Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

Serikali Yawasilisha Muswada wa Kulitangaza Jiji la Dodoma Makao Makuu ya Nchi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo leo amwewasilisha Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi katika mkutano wa kumi na mbili wa kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Jafo amesema dhumuni la muswada huo ni kupendekeza kutungwa kwa sheria ambayo italitangaza rasmi Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Jafo amesem chimbuko la hoja ya kutunga sheria hiyo ni kukosekana kwa sheria inayotambua na kuweka misingi ya uendelezaji wa makao makuu ya nchi, hivyo hatua ya kulitambua jiji la Dodoma kama makao makuu ya nchi itachochea ukuaji wa mji wa Dodoma na maeneo yanayozunguka moka wa Dodoma kiuchumi na kijamii.

“Kukosekana kwa sheria inayotambua Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kulisababisha uendelezaji wa makao makuu ya nchi kutofikia malengo, hivyo msingi wa kutunga sheria hii ni kutambua kisheria jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi” alisema Waziri Jafo.

Akifafanua kuhusu muswada aliowasilisha mbele ya Spika Job Ndugai, waziri Jafo amesema muswada huo utakuwa na vifungu sita vikiwemo vya utangulizi, matumizi, tafsiri ya maneno yaliyotumika, kulitangaza Jiji la Dodoma kama makao makuu ya nchi na mwisho ni kifungu ambacho kimeweka masharti ya kubadilisha makao makuu ya nchi.

Uamuzi wa kuwasilisha muswada wa kulitanganza jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na serikali, ni mwendelezo wa hatua za kimageuzi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani   Jafo akiwasilisha Bungeni maelezo ya Serikali kuhusu muswaada wa sheria ya kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018( The Dodoma Capital City ( Declaration) Bill, 2018.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akisisitiza jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza akiapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job NdugaiS leo Jijini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimpongeza mbunge wa Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza mara baada ya kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job  Ndugai leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali Bungeni Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwezesha mikoa kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ili kuinua uchumi wa mikoa hiyo.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.  Dkt. Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali katika kuinua sekta ya kilimo hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene akisisitiza kuhusu faida za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi yetu leo Bungeni  Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wabunge wakifuatilia  mkutano wa 12 kikao cha kwanza cha Bunge leo Jijini Dodoma. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

MAMA AMMWAGIA MWANAYE MAFUTA YA TAA NA KUMCHOMA MOTO

$
0
0
Mtoto wa Kike mwenye umiri wa miaka  13, (Jina limehifadhiwa) ameunguzwa baada ya kumwagiwa mafuta ya taa na  kisha kuwashwa na kiberiti na mama yake mzazi.

Binti huyo amelazwa katika hosptali ya St, Joseph Mbweni katika wodi ya watoto akiwa hawezi hata kutoa maelezo  vizuri.

Akizungumza jinsi mtoto huyo alivyofikishwa hospitalini hapo, Dkt,  Valentino Francis Bangi amesema, mtoto alifikishwa hospitalini hapo alfajiri ya Agosti 31 kuamkia Septemba Mosi mwaka huu akiwa katika hali mbaya, alikuwa ameunguzwa na moto sehemu ya mbele ya  kifua na usoni.

Dkt, Bangi amesema, mtoto huyo alipofikishwa hospitalini hapo alikuwa hawezi kupumua wala kuongea, lakini walimpatia huduma ya kumuweka katika hali nzuri na kuanza kurudi katika hali ya ubinadamu .

Dkt. Bangi amesema moja ya huduma waliyoifanya ni kumuoongezea maji pamoja na kumpatia huduma nyingine ya kumfanya apumue.
‘kwa sasa hali ya mgonjwa, anaendelea vizuri tofauti na alivyokuwa kwa sababu alikuwa hawezi hata kuongea, lakini sasa hivi anazungumza ambapo amelazwa wodi ya watoto hospitalini hapa.


Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii, wa Hospitali hiyo,  Angela Isingo ambaye anashughulikia masuala ya watoto, amesema tukio hilo linasikitisha , kwani wamemuhoji  binti huyo amesema aliyemfanyia kitendo hicho ni mama yake mzazi.

