Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO

$
0
0
Serikali imeazimia kurudisha ikolojia ya hifadhi ya Ngorongoro katika mazingira yake ya asili na kusisitiza kuwa shughuli zote za kuharibu na kuchafua  ikolojia hiyo vitadhibitiwa kwa nguvu na uwezo wote.
Akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa lengo la ziara yake ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Mamlaka hiyo mwezi Machi 2017.


Katika ziara yake mapema mwaka jana pamoja na mambo mengine Waziri Makamba aliagiza Mamlaka hiyo kuchukua hatua za haraka na kuwaelekeza wamiliki wa hoteli na loji hususan zilizoko katika kingo za kreta katika bonde la Ngorongoro kutafuta vyanzo mbadala vya maji na kuondokana na kutegemea chanzo cha chemichemi za Lerai.


Aidha, Waziri Makamba aliagiza kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kudhibiti mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro kwa kuunda jopo la wataalamu kutoka Tume ya Sayansi na Tecknolojia,  Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Hifadhi za Taifa za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Ngorongoro ili kufanya utafiti wa kina na wakisayansi wa kubaini mbinu mpya ya kupambana na mimea hiyo vamizi inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama kama malisho.


Akitoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo Kaimu Mhifadhi wa Ngorongoro Dkt. Maurus Msuha amesema kuwa Mamlaka ya Ngorongoro iliwaandikia barua wamiliki wote wa hoteli na loji  na kufanya tafiti kupitia kwa wataalamu elekezi wawili tofauti ambao kwa pamoja walishauri kuandaliwa kwa mkakati wa usimamizi na matumizi ya maji ndani ya Mamlaka ya Ngorongoro utakaokuwa suluhisho la matatizo la maji bila kuathiri mifumo ya ikolojia katika Hifadhi.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akiwa katika kikao na wadau na wamiliki wa hoteli zilizopo katika kingo za kreta katika bonde la Ngorongoro. Pamoja na mambo mengine Waziri Makamba amewata kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya kutibu maji taka ili yaweze kutumika tena na kuwataka kufahamu kwa matumizi ya maji kutoka ndani ya kreta hitimisho lake linakaribia, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akipata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Dkt. Linus Munishi mtafiti kutoka Taasisi ya Nelson Mandela. Taasisi hiyo imetenga eneo maalumu la majaribio ya kuua mimea vamizi bila kuathiri mazingira, utafiti unao onekana kufanikiwa.
Pichani ni mmea vamizi ambao unaathiri sana malisho ya wanyama katika bonde la Ngorongoro kreta. Serikali inachuka hatua za haraka kudhibiti mmea huo unaosambaa kwa kasi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa  Simiyu, Anthony Mtaka wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.
 Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu  Mhandisi Albert Kent, akimuoesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, nyumba za Mhandisi Mshauri zilizojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya CHICO katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Muonekano wa kazi za ujenzi zikiendelea kwenye daraja la mto Simiyu katika barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7, Mkoani Simiyu
Imetolewa na Kitengo cha  Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano.


UJENZI unaondelea wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa Km 49.7 kwa kiwango cha lami unatarajiwa kufungua mkoa wa Simiyu na mikoa jirani ya Mara, Mwanza na Shinyanga  hivyo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe mkoani Simiyu wakati akikagua barabara hiyo inayojengwa na mkandarasi wa kampuni ya CHICO na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo toka ulipoanza mwezi Oktoba mwaka 2017.

"Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa na nina imani mkandarasi atamaliza mapema mradi huu",amesisitiza Waziri Kamwelwe.

Aidha, ameupongeza uongozi wa mkoa huo na Wakala wa Barabara (TANROADS), kwa kusimamia mradi huo usiku na mchana na kuwataka kutoa taarifa muda wowote endapo kutakuwa na changamoto zinazoweza kukwamisha mradi huo.

