Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 246 | 247 | (Page 248) | 249 | 250 | .... | 3270 | newer

  0 0

  President Robert Mugabe of the Republic of Zimbabwe awaits to receive Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation.  Minister Membe paid a courtesy visit earlier today at President Mugabe's State House on behalf of President Jakaya Mrisho Kikwete.

  President Mugabe receives and welcomes Minister Membe to the State House.  Witnessing the special moment is Hon. Simbarashe Mumbengegwi, Foreign Minister of Zimbabwe.  

  President Mugabe shares some few laughters with Minister Membe during their meeting earlier today at his State House in Harare, Zimbabwe.  

  Hon. Membe was in Zimbabwe to deliver the Southern Africa Development Community (SADC) Electoral Observer Mission Report, based upon the presidential elections that took place on July 31st, 2013.  Tanzania was a former Chair of the SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation under the Chairmanship of His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania. 

  Minister Membe takes time to explain to President Mugabe about the SADC's final report on the Zimbabwe's election.  H.E. Robert Mugabe was elected to his seventh term as President of Zimbabwe with 61%, leaving his opponent Prime Minister Morgan Tsvangirai with 34% of votes, according to the election commission in Zimbabwe.

  Also in attendance was Ambassador David Kapya.

  Also present were Hon. Simbarashe Mumbengegwi (seating-left), Foreign Minister of Zimbabwe and Ambassador Adadi Rajab (seating 2nd left) of the United Republic of Tanzania in Zimbabwe.

  President Mugabe walks off Minister Membe, after they finished their discussion earlier today at his State House in Harare, Zimbabwe.  Also in the photo is Ambassador Selma Ashipala-Musavyi, Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs in the Republic of Namibia.  All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation 

  0 0

  Meneja Uhasibu wa Maxcom Africa,Bi.Lucy Kanza akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Road License kwa kutumia huduma ya M-PESA.Wanaoshuhudia katika ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo.
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa (katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo na kushoto ni Meneja wa Uhasibu wa Maxcom Africa,Bi.Lucy Kanza.
  Mmoja wa waandishi wa habari kutoka kituo cha Channel Ten Bw.Fred Mwanjala(katikati)akiuliza swali katika uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)wakifuatilia jambo kwa umakiini wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia huduma ya M-PESA.

  Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini - TRA leo imezindua rasmi mfumo wa ulipaji wa ada za magari - Raod License kwa kutumia utatartibu wa M-pesa huku tayari mfumo huo ukionekana kukubalika zaidi na walipa kodi hiyo nchini.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es salaam Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa kampuni ya Vodacom Kelvin Twissa amesema kuzinduliwa kwa utaratibu huo ni mwendelezo wa namna ambavyo maisha ya watanzania yanavyozidi kuwezeshwa kuwa rahisi wakati ambapo M-pesa inazidi kuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya Mtanzania.

  Twissa amesema ukuaji wa kasi wa matumizi ya M-pesa unathibitisha umuhimu wake hapa nchini na kuongeza kuwa kutumika kwenye ukusanyaji wa kodi ni hatua nyingine muhimu kwa faida ya walipa kodi ambapo sasa M-Pesa ni sehemu ya maisha ya watanzania na hakuna tena sababu ya kupanga foleni ndefu na kutumia muda mwingi.

  "Ni Wakati mwingine M-pesa inavyowapa wananchi na walipa kodi wengine wote hapa nchini utataribu mwepesi, rahisi, salama na wa uhakika zaidi wa kulipa ada za leseni ya magari kwa urahisi zaidi wakati wowote mahali popote."Alisema Twissa

  "Tunapotambua umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya nchi hatuna budi kufurahia hatua hii ambayo tayari katika kipindi cha muda mfupi kisichozidi wiki mbili M-pesa imeshaonesha mafanikio makubwa katika makusanyo, hili linatupa furaha kama kampuni na ni wazi kila mmoja analifurahia."Aliongeza Twissa.

  Twissa amesema Vodacom itaendelea kuuwezesha mfumo wa M-pesa kuwa wenye kutoa suluhisho la masuala mengi zaidi ili kukidhi shabaha ya kampuni hiyo ya kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya huduma za simu za mkononi.

