kutoka Mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania
Mratibu wa Novelty Youth Centre Tanga ambae pia ni Mjumbe, Ndg. Jasson Eliakimu akizungumza jambo wakati wa semina ya Mabadiliko ya Sera ya Mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

  Baadhi ya wajumbe wakifuatilia semina ya Mabadiliko ya Sera ya Mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. 

TUMEJIDHATITI KUPUNGUZA FOLENI ENEO LA TAZARA- MHANDISI MFUGALE

$
0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO
Serikali Kupitia Wakala wa Barabara TANROADS  leo imesimamia zoezi la kuanza majaribio ya kutumia  Barabara za juu flyover zilizoko katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere,  ambazo ujenzi wake umemalizika hivi karibuni.

Zoezi  hilo ambalo lilianza saa 3:00 asubuhi limepokelewa vyema na waendesha magari na wananchi kwa ujumla na majira ya saa sita mchana eneo la TAZARA limeonekana tupu huku watazamaji wakishangaa na nyuso zao kuonekana za furaha kwa kazi nzuri ya Serikali yao.

Kuanza kutumika kwa barabara za juu eneo hilo la TAZARA kunafuta mlundikano wa magari ya mizigo toka bandarini kwenda mikoani na abiria wa ndege waingiao na kutoka Uwanja wa kimataifa Dar es Salaam  kutumia muda mwingi kwenye barabara za Nyerere na Mandela hadi saa moja au zaidi badala ya dakika 20 za sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TANROAD Mhandisi Patrick Mfugale, ameeleza kuwa barabara hizo ziko tayari kwa matumizi kwa waendeshaji wa magari jijini Dar es Salaam, na kuwahakikishia kuondokana na foleni eneo hilo la TAZARA.

“tumeamua kupunguza foleni kutoka mjini kwenda  uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na kutoka Ubungo kwenda bandarini ambapo kwa sasa kunafikika kwa dakika chache tofauti na hapo zamani watu walikuwa wanatumia zaidi muda wa saa moja lakini sasa hivi ni dakika 20 tu”, Mhandisi Mfugale.

Mhandisi Mfugale alifafanua kuwa wakazi wa Dar es Salaam sasa wataondokana na tatizo la foleni kama hapo mwazo ampako kulikuwa na msongamano wa magari na watu lakini kwa sasa barabara hizo za juu flyover zitasaidia kupunguza  tatizo hilo.
Magari yakipita kwa ajili ya majaribio leo (Jumamosi septemba 15, 2018 barabra za juu flyover ya Mhandisi Patrick Mfugale lililopo eneo la TAZARA Jijini Dar es Salaam ambalo hivi karibuni linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli. Picha na Paschal Dotto –MAELEZO

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA URITHI FESTIVAL

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii kwa uchumi wa nchi yetu, na kwamba ili kuweza kupata watalii wengi zaidi lazima kuwa na usafiri wa anga ulio na uhakika; ndiyo maana Serikali imeamua kufufua shirika letu la ndege (ATCL) na tayari Serikali imenunua ndege mpya saba.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Tamasha la Mwezi  wa Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania linalojulikana kama Urithi Festival liliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, Jijini Dodoma.

“Ni wazi pia kwamba utalii unahitaji usafiri bora na wa uhakika wa nchi kavu, hususan reli na barabara.  Kwa kujua hili, Serikali imeamua kujenga reli mpya ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, katika awamu hii ya kwanza. Vilevile, Serikali inakarabati reli yetu ya zamani kutoka Tanga hadi Arusha. Ukarabati wa reli hii utawezesha pia kuanzisha utalii wa reli (railway tourism) utakaohusisha vivutio mbalimbali, hususan Milima ya Usambara (Lushoto), Hifadhi ya Taifa Mkomazi, na Mlima Kilimanjaro. Kwa upande wa barabara, barabara nyingi kuu na za mijini zinajengwa kwa kiwango cha lami.” Alisema Makamu wa Rais

Makamu wa Rais amebainisha kuwa Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na rasilimali nyingi za asili ikiwemo milima, misitu, mito, maziwa, bahari, wanyama wa aina mbalimbali na urithi wa utamaduni wa aina mbalimbali.