Akizungumzia kuhusu Kiwanja cha Ndege cha Simiyu, Mhandisi Kamwelwe amemueleza Mkuu wa Mkoa  kuwa hatua za awali zinaendelea katika kuhakikisha kiwanja hicho kinajengwa ili kufungua mkoa huo katika sekta za usafirishaji na uwekezaji.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

UZINDUZI WA MFUMO WA KIELETRONI WA KUSAJIRI WAKAAZI WA ZANZIBAR (E-ID CARD) SEPT 4, 2018

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt. Hussein Khamis Shaban akizingumza na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali viliko Zanzibar kuhusiana na uzinduzi wa Mfumo wa Uimarishaji wa usajili wa taarifa vitambulisho vya Mzanzibar (ZAN ID) na Ofisi za Wilaya na Mkoa uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 4-9-2018 katika Wilaya ya Dunga Wilaya ya Kati Unguja. Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt. Hussein Khamis Shaban, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Wilaya ya Kati Dunga. Mkoa wa Kusini Unguja. Mwanasheria wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar, Hamid Haji Machano akijibu na kutowa ufafanuzi wa maswali yalioulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la uzinduzi wa usajili wa Vitambulisho vya mzanzibar kwa njia ya kisasa.

WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatakaWatanzania waishio nje ya nchi wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao kwa kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inaamini kuwa Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi endapo wananchi wake watatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakatiakizungumza na Watanzania waishio nchini China kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzani uliopo jijini Beijing. 

Alisema nchi zote zilizoendelea zilihakikisha kuwa wananchi wake wanaelewa na kutekeleza matamko yanayowahamasisha kufanya kazi, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania popote walipo kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu.’

Waziri Mkuu alisema China ambayo imefanikiwa kuwa moja kati ya nchi zenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, imefika hapo kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na wananchi wake, ambao waliamua kuunga mkono juhudi za Serikali yao kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi wakiwa ndani au nje ya nchi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya ambayo inachafua jina na heshima ya nchi yao kimataifa. “Tanzania ni nchi nzuri na inaheshimika duniani, nawasihi wote mnaoishi nje muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga alisema mwelekeo wa Diplomasia ya Tanzania Kimataifa hivi sasa ni kiuchumi (economic diplomacy), hivyo Watanzania waishio nje wanapaswa kuwa wabunifu, makini katika kutafuta fursa zenye manufaa kwa nchi yao.

Alisema Diplomasia ya Uchimi si kupeleka Tanzania wawekezaji tu bali wawekezaji katika viwanda ambavyo kila vinapojengwa vinachangia kuinua uchumi wa Taifa.Kwa upande wake,Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwaasa vijana kuitumia teknolojia ya mawasiliano na mitando ya jamii kutafuta habari na taarifa muhimu hasa nafasi za masomo ili kujiendeleza kielimu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 03, 2018.

MTENDAJI MKUU TFS ATOA NENO KWA WASHIRIKI MISS TANZANIA 2018

$
0
0
*Awataka wawe mabalozi kuhimiza uhifadhi wa misitu,utalii wa ndani
 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

WAREMBO wa Shindano la Miss Tanzania 2018 wametajwa kuwa mabalozi wazuri wa Vivutio vya Utalii nchini ikiwemo Rasilimali za Misitu na Nyuki pamoja na Maporoko.

Akizungumza na Warembo hao jijini Dar es Salaam wakati anawaaga wakielekea katika hifadhi ya Amani mkoani Tanga, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amewataka walimbwende hao kutumia weledi, uwezo Kitaaluma na nafasi katika jamii kusaidia uhifadhi wa misitu.

Prof. Silayo amewataka warembo hao kutangaza Misitu hiyo mazuri yake ili iweze kutumika kutoa huduma za kiutalii na kuonesha thamani yake iliyosimama.Amesema uhifadhi wa misitu unaifaida nyingi na moja ya faida misitu ni cha chanzo uhifadhi wa maji na kuongeza pamoja na hewa safi.

Amesema kuwa TFS itatumia sehemu ya washiriki hao wa Miss Tanzania mwaka huu kwa ajili ya kuwa malozi ambao watashiriki kikamilifu kuhimiza uhifadhi misitu.Amefafanua watawajengea uwezo katika kuhakikisha wanaifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa na zaidi kuna maeneo mengi ya misitu ambayo imehifadhiwa ambayo inahitaji mabalozi wa kutangazwa.