  "Tumekuwa imara wakati wote tangu M-pesa ilipozinduliwa nchini mwaka 2007, hata hivyo bado tunashauku ya kufanya mapinduzi makubwa zaidi kupitia M-pesa tukitambua kwamba hiyo ni kiu ya kila mmoja kuzingatia kile ambacho tayari M-pesa inayaywezesha kupitia viganja vya mikono yao."Alisema Twissa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo amesema M-pesa imeleta urahisi zaidi kwa Mamlaka katika ukusanyaji wa ada za leseni ya magari .

  "Ni jambo jema kwa mamlaka kuona inawapatia wateja wake(walipa kodi)utaratibu rahisi zaidi kwao katika kuwawezesha kutimiza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi pasi na kuwepo usumbufu wa aina yoyote huku pia utaratibu huo ukileta ufanisi kwa mamlaka."Alisema Kayombo.

  Amesema TRA ina imani kuwa ushirikiano wake na Vodacom utakuwa wenye tija zaidi katika siku zijazo kwa kuhakikisha mfumo wa M-pesa unatoa uwezo zaidi kwa walipa kodi kuutumia katika kuleta urahisi kwao kulipa kodi mbalimbali.

  Inakidiwa kuwa katika kipindi cha wiki mbili TRA imekusanya kaisi cha Bilioni 2 cha malipo ya ada za magari kupitia M-pesa pekee.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia(kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam(katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hebert Mrango.
  Waziri waUjenzi Mh. Dkt. john Magufuli (kushoto) akimkabidhi nyaraka Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia (kulia) leo jinini Dar es Salaam,walipokutana na kuzungumza masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha ushirikiano katika nyaja za usafirishaji .(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango.
  Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) akiaagana na Waziri wa Usafirishaji kutoka Malawi (kulia) Mh. Sidik Mia pamoja na baadhi ya ujumbe wake baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam,(katikati mwenye tai nyekundu) ni Waziri wa Nishati wa Malawi Mh. Ibrahim Matola. Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwenyekiti wa Asasi ya Kisiasa ya Konrad Adenauer Foundation ya Ujerumani, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Rais Mstaafu wa Bunge la Umoja wa Ulaya Dkt. Han-Gert Pottering (kushoto) kwa Makamu, aliyeongoza na Ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Sept 3, 2013 kwa mazungumzo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Asasi ya Kisiasa ya Konrad Adenauer Foundation ya Ujerumani, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Rais Mstaafu wa Bunge la Umoja wa Ulaya Dkt. Han-Gert Pottering, aliyeongoza na ujumbe wake baada ya mazumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Sept 3, 2013. Picha na OMR

  0 0


  0 0

   Wanaharakati  wa  mtandao  wa kijinsia  Tanzania  (TGNP)  wakiwa katika maandamano  ya  miaka 11 ya  tamasha la TGNP nchini na maadhimisho ya miaka 20  ya harakati  za ukombozi wa mwanamke
  Na  Francis Godwin Blog
  WANAHARAKATI  wa mtandao   wa  jinsia  Tanzania (TGNP) wamefanya maandamano makubwa  ya kuazimisha  miaka 20 katika  kupinga  vitendo  vya ufisadi pamoja na ukandamizaji  wa  wanawake .

  Huku mtandao  huo ukidai  kuwa  umejipanga  kuendeleza  mapambano  ili  kuwawezesha  wanawake  wa pembezoni  kuchukua  madaraka  ya  uongozi katika chaguzi  mbali mbali ili  kusaidia  kuwakomboa  wananchi  wa  pembezoni .


  0 0

  Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited yesterday confirmed receipt of a full operating license issued to them by the Bank of Tanzania.  The license empowers Dun & Bradstreet to offer Credit Bureau and related services in Tanzania.
  The issuance of an operating license by Bank of Tanzania to Dun & Bradstreet brings an end to the long wait of the financial sector for D&B’s services and opens up a new and expectedly rewarding chapter for lenders who seek secure lending, borrowers who seek easy access to credit and other stakeholders who are keen on seeing a stronger and more vibrant economy driven by Tanzania’s financial sector.