Isingo amesema mtoto huyo ameeleza chanzo cha tukio hilo kwamba, “binti alirudi usiku kutoka shule, mama yake akamuuliza kibubu cha pesa kiko wapi?, kwa sababu ndani kulikuwa na vibubu viwili havionekani kwa hiyo akaenda moja kwa moja kwa huyo mtoto na kumuuliza, anasema mtoto alimjibu kuwa hafahamu kibubu kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji tena kuwa akitafute hadi akipate, akasema akazunguka akapata kibubu kimoja, na pale  ndani haishi peke yake ana baba yake na  ndugu zake wawili na dada yake mkubwa mmoja.

Akasema licha ya kumjibu mama yake kuwa hafahamu kibubu hicho kilipo, mama yake akaendelea kumuhoji kuwa, lazima aseme kibubu kilipokwenda ndiyo mama yake akachukua mafuta ya taa akamwagia na  kisha  akachukua kiberiti kumuwasha.

SERIKALI YAELEZEA MBINU ZA KUKABILIANA NA UMASKINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
akijibu maswali katika kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa inazingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala (ccm), Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na mwaka mmoja, pamoja na Mwongozo wa Bajeti kugawa rasilimali fedha na watu katika kukabiliana na changamoto za umaskini nchini.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe. Daniel Nicodemus Nsanzugwanko (CCM), aliyetaka kujua mbinu za Serikali katika kuhakikisha mikoa maskini nchini inapata rasilimali fedha na watu ili iweze kuondokana na hali hiyo ya umaskini.

Dkt. Kijaji alisema kuwa mgawanyo wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huenda sambamba na mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utekelezaji, usimamizi, uperembaji na kutoa huduma kulingana na aina ya miradi.

Aidha Mhe. Nsanzugwanko alihoji hatua zilizochukuliwa na Serikali katika Mkoa wa Kigoma ili kujenga ulinganifu katika maendeleo.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema Serikali imebainisha  maeneo na miradi ya kimkakati kwa ajili ya utekelezaji ili kufungua fursa za kiuchumi  mkoani huo.

Alieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya kimkakati yaliyobainishwa na kuanza kutekelezwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 ni pamoja na mradi wa upanuzi na ujenzi wa Uwanja wa Ndege Kigoma.

“Miradi mingine ni mradi wa uzalishaji wa umeme wa maji katika maporomoko ya mto Malagarasi MW 44.7, kuanzisha na kuendeleza eneo huru la uwekezaji Kigoma, mradi wa gridi ya Kaskazini Magharibi kv400 na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali jingine, Mhe. Nswanzugwanko alitaka kujua kwa nini Serikali isitenge shilingi bilioni 5 kila mwaka kwa kila mkoa ili kuondoa tishio la mikoa hiyo kuachwa nyuma kimaendeleo.

Mhe. Dkt. Kijaji alieleza kuwa kwa sasa Serikali haina sera wala mwongozo wa kutenga shilingi bilioni 5 kila mwaka kwa kila mkoa ili kukabiliana na changamoto za umasikini.

Alifafanua kuwa hoja ya kutenga shilingi bilioni 5 kwa kila mkoa kila mwaka ni lazima ifungamanishwe na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala. 

DKT MENGI ATEULIWA KUWA MLEZI WA SERENGETI BOYS

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF)leo Jumanne Septemba 4,2018 limemtangaza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi kuwa mlezi wa timu ya Taifa ya Vijana U17 "Serengeti Boys"

Dkt Mengi amekuwa akiifuatilia kwa karibu timu hiyo na amekuwa mmoja wa wadau wakubwa wa soka la Vijana.  Akiwa 

ni mpenda maendeleo ya mpira wa Miguu hususani soka la Vijana na amekuwa shabiki mkubwa wa Serengeti Boys.

TFF tunaamini tutashirikiana vizuri na Dkt  Mengi katika maendeleo na ustawi wa soka la Vijana na ni mwanamichezo ambaye hakika amekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuendeleza soka la Vijana. 

Mara kadhaa amekuwa akiwasiliana na TFF kufuatilia maendeleo ya timu ya Taifa ya U17 kwenye mashindano mbalimbali. 

TFF wamefarijika kwa Dkt Mengi kukubali kuwa mlezi wa timu hii ya Serengeti Boys na wanaamini kwa pamoja wataifanya timu hii kuwa msingi mzuri katika maendeleo ya ustawi wa soka la Vijana. 


Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Ndugu Reginald Mengi .

