Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA NAIBU GAVANA WA JIMBO LA JIANGSU NCHINI CHINA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiang kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiang (kushoto) kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing nchini China, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Gavana wa Jimbo la Jiangsu nchini China, Bw. Guo Yuan Qiang kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika - FOCAC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TMA KUCHOCHEA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA SEKTA MBALIMBALI ZA KIUCHUMI NA KIJAMII

0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeandaa mkutano wa wadau mbalimbali kwa ajili ya msimu wa mvua za Vuli (Oktoba hadi Desemba, 2018) ambao unalenga kupata maoni ya wadau jinsi utabiri wa Msimu wa Mvua za Vuli utakavyoweza kutumika katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushirikishwaji wa Wadau Katika Kuchochea Matumizi Ya Taarifa Za Hali Ya Hewa”.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Agnes Kijazi alisema kuwa lengo kubwa la mkutano huo ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii hapa nchini.

‘lengo kubwa la mkutano huu kama ilivyo katika kauli mbiu ni kuchochea matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, ambapo katika mkutano huu, mtapata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa wa msimu wa Oktoba hadi Disemba, 2018 na hivyo kuwa na majadiliano yenye lengo la kuchangia juu ya athari zitakazopatikana katika sekta zenu kutokana na utabiri huo na hatimaye kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari hizo’. Alisema Dkt.Kijazi. 

Aidha aliongezea kuwa mkutano huo ni sehemu ya kubadilishana uzoefu kati ya wataalamu wa TMA, Sekta mbalimbali na Washirika wa Maendeleo hivyo basi ni sehemu muhimu ya ushirikishwaji wa wadau katika kujenga na kuimarisha utoaji na matumizi ya huduma za hali ya hewa katika jamii akisisitiza kuwa kauli mbiu imechaguliwa ili kuakisi jitihada za Mamlaka katika uandaaji na utoaji wa huduma shirikishi. 

MANDHARI YA TASWIRA KUTOKA JIJINI BEIJING,CHINA

0
0

 Kwa mujibu wa wenyeji wanaeleza kuwa hili ndilo jengo refu zaidi kuliko yote jijini Beijing,lina ghorofa 108.
Mandhari tulivu  ndani ya mtaa  wa Xinyuanxili middle street,Chaoyang  jijini Beijing,utunzaji wa mazingira na usafi katikati ya mji ni wa hali ya juu kabisa.Picha na Michuzi Jr-Beijing.

MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI WA KILIMO WA CHINA

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu wakati alipotembelea Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo iliyopo Beijing Septemba 3, 2018. Majaliwa yupo nchini China kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Afrika na China – FOCAC



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu (kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo iliyopo Beijing, Septemba 3, 2018.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu wakishuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano katika masuala ya Uvuvi kati ya China na Tanzania kwenye ukumbi wa Wizara ya Kilimo ya China katika jiji la Beijing, Septemba 3, 2018. Wanaotia Saini ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (kushoto) na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Chanfu (wanne kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa wizara hiyo jijini Beijing, Septemba 3, 2018. Wengine pichani ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Rashid Ali Juma. (wapili kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (watatu kushoto), Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki na Naiba Waziri wa Kilimo wa China, Qu Dongyu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiagana na viongozi wa Wizara ya Kilimo ya China baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo, Beijing nchini China, Septemba 3, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKONGORO NYERERE AWATAKA WAKAZI WA ZAVARA KUMCHAGUA WAITARA

0
0
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Kupitia Chama Cha Mapinduzi Mwita Waitara akizungumza na wakazi wa kata ya Buyuni wakati wa Mkutano wake kampeni wa kuomba kura kwa wakazi wa Mtaa wa Zavara.
 Wabunge wa Bunge Jamhuri la Muungano kwa Tiketi ya CCM Wakicheza kwa furaha wakati wa mkutano wa kampeni


Wakazi wa Mtaa wa zavara waliojitokeza katika Mkutano wa kampeni kumsikiliza Mwita Waitara.

Mradi wa umeme wa Makambako - Songea wakamilika

0
0
 Zaidi ya shilingi bilioni 9.1 za mafuta mazito kuokolewa.
Na Zuena Msuya, Njombe
Waziri wa Nishati,  Dkt. Medard Kalemani, amesema kuwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya kV220  kutoka Mji mdogo wa Makambako mkoani Njombe hadi Songea mkoani Ruvuma umekamilika na utazinduliwa muda wowote kuanzia sasa.

