Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

SIMIYU YAANDAA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI, YAAHIDI KUTOA ARDHI YA UWEKEZAJI BURE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Serikali mkoani Simiyu imesema imeandaa mazingira wezeshi kwa wawekezaji katika Fursa  mbalimbali za uwekezaji  ikiwemo viwanda, kilimo na teknolojia, ambapo imejipanga kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo , Mhe. Anthony Mtaka katika Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Kiswaga amesema mkoa huo ni mkoa wenye ajenda ya maendeleo, hivyo umejipanga katika kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji katika fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo, ikiwa ni pamoja na  sekta ya viwanda, kilimo, tekonolojia mbalimbali, uchimbaji wa visima na fursa nyingine, ili kufikia lengo la  kuufanya mkoa huo kuwa  katika nafasi nzuri kiuchumi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE) Taifa, Bw. Fredy Manento, akitoa taarifa ya Chama hicho wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

“Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi mkifika hapa chagueni tu sehemu mje kuwekeza, mtu atakayekuja kujenga kiwanda kikubwa, kizuri ardhi tutampa bure, sisi tutamuuliza tu kwamba tuandike jina gani kwenye hati na tutamkabidhi hati yake, kwa hiyo ATAPE pelekeni salamu kwa wawekezaji wenzenu kuwa ardhi ya uwekezeaji Simiyu ni bure, ninyi mtafute mtaji tu” alisema Kiswaga.

Ameongeza kuwa wawekezaji wote watakaowekeza mkoani Simiyu watapata soko la uhakika la bidhaa zao, huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu na mikoa inayouzunguka ina wakazi wasiopungua milioni 10 ambao watakuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa zao watakazozalisha.

Aidha, Kiswaga ametoa wito kwa wawekezaji wote wakiwemo ambao ni wanachama wa  Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), kuwekeza katika ujenzi wa hoteli na hosteli katika Eneo la Nyakabindi mahali ulipo Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi ili kukabiliana na changamoto ya malazi.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE), wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (hayupo pichan) wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI

Ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Terminal 3 wakamilika kwa asilimia 81, kumalizika Mei 31 mwakani.

$
0
0
Na Grace Semfuko- MAELEZO.

Ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam (Terminal 3) umekamilika kwa asilimia 81, na miezi minane ijayo kazi zote za ujenzi wa majengo na mahitaji yote ya uwanja yatakuwa yamekamiliki na tayari usafiri wa anga wa Tanzania kukidhi mahitaji yote ya kisasa kimataifa.

Ujenzi huo unaojengwa na kampuni ya Bam International ya Uholanzi ikisaidiwa na kampuni zingine 21 za kihandisi za ndani na nje ya nchi, ujenzi ulianza Juni mwaka 2013 na utakamilishwa Mei 31, 2019 kwa gharama Yuro 254 milioni, sawa na shilingi Bilioni 560 za kitanzania.

Akizungumza uwanjani hapo Msimamizi wa Jengo hilo kwa upande wa Mradi huo kutoka Wakala wa Taifa wa Barabara TANROADS, Mhandisi Burton Komba, amesema ujenzi huo unaendelea vizuri na kwamba kukamilika kwake kutarahisisha kusafirisha Abiria wa Kimataifa ambao kwa sasa wanahudumiwa na Uwanja huo jengo la pili (Terminal 2).

“Uwanja wa Ndege wa Kimataifa jengo la tatu utakamilika mei 31 mwakani ambapo utahudumia Abiria milioni 6 kwa mwaka,hii itasaidia kuhudumia abiria wengi zaidi ambao walikuwa wakihudumiwa na Terminal 2, (jengo la pili)”.

Kukamilika kwa uwanja huu wa jengo la tatu ambapo huduma zote zimewekwa katika viwango vya juu vya kimataifa na hivyo jengo hilo kutumika kutoa huduma za viwango vya kundi la watu muhimu (VIP) na watu mashuhuri kibiashara (CIP).

Mhandisi amesema wakati jengo la pili linajengwa lengo lilikuwa ni kuweza kumudu abiria milioni moja na nusu lakini akasewma kwa sasa jengo limekuwa likihudumia zaidi ya idadi hiyo, “tumekuwa tukifikia abiria milioni mbili na nusu” alisema Mhandisi Komba.