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA BARABARA YA NYAMUSWA-BUNDA-KISORYA-NANSIO , AHUTUBIA WANANCHI WA NANSIO UKEREWE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshika mkasi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kisorya kabla ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Ualimu Murutunguru kilichopo Nasio Ukerewe mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati akipokuwa akisikiliza maelezo ya mradi wa maji wa Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ukerewe mara baada ya kuwasili akitokea Kisorya mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara Barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisorya-Nansio km 121 katika sehemu ya Barabara ya Bulamba Kisorya km 51 katika sherehe zilizofanyika Kisorya Bunda mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakati akitoka kukagua pampu za kusukuma maji katika mradi wa maji uliopo Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.PICHA NA IKULU


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Maafisa waendeshaji wawili wa Kampuni ya Majembe wapandishwa Kizimbani

$
0
0
Maafisa waendeshaji wawili wa Kampuni ya Udalali ya Majembe,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 4, 2018 wakikabiliwa na shtaka la kujifanya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

 Wakili wa Serikali Christopher Msigwa amewataja washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega kuwa ni Mussa Kanena (39) na Malaki Malima (40).

Akisoma hati ya mashtaka, Msigwa amedai Machi 19, 2018 jijini  Dar es Salaam, washtakiwa kwa nia ya kudanganya walijifanya kuwa ni watumishi wa umma walioajiriwa na  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wakijua kuwa si kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wote wawili wamekana kutenda kosa na ni  mshtakiwa Malaki pekee aliyefanikiwa kukamilisha masharti ya dhamana, ila ametakiwa kuwasilisha hati ya kiapo itakayotambulisha majina yake ya Mark Malaki Malima na Malaki Malima kufuatia mdhamini wake kuwasilisha barua ya dhamana iliyokuwa na jina la Mark Malaki Malima huku katika hati ya mashtaka ikiionyesha Malaki Malima.

Mshtakiwa alipoulizwa juu ya majina hayo alidai yote ni majina yake hivyo ametakiwa kupeleka hati ya kiapo kuonyesha hayo yote ni majina yake.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo, bado haujakamilika.

Mshtakiwa Mussa amepelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana.

Katika masharti ya dhamana, washtakiwa waliamuriwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoka atakayesaini bondi ya Sh milioni 2.

Kesi imeahirishwa hadi Septemba 18,mwaka huu.

Article 0


BUNDESLIGA YAWA MOTO, LIVE KWA KISWAHILI KUPITIA STARTIMES

$
0
0
MSIMU wa Bundesliga kwa Kiswazi umeanza rasmi ikiwa ligi yenye kasi na maarufu kwa kuzalisha wachezaji Vijana wenye vipaji. Kwa mara nyingine Kampuni ya Star Media   imewaletea wateja wao msimu mpya wa Bundesliga wakiwa na  matarajio  makubwa sana kwa timu zote hivyo wateja wao  watafurahia.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja masoko wa Startimes David Malisa kuhusiana  kurejea kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga msimu wa 2018/19 amesema kuwa  ligi hiyo ya Ujerumani ni miongoni mwa ligi kubwa na bora kabisa barani ulaya, ikiwa na wachezaji mahiri kama mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Lewandowski, Marco Reus, mjamaica Leon Bailey na wengine wengi. Katika msimu huu wa 2018/19 StarTimes imezidi kuinogesha Bundesliga kwani itakuwa ikitangazwa kwa lugha ya. Kiswahili.

“Ikumbukwe kwamba StarTimes pekee ndio tunaonyesha ligi ya Bundesliga na sasa burudani inaongezeka maradufu kwa sababu mechi zitatangazwa kwa lugha yetu ya nyumbani yaani Kiswahili, na wachambuzi makini kabisa wenye weledi katika soka la ulaya. Pia mechi zote zitakuwa zikipatikana kwa kiwango cha HD kwenye chaneli zetu za Michezo”. Ameeleza Malisa. David Malisa, Meneja Masoko.
Meneja masoko wa Startimes David Malisa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kurejea kwa msimu wa pili wa kutazama kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga 2018/19 kupitia king'amuzi cha Startimes. kulia ni Meneja Maudhui wa StarTimes,  Zamaradi Nzowa.
Meneja Maudhui wa StarTimes,  Zamaradi Nzowa akizungumza na waandihsi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa kutazama kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga 2018/19  katika ofisi za kampuni hiyo leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga Abduli – Aziz Abubakari Chende "Dogo janja" akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na ligi hiyo. Kushoto ni Meneja masoko wa Startimes David Malisa.