Makamu wa Rais amesisitiza ni vyema kwa umoja wetu tuweke nguvu kufanya Urithi wa utamaduni wetu kuwa ni zao la uhakika kwenye sekta ya utalii na ukarimu. Vilevile, thamani ya utamaduni inaonekana kwenye sekta nyingine kama elimu, afya, michezo, kilimo, viwanda na maendeleo ya jamii.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi Tamasha la Urithi (Urithi Festival) katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.  
 Mtoto wa Shaaban Robert, Mzee Ikbali Robert akionyesha Tuzo ya Nguli wa Lugha ya Kiswahili katika Uandishi ya Urithi Festival ya mwaka 2018 aliyokabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ishara ya kutambua mchango mkubwa wa Baba yake Mzee Shaaban Robert. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo ya Nguli wa Sanaa za Ngoma ya Urithi Festival mwaka 2018 Mjukuu wa Mzee Morris Nyunyusa kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kutunza na kudumisha utamaduni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono na kikundi cha Eddie Collection wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Urithi (Urithi Festival) kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KUSOMA  ZAIDI BOFYA HAPA

Bodi Mpya ya Mfuko wa PSSSF Yazinduliwa

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  amezindua Bodi  mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kuiagiza Bodi hiyo kutekeleza miradi ya kimkakati ili lengo la kuanzishwa kwa mfuko huo litimie.
Akizungumza leo Jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi huo amesema kuwa wanachama wana matarajio makubwa na utendaji wa Bodi hiyo, hivyo jukumu lake ni kuhakikisha kuwa inafanya tathmini ya miradi yote iliyokuwa inatekelezwa na mifuko iliyounganishwa ili kuona namna bora ya kuiendeleza.
"Jukumu lenu kama Bodi ni kuhakikisha kuwa miradi kama ule wa Kiwanda cha kuzalisha viatu Karanga inaendelezwa kwa maslahi ya nchi yetu, sambamba na miradi yote ya kimkakati iliyopo ni vyema mkaharakisha mchakato wa kuifanya ianze mara moja kwa kuwa matarajio ya Serikali ni kuona mfuko huo unakuwa imara, endelevu na unatoa huduma bora ya Hifadhi ya Jamii"; Alisisitiza Mhe. Mhagama.
Akifafanua amesema kuwa sekta ya hifadhi ya Jamii imetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii kwa kuwekeza shilingi Trilioni 11.79 katika vitega uchumi ikiwemo miundombinu, daraja la Kigamboni, Ujenzi wa Hospitali, Vifaa tiba na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.
"Tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, ushirikiano, nidhamu, uadilifu na weledi wa hali ya juu, uongozi wenu ndiyo utakaowezesha PSSSF kukidhi matarajio ya wanachama"; Alisisitiza Mhagama.
Akizungumzia uwajibikaji kwa menejimenti na wajumbe wa Bodi, Waziri Mhagama amewaasa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za matumizi ya fedha na rasilimali za mfuko huo ili kuleta tija kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  akizungumza kuhusu umuhimu wa Bodi  mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kusimamia rasilimali fedha kwa kutekeleza miradi ya kimkakati katika mfuko huo wakati akizindua Bodi hiyo leo Jijini Dodoma.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Mhandisi Mussa Iyombe akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua Bodi  mpya ya Mfuko huo leo Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Eliud Sanga akitoa taarifa fupi ya utendaji kazi wa mfuko huo wakati wa hafla ya kuzindua Bodi mpya ya mfuko huo ambapo  tayari umeshafungua Ofisi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Ofisi moja Tanzania Visiwani ikiwa ni moja ya hatua za kuwahudumia wanachama wake katika mikoa yote hapa nchini.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi  mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi mpya ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo leo Jijini Dodoma. kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo Mhandisi Mussa Iyombe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Eliud Sanga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JAFO AAGIZA USAFI NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA.