  According to Mr. Miguel Llenas, CEO of Dun & Bradstreet Credit Bureaus, the news of the issuance of an operating license to Dun & Bradstreet Credit Bureau Tanzania Limited by Bank of Tanzania was received with pleasant delight but also with the understanding that this is an immense responsibility. According to him, “We are delighted at the news of the issuance of the license by Bank of Tanzania and we thank them for taking this positive step by giving us the opportunity to bring our expertise to the benefit of all Tanzanians and everyone who does business in Tanzania.  We consider ourselves a vital part of the financial sector and are well prepared to play our role in protecting and strengthening Tanzania’s economy through its financial sector.”

  Also speaking on the news of the issuance of the license by BoT, General Manager Dun & Bradstreet Credit Bureau in Tanzania – Adebowale Atobatele expressed high optimism that with the support of the B.o.T and the collaborative efforts of all stakeholders, the Credit Reference System as championed by BoT delivers the much anticipated benefits. Mr. Atobatele said, “We are glad that we are finally kicking-off operations in Tanzania and we are very optimistic that with everyone playing their role responsibly, we will be able to create and deliver superior value to all stakeholders.  With the commencement of operations by Dun and Bradstreet Credit Bureau in Tanzania, Banks can now look forward to processing loan applications faster, reducing operational costs and with better information; furthermore, the banking public can now look forward to getting easy access to credit.”

  Dun & Bradstreet is present in 200 countries and has deployed its Credit Bureau solutions in several countries across Africa, Middle-East and Asia.

  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Oman ukiongozwa na Waziri wa Habari wa Nchi Hiyo Dr. Abdulmun Mansour Bin Said Al- Hasani hapo Ofisi kwake Vuga Mjini Zanzibar.
   Waziri wa Habari wa Nchi Hiyo Dr. Abdulmun Mansour Bin Said Al- Hasani akiagana  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya ujumbe wake kuzungumza yane hapo Ofisini kwake  Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Ujumbe wa Serikali ya Oman ambao pia upo Zanzibar kushiriki Kongamano la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiislamu. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari wa Nchi Hiyo Dr. Abdulmun Mansour Bin Said Al- Hasani  na kushoto yake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar  Said Ali Mb arouk.
  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
  --------------------------------------------
  Na Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  Uhusiano wa  kubadilishana nyaraka za Kihistoria kati  ya Oman na Zanzibar  unaweza kuwasaidia wananchi  wa pande  mbili  pamoja na watafiti wa masuala ya Kihistoria kuelewa kwa kina maingiliano ya muda mrefu yaliyopo kati ya  Wazanzibar na Waoman ambayo yanafanana  Kisilka na Kiutamaduni.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi sita wa Serikali ya Oman ulioongozwa na Waziri wa Habari wa Nchi hiyo Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani aliokutana nao hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Balozi Seif alisema Zanzibar na Oman zimekuwa na uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu tokea karne ya 18 ambao umethibitishwa na wataalamu pamoja na watafiti wa mambo ya Kihistoria kutoka vyuo vikuu tofauti Duniani.
  Alielezea haja kwa Viongozi na Wananchi wa Oman na Zanzibar kuendelea kushikamana na kushirikiana katika masuala mbali mbali ya maendeleo yatakayosaidia ustawi wa vizazi vya sehemu zote mbili rafiki.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Serikali ya Oman  kupitia ushirikiano wa mamlaka  ya kumbu kumbu na nyaraka ya Oman na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } kwa kuandaa Kongamano la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiiislamu kwa Nchi za Mashariki mwa Bara la Afrika.
  Balozi Seif alisema  uamuzi huo wa kufanywa kwa kongamano hilo  hapa Zanzibar umekuja wakati muwafaka kwa wataalamu wa mambo ya Kale kubainisha kwamba  Historia ya Uislamu imeanzia hapa Zanzibar.
  “ Nimefurahi kusikia kwamba Historia ya Uislamu imeanza Zanzibar. Inaonyesha watafiti wameliona hili kutokana na asilimia kubwa ya wakaazi wa Visiwa vya zanzibar  kuwa  waumini wa Dini ya Kiislamu sambamba na Utamaduni wake “. Alieleza Balozi Seif.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alishauri tafiti za Wataalamu wa masuala ya Historia ambazo zitaibuka katika Kongamano hilo  zielekezwe zaidi kunufaisha wananchi  na waislamu wa ukanda wote wa Afrika Mashariki.
  “ Tafiti hizi za Wataalamu wetu wa Kihistoria itapendeza kama zitaendelea kubakishwa katika maktaba zetu ili zisaidie wananchi, waislamu na hata wasomi wetu wa vyuo vikuu vya ukanda wetu wa Afrika Mashariki “. Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
  Naye Kiongozi wa Ujumbe huo wa Serikali ya Oman Waziri wa Habari wa Nchi hiyo   Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani alisema ipo haja ya kuendelea kuhifadhiwa kwa Historia iliyopo ya Zanzibar na Oman kwa faida ya vizazi vijavyo.
  Dr. Abdulmumin alieleza kwamba upeo wa tabia za watu wa oman na Zanzibar unaolingana ndio unaochangia na kushawishi wageni na watalii wa mataifa mbali mbali  duniani  kupendelea kuzitembelea nchi hizi zinazofanana kiutamaduni.
  Waziri huyo wa Habari wa Oman alifahamisha kwamba Kongamano  hilo la ustarabu wa Kiislamu linalofanyika hapa Zanzibar  mbali ya utafiti uliopatikana lakini pia litafungua uhusiano katika Nyanja nyengine za maendeleo kwa nchi shiriki.
  Dr. Abdulmumin alielezea faraja yake kutokana na umuhimu wa udugu uliopo  kati ya watu wa Oman na Zanzibar ambao umepelekea waoman wengi  kujitokeza kushiriki kwenye kongamano hilo.
  Alifahamisha kwamba ipo ishara ya kuendelea kwa ziara za mara kwa mara kati ya watu wa pande hizo mbili.
  Kongamano hilo la siku tatu linalofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya La Gemma Della East Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kushirikisha Mataifa yapatayo 17 lina lengo la kuitangaza Zanzibar katika Nyanja za utafiti na Taaluma Kimataifa.
  Hilo ni kongamano la Pili la Kimataifa la Ustarabu wa Kiislamu  kufanyika likitanguliuwa na lile la mwaka 2012 lililofanyika Nchini Uganda na kutolewa uamuzi wa kongomano linalofuata kufanyika hapa Zanzibar kutokana na  Historia yake  iliyopo  sambamba na uhusiano  wa karibu iliyonayo na Mataifa ya Kiarabu. 