ZAIDI YA WANAFUNZI 6000 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU DARASA LA SABA MKURANGA

$
0
0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mhadisi Mshamu Munde akizungumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii leo kuhusu wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba unaoanza kesho Jumatano 5-6 Septemba wasimamiee kwa weledi na wanafuzi wafanye kwa waminifu.

Mitihani ya taifa ya darasa la saba inatarajiwa kuanza kesho nchini kote hivyo walimu wameombwa kusimamia mitihani hiyo vizuri na wale watakaokiuka sheria za usimamizi wa mitihani hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao huku zaidi wanafunzi 6000 watafanya mtihani huo.

Akizungumza Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema kesho wanafunzi wa darasa la saba nchi  nzima wanafanya mtihani wao wa mwisho kwahiyo amewaomba walimu wanaosimamia mitihani hii wafanye kazi yao kwa uadilifu na kufuata sheria muache udanganyifu.

Aidha amewataka wanafunzi kuwa watulivu katika pindi chote cha mitihani ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao hiyo nakuiletea sifa wilaya ya Mkuranga."Mwaka Jana Mkuranga tulishika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Pwani naamini tunaweza pia kuwa wa kwanza kitaifa kama wanafunza watatumia nafasi ya kesho kufanya mitihani vizuri"alisema Abeid

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa halmashauri hiyo imejiandaa vizuri kwani mpaka sasa vifaa vyote vinavyohusiana na mitihani vimeshakamilika."mandalizi ya mitihani yanahusisha vifaa vya mitihani,na mafunzo kwa wasimamizi wote wa mitihani vyote vimakailika ikiwemo masurufu,usambazaji wa mitihani na magari"alisema

Alisema kuwa zoezi hilo ni la kitaifa na serikali imewekeza fedha nyigi kwahiyo anawasihi wasimamizi wawe waadilifu wasijihusishe na vitendo vya udanganyifu wataitia serikali hasara kwa sababu imetumia pesa nyingi na kutoa rai kwao wafanye kazi kwa weledi.

Aidha alitoa wito kwa wanafunzi kufanya mitihani yao kwa uaminifu mkubwa wadifanye udanganyifu wa aina yeyote ile kwani utawaletea hasara kubwa

Hata hivyo zaidi ya wanafunzi 6000 wilayani mkuranga wanatarajiwa kuanzà mitihani wao wa mwisho wa kumaliza Elimu ya msingi hapo kesho

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE SEPTEMBA 04, 2018

Tanzia: Mtafiti bingwa wa afya ya mama na mtoto Dr. Mbaruku aaga dunia

$
0
0
Mkurugenzi na wafanyakazi wa Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) wanasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao DK. Godfrey Mbaruku kilichotokea ghafla siku ya tarehe 2 Septemba 2018 nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. Mpaka mauti yanamfika Dr. Mbaruku alikuwa Mtafiti Mkuu kwenye miradi. Dr. Mbaruku aliwahi kuwa Naibu Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Afya Ifakara kati ya 2009 na 2015.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani na mazishi yanatarajia kufanyika Dares Salaam siku ya Jumatano tarehe 5/09/2018 katika Makaburi ya Kinondoni.

Uongozi wa Taasisi ya Afya Ifakara unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, wafanyakazi na wadau mbali mbali wa afya kwa msiba huu mkubwa.

IMETOLEWA NA IDARA YA RASILIMALI WATU
TAASISI YA AFYA IFAKARA
MIKOCHENI, DAR ES SALAAM
Septemba 4, 2018

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 5, 2018

PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA.

$
0
0
SHIRIKA la ndege la Kitanzania Precision Air limedhamiria kuanzisha safari za kwenda Chato na makao makuu ya nchi mkoani Dodoma. Shirika hilo lenye miaka 25 tangia kuanzishwa kwake kwa sasa linafanya safari za ndani zipatazo kumi. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Meneja Masoko na Mawasiliano Hillary Mremi amesema, Precision Air imegundua kuna fursa ya kutanua soko lake kupitia safari hizo za Chato na Dodoma na kwamba tayari wameshaanza mchakato wa kutathimini masoko hayo ili kuandaa safari zitakazo kidhi mahitaji ya maeneo hayo. 