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amewaagiza Viongozi wa Jiji la Arusha kudumisha usafi ili kulinda miundombinu ya barabara ambazo zimejengwa jijini humo kwa gharama kubwa. Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha kukagua miradi mbalimbali inayo tekelezwa chini ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Katika ziara hiyo,Waziri Jafo hakupendezwa hata kidogo na uchafu uliooneka kutapakaa ndani ya mifereji hiyo ambayo imejengwa hivi karibuni chini ya mradi wa uendelezaji Miji mkakati (TSCP).

 Kufuatia hali hiyo, Jafo ameugiza uongozi wa jiji hilo kuunda makundi ya wamama na wajane ambao wapo tayari kufanya usafi ili kila kikundi kikabidhiwe barabara yao kwa ajili ya kuitunza huku wakipata kipato ambacho kinaweza kikawasaidia kulea watoto na familia zao. 

 "Barabara za lami nzuri pamoja na mifereji iliyojengwa na zinazoendelea kujengwa zimeonekana kujaa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha miundombinu hiyo kuharibika haraka,"amesema Pamoja na ukaguzi wa miundombinu ya barabara inayojengwa Jijini Arusha Jafo alitembelea kituo cha afya Kaloleni kilichopokea shilingi milioni 400 kutoka serikali huu lakini alikuta ujenzi haujaanza. Kutaokana na hali hiyo Jafo ameuagiza uongozi wa Jiji la Arusha kuanza ujenzi huo kabla ya kumalizika kwa wiki ijayo na ametaka ujenzi huo uwe umekamilika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu ya barabara.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu ya barabara.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa Jiji la Arusha akikagua miundombinu mbalimbali.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa jiji la Arusha alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni kukagua ujenzi wa miundombinu.

NEC YAVITAKA VYAMA NA WAGOMBEA KUZINGATIA NA KUHESHIMU SHERIA SIKU YA KUPIGA KURA

$
0
0


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vya siasa, wagombea, wananchi na watendaji wa uchaguzi kuzingatia na kuheshimu matakwa na masharti ya Sheria za Uchaguzi, Sheria za Nchi na Maadili ya Uchaguzi wakati wa upigaji kura, kuhesabu, kujumlisha kura, na kutangaza matokeo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika kesho Jumapili kwenye majimbo ya Ukonga na Monduli na kata 9 za Tanzania Bara.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage katika risala yake kuelekea uchaguzi huo mdogo unaofanyika kufuatia sababu mbalimbali ikiwamo wabunge na madiwani kujizulu, kufariki, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama.

Jaji Kaijage aliwataka wadau hao wa uchaguzi kushirikiana na Tume kuhakikisha kuwa viashiria vya kuvunjika kwa amani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi utakaofanyika uwe huru, wazi na wa haki.
Mbali na wito huo, Mwenyekiti huyo aliwasihi wapiga kura wote waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na wanaoishi kwenye maeneo yanayofanya uchaguzi mdogo, kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi cha takribani miaka miwili ijayo. 

“Wananchi wafanye na kutekeleza zoezi la kuwachagua wawakilishi wao bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi kwani chini ya Kanuni ya 3.1 (b) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Serikali imepewa wajibu wa kuhakikisha kuwa kuna hali ya usalama, amani na utulivu katika kipindi chote cha Uchaguzi.”, aliongeza Jaji Kaijage na kusisitiza kuwa:

“Ni matumaini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa, hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya Uchaguzi ambayo imekuwepo hadi hivi sasa, itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu mdogo unafanyika na kumalizika salama kwa ustawi wa Taifa letu.”