Dkt. Kalemani alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi huo katika Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe, ambapo aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). 

Dkt. Kalemani alisema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaokoa zaidi ya shilingi bilioni 9.1 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa kununua mafuta mazito yaliyokuwa yakitumika kuzalisha umeme katika Mikoa ya Njombe, Ruvuma na Wilaya 8 zilizokuwa hazina umeme wa Gridi ya Taifa.

“ Kukamilika kwa mradi huu ambao ulianza mwaka 2016, kutaondoa adha na gharama ya kutumia mafuta mazito katika kuzalisha umeme kwa maeneo yaliyokosa umeme wa gridi ya taifa kwa miaka mingi ukiwemo Mkoa wa Ruvuma,”  alisema Dkt. Kalemani.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akizungumza na mkandarasi anayejenga miundombinu ya kusambaza umeme  kwa wananchi kupitia mradi wa Makambako hadi Songea, (kushoto) ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikagua mradi wa njia ya kusambaza umeme kutoka Makambako hadi Songea.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa njia  ya kusambaza umeme kutoka Makambako hadi Songea, wakati akikagua utekelezaji wa mradi huo ambao tayari umekamilika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO

0
0
 Balozi Seif akionyesha mshangao wake kutokana na  baadhi ya Mashine  nzima kutofanya kazi kutokana na ukosefu wa Wahandisi wa kuziendesha kwa sababu za kustaafu na wengine kufariki Dunia.
 Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali Ndugu Yussuf  Kulia Masururu akimkaguza sehemu mbali mbali balozi Seif kujionea hali halisi ya Mazingira ya Karakana hiyo. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mihayo Juma N’hunga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akiangalia baadhi ya vitengo vya Karakana Kuu ya Serikali iliyopo Chumbuni alipofanya ziara ya ghafla kwenye Taasisi hiyo ya Uhandisi.Aliyepo Kulia ni Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali Ndugu Yussuf  Masururu na nyuma ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mh. Mohamed Ahmed Salum.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameukumbusha Uongozi wa Karakana Kuu ya Serikali kuandaa mapendekezo yatakayotoa mwanga wa kuifufua Karakana hiyo ili itoe huduma imara zilizokusudiwa kutokana na uwepo wa azma ya kujengwa kwake.

Alisema mapendekezo hayo ambayo tayari alikwisha yaagiza kwa Uongozi huo kufuatia ziara yake aliyoifanya kwenye Karakana hiyo karibu Miaka Mitano iliyopita ni vyema yakaainisha vyema mpango Mkuu wa muda mfupi wa kati na mrefu.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Karakana hiyo iliyopo Chumbuni kuangalia uhalisia  wa mazingira halisi ya uwajibikaji wa Watendaji wake na changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

TUNAHITAJI WAWEKEZAJI KWENYE MAZAO YA KILIMO, SAMAKI NA MIFUGO-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji wawekezaji wakubwa kutoka China ambao watawekeza kwenye viwanda vya mazao ya kilimo, samaki na mifugo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu, Septemba 03 ,2018) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa China, Bw. Han Changfu, jijini Beijing.

Alisema  katika kipindi hiki ambacho Tanzania imeamua kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda, China ni nchi sahihi kushirikiana nayo kwa sababu inawawekezaji wa kutosha.

“China ni rafiki yetu na pia imepiga hatua kubwa kwenye teknolojia ya viwanda, hivyo tunahitaji kuendelea kushirikiana nayo ili tuweze kupata na teknolojia sahihi ya viwanda mbalimbali.”

Waziri Mkuu alisema Serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziko tayari wakati wowote kuwapokea wawekezaji kutoka China.

Alisema wawekezaji hao watapatiwa ardhi ya kujenga  viwanda ambavyo vitatumia mazao ya kilimo, mifugo na bahari hasa samaki  ambayo mengi yanapatikana kwa wingi nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Tanzania inahitaji kupata soko la mbaazi na soya nchini China ili kuwawezesha wakulima wake kuwa na soko la uhakika la mazao hayo.