Jengo hilo la tatu litakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege 17 hadi 19 zikiwemo ndege kubwa kwa wakati mmoja na hivyo kumudu abiria hadi milioni 6 kwa mwaka, pia eneo la nje ya uwanja kuna nafasi ya kuegesha magari 2,000 kwa dhamira ya kushusha na kupakia abiria wanaokuja na kuondoka nchini.

Kukamilika kwa ujenzi huo ni juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha miundombinu inaboreshwa, lengo likiwa ni kufanikisha usafiri wa anga kasasa zaidi ili kuleta tija kwa uchumi wa Tanzania toka abiria na mizigo ya ndani na mataifa mbalimbali duniani.

SIKU YA MOYO DUNIANI KUADHIMISHWA KWA KUPIMA MAGONJWA YA MOYO

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha madaktari wa moyo nchini Dkt. Robert Mvungi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati alipotambulisha siku ya moyo duniani ambayo itafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Septemba 29,2018.

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
MAADHIMISHO ya siku ya moyo duniani yenye kauli mbiu ya "My "Heart, Your hear" (Moyo wangu, moyo wako) yanatarijiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu katika Mikoa mbalimbali na jumbe mbalimbali  kuhusu ugonjwa wa moyo kutolewa.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa chama cha madaktari wa moyo nchini Dkt. Robert Mvungi ameeleza kuwa sherehe hizo katika Mkoa wa Dar es salaam zitaongozwa na kiongozi kutoka Wizara ya Afya na zitafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na klabu mbalimbali za mazoezi kutoka Wilaya zote zitakutana viwanjani hapo wakitokea katika maeneo yao.

Aidha ameeleza kuwa hospitali mbalimbali zitashiriki katika maadhimisho hayo zikiwemo zile za hospitali za serikali na watu binafsi kama vile Mloganzila, Amana, Temeke, Aga Khan na Kairuki hospitali.

Pia amesema kuwa Mikoa mbalimbali itaadhimisha siku hiyo katika maeneo yao ikiwemo Moshi katika viwanja vya hospitali ya Kilimanjaro Christian Centre,  Mwanza wataadhimisha siku hii katika viwanja vya hospitali ya Bugando, na Mbeya wataadhimisha siku hiyo  katika viwanja vya hospitali ya rufaa ya Mkoa na maandamano katika Mikoa hiyo itaanzia kwenye ofisi za wakuu wa Mikoa na kumalizika kwenye maeneo yaliyopangwa ambapo upimaji wa magonjwa ya moyo na elimu itatolewa na kwa Mkoa wa Dodoma maadhimisho hayo yatafanyika katika hospitali ya Benjamini Mkapa.

Mvungi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kujua namna ya kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo yanaweza kuzuilika kwa asilimia 80 kwa kuishi maisha ya afya nzuri, kufanya mazoezi, kutovuta sigara na kuepuka mwili mkubwa(obesity.)

SERIKALI YAANZA KUTUMIA NDEGE KULINDA MISITU

$
0
0
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imeanza kutumia safari za anga kufanya doria katika kukabiliana na changamoto kubwa inayoikabili serikali katika uhifadhi wa Sekta ya misitu na maliasili kwa jumla.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TFS Professa Dos Santos Silayo, amesema lengo la doria hizo ni kuhakikisha ulizi unaimarishwa katika maeneo yote ya misitu ambayo TFS imepewa dhamana ya kuilinda.

“Nimeelekeza watendaji wangu kufanya doria ya anga kuanzia leo na tutaanza na Kanda ya Mashariki na nizitake kanda nyingine zijipange, maeneo/misitu korofi myabaini na kutafuta ramani zake. Nitawatumia ndege kwa ajili ya doria kutambua uharibifu.

“Tumekuwa tukifanya doria za misitu lakini tumekuwa tukiwiwa vigumu kuyafikia maeneo yote, lakini kupitia doria za anga sasa tutajua kila kinachoendelea kwenye eneo la misitu na kwa kutumia vikosi kazi vyetu tutafanya ulinzi kwa uhakika zaidi,” amesema Profesa Silayo.

Professa Silayo aliongoza kuwa ili kuongeza tija TFS itashirikiana na Wakuu wa wilaya pamoja wa wataalamu wa ardhi wa maeneo husika.