"TFS pamoja na wadau wengine wakiwamo wa utalii nchini ambao wapo Wizara ya Maliasili na Utalii tumeamua kushirikiana na  ya Miss Tanzania kuhakikisha washiriki watano wa Miss Tanzania tunawatumia kuutangaza vivutio vya utalii na uhifadhi misitu,"amefafanua Profesa Silayo.
 Washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea Msitu Amani mkoani Tanga.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Profesa Dos Santos Silayo(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Miss Tanzania mwaka 2018 baada ya kuzungumza nao kuhusu umuhimu wa warembo hao kuutangaza uhifadhi wa misitu na utalii nchini
 Muandaji wa Mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2018 Basila ambaye pia amewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 1998 akiwa na Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Sontos Silayo wakati wakizungumza na washiriki wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini afanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi.

TAWLA yaanzisha kampeni ya kuandika wosia kwa wamasai na wameru

$
0
0
Seif Mangwangi, Arusha
CHAMA cha wanasheria wanawake (Tawla), kimeanza kampeni ya kuhamasisha Jamii ya kabila la  maasai na wameru kuandika wosia kabla ya kufariki dunia kufuatia kuwepo kwa matukio mengi ya unyanyasaji baada ya mmoja katika familia kufariki.

Akizungumza jana katika kampeni hiyo iliyofanyika kwa wananchi wa vijiji vya ngaramtoni, emaoi na olmotonyi katika kata ya olmotonyi wilayani Arumeru, Afisa sheria kutoka Tawla, Neema Ahmed alisema ofisi yao imekuwa ikipokea matukio mengi ya wanawake kunyanyaswa baada ya waume zao kufariki.

Alisema wajane katika familia nyingi za jamii ya kimaasai na kimeru wamekuwa mafukara kutokana na kunyang’anywa mali na mashemeji mara baada ya waume zao kufariki dunia bila kuacha maandishi yanaayoonyesha urithi wa mali.

“Lakini cha kushangaza hizi mali zinazogombewa unakuta ulizitafuta na mme wako lakini inapotokea ukafariki dunia wanaibuka mashemeji na hata wakati mwingine wakwe wanawanyang’anya, sasa kama kutakuwa na wosia hakuna atakaeweza kuingilia mali za marehemu, “ alisema.
 Wananchi wa kata ya Olmotonyi wakiwasikiliz Mafisa sheria wa chama cha wanawasheria wanawake (Tawla), Neema Ahmed, na Aika Palangyo katika kampeni kuhusu suala la uandishi wa wosia.
 Wananchi wa kata ya Olmotonyi wakimsikiliz afisa sheria wa chama cha wanawasheria wanawake (Tawla), Neema Ahmed ( hayupo pichani), akiwahamasisha kuhusu suala la uandishi wa wosia.
Mwanasheria wa Tawla Aika Palangyo aliwaeleza wakazi wa kata ya Olmotonyi namna wosia unavyoandikwa.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA USHIRIKIANO KATI YA CHINA NA AFRIKA ULIOANZA JIJINI BEIJING

$
0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wakuu wa Afrika na China baada ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping kufungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya Tanzania na China Kwenye ukumbi wa Mikutano wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAADHIMISHO YA WAHANDISI TANZANIA KUFANYIKA AGOSTI 5-7, UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Ngwisa Mpembe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana naMaadhimisho ya Siku ya Wahandisi hapa nchini Bodi ya Usajili Wahandisi nchini.
 Kaimu Msajili toka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari picha za wahandisi waliokuwepo kipindi cha uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1968 wakati akizungumza na waandishi wa habari jiji Dar es Salaam leo.
  Kaimu Msajili toka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Patrick Barozi (kulia) akionesha kwa waandishi wa habari hati iliyosainiwa na Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere mwaka 1968 ili kuanzishwa kwa bodi hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania, Mhandisi Ngwisa Mpembe.
Msajili Msaidizi wa Bodi ya usajili wa Wahandisi (Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

BODI ya usajili ya wahandisi kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake pia wahandisi wataalam watakula kiapo cha utii, Maadhimisho hayo  yatafanyika katika ukumbi wa DiamonJubilee jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 5 hadi 7.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mhandisi Ngwisa Mpembe amesema kuwa Jumuiya ya wahandisi nchini, taasisi na mashirika ya kihandisi, jamii ya wafanyabiashara pamoja na jamii kwa ujumla kuwa siku ya wahandisi Tanzania itaadhimishwa Agosti 5-7.