Alisema Tanzania hivi sasa inakabiliwa  na tatizo la ukosefu wa soko la mazao hayo, baada ya wakulima kuitikia wito wa Serikali  wa kuwataka walime mazao hayo kwa ajili chakula na biashara.

“Tumelazimika kutafuta masoko ya mazao hayo hapa China ili kutowakatisha tamaa wakulima wetu kwani itakuwa vigumu kwao kuendelea kulima mazao hayo kwa wingi bila ya kuwa na uhakika wa soko.”

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo wa China alisema nchi yake iko tayari kutoa elimu na mafunzo kwa Watanzania hasa kwa kuandaa semina zitakazowawezesha washiriki kuongeza ujuzi wao, hatua ambayo itawasaidia Maafisa Ugani wetu kufanya kazi zao vizuri zaidi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA

0
0
NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA
JUMLA ya watahiniwa 35,430 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unaonza kesho mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Sussan Nusu wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema kuwa mtihani huo utakaofanyika kwa siku mbili mfululizo na kuongeza kuwa kati ya watahiniwa hao watoto wa kiume ni 16,706 na watoto wa kike ni 18,724.

Nusu alisema jumla ya watoto 34,762 ni kutoka shule Serikali za kawaida ambapo wanafunzi wa kiume ni 16,359 na wasichana 18,403 na wanafunzi kutoka shule zinazofundisha kwa lugha ya Kiingereza ni watoto 651.

Alisema jumla ya wanafunzi 17 wenye mahitaji maaluma ikiwa ni wenye uoni hafifu 10 na wasioona kabisa saba nao wanatarajia kufanya mtihani humo.

Afisa Elimu huyo wa Mkoa alisema maandalizi zoezi hilo yamekamilika na vifaa vyote muhimu vimeshafikishwa katika maeneo husika na wasimamizi wanatakiwa kupelekwa katika vituo walivyopangiwa.

Nusu aliwataka Wasimamizi wote Mkoani hapa kuwa makini na kuzingatia uaadilifu wakati wote wa usimamizi wa mitihani na kuongeza kuwa ni vema wazingatie maelekezo yote waliopewa wakati wa semina.

Kwa upande wa wazazi aliwataka kuhakikisha wanakaa na watoto wao na kuwapa maneneo ambayo yatawapa moyo ili waweze kufanya mitihani yao kwa kuniamini na kutumia mafunzo yote waliopatiwa

Alisema wazazi pia wanalo jukumu la kuhakikisha watoto wao wote waliosajiliwa kufanya mitihani isipokuwa kwa wale wenye kibali cha Daktari.

Nusu alisema kuwa hadi kufikia leo ni mtoto moja kutoka Urambo mkoani humo ambaye hataweza kufanya mitihani kwa sababu ni mgonjwa na Daktari amesema apumzike.

Kuhusu watoto aliwataka kujiamini kwani mtihani wanaoenda kufanya ni sawa na ile ambayo wamekuwa wakifanya kama vile ya utimilifu na inayoandaliwa na walimu wao.

Watoto wanaomaliza mwaka huu mkoani Tabora waliandikishwa kuanza Darasa la Kwanza mwaka 2012 wakiwa 41,789 ikiwa ni wavulana 21,898 na wasichana 19,600.

MBILINYI ANG'AKA KUPAKAZIWA ASISITIZA ANACHEZA TAIFA SEPTEMBA 15

0
0
Na Mwandishi Wetu
BONDIA machachali nchini Vicent Mbilinyi anatarajia kupanda ulingoni Septemba 15 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa kuzipiga na Saidi Kidedea mpambano wa raundi 6 ambambo watakuwa wakisindikiza mpambano wa Fred Sayuni na Haidari Mchanjo

akizungumzia mpambano uho Mbilinyi amesema amejiandaa vya kutosha hivyo wamewataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi na maandalizi yake kwani yupo vizuri kila idara na anachotaka yeye ni ushindi wa K.O ya mapema ili asiwasumbuwe majaji watakaokuwepo siku hiyo