Akizungumzia mara baada ya kufanya doria ya anga, Meneja Msaidizi wa TFS, Kanda ya Mashariki, Bernadetha Kadala alisema doria hio imewawezesha kuona kwa karibu zaidi hali halisi ya misitu iliyopo kwenye Kanda za Mashariki na kufahamu kuna nini kinachotokea kwa wakati huo na hivyo itawawezesha kufanya ulinzi kwa weledi.
 TFS ikifanya doria ya anga ikionyesha baadhi ya wananchi wakiwa wanatengeneza jahazi kwa kutumia miti waliyovuna kinyume na taratibu kutoka msitu wa Mohoro River Wilayani Rufiji mapema jana. 
TFS ikifanya doria ya anga ikionyesha mistu wa Hifadhi wa Rufiji Delta ukiwa katika hali nzuri baada ya wananchi kuelewa umuhimu wa kuhifadhi mikoko kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. Picha na TFS.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAKUKURU YAWASAKA HANSPOPE NA LAWUO KWA KOSA LA UDANGANYIFU

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawatafuta washtakiwa, Zacharia Hanspope ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya Simba Sports Club na ndugu Franlin Peter Lauwo ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ranky Infrastrure & Engineering iliyopewa zabuni ya kujenga uwanja wa Simba kujibu kesi ya jinai namba 214/2017.

Akizungumza na Waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo amesema Mshatakiwa wa kwanza, Zacharia Hanspope aliondoka nchini mnamo April 8 ,2018 kupitia mpaka Horohoro kwa kutumia Passport namba TA00422.

“Mfanyabiashara aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Sports Club ambaye alizaliwa Iringa Mjini ambaye kabla ya kuondoka alikuwa anaishi Mlalakuwa Mikocheni ambaye amebainika kuwa anamiliki hati za kusafiria tatu ambapo moja ni hati ya kusafiria ya Afrika Mashariki na hati mbili za kusafiria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotolewa kwa vipindi viwili tofauti ambapo hati ya kwanza yenye nambari AB710516 ya 16 April 2016 na nyingine ni hati yenye nambari AB 92 9732 Iliyotolewa tarehe 16 Novemba 2017”amesema

Amesema kuwa mshatikiwa namba moja anashtakiwa kwa kwa kosa la kutoa taharifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi K/F106(1)(A)&(C) Cha kodi ya mapato chini ya sharia ya kodi namba 332.R.E 2008 kwamba kati ya washtakiwa wenzake Evans Aveva na Godfrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania .

Amesema kuwa maelezo hayo yalikuwa kwamaba Simba Sports Club wamenunua nyasi za Bandia kutoka kampuni ya Ninah Guanzhou Trading Limited kwa thamani ya Dola za Marekani 40,577.00 USD , Maelezo ambayo yalikuwa ya uongo kwania nyasi hizo zilinunuliwa kwa 109,499.00 USD.

Generali Mbungo alimtaja ndugu Franklini Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi bila ya kusajiliwa K/F22(1)(D) Cha usajili wa wakandarasi Sura ya 235 ya 2002 Kwamba kati ya Machi 2016 na Septemba 2016 Mshatakiwa alifanya kazi za ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Simba Sports Club Uliopo Bunju Manispaa ya Kinondoni kwa thamani ya Tsh 249,929,704 wakati akiwa ajasajiliwa katika bodi ya wakandarasi Tanzania hivyo kisheria alikuwa haruhusiwi kufany akazi hiyo.

Prof. Kamuzora –Tuwajengee Vijana Wetu Uwezo Kifikra

$
0
0
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu ) Prof .Faustin Kamuzora akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi zilizoko Msasani leo (jana) alhamisi Septemba 13, 2018 Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano baina yake na Watendaji wa Taasisi hiyo kuhusu namna bora ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia ujasialiamali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ujasiriamali na Ushindani Nchini (TECC) Sosthenes Sambua na wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanchi Kiuchumi (NEEC) Bang’i Issa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ujasiriamali na Ushindani Nchini (TECC) Sosthenes Sambua (wa kwanza Kulia) akieleza jambo kwa Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu ) Prof .Faustin Kamuzora (wa pili kulia) katika mjadala kuhusu njia bora ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia ujasiariamali. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF). Kongamano hilo limefanyika leo (jana) alhamisi Septemba 13, 2018 katika ofisi za TPSF zilizopo Msasani Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu ) Prof .Faustin Kamuzora akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, mara baada ya mkutano baina yake na Watendaji wa Taasisi hiyo kuhusu kuwainua vijana kiuchumi kupitia ujasiariamali uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Umeme wa Uhakika Kuchagiza Ukuaji wa Viwanda Kanda ya Kusini

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani 
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
SERIKALI  imetumia kiasi cha shilingi bilioni 216 kukamilisha mradi wa Umeme wa Makambako hadi Songea ikiwa ni moja ya miradi ya kimkakati yenye lengo ya kufanikisha sera ya Tanzania ya viwanda.

Akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa ifikapo mwisho wa mwezi Septemba mitambo ya mradi huo itawashwa na wananchi wa mikoa ya Njombe na Ruvuma wataanza kufurahia umeme wa uhakika kutoka gridi ya taifa. 

"Mradi huu utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi kwani wataunganishiwa umeme kwa bei nafuu ya mradi wa REA ambayo ni elfu 27 tu na kuwanufaisha wateja 22,700 hali itakayowawezesha wananchi kutumia umeme huo kwa ujenzi wa viwanda na shughuli za maendeleo katika maeneo yao" Alisisitiza Dkt. Kalemani

Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaokoa fedha kiasi cha Shilingi bilioni 9.1 ambazo zinatumika kununua mafuta mazito yanayotumika kwenye mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Madaba, Ludewa, Mbinga, Namtumbo na Songea Mjini. 

Akielezea ujenzi wa mradi huo uliotekelezwa na Serikali ya Tanznaia kwa kuhsirikiana na Serikali ya Sweden, Waziri Kalemani amesema mradi huo umetekelezwa kwa awamu mbili. "Sehemu ya kwanza ya mradi huu imehusisha ujenzi wa vituo vitatu vya kupooza na kusambaza umeme mkubwa wa msongo wa KV 220 vilivyojengwa Makambako, Madaba na Songea na sehemu ya pili ilihusisha ujenzi wa miundo mbinu ya kusafirisha umeme". 

Akizungumzia mradi wa REA awamu ya tatu ambao unatarajiwa kuunganisha vijiji 5100 kwenye mtandao wa umeme Dkt. Kalemani amesema vijiji 818 tayari vimeshaunganishwa tokea kuanza kwa mradi huo mwezi Julai mwaka huu. 

Aliongeza kuwa lengo la Serikali kufikisha umeme katika Vijiji 12,268 ni kutekeleza azma ya kufikisha umeme kwa kila mwananchi bila kujali anaishi mjini au kijijini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa upande wa mradi wa Kinyerezi Dkt. Kalemani amesema mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na megawati 218 tayari zimeshaingizwa kwenye gridi ya Taifa. Megawati za umeme zilizobaki zinatarajiwa kuingizwa kwenye gridi ya taifa kabla ya mwanzo wa mwezi Oktoba.

MIAKA MITATU YA JPM IMEONGEZA ARI YA KUFANYA KAZI-MAJALIWA

$
0
0
*Ameimarisha nidhamu, uadilifu kwenye utumishi wa umma

*Ameboresha miundombinu ya reli, barabara, nishati, elimu na afya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, amefanikiwa kuimarisha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji ndani ya utumishi wa umma pamoja, kukemea uzembe na kujenga ari ya kufanya kazi.

Mafanikio mengine ni ununuzi wa meli katika ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria pamoja na kufufua Shirika la Ndege la Tanzania ili kuimarisha usafiri wa anga na kukuza sekta mtambuka zikiwemo za utalii, afya, kilimo na kujenga reli ya kiwango cha kimataifa (SGR).

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novema 6, 2018.

Amesema mafanikio mengine yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli ni kuendesha vita dhidi ya rushwa na ufisadi kwenye taasisi za umma sambamba na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na kuimarisha ulinzi wa rasilimali za nchi ikiwemo madini na maliasili.

“Kujenga vyanzo vipya vya umeme kama vile mradi wa kuzalisha umeme wa maji megawati 2,100 katika bonde la mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), kusambaza umeme hadi vijijini sambamba na kuongeza kasi ya utekelezaji wa  miradi ya awamu ya tatu ya mpango wa REA ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania).”