“Kumekuwa na matukio muhimu katika maeneo haya, kwa upande mmoja na  hatua ya Serekali kuhamia Dodoma ni dhahiri itaongeza safari za watu kwenda na kutoka Dodoma. Precision Air kama shirika linalongoza kwa kuwa na mtandao bora wa safari na Shirika pekee la Ndege ambalo ni mwanachama wa IATA nchini Tanzania tumedhamiria kuanzisha safari za Dodoma ili kuwawezesha wateja wetu wanosafiri kupitia mtandao wetu mpana wa safari kuunganisha safari zao kwenda Dodoma," ameeleza Mremi. 

Akiongelea dhamira ya Precision Air kuanzisha safari za Chato, Mremi amesema ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Chato umefungua milango kwa Precision Air kujitanua zaidi katika ukanda wa Ziwa.  Huku safari za Chato zitalenga kuhudumia mkoa wa Geita ambao una shughuli mbali mbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Uchimbaji wa madini, Uvuvi na Utalii.

“Tunapenda kuipongeza serekali yetu kwa jitihada zake za za kuboresha viwanja vyetu vya ndege, jambo ambalo litatuwezesha sisi watoa huduma kuanzisha safari nyingi zaidi ambazo zitaifungua nchi na kuongeza kasi ya maendeleo. Mipango yetu ni kuanzisha safari zetu za Chato na Dodoma katika majira ya joto mwaka 2019," amefafanua Bw.Mremi. 

Precision Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi,Shirika la ndege la Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika ya ndege ya nayoheshimika Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani na nje kuelekea sehemu takribani 11. Ikitokea Dar es Salaam (makao makuu) Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kahama, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar, Seronera,Nairobi na Entebbe

RC ALLY HAPI:MAJENGO YA UWANJA WA NDEGE WA NDULI YANAHARIBU TASWIRA YA KUIJENGA IRINGA MPYA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile alipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa Nduli kwa kufahamu maendeleo ya ukarabati mdogo wa uwanja huo na kubaini baadahi ya changamoto zinaukabili uwanja huo hasa katika swala la majengo kuto kidhi mahitaji ya wasafiri 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa kwenye eneo ambalo linafanyiwa ukarabati mdogo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa ndani katika sehemu ya abiri ambao wanasubiri kusafiri. 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MKUU wa mkoa wa Iringa Ally Hapi hajaridhishwa na hali halisi ya uwanja wa ndege wa nduli uliopo kata ya nduli kuelekea kuijenga Iringa mpya kwa maendeleo ya wanairinga.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ukarabati mdogo unaoendelea katika uwanja huo,hapi alisema kuwa uwanja huo wa ndege unahitaji ukarabati wa maana ili kukidhi mahitaji ya watumiaji na kukuza maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa.

“Nimetembea kwenye maeneo mengi ya uwanja huu hayaridhi wala hayavutii kwa wawekezaji kuja mkoani hapa kwa kuwa saizi wawekezaji wengi wanapenda kutumia usafiri wa anga hivyo ni lazima kuwa na kiwanja cha ndege ambacho kitakidhi na kuvutia watalii na wawekezaji wanapokuja mkoani hapa” alisema Hapi

Hapi alisema kuwa jengo la wageni la uwanja huo ni dogo,halina ubora unaotakiwa na halikidhi kuwa katika uwanja huo ambao hivi karibuni utaanza kupokea wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.

RAIS DKT. SHEIN AZINDUA VITUO VYA MFUMO WA KIELEKTRONI WA KUSAJILI WAKAAZI WA ZANZIBAR (E-ID CARD)

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua jengo la Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika katika Wilaya kati Mkoa wa Kusini Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo ya kifundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt. Hussein Khamis Shaaban mara baada ya uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii na Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya Dunga uliofanyika leo katika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Mfumo wa Usajili wa Kieletroniki na Ofisi za Usajili wa Vitambulisho Wilaya ya Dunga wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia hafla hiyo.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SMZ na Wafanyakazi wa Wakala wa Usajili, baada ya hafla ya uzinduzi huo, uliofanyika Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

ZAIDI YA WANAFUNZI 6000 KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU DARASA LA SABA MKURANGA

$
0
0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga,Mhadisi Mshamu Munde akizungumza na Michuzi Blog leo kuhusu wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba unaoanza kesho Jumatano 5-6 Septemba wasimamiee kwa weledi na wanafuzi wafanye kwa waminifu.