aliendelea kwa kusema kumeibuka n mapromota matapeli ambao wametengeneza mabango na kuweka picha yangu mimi na Cosmas Cheka kuwa nacheza siku hiyo mimi kama mimi ni bondia ninae jijua waeamuwa kunipaka matope na kuaribiana tu mimi sina mpambano na Cheka pambano ninalolijua mimi ni la taifa ninacheza na Saidi Kidedea ambapo nimesaini kwa Super D Boxing Promotion ambao ndio nimesaini nao kwa sasa

nae mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion iliyo jizatiti kuendeleza shughuli za mipambano ya masumbwi nchini alisema mbali na pambano hilo rinalosubiliwa na mshabiki lukuki siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atakumbana na George Dimoso wakati Mohamedi Kashinde ata vaana na Sadiki Momba na Issa Nampepeche atakabiliana na Faraji Sayuni na Bakari Mbede atakutana uso kwa uso na Frenk John

mapambano hayo yote na mengine yataanza saa 12 jioni yani itakuwa mapema ili ngumi hizo ziishe kwa wakati uliopangwa 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini

KONDO ATUHUMIWA KUMUUA MKEWE KISA KUCHAT NA SIMU-RPC WANKYO

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
JESHI la polisi Mkoani Pwani ,limefanikiwa kumkamata Salum Mzee Kondo (38),fundi ujenzi mkazi waKidongoChekundu ,Bagamoyo aliyehusika na tukio la mauaji ya mkewe Mwajuma Omary (27) kisha kutoroka baada ya kutenda kosa hilo.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa septemba 2 mwaka huu ,Yombo Buza jijini Dar es salaam ambako alikimbilia baada ya kufanya kitendo hicho Agosti 31 2018, saa 9 alasiri huko Kidongochekundu.

Akiweka bayana kuhusiana na tukio hilo kwa waandishi wa habari ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema, mtuhumiwa alipokamatwa alikiri kutenda kosa hilo ,na kudai alichukua hatua hiyo kutokana na wivu wa kimapenzi .

Alieleza kwamba , mkewe alikuwa akichat na simu huku akiwa anacheka mwenyewe ndipo alipoamua kumnyang'anya simu na kukuta message alizokuwa akichat na mwanaume mwingine .

"Jambo hilo lilisababisha mgogoro kati yao ,ambao ulisuluhishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Magomeni B, lakini marehemu alishikilia kuchoshwa kuishi na mumewe huyo na kuomba kupewa talaka na mumewe aligoma kutoa talaka " alifafanua Nyigesa .

Pamoja na hilo ,Nyigesa alisema wawili hao walikuwa na mgogoro mwingine, uliotokana na mtuhumiwa kuchukua ATM Card ya marehemu mkewe na kwenda kutoa sh.50,000 bila ridhaa yake.

Alibainisha ,jambo hilo lilimsababisha marehemu mkewe kuondoka nyumbani wanakoishi na kwenda kuishi kwa baba yake mdogo.

Kamanda huyo alieleza ,ilipofika tarehe 31 agost mwaka huu alimpigia simu mumewe kuhitaji fedha zake hizo ambapo mumewe alimwambia aende nyumbani kwao akachukue na mkewe huyo (marehemu)aliendelea kushikilia kutaka fedha zake na talaka ndipo mtuhumiwa kwa hasira alimkaba na kumsababisha kifo .

Baada ya kutenda kosa hilo mtuhumiwa alimfunika marehemu kwa shuka ndani ya chumba walichokuwa wakiishi na kuacha ujumbe kuwa ameua kutokana na wivu wa kimapenzi .

Kwa mujibu wa Nyigesa ,Ujumbe huo uliendelea kueleza ,mtuhumiwa nae anaenda kujiua hivyo mali zote walizoacha ni za watoto wawili waliozaa na marehemu .

JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LAMKAMATA FUNDI NA MMILIKI WA KIWANDA KIDOGO CHA KUTENGENEZA SILAHA HARAMU

0
0
NA  TIGANYA VINCENT RS TABORA.
JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamsikilia mkazi wa kijiji cha Kinamagi Kata ya Kigwa wilayani Uyui Mrisho Juma (44) kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha Kutengeneza silaha za kienyeji  aina ya Gobore.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Emmanuel Nley imesema kuwa Juma alikamatwa Septemba 02 mwaka huu  nyumbani kwake akiendelea na utengenezaji wa silaha hizo.