UFARANSA YAAHIDI KUZIDISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA

$
0
0
Na Khadija Khamis – Maelezo 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter amesema nchi yake itaendelea kuongeza ushirikiana wake na Tanzania katika masula ya Uchumi, Kijamii na Utamaduni. Balozi Frederic Clavieter alieleza hayo katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar Migombani alipofanya ziara ya kutembelea ofisi hiyo akiambatana na Maseneta watatu kutoka Ufaransa.

Maseneta waaliofutana na Balozi Clavieter ni Ronan Dantec kutoka Jimbo la Loire-Atlantique, Cyril Pellevat wa Jimbo la Haute-Savoie na Seneta Bernard kutoka Jimbo la Paris .Alisema katika kuimarisha ushirikiano huo, Ufaransa imeamua kuongeza msaada wake kwa Tanzania kutoka Euro milioni 50 kwa mwaka kufikia Euro milioni 100 ili kuharakisha maendeleo yake.

Alisema mahusiano kati ya Ufaransa na Tanzania ulianza muda mrefu uliopita na wananchi wa mataifa hayo mawili wamekuwa na ushirikiaano mkubwa katika masula ya Utamaduni kwa kushiriki katika Matamasha mbali mbali yanayoandaliwa na nchi hizo. Alisema ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo hivi sasa yameleta maafa makubwa katika baadhi ya nchi hasa nchi changa.

Balozi Frederec amefurahishwa na kuona vijana wa Zanzibar wanajifunza lugha ya Kifaransa na ameshauri vituo zaidi vya kufundishia lugha hiyo viongezwe ili kuimarisha zaidi Utamaduni wa nchi hizi mbili. Aidha alisema kujitokeza vijana wengi kujifunza Kifaransa kutawasaidia vijana hao kupata ajira kwani zaidi ya Watalii 20 elfu kutoka Ufaransa wamekuwa wakitembelea Zanzibar kutokana na vivutio vingi vya Utalii viliopo.


Rais wa Jumuiya ya Utamaduni ya Ufaransa na Zanzibar Khamis Abdalla Said akiwakaribisha Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter na maseneta watatu kutoka Ufaransa na wageni waliohudhuria hafla maalumu iliyofanywa na viongozi hao katika kituo cha Jumiya hiyo Migombani Mjini Zanzibar. 
Balozi wa Ufansa nchini Tanzania Frederic Clavieter akizungumza wageni waalikwa waliohudhuria hafla maalumu katika Ofisi ya Jumuiya ya Ufaransa na Zanzibar iliopo Migombani Mjini Zanzibar 
Seneta Ronan Dantec kutoka jimbo la Loire-Atlantique akizungumza na wageni waliohudhuria hafla maalumu iliyoandaliwa na Jumuiya ya Ufarans na Zanzibar katia ofisi zao ziliopo Migombani Mjini Zanzibar 
wageni waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter wakati balozi huyo akifutana na maseneta RonaDantec, Cyril Pellevat na Bernard Jomier walipotembelea Ofisi ya Jumuiya Ufaransa na Zanzibar.

Wageni waliohudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavieter wakati balozi huyo akifutana na maseneta RonaDantec, Cyril Pellevat na Bernard Jomier walipotembelea Ofisi ya Jumuiya Ufaransa na Zanzibar. 


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>

DKT TIZEBA AWASILISHA TAARIFA YA ZAO LA KAHAWA KWA KATIBU MKUU CCM, USHIRIKA WAUNGWA MKONO KWA KAULI MOJA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Dodoma

Katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania masoko ya Kahawa yamekuwa yakiendeshwa kwa mfumo wa ushirika na soko huria, Mfumo wa soko huria uliruhusu makampuni na watu binafsi kununua mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima pasipo udhibiti hali iliyopelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo bei isiyokuwa na tija kwa mkulima, ubora hafifu wa mazao, ukwepaji wa kodi kwa wanunuzi na ukosefu wa takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo.