Mitihani ya taifa ya darasa la saba inatarajiwa kuanza kesho nchini kote hivyo walimu wameombwa kusimamia mitihani hiyo vizuri na wale watakaokiuka sheria za usimamizi wa mitihani hatua Kali zitachukuliwa dhidi yao huku zaidi wanafunzi 6000 watafanya mtihani huo.

Akizungumza Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Abeid amesema kesho wanafunzi wa darasa la saba nchi  nzima wanafanya mtihani wao wa mwisho kwahiyo amewaomba walimu wanaosimamia mitihani hii wafanye kazi yao kwa uadilifu na kufuata sheria muache udanganyifu.

Aidha amewataka wanafunzi kuwa watulivu katika pindi chote cha mitihani ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao hiyo nakuiletea sifa wilaya ya Mkuranga."Mwaka Jana Mkuranga tulishika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Pwani naamini tunaweza pia kuwa wa kwanza kitaifa kama wanafunza watatumia nafasi ya kesho kufanya mitihani vizuri"alisema Abeid

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa halmashauri hiyo imejiandaa vizuri kwani mpaka sasa vifaa vyote vinavyohusiana na mitihani vimeshakamilika."mandalizi ya mitihani yanahusisha vifaa vya mitihani,na mafunzo kwa wasimamizi wote wa mitihani vyote vimakailika ikiwemo masurufu,usambazaji wa mitihani na magari"alisema

Alisema kuwa zoezi hilo ni la kitaifa na serikali imewekeza fedha nyigi kwahiyo anawasihi wasimamizi wawe waadilifu wasijihusishe na vitendo vya udanganyifu wataitia serikali hasara kwa sababu imetumia pesa nyingi na kutoa rai kwao wafanye kazi kwa weledi.

Aidha alitoa wito kwa wanafunzi kufanya mitihani yao kwa uaminifu mkubwa wadifanye udanganyifu wa aina yeyote ile kwani utawaletea hasara kubwa

Hata hivyo zaidi ya wanafunzi 6000 wilayani mkuranga wanatarajiwa kuanzà mitihani wao wa mwisho wa kumaliza Elimu ya msingi hapo kesho

UMOJA WA VILABU VYA WAANDISHI WA HABARI WAMPA TUZO AZORY GWANDA

$
0
0

Jopo la majaji wa Tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2018 limemtangaza Mwandishi wa habari I wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2018.
Tuzo hiyo imetangazwa leo Jumanne Septemba 4,2018 wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.
Kushoto ni Absalom Kibanda Mhariri mkuu kutoka gazeti la. Mtanzania akikabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi 2018 kwa mke wa Azory Gwanda.Katikati ni rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo.
Mbali na kukabidhiwa tuzo hiyo,pia amekabidhiwa cheti cha utambuzi pamoja na shilingi milioni 10.

Na Seif Mangwangi,Arusha
UMOJA wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), imemtangaza Mwandishi Azory Gwanda ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba mwaka jana kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi kwa mwaka 2018.

Gwanda aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni ya mwananchi communication akiandikia gazeti la Mwananchi alipotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa katika kazi zake za kihabari katika maeneo ya Kibiti na Rufiji.

Tuzo hiyo ya Daudi Mwangosi sambamba na kiasi cha shilingi milioni kumi (10), alikabidhiwa mke wa Gwanda, katika mkutano mkuu wa mwaka wa UTPC.

Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo, Absolom Kibanda aliiomba Serikali kutofumbia macho matukio ya utekaji wa waandishi wa habari kwa kuwa yanatoa ishara mbaya kwa jamii na kuminya uhuru wa habari.

Alisema Rais Dkt John Magufuli amekuwa rafiki mkubwa wa vyombo vya habari hivyo alimtaka kutoishia kuwa rafiki na badala yake achukue hatua dhidi ya matukio ya utekwaji na kuteswa kwa waandishi wa habari.

DC PANGANI AWATAKA WASHIRIKI WA MISS TANZANIA KUTANGAZA UTALII

$
0
0
Washiriki wa Miss Tanzania 2018.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2018 kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Amesema lengo ni  kusaidia kuongeza idadi ya watalii nchini huku akiwahakikishia warembo hao Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeamua kutoa kipaumbele kwa vijana kutimiza ndoto zao.

Abdallah  ambaye ndio Mkuu wa Wilaya mwenye umri mdogo kwa wakuu wa wilaya nchini amesema hayo wilayani Muheza mkoani Tanga  baada ya kuwapokea warembo 20 wanaoshiriki shindano hilo.