"Siku ya wahandisi ni siku pekee kwa wahandisi wa Tanzania kuweza kuonyesha yale wanayoweza kufanya kwa maendeleo ya taifa". Amesema Mhandisi Mpembe.

Amesema kuwa  maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika kama majadiliano ya kitaaluma, kiapo cha wahandisinwatalaam, maonyesho mbalimbali ya kiufundi na biashara, kutoa tuzo kwa wahandisi na waliosaidia uhandisi ndani ya miaka 50, kutambua na kuzawadia na kuwatambua wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwaka wa mwisho wa masomo 2017/2018.

Maadhimisho ya siku ya wahandisi Tanzania 2018 inafanyika kila mwaka na mwaka huu ni mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake.

CHINA KUTOA DOLA BIL. 60 KWA MAENDELEO YA AFRIKA

$
0
0


RAIS wa China, Xi Jinping amesema China itatoa jumla ya dola bilioni 60 za Marekani kwenye mpango wake wa miaka mitatu ya ushirikiano na Afrika katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 03 ,2018) wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika jijini Beijing nchini China.

Rais Jinping ameahidi kuwa nchi yake itatoa ushirikiano ili kuhakikisha kwamba amani ya kudumu inapatikana Barani Afrika, hatua ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.

Maeneo mengine ambayo Rais huyo ameahidi kuwa China italisaidia Bara la Afrika ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, ushirikiano katika sekta ya biashara na huduma za afya.

Kadhalika, Rais Jinping amesema China itatoa nafasi za mafunzo ya kilimo bora na mafunzo ya ufundi kwa watalaam kutoka nchi za Afrika ili kuchangia katika maendeleo ya uchumi. 

Amesema hivi sasa anaamini kwamba China na nchi za Bara la Afrika wako karibu zaidi na wanashirikiana vizuri sana katika shughuli za kimaendeleo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mkutano huo ulianza kwa sherehe ya ukaribisho na baadae viongozi kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antyonio Geterres walipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na mwenyeji wao Rais wa China. 

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo alisalimiana na Rais Jinping baada ya ufunguzi. Mkutano huo utaendelea kesho ambapo viongozi wengi kutoka Bara la Afrika watapata nafasi ya kuzungumza.

Kamati ya Bunge yawataka wananchi kuacha kukwamisha miradi ya maendeleo

$
0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiongoza mkutano wa Wadau wanaohusika katika  utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji ya Bonde la Mto Rufiji,uliofanyika mkoani Njombe.
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ussi Pondeza ( katikati), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( kushoto) na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga (kulia) wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa wadau wanaohusika na  utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji bonde la mto Rufiji, uliofanyika mkoani Njombe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa nne kulia) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ( katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na viongozi mbalimbali kutoka mkoa wa Njombe walioshiriki mkutano wa wadau wa utekelezaji mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya maji ya bonde la mto Rufiji, uliofanyika mkoani Njombe.Kamati ya Bunge yawataka wananchi kuacha kukwamisha miradi ya maendeleo 
Na Zuena Msuya Njombe,

KAMPUNI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imewataka wananchi kuwa wazalendo na kujali maslahi ya nchi na taifa katika kutekeleza miradi ya mikubwa ya maendeleo ukiwemo mradi kuzalisha umeme wa maji wa megawati 2100 katika maporomoko ya bonde la Mto Rufiji. 

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Ussi Pondeza, mkoani Njombe wakati wa mkutano wa Wadau wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji katika maporomoko ya bonde la mto Rufiji.

Pondeza alisema kuwa,  Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kupenda kuangalia maslahi yao binafsi kwa kutaka malipo makubwa ama fidia zinazoweza kuepukwa  pindi Serikali inapoanzisha miradi mikubwa ya maendeleo bila kujali kuwa miradi hiyo ni kwa manufaa ya Watanzania wote.