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameimarisha huduma za afya hususan upatikanaji wa dawa, vifaatiba katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za wilaya na utoaji Elimumsingi Bila Malipo kwa watoto wa Kitanzania.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Kumi na Mbili  wa Bunge jijini Dodoma, Septemba 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na wabunge baada ya kusoma hotuba ya kuahirisha Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge jijini Dodoma Septemba 14, 2018. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. KIJAJI - UWEKEZAJI WA MSHAHARA NI JUKUMU LA MFANYAKAZI

$
0
0
Na. WFM
Serikali imeeleza kuwa uwekezaji wa mishahara kwa wafanyakazi nchini ni jukumu la mfanyakazi mwenyewe kwa kuwa mshahara ni mali ya mfanyakazi hivyo anaweza kuutumia kwa kuwekeza au kuto kuwekeza.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Viti maalum Mhe. Mwantum Dau Haji, aliyetaka kujua Serikali inasema nini kuhusu uwekezaji wa mishahara kwa watumishi wa umma na kuwepo kwa ucheleweshaji wa mishahara kwa Watumishi wa Umma..

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa upande wake inawalipa mishahara wafanyakazi wake kwa wakati kwa kuzingatia waraka wa Hazina namba 12 wa mwaka 2004 ambao unaitaka Serikali kulipa mishahara kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi.

“Kumbukumbu za malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma zinaonesha kuwa, kuanzia Julai 2017 hadi Agosti 2018, watumishi walilipwa mishahara yao kati ya tarehe 20 na 24 ya kila mwezi hivyo napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu na umma kwa ujumla kuwa hakuna ucheleweshaji wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma” alieleza Dkt. Kijaji.

Aidha Serikali imekuwa ikiwatendea haki wafanyakazi wake katika upandishaji wa madaraja na kila mwaka wafanyakazi hupandishwa madaraja.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)

WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA MWAKINYO KWA KUMCHAPA MUINGEREZA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempongeza mwanamasumbwi wa Kitanzania Bw. Hassan Mwakinyo (23) kwa kumchapa bkondia Mwingereza Bw. Sam Egginton.

Bw. Mwakinyo alimchapa Bw Egginton kwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika Jumapili, Septemba 9, 2018, huko  Birmingham nchini Uingereza.

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 6, 2018.

Amesema bondia huyo amelipa Taifa heshima kubwa kwa kulitangaza kimataifa katika Nyanja ya michezo, hivyo amewataka wanamichezo wengine nchini waige mfano wake.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu  ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake (Kilimanjaro Queens) kwa kutwaa kombe la Afrika Mashariki. 

Pia ameipongeza timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kuwa washindi wa tatu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).  

“Hongereni sana wanamichezo wetu na endelezeni moyo huo wa kizalendo mliouonesha katika kulitangaza Taifa letu.

Pia Waziri Mkuu amesema mwaka 2019 Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON-U17) yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika.

Amesema hiyo ni fursa nyingine ya kipekee ya kulitangaza Taifa letu katika nyanja za Kimataifa, hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na maandalizi, ambayo yatahusisha ukarabati wa viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo. 


Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi watumie vizuri uwepo wa mashindano hayo kujiongezea kipato hususan kupitia biashara ya bidhaa na huduma kwa wageni, pia amewataka wawe wazalendo kwa kuunga mkono timu zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa ili zipate mafanikio.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bondia Hassan Mwakinyo kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Septemba 14, 2018. Mwanamasumbwi huyo hivi karibuni alimtwanga kwa TKO, Bondia Sam Egginton wa Uingereza katika pambano lililofanyika Birmingham. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU AMEMPONGEZA BONDIA HASSAN MWAKINYO, KILIMANJARO QUEENS NA SERENGETI BOYS KWA KUFANYA MAAJABU

$
0
0

WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza mwanamasumbwi wa Kitanzania Hassan Mwakinyo (23) kwa kumchapa bondia Mwingereza Bw. Sam Eggintonkwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika Jumapili, Septemba 9, 2018, huko Birmingham nchini Uingereza.
 Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo (Ijumaa, Septemba 14, 2018) wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 6, 2018. Amesema bondia huyo amelipa Taifa heshima kubwa kwa kulitangaza kimataifa katika Nyanja ya michezo, hivyo amewataka wanamichezo wengine nchini waige mfano wake.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameipongeza timu ya Taifa ya Wanawake (Kilimanjaro Queens) kwa kutwaa kombe la Afrika Mashariki. Pia ameipongeza timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kwa kuwa washindi wa tatu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
 “Hongereni sana wanamichezo wetu na endelezeni moyo huo wa kizalendo mliouonesha katika kulitangaza Taifa letu. Pia Waziri Mkuu amesema mwaka 2019 Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON-U17) yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika.
 Amesema hiyo ni fursa nyingine ya kipekee ya kulitangaza Taifa letu katika nyanja za Kimataifa, hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na maandalizi, ambayo yatahusisha ukarabati wa viwanja vitakavyotumika katika mashindano hayo.
 Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi watumie vizuri uwepo wa mashindano hayo kujiongezea kipato hususan kupitia biashara ya bidhaa na huduma kwa wageni, pia amewataka wawe wazalendo kwa kuunga mkono timu zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa ili zipate mafanikio.

POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuimarisha ulinzi uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga na Kata ya Vingunguti unaotarajia kufanyika Septemba 16 mwaka huu.

Limesema halitamvumilia mtu yoyote  atakayebainika kufanya kuvuruga katika mchakato huo na kwamba atakeyakamatwa matokeo ya uchaguzi atayasikia akiwa mikononi mwa Polisi.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati anazungumza namna walivyoimarisha ulinzi katika maeneo ambayo uchaguzi mdogo.

Amesisitiza jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kabla, baada ya uchaguzi hadi matokeo yanapotangaza na mshindi kutangazwa.
“Napenda kuwatoa hofu wananchi jeshi la Polisi limejiandaa kwa kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa uchaguzi huo.

“Tunawaonya waliopanga kufanya vurugu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Rai ya jeshi la Polisi kwa wananchi ni kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa kufuata sheria na taratibu watakazoelekezwa siku ya hiyo na wahusika wa uchaguzi bila kuleta vurugu au wao kuwa chanzo cha vurugu,”amesema.

 Mambosasa ameongeza kila kituo cha kupiga kura kutakuwa na askari wa vikosi mbalimbali kwa ajili ya kufanya doria kila sehemu wakiongozwa na askari maalumu wa kikosi cha kutuliza ghasia.
Amewahakikisha jeshi hilo kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa mtu yeyote au kikundi chchote chenye nia ya kufanya vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na kanuni au sheria ya uchaguzi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akionesha bastola zilizokamatwa na jeshi la polisi katika msako wa wa kutafuta waharifu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Bastola na Magazini na Risasi zilizokamatwa katika msako wa waharifu Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na msako wa waharifu jijini Dar es Salaam.

UBALOZI WA CHINA WAMKABIDHI ZAWADI DK.TULIA

$
0
0

*Ni kwa ajili ya washindi wa Tulia Traditional Dances Festival 
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust Dk.Tulia Akson ameushukuru Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kumkabidhi pikipiki 10 kwa ajili ya washindi watakaopatikana kwenye tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018.

Dk.Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge amekabidhiwa pikipiki hizo leo katika ubalozi huo na Mwakilishi wa Balozi wa China Tanzania nchini Xu Chen.Thamani ya pikipiki hizo ni Sh.milioni 21,600,000.

Akizungumza baada ya kupokea pikipiki hizo Dk.Tulia amesema anaushukuru ubalozi huo kwa kutoa zawadi hizo kwa ajili ya washindi wa tamasha hilo litakalofanyika kuanzia Septemba 18 hadi Septemba 22 mkoani Mbeya.

“Kwa niaba ya Taasisi ya Tulia Trust tunatoa shukrani zetu kwa ubalozi wa China nchini Tanzania kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi kwa kutoa zawadi kwa ajili ya washindi.

“Mwaka jana walitoa pikipiki 10 ambazo tulikabidhi kwa washindi.Lengo la tamasha hili ni kukuza utamaduni wetu na tumeanza na ngoma za asili.Pia  tunataka wanaoshiriki pia wajikwamue kiuchumi,”amesema Dk.Akson.

Akifafanua zaidi kuhusu zawadi kwa washindi Dk.Askon amesema mshindi wa kwanza kwa idadi iliyopo watapata zawadi na kwamba jumla ya vikundi 108 vitashiriki.