Kamanda Nley alisema kuwa mtuhumiwa alikutwa na gobore tatu akiendelea kuzitengeneza pamoja na bastola moja ikiwa imekamilika.

Alisema kuwa hata watuhumiwa ambao wamekuwa wakimatwa na gobore wamekuwa wakidai kununua kwake na ndipo Jeshi la Polisi liliweka mtego na kumukamata Kwa mujibu wa Kamanda  Nley baada ya kumhoji mtuhumiwa alikiri  kuwa ndiye mtengenezaji wa silaha hizo na uziuza maeneo mbali mbali mkoani hapa.

Kufuatia tukio hilo Kamanda wa Polisi ametoa wito kwa wananchi ambao wanamiliki silaha bila kufuata utaratibu wajisalimishe kabla hatua kali dhidi yao hajachukuliwa.

Wakati huo huo Kamanda huyo amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwashikilia Askari Polisi kumi(10) wa Wilaya ya Igunga wakihusishwa na kifo cha Selemani Jumapili  waliyekuwa wamemkamata kwa mahojiano.

Nley amesema kuwa Wataalamu kutoka Makao Makuu wa Jeshi hilo wanaendelea na mahojiano na askari hao na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu Jumapili ulifanyiwa uchunguzi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora na taarifa ya matokeo itatolewa Mahakamani.

Alisema Jumapili alikamatwa na Polisi hao waliokuwa katika misako Agosti 29 saa nane mchana  na baadaye akiwa katika Kituo cha Polisi alionekana mgonjwa na kukimbizwa Hospitali na ilipofika saa tano usiku alifariki wakati akipata matibabu kwenye hosptali ya wilaya Igunga alipokuwa akipata matibabu.

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

0
0

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Wankyo Nyigesa ,akionyesha moja ya gari iliyoharibika vibaya,katika ajali iliyohusisha magari mawili ambayo yamegongana uso kwa uso, barabara ya Dar es salaam-Morogoro eneo la Mbala ,Chalinze Mkoani Pwani,na kusababisha vifo vya watu wawili.
(picha na Mwamvua Mwinyi)

NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
WATU wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa ,katika ajali iliyohusisha magari mawili ambayo yamegongana uso kwa uso huko barabara ya Dar es salaam -Morogoro eneo la Mbala ,Chalinze Mkoani Pwani .

Akielezea kuhusiana na ajali hiyo ,kamanda wa polisi mkoani humo ,(ACP) Wankyo Nyigesa alisema, imetokea usiku wa kuamkia septemba 4 majira ya saa 9.30 alfajiri.

Alisema gari namba T.542 DMJ/ 680 DKS aina ya Howo mali ya kampuni ya Gulf Agent ikitoka Dar es salaam kuelekea Chalinze ikiendeshwa na dereva Ramadhani Kibingo ( 38) mkazi wa Mbagala iligongana na gari T.405 DLV/ 904 DMN aina ya Daf mali ya kampuni ya RAS Logistic (T) ltd iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Dsm ikiendeshwa na dereva bado kufahamika jina lake (35-40).

"Ajali hii imesababisha vifo vya dereva huyo aliyekuwa akiendesha gari yenye namba T.405 DLV/904 DMN aina ya Daf na tingo wake ambao bado nae kufahamika jina, mme ( 25 - 30 )" alisema Wankyo.

Wankyo aliwataja majeruhi kuwa ni dereva  Ramadhani Kibingo na tingo wake Ibrahim Said, Mzigua (28), mkazi wa Dar es salaam waliokuwa ndani ya gari T.542DMJ/680 DKS. 

Kwa mujibu wa kamanda huyo ,magari yote yameharibika kutokana na ajali hiyo iliyotokea.

Alisema ,miili ya marehemu imepelekwa hospital ya rufaa Tumbi kwa uchunguzi na kuhifadhiwa na majeruhi wamepelekwa kituoa cha afya Chalinze kwa ajili ya matibabu na hali zao sio mbaya. 

Dereva wa gari T.542 DMS/680 DKS aina ya Howo ,anashikiliwa chini ya ulinzi wa polisi kituo cha afya Chalinze. 

Chanzo cha ajali ni dereva huyo ambae anadaiwa alijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhali na kugongana uso kwa uso na gari T.504 DLV/904 DMN aina ya Daf.