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Bw Alpesh Patel ambao ni watengenezaji wa vifaa vya plastiki yakiwemo matanki ya kuhifadhia maji ya SIMTANK akisoma taarifa fupi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa Tanki jipya la Kuhifadhia maji liitwalo SIMTANK la Bluu lenye Ubora wa hali ya juu wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya uliofanyika katika ofisi zao zilizopo Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu Wa Kampuni ya SILAFRICA Alpesh Patel akimuonyesha Mwanafunzi Wa Shule ya Msingi sehemu ya Kukata Utepe Ikiwa kama Ishara ya Uzinduzi wa SIMTANK jipya lenye ubora wa hali ya juu wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya uliofanyika katika Ofisi zao zilizopo Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam
  Baadhi ya wanafunzi wanaosomeshwa na Kampuni ya SILAFRICA ikiwa kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii wakiwa makini katika uzinduzi wa SIMTANK jipya lenye ubora wa hali ya juu.
  Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Alpesh Patel Akikata keki yenye mfano wa SIMTANK lililozinduliwa leo jijini Dar Es Salaam pamoja na Mwanafunzi wa Shule ya Msingi kama Ishara ya Kuzindua tanki Jipya la SIMTANK la Bluu linalotengenezwa na kuuza na Kampuni ya SILAFRICA kupitia kwa mawakala wake
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Alpesh Patel ambao ni watengenezaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo matanki ya kuhifadhia maji ya SIMTANK akionyesha ubora wa tanki hilo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) endapo tanki hilo la SIMTANK la bluu hata kama likikanyagwa au kukandamizwa baadae linarudi kwenye hali yake ya kawaida bila kuwa na nyufa au kupasuka
  SIMTANK jipya kutoka Kampuni ya SILAFRICA ambao ni watengenezaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo Mantaki ya SIMTANK likiwa limeminywa Na gari la kubeba vitu vizito wakati wa uzinduzi wa SIMTANKI jipya la Bluu katika ofisi zao zilizopo Maeneo ya Chang'ombe Jijini Dar Es Salaam jana
   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SILAFRICA Bw Alpesh Patel ambao ndio watengenezaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo matanki ya SIMTANK akionyesha tanki la SIMTANK jipya lililominywa na gari la kubeba vitu vizito wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya lenye ubora wa hali ya Juu baada ya kuanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida mara baada ya kuminywa na gari la kubeba vitu vizito wakati wa uzinduzi wa SIMTANK jipya la bluu uliofanyika jana Katika Ofisi zao zilizopo Maeneo ya Chang'ombe jijini Dar Es Salaam
  Baunsa wa Wa SIMTANK akionyesha uwezo wake wa kutunisha misuli ikiwa kama ishara ya kuonyesha kuwa matanki yote yanayotengenezwa na kampuni ya SILAFRICA yana ubora wa hali ya juu na magumu na yenye kuaminika na wateja zaidi ya Milioni Moja Afrika Mashariki.