Alitoa angalizo kuwa,  tabia hiyo imekuwa ikichelewesha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo  na hata wakati mwingine kukwamisha utekelezaji wake. 

"Baadhi yetu sisi watanzania sijui tuna tabia gani, tunaletewa mradi kwa maendeleo yetu wenyewe lakini kwa vile ni wabinafsi tunaanza kukwamisha kwa kutaka fidia ili mradi mtu upate fedha! unasahau kuwa hizo ni juhudi za Serikali katika kutuletea maendeleo sisi wenyewe,” alisema Pondeza.

Aliongeza kuwa,  kuna baadhi ya watu wakikosa huduma fulani huilalamikia Serikali kuwa haijafanya kitu hali ya kuwa wao ndio walikuwa wakizuia utekelezaji hivyo aliwataka wabadilike.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA.                          

Wanahabari wafundwa juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Nchini

$
0
0
WAANDISHI wa Habari wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kuihabarisha jamii ili kuepukana na janga hatari la ugonjwa wa Ebola.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  ameyabainisha hayo wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa waandishi wa namna ya kutoa taarifa za ugonjwa huo wa Ebola.
Jamii imetakiwa kujua dalili za ugonjwa huo wa Ebola kwa kina kwani kupitia Wanahabari,mafunzo hayo yatasaidia sana kutoa elimu na itaenea maeneo mengi.

“Ugonjwa huu wa Ebola kiukweli ni ugonjwa hatari. Na tokea kutokea katika nchi za wenzetu umesababisha madhara makubwa sana ikiwemo Uchumi ikiwemo masuala ya biashara na uwekezaji.

Imebainishwa kuwa madhara ya kiuchumi juu ya Ebola yangeuwa watu wengi zaidi kuliko ugonjwa wenyewe. Sisi tulikuwa na wasiwasi sana ndio maana tulienda wenyewe huko kufuatilia..mimi nilienda mipakani Rusumo na Mganga Mkuu yeye alienda mipaka ya Ngala na maeneo mengine.” Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Na kuongeza kuwa, tatizo kubwa ni suala la wasafiri wanaopita njia za panya kwani zimekuwa zikiwapa changamoto na wameomba Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanalinda maeneo hayo.
 Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa Semina jinsi  ya kurepot Kuhusu ugonjwa wa Ebola na namna ya kuzuia usiingie nchini.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Adiele Onyeze Akizungumza na waandishi wa habari kuhusukushirikiana na Tanzania katika kuzuia milipuko ya magonjwa mbalimbali ikiwemo  ugonjwa huo wa Ebola ambao umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara katika nchi za Afrika leo katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa Kimila kutoka Jamii ya Kimasai Tanzania wamlilia Waziri

$
0
0
Viongozi wa Kimila kutoka Jamii ya Kimasai Tanzania wamlilia Waziri
Mwakyembe kuhusu eneo la kufanyia Mikutano ya Kimila.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison
Mwakyembe (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Kimila kutoka jamii ya Kimasai nchini akiwa ameshikana
mkono na Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu wa Kimasai Tanzania Chifu.
Isack Meijo Ole Kisongo (wapili kulia) mara baada ya viongozi hao
kuwasilisha malalamiko yao leo Jijini Dodoma kuhusu mgogoro wa eneo
la kufanyia mikutano ya kimila lililoko Mjini Arusha kupunguzwa pamoja
na jengo lao walilojengwa kusimamishwa ujenzi kwa zaidi ya miaka kumi
hivyo kusababisha changamoto ya utekelezaji wa shughuli zao za
kimila,wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Ukoo wa Laizer Tanzania
Bw.Oltetiai Sozi,anayemfuata (wapili kushoto) ni Mwenyekiti wa Ukoo wa
Mollel Tanzania Bw.Saitabau Mollel, kutoka kushoto wa kwanza ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Dira kwa Jamii ya Kimasai Tanzania Zablon Ole
Muterian.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Dira kwa Jamii ya Kimasai Tanzania Bw.
Zablon Ole Muterian (kulia) akimwonyesha Mheshimiwa Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ( baadhi ya nakala
za barua,taarifa na picha zinazohusu mgogoro wa eneo lao la kufanyia
mikutano ya kimila kwa jamii ya Kimasai nchini lililopo Arusha Mjini
namna lilivyopunguzwa na zuio la kujenga ukumbi wao wa mikutano
ulivyofanyika na kusababisha kero kwao wakati wa kufanya mikutano yao
ya kimila kitaifa kwa kila mwezi katika kikao kilichoendeshwa na
Mheshimiwa Waziri,wakiwemo viongozi wa Idara ya Utamaduni pamoja na
wazee hao wa kimila kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Viongozi wa Kimila kutoka Jamii ya Kimasai Tanzania wakimsikiliza
kwa makini Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokuwa akiwaeleza hatua
atakazo chukua katika kufanikisha anatatua mgogoro wao kuhusu eneo lao
la kufanyia shughuli za kimila lililopo Mjini Arusha, leo Jijini Dodoma
mara baada ya wazee hao kumweleza changamoto wanazozipata katika
kuendesha shughuli za za kimila tangu ya eneo hilo lilipopunguzwa.