Kutokana na changamoto za mfumo wa soko huria, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli iliamua kurejesha ununuzi wa mazao matano ya kimkakati (Korosho, Tumbaku, Pamba, Kahawa, na Chai) kupitia vyama vya ushirika tangu mwaka 2016 ili kunufaisha wakulima, wanunuzi/wafanyabiashara na serikali.


Hayo yamebainishwa jana tarehe 14 Septemba 2018 na Mhandisi Mhe Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao makuu maarufu kama White House, Mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Makongoro Nyerere, Naibu waziri wa Kilimo, Mhe Omary Mgumba, wataalamu kutoka wizara ya kilimo akiwemo Naibu katibu mkuu Prof Sizya Tumbo, Mrajis wa vyama vya ushirika,vyama vya ushirika na wawakilishi wa wakulima kutoka maeneo yanayolima kahawa.


Katika taarifa hiyo Dkt Tizeba alieleza kuwa kamwe hawezi kuruhusu mtu mmoja mmoja au kundi la watu kuvunja ushirika ambao hivi karibuni umeanza kuimarika mahususi kwa ajili ya kumkomboa mkulima uamuzi ambao umebainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 katika sura ya pili ibara ya 22 ikisisitiza kuviimarisha na kuviwezesha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji wa thamani na biashara.


Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo akitoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini kwa Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Washiriki wa mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa wakifatilia kwa makini taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. 
Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi akizungumza mara baada ya Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo kutoa ufafanuzi kuhusu zao la kahawa wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma. 
Wataalamu kutoka wizara ya kilimo wakifatilia mkutano wa uwasilishaji wa mwenendo wa zao la kahawa taarifa iliyowasilishwa na Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo mbele ya Dkt Bashiru Ali Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi mkutano uliohudhuriwa na wabunge kutoka maeneo yote yanayozalisha kahawa, Jana Tarehe 14 Septemba 2018 katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi maarufu White House Mjini Dodoma.

POLEPOLE AHITIMISHA KAMPENI ZA UDIWANI VINGUNGUTI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 Kampeni za  udiwani kata ya Vingunguti Zimefungwa leo katika uwanja wa Msikate tamaa, ambapo pole pole alikuwa mgeni rasmi na kuwaeleza Waliofika kwenye mkutano huo kuwa chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Dkt John Pombe Magufuli kimefanikiwa  mambo mengi ya maendeleo  ambapo hata wapinzani wamekosa hoja za msingi.


 "Watu wenye akili zao vijana na kama Kumbilamoto na akinamama mtatiro wameona Mazuri ya CCM na kuamua kumuunga mkono Rais, nami na waaomba  kesho siku ya jumapili tarehe16/2018 wakazi wa Vingunguti mpigieni kura Omary Said Kumbilamoto mapematu tuwetumeshinda Jina lake kwenye karatasi litakuwa nambambili"amesema


 Viongozi wengine waliomwombea kura Kumbilamoto ni pamoja na mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu , Bonna Kaluwa, wa Segerea, Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es salaam Frank Kamugisha na Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM akitokea CUF  na Wenyeviti saba wa Mitaa ya kata hiyo.


Katika hatua nyingine Diwani wa kata ya Buguruni kwa mnyamani Shukuru Dege leo amejivua uanchama wa Chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM, ambapo amesema ameamua kujiunga na CCM kwa kuwa CUF imepoteza mwelekeo na pia ameamua kuunga mkono serikali ya awamu ya tano.