Pia amesema tamasha hilo ni endelevu na linafanyika kwa mara ya tatu mfululizo na lengo kuu ni kukuza utamaduni wetu, pia iwe sehemu ya kuwawezesha wananchi kujenga uchumi,”amesema.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akipokea hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kutoka kwa Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akisainiana hati ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ubalozini hapo jijini Dar es Salaam, jana. Pikipiki hizo zitatolewa kwa washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jini Mbeya. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania, Xu Chen, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya zawadi ya Pikipiki 10 kwa ajili ya washindi wa kwanza 10 kutoka katika kila kundi kwenye Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 linalotarajia kuanza Septemba 18 hadi 22 jijini Mbeya.
(Picha na Muhidin Sufiani)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO SEPTEMBA 15 UWANJA WA NDANI WATAIFA

$
0
0
Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Georger Dimoso kushoto na Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuzipiga kesho jumamosi Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Mabondia Georger Dimoso kushoto akitambiana na Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' baada ya upimaji wa uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwatambulisha mbele ya wahandishi wa habari mabondia Saidi Bakari 'Kidedea' kushoto na Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Mabondia Saidi Bakari 'Kidedea' kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kumaliza kupima uzito katikati ni Promota Rajabu Mhamila 'Super D baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Promota wa mpambano wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Frank John kushoto na Bakari Mbede baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya jymamosi Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Bondia Frank John kushoto akitunishiana misuli na Bakari Mbede wakati wa kupima uzito kwa mabondia hawo watazipiga siku ya jumamosi Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondiaImani Mapambano kushoto na Paul Kamata baada ya kupima uzito kwa ajili ya kuzipiga kesho jumamosi Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.
Mabondia Imani Mapambano kushoto akitambiana na Paul Kamata baada ya upimaji wa uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BREAKING: TAKUKURU YAWASAKA ZACHARIA HANSPOPE NA FRANKLIN LAUWO KWA KOSA LA UDANGANYIFU

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawatafuta Zacharia Hanspope ambaye aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Simba Sports Club na ndugu Franlin Peter Lauwo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ranky Infrastrure & Engineering iliyopewa zabuni ya kujenga uwanja wa Simba kujibu kesi ya jinai namba 214/2017. 

 Akizungumza na Waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo amesema Mshatakiwa wa kwanza Zacharia Hanspope aliondoka nchini mnamo April 8, 2018 kupitia mpaka Horohoro kwa kutumia Passport namba TA00422. 

 “Mfanyabiashara huyu aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba Sports Club na ambaye alizaliwa Iringa Mjini kabla ya kuondoka alikuwa anaishi Mlalakuwa Mikocheni ambako amebainika kuwa anamiliki hati za kusafiria tatu ambapo moja ni hati ya kusafiria ya Afrika Mashariki na hati mbili za kusafiria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotolewa kwa vipindi viwili tofauti ambapo hati ya kwanza yenye nambari AB710516 ya 16 April 2016 na nyingine ni hati yenye nambari AB 92 9732 iliyotolewa tarehe 16 Novemba 2017,” amesema 
 Amesema kuwa mshatikiwa namba moja anashtakiwa kwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi K/F106(1)(A)&(C) Cha kodi ya mapato chini ya sharia ya kodi namba 332.R.E 2008 kwamba kati ya washtakiwa wenzake Evans Aveva na Godfrey Nyange walitoa maelezo ya uongo kwenye ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania.
Amesema kuwa maelezo hayo yalikuwa kwamba Simba Sports Club wamenunua nyasi bandia kutoka kampuni ya Ninah Guanzhou Trading Limited kwa thamani ya Dola za Marekani 40,577.00 USD, maelezo ambayo yalikuwa ya uongo kwania nyasi hizo zilinunuliwa kwa 109,499.00 USD.

Generali Mbungo alisema Franklin Lauwo anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya ukandarasi bila ya kusajiliwa K/F22(1)(D) Cha usajili wa wakandarasi Sura ya 235 ya 2002 Kwamba kati ya Machi 2016 na Septemba 2016 Mshatakiwa alifanya kazi za ukandarasi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa Simba Sports Club Uliopo Bunju Manispaa ya Kinondoni kwa thamani ya Tsh 249,929,704 wakati akiwa hajasaliwa katika bodi ya wakandarasi Tanzania hivyo kisheria alikuwa haruhusiwi kufanya kazi hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Generali John Mbungo akiongea na wanahabari jijini Dar es salaam leo


DKT. TULIA APOKEA ZAWADI YA PIKIPIKI 10 KUTOKA UBALOZI WA CHINA

MICHUZI TV: AJALI ZA MBEYA ZATAFUTIWA UFUMBUZI...

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA SEPTEMBER 14, 2018

MICHUZI TV: POLISI DAR YAWAONYA WATAKAOFANYA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI JIMBO LA UKONGA

BBC SWAHILI: JK AMZUNGUMZIA MAREHEMU KOFFI ANNAN

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images