  0 0

  LEO UMETIMIZA MWAKA MMOJA KAMILI TOKA ULIPOTUACHA GHAFLA BAADA YA KUUGUA GHAFLA SANA. HATUNA CHA KUSEMA TUNAAMINI UMEKWENDA KUTUANDALIA MAKAO YA MILELE ILI SISI NASI TUKUTANE HUKO, MAANA HUKU DUNIANI TUKO MATEMBEZINI TU.
  VICK UMETUACHA KATIKA MAJONZI MAKUBWA NA MASWALI MENGI! KIFO CHAKO KIMETUSHTUA WENGI MAANA KIMETOKEA MIEZI MIWILI TU BAADA YA HARUSI YAKO. LAKINI KWAKUWA TU WAKRISTU TUNAAMINI MUNGU AMECHUMA UA ZURI KATIKA BUSTANI YAKE NA KAZI YAKE SIKU ZOTE HAINA MAKOSA. TUMEKUBALI YOTE! TUPO KAMA ULIVYOTUACHA, TUNAENDELEA KUKUENZI KWA HAYO INGAWAJE BADO MAJARIBU NI MENGI.

  UNAKUMBUKWA NA MIMI MAMA YAKO LYDIA, BABA JAPHET MBWANA, MUMEO MPENZI EMMANUEL KILATO, NDUGUZO MERCY, GODFREY NA VIOLLA, MAMA MKUBWA, WAJOMBA, WAKWE ZAKO, WANA UKOO WOTE, MAJIRANI WA LUMALA - MWANZA, GEITA NA DODOMA, WAFANYAKAZI BENKI KUU MWANZA, WANAJUMUIA YA FIDEL – PAROKIA YA PASIANSI, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

   MISA YA KUMALIZA MSIBA ITAKUWA NYUMBANI KWAO LUMALA B TAREHE 7/9/2013 SIKU YA JUMAMOSI SAA NANE MCHANA, KARIBUNI SANA

  RAHA YA MILELE UMPE EEH! BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWNGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI

  AMINA!