Pamoja na hayo Mgombea wa kata hiyo Omary Said Kumbilamoto amesema amefurahishwa na wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba tena kesho kumpigia kura kwa wingi iliaendeleekuwatumikia  akiwa CCM na kuwaletea maendeleo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwisho wa Kampeni za Mwisho Udiwani kata ya Vingunguti
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa , Humphrey Polepole akimnadi mgombea wa Udiwani wa kata ya Vingunguti Kupitia CCM , Omary Kumbilamoto
 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Vingunuti Omary Kumbilamoto akiomba Kura kwa mara ya mwisho wakati w akuhitimisha kampeni
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo kupitia  Chama Cha Wananchi CUF ,Sharifu Mbulu akizungumza mara baada ya kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni Vingunguti
 Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza Jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika Mkutano wa kuhitimisha Kampeni Vingunguti
 Aliyekuwa Diwani wa Mtoni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam , Benard Mwakyembe akizungumza wakati wa Mkutano wa kuhitimisha Kampeni kat aya Vingunguti



WANANCHI WILAYANI BARIADI WARIDHIA KUACHIA MAENEO YAO KUPISHA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu 

Wananchi wa Vijiji vya Igegu na Nga’arita Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wameridhia kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mkoani Simiyu ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Igegu wilayani .

Wananchi hao wameyasema hayo Septemba 14, 2018 wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uthamini na upimaji wa maeneo hayo, ambalo linatarajiwa kumalizika baada ya mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia sasa.

Wamesema kuwa wamefurahishwa na hatua ya Serikali kujenga Kiwanja cha Ndege wilayani Bariadi na kwa kuwa ujenzi huo ni suala la maendeleo hawawezi kupinga, huku wakiiomba Serikali kuhakikisha wanalipa fedha za fidia kwa wakati mara tu baada ya kukamilisha zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo hayo.

“Kwa kuwa ujenzi wa kiwanja cha ndege ni maendeleo hatuwezi kukataa kutoa maeneo yetu, tumekubali kutoa maeneo ila ombi letu kwa Serikali tunaomba tulipwe fidia ya maeneo yetu kwa wakati na tulipwe kwa haki” alisema Ndaturu Malemi mkazi wa Kijiji cha Igegu.

“Tumekubali kutoa maeneo yetu Uwanja wa Ndege ujengwe, ushauri wangu tu ni kwamba kwa kuwa tunaelekea msimu wa kuandaa mashamba baada ya tathmini tunaomba tuliokuwa na maeneo hapa tuambiwe mapema kama ujenzi utaanza au tunaweza kuendelea na shughuli za kilimo”alisema Mahembe Mayumba mkazi wa Kijiji cha Igegu
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ng’arika Kata ya Sapiwi Septemba 14, 2018 wilayani humo, katika Uzinduzi wa zoezi la uthamini na upimaji wa maeneo ambayo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Simiyu kitakapojengwa . 
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Bi.Beaster Dotto Madale akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu,  uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018. 
Afisa Ardhi Mkuu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Bi. Cecilia Mwing’uri akifafanua jambo katika Mkutano wa kuzindua Zoezi la uthamini na upimaji wa eneo la Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mkoa wa Simiyu, uliofanyika katika Vijiji vya Igegu na Ng’arita wilayani Bariadi Septemba 14, 2018. 
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ng’arita katika Kata ya Sapiwi Wilaya ya Bariadi, wakinyoosha mikono yao juu kumhakikishia Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Festo Kiswaga kuonesha utayari wao wa kuachia maeneo yao kupisha Ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha mkoa huo, wakati wa Mkutano wa kufungua Zoezi la tathmini na upimaji wa maeneo hayo, Septemba 14, 2018. 

CCM YAFUNGA KAMPENI MONDULI KWA KISHINDO

$
0
0
Chama cha Mapinduzi(CCM) leo kimehitimisha kampeni zake za ubunge jimbo la Monduli kwa aina yake kutokana na wapambanaji wake kujipanga vyema katika kubwaga sera wakimnadi mgombea wa chama hicho Julius Kalanga.

Kampeni hizo zimefurika mamia ya wakazi wa jimbo hilo katika eneo la Mto wa Mbu na zimefungwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogoro na mgeni mashuhuri Selemani Jafo ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI).