Wakati huo huo ,Wankyo alikemea ,madereva ambao sio makini na wanaoendesha bila tahadhali na kusema sheria itachukua mkondo wake kwa Dereva anaekiuka sheria za usalama barabarani .

Serikali Kujenga Kingo Maeneo Yanayozungukwa na Maji

0
0
 Na Lilian Lundo, MAELEZO - Dodoma. 
SERIKALI ya Awamu ya Tano kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira imeanzisha miradi ya kujenga kingo katika maeneo yanayozungukwa na maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba jana  katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) na kuratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO).

"Ujenzi wa kingo katika Bahari ya Hindi kumesaidia bahari kutoichukua barabara kwa zaidi ya miaka 70 ijayo," alisema Makamba.

Aidha, Makamaba amesemawameanzisha mifumo mbalimba itakayowezesha kukagua viwanda na kuwaelekeza wenye viwanda juu ya utunzaji wa mazingira ikiwemo kuongeza idadi ya wakaguzi wa mazingira.
 
Amesema, kitu kikubwa ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inajivunia ni kuondoa viroba nchini kwani vilikuwa vikichafua mazingira kwa kiasi kikubwa. Vile vile imeteua wakaguzi wa mazingira ambao watahakikisha wanazuia matishio ya mazingira yanayotokea mara kwa mara.

Makamba amesema, ushirikiano wa Zanzibar na Tanzania Bara haupo tu katika sekta za kimuungano bali zinashirikiana vizuri hata katika sekta zisizo za Muungano

Hata hivyo, Ofisi ya Makamu wa Rais  ipo katika hatua ya mwisho ya kuifanyia mapitio Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 1997 kutokana na sera hiyo kupitwa na wakati, hivyo iweze kujumuisha changamoto mpya zilizojitokeza  ikiwa ni pamoja na ongezeko la kemikali za sumu taka zinazotokana na vifaa vya kie-elekroniki, masuala ya matumizi ya bioteknolojia ya kisasa, mabadiliko ya tabia nchi, viumbe vamizi na masuala ya biofueli.

PROF.MKUMBO AWATAKA WANASHERIA KUSIMAMIA SHERIA WANAZOZIWEKA

0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akiwa pamoja na washiriki wote wa mkutano wa wanasheria wa Sekta ya Maji.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na wanasheria wa Sekta ya Maji (hawamo pichani), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Simon Nkanyemka (kulia) na Mwenyekiti wa kikao hicho, Bernadetha Mkandya kutoka DAWASA.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Simon Nkanyemka akizungumza, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (katikati) na Mwenyekiti wa Kikao hicho, Bernadetha Mkandya kutoka DAWASA.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wanasheria wa Sekta ya Maji.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewataka wanasheria wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na taasisi zake kuhakikisha wanasimamia sheria wanazoziweka, ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kuisababishia Serikali hasara na kukwamisha maendeleo ya Sekta ya Maji.

Profesa Mkumbo amezungumza hayo katika mkutano uliowakutanisha wanasheria 36 kati ya 41 kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, pamoja na wanasheria wa wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma; lengo la mkutano huo likiwa ni kuboresha utendaji wa wanasheria katika Sekta ya Maji katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.

Amesema kama washauri na wasimamizi wa sheria katika Sekta ya Maji waendelee kusimamia vyema sheria, taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali na kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na ufanisi; kuzingatia kanuni za maadili na utendaji kazi wa wanasheria. 

Wakihakikisha kuwa wanaifahamu vizuri sekta na vipaumbele vyake na kuvitekeleza; wakitoa ushauri pasipo woga pamoja na kuongeza ujuzi katika utendaji wao wa kazi.

WIKI HII NDANI YA DStv!!

0
0
Mashindano mapya kabisa ya UEFA Nations League yanaanza kutimua vumbi wiki hii huku pazia likifunguliwa na magwiji wawili wa Soka siku ya Alhamisi. Ambapo Ufaransa (Mabingwa wa Dunia) watacheza dhidi ya Ujerumani (Mabingwa wa Dunia waliopita). Kisha kuendelea na Albania dhidi ya Israel siku ya Ijumaa, huku Italy ikiikaribisha Poland siku hiyo hiyo ya Ijumaa na kumaliziwa na Turkey vs Russia.