  0 0

  Na Mashaka Mhando 
  BENKI ya NMB  imetoa mafunzo ya wiki mbili kwa vyama vya ushirika vya wakulima wa mpunga na SACCO'S wilayani Korogwe, mafunzo yaliyolenga kuwaongezea uwezo wa namna watakavyoweza kuviendesha vyama hivyo katika dhana nzima ya kuondoa umasikini kwa wanachama wao. 
   Mafunzo hayo ambayo yalikuwa yakitolewa na mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Alfred Chonya yalianza tangu Agosti 17 mwaka huu na kufungwa Septemba 3 na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Bw Mrisho Mashaka Gambo kwenye aliyofanyika kwenye ukumbi wa Matunda katika mji mdogo wa Mombo wilayani Korogwe. 
   Akizungumza katika mafunzo hayo Bw Gambo alisema ni ushahidi uliokuwa wazi kwa benki ya NMB ambayo imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali katika wilaya hiyo kila inapoombwa hivyo mafunzo wanayotoa kwa wana-ushirika yatasaidia mbinu bora na uelewa wa namna kuendesha vyama hivyo vya ushirika kutokana na kwamba mara nyingi kumnekuwa na matatizo. 
   "Kazi ya kutoa elimu ilikuwa itolewe na serikali kupitia maofisa ushirika waliopo, lakini wenzetu wa NMB kwa kujali namna ya kushirkiana na wateja wao, wameonelea ni vema wakatoa mafunzo haya, kwa niaba ya serikali tunawapongeza na tunawaomba muwe na moyo huo wa kuwasaidia wateja wenu,"alisema. 
   Alisema serikali kuanzisha ushirika lengo lake lilikuwa kuwakomboa wakulima na wana-ushirika mbalimbali hivyo suala la NMB kutoa mafunzo hayo kutakuwa ni ukombozi mkubwa ingawa alisema mara nyingi mafunzo huwa yanatolewa kwa viongozi wa ushirika akaonesha haja ya wakati mwingine ni vema wanachama nao wakafaidika na mafunzo ya namna hiyo. 
   Bw. Gambo alisema serikali ina nia njema ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili waweze kujikwamua kiuchumi na suala la benki ya NMB kusaidia vikundi hivi katika wilaya yetu ni jambo la faraja kubwa kwa sababu litawafanya waweze kuendesha vikundi vyao kwa utaalamu na umahiri wa kufunga mahesabu na kukopa kwa makini na marejesho yake. 
   Awali mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Chonya ambaye alisema mafunzo hayo wameyatoa kupitia idara mpya ya NMB ya maendeleo ya Kilimo (NFAD) 'Foundation For Agricultural Development', alisema vikundi mbalimbali walivyowapa mafunzo waliweza kuwafundisha wajibu wa bodi za mikopo, wajibu wa katibu au meneja wa sacco's, Misingi ya Utawala Bora, Sifa ya kiongozi wa bora na wajibu na haki kwa wanachama.
   "Tumeweza kuwapa mafunzo haya katika ngazi mbalimbali kwa mfano unaposema sifa ya kiongozi bora ni ipi ni lazima awe mkweli daima, huongoza kwa kuonesha njia na pia awe anafuata misingi ya utawala bora kwa kuwa mwanimifu kwa wenzake na yale anayoyafanya," alisema Bw Chonya. 
   Meneja wa NMB tawi la Korogwe Bw Erasto Mwamalumbili, alisema benki hiyo imeanzisha idara hiyo mpya kwa lengo la kuwafuata wananchi kule walipo hasa katika maeneo ya vijijini kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kukopesheka kwa ajili ya kuongeza mitaji yao ya kilimo na vyama vyao vya ushirika. 
   Alisema baada ya mafunzo hayo ya awamu ya kwanza wanatarajai watatoa tena mafunzo ya awamu ya pili ili waweze kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika vilivyopo katika wialya hiyo ya Korogwe. 
   Akitoa shukurani zake Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu', alishukuru benki hiyo akieleza kwamba imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi hasa waliokuwa vijiji na kwamba atakuwa balozi wao bungeni kwa kuishawishi serikali itazame kwa jicho la pekee kwa vile imekuwa ikiwasaidia mno wakulima na wananchi kwa ujumla wenye kipato cha chini.
   Wanachama wa sacco's wakisikiliza kwa makini ufungaji huo.
   Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Bw Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu', akichangia neno la shukurani
   Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi CCM, Bw Nassoro Hemed 'Malingumu' (shoto) akimpongeza meneja wa benki ya NMB tawi la Korogwe Bw Mwamalumbili kuhusu namna alivyoweza kuwaasaidia wajasiriamali wadogo kwa mikopo ya JK.
   Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhe. Mrisho Gambo akizungumza wakati akifunga mafunzo hayo.
  Picha ya pamoja ya viongozi wa NMB kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya korogwe,

  0 0

  Mhe. Balozi Steven Matenje wa Malawi akiwa na Mhe. Palan Mulonda,Balozi wa Zambia nchini Marekani,(kulia) na Mhe. Martin Andjaba, Balozi wa Namibia nchini Marekani (kushoto)na Bw.Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC katika hafla ya uzinduzi wa Malawi Washington Foundation iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
  Mhe. Balozi Steve Matenje,Balozi wa Malawi nchini Marekani akimkaribisha Bw. Suleiman Saleh nyumbani kwake Potomac,Maryland katika hafla ya uzinduzi wa Malawi Washington Foundation mwishoni mwa wiki.