MANONGA QUEENS YAILAZA SINGIDA WORRIER MECHI YA KIRAFIKI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TIMU ya Wanawake ya Mkoani Tabora katika jimbo la Manonga maarufu kama Manonga Queens wameichapa timu ya Singida Worrier bao 2-0 kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja Namfua Mkoani Singida.

Manonga Queens walianza kuchungulia nyavu za Singida Worrier mnamo dakika ya 32 na waliandika bao la kwanza kupitia Ashura Shaabani.

Katika kipindi cha pili Singida Worrier walipata pigo la pili baada ya Ashura Shaban kwa mara nyingine kuifungia timu yake bao la pili mnamo dakika ya 85, na matokeo hayo yalidumu hadi dakika 90 zilipokamilika na Manonga Queens kutoa kifua mbele dhidi ya wwnyeji wao Singida Worrier.

Akizungumza baada ya mtanange huo kocha wa Manonga Queens Khamis Abihud amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa mgumu wachezaji walijituma na kuibuka na ushindi huo mnono ukiwa ugenini na ameeleza kuwa wamejizatiti katika kufuzu ligi kuu daraja la kwanza.

Ashura Shaban ambaye aliipatia timu yake mabao 2 ameeleza kuwa mazoezi, maagizo ya mwalimu na ushirikiano kutoka kwa wadau hasa Mbunge wa Manonga Seif Gulamali unazidi kuwapa ari na kasi zaidi ya kujituma katika soka.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali(katikati) akikabidhi mipira kwa viongozi na wachezaji wa Manonga Queens timu ya jimboni hapo ambayo inashiriki mpira ligi daraja la kwanza kwa wanawake.

China Kushirikiana na Nchi za Afrika Katika Mambo Nane

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO

Beijing-CHINA

RAIS wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping amesema, Serikali ya nchi hiyo ipo tayari kushirikiana na Afrika katika maeneo makubwa nane katika kipindi cha miaka mitatu ijayo itayojikita katika masuala ya viwanda, miundombinu, biashara, kilimo, ulinzi na usalama pamoja na mazingira. 

Akifungua Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Bara la Afrika (FOCAC) leo Beijing China na Rais Xi Jinping ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo amesema katika masuala ya viwanda, uchumi wa Bara la Afrika na usafirishaji wa bidhaa utaendelea kupewa kipaumbele na Serikali ya China pamoja na makampuni yake yanahimizwa kuwekeza katika nchi za Afrika.

Kuhusu sekta ya kilimo, Rais Xi Jinping alisema Serikali ya China imepanga kuanzisha miradi 50 itayogharimu kiasi cha Yuan Bilioni 1 (Dola Milioni 147) itayosaidia masuala ya dharura na majanga mbalimbali ya kibinadamu sambamba na hilo, Rais Xi Jinping ameahidi kupeleka wataalamu 500 wa masuala ya kilimo ili kusaidia maendeleo ya sekta hiyo Barani Afrika.

Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu, Rais Xi Jinping amesema Serikali ya China itafanya juhudi na Umoja wa Afrika kuunda mpango wa ushirikiano wa Miundombinu baina ya Bara la Afrika na China na kusaidia makampuni ya Serikali ya China kupata fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Afrika uliofunguliwa na Rais huyo kwenye ukumbi wa Great Hall of the People uliopo Beijing, Septemba 3, 2018. Mheshimwa Majaliwa amemwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 .


TANZANIA YAPATA MWAKILISHI WA HESHIMA HONG KONG NA MACAO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki kwa pamoja na Bibi Annie Suk-Ching Wu wakisaini Mkataba kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania huko Hong Kong na Macao. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Beijing, China na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda pamoja viongozi wengine ambao wapo nchini China kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC). 
Balozi Mbelwa na Bibi Wu wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini 
Mhe. Waziri Mahiga akitoa hotuba kumpongeza Bibi Wu kwa kukubali kuiwakilisha Tanzania kwenye maeneo hayo na kumtaka kuiwakilisha vema nchi 
Mhe. Waziri na viongozi wengine wakisubiri kuanza kwa ratiba 
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mbelwa na Bibi Wu mara baada ya kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuiwakilisha Tanzania Hong Kong na Macao
Picha ya pamoja na viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo 
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda akiteta jambo na Mhe. Balozi Mbelwa 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Bibi Justa Nyange akiwa na Maafisa ambao walikuwepo kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima kwenye majimbo ya Hong Kong na Macao ya nchini China 

Rais Magufuli atengua na kuteua Katibu Mkuu na Kamishna wa Kazi

RAIS DKT. MAGUFULI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA UJENZI WA MELI MPYA, CHELEZO, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA NA MV BUTIAMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia zoezi la utiaji saini Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika Bandari ya Mwanza Kusini mara baada ya kushudia utiaji saini wa Mikataba mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa Meli mpya ya abiria na mizigo, Chelezo, ukarabati wa Meli za Mv Victoria na Mv Butiama, Mikataba ambayo ilisainiwa kati ya Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania Marine Services Company (MSCL) na Kampuni tatu za Korea Kusini ambazo ni M/S STX engine Co ltd, Saekyung Construction ltd na KTMI Co ltd.
Mfano wa Meli mpya itakayojengwa ambayo Mkataba wake umesainiwa. Meli hiyo itakuwa na Urefu wa Mita 90, Kimo mita 10, uwezo wa kubeba abiria 1200 magari madogo 20, mizigo tani 400 na itakuwa ikisafiri kwa muda wa masaa sita tu kutoka Mwanza mpaka mkoa wa Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Yong watatu kutoka kushoto waliokaa,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella wakwanza kulia waliokaa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe watatu kutoka kulia pamoja na wabunge mbalimbali wa mikoa ya Kanda ya ziwa.

TANZANIA YAPATA MWAKILISHI WA HESHIMA HONG KONG NA MACAO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki kwa pamoja na Bibi Annie Suk-Ching Wu wakisaini Mkataba kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania huko Hong Kong na Macao. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Beijing, China na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda pamoja viongozi wengine ambao wapo nchini China kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC).
Balozi Mbelwa na Bibi Wu wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini
Mhe. Waziri Mahiga akitoa hotuba kumpongeza Bibi Wu kwa kukubali kuiwakilisha Tanzania kwenye maeneo hayo na kumtaka kuiwakilisha vema nchi
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mbelwa na Bibi Wu mara baada ya kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuiwakilisha Tanzania Hong Kong na Macao
Picha ya pamoja na viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda akiteta jambo na Mhe. Balozi Mbelwa
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bibi Justa Nyange akiwa na Maafisa ambao walikuwepo kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima kwenye majimbo ya Hong Kong na Macao ya nchini China

MTANGAZAJI SUNDAY SHOMARI WA VOICE OF AMERICA ATWAA TUZO, AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUMPIGIA KURA KWA WINGI

$
0
0
Napenda kuchukua nafasi hii kwa heshima na taadhima kuwashukuru sana watanzania wote mliojitolea kunipigia kura huu ni ushindi wetu sote na kazi kubwa mmeifanya. Mungu awabariki.
- SUNDAY SHOMARI
Viewing all 110137 articles
Browse latest View live




Latest Images