Jumamosi Switzerland itacheza dhidi ya Iceland, Finland vs Hungary wakati England wakicheza dhidi ya Spain. Na siku ya Jumapili Germany itacheza dhidi ya Peru, France itacheza dhidi ya Netherlands, Bulgaria vs Norway Na Denmark vs Wales!

Mechi hizi zote utazipata ndani ya DStv kuanzia kifurushi chako cha Bomba kwa sh.19, 000 tu! Bila kusahau Jumamosi hii, DStv inakuletea mtanange wa kukata na shoka pale Uganda (The Cranes) watakapozichapa na timu yetu ya Taifa Tanzania yaani Taifa Stars. Macho Na masikio tutayaelekeza Uganda, tarehe 8/9/18 ndani ya Supersport 8 ya kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu ndani ya DStv pekee!

Moto Hauzimi na kama Sio DStv Potezea!

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, ALA KIAPO CHA UJUMBE TUME YA UTUMISHI, JESHI LA POLISI, MAGEREZA NA UHAMIAJI

0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akila kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, pamoja na Uhamiaji. Kiapo hicho kilifanyika katika Ofisi za Mahaka Kuu ya Tanzania, leo Septemba 4, 2018 jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama akila kiapo cha uadilifu mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, pamoja na Uhamiaji.
Jaji Kiongozi, Dkt. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (meza kuu) akifanya mazunguzo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(kulia) baada ya kula kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Uhamiaji.
Jaji Kiongozi, Dkt. Eliezer Feleshi wa Mahakama Kuu ya Tanzania(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike(kushoto) mara baada ya kula kiapo cha kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi kwa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza na Uhamiaji. Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Magereza, Uwesu Ngarama. (Picha na Jeshi la Magereza).

SERIKALI YAELEZEA MBINU ZA KUKABILIANA NA UMASKINI

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali imeeleza kuwa inazingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala (ccm), Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na mwaka mmoja, pamoja na Mwongozo wa Bajeti kugawa rasilimali fedha na watu katika kukabiliana na changamoto za umaskini nchini.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe. Daniel Nicodemus Nsanzugwanko (CCM), aliyetaka kujua mbinu za Serikali katika kuhakikisha mikoa maskini nchini inapata rasilimali fedha na watu ili iweze kuondokana na hali hiyo ya umaskini.

Dkt. Kijaji alisema kuwa mgawanyo wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huenda sambamba na mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utekelezaji, usimamizi, uperembaji na kutoa huduma kulingana na aina ya miradi.

Aidha Mhe. Nsanzugwanko alihoji hatua zilizochukuliwa na Serikali katika Mkoa wa Kigoma ili kujenga ulinganifu katika maendeleo.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema Serikali imebainisha  maeneo na miradi ya kimkakati kwa ajili ya utekelezaji ili kufungua fursa za kiuchumi  mkoani huo.

Alieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya kimkakati yaliyobainishwa na kuanza kutekelezwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 ni pamoja na mradi wa upanuzi na ujenzi wa Uwanja wa Ndege Kigoma.

“Miradi mingine ni mradi wa uzalishaji wa umeme wa maji katika maporomoko ya mto Malagarasi MW 44.7, kuanzisha na kuendeleza eneo huru la uwekezaji Kigoma, mradi wa gridi ya Kaskazini Magharibi kv400 na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa”, alisema Dkt. Kijaji.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijibu maswali katika kikao cha Bunge leo Jijini Dodoma.



KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: TUNAHITAJI WAWEKEZAJI KWENYE MAZAO YA KILIMO, SAMAKI NA MIFUGO - MAJALIWA

DK.SHEIN AZINDUA OFISI MPYA ZA WILAYA-DUNGA NA UIMARISHAJI MFUMO WA WAKALA WA USAJILI MATUKIO YA KIJAMII

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt.Hussein Khamis Shaaban (kulia) mara baada ya kuzindua Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya- Dunga na Uimarishaji wa Mfumo wa Matukio ya Kijamii katika hafla iliyofanyika leo katika Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,(kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika leo Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,(kulia)Makamo wa Pili wa rais Balozi Seif Ali Idii,Mama Mwanamwema Shein na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri (kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua jengo la Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika leo katika Wilaya kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images