Ambapo walifika mkoani Tanga kwa ajili ya kutembelea vituo vya utalii vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu nchini(TFS) ambapo amewahakikishia kwenye hifadhi hiyo kuna utalii ambao haupo mahali kokote duniani zaidi ya Misitu ya Amani.

Hivyo amesema ujio wa warembo huo ni muhimu na kuwataka wawe mabalozi wazuri wa kuutangaza utalii

"Tanzania  ina vivutio vingi sana,mfano kwa  wilaya ya Pangani tuna mbuga  Sadan ambayo ndio mbuga ambayo imepakana na bahari barani Afrika.

" Pia tuna majengo ya kale kwa kifupi Pangani haitofautiani na Zanzibar.Tujitahidi kuutangaza utalii wa ndani ili tusaidie kuleta pato la Taifa,"amefafanua.

Ameongeza kupitia utalii wa ndani warembo hao watajipambanua kwakutumka fursa zilizopo ili kujipatia fursa za ajira.

Wakati huo huo Meneja Masoko na Uwekezaji wa TFS Mariam Kobelo  ameeleza kwamba malengo ya kuwapeleka  warembo hao katika vivutio hivyo ili waone vivutio na kisha kuvitangaza vivutio.

"TFS itatumia warembo hao kama chombo cha kutangaza utalii wandani kwa upande wa mazingira,kwa kufanya hivyo watasaidia kuongeza pato kwa sbabu tutawatumia kama chombo cha kutangaza utalii wa mazingira,mito inayoteteresha maji,misitu na vinginevyo.

Warembo hao kwa wakiwa katika hifadhi ya msitu asili wa Amani wamepata nafasi ya kuelezwa vivutio vinavyopatikana na hasa vinyonga wa pembe tatu ambao wanapatikani katika hifadhi hiyo.

Kwa upande wa warembo hao wamefurahishwa kutembelea hifadhi hiyo kwani wamepata nafasi ya kushuhudia vivutio mbalimbali vya utali

Kwa kukumbusha mashindano ya Miss Tanzania yanatarajia kufanyika Septemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

SERIKALI KUUNDA KIKOSI KAZI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifungua mkutano wa wadau wa Mazingira  Jijini Arusha. Mkutano huo umeshirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali na zile zisizo za kiserikali kwa lengo la kujadili changamoto ya mimea vamizi yenye athari hapa nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akifuatilia mawasilisho ya mimea vamizi kutoka kwa Mtaalamu wa COSTECH (hayupo pichani). Kulia ni Mhe. Nape Nnauye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi na Maliasili.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa wadau wa kujadili changamoto za mimea vamizi. Mkutano umefanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha. Mstari wa mbele katika picha ni waheshimiwa wabunge waliohudhuria.


KATIKA jitahada za kupambana na mimea vamizi nchini ambayo kwa kiasi kikubwa ina athari kwa uchumi wa Nchi yetu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amewakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali, asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali, Wenyeviti wa Kamati za Bunge za Ardhi na Maliasili, Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ili kwa pamoja waweza kujadili namna bora ya kupambana na mimea vamizi ambayo imetapakaa kwa kasi katika maeneo mbalimbali hapa nchi.


“Pamoja na kwamba viumbe vamizi wageni ni janga kwa makazi asilia ya viumbe, lakini hatujalishughulikia kikamilifu, kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia na kukabiliana na viumbe hivi. Kwa muktadha huo, leo tumepata fursa adimu na adhimu kutafakari kuhusu hali ilivyo kwa sasa, changamoto zilizopo na kujadili mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo la viumbe vamizi wageni hapa nchini” Makamba alisisitiza.


Wadau waliohudhuria mkutano huo wameitaka Serikali kuongeza nguvu katika kupambana na tatizo hilo kwa kuibua miradi mbalimbali kote nchini ili kwa pamoja kuwa na mkakati wa kitaifa wa kupambana na hali hiyo ambayo ina athari kubwa kiutalii.


Mhe. Innocent Bashungwa Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira amesema kuwa suala kubwa ni kuuongeza bajeti kila mwaka katika sekta ya usimamizi wa mazingira pamoja na kuanzishwa kwa Mfuko wa Mazingira.

Viewing all 110031 articles
Browse latest View live


Latest Images