  Mhe.Steve Matenje,Balozi wa Malawi nchini Marekani amesisitiza kwamba Tanzania na Malawi ni nchi ndugu na zenye historia kubwa baina ya wananchi wake na kubainisha kwamba tofauti katika suala la mpaka katika Ziwa Nyasa litamalizika si muda mrefu. Balozi Matenje aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Washington Malawi Foundation iliyofanyika nyumbani kwake Potomac, Maryland.
  Balozi alimweleza hayo Bw. Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC ambaye alimwakilisha Mhe.Balozi Liberata Mulamula katika uzinduzi huo.
  Balozi Matenje aliendelea kusema kwamba anaamini udugu uliopo baina ya wananchi wa Malawi na Tanzania ndio unaompa imani kubwa kwamba suala la mpaka litapatiwa uvumbuzi wa kudumu na kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.  0 0

   
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi  nchini Mhandisi Prof.Lyatuu Mrema(kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habar i(hawapo pichani) kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini iatakayofanyika Septemba 5 na 6, 2013 jijini Dar es Salaam ambapo itwashirikisha karibu wahandisi 1000, Katika siku hiyo pia kutakuwepo na mabanda 50 ya maonyesho ya kihandisi, utoaji wa tuzo pamoja  na kula kiapo  cha Wahandisi Wataalamu. Kulia ni Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Mhandisi Steven Mlote.
  Picha na Mwanakimbo Jumaa - MAELEZO
   
   

   
   
   
   

   
   

   

  0 0

  WASHINGTON, September 4, 2013 –Children in sub-Saharan Africa are now less likely to die from diarrhea and pneumonia, but these illnesses are still the most common causes of childhood death and sickness in most African countries, according to a new report published today. 

  Loss of health due to diarrheal diseases dropped 34% between 1990 and 2010, lower respiratory infections (LRIs) such as pneumonia dropped 22%, and protein-energy malnutrition was down 17%. Several countries documented striking progress, with Malawi reducing diarrheal diseases by 65%, Burundi decreasing LRIs by 44%, and Benin reducing measles by 84% during this time. 

  Malaria and HIV/AIDS were the leading causes of premature death and disability in 2010 for the region. But in some countries, there has been significant progress in recent years. Between 2000 and 2010, Rwanda recorded a 56% decrease in the rate of healthy years of life lost from malaria, while Botswana cut the rate of premature death and disability from HIV/AIDS by 66%.

  These are some of the findings from the new report The Global Burden of Disease: Generating Evidence, Guiding Policy – Sub-Saharan Africa Regional Edition, published today by the World Bank and the Institute for Health Metrics and Evaluation (IHME). 

  “The rapid shifts in disease burden place poor people in low- and middle-income countries at high risk of not having access to appropriate services and incurring payments for health care that push them deeper into poverty,” said Timothy Evans, Director of Health, Nutrition, and Population at the World Bank Group. “The data in these new reports are critical inputs to the efforts of policymakers in countries towards universal health coverage that aim to improve the health of their people, communities, and economies.” 

  The report also finds that nutritional deficiencies were the leading cause for disability in childhood, mental and behavioral disorders accounted for the most illness during adolescence and young adulthood, while musculoskeletal disorders were the largest drivers of disability in adulthood. 

  In the region’s upper- and middle-income countries, non-communicable diseases emerged as a significant health threat. From 1990 to 2010, substantial increases in premature mortality and disability were recorded from stroke (up by 31%), depression (up by 61%), diabetes (up by 88%), and ischemic heart disease (or coronary artery disease, up by 37%). Amidst the region’s rapid economic growth, early death and illness from road injuries increased by 76% between 1990 and 2010. Health loss from interpersonal violence also climbed during this time, particularly in the Democratic Republic of the Congo and Lesotho. 

  “The health landscape in sub-Saharan Africa is changing in unexpected ways,” said Dr. Christopher Murray, IHME Director and one of the lead authors of the GBD study. “Addressing chronic disease and certain communicable diseases will continue to be important, but people in sub-Saharan Africa are dealing with a greater range of illnesses today that aren’t fatal but are definitely disabling.”