Timu ya wapambanaji wengine iliyokuwa kwenye kampeni hizo kwa siku zote iliongozwa na William Ole Nasha, pamoja na timu ya wabunge mahiri Joseph Msukuma, Sixtus Mapunda, Catherine Magige, Ester Mahawe, Venanse Mwamoto, Dk. Kiluswa, Mariam Ditopile, Matha Mlata, Dk. Godwin Mollel, Anna Lupembe, Edwin Sanda, Godluck Mlinga, Jitu Son, Fratei Massey, na viongozi wengine wa Jumuiya zote za CCM Taifa.

Wapambanaji hao wamewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua mgombea huyo kuwa Mbunge wao ili aweze kutatua vyema kero zinazowakabili kwa kushirikiana vyema na wabunge wengine huku wakiahidi kumsaidia kuwasilisha bungeni kero za watu wa Monduli ili zitatuliwe na serikali.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Rodrick Mpogoro akiwa na viongozi wengine katika ufungaji wa kampeni za ubunge jimbo la Monduli.

Mbunge wa Kisarawe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Selemani Jafo akizungumza katika ufungaji wa kampeni za ubunge jimbo la Monduli.

Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli
Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli

Wananchi waliohudhuria kampeni za ubunge za CCM jimbo la Monduli

Jafo awajia juu Jiji la Arusha juu ya uboreshaji wa Kituo cha Afya Kaloleni

$
0
0
Na Nteghenjwa Hosseah, ARUSHA. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewajia juu viongozi wa Jiji la Arusha kwa kutaka kubadilisha matumizi ya Tsh Milioni.400 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Ukarabati wa Kituo cha Afya Kaloleni, baada ya uongozi wa Jiji hilo kutaka kuzipeleka katika kituo cha Afya Moshono. 
 “Fedha hizi zimeletwa kwa Makusudi Maalumu na mimi nakifahamu kituo hiki cha Kaloleni najua mahitaji yake sasa mnapotaka kuhamisha fedha hizi na kuzipeleka Moshono siwaelewi” Alisema Waziri Jafo.
Aliongeza kuwa "Fedha hizo zitumike kuboresha Kituo cha Afya Kaloleni kama maagizo ya awali yalivyokuwa hayo mabadiliko mimi siyaafiki".
 Alisisitiza kunawakati ni lazima nyie wataalam wa Jiji mjiongeze haiwezekani serikali ilete fedha kwaajili yakuwahudumia wananchi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa Kaloleni nyie mnataka kupeleka hela Kituo cha Afya Moshono sitaki kusikia. 
 Jafo ambaye alifanya ziara katika kituo hicho kwaajili ya kujionea kama kweli fedha hizo alizoagiza zitolewe katika kituo hicho zimeshaanza kutumika na kubaini tangu Juni 26 mwaka huu fedha hizo zilipotolewa hadi sasa hakuna ukarabati wowote uliofanyika. 
 Naye Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dkt, Simon Chacha alikiri ni kweli fedha hizo zililetwa na walitaka kuzipeleka kituo cha Afya Moshono lakini kwa maagizo ya Waziri Jaffo watajenga jengo la X-Ray, sehemu ya kusubiria wagonjwa (waiting bay), jengo la kufualia na kukarabati chumba cha meno, dawa, maabara na mfumo wa maji taka.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akiwasili katika kituo cha Afya Kaloleni wakati wa ziara yake Jijini Arusha.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Kulia) akitoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt.Simon Chacha.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Kwanza kushoto) akikagua chumba cha huduma ya meno wakati wa ziara yake katika kituo cha Afya Kaloleni Jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kulia) akipata maelekezo toka kwa Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dkt. Simon Chacha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kwanza kulia) akikagua ramani ya jengo la upasuaji na wodi ya wazazi iliyofanyiwa marekebisho kulingana na eneo la kituo kuwa  dogo kujenga kwa ramani iliyotolewa awali.

Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images