  The report also identifies trends in leading risk factors that cause the most disability in the region. Under-nutrition during childhood and household air pollution were among the leading factors behind premature death and disability. 

  Detailed findings for Sub-Saharan Africa and each country in the region are available online in a series of country profiles and data visualization tools


   Watch a live webcast on the presentation of the reports on September 4, 2013, from 10-11:30 a.m. EDT:http://live.worldbank.org/global-burden-disease-webcast.
   On Twitter, join the conversation at @worldbankhealth and @IHME_UW, or follow #GBD2010.

   0 0

   Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma mpya ya Airtel Yatosha inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, sasa kwa shilingi 499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet cha 125MB.

   Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kuboresha vifurushi vyake vya huduma ya Airtel yatosha hivyo kuvifanya kuwa bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.

   Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo , Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "huduma ya Airtel Yatosha inaendelea kutosha kuliko yoyote nchini! sasa vifurushi vya Airtel yatosha vya siku zimeendelea kuboreshwa na kuwa vya gharama nafuu zaidi, kwa shilingi 499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet cha 125MB. Bei ni poa na ya gharama nafuu ukilinganisha na huduma nyingine za vifurushi zinazotelewa sokoni"

   Bi Singano alisema Sambamba na hili vifurushi vya Airtel yatosha vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa masaa 24 na 1 la nyongeza siku saba za wiki.

   Kikubwa na kizuri zaidi mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata nafasi ya kuingia kwenye promosheni yetu kabambe ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba na kujishindia pesa taslimu au nyumba za kisasa zilizoko Kigamboni jijini Dar es saalam".

   "Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuboresha huduma zake ikiwemo Airtel money yatosha pamoja na vifurushi vya Airtel yatosha vilivyo na gharama nafuu na kukuwezesha kuwasiliana kwa gharama nafuu zaidi ndani na nje ya nchi". aliongeza mmbando.

   Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa kupiga *149*99# na kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake. Airtel yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi na vifurushi vyake vinadumu kwa masaa 25 kwa siku.

   0 0

   Kero za Tanzania ni wavuti inayokuwezesha wanajamii wa Kitanzania kutuma kero zao kwa njia ya mtandao na wahusika kuchukua hatua stahili. 


   Kumbuka, kero ni vitu vilivyo wazi kwa kila mtu hivyo usitume ripoti za siri au taarifa za kichunguzi. Sisi tunapokea KERO tu. Tuma kero yako online kwa kwenda http://kerotz.com/tuma-kero.html au kwenye email info@kerotz.com au kwenye Facebook ya KeroTz

   0 0

    Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akimpatia tiketi ya ndege na nyaraka zinginezo, Nuru Sinna ambaye ametimiza vigezo kwenda kufanya kazi Dubai, Falme za Kiarabu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam hivi karibuni. Wanaoshuhudia  ni  Jaffari Kingwande  (wa pili kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bravo Job Centre iliyofanikisha kupata kazi hiyo pamoja wengine wengi watakaokwenda siku za usoni.Wa pili kushoto ni Mohamed Omari Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo.
    Mtemvu akionesha nyaraka ikiwemo viza, vibali vya kazi pamoja na tiketi ya Nuru Sunna kwenda Dubai. Jaffari Kingwande  (wa pili kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bravo Job Centre iliyofanikisha kupata kazi hiyokufanyakazi.
    Mtemvu akizungumza katika mkuta na waandishi wa habari, Dar es Salaam, kuhusu changamoto mbalimbali ambazo anazipata katika jitihada zake za kuwatafutia kazi watanzania Falme za Kiarabu. Alisema kuwa baadhi ya maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwemo Waziri Belnald Membe wanashiriki kukwamisha jitihada hizo.

   0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Omar Yussuf Mzee,kuwa Waziri wa Fedha,katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
   Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohamed,(kushoto) Waziri Machano Omar Saidi,na Waziri Haji Faki Shaali,(hawana Wizara maalum) na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif,(kulia) wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar kushuhudia kuapishwa kwa Omar Yussuf Mzee kuwa Waziri wa Fedha, leo asubuhi.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha Omar Yussuf Mzee,baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Fedha,katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  older | 1 | .... | 246 | 247 | (Page 248) | 249 | 250 | .... | 3270 | newer